Binti
aliondoka kwa hasira, baada ya kuongea na baba yake kwenye simu, na kuniacha
nikiwa nimeduwaa, hasa kutokana na kauli yake pale alipokuwa akiwasiliana na
baba yake, kuna maneno yalinifanya nihisi kuwa kuna jambo limetokea huko kwa
baba yake;
‘
Wapi,....kwani wewe upo wapi,?’
‘Lakini ulisema umerudi nyumbani
kijijini,....’
‘Oh, kwanini, kuna nini kimetokea?’
‘Baba ....una uhakika na hilo ...unasema
kuwa wamekugeuka,...akina nani?’
‘Msaliti mkubwa wewe..utaona.....’
‘Msaliti
mkubwa, wewe...’ hivi haya maneno yalikuwa yakielekezwa kwangu,au kuna mtu
mwingine, na huenda alikuwa akielekeza hizo shutuma kwangu, kwa jambo gani
nililolifanya hadi nipewe shutuma hizo, au ni kuhusu mdada labda...
‘Yawezekana
ikawa ni kuhusu mdada, huenda, wamegundua kuna kitu kinaendelea kati yangu mimi
na yeye, au mdada keshatuma hizo picha mbaya kwa huyo mzee, lakini mdada hawezi
kufanya hivyo, sasa ni kwanini niitwe msaliti, labda sio mimi..’ nikawa
najiulza maswali mengi,
‘Ngoja niingie
huko huko ndani nikamsikilize mdada, ni lazima anafahamu ni kitu gani
kinaendelea, ... nahisi kuna tatizo kubwa sana....’nikasema na kurudi kule
kwenye hiyo ofisi ambapo nilimuacha mdada na wakili, na nilipoingia nilimkuta
mdada akiongea na simu
‘Hali yake
inaendelea vipi?’ akauliza mdada kwenye simu, na aliweka spika ya nje, kwahiyo
unasikia huyo mtu wa pili anasema nini, nafikiri alifanya hivyo, ili wakili
wake asikie ni kitu gani wanaongea na huyo mtu mwingine.
‘Hali yake
hadi sasa haijajulikana, kwani aliingizwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi,
ni mshutuko, na inawezekana ikawa ni kiharusi...lakini yote tunasubiri taarifa
ya dakitari..’sauti ikasema.
‘Kwahiyo pia
inaweza ikawa ni mshituko tu, ...na kupoteza fahamu, sio lazima iwe ni
kiharusi, namfahamu sana huyo mzee, ni mtu wa mazoezi, lakini, ooh, binti yake
anafahamu?’ akauliza
‘Sizani kama
anafahamu, maana nilivyosikia alikuwa chumba cha mkutano akiongea na mchumba
wake..kwani hujaonana na huyo binti, kwani anakutafuta sana.’sauti ikasema,na
mdada akamwangalia wakili, hakuniangalia mimi, ni kama vile hakujua
nimeshaingia.
‘Alikuwa
hapa, nimeshaonana naye, sina uhakika kama ameshaondoka,..hebu subiri kidogo....’akasema
alipogeuka na kuniona akaniuliza;
‘Huyo
mwanamke wako yupo wapi?’ akaniuliza
‘Wa nini
tena, ...mwenyewe ulikuwa unashinikiza aondoke, sasa tena unamuhitajia, wa
nini?’ nikamuuliza nikionyesha kutokujali.
‘Baba yake kapatwa
na mshituko, kadondoka na kupoteza fahamu, sasa hivi kakimbizwa hospitalini,
ndio maana nataka kufahamu wapi lipo,...’akasema
‘Unasema,
nani, mzee wake, haiwezekani, wapi hiyo imetokea?’ nikauliza nikionyesha
mshituko na mshangao, na mdada akawa kashikilia ile simu, akaiweka hewani na
kusema;
‘Nitaongea
na wewe baadaye, fuatilia kwa makini, kwani nahisi kazi imekwisha....’akasema
na kuiweka simu yake mezani, akaniangalia na kusema
‘Unauliza
wapi imetokea, huyu mzee, alipatwa na mshituko huo akiwa humu humu kwenye hili
jengo..kwenye ofisi nyingine...’akasema
‘Lakini
nijuavyo mimi, huyu mzee kesharudi kijini...’nikasema
‘Ndio hivyo,
jua hivyo hivyo,..anyway, ni muhimu
kama binti yake hajafahamu ikatafutwa jinsi y kumfahamisha, maana huyo ni mzazi
wake, na hatujui uhimili wake, japokuwa anaonekana mkorofi, je wakili
unasemaje?’ akauliza
‘Kwani
umemuacha wapi huyo binti?’ akauliza huyo wakili
‘Mimi
ninachoshangaa ni kuwa, muda mchache tu, huyo binti alikuwa akiongea na baba
yake, kwenye simu, na sikuweza kufahamu wameongea nini, ila kunaonyesha kuwa
kuna tatizo, yeye alipomaliza kuongea na simu, akaondoka kwa haraka, hakutaka
hata kuniambia lolote.....’nikasema
‘Nahisi alipomaliza
kuongea naye, ndio akapata taarifa zilizomshitua, ...nahisi ndivyo
ilivyotokea,...kakutana na mambo mengi kwa wakati mmoja, ya kifamilia, ya
kikazi, na mambo yake binafsi, akashindwa kuhimili, ..’akasema mdada.
‘Hili sasa linaweza kuathiri mambo mengi, lakini kwa upande wetu, ni nafasi pia ya kujipanga vyema, na ni muhimu kujiandaa kwa lolote lile...’akasema
wakili.
‘Mhh, kweli
linaweza kuharibu mpango wote, hata hivyo, ni jambo gani lililompelekea huyo
mzee kupatwa na mshituko, na muda huo alikuwa akiongea na nani, ni muhimu sana
hilo tukalifahamu...’akasema mdada
‘Huyo mtu
wako hajafahamu zaidi, inabidi umuulize, ili tujue ni nini cha kufanya, ....’akasema
wakili
‘Mhh, kweli safari
hii mzee kapatikana, na ujanja wake wote huo, kashindwa kupambana na kashikashi
za mihamaniko ya dunia, nilishamuambia kuwa hayo anayoyafanya yatampeleka
pabaya, lakini alijiona hawekaniki, sasa...sijui, lakini, jamani mwili wa
binadamu sio mali kitu, kama namuona vile...’akasema mdada kwa sauti ya huruma
‘Kwani
imekuwaje, na kapata taarifa gani mpaka apoteze fahamu?’ nikauliza nikiwa
nahangaika kumpigia mchumba wangu lakini simu yake ilikuwa haipatikani.
‘Hayo na
mengine tutayafahamu baadaye, huna haja ya kumpigia simu mtu, unataka kumpigia
nani?’ akauliza mdada
‘Ni lazima
nifahamu , huyo binti, atakuwa wapi, je keshapaa taarifa....’nikasema
‘Hilo kwa
sasa lisubiri, sisi tuendelee na yetu, maana haya yetu hayasubiri mtu, kesi
bado hajatenguliwa, yaliyopo ni maombi tu, kisheria, bado tuna kesi mahakamani,
na mtu aliyekuwa akiibeba ndio huyo, taabani....’akasema wakili.
‘Ina maana
huyo mzee, ndiye aliyekuwa akinisaidia, mbona mumesema ni nyie...?’ nikauliza
‘Hata kama
ni yeye, lakini ni kutokana na juhudi zetu, na shinikizo zetu, bila sisi yeye
asingelifanya lolote, kwanza alishakuona ni msaliti...’akasema mdada
‘Msaliti,
msaliti wa nini?’ nikauliza nikikumbuka kauli ya mchumba wangu.
‘Kwani hilo
ni siri, yule mzee, ana masikio,yanayosikia kila kitu kinachoendelea, hasa kwa
watu wake muhimu, ana macho yanayoona mbali, kuliko unavyofikiria wewe..sioni
ajabu kulifahamu hivyo, japokuwa yeye mwanzoni alilichukulia kuwa ni sehemu ya
utendaji wangu, kwa kazi aliyonipa.....’akasema
‘Kazi gani
aliyokupa..?’ nikamuuliza
‘Kukuchunguza
wewe....hivi hilo nalo ni swali la kuniuliza,....wewe mwanaume, fahamu kuwa
hadi kufikia hicho cheo, ni kutokana na mimi, taarifa zangu kwao, na kuonyesha
kuwa wewe ni mtu unayeweza hiyo kazi,...labda wapo wengine, mimi sijui, lakini
kwa pendekezo langu, mimi niliona kuwa unafaa.....kwa jinsi wanavyotaka wao....’akasema
‘Mimi
sikuelewi mdada, kwani wewe ni nani kwao, unafanya kazi gani, ..?’ nikamuuliza
‘Hayo
maswali haya maana kwa sasa...mimi ni katibu muhutasi wa kampuni ya bosi wako,
inatosha wewe kufahamu hivyo, mengine ni uchakaramu wa mjini, ukiwa mjanja
hulali njaa, huoni, nilivyokusaidia, ni ujanja wa mdomoni na akili ya
kupangilia maneno, na mengine kidogo...’akasema akijiangalia mwilini
‘Jamani muda
unakwenda, naona tufanya chochote,....kama vipi niachieni nifanay nionavyo ni
vyema kwani kwasasa hata sijui kama mumejiandaa kwa lolote lile...’akasema
wakili
‘Ni kweli,
kwani akili yangu haipo sawa kwa sasa, ni muhimu nikafahamu kama huyo mzee
anaumwa, ili na mimi nikamuone’nikasema
‘Hakuna
aliyesema anaumwa,..na hilo tukio halitakiwi kufahamika, ujue hilo, ...usije
ukakurupuka hapa na kukimbilia huko, sijui wapi, ukasema kauli kama
hiyo....’akasema mdada
‘Kwanini?’
nikauliza
‘Hayo ni
maswala ya kiusalama zaidi, kwanza jiulize kwanini bado yupo hapa, na wewe
unafahamu kuwa yupo huko kijijini, hata mtoto wake, mwenyewe hafahamu
hilo,...huyo sio mwenzako...haya mambo yana utaratibu wake, usije ukaropoka
ovyo...’akasema mdada.
‘Kwahiyo
mnasemaje?’nikauliza
‘Kwanza hapa
kunahitajika vielelezo , kwa mfano huyu mhasibu alifika hapo kwasaabbu
gani,..na aliondoka muda gani, ...kitu ambacho ni muhimu sana, pia kuhusu huyu
mtu mwingine, ni nani,..unajua hili limekuwa kitendawili kwa hawa
wapelelezi.....’akasema
‘Lakini
unahisi ndiye aliyemuua huyo jamaa?’ aakuliza mdada
‘Kwa
asilimia kubwa inaoneka ndiye aliyefanya hivyo,...na akipatikana basi sisi hi
kesi haipo tena...’akasema
‘Kitu
kinachoulizwa na wengi, unajua dunia hii ni kijiji, watu wameshafahamu kuwa
mhasibu amependekezwa kwenye hiyo nafsi, waandishi wanauliza ni kwanini, wakati
yeye ni mshukiwa,... unaona hapo, ndio maana nahisi mzee, alipokabiliwa na haya
maswali akaanza kuzongwa na shinikizo la damu,...’akasema mdada
‘Sizani kama
ni kuhusu hoja hiyo, hata hivyo mzee, yeye hahusiki kwenye uteuzi huo, yeye alipendekeza tu, na kwa vile wanamuamini ndio maana wakalikubali pendekezo lake, mimi nahisi kuna jambo jingine limejificha hapo...lakini, hata hivyo huyu mzee, nahisi ana jambo, mimi simwamini sana, eti wakili, hivi huyu mzee unamuamini
sana?’ akauliza mdada
‘Mimi
namwamini sana, ni mtu aliyefanya kazi yake kwa uhodari, na haat ukiangalia sehemu alizokuwa akifanya kabla ya kustaafu, alikuwa mchapakazi,na ndio
maana serikali inaendelea kumtumia kwenye shughuli mbali mbali, mimi sioni kama ana tatizo....’akasema wakili
‘Yah, ni iwe
hivyo....lakini hisia zangu zinanituma vingine, sijui, ...wakati mwingine,
nahisi ni kwa vile tumechefuana kuhusu binti yake, lakini wakati mwingine,
nahisi kuna jambo limejificha,...na ni lazima nilifahamu....’akasema mdada
‘Ili iweje,
mbona unaingilia kazi za watu,....?’ nikamuliza mdada
‘Kazi za
watu.....nimeshakuambia sisi ni mission town, mambo kama hayo ndiyo yanatufanya
tuishi hapa mjini, tuonekane watu....ni hatari lakini salama...’akasema mdada
akiandika kitu kwenye kitabu chake cha kumbukumbu.
‘Sasa je
vile vielelezo vinavyohitajika kwa mwanasheria mwendesha kwa ajili ya hii kesi
vitapatikana...anavihitajia leo, ili ajirizishe, pili ni kuhusu tukio lenyewe,
ni lazima tuliangalie kwa jicho jingine..’akasema wakili
‘Hivyo
vitapatikana hakuna shida, mimi mtoto wa mjini, wewe nipe muda, hiyo ni kazi
ndogo sana kwangu, ngoja niwasiliane na vijana wangu, nione wamefikia wapi...’akasema
mdada
‘Lakini mimi
naona hiyo ni kazi ya polisi, nakumbuka mlishaniambia hivyo...’nikasema
‘Kwa muda
ule ndivyo ilitakiwa iwe hivyo, lakini kwa hali inavyokwenda ni muhimu na sisi
tujiandae kwa lolote lile, kwani sasa imeshatangazwa hali ya hatari, kila mtu
anajiangalia yeye mwenyewe kwanza, serikali imeshaamuka, ....’akasema mdada
‘Kwani kuna
nini kinachoendelea, unafahamu hadi sasa sijui haya yote ni kwa ajili gani,
hebu nipeni ufununu?’ nikauliza na mdada akamwangalia wakili, na wakili
akasema;
‘Sikiliza
ndugu, hicho cheo ulichopewa, sio bure, kuna watu wana masilahi nacho,na ndicho
kimeleta kizaa zaa, na mambo mengi yameshaanza kuwekwa hadharani, kwa hivi sasa
uwe makini kwa hilo, pili, ni vyema tukajipanga kisheria, hatujui ni kitu gani
kinaendelea mpaka sasa...’akasema mwanasheria
‘Sawa mimi
sina shida, maana kwangu mimi ni sawa tu kiwepo au kisiwepo , mimi tayari nina
kazi yangu, sikufikiria kama nitapewa wadhifa kama huo,na sehemu nyeti kama
hiyo..’nikasema
‘Ni lazima
ukipate, ni muhimu sana...’akasema mdada
‘Kwa hali
ilivyo naona ni hatari, naweza kuambiwa yote yaliyotokea ilikuwa kwa ajili ya
mimi kuipata hiyo kazi, ...sipendi hali kama hiyo, ni bora nifanye kazi yangu
ya kawaida tu, kuliko kufanya kazi ya kuniweka roho juu...’nikasema na mdada
akaniangalia kwa muda halafu akasema
‘Wewe ni
mwanaume, unatakiwa uwe ngangari, usiogope, wakati mwingine, inabidi ufanye
kazi za hatari, ili kuweza kufika mahali fulani, usiogope, kuna watu wengi wapo
nyuma yako, cha msingi ni kutusikiliza..’akasema mdada na kumwangalia wakili
‘Sasa
unaweza kuandika chochote, ili nipate muda wa kufuatilia hivyo vielelezo?’
akamuuliza wakili
‘Kama
mnataka iwe hivyo, niachieni nifanye kazi yangu, ..siunajua mambo yenyewe
yalivyo, natakiwa nikae ni wale watu, niwaweke sawa, baadaye, haat nikiomba
kuoanana na mwendesha amshitaki, inakuwa haina ugumu tena.....’akasema wakili
‘Huyo
mwendesha mashitaka, kama unataka mimi naweza kuonana naye, ila uwe nyuma
yangu, ..nafahamu jinsi gani ya kumpata...’akasema mdada na mimi nikamwangalia
kwa mashaka, kwa jinsi anavyojiamini
‘Unaweza
kufanya hivyo?’ nikauliza na mdada akaniangalia huku akionyesha uso wa
kutabasamu akasema
‘Katika dunia
hii ukijiamini, hakuna kisichowezekana,mimi naweza kuonana na yoyote yule, na
nikaongea naye shida zangu, na mara nyini nafanikiwa,...hilo sina shaka nalo,
cha muhimu ni kuwa na uhakika na hicho ninachotaka kuongea na huyo
mtu....ukweli, uwazi, na kujiamini, vinanisaidia sana...’akasema mdada na mara
simu yake ikalia, akaiangalia na kuipokea
‘Niambie...’akasema
na kuanza kusikiliza kwa muda, bila kusema neno, baadaye akasema
‘Kazi nzuri,
kwahiyo, keshatoka na anaendelea vizuri, ila hatakiwi kuonana na watu,je ni
nani aliongea naye kwa mara ya mwisho?’ akauliza
‘Mpelelezi,
yupi huyo?’ akauliza
NB: Haya
yalitokea na yanaendelea kutokea katika jamii zetu, tuone ni nini kitafuata baada ya hapo, je mhasibu ataipata hiyo kazi, ni kwanini mzee akashikwa na mshituko, na huyo mzee ni nani...
WAZO LA LEO:Dhuluma inaposhika hatamu, haki inapotea,
watendaji wanakuwa wagumu kutimiza wajibu wao, ukiangalia kwa makini sababu kubwa
ni hali ngumu. Wenye nacho wanakuwa
hawatosheki, wanataka zaidi na zaidi,na kujiwekea namna ya kupata zaidi na
zaidi na ili wapate inabidi kuchukua hata kile kidogo cha wasio nacho, haki
inakwenda kwa wasiostahiki...Haki ikipotea, amani haitakuwepo, hata kama
tutajidanganya kwa nguvu za dola.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment