Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, October 17, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-11


Nilipogeuka nikajikuta tukiwa tunaangaliana nahuyo rafiki wa mume wangu, kumbe alishafika, na sikuwa nimejua kuwa yupo nyuma yetu anatusikiliza, na sikufahamu ameyasiki amangapi,na  uso wangu ulipokutana na wake, mengi yakajiaeleza,kwani.....nilikuwa nimeshabadilika sura kwa hasira, uso uliokuwepo ulikuwa uso uliojaa hasira chuki...na .....

Huyo rafiki wa mume wangu aliponiona jinsi nilivyobadilika sura,kwa vile ananifahamu akajua  akaniangalia kwa macho ya mshangao na kwa muda, tukawa tumeangaliana na yeye bila yoyote kusema neno, na nilihisi kuwa  kama hakuwa amesimama hapo kwa muda mrefu na kusikiliza mazungumzo yetu, basi atakuwa amefikiria tulikuwa tunamsema yeye, hasa kwa vile nimemgaukia na kuonyesha chuki za waziwazi,japokuwa hazikiwa zimelengwa kwake...

Cha ajabu akilini mwangu kwa muda ule nilikuwa simuoni yeye, akilini mwangu nilikuwa nimejaribu kujenga taswira ya huyombaya wake asiyejulikana, huyo mdudu mtu, ambaye nahisi ndiye kamghilibu mume wangu,.....

Nilikuwa nimejaribu kujenga taswira ya sura ya huyo msaliti wangu, lakini sikuweza kuiweka akili vyema, maana sikuwa na hisia na mtu yoyote, kwahiyo nikawa naona sura za watu wengi wengi, na kujenga hisia za mtu asiyekuwepo,na hali hiyo ilinifanya hata kichwa kianza kuuma, nilifumba macho kwa muda kidogo, hlafu nilipohisi kuwa akili yangu imetulia ndio hapo nikayafumbua macho yangu, na nilijikuta naangaliana uso kwa usona na huyo rafiki wa mum, kumbe alishanisogelea...na alikuwa kama anataka kusema neno, sikumpa nafasi hiyo.

Nikasogea nyuma kujenga nafasi, sikutaka anishike, kwani angelishika , huenda hasira zilizojijenga akilini mwangu zingemshukia yeye, na hapo hapo nikageuka kuangalia hapo alipokuwa kasimama rafiki yangu, ...oh hayupo!

Wakati nageuka, ili nikabiliane na rafiki yangu kwa kutoa amri kuwa aondoke, nilikuwa nimeshaanza kurejesha uso wangu katika hali nzuri. Nilitaka niwe muungwana, na kuondoa hisia mbaya iliyokuwa imekwisha kujijjenga akilini mwangu, kwanini niwakasirikiea watu wasio na hatia, nikajiuliza, na nilipogeuka oh,  nikakuta rafiki yangu huyo hayupo, keshaondoka, ...nigaueza kichwa huku na huku nikimtafuta rafiki yangu huyo, lakini hakuwepo,  sikuweza kumuona, ni kama mtu aliyeyuka na kupotea hewani.....

Endelea na kisa chetu..

`Huyu mtu vipi, ....?’ nikauliza kwa sauti, na aliyeijibu ni rafiki wa mume wangu, akisema.

‘Kwani ulimuhitaji tena, ...nahisi kaondoka, maana umeshampa kazi, na hakuona haja ya kusubiri..maana ulivyobadilika, kwa yoyote asiyekujua, angetamani kukimbia,....’akasema huyo rafiki wa mume wangu, na mimi nikageuka kumwangalia, na wakati huo uso wangu ulisharejea katika hali yake ya kawaida, nikasema.
‘Oh, sijui, ni kwanini nahisi hivyo..nahisi kama nataka kupasuka, nahisi kama ....’nikakatiza kuongea.

‘Kwa hali kaam hiyo nakushauri utilize kichwa chako...unapokwenda huko sio kwema,...na cha ajabu nakushangaa, kwanini unampa  kazi fisi ya kuchunguza kupotea kwa mifupa ...’akasema docta na mimi kwa muda ule sikumuelewa ana maana gani maana bado nilikuwa nikigeuka huku na kule kumtafuta huyo rafiki yangu.

‘Hayo ni yangu ya yeye, hayakuhusu....’nikasema.

‘Lakini ni yetu, maana mimi ndiye niliyekushauri uongee naye, ili ujue kama anafahamu lolote, lakini sikuwa na maana kuwa umpe kazi ya kumchunguza mumeo...’akasema.

‘Ok, lakini kaondokaje kwa haraka kiasi hiki, na hakutakiwa kuondoka kwanza, maana nilikuwa sijamalizana naye....nilikuwa nataka kuongea naye maswala mengine’nikasema.

‘Ndio keshaondoka, maana aliogopa, ...ulivyobadilika sura alihisi kabisa unamlenga yeye, na siku hizi naona sura yako inazidi kujenga umbile jingine hasa ukikasirika, unaonekana kama mkatili, wakati so tabia yako, yoyote angelikuona ulivyokuwa angehisi wewe ni mtu unayetaka kuua, hivi kweli una nia hiyo?’ akaniuliza.

‘Nia  gani hiyo unayoizungumzia wewe?’ nikamuuliza huku nikishika simu yangu mkononi na kuanza kutafuta namba.

‘Ya kutaka kumjua huyo msaliti wako, na kumfanya  jambo ambalo nahisi litakuwa ni baya sana...’akasema.

‘Wewe ndiye uliyejenga hizo hisia kichwani mwangu, sikuwa na wazo hilo kabisa, ..sasa unaniuliza kitu ambacho unakijua ni nini madhara yake..sipendi haya, nayafanya ili kuondoa hizo hisia zako ambazo naona kama zinanipeka kubaya.....’nikasema.

‘Mimi nilikushauri, kuwa ujaribu kuchunguza kama mume wako ana tatizo, kwa vile umesema wewe na yeye hamna matatizo, ..na kama nyie wawili hamna matatizo ndani ya ndoa yenu, basi kuna tatizo linatoka nje ya ndoa yenu, je ni tatizo gani, tukajenga hoja kuwa huenda akawa ana mtu nje, kama si hivyo, basi huenda, kweli kuna kitu kingine kinamsumbua, ...sasa wewe kama mwenzako na umeona hali kama hiyo, ni wajibu wako kufanya jambo, kwa maslahi ya mwenzako, kwa masilahi ya ndoa yenu....’akasema huyo docta.

‘Nimekuelewa,..ila mimi nakuonya, kama kutakuwa hakuna jambo, ni uzushi wako, ni njama zako za kutaka kunifitinisha mimi na mume wangu, ni njama za kuiharibu ndoa yangu,sitakusamehe kwa hilo, nitasahau yote ya nyuma, na nitahakikisha, unadhalilika,....’nikasema nikijaribu kuirejesha ile sura ya chuki...

‘Ina maana mimi kwa kutoa ushauri wangu huo ndio nimekuwa mtu mbaya, ndio unafikia, kuniangalia kama unataka kuniua....mimi sina nia mbaya, na nina uhakika, kuna tatizo kwa mume wako, japokuwa sijakuwa na uhakika ni tatizo gani ...’akasema akijaribu kunisogelea na mimi nikarudi nyuma.

‘Sikiliza ...nikuambie, nina uhakika mume wako yupo kwenye matatizo,hilo mimi sina wasiwasi nalo....kama unahitaji msaada wangu nitakusaidia, lakini kama ...unahisi kuwa mimi nina nia mbaya na ndoa yenu, basi, nitakuachieni wenyewe....lakini msije nilaumu,’akasema.

‘Hakuna aliyekuomba msaada, amua utakavyo....’nikasema kwa sauti kavu ya kuashiria chuki huku nimeshika kiuona, na yeye akaniangalia na safari hii alionekana kukasirika, alikuwa kakunja uso, mimi sikujali...

*******

Baada ya kumpa kazi hiyo rafiki yangu, na yeye kuondoka bila kuaga, nilijaribu kutuliza kichwa changu, na akilini nikawa najaribu kuwaza, mazungumzo yangu na rafiki yangu huyo aliyeondoka bila kuniaga, nilijaribu kuwaza, kama kuna jambo ambalo nimeliongea, na likamfanya mwenzangu akwazike...lakini sikuona jambo lililostahili kumkwaza yeye, nilichotaka ni yeye kunisaidia kumtafuta huyo mdudu mtu,....nikaona nisipoteze muda nikainua simu yangu na kuiweka mdomoni, wakati huo nilikuwa nimeshaipiga namba ya huyo rafiki yangu.

Kwanza simu iliita kwa muda bila kupokelewa, lakini wakati inataka kukatika, akaipokea, na mimi nikamuuliza kwa haraka ni kwanini kaondoka bila kuniaga.., yeye akajibu kwa haraka tu;

‘Niliona rafiki wa mume wako ameshafika , na kama ulivyosema mazungumzo hayo yalikuwa baina yangu  mimi na wewe, nikaona niondoke haraka....kwani kuna tatizo jingine?’akasema na mimi nikamuelewa.

‘Lakini nakuona kama hukuipokea kazi niliyokupa kwa mikono miwili, na sikuona kwanini, kama ni kuhusu kuwa ndio umetoka kujifungua na ulihitajia muda wa kupumzika, hilo nalifahamu sana, na sikuona kama kazi hii ina uzito wa kukufanya ushindwe kuifanya kutokana na hiyo hali, ni kazi unayoweza kuifanya hata bila ya kutumia nguvu, kwani wewe una vyanzo vyako vingi vya kukusaidia bila ya hata ya wewe kutoka nyumbani kwako, na bila ya hata watu wambea hawajaliweka masikioni mwao,..kuna tatizo gani jingine linalokufanya usite kuifanya hiyo kazi,...?’ nikamuuliza.

 ‘Oh, rafiki yangu, sijakuambia kuwa sitaifanya hiyo kazi, toka lini nikakataa kazi yako, nafahamu nipo kwenye mkataba na wewe, na niwajibu wangu kutimiza kila utakachoniambia, lakini nilitaka nikuweke wazi,...’akasema na kutulia kidogo, halafu akaendelea kuongea kwa kusema;

‘Ujue mimi na wewe hatutakiwi kufika hapo ulipofikia wewe, na sikukutegemea kuwa hili tatizo lingekuwa ni ..’akatulia kidogo, halafu akawa kama analia, japokuwa hakuonyesha hiyo hali, na akaendelea kuongea akificha hiyo hali, lakini nilihisi kama analia, sikutaka kumkatisha, akaendelea kuongea kwa kusema.

‘Kwa vile sisi ni marafiki sana, naona ni bora tuambizane ukweli...’akasema.

‘Sema nakusikiliza....’nikasema na yeye akaendelea kuongea bila kujali kuwa na mimi nilikuwa naongea akasema;

‘Hata hivyo kama ulivyosema, ...kama ilivyo ndio kwanza nimetoka kujifungua, hata kuja hapa nilikuja tu kwa vile wewe ni rafiki yangu,na ajali hiyo kwa shemeji inanigusa na mimi, ....lakini hebu jaribu kuniangalia, na mimi, ndio nimetoka kujisfungau, kitoto change bado kichanga, hali yangu bado haijawa safi, nahitajia muda wa kutulia kwanza, nahitaji muda wa kukaa na mwanangu na pia nipo kwenye maandalizi ya ile safari ya kwenda nje kusoma....nahisi kazi hiyo sitaweza kuifanya ipasavyo,.....’akasema rafiki yangu huyo.

Kwanza nilishangaa, maana haijatokea nimuombe kitu rafiki yangu huyu akatae kwa kutoa visingizio vya moja kwa moja kihivyo,na ni mtu anayenijali sana, na kwa hili nilitarajia kuwa angeliunga mkono moja kwa moja, ..na niliona ajabu sana maana mimi ndiye nilimuwezesha hadi hapo alipo, na hata hiyo safari ya kwenda kusoma ni mimi niliifanyia kazi, japokuwa sikuwa makini sana kufahamu ni lini anaondoka kwani hatua iliyokuwa imebakia. Ilikuwa ni kukata tiketi, lakini kwa vile alishafikia hatua ya kujifungua, zaoezi hilo likasitishwa kwa muda,...

Akili ikaanza kukumbuka fadhila zangu juu yake...

*********

Rafiki yangu huyu, niliamua kumsaidia  japokuwa wazazi wake wana uwezo, na kwa vile niliona kuwa tatizo lake halikuwa mbali sana na tatizo langu, na mimi nimeliweza kulitatua tatizo langu, nikaona na mimi nimsaidie rafiki yangu aachane na kusmba ya kuwategemea wazazi, ili aweze kusimama  kwa miguu yake mwili.

Tatizo lake kubwa, japokuwa linatokana na hali ya ulezi, kwani ilionekana alikuwa akidekezwa sana, kila akitakacho alikuwa kikipata, na akawa kajenga hali ya kujiona, hana shida...wanazo, lakini hakutambau kuwa hicho anachojivunia sio chake, ni mali ya wazazi wake,..

Mimi nikataka kuiondoa hiyo hali,na kumjenga awe mtu mwingine wa kujiamini...lakini baya zaidi, wazazi wake walifikia hatua ya kutaka binti yao aolewe na mtu waliyeona kuwa aatamfaa, na binti yaohakuwa tayari naye, kama alivyokuwa hayupo tayari kwa wanaume wengi waliomtaka kumuoa kabla ya huyo ambaye wazazi wake, waliamua kumshurutisha...ndio maana tatizo lake nikalichukulia sawa na la kwangu..

‘Hawa wazazi wangu siwaelewi, kama wamenichoka, na huenda wanaona mimi ni mzigo kwao, waniambie, lakini sio kunitafutia mwanaume,....hivi wananionaje mimi, eti niolewe na yule mzee, ..eti kwa vile ni tajiri, ....hapana, siwezi kuishi na yule mzee, hata siku moja....’akaniambia.

‘Lakini yule sio mzee,ukiangalai umri wako na yeye, huwezi kumuita yule mzee, yule ni saizi yako kabisa, au unataka kuolewa na dogodogo, usidanganyike, huko umeshakupita, sio kwako tena, huyo unayemuona ni mzee, ndiye saizi yako...’nikamshauri.

‘Simpendi, na simtaki....’akasema na mimi nikamuelewa, nikaona nimsaidie na nione vipi nitaweza kumfanya aishi maisha bila ya kutegemea wazazi wake, , kwani kwa muda huo alikuwa ameshakosana nao kabisa..na wazazi wake, walisema kuwa binti yao huyo kazidi kwani kila mchumba anayemfuata yeye anamkataa,

‘Basi rafiki yangu mimi naona nikusaidie kwa hilo, unaonaje tukiwa washirika, ....?’ nikamuuliza.

‘Washirika kwa vipi, ..mimi ninachozungumzia hapa ni hilo wazo la wazazi wangu la kuolewa, sio swala la kazi, kama ni kazi ninaweza kwenda kutafuta popote....’akasema.

Mimi namfahamu sana rafiki yangu huyo , hawezi kupata kazi ya kuajiriwa akatulia, sizani kama anaweza kuhimili sheria na taratibu za kazi, mara ngapi anaajiriwa na baada ya hata mwezi kuisha keshakosana na muajiri wake,...niliona niishi naye mimi ninayemfahamu, lakini kwanza nilitaka nimjenge kutokana na jinsi ninavyomfahamu mimi,..kwa vile namfahamu sana toka utotoni, tumekuwa pamoja, na tabia zetu hazitofautiani sana.

Urafiki wetu ulianzia tukiwa wadogo, tukisoma pamoja,na yeye alikuwa akipenda sana kazi za upelelezi, kutokana na kusoma vitabu mbali mbali vya hadithi za kipelelezi, na kuangalia sinema za namna hiyo,na hiyo ilikuwa ni ndoto yake kuwa akimaliza shule atajiunga na kazi za upelelezi,lakini ndoto yake hiyo haikuweza kufanikiwa, tulipomaliza shule, akajikuta akifanya kazi nyingine kutokana na matakwa ya wazazi wake, ambazo hakuweza kuzifanya itakawavyo, akaanza kutafuta sehemu nyingine, na hata huko hakuweza kukaa muda mrefu,ikawa mtu wa kubadili kazi, mara leo yupo hapa , kesho yupo kule.

Basi siku hiyo alipokuja kwangu na malalamiko hayo juu ya wazazi wake, nikakumbuka ile ndoto yake wakati akiwa shule, nikaona kwa vile tumekuwa watu wakusaidiana, kupendana, toka utotoni, ngoja na mimi nijaribu kumsaidia nionavyo mimi, na ndipo nikamap wazo langu hilo nikamwambia;

‘Rafiki yangu mimi nataka kuifufua ile ndoyo yako ya shuleni, upo tayari....?’nikamwambia na yeye akawa kama hakunisikia,kwani wakati huo alikuwa anacheza na simu yake, nafikiri alikuwa akiandika ujumbe kwa watu wake, na baadaye akasema;

‘Ndoto ipi...?’ akaniuliza kwa dharau, na huku akiendelea kuangalia simu yake.

‘Kwanza rafiki yangu nakutaka unielewe, nikiongea na wewe uhakikishe kweli unaongea na mimi, ....kama bado una tabia za utoto, hutafika mbali, weka hiyo simu pembeni, nataka tuongee kikubwa....’nikasema kwa sauti ya ukali, na yeye aliponiangalia usoni akakutana na uso wa kazi, uso unaoashiria amri, akashangaa, kwanza, halafu akabetua mdomo, na kusema.

‘Ok. Bosi, maana kwa vile wewe ni bosi kwenye kampuni zako unafikiria kila mtu utamsimamia hivyo hivyo..lakini kwa vile nimekwama, nitakusikiliza bosi....’akasema huku akiiweka simu yake pembeni.

‘Nakumbuka wewe ulikuwa na ndoto ya kuwa askari mpelelezi...lakini haikuwezekana, sasa nataka hilo liwezekane, hujachelewa, utakwenda kusomea hilo, lakini sio askari mpelelezi wa kipolisi, nataka uwe mpelelezi wa watu binafsi,...mpelelezi muhutasi,  hiyo si inawezekana...?’ nikamuuliza. Na yeye kwanza akawa kama haamini hilo kwani muda umeshapita, na huenda hakuwa na wazo hilo tena.

‘Mhh, hilo nilishalitoa akilini, hayo yalikuwa ya kishule, ...sijui kama inawezekana, sina uhakika na hilo.na hiyo kazi inapatika kweli, maana nahisi nitahitajika kwenda jeshini, na huu mwili sizani kama utakubali shuruba, na amri.....’akasema.

‘Inawekana,....kwanini isiwezekane, kila kitu ni nia, kila kitu ni utashi, na dhamira ya kweli, sasa hivi vipo vyuo vingi tu vya kutoa hayo mafunzo, na hata kwenye mitandao kuna elimu kama hiyo, tuifanyie kazi, ...na na kwa vile mimi nakuhitajia kwenye mambo yangu,...tushirikiane, tutaweza...upo tayari....?’nikamuuliza.

‘Sijui...tuone ,..’akasema na mimi nikafahamu kuwa yupo tayari, nikamwambia ili aonyeshe dhamira ya kweli, basi ahangaike mwenyewe kuvitafuta hivyo vyuo, na mimi nitamsaidia kwa hali na mali. Na kweli baada ya siku kadhaa akasema keshapata chuo cha namna hiyo, na yupo tayari kwa masomo, na mimi nikamwambia nitawasiliana na wahusika wa hicho chuo.

‘Kwani ni mpaka wewe uwasiliane nao, cha muhimu ni maombi, na maombi nimeshatuma na wao wameshanikubali, kilichobakia na malipo..hakuna zaidi....’akasema.

‘Usijali..malipo nitalipa, lakini kama nilivyokuambia, mafunzo hayo ni kwa ajili ya kazi zangu, kwahiyo nataka niongee nao, nione jinsi gani wanaweza kukupika nitakavyo mimi....’nikasema na kweli nikaenda kuonana na wahusika wa hicho chuo, na tutakakubaliana, kwani nilitaka kwanza wamjenge huyo binti kikakamavu, na kuondoa ulegelege wa kutegemea wazazi,..na wao wakasema hiyo kwao ni kazi ndogo tu.

Sikuamini, huenda ni kwa vile, alikuwa na ndoto hiyo, au ni dhamira tu, ilimtuma ajitume hivyo, kwani, aliweza, na akafuzu vizuri sana, na kuna muda aliombwa ajiunge na askari polisi, lakini yeye mwenyewe alikataa, na akaja kwangu na kusema yupo tayari kwa kazi zangu, na tukaingia naye mkataba, akawa ni mtu wangu na hilo lilikuja kunisaidia sana kibiashara.....na kwa usalama wangu binafsi.

Nikawa kila mara nampa kazi, au au wakati mwingine anapata kazi zake binafsi, na haikutokea siku nikampa kazi, akaikataa,...na hata nilipoona umri unazidi kwenda, haolewi, nikamshauri atafute mume wa kuzaa naye, na hilo akakubali, leo hii nampa kazi ndogo, anaikataa kinamna  nikajikuta nikishikwa na mshangao..kwanini anaikataa hiyo kazi, hakukataa moja kwa moja, lakini kulalamika kwake,  sio kawaida yake...

‘Kuna nini hapa....’nikajiuliza.

NB: Je ataikubali hiyo kazi.


WAO LA LEO: Mara nyingi tunapokuwa na shida, tunasahau kuwa wenzetu pia na wao wana shida kama hizo za kwetu au huenda shida zao ni zaidi ya shida zetu, wakati huo wa shida, hatujali shida za wenzetuo,cha muhimu kwa wakati huo ni shida zetu, tunachotamani  ni jinsi gani ya kusaidiwa, ni jinsi gani, shida zetu zitachukuliwa kipaumbele, na hapo utaanza kuwachuja marafiki zako, na rafiki utakayemuona ni wa kweli kwako ni yule atakayesimama kwenye shida zako, na kutetea hoja zako.

 Tukumbuke kuwa,sisi sote ni wanadamu, na shida zimeumbiwa kwetu, na kwahiyo sote ni wahitajia,kama ni hivyo basi,  ili tuwe sawa, tujaribu kuona shida za wenzetu zina umhimu sawa sawa na shida zetu.

Ni mimi: emu-three

No comments :