Ni mwaka jana tu tulikuwa na mgeni wetu huyu tunayetarajia
kumpokea hivi karibuni, mwenyezimungu akitujalia. Na tulikaa naye masiku
yasiyozidi siku thelathini,na baadaye akaondoka., na huenda wengi wetu mgeni wetu huyo alifika na akatuacha
kama alivyotukuta. Tulisahau kuwa mgeni huyu kwetu ni neema, isyoyofanana
na kitu chochote na akija akaondoka bila
ya wewe kutakasika basi tena, wewe upo hasarani
Mungu akipenda tutakuwa naye tena, na ni wakati wako huu wa
kujirudi usifanye makosa kama ya mwaka jana, kwani bahati wakati mwingine haiji mara mbili,…Mgeni
wetu huyo akija, tunahitajika tufanye mambo muhimu yafuatayo;,
Kwanza ni, kuwa wapole, kupendana, kusaidiana, ikiwa na
maana ya kurehemeana,
Pili tukiwa naye tunahitajika kutubu madhambi
yetu kwa, kumuomba mola atusamehe yale mabaya , na maovu tuliyoyatenda, maana
mwaka mzima kama binadamu tumekuwa ndani ya dimbwi la maasi, yapo matendo
tuliyotenda kwa viungo vyetu, kwa dhahiri au kwa bahati mbaya , yawe ya
kutenda, yawe ya kuona au kusikia, yote haya mgeni wetu atatusaidia
tuyafute kwa sharti kuwa tuwe wakweli na tutubu ukweli wa kutubia.
Na ukishamaliza kutubia unasamehewa na kuwa huru, mbali kabisa na madhambi,
unakuwa msafi kama siku ile ya kuzaliwa,…unataka nini tena we mwanadamu,, baada ya hapo mgeni wetu huyo ataondoka, akijua
kuwa amekusaidia kuwa huru, kuwa mbali kabisa na madhambi ambayo yangekutia kwenye moto wa jahanamu.
Je wewe huoni umuhimu wa mgeni huyu, ..ni nini
unahitajia katika dunia hii, . …angalia wangapi ulikuwa nao na sasa hawapo,
kweli walipenda kuondoka, …na wao walikuwa wamekusduia kuwa mwezi huu ukifika watafunga,
lakini mola keshawachukua. Basi kwa vile wewe umejaliwa kukutana na mgeni huyu
tena, na umeshajua ni nini anahitajia,, kwanza jiandae kumpokea vyema…na kwa vile
umeshajua kuwa mgeni wetu huyu ni mtakatifu, basi, na wewe jiandae kitakatifu kwa
kuwa msafi wa mwili na roho.
Tuacheni dhana potofu za vunja jungu hizo dhana
za kupandikizwa ili mvunje imani yenu, na mjikute mpo wachafu mkutane na mgeni wetu
huyo tukiwa wachafu.,…je kweli unaweza kwenda kumpokea mgeni wako ukia mchafu,..haiwezekani.
Kwahiyo tujitahidi sana, tusiige tabia za ibilisi na
shetani aliyelaaniwa. Kwani ukifanya hivyo, ukajiunga na hawo wanaovunja jungu, basi ni kama
vile unamuaga shetani ….kuwa ooh, rafiki yangu unaondoka tutakutana mwezi
ukiisha...
Cha muhimu ni kujikurubisha kwa mola wako, kwa
kuanza kuandaa sehemu zako za ibada, ambapo utaweza kumkaribisha mgeni huyu,anza kwa kutubu dhambi zako kwa kuwaomba msamaha wale wote uliowakosea, wakumbuke
mayatima, wakumbuke wagonjwa, wasiojiweza, wadaiwa, wanaohitajia ada za shule, ukumbuke kutoa sadaka, kuwaaombea waliotangulia, na kila mara mdomo
wako uwe ukimtaja muumba wako.
Karibu mgeni wetu mtukufu Ramadhani.
Blog yenu ya Diary yangu inawatakia kila la heri, na funga njema yenye mazingatio kwenye mwenzi mtukufu wa Ramadhani.
NB: Nilikuwa nimefiwa na ndugu yangu, mungu amlaze mahali pema peponi, ndio maana sehemu inayofuata ya kisa chetu cha WEMA HAUOZI, haikuweza kuwepo hewani, tunajaribu kuiweka hewani, ...soooon
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Tupo pamoja m3
Kila la kheri kwa kipindi hiki cha ramadhani. Na polwesana kwa msiba.
POLESANA KWA MSIBA NA ASANTE KWA KUTUPA NASAHA NZURI ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NADHANI KILA ATAKAYESOMA HAPA ATAPATA CHA KUFANYA
Post a Comment