‘Wewe nenda kaoge, leo nitakufungua macho kidogo
tu,...uonge dunia inavyoliwa, kwa mrija, cha muhimu kwa sasa ni muonekano nadhifu,kaoge, ukitoka nguo hizo
hapo,nataka leo uvae itakawavyo na wao, ...kwani huko kuna uvaaji wake,...’akasema
‘Uvaaji wake
kwa vipi?’ nikauliza
‘Kila kitu
kipo tayari, wewe ni kuvaa tu, hizo kwa vipi hazina maana, ukimaliza kuoga,
nguo utazikuta hapo kabatini, mimi nakusubiria nje, kuna mtu nataka kumpigia
simu, fanya haraka kidogo, muda umekwenda, ...nataka leo angalau kidogo uone
starehe za hii dunia ,...’akasema
‘Umesema
huko kuna uvaaji wake, mimi hapo ....’nikaanza kuongea
‘Hebu jail muda
kwanza, kwani unataka kujua nini...?’ akauliza.
‘Mengi tu,
ulishaniambia kuwa nikitaka kujua au kupata mengi, ni mimi nikubali, kila mara
unaniweka hewani, mimi sitapenda kwenda huko mpaka niwe na uhakika nakwenda
wapi na kufanya nini...’nikasema
‘Hahaha,
masikini mhasibu, unafahamu ni kweli, unalozungumza, siwezi kukulaumu,lakini
ukiuchunguza moyo wako ndani, unataka, na kila mmoja anataka kuwa mtu fulani,
au sio...sizani ungelipenda kuwa kama ulivyo, sasa leo nataka nianza kukufunda
kwa vitendo....’akasema
‘Mhh, kwa
vipi?’ nikauliza
‘Kwanza nilishakuambia
kuwa kila mmoja anataka kupata, lakini ili upate, unatakiwa ujitoe, uhangaike,
...na hapa ni pagumu, kuna mitihani yake, kuna kujitoa muhanga, kuna mambo
mengi yanahitajika ili upate jambo, sio kila jambo ni rahisi tu, hasa kupata
mali....mmh, kuna wengine wanafikia kutoa makafara,kujitoa mhanga na vitu kama
hivyo, na ukiangalia nia na lengo ni kupata...’akatulia akiangalia saa yake.
‘Hapa, kwa
hawa watu, wanajinsi ya kumpima mtu, kuna mambo mengo unaweza kukutana nayo, na
hata kuumizwa, na wengine hupoteza maisha kabisa, wakasahaulika,hayo ni kwa
ajili ya kukupima imani yako,je unaweza...’akatulia
‘Mimi
sikuelewi,...ina maana unaniingiza kwenye mambo ya ushirikina?’ nikamuuliza
‘Ni nini
maana ushirikiana?’ akauliza kwa mshangao
‘Mambo kama
hayo ya kafara,...siumesema mwenyewe...’nikasema
‘Hata kwenye
dini kuna kafara, au sio...kafara sio lazima ufanye ushirikina, ni ile hali ya
kujitoa kwa hali yoyote, hata ikibidi kutoa damu...ili kuondoa
vikwazo...wenzako hapa wameiweka hii kafara kisayansi zaidi, siwezi kukuambia
zaidi, lakini cha muhimu ni kuamini kuwa baada ya hapo utapata....’akasema
‘Utapata
nini?’ nikamuuliza nikiwa bado nimesimama na yeye akiwa kasimama akiwa tayari
kuondoka.
‘Kwani watu
wanatafuta nini katika hii dunia..?’ akaniuliza akiniangalia kwa macho ya
kunishangaa
‘Mhh, uhai,
na, ...’nikawa najiuma uma na yeye akasema
‘Ni mali, utajiri,
na maisha bora, au sio?’ akawa kama ananiuliza
‘Yah, ndio
hivyo, inategemea kwa vipi, kwahiyo unataka kusema nini...?’ nikamuuliza nay
eye akaangalia saa , inaonekana nilikuwa nampotezea muda, lakini hapo hapo
hakutaka kunilazimisha kitu ambacho sio kawaida yake, nikahisi kuna kitu muhimu
sana kwangu mimi kuwepo huko.
‘Kwahiyo,?...unaniuliza hapo, ....jibu unalo wewe mwenyewe,
..usingelitoka huko kwenu kijijini kuja kutafuta kazi hapa mjini,..kama hoja ni
maisha tu, hata kijijini yapo, hata kijijinu riziki ipo tu, ungelikaaa huko
huko kijijini ikajipa,au sio, lakini ulihangaika hadi hapa,...unaona hoja
hapo...’akasema
‘Ndio maana
nauliza kwahiyo unataka mimi nifanye nini..?’ nikamuuliza
‘Ninachotaka
wewe kwanza ni kuona, ni kufuta huo utongotongo,ilivyo kihalisia ukiona
utaamini,...na nina uhakika kama una akili yenye kutafakari,utafanikiwa, na
kufanikiwa huko hakutakuja bure bure , maana kila mtu kapewa akili, kila mtu
ana kipaji chake chenye thamani tu tatizo ni kuwa hatujijua..’akasema
‘Mhh, , ...’nikaguna
na yeye akasema
‘Hakuna cha
kuguna hapo, ...kinachohitajika ni kukitafuta kipaji chako, kile chenye
thamani, ukitumie, wewe unajiona una akili ya kuweka mahesabu sawa, au sio?,
lakini inawezekana isiwe ndio kipaji chako, wenzako wana ujuzi wa kukitafuta
kipaji chako,....kitajulikana ukitaka, na kujiunga kwenye kundi, wao
wanakushauri ni nini cha kufanya, watakitumia kipaji chako na wewe mwenyewe
utashangaa,..,’akasema
‘Unapsema
wanzako, hao ni akina nani?’ nikamuuliza na yeye akanitupia jicho na
kutabasamu, akasema;
‘Hayo
maswali yako uwe makini nayo,....’akasema na kutulia kwa muda, halafu akasema
‘Nikuambie
jambo katika hii dunia, kuna watu wapo kwenye makundi mbali mbali, wapo wengi tu
huku na kule,wao wanaamini kuwa ni wanachama wa kundi fulani, wameamini tu, na
wanatumiwa tu, lakini hawajui kuwa wanatumiwa kwa masilahi ya wengine,...
'Kiukweli watu hao wapo kama
bendera kufuata upepo, wanajiita wanachama,
...waulize chama ni nini, kina nini ndani yake, madhumuni yake nk...hawajui
kabisa, lakini wanaamini kuwa ni wanachama....unaona hapo, sasa mimi sitaki uwe
humo kama wao, nataka uwe humo kama mtendaji...’akaniangalia kwa makini na mimi
nikatulia
‘Mtendaji...?’
nikajiuliza na yeye akajifanya kama hakusikia na kusema;
‘Lakini
kwenye vyama, au makundi, ili mambo yaende vyema, ni lazima hao watu wawepo...’akasema
na kuniangalia moja kwa moja usoni, na mimi nikawa nimetulia tu.
‘Ninasemea hao,
bendera fuata upepo, wapiga makofi, wapiga kura,...ili waweze kuwaficha watu
maalumu,maaliwatani, matajiri, ambao kazi yao inaitwa ufadhili, ..’akatabasamu.
‘Hivi kweli mkono
utatoa tu, hakuna kitu kama hicho, mkono utoao ndio unaopewa...hapi ndio hawa
wenzetu walipojikita, wanaitwa wafadhili, lakini mumo ndimo wanapofanyia mambo
yao...ni muhimu sana hapo, nimejifunza mengi hapo....’akatabasamu.
‘Dunia hii
ukiwa na akili, haki ya mungu huwi masikini, ...nakuambia hilo, ukiwa masikini
umetaka mwenyewe,’akatikisa kichwa kama kukubali jambo.
‘Sasa katika
hilo kundi kuna watu wapo tu, wanatumiwa tu, ili neno likamlike, ambalo wengi
wanalifahamu kama demokrasia...,si ndio hivyo?’ akaniuliza
‘Yah, ndio
hivyo...’nikasema
‘Siasa hiyo
bwana, ndio maana kuna kitu kinaitwa ni
nini, wengi wape,...bila kuwa na hao
wengi, hawo watu maalumu hawatapata kitu, watashindwa kufanya mambo
yao...kutokana na hao watu wengi, ndio ufadhili wao unapoonekana,..sasa
kiujumla, ...kila mmoja anatakiwa kufika huko..lakini kwa spidi yake, ...kama wewe utaamua kulala haya...’akasema na
kuniangalia na mimi nikabakia kimiya
‘Utaona kama
ni ndoto fulani ya kufikirika,...lakini mimi nimeifanyia kazi hiyo kivitendo, na matokeo yake mnayaona, ...haya wa kusema ni ndoto waache waendelee hivyo hivyo, hebu niembie ukweli, wewe unanionaje kwa sasa, angalia mwenyewe, hivi sasa,nina nyumba nzuri, nina gari nzuri, ..nina miradi mingi tu,hata
mingine bosi haifahamu ....naanza kupanda daraja, lakini ili ufike huko nahitajika
kumpata mwenza wa kufikia mahala fulani,mwaminifu anayejua kutunza siri, lakini
hayo sio muhimu kwa sasa ....’akatulia
‘Unasema
mwenza, una maana mume au?’ nikamuuliza
‘Mhh, jibu
hilo unalo mwenyewe....’akatulia na kuniangalia kwa makini.
‘Sasa kwenye
nadharia hiyo, ni lazima kuwe na watu, ...wengi tu, wasiojua ni nini
kinachoendelea, lakini ni wanachama, wanaamini hivyo,..ni muhimu kujaza wafuasi
wengii kwa ajili ya kuombea misaada, wengi tu hata kama hawajui nini
kinachoendelea, ilimradi ni washabiki tu, hawa wengine watakuja kusaidia kwenye
kutoa makafara, kwenye kupiga kura,na vitu kama hivyo...geresha-geresha za
namna hiyo, ni, ujanja ujanja,mbinu za aina yake...watu wanalimbikiza,
wanatajirika, huku wewe umelala, ndugu yangu amuka...’akasema.
‘Sikuelewi,.....’
‘Kwasasa
hutanielewa,....utakuja kunielewa tu, ...ila muda ni muhimu sana, kumbuka, hao
ndio wameshikilia file lako la kesi yako,....nakudokezea tu...natumai hapo
utanielewa, ni lazima ukubali huna ujanja, ina maana kweli wewe hutaki kufikia
kwenye kundi la mwenzetu.... mwenzetu ni hatua ya juu sana..
‘Hahahaha, hata
mimi mwenyewe sijafikia huko,.....samahani nimeongea sana, hata nisivyostahili
kukuambia, nenda kaoge...’akainuka na kutoka, na kuniacha hapo chumbani.
Nikabakia nimeduwaa, nikijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu na mara
nikakumbuka usemi wa wakili wa kampuni....
‘Inawezekana upo ndani ya hilo kundi
bila ya wewe mwenyewe kujijua, ukawa unatumiwa, lakini anyway, yote ni wewe tu,
nikuambie ukweli, ni ukweli wako tu, ndio utakaoweza kukuokoa,....’
‘Ukweli wangu...!,ukweli upi huo...’
nikajiuliza
‘Ni ukweli wako tu ndio utakaoweza kukuokoa
vinginevyo, utaniambia...’
Maneno
haya yaliendelea kunirudia kichwani, hadi namaliza kuoga, nikavaa zile nguo
nakuonakana mtu mwingine kabisa...nikatabasamu, na mara mdada akarudi na aliponiona
nimeshavalia, akatabasamu na kusema,...
‘Sasa upo tayari,...chukua mawani haya meusi, hii ni moja
ya alama za kundi...nahisi watakuamini, japokuwa , nina imani wewe bado
hujajiamini....na nakuonya usipokubali, sizani kama watakupa nafasi ya kufikiri
mara mbili, watakufanya kafara .....’akasema
‘Una maana
gani kusema hivyo?’ nikamuuliza
‘Usijali,
...cha muhimu ni kuwa na mimi, na ukubali kuwa mimi ni mtarajiwa wako, vinginevyo, huenda ukawa historia....’akasema
na hapo hapo nikakumbuka yale maneno ya mwisho ya yule wakili;
‘Nikuambie ukweli, ni ukweli wako tu,
ndio utakaoweza kukuokoa,vinginevyo, itabakia historia kuwa kulikuwa na mtu
kama wewe.....’
NB: Naishia
hapa kwa leo
WAZO LA LEO: Kujiamini katika mambo yetu yawe ya
kikazi au maongezi tu, ni muhimu sana, lakini huwezi kujiamini hivi hivi tu, ni vyema kwanza kufahamu ni kitu
gani unachokifanya(kukiongelea), kwa kukisomea au kwa kukifanyia utafiti ,
usiongee kiubishi tu wakati huna rejea zozote za matendo au za maandishi.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Mnyonge mnyongeni lkn mpeni haki yake, unastahili pongezi mkuu, una vitabu vingapi, mbona hakuna tangazo kwenye blog yako?
HONGERA
Kwa kweli uko juu, nitakupa hongera sana, kipaji chako ni cha hali ya juu.
Post a Comment