Kesi ilianza kwa kasi sana washitakiwa wote walikana
mashitaka yao, na haikukubalika dhamana yoyote, kwasababu zilizotajwa kuwa ni
za kiusalama kwao.Wanandnugu waliposikia hivyo, hasa akina mama ambao waume zao
ndio hawo walikamatwa kama washitakiwa, walilalamika sana, na hata wengine
wakatishia kuandamana.
‘Msifanye hivyo, jamani, kwasababu kushikiliwa kwa waume
zenu ni kwa manufaa yao…kama hawana makosa wataachiliwa, lakini kwa uchunguzi
wetu, tumegundua kuwa ni bora kuwashikilia huku, ili ushahidi usije
ukaharibiwa, na pia tumegundua kuwa hata usalama wao upo hatarini, kama tutawaachia.’akasema
mzungumzaji wa muendesha mashitaka hayo.
‘Kwa manufaa gani, wakati sisi tunakufa njaa…hamjui hawo
wanaume ndio majembe yetu…tupeni basi pesa za matumizi’akalalamika mwanamke
mmoja.
‘Je kama tukiwaachia wakauwawa, ..nyinyi hamjua jinsi gani
hilo kundi lilivyojipanga, memeshuhudia mauaji mangapi hapo kijijini,
hamjachoka nayo….Ni heri iwe hivyo, kwasababu hamjui kabisa ni hatari gani
iliyowakabili hawo waume zenu, ..nyie nendeni nyumbani mkabangaize hicho
kilichopo, na msije mkajaribu kuandamana, mtaishia wote jela…’huyo msemaji
akawaambia, akijua kuwa kwa kuwaambia hivyo huenda hawo akina maam watatishika.
‘Kwasasa hatuogopi, kuishia jela kwani kuna tofauti gani,
maana hivi sasa tupo kama wafungwa, hatuna uhuru, hatuna amani….bora tu tuje
take huko rumande na waume zetu…ili muweze kutulisha na ikibid chukueni na
familia zetu zote…watoto wanakufa njaa, wengine hawaendi shule kwasababu
wanahitajiwa ada….’wakasema.
‘Ina maana hiyo ada imedaiwa kwa siku hizi chache tu, kama
mlikuwa hamjaliap ada, hilo ni swala lenu, haliwezi likatokana na kukamatwa kwa
hawa watu, maana hata wiki mbili hazijaisha…’akasema huyo msemaji.
‘Wewe kwasabbu muajiriwa, unajau utapaat mshahara, hujui
maisha ya watu wa hali zetu, uispokuwepo kweney kijiwe kwa siku moja,
hamli..tunabangaiza bora ziku ziende, …sasa siku ngapi tunagangaika kiguu na
njia kufuatilia maswala ya waume zetu…’waakzidi kulalamika.
‘Lakini kwanini muwafuatilie, na sisi tumeshawaambia kwanini
wamekamtwa, na wapo kwenye usalama,wasiwasi wenu ni nini…..?’ akauliza huyo
msemaji akipandisha hasira.
‘Tatizo lako hujui maisha yetu, je tuspowaona hawo waume,
wakatuelekeza wapi tungepate chochote, au kama ana akiba kaweka wapi tutawezaje
kuishi..nyia hamjui maisha yetu…waume zetu ndio kila kitu, wao ndio wanatunza
akina za ndani, wao ndio wadhamini, kama tukitaka kukopa,….sasa mnafikiri
tutaishije…’wakalalamika.
‘Ina maana nyie waume zenu walikuwa hawawashirikishi kwenye
maswala ay akiba au wapi kukitokea matatizo muweze kujikimu…?’ akawauliza.
‘Toka lini sisi wanawake tukashirikishwa kwenye mambo hayo…wewe
sasa unataka kuingilia mambo ya ndani ya familai zetu…sisi tumeshakuambia, kama
tusipowaona, kila siku hatutaweza kula…..na mkizidi kuwashikilia, tutakuja na
familia zetu….’wakasema na wote wakasema
‘Sawa, tutawaletea watoto…muwaleee, ili muone ugumu tunaokabiliana nao….’wakasema kwa sauti.
Baadaye akabidi kiongozi mmoja wa serikali kuja kujaribu
kuwaelimisha ili waelewe kwanini
imefanyika hivyo, na huyo kiongozi hakuwa na cha zaidi, akazidi kusisitiza kuwa
kukamatwa kwa wanaume zao, ni kwa ajili ya usalama wao, kwani ilikuja
kugundulikanana kuwa wengi wao walikuwa hatarini
kwasababu walitaka kusaidia kutoa taarifa za kundi haramu, ambalo ndilo
limekuwa chanzo cha matatizo yote hapo kijijini.
‘Sisi ni serikali na moja ya kazi zetu ni kuhakikisha
usalama wenu, na kwa vile tumegundua kuwa kuna watu wamejifanya wao ni zaidi ya
sheria, wakajitungia mamlaka yako wenyewe, na kuanza kuharaibu amani ya kijiji
kwa masilahi yao binafsi,tumeamua kupambana nao, na wote watafikishwa mbele ya
sheria, na kuwajibishwa…na ili tufanikiwe hili, tulihitaji msaada wa raia wema,
ambao baada ya kaunza kutimiza wajibu, hilo kundi likaanza kuwaatishia amani,na
imegundulikana kuwa hata hawo wlaikuwawa kabla ni kwa ajili hiyo hiyo………
‘Msitudanganye…mbona wengine wapo nje….’akasema mmoja wa
akina mama
‘Kwa vile pia hawa watu wamo ndani yenu, na mnaishi nao ,
itatuwia vigumu kwetu kuwalinda, ndio maana tumeamua kuwahifadhi sehemu ambayo
ina ulinzi wa uhakika….na hawo waliopo nje, hawajatishiwa ..na tukigundua kuwa
na wao wanahusika au kama wanaweza kutusaidia, na wao tutawachukua kwa nia
njema…’akasema huyo mtu wa serikali.
‘Toka lini jela ikawa ni sehemu ya ulinzi,…mnataka kutuulia
waume zetu bure…hilo hatukubali, kama wanahitajika kwa ajili ya ushahidi tu, kwanini
muwashike, na kama mumegundua kuwa wana makosa,basi wakubaliane dhamana….sisi
tumeshatimiza masharti yote ya dhamana,kwanini mnatukatalia, au mnatutaka na
sie..tuwe tunakuja hapa kila siku….’akasema mama mmoja kwa sauti na wengine
wakashangailia.
‘Sisi kama serikali, tumeliona hilo, na kwa vile tunajua ni
nini tunachokifanya, hatutarudi nyuma, kwani tusipofanya hivi, ….baadaye mtakuja
kutulaumu,..ni bora nusu shari, kuliko shari kamili…tunaomba mrejee majumbani
kwenu msubiri kesi hii iishe, na tunaomba msaada wenu ili tuweze kulimaliza
hili tatizo…haraka iwezekanavyo, na kama mnavyoona kesi hii imepewa kipaumbele,
itasikilizwa ikiwezekana kila siku, ili iishe haraka….’akasema huyo mkuu wa
serikali.
‘Sisi kama kesho wanaume zetu hawataachiwa, au kupewa
dhamana, sisi tutaandamana na safari hiyo tutakuaj na familia zetu….’ Akasema
huyo mama na wenzake wakamshangilia
Yule mtu wa serikali akamgeukia askari aliyekuwa na naye
akamnong’neza kitu, na yule askari akaondoka, na baadaye wale akina mama
wakatawanyika kurudi makwao. Na usiku wake baadhi ya akina mama wakakamatwa kwa
kosa la kuchochea ghasia.
*********
‘Hebu tuambie haya matukio ya mauaji yanayoendeshwa hapo kijijini
unayaelewaje, je kwa mafano siku ya tukio
la kuuwawa wale vijana wewe ulikuwa wapi?’ akauliza mshitakiwa mmojawapo ambaye
baada ya kuuliza hili swali aligeuka huku na kule kama anamtafuta mtu.
‘Umeulizwa swali, …kwanini unaogopa kulijibu, una wasiwasi
gani, hakuna atakayekuzuru, ukisema ukweli…tumeshawahakikishiwa usalama wenu’akaambiwa.
‘Hamjui jinsi gani maisha yetu yalivyo hatarani, tumekuwa
tukuishi kwa wasiwasi, kwani hata kama utakaa na kuongea na mke wako kumuhusu
…’akasita kidogo.
‘Kumhusu nani, ni nani mnayemuigopa kiasi hicho, ….’?’
Akaulizwa.
‘Tatizo nyie mkiondoka hapa mnakwenda makwenu, sisi na familia
zetu tunakuwa kwenye mashaka,naomba mtuelewe hivyo….’akasema.
‘Je ni nani aliyekuja kuwatishia amani mpaka mkawa kwenye
mashaka..?’ akauliza na yeye akakaa kimiya, na sfari hii alikuwa kainama chini.
Wakili mwanadada akasimama na kumuangalai yule mshitakia,
akasema;
‘Hivi unataka familia zenu ziendelee kuishi hivyo hado
mwisho wa maisha yenu au unataka tatizo hili liishe…wewe ni mwanume kweli si
kweli?’ akamuuliza. Na yule mtu akamwangalia huyo mwanamke kwa macho yaliyojaa
mshangao.
‘Ina maana..una..ni…..’akasema kwa kigugumizi cha hasira.
‘Kama wewe ni mwanaume kweli, kwanini unamuogopa mwanaume
mwenzako, kwanini unaogopa kujibu swali….?’ Akamuuliza.
‘Kama kungelikuwa na njia ya kulimaliza hili ningefanya
lolote…na nisingeliogopa kukujibu hilo swali, lakini nijuavyo mimi, tatizo hili
haliwezekani kuisha kwa njia hii mnayotaka nyie..’akasema.
‘Wewe unapendendekeza njia gani,ifanyike ili tatizo hili
liishe..?’ akaulizwa.
‘Kwanza mumeshindwa kuwakamata baadhi ya watu, na mnakuja
kutukamata sisi ambao hatuna lolote…hii ni kuonyesha kuwa hamna uwezo wa
kupambana na hawo watu….’akasema.
‘Hawo watu ni akina nani, tuambi ili tuweze kuwakamata…’akaambiwa.
‘Kwanini niwaambie wakati nyie mumesema mumeshakamlisha
uchunguzi wenu, na sijui ni kwanini mtukamate sisi wakati hatuhusiki kwa lolote
lile…’akasema kwa wasi wasi huku akiinua uso kuangalia upande huu na ule..
‘Nimekuuliza mwanzoni wewe ni mwanaume au sio mwanaume,
hukuweza kujibu ina maana hujiamini…..’akasema huyo wakili mwanadada akimkazia
macho.
‘Mimi ni mwanaume….unataka nikuonyeshe vipi kuwa mimi ni
mwanaume wkati unaniona kuwa mimi ni mwanaume…’akasema kwa sauti ya ukali.
‘Kuvaa nguo za kiuwanaume sio sababu, nyie si ndio majumbani
mnatamba kuwa nyie ni wanaume hamtishiki..sasa leo vipi, mbona mimi mwanamke
siogopi, nimesimama hapa kuwatetea ili haki zenu zipatikane, mbona siogopi mtu….?’
Akamuuliza na yule jamaa akajikuta akiinama chini.
‘Sasa kama wewe ni mwanaume, na unajua kutongoza…nionyeshe
huo uwanaume wako….uniangalie kama mwanaume na unijibu maswali kama mwanaume…mbona
inakuwa kama mimi ni mwanaume….’akasema huyo wakili mwanadada, na watu
wakacheka na huyo jamaa akainua kichwa na kuangalia mbele.
‘Je huko unapoangalia, kuna mtu unamuogoa, ..yeye ni mwaume
kuliko wewe?’ akaulizwa.
‘Hakuna mtu ninayemuogopa, mimi ni mwanaume…’akasema kwa
ujasiri.
‘Haya kama wewe ni mwanaume nijibu mwaswali yangu kama
mwanaume kweli….’akasema huyo mwanadada.
‘Ni nani huyo mnayemuogopa, huyo anayekuja kuwatishia amani
zenu hadi muishi kwa maisha ya mashaka….?’ Akaulizwa.
‘Mimi nilishawajibi hilo swali….mliponiuliza mwanzoni..’akasema.
‘Huko uliulizwa kwa ajili ya kutafuta maelezo yako, hapa
unaulizwa kwa ajili ya hayo maelezo yako yaweze kuwa uahshidi ili hawo watu
wakamatwe….’akasema mwakili mwanadada.
Yule mtu akainama na akawa kama anafikiria jambo, na wakili
mwanadada akamsogelea na kumshiak shavuni kwa kidole,
‘Hivi wewe kweli unaweza kumtongoza mwanamke…..’swali hili
liliwafanya watu humo ndani wacheke, na huyo jamaa akainua kichwa na kuangalia
kwa uso wa hasira, na kusema;
‘Hapo sasa umevuka mpaka…’akasema.
‘Kama wewe ni mwanaume na unaweza kumtongoza mwanamke, ongea
na mimi, je hunioni mimi ni mwanamke, mbona nakuwa kama nakutongoza wewe,….’akasema
na mara wakili ambaye alikuwa akiwatetea hawo watu akasimama na kusema wakili
anamlazimisha mteja wake kuongea kitu ambacho hakijui.
Wakili mwanadada akageuka na kuwaangalia watu waliohudhuria
hapo, akapitisha macho sehemu yote ya ukumbi , halafua akgeuka kumwangalai huyo
jamaa, ambaye alikuwa akimwangalia na pale wakili huyo aligeuka, akainama
chini, na watu walipoona hilo tendo wakacheka.
‘Je tukimkamata huyo mtu, ambaye unamuogopa, huyo mwanaume,
anayetishia wau wanaojiita wanaume, utasema kila kitu unachokijua juu yake?’
akaulizwa.
‘Kwanza ni kumkamata, pili ni kuhakikisha kweli mumeweza
kummaliza nguvu zake, ambazo sizani kama mna ubavu wa kufanya hivyo..’akasema
na wakili mwanadada akamsogelea mwenzake na kumnong’oneza kitu, na yule
muendesha mashitaka akasema;
‘Muheshimiwa hakimu, kama ulivyoona, washitakiwa wote
wamekuwa wakiogopa kusema ukweli kama walivyoweza kuelezea, wakati wanahojiwa
walipokamatwa, inaonyesha kuwa kuna mtu
ambaye anaonekana ni tishia katika kijiji, mtu huyo amekuwa ni chanzo cha haya
yote, …kwahiyo muheshimwa hakimu, tupo mbioni kumkamaat huyo mtu kutoana na
kibali chako, ili ukweli utolewe hadaharini….’akasema huyo wakili.
‘Kama mna ushahidi wa kutosha kumkamata kwanini hamumkamati…kuna
tatizo gani,?’ akauliza hakimu.
‘Kutokana na taarifa za polisi, huyo mtu , kila wanapofika
kwake, anakuwa hayupo,na hata barua alizotumiwa zimekuwa hazimfikii…cha ajabu
wanadai, aliweza kufika hadi hapa, na kujieleza, na kwa vile ni mtu wa
serikali, aliweza kujizamini, na hatukuwa na shaka naye , tulijua kwua leo
atakuweo kwenye mahakama hii tukufu, lakini kwa taarifa tulizozipata, ni kuwa
kapata ajali,…..’akasema na watu wakaguna kuonyesha kuwa sio kweli.
‘Mimi siamini haya, ina maana nyie wote mnashindwa kumkamata
mtu kama huyo, sasa natoa amri akamatwe haraka an kuwekwa rumande, ili kesho afikishwe hapa mahakamani, ili kujibu
shutuma juu yake.
Hii ni amri ya mahakama, na nikazi yako muendesha mashitaka
kuhakikisha kuwa washitakiwa wote wanafikishwa mbele ya mhakama, na sio
kuwashika baaadhi ya watu, na mwisho wa siku kunaonekana kuwa huenda kuna njama
za kuwasaidia wengine, na wengine wanateseka rumande….’akasema hakimu.
‘Muheshimiwa hakimu, tutafanya kila tuwezavyo, na kesho
atakuwa mbele ya mahakama yako tukufu….’akasema wakili na kesi ikaahirishwa na
wale washitakiwa wakarudishwa rumande.
*****
Usiku huo wake mbali mbali walikamatwa, akiwemo mke mkubwa
wa mjumbe wa nyumba kumi na wake za wazee mashuhuri , na hili likajulikana ni
kuwa walifanay hivyo ili waume zao wajitokeze, kwani kama walivyodai wananchi
watu hawo wameshindikana, na eti kila wakifuatwa majumbani kwao wanatoweka
kiajabu..
‘Nyie ndio mtasaidia waume zenu kupatikana, na
wasipopatikana mtaozea jela….’wakaambiwa, na kweli kesho yake asubuhi na mapema,
waume zao wake, wakajitokea, kasoro mjumbe wa nyumba kumi na wazee hawo wakasema;
‘Tupo tayari kujibu hizo shutuma, tunaomba wake zetu
waachiliwe kwanza….’wakasema.
‘Hiyo sio kazi yenu …ilimradi mumefika hapa, basi
mtashikiliwa kwa vile mumevunja amri ya mahakama ya kuwataka muwepo kila kesi
ikitajwa….na yupo wapo mjumbe wenu?’ wakaulizwa.
‘Kwani hamkusikia kuwa kapatwa na ajali , kalazwa
hospitalini, kama mnataka nendeni mkamuone wenyewe, sisi tumekuja kwa ajili ya
wake zetu…’wakasema.
‘Hawo kutoka kwao ni mpaka tujirizishe na usalama wao na
usalama wa watu wengine, msiwe na wasiwasi wapo chini ya usalama…nyie
mtashikiliwa kwa mujibu wa sheria….na kama huyo mnayesema kapatwa na ajali,
kama sio kweli, mtawajibika kwa hilo….’akasema na mara wakili mwanadada
akafika.
‘Nimefika huko hospitalini, mbona huyo mtu wanayedai kapatwa na ajali, hayupo huko hospitalini….’akasema na
askari wake wakaangalia kwa mashaka.
‘Lakini tulipofia usiku tulimuona…akiwa kalazwa…’akasema
huyo askari
‘Una uhakika na hilo?’ akauliza wakili mwanadada akimkazia
huyo askari macho…..
NB: Je kuna nini kinaendelea hapo, je kuwakamata hawo akina
mama itasaidia, je hizi hisia za watu kuwa hawa watu wana nguvu za ziada za
giza zina ukweli,…
WAZO LA LEO:
Kumekuwa na hisia na imani za nguvu za giza , hali hii imekuwa ikiwatia hofu
raia wengi, hasa akina mama. Imani hizi, zimefikia mbali zaidi ya kutumia viungo
vya watu, eti vinasaidia kuleta uatajiri au kinga…huu ni unyama, huu ni
uakatili, wa hali ya juu.
Dawa kubwa ya
kushinda haya ni kwanza kujua kuwa nguvu za giza hazina uwezo kwa mwanadamu, hazina
msaada wowote kwa mwanadamu, utajiri, ulinzi vinatokana na wewe mwenyewe sio
nguvu za giza, kama kweli wewe unamuamini mwenyezimungu, ambaye ndiye
aliyekuumba, mtegemee yeye na jibididhse kwenye uzalishaji mali wa kihalali, pili
ili nguvu za giza ili ziweze kufanya kazi yake ni mpaka wewe uingiwe na hofu…. Basi
jenga ujasiri, usiogope, mwamini mungu na kwa njia hiyo utaweza kuzishinda
kabisa nguvu zote za giza.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kweli kabisa we ushasikia Ni nguvu za giza hlf bdo unazifuata, wape somo ndugu yangu kanisani au msikitini ndio kuna nguvu bwana.
Post a Comment