Niliangalia saa huku nikimsubiria docta, rafiki wa mume wangu ambaye niliona amechelewa sana kurudi, nikataka niende huko huko nikajue kuna nini kianendelea, lakini kabla sijainuka pale nilipokuwa nimekaa , mara rafiki ya mume wangu akaja na mimi kwa haraka nikamuuliza,
‘Wanasemaje?’ nikamuuliza.
Endelea......
Nilipomwangalia usoni rafiki wa mume wangu nilimuona kama hana raha, japokuwa alijitahidi kutokunionyesha hivyo, na kwa vile namfahamu, sikushindwa kuligundua hilo, na hapo hapo nikamuuliza tena nilipomuuliza mara ya kwanza na akawa ananisogelea pale nalipokuwa bila kusema neno;
‘Vipi huko ulipokwenda wanasemaje, mume wangu anaendeleaje?’ nikamuuliza tena, na yeye akasema;
‘Hali yake inendelea vyema usiwe na shaka, kwani baada ya vipimo, hakuna sehemu iliyovunjika, na wasiwasi wao mkubwa ulikuw kama huenda kuna damu zimevuja ndani ya tumbo, au kama kun aathari zozote kwenye ubongo, lakini baada ya uchunguzi wameona hakuna athari kama hizo,...’ akatulia kidogo, na mimi nikawa na amani kidogo.
‘Ila kwa vile alikatwa katwa na viyoo,kuna sehemu nyingine imebidi zishonwe,...na ukumbuke kuwa walimfanyoa upasuaji, kwani mtizamo wa mwanzo ulikuwa hivyo, kuwa huenda kuna athari ndani, lakini haikuwa kubwa kiasi ha kutisha,....’akatulia na kuniangalia machoni, na ninavyomfahamu akikuangalia machoni, ujue kuna jambo kubwa anataka kukuambia.
‘Alipozindukana, na kutulia kidogo, akaanza kulalamika,maumivu ya mgongo na kiuno,...inawezekana ni kutokana na hali halisi,...lakini madakitari wanasema inabidi azidi kuwa kwenye uchunguzi zaidi, na dio maana hawakutaka watu wamuone, kabla hawajamaliza uchunguzi wao,...kwahiyo nimewaacha wakiendelea na uchunguzi huo, wameshamchukua x-ray ...’akasema huyo rafiki wa mume wangu.
‘Wewe kama docta unahisi kwanini analalamika maumivu ya mgongo na kiuono?’ nikamuuliza.
‘Mhh, huwezi kutoa jibu rahisi hivyo, maana hiyo ni ajali, lolote lawezekana, cha muhimu ni kusubiria vipimo, lakini yale muhimu yameshafanyika, na kama kuna atahri nyingine, ni za kawaida, tu....’akasema.
‘Je uliweza kuongea naye?’ nikamuuliza
‘Bado,. ..hawajaruhusu mgonjwa kuongea na mtu mwingine,...kwa hali aliyo nayo, inahitaji muda kidogo, ...’akasema.
‘Lakini ulifika karibu yake akakuona?’ nikamuuliza.
‘Hapana, hawajaruhusu mtu mwingine kumuona, mimi nilifika hatua chache, na nikamwangalia kwa mbali, alikuwa bado yupo kwenye iuangalizi wa madakitari, mimi waliniruhusu tu nimsogelee kidogo,hawataki mtu kuja kuwaharibia mambo yao...ni kawaida siwezi kuwalaumu.
‘Lakini umesema, alipozindukana, alikuwa akilalamika maumivu ....ina maana kumbe yupo macho, ameshazindukana...?’ nikauliza .
‘Ndio yupo macho, kazindukana, lakini bado madocta wamemzunguka, kila mmoja katika fani yake, nakwa muda huo, alikuwa akimshughulikia dakitari wa mifupa, ....’akasema.
‘Haya mimi sijawa sawa mpaka niende kumuona mwenyewe, naona kama mnazidi kunichanganya tu...’nikasema.
‘Shemeji mimi nilikuwa nashauri kitu,naona wewe una shughuli nyingi umeziacha bila ya maagizo,kwa vile mimi nipo likizo, ninaweza kubakia hapa, ili niliendee kuona hali ya mgonjwa, na kwa vile bado yupo kwenye uchunguzi, na huenda ukachukua muda kidogo, wewe nenda nyumbani kaweke mambo yako sawa, kama kuna lolote litajitokeza ghafla mimi nitakupigia simu, ....’akaniambia na mimi nikageuka kama kumshangaa, maana mimi ni mke wa mgonjwa na ni muhimu kuwepo hadi nimuone mume wangu, na huyu jamaa ananishauri niondoke, sikusema kitu.
Nikawa nimekaa nimetulia nikimuwazia mume wangu, ....hapo nikahisi machozi yakinilenga lenga, na kabla sijaathirika na hiyo hali, nikageuka kumwangalai docta, na yeye akaniangalia an kutabsamu, kuniondoa hofu akasema;
‘Usiwe na shaka, ...nakuhakikishia mume wako hana matatizo, ...ni swala la muda tu, utakuwa naye, ajali ni ajali, na hiyo ajali yake ilikuwa ni kubwa sana, hutegemei mtu aliyetoka pale awe hai, uhai wake bado mkubwa....’akasema na mimi sikusema kitu nikageuka pembeni, ili asije akaona machozi yaliyokuwa yamezidi nguvu.
Nilipoinua kichwa kuangalai sehemu ya nje, kwenye mlango mkubwa nikamuona rafiki yangu akija kwa mbali, na wakati huo huo rafiki wa mume wangu akawa anaongea na simu yake, na aliponiona nikiangalai upande huo wa watu wanaokuja kuona wagonjwa wake, akanisogelea na kusema;
‘Ni vyema kwa leo, hata kama tutaruhusiwa kumuona mgonjwa, wewe hakikisha huruhusu watu wengi kuonana na mume wako, hata kama ni rafiki yako ...na ulisema ulimuita rafiki yako aje, vipi hajafika bado....naona kama kachukua muda mrefu kufika, au kwa vile ni mzazi,.....’akawa kama ananiuliza, nahisi alikuwa hajamuona huyo rafiki yangu maana alikuwa kwenye kundi la watu, waliokuwa wakiingia.
‘Ninafahamu hilo hata huyo rafiki yangu sikumuita aje hapa kwasababu ya kumuona mume wangu, nimemuita kwa ajili ya kumpa kazi maalumu,..nataka kwanza niongee naye, kwa mambo fulani fulani, na yeye ndiye ninayeweza kumuagiza kwenye mambo yangu mengine....’ nikasema na huyo rafiki yangu akawa keshafika, na kutuangalia kwa mashaka, akauliza;
‘Haya nipeni habari, maana nimemuacha mtoto hapo nje, kwenye gari, ....’akasema
‘Umemuacha mtoto nje, yupo na nani?’ akauliza rafiki wa mume wangu kwa mshangao.
‘Kuna mtu yupo naye, usitie shaka...’akasema huku akiniangalia mimi machoni.
‘Haya niambie hali ya shemeji ipoje..nakuona kama unalia...’akasema na mimi nikapitisha leso machoni.
‘Kuhusu mume wangu,...mhh, bado,...sijaonana naye tangu apelekwe huko ICU, lakini kwa taarifa za kupitia huyu rafiki yake, wanasema hajavunjika mahali,....ila analalamika maumivu kwenye kiuoni...na mgongo, na hilo kwangu mimi naona ni hatari zaidi...’nikamwambia huyo rafiki yangu.
‘Kwenye kiuno..na mgongo,...ina maana aliumia sana,...mh, na sehemu hizo nyeti sana, kwani mengi yanaweza kutokea baadaye .....lakini kwa vile yupo na wataalamu, mimi sioni kwanini uwe na wasiwasi....!’ akasema huyo rafiki yangu, na maelezo yake yakamfanya rafiki wa mume wangu amuangalie kwa makini kama vile anamkanya asiwe anaongea lugha ya namna hiyo mbele yangu. Na ili kuweka mambo sawa, akasema;
‘Hana tatizo kiasi hicho, ila wanachofanya nikujirizisha tu,....kwa uchunguzi wa mwanzo hakuna tatizo, ila kwa vile amelalamika maumivu mgongoni, ndio maana wameamua kumchunguza zaidi.....’akasema huyo docta akimwangali huyo rafiki yangu, na huyo rafiki yangu akawa kama hataki kuongea na huyo docta, akawa kaniangalia mimi na kusema;
‘Kwani hiyo ajali ilitokeaje?’ akaniuliza
‘Hata mimi sijajua vyema , mambo yamekuwa ya harakaharaka sana, ila watu nilio-onana nao wanadai kuwa eti mume wangu alikuwa kwenye mwendo kasi, ...ndio ikatokea hiyo ajali, gari likawaka moto...’ nikasema.
‘Mhh, mumeo aendeshe kwa mwendo kasi, mbona hana tabia hiyo,lakini ....’akasita kidogo na kugeuka kumwangalai huyo docta, na haraka akaniangalia mimi na kusema;
‘Na hiyo ajali ilitokea wakati anatokea ....wapi?.’akasita kidogo na kumalizia hiyo `wapi’ na kugeuka kumwangalia docta inaonekana hakuwa na amani kuwepo huyo docta. Na huyo docta akawa anajifanya hatuangalii sisi
‘Sina uhakika sana....maana kama ninavyokuambia mambo yametokea kwa haraka sana,..na nilipofika nyumbani, haraka tumekuja huku, na akili ilikuwa imeshataharuki,...sina uhakika sana alikuwa katokea wapi...’nikasema na doca akasema.
‘Atakuwa alitokea maeneo ya huko kwenu, na sio kazini, kama angelitokea kazini angekuwa upande mwingine wa barabara...ukiangalia lile gari lilivyokuwa ...’akasema docta, na huyo rafiki yangu akasema.
‘Yaah, itakuwa hivyo....lakini mbona hakuwa na mwendo kasi kiasi hicho, au ni kwa vile......’akasema na huyo docta akamkatiza.
‘Kwani siku ya leo ulionana naye, uliona akiwa anaendesha gari...?’ akauliza na mimi nikainua kichwa kumwangalai rafiki yangu ambaye alikuwa katulia na nilipoona hajibu kitu, mimi nikasema;
‘Siwezi kufahamu vyema alitokea wapi, lakini kwangu nijuavyo, kama alikuwa kaenda kumuona huyo mzazi aliyesema, basi atakuwa katokea njia inayotokea kwako, nakumbuka kama alitaja maeneo ya huko unapokaa...’nikasema.
‘Alikuambia anakuja kumuona mzazi ...?’ akaniuliza huyo rafiki yangu, na docta akasema kabla huyo rafiki yangu hajajibu;
‘Unafahamu ile kona ya barabara ya kuingia barabara inayotokea bara bara kuu, pale ndipo ajali ilipotokea, sasa kwa mtizami wa haraka unaweza kabisa kujua gari hilo lilitokea wapi, ni kweli alikuwa katokea maeneo ya huko kwenu, .. ‘akasema.
‘Na ile kona mbaya, ukijifanya unajua kulizungusha gari, linageuka, kuna kona halafu kuna kilima...lakini mimi hapo sijawa na uhakika, kwa jinsi nimjuavyo shemeji,....haendeshaji gari kwa mwendo kasi kihivyo, ilikuwaje mpaka afikie hatua hiyo, na wakati huo alikuwa akielekea nyumbani kwake?.’akauliza huyo rafiki yangu.
‘Kwakweli hapa nilipo nashindwa hata cha kuongea, maana sielewi, ni kitu gani kilimfanya aendeshe gari kwa mwendo kasi, ...sijui alikuwa kalewa, au alikutwa na janga gani, maana siku hizi kama unavyojua, mume wangu kabadilika, amekuwa mlevi...’nikasema.
‘Unahisi ana tatizo, ....?’ akaniuliza huyo rafiki yangu.
‘Ndio hapa nawaza hivyo, na sijaweza kupata jibu, .....kwani mume wangu akiwa kalewa, hapendi kuendesha gari, huwa anamuita mdogo wake, .....mimi nahisi kuna jambo jingine limetokea likamfanya akimbize gari...sijui ni jambo gani, na pili alipopatwa na hiyo ajali, yeye alichojua ni kukimbilia nyumbani, ina maana hakutaka akutwe kwenye gari, hakutaka apelekwe hospitali, kwanini...’nikawa naongea kama kujiuliza.
‘Lakini kwa ujumla hakuwa amelewa hilo..nina uhakika nalo.......’akasema huyo rafiki yangu.
‘Una uhakika gani na hilo,kuwa alikuwa hajalewa,...kwani mlionana naye wapi, wakati mimi na wewe tulikuwa wote nyumbani kwako, na usiseem kumtetea shemeji yako maana namfahamu sana siku hizi, yeye siku hizi keshakuwa mlevi....’nikasema huku nikiona uchungu.
‘Mimi sina uhakika, hiyo ya kulewa, maana kama akiwa kalewa, huwa anamuita mdogo wake kumuendesha...lakini yote yawezekana huenda kwa vile mdogo wake, hakuwepo kazini, akaona aendeshe mwenyewe..na wakati keshakunywa ...na kunywa ni kunywa, unaweza unasema ninywe kidogo, ukaongeza, na kuongeza...’nikasema na rafiki yangu huyo akawa kama anataka kusema kitu lakini akasita, na wakaangaliana na docta ambaye mara kwa mara alikuwa akiongea na simu. Na alipotuona tupo kimiya akatusogelea na kuuliza.
‘Ninataka kumuona mtoto, ...’akasema huyo docta akimwangalia huyo rafiki yangu, na huyo rafiki yangu akawa anamkwepa wasiangaliane, na kugeuka kuniangalia mimi, na mimi nikadakia na kuuliza
‘Mtoto wa nini bwana, wewe kwa sasa hutakiwi kuondoka hapa, ...nataka uwe karibu ili akija docta uweze kumuuliza maswali ya msingi...’nikasema na huyo rafiki yangu akasema;
‘Sasa kuna kitu naweza kusaidia,...maana ulivyonipigia simu, ulisema unahitajia kuongea na mimi, ..inaonyesha kuna jambo unataaka nilifanye.?’ Akasema na wakati huo simu ya huyo docta, ikalia, na huyo docta akasema samhani na kuchepuka pembeni, na mimi hapo nikapata muda wa kuongea na rafiki yangu, sikutaka maongezi yangu yasikiwe na huyo docta, nikamgeukia rafiki yangu na kusema;.
‘Nilikuwa nataka unifanyia kazi maalumu, ni kazi ambayo sikuwa nataka ifanywe na mtu mwingine...,lakini kwa sasa sina jinsi, na kutokana na huyo rafiki wa mume wangu, nimeingiwa na hamasa, na mawazo yake, ...’nikasema nikiashiria kwa kichwa kumuonyesha rafiki wa mume wangu ambaye kwa muda huo alikuwa mbali kidogo akiongea na simu.
‘Unamaanisha huyo docta, ehe...mawazo yake kuhusu nini hasa..?’ akaniuliza.
‘Kwanza alianza kwa kusema kuwa eti kuna tatizo kati yangu mimi na mume wangu, ndio maana mume wangu kaamua kunywa kupitiliza, kitu ambacho sizani kama kina ukweli ndani yake, ..mimi nahisi ni uamuzi wake tu kwa vile kaona ndio sehemu ya starehe zake ...hilo nimelisema na tumeona kuwa sio kiini cha tatizo,....’nikasema.
‘Wewe umelithibitisha hilo kuwa mumeo hana tatizo na wewe, au ...docta ndiye kalithibitisha baada ya kuongea na wewe...?’ akakatisha huku akimwangalia huyo docta, ambaye alikuwa akiongea huku akituangalia mara kwa mara, kama vile anaongea jambo linalotuhusu sisi.
‘Kama lingekuwa ni tatizo kati yangu mimi na mume wangu, nisingeshindwa kulijua, na tungeliliongelea wenyewe, na isingelikuwa ni tatizo, kati yetu wawili, hakuna mwenye kumuogopa mwenzake. Na kwa mtizamo huo, ndio hapo ninakuja na wazo jingine kuwa kuna tatizo nje..tatizo hilo linaweza kuwa limetoka nje,huwa sipendagi kuingilia maisha ya mtu, si unanifahamu zangu...lakini kwa hali iliyofikia sasa , naona kuna haja ya kumchunguza mume wangu,...kwani kwa mtizamo wangu, naona tatizo hilo sasa limeingilia anga zangu...’nikasema.
‘Limeingilia anga zako kwa vipi?’ akaniuliza.
‘Wewe huoni, kama imefikia hivi, nakosa amani, siwezi kutuliza kichwa changu kwa ajili ya maendeleo , kwajili ya familia yangu, huoni kuwa ni tatizo ndani ya anga zangu,kwa hali hiyo mimi siwezi kukubali kuliachia hivi hivi, ni lazima nifenya kitu,..na ni vyema nikamuwahi huyu mtu, aliyejaribu kugusa anga zangu,...naona sio kujaribu tu, inavyoonyesha ni kuwa keshaingia ndani, na kwa namna hiyo, basi kanigusa pabaya,...nitapambana naye...’nikasema na yeye akawa ananisikiliza.
‘Kwa vipi , mpaka ukahisi hivyo, mimi sioni kuwa kuna tatizo hapo, kama ni ajali huwa zinatokea, inawezekana mtu ukatahayri, au ....inaweza ikatokea msongo wa mawazo, ..labda kama kuna jingine, lakini hebu nikuulize, hayo unayoyawaza wewe ni kutokana na mawazo yako wewe mwenyewe, au ni mawazo ya huyo rafiki yako, ?’ akauliza
‘Hata kama ni mawazo yake, lakini mimi mara nyingi sishinikizwi na mawazo ya watu,nafanya kutokana na jinsi hali ilivyo, kama kuna ukweli ndani yake, na ili nijue hilo natakiwa nifanye uchunguzi,...kwa hali ilivyo, siwezi kusema nafanya hili kutokana na shinikizo, nafanya hivi kwa vile naona ndio njia sahihi, ya kwanza kujua ukweli, pili, kuchukua hatua, ndio maana nimekuita hapa, nataka kukupa kazi,...nataka hili ulifanyie kazi mara moja...’nikasema.
‘Mhh, bado sijakupata,unataka mimi nifanyeje hapo,maana usije ukachunguza kitu ambacho umekitaka wewe mwenyewe,,...labda kama unataka nichunguze kiini cha ajali, hilo nitalipata kwa polisi moja kwa moja, halian shida, au unachotaka wewe ni kumchunguza mume wako ili kujua ana tatizo gani, niweke sawa hapo..’akasema huyo rafiki yangu.
‘Mimi kwasasa, nahisi mume wangu ana kitu ananificha,kuna jambo linamsumbua akili yake na hataki kuniambia ni jambo gani,...na kama hataki kuniambia ina maana ni jambo lisilopendeza, ambalo huenda mimi silitaki, au sitakubaliana nalo, au ni jambo keshalifanya na anaogopa litaharibu ndoa yetu, yote hayo yawezekana...’nikasema na kutulia kidogo halafu nikaendelea kuongea;
‘Ama kwa hii ajali naona ni mlolongo wa matukio, ambayo yanamuandama, huenda kwa namna moja au nyingine, yanaweza kuwa na uhusiano na hali iliyokuwepo kabla,...huo ulevi wake, unatokana na nini hasa, kama ni msongo wa mawazo, ni mawazo ya kitu gani,...yote haya ni muhimu kuyafahamu, ili kuondoa hili jinamizi linalotaka kuikumba nyumba yangu, familia yangu na ndoa yangu na wewe naona ndiye mtu unayeweza kunisaidia.....’nikasema.
‘Ok, kwahiyo wewe hasa unataka nifanye nini?’ akaniuliza.
‘Fanya ufanyalo, ila cha muhimu, nakuomba, na nasisitiza, mimi sitaki kashifa, ..na hili tumeshaonywa na wazazi wangu mara nyingi,..sasa kama kuna tatizo nataka tuliwahi mapema kabla halijafika kwa wazazi wangu,...kutokana na mtizamo wa huyo rafiki wa mume wangu, yeye anahisi kuwa huenda mume wangu ananisaliti...kitu ambacho sikubaliani nacho...mume wangu hawezi kufanya kitu kama hicho, namfahamu sana mume wangu...lakini hoja zake zinanitia mashaka, ni kama vile anafahamu jambo fulani kuhusiana na hilo...na hapo naingiwa na mashaka, kuwa huenda kua tatizo..kuna kitu kimetokea,...tukitafute haraka iwezekanavyo, ni kitu gani, ...hiyo ni kazi ndogo kwako’nikasema.
‘Eti kakusaliti, una maana gani kusema amekusaliti?’ akaniuliza huyo rafiki yangu akionyesha mshangao au wasiwasi....
‘Ina maana wewe hufahamu maana ya kusaliti..kama ana muhusiano na mwanamke mwingine wakati yeye ni mume wa mtu, utasema hilo ni nini, kama sio kunisaliti ni nini hapo, acha hiyo, au kwa vile hujaolewa nini, unaona ni kitu kidogo sana....., hapo keshavunja masharti ya ndoa,, na mimi hilo sitalivumilia,na kashfa kama hiyo haikubaliki kwenye familia yetu, na ndicho wazazi wangu walikuwa wakinisema kuwa eti familia ya mume wangu imegubikwa na mambo hayo....na mimi sitakubali hilo litokee’nikasema.
‘Mhhh..na kama limetokea utafanyaje, utachukua hatua gani....?’ akaniuliza na mimi nikamgeukia na kumtizama kwa muda, nikasema.
‘Kwanza tujue, ....cha kufanya , nikijua mwenyewe....siatavumilia uchafu huo, nitapambana na huyo aliyemghilibu mume wangu, hatanisahau maishani, kama anatadiriki kuishi....’nikasema nikitoa macho ya chuki na hasira.
‘Mhh, rafiki yangu ndio imekuwa hayo,...lakini kama ulivyosema kuwa unamfahamu vyema mume wako, sio mtu wa kufanya mambo hayo, na kama kafanya basi huenda kafanya hayo kutokana na shinikizo, na tujue kuwa mengine, tunaweza tukajikuta tumeyataka wenyewe, ..lakini kwa vile yametugusa , ...kwa vile watu wameingiza fitina zao, wakabadili nafsi zetu zenye nia njema, ...na kwa jinsi hiyo,hata lile lengo zuri la awali linageuka kuwa baya,....’akasema huyo rafiki yangu, na nilitaka kumkatiza, lakini nikaona nimpe nafasi ya kuongea huenda ana jambo anataka kunishauri.
‘Rafiki yangu tusje tukawa tunapigana na kivuli chetu wenyewe. Oh, rafiki yangu mbona imefikia hatua hii, sioni kwanini ufikie hatua ya chuki kiasi hicho....nashindwa kukuelewa rafiki yangu, maana sio wewe ninayekufahamu, ...mimi naona hayo yametokea kwa nia njema tu, ...’akasema huyo rafiki yangu akiwa kshika shavu na kuonyesha uso wa huruma , akawa ananiangalia kama haniamini kuwa ndio mimi rafiki yake, kweli nilikuwa nimebadilika kwa hasira, na mimi sikutaka kumpa nafsi nikamkatiza kwa kusema.
‘Wewe unaongea hivyo kwa vile hujaolewa,, ...unasikia nikuambie, ndoa inafungamana na masharti, na moja ya sharti kubwa ni kutokakuzini nje, nikiwa na maana kutembea nje ya ndoa, hilo ni kosa kubwa sana, je mimi kama mwanandoa ulitaka nifanye nini,... mimi kama mke niliyeolewa kihalali, sitavumilia hiyo kashfa,...’nikasema kwa hasira na kutoa macho hadi rafiki yangu akawa ananiangalia kwa amshaka.
‘Na unaposema kwa nia njema, nia njema gani hiyo unayoiongelea wewe, mimi hapo sikuelewi, maana nilitarajia uwe wa kwanza kuniunga mkono, ...sikuelewi, ....sasa nataka ulichunguze hilo haraka iwezekanavyo, kabla halijafika mbali, ..kwanza tujue je ni kweli kuna kidudu mtu, je ni kweli kuna tatizo la namna hiyo, au kuna tatizo jingine..........moyo wangu hauna wasiwasi sana, na usaliti wa ndoa, lakini mmh, kutokana na kauli ya rafiki yangu, nimeingiwa na mashaka....’nikasema na rafiki yangu huyo akawa ananiangalia huku akionyesha kutaka kusema jambo, lakini sikutaka kumpa nafasi nikaendelea kuongea.
‘Nataka umchunguze mume wangu,...nataka hili lijulikane mapema, hata kabla hajatoka hospitali, ... sitaki mimi niingie huko moja kwa moja, lakini wewe ni rafiki yangu ninayekuamini, ndio maana kila kitu tunaambizana, na huwa tunashauriana kwa kila jambo, ....wewe ndio mimi, kwahiyo chukua nafasi yangu na umchunguze kiundani shemeji yako, tumfahamu huyo kidudu mtu, ambaye ameweza kumghilibu mume wangu, siamini hilo, lakini yasemwayo yapo, huenda yupo....na kama yupo ole wake, nasema ole wake....’nikasema huku macho yamenitoka, na nilihisi rafiki yangu akiwa anaangalia sana, nikajua huenda kuna kitu anaangalia kwa nyuma yangu.
Nilipogeuka tukawa tukiangaliana na huyo rafiki wa mume wangu, na aliponiona jinsi nilivyobadilika kwa hasira, akaonyesa sura ya kushangaa, tukawa tumeangaliana kwa muda, lakini sikuwa aniona sura yake, nilikuwa nikijaribu kuiona sura ya huyo msaliti wangu, lakini sikuweza kuitambua saura ya mtu kama huyo, kwahiyo nikawa naona marue rue tu,...na akili ilipokaaa sawa, nikahisi huyo rafiki wa mume wangu anataka kusema neno, lakini akawa anasita , na mimi sikumjali sana, nikawa angeuka kumwambai rafiki yangu aondoke, na nilipogeuka nikakuta hayupo, keshaondoka, ...nigaueza uso huku na kule sikuweza kumuona, ni kama mu aliyeyuka na kupotea hewani.....
NB: Sehemu hii tuishie hapa, maana mambo hayajakaa sawa....
WAO LA LEO: Tujitahidi kuzilinda ndoa zenu kwa nia njema, na hili lianzie kwa kuhakikisha kuwa hatufanyi yale yatakayosababisha mmojawapo kutafuta kisingizio , tukumbuke kuwa akili, na mitizamo ya watu inatofautiana,hata kama ni mwenza wako bado anaweza asiwe sawa na wewe kimtizamo na kifikira....sasa tusitegeane kwa kusema `kwanini mimi..’ kwani kwasababu gani, inaweza ikaja kuleta madhara makubwa.
Ni mimi: emu-three
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment