Kuotakana na afya ya
mume wangu kubadilika, ilinibidi nia nze kufikiria upya yale niliyoyapanga,
kwanza kiubinadamu, halafu kimkataba, na zaidi huyo anayeumwa ni mume wangu.
Lakini hata hivyo, ilinibidi nifikirie zaidi jinsi gani ya kulimaliza hili
tatizo, kwani kama nitaamua kusubiria mpaka mume wangu apone, mambo mengi
yataharibika,...
Hapo nikakumbuka kuwa
wanafamilia wa mareheme Makabrasha walishapanga tukutane, kujadili mustakabali
wa mkataba aliouacha marehemu japokuwa mimi niliwakatalia kuwa siutambui,
lakini kisheria ulikuwa na mantiki, na kuna ndugu yao mwingine ambaye
alishatishia kulipeleke hilo swala mahakamani kuwa marehemu aliacha mkataba
ulidai kuwa yeye alikuwa na hisa kwenye makampuni yangu.
Hili lililozuka sasa
hivi linaweza likawa ni sababu ya kuchelewesha mambo ili mipango iliyopangwa
ifanikiwe, lakini pia inaweza ikawa ni moja ya majaribu tu, kuwa litokee hivyo
na muda kama huo ili lifanyike jamb....na mimi nina msimamo wangu kuwa
likitokea tatizo ni bora kupambana nalo , ni bora kusimama kidete, na
kuhakikisha unakabiliana na hilo tatizo, ...sikukubali kubweteka,au kukimbia
tatizo, sio tabia yangu.
‘Nitapambana na kila
anayejaribu kuingilia maisha yangu...’nikajipa moyo.
Baada ya mume wangu
kufikishwa hospitalini nikarejea nyumbani na kwanza kabisa nilihakikisha kila
kitu kipo kama kawaida, na ule mto na shuka lililotobolewa na risasi
nilivikunja vizuri, na kuvihifadhi mahaal salama, kama vitahistajika
kiushahidi. Hata ile bastola, mimi nilihakikisha siugusi bila soksi ya mkononi,
vyote hivyo nikavihifadhi sehemu salama.
Nilijua kabisa sauti
ya mlio huo wa bastola itakiwa imesikika kwa majirani, na nilishapanga jinsi
gani ya kuwajibu, niliwaambia hakuna tatizo,....sikutaka kuwaambia lolote,
kwani kila kauli utakayotoa, inaweza ikaja kukushitaji baadaye, japokuwa wengi
walipoona mume wangu akitoka na kuelekea hospitali walijua huenda yeye ndio
kaumizwa ...
Dunia haina dogo, hata
mwandishi mmoja wa habari alifika kutaka kujua zaidi nikamwambia hakuna cha
zaidi, hakuna tatizo, na ole wake akiandika mambo ya kizushi...na wananifahamu
hakuna lolote lililoandkwa kwenye magazeti.
Tuendelee na kisa
chetu....
*********
Baada ya mume wangu kukubali kwenda huko hospitalini,
japokuwa hakupendezewa sana, kwani yeye aliona ni tatizo la muda tu, na alihisi
kuwa limekwisha, kwani alivyoamuka alijiskia sio kama alivyokuwa akijiskia jana
yake, na hapo kwa kumjaribu nikamuuliza maswali kama anakumbuka kuna kitu gani
kilitokea usiku yeye alisema hakumbuki lolote, ina anahisi aliota ndoto ambayo
haikumbuki vyema ilikuwaje,
‘Kuna ndoto niliota, lakini sikumbuki ni ndoto
gani,...sikumbuki kabisa, lakini ilikuwa kama ya sio nzuri....’akasema huku
akijaribu kukumbuka
‘Jana hukuwahi kuingia maktaba usiku ukachukua kitu?’
nikamuuliza
‘Hapana, mimi sijaingia huko kabisa, hilo usinidanganye, nakumbuka
nilipotoka matembezi na mdogo wangu, .....wewe mwenyewe ulikuwepo, niliwahi
kwenda kulala,....na sikuamuka tena hadi asubuhi,’akasema akijaribu kukumbuka.
‘Na ulipolala hukuwahi kuamuka kwenda kujisaidia hata mara
moja?’ nikamuuliza
‘Nilala kama gogo, ....sikugeuza hata ubavu, hadi
asubuhi....’akasema.
‘Basi kuna tatizo...’nikasema
‘Kwani kuna nini kimetokea?’ akaniuliza
‘Nakumbuka kama ulitoka nje, ukaenda maktaba...ukachukua
kitu’nikasema
‘Sikuamuka hata mara moja, labda kama uliota, mimi nililala
fofofo...na nilipoamuka nilihisi kama nilikuwa nimeota ndoto ndeefu, lakini
sikumbuki kabisa nilota nini...’akasema
‘Hakuna shida, wewe jitahidi sana kutuliza kichwa....lakini
leo inabidi twend hospitalini wakafanye uchunguzi zaidi’nikasema.
‘Mimi siumwi mke wangu hali kama hiyo walisema inaweza
kutokea , na itapita, usiwe na wasiwasi...’akajitetea.
‘Ulitakiwa mara kwa mara uwe unakwenda kiliniki, hujaenda,
na ukumbuke kuwa uliambia kukitokea jambo lisilo la kawaida pia uende haraka
ukamuona dakitari, na unaona hali uliyo nayo, unapoteza kumbukumbu, unafanya
mambo usiku na hukumbuki kuwa ulifanya, ....ni muhimu tukamuone dakitari, hilo
halina mjadala...’nikasema.
‘Haya mke wangu, kama unaona hivyo ni vyema,
tutakwenda,.....’akasema.
‘Na utakwenda huko ukafanyiwe uchunguzi wa kina, ili tuone
tatizo ni nini, kwahiyo unajiandaa kwenda kukaa huko kwa muda...’nikamwambi na
hapo akashituka na kusema;
‘Hapana, ...siwezi kupoteza muda wangu huko, hakuna tatizo
kubwa kiasi hicho...’akasema.
‘Wewe unasema hivyo, lakini mimi niliyeshuhudia mambo ya
usiku, siwezi kukubali, ni lazima ukafanyiwe uchunguzi wa kina, kwa hiari ,
au...’nikataka kusema neno lakini yeye akakatiza na kusema
‘Sawa mke wangu nimekuelewa, nitakwenda,...nitafanya yote
wanayotaka wao, sitaki mke wangu uishe kwa mashaka, nakupenda sana mke wangu
...’akasema huku akionyesha kutokufurahishwa na uamuzi huo....
‘Ujitahidi sana, kufuata msharti ya dakitari...’nikamwambia
‘Sawa mke wangu, usijali, nitajitahidi sana,....maana nataka
kuondokana na hii hali,...unajua mke wangu niliacha kwenda kiliniki nikijua
kuwa sina tatizo tena,...najua docta atanilaumu sana, lakini ...aah, hata hivyo
najiona nimepona. Mke wangu nataka nipone kabisa tuchape kazi kama zamani.
Tukae tufanya kazi, sitaki nije kuonakana sijui kulea familia yangu...’akasema.
‘Hamna shida, siku ukikumbuka yote yaliyopita ukaniambia
ukweli moja baada ya jingine, ndio nitafahamu kuwa umepona...’nikasema.
‘Kwani sijakuambia kila kitu mke wangu, sizani kama kuna
jambo sijakuambia, eti mke wangu kuna kitu sijakuambia, ...?’akauliza
akiniangalia kwa mshangao
‘Hivyo unaonyesha kuwa hujapona, ukipona utakumbuka kuwa
hujaniambia ukweli wote, na ni muhimu sana kwangu, ni muhimu sana kwa ajili ya
familia hii...’nikasema.
‘Mhh, kweli , hakuna shida...’akasema na tukaondoka kuelekea
hospitalini.
*********
Mume wangu alipofikishwa hospitalini, na kuanzwa kuulizwa
maswali mengi nikiwepo , lakini alionekana kutokukumbuka mambo mengi ya nyuma,
na hata kilichotokea usiku hakuwa anakifahamu, na baadaye nikakaa mimi na docta
tu, muda huo mume wangu alishachukuliwa kwenye chumba cha uchunguzi, tukawa
tunaongea na huyo docta.
‘Hebu niambie kuna kitu gani kigeni kimetokea kwa mume
wako?’ akaniuliza
‘Kwanza namuona kabadilika kabisa sio yule mume wangu
ninayemfahamu, sasa sijui ni kwasababu ya hayo matatizo au anaiigiza, maana
simuelewi,..., kitabia, na hata matendo yake ni tofauti na zamani, na zaidi
anakuwa msahaulivu,...’nikasema
‘Hiyo ni kawaida...nionavyo mimi ni kwasababu ya hilo
tatizo,...na ushukuru kuwa yeye haikumuathiri sana, ....na hali yake sio
mbaya,....yanayotokea ni matatizo ya kawaida tu. Nina uhakika kuwa akitoka hapa
safari hii hali itakuwa njema kabisa,...Je kuna jingine lolote uliloligudua
ambalo hakuwa nalo kabla?’ akaniuliza na mimi nikatulia kidogo akili ikiogopa
kusema tukio la jana, sikutaka lijulikane na watu wengi, nikasema;
‘Eti docta kuna mtu anaweza kuamuka usiku akafanya kitu na
akiamuka asubuhi hakumbuki kabisa?’ nikamuuliza
‘Kwa vipi, anaamuka akiwa na fahamu zake, au anakuwa amelala,
....maana kuna ugonjwa wa namna hiyo, lakini mtu wa namna hiyo anakuwa amelala,
anaamuka akiwa usingizinini, na kutenda matendo ukiwa usingizini,..hajijui
hapo, ....’akasema.
‘Kwahiyo anakuwa kwnye ndoto, lakini tofauti ya ndoto yake
na ndoto za kawaida ni kuwa, yeye anatenda yale matendo kivitendo, ....’akasema.
‘Na hili linatokea kutokana na hiyo ajali yake?’ nikauliza
‘Ndio inaweza ikawa
hiyo ni sababu, maana ubongo ni kitu, makini sana, kikipata mtikisiko wa namna
kama hiyo ya ajali, unaweza ukaharibu mfumo mzima wa mwili, akili, ikawa sio
yako tena, ndio maana unakuta watu wanapooza viuongo, wanapoteza kumbukumbu na
wengine wanaharibikiwa kabisa...’akasema.
‘Lakini pia tatizo kama hilo linaweza kuwa ni la kurithi, huenda
familia hiyo kuna mtu mwenye tatizo kama hilo, baba,mama, au wazee wao, lakini
hili la mume wako, litakwisha tu maana kwa silimia kubwa tunaona ni kutokana na
hiyo ajali iliyomkuta, na kama ni la kizalia ndio limejitokeza sasa, tutajua
jinsi gani ya kulidhibiti..’akasema
‘Kwahiyo anaweza hata kufanya mambo mabaya bila kukusudia?’
nikamuuliza
‘Ndio... wengine wanafiki hata kuua, ukisoma visa vingu,
huko Ulaya imetokea, hata hapa kwetu, tatizo huku kwetu hatuna kumbukumbu,
lakini mambo kama hayo hutokea ...’akasema
‘Oh, sasa utawezaje kuishi na mtu kama huyo?’ nikauliza
‘Cha muhimu ni kufahamu chanzo cha matatizo hayo, je ni ya
kuzaliwa nayo, kwenye ukoo wao kulikuwa na kitu kama hicho, au ni kutokana na
majanga kama haya ya ajali,...baada ya hapo kuna utaratibu wa matibabu,....je
mume wako amekuwa na tabia kama hizo?’ akauliza
‘Nahisi ndio hivyo..jana alitoka kitandani akaenda sehemu
nyingine, akafanya matendo , na akarudi na bahati mimi nilikuwa sijui ,
nikamshitua, akadondoka akapoteza fahamu...sio kupoteza fahamu , ila alionekana
kama kalala tena,...pale alipodondoka...’nikamwambia.
‘Mtu wa namna hiyo haitakiwi kumshitua,ukimuona anafanya
hivyo, unatakiwa umfuatilie tu kimiya kimiya, ili kuhakikisha usalama wake,
kwani atafanya kila kitu anachotaka kufanya na baadaye anarudi kulala kama
kawaida, ukimshitua, unaweza ukamsababishai madhara mengine...’akasema.
‘Oh, ...sasa kama ni hivyo, mbona inanitisha docta....’nikasema
‘Usiwe na wasiwasi, mimi matatizo hayo nayafahamu sana, ndio
ujuzi wangu, hilo tutaliangalia kwa makini, kuna jinsi ya kumpima, na
tutagundua ukweli zaidi, usiwe na hofu, ..kama ni kutokana na ajali litakwisha
lakini kama ni kutokana na kizalia, tutaweza kuliangalai kwa namna nyingine
zaidi...mara nyingi tatizo hilo linahitajia muda sana kulitatua, hasa kama ni
la kizalia, na wewe mke utakuwa na kazi ya kutusaidia, ili tujue hatua kwa
hatua maendeleo yake, kwa hivi sasa tunahitajia tukae naye, tumchunguze, tuone
tatizo lipo wapi zaidi...’akasema
‘Mhh, sijui kama ni kizalia,....maana haijawahi kutokea
hivyo kabla, labda kwa vile sikuwa makini na hali kama hiyo..’nikasema.
‘Basi hiyo kazi tuachie sisi, tunafahamu jinsi gani ya
kugundua,lakini hata hivyo ningelihitajia niongee na watu wake wa asili, kuna
ndugu yake yoyote wa kuzaliwa naye, baba au mama ninaweza kuongea nao kidogo,
kwani hilo linaweza kutupunguzia muda, kama hakuna tutajua jinsi gani ya
kuligundua kitaalamu zaidi?’ akaniuliza
‘Yupo mdogo wake lakini sizani kama anafahamu lolote kuhusu
historia zao, mimi nahisi kuwa tatizo hilo limetokana na ajali....’nikasema.
‘Kama limetokana na ajali lingejitokeza mapema,tungeliligundua
siku za mwanzoni kwenye uchunguzi wetu...hata hivyo, kwa vile yupo kwenye
mikono yetu, tutaliangalia kwa mapana yake, usijali....’akasema
‘Sawa docta nitafurahi kama nitapata taarifa zake, na ni
kitu gani mumekigundua, kama ikiwezekana mapema zaidi, kama itawezekana,
vinginevyo, mimi nawategemea nyie ...’nikasema.
‘Hamna shida tutawasiliana...karibu sana..’akasema na mimi
nikaondoka kurudi nyumbani baada ya mume wangu kuingizwa kwenye wodi maalumu ya
watu kama yeye, na tuliagana, na akaniambia;
‘Mke wangu usijali, sina tatizo, na usiwe na haja ya kuja
mara kwa mara kuniangalia, mdogo wangu anatosha, yeye nitakuwa nikimtumia kama
nitahitaji kitu, wewe hangaika na familia na kazi zetu, ili mambo yasisimame...’akasema
‘Hamna shida...wewe angalia afya yako, hakikisha unafuata
masharti ya dakitari, usije ukatoroka..’nikasema
‘Kwanini nitoroke,...sijawahi kutoroka hospitalini, mimi sio
kichaa, au mfungwa,...nimekuja hapa kwa hiari yangu mwenyewe, na nitafuata kial
kitu, usiwe na wasiwasi na mimi...’akasema
‘Sawa kila-laheri...’nikasema na kuagana naye, nikaondoka
hapo hospitalini.
********
Niliondoka hapo hospitalini nikiwa sijui nifanye nini, niliona
mambo yanazidi kuongezeka badala ya kupungua, sikutarajia kabisa kuwa hali kama
hiyo itakuja kujitokeza , na kwa hali kama hiyo inabidi nishindwe kuchukua
uamuzi mwingine ,nikakumbuka mkataba wetu wa awali kuwa mmoja akiumwa hata kama
kuna kosa au tatizo kubwa, taizo hilo, au kosa hilo linasahaulika kwa muda
mpaka mmoja apone ....
Nikarudi nyumbani, na kumuita fundi ambaye nilimuagiza
abadili vitasa vyote vya makabati, ....nikasimamia hilo zoezi mpaka likamalizika,
halafu nikahakikisha kuwa kila kitu kipo sawa, sikutaka kuangalia ndani ya
makabati, japokuwa nilikuwa nataka kupitia pitia kabati la mume wangu, lakini
nikaona huo sio wakati muafaka, kwani nilijua hakuna kitu cha zaidi ndani ya kabati
hilo.
Wakati nataka kuelekea bustanini , kwani napenda sana
kupumzika kwenye bustani yangu, mara akafika, mdogo wa mume wangu, alionekana kuwa
na haraka, alisema kaja kuchukua baadhi ya vitu vyake alivyokuwa akivifanyia
kazi usiku, huwa ana kazi zake anazozifanya, hata kama hayupo ofisini, nikamwambia hakuna shida mimi nipo bustanini,
akitaka kuondoka aniambie.
‘Sawa, na kuna vitu kaka kaniagiza,nija kuvichukua
....’akasema
‘Sawa wewe mchukulia,mimi nipo bustanini, ukimaliza uje,
nataka tuongee kidogo kabla hujaondoka....’nikasema.
‘Sawa lakini nina haraka kwani kaka anahitaji hivyo vitu
vyake haraka, kaniambia nisichelewe...’akasema na mimi sikumjibu kitu nikijua
ananikwepa tu, lakini nilishajua wapi pa kumpatia, na nilipanga kuwa akitoka tu
nitambana kwa maswali muhimu,...nikaelekea bustanini na kumsubiria.
Baadaye alikuja bustanini, na kuniambia anataka kuondoka, na
alionekana kama ana wasi wasi fulani, nikamuuliza keshachukua hivyo vitu
alivyomuagiza kaka yake;
‘Ndio, lakini kuna kitu kaniagiza kaka, ...sasa kabati lake
halifunguki..’akasema.
‘Kabati gani hilo?’ nikamuuliza
‘Basi hakuna shida, ....labda ufungua sio wa kwake,
lakini...’akasema akiangalia ufungua aliokuwa nao mkononi.
‘Hivyo vitu vipo wapi, kwenye kabati lipi?’ nikamuuliza
‘Kwenye kabati lake ....la ...la ndani kule maktaba kwenu...’akasema
huku akiwa na wasiwasi
‘Ina maana umeingia chumbani kwangu bila kuniambia kwanini
usingelianiambia nikaenda kukuchukulia, ni kitu gani unakihitajia ?’
nikamuuliza
‘Mhh, niliona nisikusumbue, niliingia mara moja, kwenye
kabati la kaka, kanipa ufungua wake, kaniagiza yeye mwenyewe nikamchukulia
baadhi ya makaratasi yake ya kazini.... ’akasema
‘Makaratasi gani ya kazini, wakati dakitari kasema
hahitajiki kujishughulisha na jambo lolote la kumfikisrisha, hebu niambia ni
kitu gani alichokutuma,....kwanini hakuniambia mimi, wewe unamua kuingia kweye chumba
change hadi mkaitaba bila ya mimi kujua, ...ni taratibu gani hizo, na hiyo
tabia umeanza lini, ina maana kaka yako alikutuma hivyo, kuwa usiniambie?’ nikamuuliza
nikaona anasita sita, halafu akasema.
‘Lakini kaka ndiye kaniagiza nikamchukulie...’akasema
‘Akakuambia kuwa uingie bila kuniambia mimi, ?’ nikamuuliza
‘Lakini nilikuambia kuwa kuna vitu vya kaka anavihitajia
ukaniambie nikachukue tu...’akasema, na mimi nikaona nisiendelee na hayo
malumbano, nikaona nimuingie kwa njia nyingine.
‘Hebu niambie jana mlipoondoka na kaka yako mliongea nini?’
nikamuuliza
‘Mambo ya kawaida tu ya kimaisha’akasema huku akionyesha
kutaka kuondoka, na mimi sikujali nikaendelea kumuuliza
‘Kama yapi....nakuuliza hivyo, kwani unakumbuka jana
ulisikia mlio..’nikasema nay eye kusikia hivyo akageuka kuniangalia mara moja,
na kutulia kidogo halafu akasema;
‘Ndio hivi ilikuwa ni nini, maana nilisikia kama mlio wa
bunduki, au bastola, kuna muda nimemuliza kaka, yeye anasema hajui kama kuna
kitu kama hicho kilitokea’akasema
‘Yote hayo alifanya kaka yako, ..ndio maana nataka kufahamu
jana mliongea nini’nikasema na yeye akaniangalia kwa mashaka, na kusema;
‘Tulichongea ni mambo ya kawaida, aakitaka kujua maendeleo
yangu, na akawa anaelezea mipangilio yake kuwa yeye anataka kufanya bidii zaidi
katika kampuni zake na kuhakikisha kuwa uzalishaji unakwenda juu,
na kuhakikisha familia yake inakuwa vyema...’akasema
‘Kakuambia kampuni
zake, kwani yeye ana kampuni ngapi, na kwanini akuambie hivyo ina maana
huko nyuma mambo yalikuwa hayaendi vyema?’ nikauuliza
‘Anasema huko nyuma, alikuwa hajajitambua kuwa ana majukumu
makubwa, kiasi hicho, sasa hivi kajitambua kuwa ana majukumu makubwa kama baba
wa familia, kama mtendaji mkubwa wa makampuni yake, kwahiyo ianbidi abadilike, hataki
kuja kulaumiwa...’akasema
‘Je mliongea kuhusu mkataba?’ nikauliza na hapo akashituka
na kugeuka kuangalia sehemu nyingine, nikahisi hapo kuna jambo, kwanini
nilipotaka mkataba ameonekana kama kutahayari.
‘Umenisikia swali langu, nililokuuliza...?’ nikasema.
‘Sijui unazungumzia mkataba gani, maana sielewi mambo yenu
na kaka’akasema
‘Una uhakika na hilo, ...kuwa huelewi lolote kuhusu mkataba,
wakati jana niliongea na kaka yako akaniambia yote, kuwa wewe unafahamu
...’nikasema
‘Kaka alisema hivyo?’ akauliza kwa mshangao
‘Ndio, ...sasa niambi ukweli, jana mlipokwenda na kaka yako
hamkuongea lolote kuhusu mkataba, maana kama kakuambia kuhusi makampuni yake,
huenda kafungua kampuni nyingine mimi siijui, huenda hayo yapo kwenye mkataba
uliotengenezwa kimagendo,?’ nikamuuliza
‘Lakini shemeji umesema, kuwa mliongea na kaka kama mliongea
naye kwanini unaniuliza mimi tena, na shemeji ni vyema hayo mambo ukasubiri
kaka apone ili muongee naye vyema, ukiniuliza mimi unaniingiza kwenye mambo
yenu ya ndani, ambayo sistahili kuwepo,....’akajitetea
‘Kama ni mambo ya kifamilia, kama ni mambo yetu ya ndani
kwanini kaka yako anakutuma wewe mambo ambayo unajua ni kifamilia na unakubali,
wewe unayafanya tena kwa siri bila ya mimi kufahamu, na kwanini wewe uwepo
kwenye huo mkataba usifahamu kuhusu huo mkataba,halafu kwanini kaka yako akakuambia mkaongee naye huko
mlipokwenda , na kwanini anakuita Jembe?’ nikamuuliza na y eye hapo akawa kama
hataki kusema lolote,akaniangalia mara moja na kusema;
‘Shemeji naomba unielewe, nafanya hayo kwa vile kaka
ananituma, na mimi kama mdogo wake, ninawajibika kumtii, lakini ...sina haja ya kuingilia mambo yenu ya ndani, sitaki
kabisa kufanya jambo ambalo wewe litakuumiza, lakini pia sitaki kufanya jambo
ambalo litamuumiza kaka yangu, wakati mwingine nafanya ili kaka asije
akaathirika kutokana na kuumwa kwake,,..na yeye kama kaka anafahamu mipaak
yake, nay a kwangu, akinituma na kuniambia jambp la lifamilia anafahamu ni nini
anachokifanya, zaidi muulize yeye....’akasema
‘Hebu niambie ni jambo gani ulilofanya kwa vile kaka kakuambia,
lakini wewe hukulitaka kulifanya umelifanya ili kaka yako asije akaathirika?’
nikamuuliza na hapo akatulia kimiya, nikaona nisimpotezee muda .
‘Kuna kitu nataka nikuonyeshe na kama usiponiambia kile
ninachokuuliza inabidi niwaite polisi, maana naona wewe unashirikiana na watu
nje kuja kunifisdi...’nikasema
‘Shemeji , mimi sikuelewi, toka lini nikafanya
hivyo....’akasema
Nikachukua ile mashine ya kuchukua kanda ya video nikaweka
sehemu ambayo anaweza kuona, akaona jinsi kaka yake alivyofanya jana usiku...
‘Oh shemeji....mbona, ...oh, inaonyesha anampiga mtu,
...mbona ....’akawa hamalizii
‘Kwahiyo mlipanga kuwa mje mniue usiku,....ndio maana
uliponiona asubuhi ulionyesha kushangaa, au unajifanay hujui alichokifanya kaka
yako...?’ nikamuuliza
‘Shemeji hapana, hatujapanga hivyo, na wala sielewi kwanini
kaka alifanya hivyo....kwanini tupange kuku-ua, ’akalalamika huku akishika
kichwa akionyesha masikitiko.
‘Sasa mimi nimeamua, kwa vile kaka yako ni mgonjwa, lakini
wewe ni mzima, unaweza kuisaidia polisi kupata ukweli wa haya, kwahiyo mimi
nimeonelea niwaite polisi, wakija utawaelezea vyema, kwanini kaka yako alitaka
kuniua, kama ni ugonjwa, wao watakuwa na kmbukumbu, na ninachojiuliza ni kwanini
yeye akutaje wakati anafanya hicho kitendo, inaonyesha kuwa mliliongelea, na
huenda wewe ulikuwa karibu ukisikilizia hayo aliyokuwa akiyatenda...’nikasema
‘Shemeji sio kweli, ..mimi jana nilikuwa nimelala ,
nilichelewa kulala kidogo kwani kulikuwa na kazi nazifanya, na hata usingizi
ukanishika kwa haraka, nilikuja kuamushwa na mlio wa bunduki, sikujua kabisa ni
nini kimetokea, na nilipoamuka ndio nikakimbilia kuja kuwaona, mimi nahisi kaka
aliyafanya hayo bila kujijua,.....’akasema
‘Bila kujijua ehe,? ...., huoni anafanya waziwazi anaongea,
anakutaja wewe,wewe unasema anafanya bila kukusudia...na huyo mwanamke aliyezaa
naye ni nani, umesikia akisema kuna mwanamke wake, anampenda, ni nani huyo
mwanamke?’nikamuuliza.
‘Mimi simjui huyo mwanamke, ...naona alikuwa anaongea tu kama mtu aliyechanganyikiwa...huoni
hata sauti yake inasikika kama mtu aliyelewa, kama teja, kama mtu yupo
usingizini....’akasema.
‘Kila kitu nikikuuliza mimi unasema hujui, unasahau kabisa
mimi ni nani kwako, na ni jinsi gani nilivyojitahidi kuhakikisha umefika ahpo
ulipofika, ...sasa huenda na mimi natakiwa kufanya jambo ili niheshimike,
uniheshimu kama mke wa akka yako, ..au unaiona kuwa mimi ni mjinga wenu,
fadhila zangu ndio malipo yake haya, na sasa mnataka kuchukua kila kitu, kuniua
eeh, kabla sijafa, mtakufa nyie, na hamtachukua chochote, mtarudi kama
mlivyokuja, ...lakini kama utaniambai ukweli, mimi ni biandamu nitaangalai
jinsi gani ya kufanya...’nikasema
‘Hapana shemeji sio hivyo , kaka anakupenda sana
asingeliweza kufanya kitu kama hicho akiwa sawasawa, mimi nahisi kafanya hivyo,
kutokana na kuchanganyikiwa...na unataka nikuambia kitu gani..mimi sijui zaidi
ya hayo, msubiri kaka utamuuliza’akasema
‘Ngoja niwaite polisi, wakija utaongea nao hivyo, kwasababu
sasa mimi siiwaelewi, kuna kitu mnataka kunifanyia, na nisipojihami mapema mtanimaliza......wewe
utaweleza yote jinsi gani unavyofahamu
wewe, kwa ajil ya kumbukumbu, unasikia....’nikasema.
‘Shemeji, acha usiwapigie, subiri nikuambie, ...usifanye hivyo..’ akasema na mimi nikawa tayari
nimeshampigia simu ofisa mmoja wa upelelezi ninayemfahamu..
NB: Je ndio imekuwa hayo.
WAZO LA LEO:
Matatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu, kila mtu ana matatizo yake, na
huenda wewe kutokana na matatizo uliyo nayo unaweza kufikia kusema yako ni
zaidi ya wengine, sio kweli, kuna watu wa matatizo zaidi na zaidi,..kuna
matajiri na utajiri wao, lakini ukiingia kwenye nafsi zao hawana raha.
Hebu
mwangalie jirani yako, maisha yale yalivyo, huenda ni duni na ana shida zaidi yako, ana matatizo makubwa kuliko yako kwako,hebu
mwangalie yule ambaye ana mapungufu fulani mwilini, wengine hawana miguu,
mikono, wamepooza...lakini bado mungu anawalia waanishi, sembuse wewe uliye
mkamilifu, .Cha muhimu usikate tamaa, jitahidi, ukijua kuwa yote ni maisha.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment