Nilipomaliza kuongea
na mdogo wa mume wangu, akili yangu ilikuwa kama imepandikizwa hasira fulani,
nilitaka niongee , nifoke, kama vile nipo ofisini na wafanyakazi wangu, lakini
haikuwa rahisi , kwani nilikuwa kwenye kifungo maalumu,..kifungo cha kuwajibika
kwa mume.
Kutokana na hiyo hali, ya hasira, iliyotokana nay ale maelezo ya
mdogo wa mume wangu, sikuwa na akili ya kuangalai kushoto au kulia, kwani kama
ningeliangalia sehemu zote hizo, huenda ningelimuona mume wangu akiwa na yule
msaidizi wangu,...Mimi nilipotoka pale bustanini, niliharakisha kuingia ndani, na
kujipweteka kwenye sofa.
Wakati nipo kwenye
sofa, nikijaribu kupotezea, japokuwa haikuwezekana, maana yale maeno ya shemeji
yangu yalikuwa yakijirudia rudia kichwani, hadi ikafikia hatua ya kujiuliza ni
wapi nilipokosea, ina maana wema wangu wote niliofanya kwa wenzangu kwa nia
njema, haukuwa na maana, kilichokuwa na maana ni hayo wanayoyataka wao....
Ni wakati huo nikiwa
kwenye lindi la mawazo, ndipo, nikasikia sauti nje, ilikuwa sauti ya watu
waliokuwa wakiongea, na walikuwa wanakaribia mlangoni. Wazo la kwanza lilikuwa
kwenda kuhakikisha kama mue wangu amelala, au ameshaamuka, ....lakini kitu
kikaniambia nichungulie kwanza nje, na nilipochungulia nje kwa kupitia kwenye
dirisha ndipo nikagundua kuwa kumbe mume wangu alikuwa nje, kumbe alikuwa
ameshaamuka, na alikuwa na msaidizi wangu,na kama ilivyo kawaida yake, alipoamuka
alitaka kwenda nje, azungshwe zungushwe na kigari chake huku na kule.
Nilipoona hivyo, wazo
likanijia kuwa huenda walitoka muda mrefu, na wakafika hadi kule bustanini,
wakatuona tukiongea na shemeji yangu, ...na hapo nikakumbuka kuwa kuna kipindi
nilipokuwa nikiongea na shemeji yangu, nilimuona shemeji yangu huyo akiangalia nyuma
yangu, kwa macho yaliyokuwa yakiashiria kuna kitu alikuwa akiangalia kwa nyuma
yangu, lakini mimi nilizarau na kuzania ni ile tabia ya shemeji yangu ya
kunionea aibu..huenda muda huo, ndio aliwaona mume wangu na mfanyakazi wangu
wakitembea.
‘Kwanini shemeji yangu
hakunishitua...?’ nikajiuliza.
‘Au hakuwaona, au
aliwaona wakiwa wameshasikia kile tulichokuwa tukiongea...?’ nikaona nisiumize
kichwa, nikafungua mlango na hapo nikakutana na mume wangu, akiwa kabadilika
usoni, kwanza akaonyesha uso wa huzuni, akihuzunika kuhusu mdogo wake, na pili
akakunja uso, akijua kuwa huenda tulikuwa tukisigishana na mdogo wake hasa pale
aliponiuliza;
‘Mdogo wangu kakukosea
nini..’
Tuendelee na kisa chetu.
Kauli hiyo ilinifanya nishikwe na butwaa,na kuduwaa kidogo,
na mume wangu akauliza tena.
‘Mdogo wangu kakukosea nini..’
Aliporudia hilo swali, kwa sauti ya hasira mimi
nikamuashiria yule msaidizi wangu aondoke, nikasoegea mbele ya kile kigari-kiti
na kuchuchumaa mbele ya mume wangu, nikaweka mikono yangu kwenye mapaja ya mume
wangu na kusema.
‘Oh mume wangu
sikujua kuwa umeamuka, kwanini hukumwambia msaidizi wangu aniite nije nikutoe
mwenyewe nje, unafahamu nipo likizo kwa ajili yako...’nikasema.
‘Nimekuuliza swali na unakwepa kunijibu, hufahamu jinsi gani
nilivyojisikia nilivyoona mdogo wangu kapiga magoti mbele yako...’akasema na
hapo nikshituka na haraka haraka akili yangu ikajiweka sawa na kumwambia
‘Oh,kumbe mume wangu ulituona, nilikuwa nataniana na shemeji
yangu, nilikuwa namtishia kwa kumtania kuwa kuja kwake hapa nyumbani nikiwa
kazini, kuna ajenda ya siri, ...’nikasema
‘Ajenda gani ya siri...?’ akaniuliza akiwa ananiangalia kwa
macho yaliyojaa hasira.
‘Nilimtania kuwa huenda alikuwa akija kumsumbua mfanyakazi
wetu wa ndani...na kwambia kama ni hivyo nitakuambia halafu itakuwa mwisho
wake...nilimwambia kwa utani tu,..ndio akanipigia mgoti kusema hajafanya, na
nisije kukuambia lolote, maana anaogopa usije ukaumiza moyo wako kwa kitu
ambacho hajakifanya....’nikasema na hapo nikaona uso wa mume wangu ukibadilika,
kutoka kwenye hasira, hadi kwenye kutabasamu;
‘Na wewe bwana, mimi nilishapaniki, maana nimjuavyo bwana
mdogo, sio mwepesi kiasi hicho, cha kumpigia mtu magoti na kumuomba msamaha,
nikajua kuna jambo kubwa sana, ambalo mdogo wangu aliona bila kufanya hivyo
hatasamehewa....ni hivyo tu mke wangu au unanivunga?’akaniuliza.
‘Ndio hivyo tu mume wangu, kwani huniamini...?’ nikamuuliza
na kabla hajajibu nikasema;
‘Au wewe ulikuwa unahisi ni jambo gani, ambalo
ningelimfanyia shemeji yangu hadi anipigie magoti?’ nikamuuliza na kabla
hajasema neno nikaendelea kuongea;
‘Mume wangu, ukumbuke yeye namuona kama mdogo wangu, kama
ulivyooona tumekuwa tukijitahidi kwa pamoja kumjenga katika njia njema,ya
kumbadili kutoka kwenye tabia ya utegemezi kwenda kwenye tabia ya kuweza kuishi
mwenyewe, na hilo tumefanikiwa...’nikasema.
‘Ni kweli mke wangu, na inabidi nikushukuru sana kwa wema
wako huo, kama ingelikuwa ni mimi mwenyewe ningelishakata tamaa, maana bwana
mdogo alikuwa keshadekezwa na mama,maana yeye ni kipenzi cha mama, na wao
walifikiria kwa kmfanyia hivyo ndio wanampenda,wakawa wanamdekeza, kumbe
wanamharibu tusingelimwahi mapema, angeshajiunga na hayo makundi ya kuuza
madawa ya kulevya....’akasema.
‘Ni kweli mume wangu, hilo ni kosa wanalofanya wazazi wengi,
ambao kwa kuwadekeza watoto wao ndio wanafikiria kuwa ndio mapenzi kwa mtoto,
kumbe ni kinyume chake, wanawaharibia maisha watoto wao bila kujitambua, huko
sio kupenda, ....hakikisha mtoto unamlea katika hali ambayo ukiondoka leo
ataweza kusimama peke yake, unahakikisha anawajibika ipasavyo, kuanzia asubuhi
mpaka jioni, na wao wanafnaya kazi...fanya hivyo hata kama mtoto ataona
humpendi, lakini baadaye atakukumbuka...’nikasema.
‘Ndio maana naona hawa mabinti unavyowafanyiza kazi ,
utafikiria wazazi wao hawana uwezo, ina maana gani sasa kuweka wafanyakazi wa
ndani, kama kila kazi unataka na wao wafanye, mimi wakati mwingine naona kama
umezidi kuwatumikisha watoto wetu, huoni kama unawatesa?’ akaniuliza.
‘Hivyo ndivyo watoto wanatakiwa kuwa,hata kama kuna
wafanyakazi, wafanyakazi pia na wao ni sehemu ya familia, sio watumwa,
wanasaidiana, na niliwaambia wawe wanawaelekeza watoto wetu kazi, ili na wao
wafanye, hii itawasaidia kuwajenga kiakili, wanajua kuwa na wao wanawajibika,
ili kesho na kesho kuwa, kama hatupo....wanaweza kufanya kila kitu wenyewe. Kumbuke
haya yote ni ya kupita,leo tumatajiri kesho tunaweza kuamuka masikini, kwa maisha
haya tuliowajengea watoto wetu, wanaweza kuishi bila shida....na ndivyo
nilivyojitahidi kumfanyia shemeji yangu, alivyokuja hapa, kama tungemlegezea,
angejiunga na wavuta unga....nilishamuona ndio maana nikawa mkali sana
kwake....’nikasema.
‘Ni kweli ulijitahidi sana, mpaka akawa anakuogopa, na hata
kufikiria unamtesa, kumbe ulikuwa na malengo maalumu, nakuaminia sana mke
wangu, kwani kweli kama usingelifanya hivyo, alikuwa kwenye muelekeo wa kuingia
kwenye makundi mabaya..hasa ya madawa ya kulevya, ndipo alipokuwa
akielekea,....’akasema.
‘Na bora hakuwa ameanza kuyatumia hayo madawa huko alipotoka,
kwani kama angelianza, ingelikuwa ni vigumu sana kumdhibiti, ....elimu
aliyoipata japo likuwa bado, haiwezi kumsiamia kimaisha, lakini ilimsaidia kumfanya
aweze kupambanua mema na mabaya, na ndio maana ya elimu, japokuwa ilikuwa
haitoshi kwa maisha ya sasa, ... na tulimuwahi mapema kabla hajapotoka, na
ikasaidia kwani alituliza kichwa, na kujipanga upya, akatulia, na kufuatilia
yale yote tuliyomuelekeza, na tumefanikia, ni jambo la kmshukuru sana
mungu,..hivyo ndivyo wazazi tunatakiwa tuwe, tusaidie, hata kama sio mtoto
wako, ilimradi uanishi naye, mfanye kama vile unavyowafanyia watoto wako,utaona
matunda yake baadaye....’nikasema.
‘Nikisikia hivyo mke wangu najihisi kama nimepona, maana,
nina jembe pembeni, najisikia raha sana, nashukuru sana mke wangu sijiu hata nikupe nini..mungu mwenyewe ndiye anajua, ndio
maana najuta sana kwa hayo yaliyotokea...na kama usingelinisamehe, nilitamani
nife tu...’akasema na mimi hapo nilitakiwa kuiondoa hiyo hali kwa haraka
nikamwambia;
‘Mume wangu usijali,..nimeshakusamehe, cha muhimu ni wewe
kupona, hlo ndilo unatakiwa uliwazie jinsi gani unatakiwa kufanya mazoezi na
kuondoa mawazo....’nikamwambia
‘Nikipona mke wangu, nitakuwa na wewe bega kwa bega,
sitatetereka tena, na nimegundua kosa langu ni nini, ma kumbe ulikuwa na
malengi mazuri tu, ...hata hivyo, wakati mwingine kama binadamu, tunajisahau,
na kutokujua undani wa mwenzako, na hili nimegundua kuwa ni tatizo,
...nitajitahidi sana tuwe pamoja tuiondoe hiyo hali, au unasemaje mke wangu..?’akasema
kama ananiuliza. Sikutakiwa nimweke katika hiyo hali ya kusononeka, kwahiyo
nikajitahidi kureejsha yale mazungumzo ya mdogo wake.
‘Usijali mume wangu, cha muhimu kwa sasa, ni kuhakikisha
yale tuliyo anza nayo yanafankiwa, na hasa hili la huyo mdogo wetu na watoto
wetu pia..’nikasema.
‘Huyu mdogo wangu kwa sasa hana tatizo, keshajiweka mahali
ambapo hatuna haja ya kuhangaika naye tena,..akiharibu hatuna lawama...na kwa
watoto wetu bado wadogo, hatuna shaka nao, tutawajenga kimaadili, na
umeshafanikiwa kwa hilo, kama wanaweza kuamuka asubuhi na kuwajibika hata bila
kuelekezwa, tunataka nini tena mke wangu.’akasema.
‘Hapana bado,...bado wanahitaji kuelekezwa, ama kwa huyu
mdogo wetu naye pia bado anatuhitajia sana, ndio kwa kiasi kikubwa kakamilika, lakini
bado hajafikia ile hatua ya kuweza kuwekeza, japokuwa amekataa, lakini ni vyema
tukamsaidia akawa ana ajira yake mwenyewe, mimi sipendelei sana ajira ya
kuajiriwa, nataka ajiajiri mwenyewe,...’nikatulia kidogo na yeye akaniangalia
akitaka kusema neno, nikamuwahi kwa kusema.
‘Ajira za kuajiriwa zinalemaza sana, ukiajiriwa, kwa hali
ilivyo sasa, utapata mshahara mdogo, na siku zitakwenda, umri utakwisha, utanyonywa
wee, huku wajanja wanafaidi jasho lako, na mwisho wa siku utajikuta huna lolote
la maana,.....kwasasa tumuache kidogo, ajifunze maisha halafu na sisi kidogo
kidogo tutatumbukiza nguvu zetu, ili aanzishe jambo lake mwenyewe....’nikasema.
‘Oh, hiyo ni kweli.....sasa umenipa matumaini, kumbe
nilikuwa nimefikiria vibaya, nilipoona mdogo wangu kakupigia magoti mbele yako,
niliumia sana, nilihisi kama mimi ndio nipo pale nakuomba msamaha, nilitamani
nisimame nije nifanye jambo ....lakini kumbe hasira hasara, nilihisi kuna tatizo limetokea, kafanya jambo
baya,au kuna jambo baya kalisikia na hataki kutokee madhara, ,..’akasema.
‘Hilo halitatokea, ilimradi tu awe mkweli kwangu, na ndivyo
maisha yangu ninavyotaka yawe, kuaminiana ndio tabia yangu, tuwe wakweli,
tuambizane ukweli, kama nimekosea, niambie, na mimi ukikosea nitakuambia, unanifahamu
silazi jambo, papo kwa papo ninakupasha. Na kazi ndio msingi wa maendeleo, ni
lazima tujitume, hakuna lele mama katika maisha,...., hakuna kulala katika
maisha kama una afya huumwi, chapakazi,..., ukilala wenzako wapo macho, wapo
kwenye maabara, wanagundua, wanasonge mbele, ukiamuka huwakuti tena, ....ndivyo
napenda maisha yetu yawe hivyo, tuchape kazi....’nikasema na yeye akaniangalia,
halafu akawa kama anajikagua, nilihisi kuwa anajisikia unyonge katika hali
aliyi nayo, kuwa yeye sio mtu tena.
‘Utapona tu mume wangu, tutashirikiana na kuhakikisha kuwa malengo
yetu yanatimia, ..na malengo yetu yaendane na umri wetu, haitakiwi unafikia
umri wa kukaribu kustaafu bado unahangaika, ..unatakiwa muda huo, unakuwa na
muda wa kupumzika, hapo ndio nafasi ya hata kustarehe, unafaidi matunda yako,
ujana, ni kuhangaika uzee ni kustarehe, na nashangaa watu wanafanya kinyume
chake...mimi sijui maisha yangu yapoje..ndivyo nionavyo mimi...’nikasema na
yeye akawa kama ananishanga.
‘Wenzako starehe ni ujanani, wewe unasema starehe ni
uzeeni...’akasema akitabasamu.
‘Ukiwa kijana ndio uan nguvu za kuzalisha, mwili unahitajika
kuchapa kazi, usipoteze muda, ndio kuna starehe, lakini ziwe kwenye kuujenga
mwili, na sio kwenye kuumiza mwili,...watu tuwajibike....tutumie kila dakika
katika kuzalisha jambo,...sio kuharibu, mwili una thamani sana, kama utautendea
haki yake, uzeeni utastarehe sana...’sijui kama ninaeleweka.
‘Nakuelewa mke wangu...lakini sizani kama jamii
itakuelewa...’akasema.
‘Jamii itatuelewa tu,...jambo lolote linaanzia kwa mtu mmoja
mmoja, na baadaye wengine wanafuatia...’ nikamwambia.
‘ Ndio maana uliniona silali, sikutaka muda upite bure...’nikasema
‘Ama kwa mdogo wetu huyu, tutakuwa naye bega kwa bega, hakitaharibika
kitu cha mhumi tuwe karibu naye...labda afanye kisiri siri, tusigundue ni kitu
gani anakifanya, ...hata hivyo, kwa hatua aliyofikia, hawezi tena kufanya jambo
baya, pale alipo anawaza maendeleo tu, anawazia maisha yake ya baadaye ...’nikasema.
‘Tuombee iwe hivyo..nashakuru sana mke wangu , umeniondoa
wasiwasi, maana nilihisi kuna tatizo, hasa pale niliposikia, ukisema eeeh, japokuwa sikusikia vyema, maana masikio yangu
sijui na yenyewe yameathirika kwasababu ya hiyo ajali, nilisikia kitu kama
ukisema ; `.... msione ajabu tukitengana,
nasema ukweli kama hamtaniambia ukweli sasa tutatengana..kama asiposema ukweli,
unaweza kuchukua hatua ambayo, .....’sijui ulisema neno gani...sikusikia
vyema..niliogopa sana kauli hiyo’akasema.
‘Ni maongezi yangu na yeye, nilikuwa najaribu
kumkanya....kiutani, kuwa aniambie ukweli, kama anataka kumuoa mfanyakazi wetu
asema kweli, na aliposikia hivyo, akahisi nimekasirika , ndio akakimbilia
kupiga mgoti, ....’nikasema na mume wangu akatabasamu, na niliona mazungumzo
hayo yalimfurahisha sana, nikaamua kumuuliza;
‘Naona tukiongelea mambo ya ndoa, mapenzi, kusaidia,....mara
nyingi nakuona unafurahi sana, kwanini?’ nikamuuliza.
‘Maana hayo ndiyo maisha ya mwanadamu, ndio yanayompa mwanadamu
raha na faraja, ,..hasa kwa mke na mume, ..hata kama hamna kitu, lakini mkawa
mnapendana, mnashauriana, manapeana moyo, mtajikuta nyi ni matajiri tu, lakini
hata kama mna utajiri wa kupindukia, lakini hakuna mapenzi, hakuna mashikamano
kila mtu anawaza lake, nyi ni masikini tu...maana mioyo yenu haina raha,.....’akasema
huku kionyesha uso wa huzuni.
‘Kwahiyo unafurahi sana tukiongelea hayo mambo kuliko mambo
ya kikazi?’ nikamuuliza.
‘Kazi ina mahali pake mke wangu, na mahali pake ni ofisini,
...ofisini kazi, na nyumbani pia kazi, tutazeeka akbla umri sio wetu, ha huenda
hata tusipate muda wa kufaidi jasho letu,
nina furaha sana tukiwa hivi nyumbani tunaongea, tupo bustanini,
tunasahau kabisa mambo ya kazini, tunatimiza wajibu wetu wa ndoa, ndoa ina raha
yake, na moja ya raha yake ni kupendana, kuwa karibu, na kufurahia kile mungu
alichowakutanisha... ndoa ni raha bwana asikuambia mtu, kama mkiijulia, ndoa
yenye mapenzi ya kweli, inaleta faraja, vingievyo, unafikiri mtu utafanya nini,
ili kichwa kipoe na mihangaiko ya dunia,..’akasema kama ananiuliza.
‘Kwahiyo kumbe mume wangu ulikuwa hupendi kwa jinsi
nilivyokuwa nikifanya, mbona hata wewe ulikuwa ukifanya hivyo?’ nikamuuliza.
‘Ilibidi nifanye kama unavyofanya wewe, ili twende sambamba,
nikijua ni kwa muda maalumu, huenda itafika muda tutakuwa pamoja kama mke na
mume, tufaidi matunda yetu, na tukione tupo na raha, sasa utajiri wetu una
maana gani, sikukuelewa, nilipoona kwa ndio mtindo wako wa maisha, hakuna
kualala, hakuna starehe, hakuna kuburudika kama mke na mume, ...nikaona
nitafute njia mabadala, kumbe nilikuwa naharibu...mara nyingi, nilitaka
kukuambia, lakini sikupenda kukuuzi mke wangu’akasema
‘Mume wangu, mimi ni mke wako, na una haki ya kunishauri
pale ninapoteleza, na ni makosa ukiona mimi nafanya yale usiyopendezewa nayo,
ukanyamaza kimiya, ungeliniambia tu, ningeliskusikiliza’nikasema.
‘Kuna muda nilijarubu kufanya hivyo kimatendo, lakini
nilishindwa, kwani kila nilipokuwa nikijaribu kukusogelea nilikuona ukiwa na
kazi zako, na kuna wakati mwingine uliniambia una kazi nyingi, huna muda wa
kuchezea, unakumbuka uliwahi kuniambia hivyo, wakati huo nilikuwa nakuhitajia
sana, uwe karibu nami, kwani nilihisi ibilisi anataka kunichezea....lakini
nikashindwa, je ningekulazimisha, hapana nisingeliweza kukufanyia hivyo mke
wangu...niliona nikuache tu...nahisi nilikosea, lakini ningelifanya nini kwa
wakati huo..?’ akawa kama ananiuliza.
Nikajaribu kukumbuka kama kuna muda aliwahi kunijia
nikamwambia hivyo, inawezekana, maana nikiwa kwenye kazi, sitaki utani, ni kweli kuna muda nilikuwa na kazi nyingi
sana, na sikutaka zilale, na hapo niliweza kusema lolote, bila hata kukusudia
hivyo, sikutaka kupteza muda, ..lakini yote hayo niliyafanya kwa ajili ya
familia, kumbe mwenzangu alikuwa akipata taabu...oh, kweli nimeanza
kujitambua...
‘Oh, mume wangu ndio maana ukakimbilia kulewa..nasikitika
sana, japokuwa nitakulaumu kwa kutokuaniambia ukweli, ungeliniambia
ningekusikiliza, ungelitafuta muda muafaka ukaniambia, mimi ni binadamu
tu....kwanini hukusema?’ nikamuuliza.
‘Kulewa, nilianza kama masihara tu, nilipokuwa kwenye
starehe, kupoteza mawazo, kuna jamaa huwa tunakutana naye, sio huyo rafiki
yangu, hapana ni jamaa tu ambaye huenda naye ana matatizo yake, huwa anapenda
kusema;
‘Unafahamu mke wa kukupotezea muda, ukiwa na mawazo....unafamhamu
ndio huyu...’akawa anaigiza sauti ya kilevi mpaka nikasikia kucheka.
‘Ukiwa nyumbani na mke wako hana habari na wewe, basi kuna
mke mwingine, japokuwa yeye anahitaji gharama, lakini hana hiyana, huyu ndiye
mke wa gharama,lakini hana hiyana pombeee....’akawa anaendelea kuigisa zauti ya
kilevi na mimi nikawa nacheka.
‘Ukiwa na pombe, basi umepata mke wa kukuliwaza, yeye
anakufanyausahau yote, hata kumsahau mke wako wa ndoa, si hakutaki bwana, basi
huyu anakutaka ila tu anahitaji pesa,.....ukiwa na pesa aah, unapata mke mpya
asiye na majigambo, kazi yako ni kunywa, ni kunywa....’akawa anaigiza hiyo
sauti na mimi nikawa nacheka sana.
‘Umenichekesha kweli leo, unaigiza kama mlevi kweli, au ni
kwa vile na wewe ulikuwa ukiongea hivyo wakati umelewa....?’ nikauliza.
‘Lakini hayo yote sikufanya kwa kujitakia, ...ndio ni uzembe
wangu, nakubali, na kweli nimekosa, lakini wakati mwingine naweza kukulaum
kidogo, lakini sio sana..kidogoo tu, kuwa wewe ndiye uliyenisukuma hadi
nikaingia huko kusikofaa...’akasema na mimi nikamwangalia huku nikijaribu
kuzuia maneni yangu makali, nikasema kwa unyenyekevu
‘Mume wangu Ina maana haya yote yametokea kutokana na mimi,
kutokana na ....ndoa yetu, kwani kuna nini nimekosea, ...maana nionavyo mimi
ilikuwa ni swala la kuambizana tu...mimi nina imani kuwa kama ungelianiambia
ukweli, ningelikusikia sijui kama ningelikukaidi, lakini kwa wakati muafaka....na
je kutokana na kulewa huko huoni ndio kumekusukuma, hadi kufanya mambo
yasiyofaa...?’nikamuuliza na niliuliza nikiwa na tahadhari.
‘Ndio maana najuta sana mke wangu unisamehe sana, maana
kweli pombe ni ibilisi, kila siku iliyokuwa ikienda kwa mungu, ndivyo nilivyojikuta nikitamani mengine
mabaya, sikuwa na tabia hiyo kabla, ...maana ukinywa, raha yake muwe kikundi,
uwe na wenzako, na mwisho wake, wanakuja
hata wale uliokuwa ukiwakwepa, na na...nashindwa hata kuongea,...’akatulia,kama
anawaza jambo, haikutakiwa iwe hivyo, nikauliza
‘Kwa hawo wengine walikuwa wakijileta wenyewe, si unawaita,
au,?’ nikauliza.
‘Kwenye majumba ya starehe, sio wote wanakuja kwa lengo
moja, wengine wanakuja kwa malengo mengine kabisa, nimejifunza hilo, na hata
wale unaozania kuwa ni marafiki, wanaweza kutumiwa mwanya huo
kukughilibu..ukiwa umelewa, huwezi kutathimini mambo kihekima, unajikuta
umetenda hata yale ambayo hukukusuidia..ni pombe, sio wewe.....’akasema.
‘Ina maana pombe ndio ilikutuma utende hayo uliyoyatenda...?’
nikamuuliza.
‘Ndio maana nilikuomba msamaha, ni kweli ni pomben, kama
isingelikuwa ni pombe, nisingeliweza kufanya hayo niliyoyafanya, na kwanini
nilikunywa pombe, jiulize hilo swali, kwanini nilikuwa nakunywa hadi
kupitiliza, ukipata jibu utafahamu useme nini, na ni kweli mimi nakbali upande
wangu kuwa nimekosa, kwani mimi sio mtoto mdogo, wa kufanya hayo,...hayo niliyokuomba msamaha...’ akasema huku
akikwepa kuniangalia machoni.
‘Mhh, mume wangu hay ohayo, hayana jina, ...ok, siwezi
kukulazimisha kuniambia kwa sasa, lakini tutakuja kuayaongea, usijichoshe na
mambo mengi...’nikasema.
‘Ina maana sijakuambi makosa yangu , unataka nikuambie kila
kitu, hutakasirika mke wangu, mimi ninaweza kukuambia kila kitu, ilimradi tu,
nisikukwaze, tena kuna mtu muhimu nasikia anakuja, na akija nafikiri mambo
yatakuwa safi, unataka nikuambia mke wangu?’ akaniuliza huku akiniangalia
machoni, na mimi nikawa nimeshika shingo kwa mkono mmoja huku nikitabsamu, na
kusema;
‘Nitafurahi sana, lakini....’nikasema na mara nikasikia
sauti za nyayo za mtu akitukaribia nikageuza kichwa kimwangalia huyo mtu,
alikuwa rafiki wa mume wangu.
‘Oh, naona leo mpo na raha, maana nimesikia kicheko, ..kicheko
cha raha, ...’akasema huku akituangalia, na mimi moyoni nikasema huyu mtu ana
nini , maana kila nikiwa na kwenye nafasi nzuri ya kuongea na mume wangu hujitokeza.
‘Kwanini nisiwe na raha na mimi nipo na mume wangu..’nikasema.
‘Ni kweli hayo ndio maisha,...inatakiwa mfanye hivyo kila siku,, au mara kwa mara, au
sio rafiki yangu?’ akamuuliza mume wangu huku akimsogelea na kushikilia kile
kigari,..na mume akasema;
‘Na wewe bwana, unakuwa dakitari wa kila kitu....’akasema
‘Ni kweli natamani iwe hivyo, na nimekuja na mtu wa mazoezi,
leo tunataka kumfanyisha mume mazoezi maalumu, na kama hutajali naomba
nimchukue mume wako’akasema
‘Unataka kumpeleka wapi?’ nikauliza nikimwangalia kwa uso
uliotahayari.
‘Ndani ofcourse, tunahitajia tuyafanyie ndani, kuna vifaa maalumu
kaja navyo docta...’akasema, na sikuwa na jinsi nikakubali, na wakati wanaondoka
kuingia ndani yeye aligeuza kichwa na kuniangalia kwa nyuma, akasema;
‘Uwe makini....’akaniambia.
Nikamwangalia kwa macho ya mshangao, na nikataka kumuuliza
niwe makini kwa kitu gani , japokuwa nilifahamu ana maana gani, na yeye akasema kwa sauti ili kumuondoa mume
wangu wasiwasi,kwani alihisi kuwa umesikia hayo maneno aliyoniambia, akasema;
‘Shemeji uwe makini, usimchekeshe sana mgonjwa, maana
akicheka sana, ..anaweza kudondoak kwenye kiti chake,...’ na mume wangu
akasema;
‘Ukiona nimedondoka kwenye hiki kiti ujue kuwa nimeshapona..maana
bado nahisi sehemu yote ya chini kama sio yangu....’akasema na mimi nikawa
nawafuatilia kwa nyuma hadi tulipoingia ndani, na wakati wanahangaika
kumtayarishia, nikatoka nje kidogo, na baadaye akaja huyo rafiki wa mume wangu,
akaniambia.
‘Nimekuona ukimuhoji sana mume wako, ...huu sio wakati
muafaka, wa hayo maongezi yako...nilishakukunya ukimhamasisha kuongea, atafikia
sehemu ataongea ukweli na hivyo itamzididhia huzuni, na wewe ukiusikia huo
ukweli, ninavyokufahamu hutaweza kuvumilia, utakasirika, utasema ovyo,
unafikiria baada ya hapo kutatokea nini.....kwanini una haraka na hayo mambo,
uwe na subira na hicho unachotaka
kukijua, utakifahamu, lakini usije ukafanya jambo ambalo utakuja kujijutia.’ Akasema
na mimi nikawa namsikiliza tu.
‘Kwani mimi nimemuuliza nini kibaya,..tulikuwa tunaongea tu
na mume wangu, na kwanini wewe unayejua ukweli hutaki kuniambia, ..wewe unajifanya
kuwa unanijali, kumbe kuna mengi makubwa unanificha, hutaki kuniambia ukweli,
na huenda haya yote yasingelitokea kama ungelikuja mapema ukaniambia...’nikasema.
‘Ina maana unanilaumu mimi, ...unanichekesha, kweli,
ushindwe mwenyewe kuihudumia ndoa yako halafu uje kuwalaumu watu wengine,
umesahau mara ngapi ninakuja kuongea na wewe na kuajribu kukuelekeza halafu
wewe uannitolea nje, kuwa nimetumwa na wazazi wako kuja kukuharibia ndoa yako,
umeshahau eeh, sasa unaona yamekukuta, unataka kunilaumu....’akasema.
‘Huna maana wewe, na ole wako nikifahamu ukweli, ...ukweli
ambao ulitakiwa wewe uniambia ukanificha, ..sitakusamehe kamwe...’nikasema.
‘Unakumbuka nilishaanza kukuelezea ukweli ukasema hutaki
kugombanishwa na marafiki zako, hususanai mume wako, umeshasahau eeh, usinione
kuwa mimi ni mjinga, nafanya haya kihekima, ni bora ukawaachia wenyewe wanandoa
wakajibadili wao wenyewe, maana kijiingiza kwenye ugomvi wa wanandugu unaweza
ukaonekena wewe ni mbaya...’akasema.
‘Kwahiyo umesahau ile ahadi yako,?’ nikamuuliza
‘Ahadi gani?’ akaniuliza
‘Kuwa kamwe hutakubali mtu aniumize...’nikasema.
‘Na ndicho ninachokifanya...wewe mwenyewe utaona, si
unajifanya mpelelezi, endelea,...lakini mimi nitajitahidi kuhakikisha kuwa
hakuna mt anayekuumiza,ahadi yangu ipo pale pale, hata kama hunitaki niwe
karibu na wewe....ila nakukanya uwe mwangalifu, usichukulie mambo kwa pupa..’akasema
huku akitabasamu na kushika kidevu
‘Halafu kuna ujumbe, nimeupata, kutoka eeh, kwa rafiki yako,
yupo karibu kurejea...anasema anakuja kumaliza mambo fulani fulani, halafu
atarejea kusoma, ...sijui ni mambo gani, kwani hamjawasiliana naye ?’nikamuuliza
‘Rafiki yangu yupo?’ nikamuuliza nikionyesha mshangao.
‘Una marafiki mangapi bwana, huyo huyo,..unayemwamini
kupidukia,...nahisi ukweli sasa utagundulikana, ila bado nakukuanya, uwe makini,
hasa akija huyo rafiki yako,...huenda yatakuja kutokea mambo ambayo,
yatakufanya usiwaamini tena wale unaowaona ni marafiki zako, lakini huenda yote
umajitakia mwenyewe.....’akakatizwa, kwani alikuwa akiitwa ndani.
‘Eti nini....?’ nikamuuliza nikiwa nimeshakunja uso.
‘Tutakuja kuongea siku nyingine....lakini hebu kunjua huo uso wako please’.
NB: Tabasamu na wewe mpenzi wa blog, kisa kinaendelea, wasemaje?
WAZO LA LEO: Ndoa
nyingi zina matatizo yake, na huenda yakawa ni matatizo madogo tu, lakini kwa
wanandoa wakashindwa kuyatatua, kwa vile, hakuna anayekubali kushuka chini,
kila mmoja anajiona anafahamu zaidi ya mwingine...au mmoja anaogopa kumuelezea
mwenzake ukweli.....wewe kama rafikji tumia hekima kuwashauri, usitumie mwanya
huo kuharibu badala ya kujenga. Hekima ya ushauri ni muhimu sana kwa watu kama
hawo.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Mmh, naingawa huyu dada ndie aliemshauri rafki yke lkn pia marafiki sio wa kuwaamini kbs wanaweza wakakufanyia kitu kby ndio haya sasa yaliyomkuta mdada hembu tusubiri italavyokuwa.
Hebu tusubiri rafki yake aje tuone itakavyokuwa ila marafiki sio watu wa kuwaamini kihivyo.
Post a Comment