KATIBA ni
kitu muhimu sana katika nchi, ni kitu ambacho kila mmoja alitakiwa akifahamu na
ikiwezekana, kwa vile tumepata furusa hii, basi kila mmoja alitakiwa achangie kwa namna moja au nyingine kwani huo
ni mkataba wake na nchi yake. Mimi sio mtaalamu sana wa sheria, lakini nina
maoni yangu kidogo tu.
Kulumbana
kwa hoja ni muhimu, hilo halikwepeki, hatuwezi kukubali kila hoja kwa kauli za ndio
ndio,..hapana, ni muhimu watu waelezane na kukosoa pale panapoonekana kuna
uwalakini, kwani katiba hutungwa na watu, na watu sio wakamilifu kwa kila
jambo.
Kulumbana kutasaidia kukiweka kila kipengele kwenye stahiki yake na
kuleta tija ya mshikamano kama taifa na utaifa wetu. Tusione ajabu kwa hayo wanayoyafanya
wenzetu, cha muhimu ni hoja zenye msingi wa kujenga, kuboresha na sio kubomoa na kuharibu.
Kila mmoja
ana mtizamo wake na maoni yake,ni muhimu, basi ni vyema kila mmoja apewe nafasi hiyo, kwa
ajili ya katiba yake hiyo, lakini kwa vile Watanzania tupo wengi, itakuwa ni
vigumu kwa kila mmoja kusema lake na lisikilizwe, ndio maana wakachaguliwa hao
wawakilishi, wakiwa na kianzio cha rasimu ambayo imetokana na maoni ya wananchi,
...hicho ni kianzio, na ni msingi mnzuri wa kuboresha katiba yetu.
Sasa swali
la kuuliza hapo, hao wawakilishi walioteuliwa wanawakilisha vyama vyao au
wananchi? Jibu lipo wazi kuwa wanawakilisha wananchi, sasa vyama na itikadi za
vyama zinatoka wapi?
Kama wao ni
wawakilisha wa wananchi basi tunawaomba wavue magamba yao ya uwakilishi wa
vyama, na hilo lingelifanyika mapema kwa kula kiapo kuwa hapo sio sehemu ya
misimamo ya vyama vyao, au itikiadi zao binafsi hapo ni sehemu ya kutengeneza
kitu kwa ajili ya masilahi ya taifa. Leo wapo kwenye chama hicho wanachokitikadia,
kesho wanaweza wakawa kwenye chama kingine, lakini taifa lipo pale pale, katiba
ipo pale pale...
Sasa kwa
maoni yangu, ni kweli kuna mambo magumu sana katika kuiboresha hiyo katiba,
hilo tulielewe wote, na maamuzi yake ni magumu pia, yanagusa mambo nyeti. Kwa
mfano hilo la Muungano, ni nyeti kwani linagusa utaifa , najua kuna maswala
mengine nyeti yanakuja kama ya imani za kidini nk, haya ni mambo yanayotakiwa
umakini na busara ya hali ya juu ikiwemo kuvumiliana, ili tukwepe manung'uniko, migongano isiyo na tija. Ili iwe sehemu ya chachu za maendeleo, amani na mshikamano.
Kwa hayo
mimi niliona kama inafikia mahali kunakuwa na ugumu kupitiliza na ili kuokoa
muda, hayo maswala magumu kwanza yawekwe pembeni, tuendelee na vipengele
vingine, ambavyo havina ubishani wa makundi. Nina imani, kwa vile wote waliochaguliwa
hapo wana busara zao na hekima, baada ya kuendelea mbele kwa mjadala wa
vipengele vingine, wajumbe watakuwa wamejenga uzoefu fulani, wa kuvumiliana, na
kujiona wao ni kitu kimoja, na hapo watakuwa wameweka utaifa wao mbele, hata
wakivirudia vile vipengele vigumu, huenda kukawa na suluhu fulani la pamoja.
Mimi nina
wasiwasi kuwa tunaweza tukapoteza muda kwa mambo machache na huenda yakakimbilia kutugawa mapema na hata kujenga chuki, ...japokuwa mjadaal kama huo ni muhimu sana, lakini tuangalie mbali zaidi, tuangalie
muda, gharama, na hamasa za ushawishi kwa wananchi ambao unaanza kujengwa
kutoka kwa wanasiasa kwa kuleta mitizamo yao ya makundi tofauti, hatuoni kuwa
hii ni hatari kwa utaifa. Taifa hujengwa
na makabila dini, rangi na watu tofauti tofauti, ndio maana tunaishi pamoja,
tunavumilia,sasa hizo hisia nyingine za nyoyoni tusizitoe kwa sasa, hazina
mantiki ya kitaifa...
Jamani wanasiasa, tusianze kutoa hoja za kuonyesha hisia zetu za ndani, zenye chuki, tuwe makini kwa hilo.
Nashangaa kama viongozi wa siasa
wanarudi kwenye makundi yao mbali mbali kujenga hadhira, na hamasa fulani, ili
hoja zao zionekane zina msingi, hatuoni tunaanza kuwagawa wananchi. Kwa hivi sasa kwa nia njema ya katiba, itikadi zetu tuzipumzishe, tuwe na wimbo mmoja wa utaifa.
Mpaka hapo najiuliza, kama wanasiasa wanataka kuliinglia bunge la katiba, hao
wawakilishi wetu wana maana gani, je hiyo ndio katiba ya pamoja tunayoitaka au
ni utashi wetu ..tuwaache wawikilishi wajadili, watoe hoja, wakatae, ili
kuondoa mapungufu yaliyonekana katika katiba tuliyokuwa nayo...ila ni muhimu
sana, mabo ya itikadi za kivyama yaondolewe, hapo sio sehemu ya kampeni za
kisiasa...uongozi huo una muda wake, lakini utaifa upo pale pale....
Mimi naona
hivi kama tulishakubali kuwa hao wajumbe waliopo bungeni ni wawakilishi wetu,
hebu tuwaachie nafasi hiyo hao wawakilishi wetu, wajadili kwa mapana yao walumbane wanavyoweza, hata
kusigishana ili tuone uzuri na ubaya wa kila kipengele, sisi wananchi
tuliowatuma yetu yawe ni macho na
masikio, na hata ikiwezekana kuwaongezea hoja, tufanye hivyo kwa nia njema...
Mimi nina imani baada ya hapo kwa kuwa hao wajumbe wetu ni watu wenye
ufahamu hekima na akili, watakaa pamoja na kuyaangalia hayo walioshindwana
kihekima zaidi, waone mapungufu yake na kuona jinsi gani ya kuyaweka sawa. Tusibezane, tusikubali kutengana, hapo kama viongozi onyesheni uhodari wenu wa kusuluhishana, kuvumiliana na kujenga hoja zenye tija.
Kama
itashindikiana zaidi, basi hivyo vipengele vigumu, virudishwe kwa wananchi, wananchi
watavipigia kura, ili kila mmoja awajibike navyo, na hilo litaleta uzito zaidi kuwa
kila mmoja kashiriki kikamlifu kwenye katiba yake, hakuna kulaumiana tena, kwani wengi wape.
Ni maoni
yangu tu
2 comments :
Mambo ya siasa na mimi mbali mbali kabisa..tuendelee na kisa chetu m3
Awesome! Its in fact remarkable piece of writing, I have
got much clear idea regarding from this article.
Post a Comment