Kesi ilianza tena, na watu waliofika siku hiyo ilikuwa
haijawahi kutokea, japokuwa walipewa habari mapema kuwa hawataruhusiwa
wasikilizaji , lakini watu hawakusikia hilo, habari ya kesi hii ilikuwa
imetapaa sehemu kubwa, na kila mmoja alitaka kufika ajionee mwenyewe.
Walianza
kufika mtu mmoja mmoja, na kila aliyefika aliaambia asikaribie eneo hilo la
mahakama kama haruhusiwi, lakini kika muda ulivyozidi kwenda ndivyo watu
walivyozidi kufika, na hata ilipotimia muda wa kesi, umati wa watu ulikuwa
umejezana, eneo karibu na mahakama,
ikawa ni kazi ya ziada ya walinzi wa usalama ambao walijitahidi
kuhakikisha kuwa hakuna tatizo lolote lingeliweza kutokea tena.
‘Hatuwezi kuwaruhusu watu kuingia tena eneo hili mahakama, na
mgari yote ya wahusika muhimu yataingia moja kwa moja ndani kwa kupitia mlango
huu maalumu, nay a watu wengine ambao ni wasikilizaji tu , hatutaweza
kuyaruhusu kuingia ndani au kusimama eneo hili la karibu ya mahakama…’tangazo
likatolewa.
Ni kweli lawama kubwa
ilikuwa imeelekezwa kwa walinzi wa eneo hilo la mahakama kuwa wao walizembea
hadi yule matu akafika eneo hilo na kusababisha ajali ambayo imekuwa ni gumzo
la watu wengi, kila mmoja akisema lake..
‘Hebu jiulizeni, kwanini siku ile ya kesi mlango wakuingiza
magari haukufunguliwa mapema, inaonekana kulikuwa na njama fulani zilipangwa…ili
gari hilo la mwanadada, lisiingie mapema ndani na huyo mtu afike hapo na
kumgonga, ilikuwa imepangwa hiyo……’wakawa wanasema watu. Hata hivyo uchunguzi
uliofanyika haukugundua lolote kuhusiana na lawama hizo. Kilichoongelewa ni
kuwa huyo jamaa alikuwa mlevi tu, ….
‘Haiwezekani, kuna kitu kinafichwa hapo…’wakasema watu
walikuwa wakifuatilia sana hiyo kesi.
‘Lakini kama mahakama haiwezi kudanganya,..inawezekana ni
kweli, na huyo mlevi mwenyewe wamemchukulia hatua gani?’ wakauliza watu.
‘Nasikia kawekwa ndani na pombe zilipoisha akawa anapiga
mgaoti kuomba msamaha, kwani mwajiri wake anamfukuza kazi na yeye ndio katoka
kuajiriwa karibu, na kukabidhiwa hilo gari, kwa ajili ya kumchukua bosi
wake…’wakasema .
‘Yaani kumbe hata hilo gari sio lake….kweli hapo kaingia
choo cha kike,huyo kazi hana…’mmoja akasema.
‘Nasikia huyo bosi walifika kumwekea dhamana, lakini
akaambiwa dhamana kwa sasa haitakubalika, kwani kuna uchunguzi bado
unafanyika…’akasema mtu mmoja.
‘Hamuoni kuwa hapo kuna jambo, kwanini kama ni mlevi tu,
waendelee kumshikilia, …nahisi kuna jambo hawataki lijulikane, au ni kutokana
na uzembe wao, au kuna uchunguzi ambao huenda wakiusema utaharibu mpangilio wa
kesi yao…’wakazidi kuongea wachunguzi wa mambo.
‘Lakini yote tutayaona siku ya kesi,…tusubiri siku, ni mimi
ni lazima nifike japokwua wametoa tanagzo kuwa wasikilizaji hawataruhusiwa,
kuingia eneo la mahakama, lakini hata nikikaa nje, kusubiria inatosha.
‘Yaani uache shuguli zako kwa ajili ya hiyo kesi, halafu
utapata nini, badala ya kuhangaika na kutafuta riziki ya watoto wako, wewe
unahangaika na kesi za watu, ili kupata umbea….’akasema mwenzake.
‘Hii nayo ni ajira, hujui kuwa mimi ninauza taarifa kwa
gazeti moja la udaku,…mjini hapa,…’akasema na wote wakacheka.
******
‘Hivi leo wakili mwanadada atakuwepo?’ ilikuwa swali la kila
mtu, nawengi walifika hapo kwa ajili ya kumuona yeye, kwani kulikuwa na uvumi
mwingi, wengine walifikia kudai kuwa wakili mwanadada alipogongwa, aliathirika
ubongo, na hadi sasa hajijui…
‘Mna uhakika na hilo?’ wakaulizana watu.
‘Inawezekana kuna ukweli, maana tangu litokee lile tukio
huyo mwanadada hajawahi kuonekana hadharani…’akasema mtu mmoja.
‘Inawezekana aliumia sana, lakini hospitalini hayupo tena,
mimi nilifuatilia, nikaambiwa keshatoka, ila mimi nahisi wanafanya hivyo kwa
ajili ya usalama wake, kwani imebainika kuwa kuna watu huenda wanataka kumuua..’akafafanua
mtu mmoja.
‘Lakini kwanini watake kumuua, wakati ni mtetezi tu wa
wanyonge?’ akauliza mwanamama mmoja.
‘Kama anatetea wanyonge, ina maana kuna watu hawapendi
hivyo, kwasababu kwa yeye kufanya hivyo, hawatapata hicho wanachokitaka kwa
hawo wanyonge,….’akasema mwanaume mmoja aliyekuwa karibu naye.
‘Hata wafanye nini, mimi nina imani kuwa mwisho wao
umeshikafika, ni kutapatapa kwa mfa maji…’akasema huyo mama.
‘Usiseme hivyo wewe mwanamke, wewe unacheza na pesa, hawo
wenye pesa wanaweza wakafanay hii kesi ikapigwa tarehe, hadi watu wakachoka,
huoni ile kesi ya yule mwanadada aliyekuwa kadhulumiwa mali zake, mpaka sasa
inapigwa tarehe…’akasema huyo mwanaume.
‘Lakini wametoa sababu za msingi, kuwa wanahusika na kesi
ile , wengi wapo kwenye kesi hii, kwahiyo wameona cha msingi ni kumalizana na
kesi hii, ambayo ina umuhimu wake sana. Halafu yule hakimu aliyekuwa akisimamia
kesi hiyo alipata uhamisho, akaletwa hakimu mwingine, na huyo hakimu mwingine
kabla hajaanza kazi, na yeye, akapatwa an dharura, mama yake yupo taabani,
anaumwa sana ni wa kusikilizia, kwahiyo kaondoka kumuona mama yake.
‘Kwanini hayo yatokee …wewe hujiulize tu , unaweza ukaona ni
mambo ya kawaida, lakini wenzetu wana kila mbinu…..wewe chezea na watu wenye
pesa. Wewe huoni jinsi mataifa makubwa yanavyofanya, mfano huo tu, utakuonyesha
kuwa, pesa inaongea. ….’akasema huyo mwanaume.
‘Sasa hayo ya mataifa makubwa yanahusiana vipi nah ii
kesi…?’ akauliza huyo mwanamke.
‘Angalia kwa mfano wao wameanzisha demokrasia, kuwa wengi
wape, lakini angalia pale wanapotaka mtu fulani asiwepo kwenye madaraka,
demokrasia hiyo hiyo inaoat makengeza, utasikia visingizio kbao, na wakiona
vipi, wanasimamia vikundi vya upinzani kuhakikisha nchi hiyo haina usalama….’akasema
huyo mwanaume.
‘Lakini hayo yanahusiana vipi nah ii kesi?’ akauliza mama
mwingine, akiona kama huyo jamaa anamchanganya.
‘Hilo nimekutolea mfano jinsi gani pesa ilivyo na nguvu…matajiri
wana kila mbinu, za kuweza kubadili hali ya hewa…’akasema na wale akina mama
wakaona huyo jamaa anawachanganya na mwanaume mmoja akauliza
‘Lakini kweli mbona kesi imeanza na huyo wakili mwanadada
hajaonekana, inawezekana kweli anaumwa, au ….?’
Lakini hata kabla kabla mtu mwingine hajasema kitu, mara
gari la wakili mwanadada likaingia mbele yake kukiwa na gari jingine, lilikuwa
kama gari la waheshimiwa wanavyosindikizwa, na walipofika tu eneo la mahakama ,
mlango wa geti ukafunguliwa haraka, na magari hayo yakaingia ndani.
Gari la wakili mwanadada lilipofika tu, akatokea mtu mmoja,
aliyekuwa kwenye gari la mbele na kuja kumfungulia wakili mwanadada, na huyu
dada akatoka kwenye gari, hakugeuka kuangalia upande uli waliokuwepo watu,
ambao walianza kusukumana kutaka kumuona vyema, …yeye kwa haraka akakimblia
kwenye jengo la mahakama, kwani kesi ilikuwa ikiendelea na yeye alichelewa
kufika.
*********
Baada ya utulivu kwenye mhakama, maana watu walishindwa
kujizuia kuonyesha hamasa, zao pale mshitakiwa mkuu wa kesi hiyo alipoletwa
mbele ya mahakama, kwani wengi walishafikia kusema mshitakiwa huyo ana nguvu za
giza, na kila akitaka kukamatwa haonekani, lakini leo kafika, kwahiyo wengi
walipomuona akiingizwa, wakashindwa kuvumilia na kuanza kusimama kumwangalia
huyo mshitakiwa.
‘Ina maana nyie hamuoni mpaka msimame…’wakawa wanalalamika
watu walio kuwa nyuma.
‘Ni maajabu, huyu mtu leo kuwepo hapa mahakamani….’akasema
mama mmoja.
‘Wewe unacheza na sheria, sheria, haishindwi na nguvu za
giza hata siku moja…’akasema mama mwingine
‘Nyie tulieni, mtaishia jela…’wakaonywa na mtu wa usalama
aliyekuwa karibu yao.
*******
‘Ndugu hakimu, kutoka na maelezo yangu hayo, nahitimisha kwa
kusema kuwa shutuma hizi dhidi ya mteja wangu ni za kusingiziwa, kwani hazina
msingi wala ushahidi halisi, zote zimejengwa kwa hisia za chuki binafsi…’wakili
akawa anataka kufungua ukurasa mwingine, lakini akagundua kuwa huo ndio ukurasa
wa mwisho wa maelezo yake.
Wakili wa utetezi akahitimisha taarifa yake , na kuinama
kidogo, kuonyesha adabu yake kwa muheshimiwa hakimu. Huyu alikuwa wakili ambaye
alitafutwa kwa ajili ya kumtetea mjumbe wa nyumba kumi, baada ya wakili wa
mwanzo kupatwa na ajali ya kugongwa na gari, akijaribu kumuokoa wakili
mwanadada.
Kikawa kipindi cha kuwaita mashahidi wa pande zote mbili,
waliitwa mashahidi mbali mbali, kutokana na mpangilia wa mwendesha mashitaka, na kila aliyeitwa kila akimaliza kutoa maelezo
yake, akiongozwa na mwendesha mashitaka, wakili wa utetezi alimuhoji, na kila
alipomaliza kuhojiwa, kwa maswali ya kisheria, ilionekana kweli, huyo wakili
mpya anaweza akabdili sura ya hiyo kesi.
‘Duuh, huyu wakili jembe, maana mashaidi wote wanaonekana
kama vile wamatumwa kuongea na maelezo
yao hayana nguvu, ..’akasema mmoja wa watu waliokuwemo humo ndani, na wakati
anaitwa shahidi mwingine, mara mlango wa mhakama ukafunguliwa, na watu
wakajikuta wakigeuza shingo kuangalia ni nani aliyeingia.
Kila mmoja akajikuta kipumua, na hata hakimu, akajikuta na
yeye akimwangalia huyo aliyeingia, na sekunde chache zikapita, kabala shahidi
aliyekuwepo hapo kuendelea kuhojiwa na watetezi.
Huyu muendesha mashitaka mpya aliyeingia, alisogea hadi kwenye meza ya waendeshaji wa mashitaka, na kukaa kwenye sehemu yake, na muendesha mashitaka akamsogelea na
kuanza kuteta naye, hawakujali kusikiliza huyo shahidi anavyohojiwa, na baada
ya kuteta kidogo, hakimu akauliza kuwa kuna shahidi mwingine.
Hapo akasimama muedesha mashitaka na kusema yupo shahidi
mwingine, na alipotaka kumataja, mara akasimama huyo wakili aliyeingia na kumnong’oneza
mwenzake, na mwenzake akatikisa kichwa na kurudi nyuma, na ilionekana kuwa huyo
muendesha mashitaka mpya aliyeingia ndiye anataka kuendelea na hiyo kesi, na kusema ;
‘Yupo shahidi mwingine muheshimiwa hakimu, …anaitwa Kijana.’na watu wakaanza kunong’ona, na kama tujuavyo minong’ona ya watu wengi, ni
ngurumo, maana hata hakimu ilibidi agonge rungu lake na kusema watu watulie na
kufuata taratibu za kimahakama.
********
Upande wa utetezi, ulikuwa kimiya, na mtu aliyeonekana
kuathirika zaidi alikuwa ni mshitakiwa mkuu, ambaye ndio kwanza kesi yake
ilianza leo, baada ya kukosekana kwenye kesi zilizopita kwasababu
zilizokubalika na mahakama.
‘Hilo jina mbona ni la marehemu, mimi nina ushahidi kuwa
kijana huyo alishafariki…’akasema huyo mshitakiwa mkuu.
‘Labda wana maana yao kuweka hilo jina, usiwe na wasiwasi
nitapambana naye,….’akasema wakili wake ambaye likuwa mtu wa kujiamini sana.
‘Shahidi wetu mwingine ni Kijana, …’akasema tana huyo
muendesha mashitaka aliyeingia alikuwa kavalia mawani, iliyoonyesha kuwa huenda
kaja kuchukua nafasi ya mwanadada, na wengi walivunjika nguvu, wakijua mtu
waliyetama kumuona hatakuwepo kwenye hiyo kesi, na mara watu wakaanza
kunong’ona kila mmoja akisema lake, na hkimu akasema;
‘Tunahitaji ukimiya, na taratibu za mahakama zifuatwe,
shahidi apite mbele..’akasema hakimu, na mara kutoka mlango wa wanaoingilia
mashahidi akatokea kijana mmoja, ambaye kwanza likuwa kava kofia pana,
lilofunikwa shemu kubwa ya kichwa chake, na akaamuriwa kulivua.
Alipolivua, kila mmoja alibakia kinywa wazi, na aliyeshindwa
hata kujizuia alikuwa ni mshitakiwa mkuu, ambaye alijikuta akisema;
‘Haiwezekani,….ina maana huyu kijana hakufa…’akasema na
wakili wake akasema;
‘Una wasiwasi gani, …wewe subiri jinsi gani nitakavyomtoa
jasho,..’akasema huyo wakili wake mtetezi.
‘Kijana hebu elezea ilivyokuwa ……..’akasema mwongoza
mashitaka, baada ya kumuuliza maswali kadhaa huyo kijana, wakati anamuongoza
kutoa maelezo yake ya awali, na kabla hajajibu mlango ukafunguliwa, na watu
wote wakageuza kichwa kumwangalia ni nani tena huyo aliyeingia, …..na
haliikabadilika ghafla, maana wengine walishindwa kuvumilia na kuinuka kuhakiki
macho yake, na ikawa ni hamsa iliyofanya dakika chache zipite, kabla hakimu
hajaginga rungu lake, kuhakikisha utulivu na sheria za kimahaka, zinafuatiliwa.
‘Kwani ni nani huyo aliyeingia…?’ akauliza mshitakiwa mkuu,
ambaye kutokana na kusimama kwa watu, hakuweza kumuona vyema huyo aliyeingia,
na kipindi hicho hakimu anaamrisha watu watulie, upande ule wa waongoza
mashitaka ulikuwa umekutana kwa pamoja, wakiteta jambo, na kuweza kumzuia huyo
mashitakiwa mkuu kugundua vyema huyo
aliyeingia ni nani,
‘Ni wakili mwanadada…..!’ akasema wakili mtetezi wa huyo
mshitakiwa mkuu.
‘Eti nini..haiwezekani….’akasema mshitakiwa mkuu, na kelele
za watu wakirudi kwenye shemu zao kukaa, na wengi wao walioshindwa kujua wapo
mahamani na kuanza kushangilia walitulia sasa wakisubiria ni nini kitafuta.
NB:Kesi hiyo, shahidi asiyetarajiwa akaingia, na wakili
aliyesubiriwa kwa hamu naye akaingia, ni nini kitafuta. Sehemu hii ni kama utangulizi wa kesi yenyewe, tuwe pamoja kwenye sehemu ijayo, je kweli pesa ina nguvu kulika haki na ukweli? Na ni nini thamani ya wema.
WAZO LA LEO:
Wengi wanadai kuwa pesa ni kila kitu, ukiwa na pesa unaweza ukafanya upendavyo,
na hata kuinunua haki..Sio kweli, mbele ya haki, hata pesa, inaweza isiwe na
thamani yake, ka lengo la hiyo pesa ni kuibatlisha haki. Elewa kuwa wakati wote
haki na ukweli na ushuhuda usioshindwa kwa thamani ya pesa.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kama utakuwa Una pesa hlf hutendi haki sidhani km Ina maana na mwisho wa siku haki itaonekana tu,haya tusubirie kinachofuata.
Post a Comment