Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, July 10, 2013

WEMA HAUOZI-32


Mimi nilipoingia hapo chuoni, sikujua kuna nini kinaendelea maana nilikutana na mazingira mapya ambayo sikuyazoea, na walinikuwa wakinisumba walikuwa ni wavulana, kati yao kulikuwepo na kundi la wavulana wanne ambao kila mmoja alikuwa kija kwa wakati wake, na nakumbuka hawo hawo ndio walikuja kunipokea kwa mara ya kwanza nilipoingia hapo chuoni, mwanzoni nilijua labda ndio taratibu za hapo, wakaanza kunisifia na kila mmoja akijinadi kwa wakati wake, kuwa yeye ndio ananifaa niwe naye.

‘Jamani mimi siwaelewi…..’nikaanza kulalamika.

‘Usijali binti, sisi ndio maarufu wa hiki chuo, mimi ni kiongozi wao hawo wote wanaokuja kuja hapa, na nia yangu ni kuhakikisha wewe unaishi hapa chuoni kwa raha, na kupata huduma zote zinazostahiki..’akasema huyo mmojawapo aliyafika hapo nilipofikia, siku huyo walikuja wavulana wanne.

‘Huyu asikudanganye bwana, hana cha umarufu huyu, mimi ni pedeshee wa hapa chuoni, nitahakikisha kuwa kila wikiendi tunakwenda kula kwenye hoteli kubwa kubwa…’akasema mwingine akiwa amevalia kitanashati na herein ya dhahabu sikioni…, na akaja na mwingine na mwingine…kiasi kwamba niliona ni kero, sikuwa na mazoea ya namna hiyo. Na siku hiyo hiyo nikaenda kuuona utawala wa chuo, kulalamika, maana sikuwa na raha, sikuwa na amani….na nyuumbani nilipotoka nilikuwa mtoto wa geti kali, na niliweza kupata karibu kila kitu.

‘Kwani tatizo lako ni nini, wamekunyanyapaa,au wamekutusi….?’ Akaniuliza kiongozi wa utawala binafsi wa wanafunzi.

‘Wananikera, ….’nikasema.

‘Sikiliza binti, hayo ni maisha ya kawaida katika mazingira ya sehemu kama hii, cha msingi wewe ni kuwazarau hawo wanakujia, maana hawawezi kukulazimisha kwa kitu ambacho hukitaki, kama itatokea wanakusumbua au kukuzuru, au kukufanya ushindwe kusoma, basi toa mashitaka rasmi na sisi tutawachukuliwa hatua.’nikaambiwa na mimi nikabakia kushangaa, kwani nilizania maisha ya hapo yapo sawa n shuleni,..

‘Hapa tunafahamu kuwa nyie mumeshakuwa wakubwa na mna akili za kiutu uzima hatuwezi kuwachunga kama wanafunzi,…, kwahiyo una mamlaka ya kukubali au kukataa maombi yao….hatupeshawishi kuwa muwe wapenzi, hapana, ila wewe unatakiwa ujue kuwa sasa unaingia kwenye nafsi ya kujitambua, ….kujitetea na kuweza kuishi kwa migu yako miwili, …..’nikazidi kufafanuliwa.

Niliposikia hivyo, nikajua kumbe…..sasa mimi sio mtoto tena, sitakiwi kudeka, kama vile nilivyokuwa nikideka kwa mama na baba. Kwanza nikajifunza kuwa hayo wanayofanya hawo wavulana ni ujanja ujanja wao na tamaa zao,..ukiwaendekeza utaishia kusindikiza wenzako na lengo la kufika hapo chuoni linaweza lisifanikiwe. Basi nikawa sihangaiki na wao, wakija nawaambia nina kazi ,sina muda wa maongezi, na wakati mwingine najifungia chumbani kwangu.

Kutokana na hali hii, ya kutkupendelea urafikii wowote na wavulana,  ilianza kuwauzi hawo wavulana, na wengine wakaanza kutunga fitina, na siku moja wakabandika `punch’ wenyewe wanaita `father punch’ na humo wakatunga uwongo mwingi, kuwa mimi ninajiuza, Malaya, huku njifanya mtakatifu……..yaani kashifa zisizostahiki..

Hapo sikuvumilia nikaenda kushitaki rasmi nikiwalenga wale wale vijana wanne, na wakaitwa, na uchunguzi ulipofanyika ikagundulika kuwa wao ndio vinara wa mambo yote hayo, japokuwa huyo anayeitwa `father punch’ hakuwahi kugundulikana, na wale vijana wakapewa barua kali za maonyo.

Kunazia siku hiyo wanaume wote wakawa wananiogopa,..na wengine kunishehimu, na wengine kunichukia kabisa…. Tofauti na wasichana wengine amabo kwao kufuata fuatwa na wanaume, na kupewa mialiko mbali mbali na wavulana kwao wao waliona ni sifa na walikuwa wakishindana kwa hili na lile, mimi nikawa `maksai’ kama walivyokuja kuniita baaadaye.

Basi sikujua kuwa mambo hayo yaliwauma sana baadhi ya wanaume wa hapo chuoni, na kufikia kutaka kulipiza kisasi kama nilivyohisi, na ndipo siku moja nikiwa nimetoka kununua vifaa vyangu vya wiki, maana niliamua kufanya hivyo kila wiki, na siku nyingine zote nilikuwa chumbani kwangu nikijisomea, au darasani au maktaba, na siku moja moja nakwenda kwenye mazoezi ya viuongo.

Siku hiyo nikiwa narudi toka sokoni, na wezangu , mimi nilichepuka kidogo, nikapitia sehemu ya majengo ya  zamani…kulikuwa na bustani…na humo kulikuwa na mboga mboga, na majani ya alovera, nilikuwa nafika hapo mara kwa mara kuyachuma majani hayo ya alovera, huwa nayatumia kama dawa.

Ni wakati nayachuma , nikahisi michakato michakato, na watu wakinong’ona,..nikahisi mwili ukinisisimuka, kuashiria kuwa kuna hatari, nikaharakisha kuchuma yale majani…na mara nikasikia mtu akiruka kutokea dirishani,ina maana huyo mtu alikuwa ndani ya jengo, na sasa karukia kwa nje, sehemu ile niliyokuwa nikichuma hayo majani, nikawaangalai wenzangu, ambao walishapotea upeo wa mchao yangu,…nikaona niharakishe niondoke hapo, lakini ilikuwa kama nimechelewa, maana nilihis huyo jamaa akija kwa nyuma yangu.

Wakati nataka kugeuka tu, na bila hata kuweza kuiona sura ya huyo mtu, nikashikwa kabari, na mkono mmoja wenye kitambaa ukawekwa puani kwangu, na nilihisi harufu kali ikipenya puani kwangu na sikuweza hata kupiga chafya nikaona giza likitanda usoni. Na kabla sijapoteza fahamu kabisa nikasikia sauti ikisema.

‘Huyu sasa tumempata apate fundisho, nyie fanyeni haraka,…nitambeba hadi ndani, tufanye haraka ili  akizindukana tumeshamaliza kila kitu, nitaanza mimi,.., hakikisheni vifaa vyote vipo sawa, sogeza hiyo kamera huku..’hayo ndio maneno ya mwisho kuyasikia nikapoteza kabisa fahamu.

Nilipozindukana nilijikuta nipo juu ya meza kubwa, na pembeni wamesimama watu wakiwa wamejifunika nyuso zao, na ilionekana walikuwa wakibishana jambo, na akili yangu haikuweza kunasa maneno yao vyema kwa muda huo, yalikuwa kama yanapaa..au mwangwi, hata sura zao zilikuwa zikioenakana kwa marefu ..kuashiria kuwa akili yangu ilikuwa bado haipo sawa, na huenda ni dawa waliyoniweka puani na kile kitambaa ndiyo ilikuwa imenimaliza nguvu..

Kila dakikia zilipopita ndio akili ilipoanza kutulia na nikaanza kuona vyema na kusikia sauti zao, lakini nilijifanya kama vle bado nimezimia, na ni kweli kumbe wale wanaume walikuwa wakigombana, kila mmoja akitaka aanza yeye kufanya hayo machafu waliyokusdia, kumbe walikuwa bado….na mmoja wapo alikuwa akihangaika na kamera iliyokuwa imewekwa juu ya dirisha ikielekea pale nilipo, sikufumbua macho moja kwa moja, nikasikia mmoja akisema;

‘Ngojeni mimi nianze, kwa vile ndiye niliyefanikisha hili…’akasema na baadaye wakamaliza mzozo wao, na kukubaliana kuwa huyo mwenzao aanze,…alikuwa kajifunika uso kama wenzake,  akanisogelea na kuanza kunivua nguo, nilitulia kimiya huku nikimuomba mungu wangu;

‘Ewe mwenyezi mungu nakuomba unilinde na haya mabaya wanayotaka kunifanyia, kwani sijawatendea lolote baya, …kwa baraka za matendo yangu mema nakuomba unilinde nisizalilike na machafu haya , na dhambi zao ziwazalilishe wao wenyewe, naomba uulinde huu mwili wangu usizalilike kwani nimejaribu kujilinda kwa haya, je hayo niliyoyafanya ya kujilinda ndio matokea yake haya,….nakuomba mungu wangu unilinde…kwani kama watafanikiwa kwa hili, sitakuwa na amani ni bora nife…au naomba unichukue roho yangu , nisiona haya machafu….’nikawa namumba mungu wangu  huku machozi yakinitoka.

Yule aliyesema kuwa ndiye anaanza akawa anavua nguo pembeni huku akiwa kajifunika kabisa usoni, ilionekana matundu ya macho tu…, na wenzake pia walikuwa wakifanya hivyo hivyo, na mmojawapo akiwa bado akirekebisha kamera na alionekana kuhisi jambo, lakini hakuwaambia wenzake, akawa anakuja kunisogelea, akanishika mboni za macho na kuzifunia, nikatulia kimiya.

‘Kwani vipi, hawezi kuamua huyu, ile dawa ni kiboko, mpaka masaa mawili hadi manne, mtu mwenyewe huyu halewi, kama englikuwa mlevi, tungesema haijamuahiri sana….’akasema mmoja wapo.

‘Niliona kama anapepesa macho….’akasema.

‘Wewe endelea na akzi yako bwana, usituharibie ….. na ghafla nikasikia sauti ikisema kwa nje;

‘Nyie mnafanya hapo..?’ sauti hiyo ilikuwa kali , na wale wote humo ndani wakashituka na wengine wakaanza kuvaa nguo zao kwa haraka

‘Hebu angali ni nani, kama ni ndata mnoko, mpe buku mbili…’akasema yule aliyejifanya ni kiongozi wao

Na hawo wanaume wengine wakawa wameinama chini ili kujificha…na mara nikasikia purukushani, na kelele za mtu akisema kwa sauti.

‘Saidia huku, walinzi njooni kuna wabakaji huku…’sauti hiyo iliwafanya hawa jamaa huku ndani waanze kutafuta sehemu ya kukimbilia, na wengine wakapanda juu ya madirisha na kuruka kwa nje na kuanza kukimbia, na kama sekunde chache kulikuwa kimiya,…kuashiria kuwa nilikuwa nimebakia peke yangu huku kichwa kikiniuma sana.

‘Pole sana dada yatu….tunahisi hawajakuzuru…’nikasikia sauti kwa nyuma ikisema, na sikuweza kumuoana vyema , kichwa kilikuwa kikiniuma sana na nikapoteza fahamu, na nilipozindukana nilijikuta nipo hospitalini.

‘Unajisikiaje dada yangu?’ ilikuwa sauti ile ile niliyosikia mapema,

‘Sijui,…kwani imekuwaje?’ nikauliza.

‘Wakati tunapita mimi na rafiki yangu tullihisi kuna kitu kinaendelea kwenye majengo ya zamani, na hapo nikamwambai huyo rafiki yangu twende tukaangalie kuna kitu gani. Na tulipofika hapo ndio tukawaona hawo  wahuni wakitaka kukubaka..na tunashukuru kuwa tulikuwahi kabla hawajafanya lolote…

‘Kutokana na maelezo ya docta kasema hawo watu hawakuwahi kukufanyia lolote, ila tu madawa waliyokupulizia ndiyo yamekuathiri, na wamejariu kukupa dawa ya kuyamaliza nguvu hayo madawa waliyokupilizia, unajisikiaje kwa sasa…?’akasema huyo mwanaume.

‘Aaah, sijui..kwanini watake kunifanyia hivyo…?’ nikaanza kulalamika.

‘Kwani unamfahamu yoyote kati yao, maana tuliwaona wakiwa wamefunika nyuzo zao, na hakuna aliyeweza kukamatwa, maana wote walikimbia nje kablsa ya chuo, kuonyesha kuwa huenda sio wanachuo…na kama ni wanachuo, basi walikimbilia nje ya chuo na kurejea baadaye…?’ nikamuuliza.

‘Kwekweli sikuwahi kumuona yoyote sura yake, maana walinidaka na kuniwekea kitambaa puani, na nikapoteza fahamu…’nikasema.

‘Polisi wanafanya uchunguzi,….hata hivyo mpaka sasa hawajaweza kumgundua yoyote, kama kuna mtu yoyote unayemuhisi  , mtaje kwa polisi, maana wao watajua jinsi gani ya kumuhoji…’akasema.

‘Kwakweli kwa vile sina mazoea na wanaume wa hapa chuoni …siwezi kujua ni nani…naona wanaume wote wapo sawa, na kama ni kuhisi ninaweza nikawahisi wanaume wote wa hapa chuoni ?’

‘Ina maana hata mimi?’ akauliza.

‘Kwa hivi sasa sina uhakika ….nawachukia wanaume wote….samahanai kwa hilo,….’nikasema.

‘Pole sana, lakini sio wote wenye tabia chafu kama hizo, kwanini ubake, kama unahitaji mpenzi unaongea naye…mimi siwezi kufanya hivyo, ….’akasema.

‘Najua utasema hivyo kujikosha, lakini nyie wote tabia zenu ni moja….’nikasema nikitamani kumfukuza, lakini kwa vile ni yeye aliyeniokoa, nikaona nimstahi tu.

‘Unasema ulikuwa na rafiki yako, yupo wapi huyo rafiki yako?’ nikamuuliza.

‘Ametoka sasa hivi….’akasema huku akionyesha hali ya wivu, huenda walikuwa na lengo lao moja, na huyo alijitahidi kujionyesha kuwa yeye keshaniweka kwenye himaya yake.

Polisi walifanya uchunguzi wao, lakini hawakuweza kugundua lolote…..na tukio hilo likabakia kwenye historia za chuo, …na ulinzi ukaimarishwa, na wasichana tukaambiwa tuwaliweza kukimbia na vifaa vyao vyote.

Basi huyo mwanaume aliyeniokoa tukaanza kuzoeana naye, maana ilibidi niwe na mwanaume ili kuonyesha kuwa nina mpenzi, japokuwa sikuwa na nia hiyo kwani lengo langu lilikuwa ni kusoma, sikufika hapo kwa ajili ya urafiki na wanaume.

Huyo mwanaume akawa ndiye mlinzi wangu, na kila muda tulikuwa naye, na kwasababu hiyo, tukaanza kujenga urafiki wa karibu, na hata siku aliponitamkia kuwa anataka urafiki na mimi, sikutka kumuuzi kwa kumkatalia lakini nilikuwa bado sijaingiwa na hisia za kumpenda, kwahiyo nikamjibu kinyume na alivyotarajia.

‘Mwanadada, nakuomba sana uwe rafiki yangu mpenzi, …..’akaniambiai siku hiyo tulkiwa tunapata chakula cha jioni.

‘Usinichekeshe, tulishakubaliana kuwa wewe na rafiki yako wote ni kaka zangu, …mbona unataka kuniharibia siku yangu tena…’nikasema huku moyo nikiwa nimeshaamua kumpenda, japo kwa kulazimisha, sikuwa na hisia na mwanaume yoyote hapo chuoni hadi muda huo, kusema huyu nimempenda, sijui ni kwanini,… lakini kama ilivyo kawaida ya wanawake, sikupenda anione nina hisi again juu yake.

‘Ndio mimi ni kaka yako, ..na sitaki kukuzi , ila mimi nimekuwa moyoni nikitaabika, …kwa vile nimekupenda zaidi ya kaka, na sipendi ije itokee mtu mwingine akuchukue…na naona rafiki yangu huenda ana mawazo kama hay ohayo…..’akasema.

‘Wewe ni kaka yangu akija mtu kunichukua anakuwa ni shemeji yako, hata hivyo, mimi sipo tayari kwa urafi wowote kwa sasa, kwani lengo langu ni kusoma, na sitaki kizuizi katika kufikia malengo yangu..’nikamwambia.

‘Nakuhakikishia kuwa sitakufanyia lolote litakalokuharibia masomo yako, cha muhimu ni kuawa wewe uwe rafiki yangu mpenzi na muda muafaka ukifika, basi…tunakuwa wapenzi kamili..sina nia mbaya kwako,…’akasema.

‘Nimekuelewa….na naomba unipe muda wa kulifikiria hilo..’nikamwambia, na kwasababu hiyo nikawa namkwepa, tofauti na kabla hajanitamkia hivyo, na yeye akahisi kuwa kwa kuniambia vile nimekasirika, au rafiki yake keshanishawishi na huenda nimemkubalia yeye, au nimempenda yeye, akawa hana raha,…

Siku moja akaja chumbani kwangu, na kugonga mlango,…nikamfungulia na alionekana kama mgonjwa, nikamuuliza anaumwa;

‘Ni heri ningeliumwa nikajua moja..’akasema.

‘Kwani tatizi ni nini?’ nikamuuliza.

‘Nahisi mimekuuzi, ..na  hilo linaniuma sana moyoni, kama kuna kitu nisichokipenda katika hii dunia, tangu nikujue, ni kukufanyia jamboo linaloweza kukuuzi , au kukukosehsha raha, nakuomba kama kuna lolote baya nimelifanya au kulisema kwako, au nimelitamka na limekukasirisha nakuomba unisamehe, tuwe kama awali..’akasema.

‘Mbona hujanifanyia lolote baya,…mimi niliamua kuwa hivi tu, kwasababu mitahani inakaribia, na sikupenda kuingizia kitu kingne kichwani kwangu,na kuniharibia utaratibu wangu wa kusoma…’nikasema.

‘Sio kweli…nahisi kabisa unanikwepa kwa vile nimekuomba urafiki, kama ni hilo basi tuendelee kuwa kaka na dada, hakuna shida kwangu…huenda umempenda rafiki yangu zaidi ya mimi, lakini ..nakuomba sana unifikirie….’akasema.

‘Kwahiyo umeshindwa kunishawishi au mnashindana na rafiki yko, mboana nyie wanaume wa chuo hiki mna mambo….?’ nikamuuliza na yeye akashituka kwa kauli yangu hiyo, na kusema

‘Hapana sijashindwa, ila tu sitaki kukuudhi……………kwasababi kiukweli nakupenda sana.’

‘Hujaniuzi na wala usiwe na wasiwasi juu yangu, kauli yako niliisikia na nakuomba usipate shida kwa ajili yangu, ipo siku nitakupa jibu muafaka, lakini sio kwa sasa..nina mambo mengi kichwani, na sipendi yaniingie mambo mengine..’nikamwambia n a yeye akahisi kuna tatizo.

Na kweli kwa kipindi hicho kulikua na matatizo nyumbani, baba na mama yangu, walikuwa hawaelewani na hilo lilikuwa likisnisumbua sana akilini mwangu, na hali kama hiyo ilinifanya nisiwe napendelea urafki na wanaume,….nilihisi kuwa nitakuwa sina amani kama walivyo wazazi wangu japokuwa sikujua chanzo cha migongano yao ilikuwa ni nini…………

Siku moja nilipata taarifa kuwa mama yangu kaamua kwenda kwao na baba kabaki mwenyewe, na niliposikia hivyo nikawa sina raha kabisa na huyo rafiki yangu akahisi hilo, na ndipo akaanza kuwa karibu nami iisvyo kawaida, na nikahisi ndiye mtu wangu wa karibu kuliko wazazi, kwa vile wazazi wangu walikuwa hawaelewani, na kila ninapokwua nao, hawaishi kuzozana.

‘Oh, nakuona kama mtu wangu wa karibu kuliko hata wazazi wangu…’nikamwambia.

‘Hata mimi , na namuomba mungu uwe nami hadi mwisho wa maisha yangu..’akasema.

‘Hata mimi natamami iwe hivyo, ila naogopa isije ikatokea kama kwa wazazii wangu…’nikasema.

‘Kwani wazazi wako wana matatizo gani?’ akaniuliza, na mimi sikupenda kabisa kumsimulia mtu kuhusu matatizo ya wazazi wangu, nikamwambia, hakuna shida ni mambo ya kawaida tu. Na yeye akajaribu kunishawishi ili ajue , lakini sikuwa tayari kumwambia yoyote kuhusu undani wa ugomvi wa wazazi wangu , hata hivyo sikuwa nafahamu zaidi ya kuwaona wakizozana zozana mara kwa mara.

Siku moja nilimtembelea huyu jamaa chumbani kwake, nikiwa na lengo la kumwambia kuwa sasa nimemkubalia awe rafiki yangu mpenzi,  na hii ilitokana na mwenzangu tunayechangia chumba, yeye kila mara rafiki yake wa kiume alikuwa akifika hapo , na wanakuwa wakiongea kwa raha, na wakati mwingine wanashikana mbele yangu, sikuweza kuwakataza, lakini ilikuwa ikiniweka mahala pabaya.

‘Rafiki yangu, leo boy friend wangu atafika hapa chumbani, naona usije ukakereheka, kama inawezekana nenda ukajisomee makitaba,….’akanishauri.

‘Hamna shida, kwa vile nina kazi ya usafi, nyie ongeeni tu, nikiona vipi , nitatoka kidogo kutembea, leo sijisikii kusoma kabisa leo, nina mawazo mengi ya nyumbani…’nikamwambia.

‘Haya, maana wewe umeamua kweli, …lakini mambo ya wazazi wako yasikuumize kichwa , wao wana maisha yao na wewe tafuta maisha yako….jichanganye…huni sisi tunavyofanya, sio kwamba huko tutokapo kuna raha saana, kuna wenye matatizo zaidi yako, lakini …lazima utafaute njia ya kuyapotezea…’akaniambia.

‘Kuamua nini `mate’ wangu…kwani ulitaka nifanye nini?’ nikamuuliza kwani sikujua ana maana gani.

‘Usijifanye kuwa hutaki kuwa na rafiki wa kiume, wanaume wengi wanakutaka,lakini wewe unajifanya hutakio mambo hayo…..wakati mwingine hii inasaidia kuondoa msongo wa mawazo, unajua sisi wanadamu tumeumwa wawili wawili, yaani mke na mume, sasa huwezi kujifanya wewe ni tofauti..’akasema.

‘Ndio kwa uoni huo, lakini hayo yanakuja kwa wakati muafaka, mimi hapa nimekuja kusoma, na wakati muafaka ukifika basi nitajihusha na mambo hayoni..siwezi kuchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja….’nikamwambia.

‘Sote tunafahamu hilo, na sio kwamba kuwa na rafiki wa kiume ndio umejiingiza moja kwa moja kwenye mahusiano, hapana, ni ukaribu tu, si unaona jinsi gani nipo na mwenzangu, simpi nafasi kabisa ya kunishawishi kitamaa zaidi, siku moja moja, naamua …lakini sio kwamba ndio tumefika, huenda, nikitoka hapa sitakuwa naye tena….hapa ni kupass time tu….usinione hivi, mimi nimejiwekea mapaka yangu,….’akasema.

‘Sawa huo ni uoni wako na utashi wako, mimi nahisi kwangu itanipa shida sana, na naona bora niwe hivi hivi…hadi hapo nitakapoona sasa nahitaji kuwa na mwenza’nikamwambia.

‘Sawa basi baadaye…mimi iskiweza, na nakushangaa sana,…mimi nakwenda kwa huyo boy friend wangu, halafu tutakuja naye hapa….’akasema na kuondoka huku akiwa kajipara kiukwe ukweli….utafikiria sio mwanafunzi. Mimi niliendelea na shughuli zangu na wakati narudi chumbani, nikasikia sauti zisizo za kawaida, nikaogopa kabisa kuingia ndani ya chumba chetu na kuanza kutembea, nikijiuliza sasa niende wapi.

Sauti zile nilizozisikia zikawa zinanikera kichwani, na hata nikawaza kuhama kile chumba na kutafuta sehemu ambayo mwenzangu atakuwa na msimamo kama mimi, lakini karibu wasichana wote hapa chuoni walikuwa na marafiki zao wa kiume, kasoro mimi tu.

Kutembea kwangu nikjikuta nimefika mabweni ya wanaume, na bila kujielewa nikajikuta nikiwaza kwenda kwa yule jamaa aliyeniokoa , na moyoni nikasema, huenda sasa ni wakati muafaka, na  mimi  kuwa na rafiki wa kiume, japo tu kwa kupotezeana muda,….basi umauzi huo ulipoingia kichwani, nikaamua moja kwa moja niende kwa huyo jamaa nimwambie sasa nipo tayari kwa urafiki, na moyoni nilijua nitamfurahisha sana huyo jamaa kwani siku nyingi alikuwa akisubiria hilo jibu,……..

Nikafika kwake, na kwa vle nilishaanza kumzoeana, sikusumbuka kugonga mlango, nikafungua mlango nikaingia moja kwa moja ndani, nikitaka kumshitukizia ooh,hamadi,…nikajikuta nimesimama kati kati ya chumba huku macho yakiwa yamenitoka pima,…akili yangu ilisimama ghafla, nikabakia nimeduwaa…nikajikuta nimeshika mdomo, nikijizuai kupiga ukulele…huku nikiangalia kule ndani….

Nikahisi kichefu chefu, hasira….oh, sikuweza kuvummilia, akili ikawa imeingiwa na giza, kizunguzungu kikanijai ghafla, nikajitahidi kujizuia lakini haikuwezekana…na kelele zile nilizoziskia mle ni kama zile zile zilizokuwa zikiendelea kule nilipotoka,,..nikawa nakaribia kudondoka, na nikashituka mtu akinishika;

‘Usijali ..ndio maisha,….. kakuonyesha dhahiri kuwa hakupendi….sasa umejionea mwenyewe, anayekupenda ni mimi mwanaume wa kweli….sina mwingine hapa chuoni zaidi yaw ewe…japokuwa
sikuwahi kuwa  na wewe karibu kama huyo rafiki yangu….ambaye hakutaka kunipa nafsi hiyo…’nikahisi kizungu zungu, na kichefu chefu kikazidi kuniandama, na kama asiingelikuwa huyu jamaa  aliyekuja kwa nyuma yangu kunidaka, ningelidondoka sakafuni na kuumiza vibaya…

Na huyo ndiye huyo mwanasheria wa hiyo familia tunayemuongelea….na mapenzi yetu yalianzia hapo.

NB: Yalianzaje na kuna nini wakili mwanadada anataka kutufundisha, tuwe pamoja

WAZO LA LEO: Jenga msimamo wako wa maisha ambao unahisi upo sawa sawa, usivutike na vishawishi, na kujaribu mambo ambayo huenda yanaweza kukuleta matatizo, kumbuka mwili wa mwanadamu sio uwanja wa majaribio. Mwili na akili yako  ni mali yako vilinde hivi vitu viwili, thamini sana mwili wako, na thamini sana akili yako, katu usikubali mtu yoyote mwingine akauchezea mwili wako na akili yako kwa mambo yenye kuhatarisha maisha yako. Kumbuka likitokea tatizo kwenye hivyo vitu viwili, atakayeumia zaidi ni wewe…sio huyo aliyekushawishi, kwani na yeye ana mwili wake na akili yake. Kuwa mwangalifu.


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Unknown said...

Mh kwel mapenz yanamuda wake.

Unknown said...

Pole ndugu yangu kwa msiba sote tu njia moja muhimu ni kumuombea, pia nimependa Sana wazo la Leo.

Unknown said...

Pole ndugu yangu kwa msiba sote tu njia moja muhimu ni kumuombea, pia nimependa Sana wazo la Leo.