Upande wa mshitakiwa mkuu, hali haikuwa shwari, kwani
mshitakiwa huyo kabla hajatulia kwa mshituko wa mwanzo wa kuitwa shahidi ambaye
kwa mtizamo wake, huyu mtu alikuwa keshafariki, na sio yeye tu, watu wengi
wanaomfahamu huyo mtu, walikuwa wakijua ni marehemu. Sasa kuonekana kwake hapo,
kulimfanya mshitakiwa mkuu akose amani, japokuwa wakili wake alimthibitishie
kuwa atamsambaratisha huyu shahidi kama alivyokuwa akiwafanyia mashahidi wote
waliotangulia.
Kabla mshituko huo haujatulia, ukaongezeka mshituko
mwingine, wa kutokea kwa mwanadada, ambaye
alijua kabisa hataweza kuwepo . Akamgeukiwa wakili wake, kama anataka
kumuuliza, lakini alimkuta wakili wake naye akiwa katika mshangao, na mshituko…na
wakili wake, alipogundua hilo akajifanya kama hakuna lolote kwake, tambo zake zilikuwa pale pale, na hata pale
aliposikia mteja wake akisema;
‘Oh, huyu mtu kapona..mbona sielewi…nakumbuka ulisema….’akasema
huyo mshitakiwa na wakili wake akajifanya kutabsamu kwa dharau, na kusema.
‘Mmmh, naona kapona, au sijui…lakini usitie shaka
nipatambana naye, leo nitakuwa na furaha ya kupambana na huyu mwanadada, maana
nilikuwa nikimsikia tu, sijawahi kukutana naye kwenye kesi….’akasema wakili
huyu huku akimtizama huyo wakili mwanadada kwa macho ya hamasa.
Kwa muda huo, wakili mwanadada alikuwa akitembea
kuelekea sehemu yake, ambapo kundi la
mmawakili au waendesha amshitaka walikuwa wamekaa, akapita hadi sehemu yake na
kukaa, na alipotulia na kuweka vitu vyake sawa akamgeukia muedesha mashitakai
mwenzake aliyekuwa akiongoza hiyo kesi wakateta kidogo.
Baadaye akageuka upande ule wa washitakiwa na macho yake
yakagongana moja kwa moja na mshitakiwa mkuu, na wakili mwanadada, akatikisa
kichwa kama anakubali jambo, na mjumbe,ambaye alikuwa bado kajawa na uso wa
mshangao na mshtuko, akamgeukiwa wakili wake, na kusema;
‘Sasa uwe makini, ….huyu mwanadada ni mwerevu sana,…nataka
leo tuwahakikishie kuwa huyu dada si chochote, fanya ufanyalo, …pambana naye,
najua unajua ni nini cha kufanya…..’akasema huyo mshitakiwa mkuu, na kukatizwa na sauti ya waendesha mashitaa.
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, kwa vile mwenzangu ameshafika, na
tulikuwa tumempanga yeye kama kiongozi wa leo, nitampisha yeye aendelee na kesi
yetu,…’akasema na hakimu akatikisa kichwa kwani mwanzo aliwahi kuuliza yupo
wapi wakili ambaye aliandikwa kuwa ndiye ataongoza hiyo kesi , akajibiwa kuwa
yupo anakuja..
Kwa kipindi kile, alipokuwa akiuliza muheshimiwa hakimu,
kuwaauliza kambo hiyo ya waongoza mashitaka, wengi walikuwa hawakufahamu hakimu
alikuwa na maana gani, kwa kwa taarifa za mitaani za uvumi, zilizokuja kuenezwa
siku hiyo, ni kuwa wakili mwanadada, hali yake sio nzuri, anahitajika
kusafirishwa nje kwa ajili ya upasuaji wa ubongo, kwani ile ajali ilimuathiri
kwenye kichwa…ndio maana haajonekana na hataonekana tena kwenye kesi hiyo.
Wakili mwanadada akasogea na kumwangalia huyo kijana na
kumpa moyo, halafu akageuka kuangalia kambi ya utetezi, na macho yake yakatua
kwa mshitakiwa mkuu, akamkazi a macho mshitakiwa huyo kama vile anamsoma kwenye
mawazo yake, halafu akageuka kumwangalia wakili, akatabasamu, lakini wakili
yule wa kambi ya utetezi, alikuwa kakunja uso, ….hakujibu lile tabasamu,
bali,alibenua mdomo kidogo kuashiria dharau
‘Kijana, ….tuambie, wewe ulikuwa unafanya kazi gani kwenye
kijiji?’ akaulizwa.
‘Kazi yangu kubwa ilikuwa ni ulinzi shirikishi…’akasema.
‘Ni nani aliyekuwa akiwasimamia kwenye kazi yenu hiyo?’
akaulizwa.
‘Ni Jemedairi, ambaye sasa ni marahemu…’akasema.
‘Jemedari alikuwa na mamlaka gani kwenye kijiji…?’
akaulizwa.
‘Yeye alikuwa kiongozi wa walinzi shirikishi,..’akasema.
‘Kwahiyo yeye aliteuliwa tu kama kiongozi, ila kuna mkubwa
zaidi yake, au sio?’ akaulizwa.
‘Mhh, tunaweza kusema, hivyo, maana kwenye kijijini kuna
makundi mbali mbali ya kufanya shuguli mbali mbali, a kila kundi kunateuliwa
kiongozi wake, kwahiyo wenye kundi letu la ulinzi shirikishi , Jemedari ndiye
aliyekuwa kiongozi wetu.
‘Hiki kikundi cha walinzi shirikishi kwanini kilianzishwa?’
akaulizwa.
‘Ni baada ya kuona kuwa kuna matukio mengi ya uhalifu, basi
likatokea pendekezo kuwa kuwe na kundi kama hilo….’akasema.
‘Kwahiyo kundi hili, lilianzishwa na huyu jemedari, au
jemdari alichaguliwa kama mkuu wa hilo kundi?’ akaulizwa.
‘Jemedari alichagulia kama mkuu wa hilo kundi, …..labda
nikuelezee zaidi ni kuwa kijiji kina mkuu wake ambaye ni mjumbe, na huyo mjumbe
ana halimashauri zake, au makundi mbali mbali ya utekelezaji, na halimashauri
hizo zina viongozi ambao hupokea amri kutoka mjumbe..’akasema.
‘Kwahiyo mjume ndiye kiongozi wa juu wa hilo kundi na ndiye
mwenye mamlaka ya mwisho ya kijijini au sio?’ akaulizwa
‘Ndiyo…’akasema.
‘Kwahiyo mjumbe alikuwa na mamlaka ya kuliamrisha hilo
kundi, hata kama kiongozi wake hayupo?’ akaulizwa
‘Ndiyo…’akasema
‘Sasa turudi nyumba kidogo, katika maelezo yako ulisema wewe
umewahi kulitumikia hilo kundi lenu la ulinzi shirikishi,toka lilipoanzishwa na
ulikuwa mdogo kuliko wote, na karibu kila kazi uliwahi kuhudhuria, je unaweza
kutkumbusha kidogo, ni kazi ipi ambayo ulihudhuria, ambayo kiongozi wenu wa
kundi hakuwepo, na akawa msimamizi ni mjumbe….? akaulizwa.
‘Mbona zipo nyingi sana….mojawapo ilikuwa ya kwenda kwenye
nyumba ya mwanamama, na kumtoa kwa nguvu, baba wa kufikia wa mwanamama
huyo…..’akasema.
‘Ni nani huyo mwanamama..?’ akaulizwa.
‘Ni yule Mwanamama, ambaye ambaye alifungua kesi ya kuwa
kadhukumiwa mali yake…’akasema.
‘Kwanini mliambiwa muende kumtoa?’ akaulizwa.
‘Tuliambiwa alikiuka amri iliyomtaka atoke na kuicha hiyo
nyumba ili iwe mikonono mwa wahusika…..’akasema.
‘Je ni nini kilitokea?’ akaulizwa.
‘Tuliambiwa tutumie nguvu kumtoa, maana alikaid amri halali
ya mkuu wakijiji…’akasema.
‘Mliambiwa mtumie nguvu gani?’ akaulizwa.
‘Tuliambiwa tumfunze adabu….na tukiambiwa hivyo, sisi
wenyewe tunajua ni nini la kufanya, …’akasema.
‘Ni nini la kufanya , una maana gani kusema hivyo?’
akaulizwa.
‘Tulishawahi kufanya kazi kama hizo, na mkuu huyo
alishatuambia kuwa akisema kufunza adabu mtu mnahakikisha huyu mtu hawezi hata
kutembea….’akasema.
‘Kwanini kiongozi mkuu wa kijiji alifikia kusema hivyo, ina maana hamkuwa na tabia
hiyo ya kufunza adabu kabla, mpaka ikafika wakati kiongozi huyo mkubwa wa kijiji kuwalaumu,…..?’
akaulizwa.
‘Kwakweli tukiwa na kiongozi wa kundi, Jemedari, huwa yeye
hakubali kabisa mtu yoyote kupigwa, hasa kumtoa mtu damu, hapendi kabisa,
japokuwa yeye mwenyewe ana ahsira sana…’akasema
‘Je kwanini siku hiyo mliyokwenda kumtoa huyo mzee kwa
nguvu,hamkuandamana na Jemedari? Akaulizwa.
‘Nakumbuka ni kipindi ambacho Jemedari alikuwa amefiwa na
mdogo wake,….yeye alikuwa kwenye msiba….’akasema.
‘Kwahiyo mlipoambiwa mmfunze adabu huyo mzee, mlijua ni nini
cha kufanya,kama alivyowahi kuwaambia mfanye kama anavyotaka yeye huyo kiongozi
wa kijiji …?’akaulizwa na hapo mshitakiwa akamgeukia wakili wake na kusema;
‘Mbona huweki pingamizi huoni ….’akalalamika na wakili yake
akaweka pingamzi lakini hakimu akataka swhali hilo lijibiwe.
‘Unaona,..mimi najua ni swali gani linahitajika kuwekewa
pingamizi , huyo mwanadada ni mjanja sana haulizi swali tu kwa nia ya kuuliza,
anajua ni nini anachokifanya, lakini hata hivyo mimi ninajua zadi yake, subiri
muda wangu ukifika uone ni nini nitakachokifanya….’akasema huyo wakili.
‘Ndio tulijua ana maana gani, na tukafanya kama
alivyotarajia..’akasema.
‘Kwahiyo mkafanya nini…?’ akauliza na wakili mwanadada
alikuwa kama anaista akijua huenda swali hilo lingeliwekewa pingamizi lakini
haikutokea hivyo, akamsikiliza shahidi akiongea
‘Ndio hivyo….tulianza kumvunja nguvu za miguu, kwa kumpiga
na virungu, na wengine wakimchapa vibogo, na hata kumpiga virungu mabegani, na
kwa vile huyo mzee, alianza kupambana na sisi, ilibidi tutumie nguvu ya ziada,
na kwakweli wengi walimpiga mzee huyo bila huruma, mimi sikukubaliana na hilo,
na hata ukimuuliza mwenyewe mzee, atakuhakikishia kuwa mimi nilikuwa nikiwazuia
wenzangu wasizidishe …kipigo…’akasema huku akitupa jicho kuangalia kule
alipokaa huyo mzee.
‘Ina maana nyie kundi la watu….mlikuwa wangapi?’ akaulizwa.
‘Tulikuwa watano…vijana mashababi…’akasema huyo shahidi na
watu wakaguna kwa huruma.
‘Vijana watano wenye nguvu mkaanza kumpiga huyo mzee, bila
huruma..na nini kilitokea baada ya hapo, ….?’ Akaulizwa.
‘Kwa vile mzee huyo alikuwa sio lele mama, ilichukua muda,
na tukamzidi nguvu, na alipozidiwa nguvu wenzangu ambao labda waliumizwa,
walichukua nafasi hiyo kulipiza kisasi,wakawa wanapiga kama wanataka
kuua…’akasema.
‘Una uhakika kupiga huko, sio kwa jinsi alivyoagiza huyo
kiongozi…?’ akauliza na wakili mtetezi akaweka pingamizi na hakimu akakubali
hilo pingamizi.
‘Sawa je kuna kazi gani, zaidi ya hiyo ambayo mkuu wa
kijiji, alishiriki yeye mwenyewe…kwa kuwatuma,bila ya kushirikishwa huyo
kiongozi wetu, wa karibu?’ akaulizwa.
‘Kuna kazi maalumu, tulipewa na vijana wenzangu, hiyo
ilikuwa kazi ya siri, hata mimi mwenyewe sikujua ni kazi gani, hadi tulipofika
kwenye eneo,…’akasema.
‘Ulipofika kwenye eneo uliambiwa ni kazi gani?’ akaulizwa.
‘Mimi nilichoambiwa ni kumwangaia mafuta nyumba yam zee wa
kijiji, huyo baba wa kufikia wa Mwanamama, na nilipouliza ni kwanini,
nikaambiwa nifanye nilivyoagizwa, na nikimaliza niondoke….’akasema.
‘Je ulifanya hivyo, kama livyoagizwa?’ akaulizwa.
‘Ndio, maana moja ya mafunzo yetu, tuliyopewa ni kuwa
ukiamrishwa na kiongozi, hutakiwi kukataa, amri moja, piga, au fanya, unafanya
kama ulivyoamrishwa, ukisita, wewe utapigwa, au hata kuuwawa..kwani hiyo ni
amri kama mpo vitani….’akasema.
‘Ina maana mlikuwa mkipitia mafunzo ya jinsi gani ya kufanya
kwenye kazi zenu?’ akaulizwa.
‘Kila mara tunakuwa na mafuzo, na kuna mafunzo ama hayo, ya
jinsi gani ya kupambana na mhalifu…’akasema.
‘Ukisema kama haya, ina maana hata hayo ya kumpiga huyo
mzee, na kuchoma nyumba yalikuwa moja ya mafunzo yenu…’hapo pingamizi
likawekwa..na hakimu akakubali
‘Kwahiyo ukagundua ni kazi gani mliyotakiwa kufanya siku
ile?’ akaulizwa.
‘Ndio nikagundua, ….’akasema.
‘Kwahiyo unaweza kuiambia mahakama hii ni kazi gani hiyo
ambayo kikosi chenu kilitumwa kuifanya, ..?’ akaulizwa, na pingamizi likawekwa
na hapo hakimu akasita kidogo, na baadaye akasema pingamizi limakataliwa
shahidi ajibu swali.
‘Ni kazi ya kwenda kuchoma nyumba ya….’kabla mshitakiwa
akasema kwa sauti;
‘Mwongo huyo….’akasema na watu wakashikwa na mshangao, na
hakimu akagonga rungu yake kwenye meza na kusema ;
‘Futateni taratibu za mahakama, na wewe wakili wa utetezi
mzuie mtu wako asivunje taratibu za mahakama…’
Na wakili wa utetezi akaomba msamaha, na kusema kosa hilo
halitarejewa tena halafu akamgeukiwa mteja wake, na kumnong’onezea kitu, lakini
mteja wake, akaonekana kukasirika, na ilionyesha kama vile hana amani tena na
huyo wakili wake
NB: Je ni nini kitafuata..
WAZO LA HEKIMA: dhuluma na ukatili, hauna heri, na mtendaji wa mambo
hayo, hana amani , na kila mara hujishuku au kuwashuku wenzake vibaya. Kwanini
uwe na maisha yasiyo na amani, kwanini ujitese kwa kutenda dhuluma wakati
unafahamu athahri zake,…kumbuka kuwa dhuluma katu haina mwisho mwem
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Hakika hapa ni bonge la shule kila uingiapo hapa ni kukusanya elimu tu. Pia wazo la leo ni funzo zuri sana...PAMOJA DAIMA.
Mmmh, haya ndugu wa mm,
Post a Comment