`Bibi yako alipoamuka asubuhi akaenda chumba alicholala huyo
mzazi, akiwa na mpangilia wa kumsaidia kuoga na kumkanda na maji ya moto,…..akafika
kwenye chumba cha huyo mzazi na kugonga mlango, lakini kulikuwa kimiya, ….basi
akaamua kuingia, na kumkuta mtoto mchanga yupo peke yake kitandani, akiwa bado
amelala.
Kipindi hicho nyumba yangu ilikuwa ya miti, iliyokandikwa
kwa udongo, na kuezekwa kwa majanii sio hii, hii ilikuja kujengwa baadaye na
mama yako….’akasema babu, na tukawa wote tunaiangalia hiyo nyumba kwa macho.
Babu akaendelea kuhadithia ….
‘Huyu mtu atakuwa amekwenda wapi asubuhi hii…’bibi yako akawa
anauliza kwa sauti na mimi nikamsikia na nilipoona anaendelea kujiuliza hivyo,
ikabidi na mimi nimuulize kwa sauti, toka kwenye chumba chetu;.
‘Ina maana huyo mzazi hayupo huko ndani kwake?’ nikauliza
‘Hayupo…hata huko nje, haonekani,….sijui atakuwa kaenda wapi
asubuhi hii, na ile hali alitakiwa asitoke nje, kwani ubaridi ni mkali sana. …’akasema
bibi.
‘Kaondoka na kitoto?’ akauliza babu.
‘Aheri angeliondoka naye, nisingelikuwa na wasi wasi kiasi
hicho, lakini mtoto kaachwa peke yake hapo kitandani, na bado kamelala…’bibi
yako akasema na mimi nikatoka kule chumbani na kuja kuungana naye kuhakikisha
hayo anayozungumza bibi yako, na kweli huyo mzazi hakuonekana.
Masaa yanakwenda, mzazi haonekani, na mtoto anaanza kulia
njaa, hapo ikabidi tuanze kuhangaika, …kutafuta maziwa, na uzuri ni kuwa
tulikuwa na ng’ombe wa maziwa, kwahiyo hatukupata shida sana ya kumlea huyo
mtoto…kichanga kikaanza kutumia maziwa ya ngombe.
Masaa yalivyozidi kwenda bila ya kuonekana huyo mzazi,
tukaanza kuingiwa na wasiwasi, kwani, hakukuwa na dalili yoyote ya mzazi, na
hata tulipofanya utafiti, hatukuweza kugundua kuwa huyo mzazi alielekea wapi. Hakuna
hata jirani mmoja aliyemuona huyo mzazi. Na badala ya majirani kutusaidia
wakawa wanatuangalia kwa jicho baya…na hata wale wasio na subira, wakaanza
kusema;
‘Kaanza …mambo yake….’
Mimi nilivyosikia hivyo, nikasema ‘Mke wangi ni vyema
tukamfahamisha mjumbe, maana hili linaweza kuwa tatizo, unakumbuka lile tatizo
la mwanzo lilivyotuletea matatizo, hili linaweza likatupeleka pabaya….’nikamwambia
bibi yako.
‘Maneno ya watu unayajali, mimi sijali, kwa vile sijawahi
kufanya lolote baya kama wanavyodai wao,….kama nimepangiwa kuwawa kwa mikono
yao,….siwezi kuzuia hilo, waache waje waniue….’akasema bibi yako.
Na kweli kwa tabia ya bibi yako alikuwa hajali, kwani maneno
waliyokuwa wakiongea watu, kama angelikuwa na roho nyepesi angelishikwa na
shinikizo la damu, lakini sio bibi yako. Bibi yako alikuwa jasiri, na hasa pale
alipoona kuwa analolifanya lipo kwenye haki…atalisimamia hadi hatua ya mwisho.
Mimi sikutulia, nikamuacha bibi yako akimuhangaikia huyo
kichanga, nikaenda kuongea na mjumbe, na mjumbe akasema kiutaratibu inatakiwa
yapite masaa ishirini na manne, ndio taarifa zifikishwe kwenye vyombo vya
usalama.
Nikarejea nyumbani na kumkukuta bibi yako akiwa analea
kichanga, na siku hiyo ikapita, sikuwahi kukumbuka tena kwenda kwa mjumbe,
tukawa tunakilea hicho kichanga kama mjukuu wetu, maziwa yapo, tuna shida gani.
Waache watu wasema wakichoka watalala…kumbe wenzetu walikuwa na yao moyoni….
‘Walimwengu ni watu wabaya sana mjukuu wangu, sijui huo
uvumi ulianzia wapi, maana kuna kisa cha kwanza kilikuwa hivi hivi, ….wema wa
bibi yako ukawa umegeuka kuwa shubiri kwake. Kama nilivyokuambia kuwa bibi yako
alikuwa mkunga, kwahiyo wasichana waliofikia kujifungua, ambao walishindwa
kwenda mahospitalini, walikuwa wakimuita bibi yako kwenda kusaidia kuwazalisha.
Na hata wengine kufika hapa nyumbani
‘Kazi hii ya ukunga sio mchezo, na wengi walikuwa wakimuita bibi
yako wakiwa kwenye hali mbaya, bibi yako alikuwa akijitahidi kadri ya ujuzi
wake kuwasaidia, lakini kuna mengine yalikuwa juu ya uwezo wake, na kwasabbu
hiyo, ilifikia wakati mwingine mtoto kupoteza uhai, au hata mzazi mwenyewe…hayo
yakitokea ilikuwa ni shida kwa bibi, watu walikuwa wakimshutumu…
‘Hutaamini mjukuu wangu, ….ilifikia hatua sasa watu wanaanza
kugeuza maneno kuwa bibi yako ndiye aliyekuwa akiwaua….hawo wazazi walishikwa
na uchungu na kwasababu mbali mbali wakaweza kupoteza uhai, au watoto wao
kufariki….’akasema babu na kutulia kwa uchungu.
‘Mimi nilimshauri bibi yako aachane na kazi hiyo, maana
haina faida kwake, ukizingatia kuwa kazi kubwa aliyokuwa akiifanya hakuwa
akipata malipo ya maana, inakuwa kama kujitolea tu, na yule aliyeweza kumlipa
chochote, alipokea, lakini wengi walikuwa hawana cha kumlipa bibi yako, …nay
eye hakujali, akarizika,…lakini wema wake huo haukuonekana….
Siku moja usiku alikuja msichana mmoja, akiwa mja mzito,
msichana huyo, alisema kuwa hana pesa, na wazazi wake, wameshindwa kumsaidia…na
hospitali ni mbali,….na mwanaume wake aliyempa huo uja uzito, ni jamaa ambaye
naye hana mbele wala nyuma…kwahiyo akaona aje akae hapa nyumbani , kwani
anahisi dalili za machungu….
‘Hilo halitawezekana, …umeshasikia watu wakiongea vibaya
kuhusu mke wangu..mimi sikubalianai na hilo….nakushauri uende kwa mjumbe atajua
jinsi gani ya kukusaidia’nikasema
‘Basi kwa vile ni usiku nitalala hapa, na kukipambazuka
nitaondoka…’akasema huyo binti, na hatukuwa na
jinsi, tukakubali, kwani hakuwa
ameonyesha dalili zozote mbaya, …lakini ninajuta kwanini tulimkubalia..
‘Mjukuu wangu ilipofikia usiku wa manane huyo binti
akazidiwa,akaanza kupiga kelele, akidai tumbo linamuuma sana, na hapo bibi yako
akamchunguza akasema ….anakaribia kujifungua na hakuna muda wa kupoteza, ina
maana alitakiwa kusaidiwa kwa haraka, ili ajifungue, na usiku kama ule,
tusingeliweza kwenda kwa mjumbe….
Hapo kukawa hakuna jinsi, bibi yako akafanya kazi hiyo ya
ukunga bila kupenda. Lakini kumbe yule binti alikuwa na matatizo kabla, kumbe
hakuwa na damu ya kutosha, na hata alipojifungua alipoteza damu nyingi sana, ….’
Akatulia babu akikohoa.
‘Kwanza huyo binti alijifungua salama, na bibi yako
akajaribu kumpa dawa, na majani ya kuongeza damu, lakini haikusaidia, ilipokaribia
asubuhi, hali ya huyo binti ikawa mbaya, mimi nikakimbilia kwa mjumbe,
ntuliporejea na mjumbe na watu wengine wawili, tukamkuta huyo binti keshapoteza
uhai…..’ Babu alipofika hapo akatulia, akionyesha wasiwasi, utafikiria ndio
hiyo siku tukio lilipotokea….
‘Ilikuwa kesi kubwa sana, ikishinikizwa na huo umbea uliokuwa
umezagaa, basi ikawa ndio sababu, ..bibi akashikiliwa na polisi, na akajikuta
analala kituo cha polisi kwa siku mbili, na hata alipotoka hakuwa na amani,
watu wakawa wanamnyoshea vidole, wakimuita majina mbaya….akawa sasa hana amani
tena…na ujasiri wa bibi ukaanza kupungua, na yeye sasa akaanza kuogopa.
‘Jamani hivi hawa watu wana akili kweli…mimi sijamtuma mtu
kunichukua kama mkunga na kila mara nawashauri kuwa ni vyema wakaenda
hospitalini, lakini hawasikii, ….sasa mimi nimefanya kosa gani,…mimi naufahamu
ukunga vyema, lakini kuna mambo ambayo yanahitaji utaalamu zaidi,…na mimi nimejitahidi
kadri ya uwezo wangu,yameshindika, kama hayo ya kupungukiwa na damu, mimi
siwezi kuwaongezea damu kwa haraka, sina vifaa….’akawa analalamika bibi yako.
‘Huo ndio mtihani wa kutenda wema,….mimi nilikushauri mapema
kuwa achana na kazi hiyo, lakini hukutaka kunisikia….’nikamwambia bibi yako
yeye alisema
‘Mimi natenda hayo kwani ni wajibu wangu,… kwa hali zote
zilizotokea, kama ulivyoona, sikuwa na jinsi , nisingeliweza kuwatelekeza hawo
watu, na mahospitali yetu yapo mbali na huku kijijini, ..’akasema.
‘Hilo ndio tatizo, na hata ungeliwaamusha watu usiku kama
ule….wangechukua muda kufika, ilibidi ujitaidi kwa kadri unavyojua,….siwezi
kukulaumu mke wangu, lakini watu hawajui, na inavyoonyesha kuna watu kwa
makusudi wamepandikiza huo uwongo….’nikasema.
‘Haya tumuachie mungu,….najua ipo siku wema wangu utazaa
matunda, hata kama sio kwangu, lakini kwa yoyote yule atakayekuwa upande wangu,
…kwani kwa uhakika, hata siku moja wema hauozi…’huo ndio ulikuwa usemi wa bibi
yako.
‘Bibi yako alikuwa na tabia moja, kuwa hapendi kutegea,
anapenda sana kujitolea, kwa kazi yoyote yeye yupo mstari wa mbele…kama ilivyo
mimi, ….ndio maana nawaasa mara kwa mara kuwa mjenge tabia ya kujituma,…usiwe
na tabia ay kutegea,..wewe uwe msitari wa mbele kwa kila jambo linalohitaji
kujitolea, kuna faida kubwa sana….’akasema babu
‘Kwa imani yangu mimi, niliyofundishwa na babu yangu….aliniambia
kuwa kila jambo, mwanzo wake ndip kwenye baraka, kwahiyo kama likitokea jambo,
ukawa wa kwanza kujitolea, zile baraka zinakushukia wewe..na zinazobakia
kidogo, zitachukuliwa na hawo watakaokuja baadaye. Na pia hata kwenye tukio la
masikitiko, au ajali, ile halai ya kwanza ya tukio, inatakiwa uonyeshe ujali
wako kwa mungu wako…kuwa mungu ndiye kawezesha hayo….’babu akatulia akiwaza
jambo.
‘Kwahiyo babu ilikuwaje kwa bibi…?’ mimi nikauliza, nikiwa
na hamasa ya kujau ni nini kilimkuta bibi na hapo babu akaniangalia kwa muda
bila kusema neno, na baadaye akasema;
‘Unajua watu walifikia hadi kuandamana kuja hapa nyumbani
kumzuru bibi yako,…’akasema babu
‘Kwasababu gani lakini ….’ikabidi niulize maana niliona kama
vile babu alikuwa hataki kusemi wazi kwanini bibi alikuwa akiandamwa na watu
kiasi hicho, mpaka hapo sikuwa nimeona ubaya alioufanya bibi hadi watu
wamchukie kiasi hicho.
‘Watu walimzushia bibi yako kuwa ni mwanga…eti bibi yako ni
mchawi…hahaha’babu akawa kama anaigiza kucheka, na kusema;
‘Bibi yako hajui hata chembe moja la uchawi….zaidi ya huo
utaalamu wa ukunga alioupta toka kwa bibi yake,….mimi ni shahidi na mungu pekee
ndiye anajua….lakini watu hawakuniskia, wakawa wamezingirwa na imani hiyo, ….inasikitisha
sana….’Akasema babu kwa uchungu, na alipotamka maneno haya, nikajikuta
nikishituka na kumkazia babu macho
‘Eti nini….mbona sioni ukweli wa hayo, mtu kujitolea
kusaidia watu,…ndio iligeuka kuwa hivyo,…?’ nikauliza.
‘Ndio ilivyokuwa kwa bibi,…na hata mjumbe alipoingilia kati
haikusaidia kitu, ilibidi bibi yako ahame mji kwa muda…na watu wakaahidi kuwa
wakimuona tena hapa kijijini watamuua,….’akatulia babu.
‘Lakini mtu kwao, bibi yako hakujali, alikaa kidogo huko
alipokwenda na baadaye akarejea na walipomuona wakawa wananong’onezana kuwa eti
ikitokea jambo jingine….linalofanana na hilo, eti bibi yako akiua mtu mwingine,
watahakikisha na yeye wanamuua…..’akasema babu kwa uchungu.
‘Na kweli walifanya hivyo…?’ nikamuuliza babu, na hapo
akainamisha kichwa akionyesha masikitiko, na alikaa hivyo kwa muda, nikajua
alikuwa akilia kimoyo moyo, maana wanaume wengine hawalii kwa sauti,….wanalia
ndani kwa ndani…na ndivyo alivyofanya babu
Alipoinua kichwa kuniangalia, niliona macho yake yakiwa
yamejaa ukungu, ….na mara machozi yakaanza kumtoka.
NB: Inasikitisha, lakini ndivyo wanadamu tulivyo…..tutazidi
kupashana kuhusu kilichotokea kwa bibi huyu..
WAZO LA LEO:
Tusiwe na tabia za kuamini mambo ya kishirikina, ..….kwani hizo ni imani zisizo
na ushahidi wa kitaalamu, …tunaweza tukajikuta tukigombana ndugu kwa ndugu,
majirani kwa majirani kutokana na uzaifu huo.
Swali ni kuwa Je una uhakika gani kuwa mtu fulani ni
mchawi?....Kama una uhakika huo, basi ufikisheni huo ushahidi kwenye sheria,
ili haki itendeke,….tukichukulia sheria mkononi, tunaweza tukahukumu mtu asiye
na hatia, na wenye hatia wakaendelea kutenda makosa hayo.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Thanks for sharing your info. I truly appreciate your efforts and I am waiting for your next write
ups thanks once again.
Check out my web site - galaxy s4
I'm gone to convey my little brother, that he should also pay a visit this web site on regular basis to take updated from hottest news update.
Feel free to visit my blog post :: hcg diet direct
Also see my website > hgc diet
Post a Comment