‘Sasa niambie ukweli ulivyokuwa, niambie kila
kitu, bila kunificha ili nione nitafanya nini.. sijapata taarifa yoyote kutoka
polisi, lakini kuna mtu wangu atanifahamisha, ni nini kinachoendela, na wakati
tunasubiria,..ni vyema nikajua ni kitu gani kilitokea....’akasema wakili huo,
na mara bosi yeye akainuka na kusema;
‘Mimi naona niwaache, nafika ofisini, halafu
nitakuja kujua mumefikia wapi, sijui swala la dhamana, maana kama walivyosema,
hutakaa hapa inabidi aende gerezani, hayo nakuachia wewe wakili,jitahidi
dhamana ipatikane....’akasema
‘Niende gerezani kwa kosa gani, mimi sina
kosa..’nikajitetea
‘Yote inategemea wewe,..... hatujui polisi wana
ushahidi gani na kulitokea nini, kwani wamejitahidi kuficha habari zote, hakuna
anayefahamu kilichotokea ni wewe ambaye ulikuwepo kwenye hilo tukio unaweza
kutuelezea , muelezee wakili,sio mimi...’akasema bosi.
‘Lakini mimi sijui zaidi...nimeshakuambia
bosi..’nikasema
‘Ongea na wakili, ujue yeye ndiye
atakayekusaidia, kauli yako haitasaidia kitu , huenda ukaongea jambo likawa
ndio kitanzi chako....huyo hapo wakili, mimi sina ninaloweza kukusaidia,
usiposhirikiana na wakili wetu huyo, usije ukajilaumu...’akasema bosi.
Mimi nikamwangalia bosi, na alipokuwa
akiondoka, niliona ni kama mzazi, anakuacha baada ya kufanya kosa, na
ulitegemea yeye akusaidia, lakini kumbe hata yeye hana uwezo nalo, nikajua sasa
nijipange kivyangu, hata hivyo, sikuwa tayari kuelezea kila kitu kwa masilahi
yangu binafsi
Bosi alipondoka nikabakia mimi na wakili...nikamwangalia,
akifungua makabrsha yake, na akawa anaandika jambo, kabla haajanza
kunihoji,akachukua simu yake, yenye sehemu ya kurekodi sauti, akaiwasha na
kuiweka mbele yetu, halafu akaniangalia na kusema;
‘Haya kama alivyosema bosi wako, nataka
unieleze kila kitu, na ni vyema, ukaniambia wewe na mdada, wewe na huyo mtoza
ushuru mnafahamiana vipi...kwanza elezea siku hiyo ya tukio ilikuwaje..
Nikamuelezea kwa kifupi kuwa mimi nilifika kwa
mdada na bosi kwa ajili ya kumjulia hali na tukaona kuna umuhimu wa kumsaidia,
kwahiyo tukapanga tukae naye, baadaye bosi akaondoka, na mimi nikabakia na
mgonjwa
‘Wakati bosi wako anaondoka mdada alikuwa
hajaamuka?’ akaniuliza
‘Ndio alikuwa hajaamuka...’nikasema
‘Mhh, alipoondoka bosi wako wewe ulikuwa wapi
muda wote, ulikuwa ndani na mgonjwa au ulikuwa sehemu nyingine?’ akaniuliza
‘Nilikuwa chumba cha maongezi, ambapo tulikuwep
hapo tangu awali, mimi na bosi, na bosi alipoondoka niliendelea kukaa
hapo,...japokuwa mara kwa mara nilikuwa naingia chumbani kwa mdada kuchungulia
kama kaamuka, ...’nikasema
‘Ni muda kama unakumbuka vyema, mdada
alizindukana, kutoka kwenye nguvu za dawa alizopewa,au ulijuaje kuwa kaamuka?’
akaniuliza
‘Kuna muda nilikuwa naongea na simu, ...nahisi
ndio muda alizindukana..’nikasema
‘Kwanini unasema unahisi...?’ akauliza
‘Kwasababu nilipokwenda kama kawaida yangu
kuangalia chumbani kwake, nilikuta hayupo..’nikasema
‘Ulikuta hayupo, una maana gani kusema hivyo?’
akauliza
‘Nilikuwa naongea na simu, nikamaliza, lakini
kuna muda nilihisi kun kitu kimelia, au mtikisiko wa kitu, ndipo nikaenda chumbani
kwake, nikakuta hayupo kitandani, nikajua labda yupo chooni, lakini huko napo
hakuwepo, nilipotoka kwenda chumba chake cha makitaba nikamkuta yupo anaangalia
laptop yake, nahisi kuna kitu alikuwa akifanya....’nikasema
`Ulikuwa ukiongea na nani kwenye simu?’
‘Na hilo natakiwa kuongea, mambo mengine ni ya
kwangu binafsi...’nikasema
‘Kwa hali ilivyo, huna budi kuongea kila kitu
hata kama ni mambo yao binafsi, mimi nitakushauri kuwa hili uongee a hili
usiongee, muda wake ukifika, ...ni muhimu sana ukaniambia kila kitu...’akaniambia
‘Nilikuwa naongea na mchumba wangu...’nikasema
‘Mchumba wako yupo wapi,?’ akaniuliza
‘Yupo huko kijijini...’nikasema
‘Mlikuwa mnaongea nini hasa...maana mdada
aliweza kuamuka, na usiweze kufahamu, huenda alisikia mlichokuwa mkiongea, na
huenda ikawa na sababu ya tukio zima, ndio maana nakuuliza ili niweza kujua
lipi ni lipi ni muhimu kwa wakati kama huu...’akaniambia
‘Alikuwa akinikumbushia kuhusu ahadi yangu ya
ndoa...ni maswala hayo, na mimi nikamwambia nipo kwenye maandalizi,..na
niliposikia huo mlio, au mtikisiko, nikaacha kuongea naye, nikakimbilia
chumbani kwa mdada kuangalia kumtokea nini...’nikasema
‘Wewe na mdada mpoje, kuachia mbali maswala ya
kufanya kazi pamoja, hamna urafiki wa karibu?’ akaniuliza
‘Sio kihivyo...hapana, yeye ni mfanyakazi
mwenzangu tu, ...’nikasema na wakili akaniangalia kwa makini.
‘Ni muhimu ukaniambia ukweli, kwani polisi
watafanya uchunguzi wa nyendo zako, watagundua yote, na mimi usiponiambia
ukweli, nikaongea jambo, ambalo ni tofauti na walivyogundua wao, tutaonekana
sisi ni waongo....unielewe hivyo, ...’akaniambia
‘Ndio hivyo mimi na mdada, ni ukaribu wa kikazi
tu, sina zaidi na yeye....’nikasema nikimkwepa tusiangaliane.
‘Hamjawahi kufanya jambo jingine tofauti na
maswala ya kikasi, mkawa mumeshirikiana wewe na mdada,..?’ akaniuliza
‘Hapana sijawahi kufanya hivyo, mimi na mdada
tunajuana kazini tu, tukitoka kila mtu na lake...’nikasema
‘Una uhakika na hilo?’ akaniuliza.
‘Ndio hivyo kwanini nikufiche....mimi nina
mchumba wangu na kama nilivyosema nilikuwa naongea naye kwa ajili ya maandalizi
ya harusi, ...sina mambo mengine na mdada.
‘Huwa mkitoka kazini hamkutani mahali mkaongea
mkanywa, mkala...?’ akaniuliza
‘Kwa mara chache sana....lakini sio kwa
kuzoeana kiundani , hapana...’nikasema
‘Ujue kila ninachokuuliza kina maana yake,
usitake nije kupata taabu ya kutafute ukweli, ni vyema ukasema ukweli, ili
unirahisishie kazi...ufahamu mimi sifahamu chochote kuhusu wewe na mdada, na
tukio zima, na natakiwa nikitoka hapa nikafanya uchunguzi ...’akasema
‘Uchunguzi wa nini na mimi ninachokuambia ndio
ukweli wenyewe....’nikasema
‘Nikuulize tena, kuacha maswala ya kikazi, wewe
na mdada hamna mambo mengine mnayoshirikiana naye?’ akaniuliza
‘Hakuna...na kwanini mdada, kwani yupo kuna
nini kimetokea kwake, ...hajambo yupo hai...?’ nikajiukuta nauliza maswali
mengi.
‘Majibu yake tutayapata hivi karibuni....cha
msingi kwa sasa nikujua ukweli wa tukio zima, na wewe na mdada mpoje, wewe na
huyo mtu mwingine mnajuana vipi na kulitokea nini siku hiyo ya tukio...’akasema
‘Haya hebu turudi siku hiyo ya tukio,..ulisema
uligundua kuwa mdada yupo chumba cha maktaba, ulipotoka kwenda kumuangalia au
sio?’akauliza
‘Ndio.....’nikasema
‘Alikuwaje, maana huyu mtu alikuwa mgonjwa,na
sasa kaamuka yupo anafanya jambo kwenye laptop yake, ulimuonaje ?’ akaniuliza
‘Alikuwa safi tu, huwezi kutambua kama ni yule
aliyekuwa akiumwa, na ndipo nikamuuliza hali na tukaanza kuongea mambo mengi
tu, ...’nikasema
‘Mliongea nini hasa ...?’ akaniuliza
‘Mambo mengi ya kimaisha kwani yeye ni
mfanyakazi mwenzangu na tumezoeana kwahiyo mnapokutana mnakuwa na mengi ya
kuongea, siwezi kusema kila kitu...’nikasema
‘Sikiliza, ...wewe umeniambia kuwa wewe na
mdada mnajuana kikazi zaidi, sasa hivi unasema kuwa mliongea naye mambo mengi
zaidi ya kimaisha, ...’akasema akikunja uso kuonyesha kuwa ninamficha jambo.
‘Kuongea ni kitu kingine, mnapokuwa ofisini
mnaongea mengi japokuwa hamna mahusiano nje, mkitoka hapo kila mtu na lake...’nikamwambia
‘Uwe makini na kauli zako..hapo moja kwa moja
nimegundua kuwa kuna kitu unanificha,....inaonekana wewe ni mdada mpo zaidi ya
kikazi...’akasema
‘Wewe wasema hivyo, ....kwa mdada ni mwepesi
kumzoea kwasababu ni mcheshi,na nivyo ilivyokuwa kwangu, lakini sio ukaribu
hadi mambo nje ya kazi,....’nikamwambia
‘Mliongea maswala ya kimaisha kama yapi, kuwa
unajenga kuwa una mchumba kuwa kuhusu nini hasa?’ akaniuliza
‘Kama hayo, alitaka kujua mipango yangu ya
kimaisha nikioa,...utani mwingi, ukikutaa na mdada tunaongea mengi kama
tumezoeana sana, lakini sio kihivyo...’nikasema
‘Mkaongea hivyo mpaka saa ngapi, au hamkulala
kabisa mkawa mnaongea tu?’ akaniuliza
‘Hapana tuliongea kwa muda, baadaye akamalizia
kazi zake na yeye akaenda kulala..’nikasema
‘Alipokwenda kulala wewe ukabakia hapo makitaba
au ulikwenda wapi?’ akauliza
‘Nilikwenda chumba kile nilichokuwa awali, hadi
asubuhi, na ndipo...’nikataka kusema akanikatisha
‘Subiri usiende mbio,...’akasema
‘Wakati unaongea na mdada, ni kitu gani hasa
alikuambia anakifanya maana anaumwa na mara kaamuka na kitu cha kwanza ni
kukimbilia laptop yake...?’ akauliza
‘Kwakweli mimi sijui maana nilijaribu kadri
niwezavyo nisimsumbue, au kumuuliza swali litakalomkwanza na kama tulivyoambiwa
na docta, tusimkwaze, kwani akikasrikia, ndio anakuwa sio yeye tena...’nikasema
‘Sio yeye kama vipi anakuwaje, akikasirika..?’
akaniuliza
‘Hayo naomba uje umuulize dakitari wake, ana
nafasi nzuri ya kukuelezea vyema zaidi yangu..’nikasema
‘Ok, sawa nataka unieleze kwa mtizamo wako,
hayo ya kitaalamu sawa, nitamuuliza dakitari lakini wewe unasema akikasirika
anakuwa kama sio yeye, ina maana ulishawahi kuona akiwa hivyo,...ni mara ya
ngapi kuwa hivyo, ...kama ulivyosema anakuwa kama sio yeye...?’ akauliza
‘Mhh, ilitokea mara ya kwanza wakati naongea
naye, nikamuuliza maswali ambayo nahisi hakuyapenda,..yakamkumbusha maisha yake
yaliyopita,..na ndivyo inavyokuwa akikumbuka maisha yake yaliyopita anabadilika
kabisa, anakuwa mtu mwingine tofauti na anaweza kufanya jambo baya....hata...’nikatulia
‘Hata kufanya nini?’ akauliza
‘Hata kujeruhi, kupiga na kufanya lolote
baya....’nikasema na hapo akageuka na kuangalia saa yake, mara simu yake
ikalia, akaiangalia, na kuniambia;
‘Samahani naongea na simu,..na wakati naongea,
hebu jaribu kukumbuka vyema, maana hadi hapo sijapata kitu cha kuweza
kukusaidia wewe...ndio tunaweza kusema mdada alibadilika akafanya
yaliyofanyika, lakini.....’akatulia na kuangalia simu yake ambayo ilikuwa bado
inaendelea kulia
‘Ok, samhani,...’akasema na kuweka simu yake
sikioni na akawa anasikiliza kwa muda, bila kusema kitu, baadaye akasema;
‘Sawa nitakupigia baadaye, ....’akasema na
kunigeukia
‘Sasa mambo yameiva,....’akasema
‘Kwa vipi unasema hivyo?’ nikamuuliza
‘Hii sasa ni kesi ya mauaji..’akasema
‘Mauaji ya nani?’ nikamuuliza nikianza kuhisi
wasiwasi, na shinikizo la damu likaanza kupanda
‘Mtoza ushuru kauwawa...kwa kupigwa
risasi,...na bastola yake mwenyewe, na kwa ushahidi wa alama za vidole, wewe na
mdada mnahusika..’akasema
‘Kwa vipi mimi sikuwahi kuishika hiyo bastola...?’
nikauliza na kujitetea
‘Umeishika..., hizo alama zako za vidole
zingefikaje kwenye hiyo bastola, hapo inabidi uniambie ukweli ulivyokuwa,
ukinificha nitashindwa jinsi gani ya kukusaidia,....’akaniambia.
‘Mimi nilitaka kuichukua, na wakati nataka kufanya
hivyo, nikapigwa na kitu kichwani na kupoteza fahamu, sikuwahi kuishika
kabisa...’nikasema na ndivyo ninavyokumbuka hivyo, nilishangaa kusikia kuwa
alama zangu za vidole zipo kwenye hiyo bastola.
‘Kwa mujibu wa polisi, wao wamepima na kukuta
alama zilizopo kwenye hiyo bastola ni za kwako, na za mdada, na marehemu, hakuna
alama nyingine...’akatulia na kuniangalia.
‘Mimi nina uhakika sikuigusa kabisa...’nikasema
na huyo wakili alionekana haniamini akatikisa kichwa kutokukubaliana na mimi,
akasema;
‘Ni muda wa wewe kuniambia ukweli ilikuwaje,
ukinificha ujue sasa kitanzi, ni chako...mdada atajitetea kuwa ana matatizo ya
akili,..lakini wewe utajitetea vipi, wakati alama za vodole vyako zimeonekana
kwenye hiyo bastola....’akasema na kutulia.
‘Nakuapia ....mimi sikuigusa kabisa hiyo
bastola, sijui kwanini alama za vidole zionekane kwenye hiyo bastola...’nikasema,
na yeye akaniangalia kwa makini, halafu akasema;
‘Mhh, sizani kama kesi hii itakwenda vyema,
naona nimtafaute mtu mwingine, ....ungeniambia ukweli wote, ningekubali
kuishughulikia, lakini naona kabisa unanificha,..sitaki lawama,..’akasema
‘Sasa unataka nikuambie uwongo...’nikasema
halafu yeye akasema;
‘Mimi ninakupa dakika tano za kufikiria,.....kuna
mtu nampigia simu nikimaliza kuongea naye, nataka uniambie kila kitu..vinginevyo,
mimi naosha mikono.’akasema na kusogea pembeni na akawa anampigia mtu simu.
Nikabakia nikijiuliza nifanye nini, maana
nikiongea ukweli, nitakuwa nimharibu kabisa mahusiano yangu na mchumba wangu,
na baba mkwe, hatakuwa radhi na mimi, na mengine ya kwangu na mdada
yatajulikana, yale mapicha mabaya yatatakiwa kama ushahidi....hilo siwezi
kufanya hata siku moja
‘Lakini nisiposema ukweli..itaonekana
nimeshirikiana na mdada kwenye mauaji...kwa hiari yangu, kitu ambacho sio
kweli...sasa nifanye nini.’nikawa najiuliza huku muda ukikimbia kuliko maelezo,
na wakili akawa kamaliza kuongea na simu, akanisogelea na kusema
‘Haya ongea ukweli..ulivyokuwa na mahusiano
yako na mdada....’akasema
NB: Zawadi kidogo ya wikiend
WAZO LA LEO: Usiogope kusema
ukweli,hata kama kwa kusema hivyo,utaumia, ukificha ukweli ukasema uwongo, hata
ukija kusema ukweli tena, uaminifu wako utakuwa umepungua, hutaaminika tena.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment