Mama akawa anaendelea
kunisimulia kuhusu maisha yake kuthibitisha yale aliyonismulia babu, na safari
hii alionekana akiongea kwa hisia iliyojaa huzuni, ….na hata machozi yakaonekana
kumlenga lenga,machoni….
Hali ya mume wangu ilikuwa mbaya sana, ilifikia hatua
tukasema sasa ndio safari imefika, tukabakia kusikilizia, maana kutokana na
kuumwa ugonjwa wa kifua kikuu, na kwa ubishi wake,akawa bado anakunywa, na
kwasabbu ni mzaifi, pombe kidogo, inamlewesha sana na mabaya zaidi akawa hataki
kula,…’hapo mama akatulia kidogo, halafu akasema;
‘Sasa ndio likazuka hilo la kapigwa, siamini kuwa
walipigana, hakuwa na nguvu za kupigana, nay eye anajua hilo, labda kuongea,
oooh, mume wangu mbishi, sasa sijui labda walibishana na huyo mwenzake ndio
walifikia hatua hiyo, au labda huyo jamaa alipotoka kwangu, akaona hasira
akazimalizie kwa mume wangu…sijui, na sikutaka kuulizia, kwani hatukuwa na muda
huo tena
‘Ila kwa ujuma kipigo alichopigwa sio kipigo cha kitoto,
maana hata pale aliposafishwa uso, …uso wote ulikuwa umevimba hata macho
yalikuwa hayaonekani….uso umehumuka….alibadilika kabisa….
‘Huu ni unyama…..’akawa anasikitika yule dakitari aliyekuwa
akimsafisha huyo mgonjwa, na hakuvumilia, akamuita muuguzi mwenzake, ambaye
alikwenda kumuita polisi, na polisi alipomuona huyo mgonjwa,….
‘Huyu mtu ni mwizi…?’ akauliza
‘Hapana tulikuta akipigwa na mwenzake…’tukasema
‘Ulevini sio..?’ akauliza
‘Hawakuwa ulevini, tuliwakuta njiani, na inavyoonyesha
walikutana, kwani huyo mwenzake alikuwa kwangu, na alipotoka akakutana na huyu
mgonjwa,….ni mgonjwa, kama unavyomuona, hakukuwa hata na sababu ya kugombana na
yeye…’nikasema.
‘Haiwezekani, lazima kuna sababu, …..na ni bora huyo jamaa
tumkamte, na ataeleza vizuri….’akasema huyo askari, na kweli, hawakupoteza
,muda, waliondoka kwa haraka kwenda kumkamata huyo jamaa aliyempiga mume wangu,
lakini walipofika waliambiwa mtu mwenyewe yupo taabani, hajiwezi na yeye,
amekuwa kama kachanganyikwa, na muda huo alikuwa kafungwa kamba.
‘Kuna tatizo gani kwenye hiki kijiji ….?’ akauliza huyo
askari polisi akimgeukia kiongozi wa serikali mwenye dhamana hapo kijijini.
‘Tatizo ni hawa watu wachache wanaojichukulia sheria
mikononi mwao, tunajaribu sana kuwaelimisha lakini inakuwa vigumu kwao
kutuelewa,…nafikiri imefikia hatua sasa sheria ichukue mkondo wake, maana hata
sisi viongozi tunakuwa katika wakati mgumu, na hata kutishiwa maisha yetu,
….watu wengine hasira zao ni mbaya sana…’akasema huyo mheshimiwa.
‘Kwanini hamtoi taarifa, mnasubiri hadi hali iwe mbaya kiasi
hiki, …..taarifa nyingi za vifo visivyojulikana zimefika ofisini, na
ukichunguza, hakuna ushahidi, hakuna maelezo mazuri ya kutusaidia, sasa
mnafikiri sisi tutawasaidiaje…mkilinda uhalifu, mjue ni kama mtu anamlinda
nyoka mwenye sumu ndani ya nyumba yake, ipo siku itamuuma….’akasema huyo askari
‘Tumeshaleta taarifa hiyo kwa maandishi, na jibu tulilopata
ni kuwa mtalifanyia kazi, sasa sisi mlitaka tufanye nini zaidi…’akalalamika
huyo mkuu.
‘Tunahitaji maelezo ya kina, nyie hamsemi, ni nini chanzo,
ni nani anahusika, mnafichana, mnaogopana, kama mkiogopana, eti kwa vile mtu
fulani ni mchawi, basi…tutashindwa kufanya kazi yetu….’akasema huyo askari.
‘Tumekuelewa afande,….’akasema huyo muheshimiwa akionekana
kuchoka.
‘Sasa sisi tutaanza kamata kamata, hasa kwa hawa watu wenye
sifa ya hasira,. ….si wana hasira sio, basi kuna kazi ya kuondoa hasira zao,
….kama watu kama hawo wana hasira, sisi tutazimaliza,….kwanini wasitumie hasira
zao kwenye kulima, au kuvunja mawe, wanazitumia kuharibu sura za watu….?’ Akawa
kama anauliza huku akiwageukia watu waliokusanyika hapo.
‘ Mimi huyo mtu kama ningemkuta mzima, angejuta, maana hizo
hasira zake zingeliishia pabaya….ole wake, na ole wanu, mtu mwingine atakayejifanya ana hasira…basi
atakuwa ndiye mfano, sasa na sisi tutazionyesha hasira za dola, na huyo mtu
apelekwe hospitaki, atakuwa chini ya ulinzi mkali akipona ana kesi ya kujibu….’akasema
huyo askari, na kuwaangalia watu waliokuwepo hapa, na baadaye akasema;
‘Mbona mnatupa shida sana hiki kijiji , mnataka tuwaonyeshe
kazi yetu sio,…haya mtaiona, kuanzia sasa mtaiona kazi yetu..’akasema huyo
askari, na kuondoka, na haikupita mtu, kundi la maaskari likaja na kuanza
kuwazoa watu, kila aliyekutwa mitaani bila kazi akabebwa kwenye gari lao,….
******
Siku ya pili nilikwenda kumtembelea mume wangu, na nilimkuta
akiwa bado kalala, uso kidogo ulikuwa unatazamika, uvimbe ulishaanza kupungua…
nikamuamusha ili apate kunywa kifungua kinywa, lakini alikataa kabisa kunywa
uji, alisema mdomo umevimba, na una madonda, hawezi kula. Nilikwenda kuongea na
docta kungalia jinsi gani tutamsaidia, docta akasema;
‘Huyo kaumizwa sana mdomoni, …..mpe uji kidogokidogo,…baadaye
tutamuwekea maji yenye lishe, ……lakini kwa sasa jaribuni kumnywesha huo uji
kidogo kidogo…’akasema.
Tulifanya hivyo, lakini ilikuwa ni kazi ya kulishana kama
mtoto mdogo, hakutaka kula kabisa, na muda wote alikuwa akilalamika maumivu,
maana hata mbavu zilikuwa zimejeruhiwa, kifua ndio usiombe, alikuwa akikohoa
utafikiri ni gari linapandisha mlima.
Kwa ujumla baba yako alikuwa katika hali ya kusikitisha
sana,….kipindi hicho wewe ulikuwa mdogo,…na likuwa akikupenda sana. Na jinsi
nilivyomuona mume wangu akiteseka vile, hata mimi hasira zilinipanda, na
moyoni, nilikuwa sina amani tena na huyo mtu aliyempiga mume wangu. Nilitamani
kama ningelikuwa mwanaume, niende nikapigane naye, hadi hasira zangu zishuke…
‘Mume wangu, jitahidi kula, maana usipokula dawa hazitaweza
kufanya kazi….’nikawa namwambia lakini ilikuwa ni vigumu kwake, …..ilifikia
hatua, ndugu zake walikuwa wanakuja, kuanza kumkaripia, lakini hawakujua kuwa
yey hapendi iwe hivyo…ina maana hamu ya kula ilikuwa haipo tena.
‘Ni heri kufa kuliko haya mateso ninayoyapata…..kila sehemu
inauma, ….mdomoni kuna vidonda, ….huyu mtu alikuwa akinipiga ngumi za mdomoni,
sijui mdomo wangu ulimkosea nini…’akawa anaongea na sauti yake ilikuwa ikitoka
kama mtu aliyezibwa mdomo.
‘Kama ningelikuwa na afya yangu, …asingeliweza kabisa
kufanya hivi…..ningepambana naye kiume, lakini alijua kuwa sitaweza kujitetea,
basi akanifanya gunia ….ole wake nipone….’akawa anasema huku machozi yanamtoka.
Wiki ilipita, na baadaye hospitakini, walimruhusu wakisema
kwa sasa kinachohitajika ni dawa, kula na kufuata masharti, haina haja ya yeye
kuendelea kulazwa hapo hospitaini, akaendelee kutibiwa nyumbani. Na mmoja wa
madakitari akashauri kuwa pia tunaweza kutumia tiba mbadala.
‘Siku hizi kuna dawa nzuri tu, ila muwe makini, sio dawa
zote zinasaidia, na pia hakikisheni kuwa dawa hizi anazotakiwa kutumia,…za
kifua kikuu, haachi hata mara moja….’akasema.
Sisi kwa uoni wetu mfupi, tuliona ni dalili ya kuwa hatapona
tena. Tukamchukua hadi nyumbani, na ikawa kazi ya kumtibia kwa hizo dawa za
kifua kikuu na dawa za tiba mbadala, kuna muda dawa hizo zilisaidia, lakini
huyu mume wangu pale akipata nafuu kidogo anachojua yeye ni pombe. Akawa
aanvunja masharti moja baada ya jingine.
Akaanza kuchoka , na hali yake ikazidi kuzorota, na alipozidiwa
kipindi hiki, hali yake ikawa mbaya zaidi ya hata ile ya mwanzo, akawa ni mtu
wa kitandani , kila kitu kinafanyikiwa kitandani, alibakia mifupa mitupu …ndugu
na jamaa zake waliokuwa wakifika fika wakawa hawafiki tena, nikabakia mimi na
yeye.
Babu yako ndiye aliyekuwa mtafutaji,…..mimi biashara
zikasimama, na hali ilivyozidi kuwa mbaya, tukaanza kutumia mtaji, hali ikaanza
kuwa mbaya zaidi, hata nyumba ya babu yako ambayo ilikuwa kukaribia kuisha
ikabidi isimame, sikuwa na kitu tena, pesa yote ikaniishia vikabakia vitu vichache
dukani. Na siku moja wakatuingilia wezi kwenye duka langu, wakakomba kila
kitu,…tukabakia mkono mtupu, …
‘Hili sasa ni janga……’nikasema.
‘Hapa kuna kitu, nahisi kuna jambo linakwenda kinyume,
…..’akasema babu yako. Babu yako sio mtu wa kukata tamaa mapema, na akisema
jambo ujue kweli limemfika, na mara nyingi akisema jambo, ujue kuna ukweli
ndani yake.
‘Baba unafikiri tumefanya nini kibaya hadi tukutwe na
majanga yote haya?’ nikamuuliza.
‘Nahisi mume wako kuna makosa aliyafanya, ….nilijaribu
kumdadisi sana, nimegundua kuwa kuna dhuluma aliifanya, na alipata muda wa
kutubu, lakini hakufanya hivyo, alitakiwa kwenda kwa huyo aliyemfanyia hivyo, angalau
akamuombe msamaha, lakini hakufanya hivyo, na sasa…nahisi, keshachelewa…’akasema
.
‘Baba una maana gani kusema keshachelewa….kwani sisi
hatuwezi kufanya kwa niaba yake?’ nikamuuliza.
‘Hali yake ilivyo, inaashiria hivyo…hizi ndoto zangu sio za
kawaida, naona nisafiri kidogo, nikirejea tutajua ni nini la kufanya, ….toba ni
yeye mwenyewe mkosaji na mkosewaji,….nikirudi tutaliangalia hilo, kuna dawa
zinahitajka, za tiba mbadala kwa matatizo kama hayo, unakumbuka zilivyomsaidia
mwanzoni, ..zile hazipatikani hapa, na mpaka huko milimani…kwa wenzetu wacha
mungu…’akasema na kweli kesho yake akazifuatilia.
Siku alipoondoka, mume wangu akawa kama kapata nafuu,
nakumbuka usiku huo tuliongea naye sana, kiasi kwamba nilijua kuwa keshaanza
kupona, akawa ananisimulia enzi nzetu za ujana, tulipoanzia urafiki wetu,
akasimulia maisha baada ya mimi kupata ujauzito wako…yaani tuliongea saana,hadi
raha, na moyoni nikawa anmuomba mungu hiyo hali iendelee kuwa hivyo, kwani ni
dalili njema.. ..
‘Mke wangu, nataka kesho ukamtafute yule mtu wa ardhi, yule
aliyetusaidia hadi tukaweza kuandikisha hati ya nyumba,….’akasema
‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza kwa mshangao.
‘Unajua mke wangu nimekumbuka jambo…ile hati niliandika jina
langu, na kipindi kile nilifanya kwa hasira, sasa nimegundua kuwa nilifanya
makosa. Sikustahili kabisa kuandikisha jina langu, maana hii nyumba ni yako,
ulijenga kabisa kwa pesa zako….sasa iweje, niandike jina langu….’akasema.
‘Lakini wewe ni mume wangu, na wewe na mimi ni kitu kimoja,
ndio maana nikakubali tukafanya hivyo , mimi sioni ubaya…’nikasema.
‘Hapana kwa hali kama hii….inahitajika tubadi hiyo hatii
haraka, ….nahisi nimetenda ubaya, ..je huoni kuwa nikifa watu wakiona hiyo
hati, watakusumbua, …nawafahamu sana ndugu zangu, naomba kesho fanya hima
tubadili hiyo hati ya nyumba..’akaniambia.
‘Mume wangu hilo lisikutie shaka, hakuna mbaya atakayekuwa
na moyo sugu wa kufanya hivyo, wote wanafahamu kuwa nyumba hii ni yetu,
japokuwa nimejenga mimi,….lakini mimi na wewe ni kitu kimoja. Hakuna asiyejua
hilo, ndugu zako wote wanafahamu hivyo,..na kwanini ufikirie kufa, wakati hali
yako inaonyesha kutengamaa….?’ Nikamuuliza.
‘Kufa hakuna hodi…..lakini dalili hazijifichi..mimi nikifa
hakuna shaka, kila dalili ipo, na kwanini niendelee kuishi, na kukutesa mkewe,
angalia unavyoteseka, nakuonea huruma sana mke wangu, angalia ndugu, jamaa wote
wametukimbia, na hali inazidi kuwa mbaya, umaasikini umetuingia , magonjwa ndio
haya, sio kwamba napenda kukutesa hivi…sipendi kabisa mke wangu…najuta sana
kwani ukiangalia nahisi haya yote yanatokana na mimi…’akasema.
‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza.
‘Mke wangu sikupenda kabisa kukusimulia maisha yangu ya
gizani, …sipendi lakini wakati mwingine nahisi unastahili kuyafahamu….’akasema.
‘Mume wangu achana na hayo…wewe tulia, tuliza moyo wangu,
tuganga haya yaliyopo, hali yako haitaki magumu, unatakiwa utuize kichwa…’
nikamwambia, lakini ilionekana kuwa alikuwa na dhamira yake, akasema;
‘Mke wangu nimepitia maisha mabaya,…kipindi kile
ulipoonadoka, nilijiingiza kwenye kundi haramu, …na humo kwa tamaa ya kutafuta
utajiri nilijikuta nikifanya mambo mabaya sana, yote ikiwa kutafuta mali,….na
moyoni nilifanya hivi kwa ….. ili tukikutana niwe mtu miongoni mwa watu.
Mawazoni nilijua utakuwa umekutana na tajiri, sasa roho ikawa inaniuma, kuwa
huenda umenikimbia kwa sababu hiyo, sikuwa na mawazo kuwa umenikimbia kwa
kitendo nilichokufanyia ….sasa sikutaka nishindwe kukupata,kwahiyo nikaanza
kutafuta utajiri kwa nguvu….’akasema.
‘Lakini hayo yamepita mume wangu, sasa hivi umebadilika,yaache
kama yalivyo …na ukipona unaweza kwenda kutubu dhambi zako kwa hawo
uliowafanyia ubaya, kama unawafahamu…lakini hata hivyo hakuna ambaye atakuwa na
kinyongo na wewe kwa hali uliyokuwa nayo….umeshateseka vya kutosha…’nikamwambia.
‘Mhh, utatubuje dhambi za kuua…’akasema
‘Ina maana uliwahi kuua?’ nikamuuliza.
‘Mke wangu, nakuambia nilijiunga na kundi haramu, kundi la
ujambazi, na kuna wakati tulikuwa tunakwenda kupora kwenye maduka tukiwa na
silaha, sijui wenzangu walizipatia wapi, na wao ndio walionifundisha kutumia
silaha,….kwa vile niliona raha kuikamata, basi walipokuwa wakiamrisha
ua….nafyatua, mke wangu nimeua,na kila nikiwaza hilo, ndio maana naishia kulewa
..’ akatulia kwa muda, halafu akasema;
‘Sijui kwanini nilibadiliak kiasi kile, lakini nilikuwa
sipendi, kufanya hivyo, wenzangu walikuwa wakinisukuma nifanye hivyo, na kwa
vile nilikuwa nikitafuta pesa, nikajikuta nimeingia bilA kupenda kwenye makundi
haramu,….’akasema.
‘Oh, ….hayo yamepita mume wangu, kama ulifanya hivyo, na
umekiri makosa yako, mungu atakusamehe, iliyobakia sasa ni wewe upone, na
ukipona kama nilivyokuambia utakwenda kuwaomba msamaha, hawo
uliowakosea…’nikamwambia.
Mke wangu,…sizani kama nitapata muda huo..naomba iwe hivyo,
na kweli nikipona, itakuwa kiguu na njia kwa kile niliyemfanyia huo
ubaya,…..nikipona, nitakuwa mtu mwema sana,..nitaacha pombe, nitaacha sigara,
nitakuwa mcha mungu,….nikipona mke wangu,…sitarudia tena, nakupenda sana mke
wangu, …’akasema na usingizi ukawa unatunyemelea, na kabla hajalala, akasema.
‘Ukumbuke mke wangu kufuatilia kubadilisha hati ya nyumba,
ni muhimu sana….’akasema na usingizi ukampitia.
**********
Nilipoamuka babu yako alikuwa amerudi na dawa na alikuwa kakaa
nje, na kuzianza kuzitengeneza, na mimi, nikadamka kwenda kumuona huyo
aliyetusaidia kubadili hati ya nyumba, ….maana kulikuwa na mwendo kidogo wa
kutembea. Niliamua kufanya hivyo, kwani mume wangu aking’ang’ania kitu,
hatatulia mpaka ukitekeleze. Basi nikafanya hivyo, kwani hata babu yako
alikubalina na hilo kabla ya kuondoka nilimwangalia mume wangu ambaye likuwa
bado amelala, na alifunua macho kidogo, akataabsamu akasema,
Hapo mama akatulia, …na machozi yakaanza kumtoka, nilitamani
nimwambie mama asiendelee kama kuongea huko kunamzidishia uchungu, lakini
sikuweza kumnyamazisha , nilitaka nijue yote, na alipotulia kwa muda, akasema;
‘Hilo ndilo tabasamu la mwisho la baba yako…lipo akilini
mwangu wakati wote….’akasema na kuinama, baadaye akainua kichwa na kuendelea
kuongea akasema;
Mume wangu alipotabasamu hivyo, akasema; ‘Nenda mke wangu,
ni muhimu sana, nakupenda sana mke wangu, ..’akafumba macho, na mimi nikajua
kuwa amelala.
‘Baba nitarudi mapema tu, kama nikichelewa, naomba umnyweshe
huo uji upo tayari kwenye chupa,…’nikamwambia babu yako.
‘Usiwe an shaka, kwanza hiyo dawa yenyewe inahitajika kuweka
kwenye uji,…kwahiyo hilo niachie mimi, huyu ni mtu wangu tunajuana,
nikimnywesha mimi atakunywa, siunona wewe mwenyewe……’akasema babu yako, na ni
kweli ukitaka baba yako anywe uji au ale chakula, uhakikishe babu yako yupo.
‘Mimi nitaiweka hii dawa kwenye uji kabla ya
kumnywesha,….hii dawa akiinywa tu, kesho utaniambia,..atakuwa mzima kabisa, cha
muhimu asirudie tena pombe..’akasema na mimi nikaondoka.
Nilifika kwenye ofisi
za wilaya, na kuingia ofisi za ardhi na majengo, lakini huyo mtu anayehusika na
kubadili hati, alikuwa kasafiri, ila walianiambia kuwa akirudi watamtuma afike kwangu
kwa haraka, ila walinishauri kuwa inahitajika pia huyo mume wangu andike barua
ya kuomba hayo mabadiliko, ikiwa na sahihi yake, halafu baadaye kuna fomu za
kujaza. Basi nikaondoka nikiwa sina mashaka,….sikuwa nimelitilia maanani sana,
kwahiyo nikarejea nyumbani.
Nilipokaribia nyumbani kwangu, nikahisi mwili ukinisisimuka,
….nilihisi hali isiyo ya kawaida ikinijia mwilini, nilihisi wasiwasi ..nikajipa
moyo kuwa hakuna kitu kibaya kitatokea….nikafika kwangu na nikamkuta babu yako
akiwa kakaa kati kati ya mlango panga likiwa mkononi.
‘Baba vipi mgonjwa anaendelea vipi?’ nikamuuliza huku
nikitaka kumpita niingie ndani na nilihisi kama anataka kunizuia, lakini
baadaye akasogea pembeni na kusema;.
‘Mwanangu…karibu ukae kwanza, maana hiyo dawa,….kama
angeliwahi kuinywa, tungelizungumza mengine, lakini hakuwahi kuinywa,….’akasema
na moyo wangu ukalipuka , nikahisi kizungu zungu, sikusubiri kusikiliza zaidi ,
nikampita baba kwa haraka na kuingia ndani.
Niliingia ndani alipokuwa kalala mgonjwa, nikakuta kitanda
kipo kitupu….nikashikwa na bumbuwazi, maana mgonjwa alikuwa akihudumiwa kila
kitu kitandani, nakujiuliza ina maana mgonjwa keshapona, …sikuamini, nikarudi
hadi pale alipokuwa kakaa babu yako, nikamkuta kasimama kashika mashavu kwa
viganja vyote viwili, huku kainama chini.
‘Baba mgonjwa yupo wapi, mbona hayupo ndani?’ nikauliza.
‘Kachukuliwa na ndugu zake, ….ndugu zake wamekuja hapa na
vurugu nyingi, kulikuwa na mapigano hapa, ….wao wamesema wanamuhitajia ndugu
yao , kwani wanataka wakamtibie wenyewe, wanadai wamegundua dawa ya kumtibia,
na kuendelea kukaa hapa hatapona. Wanadai kuwa wewe ndiye kikwazo cha ndugu yao
kupona, ….’akasema kwa hasira.
‘Wana maana gani hawa watu, siku zote nahangaika peke yangu
na mgonjwa, hakuna hata mmoja aliyekuja kunisaidia…tunahangaika mimi na wewe
baba yangu. Hebu fikiria wewe baba hujatuzaa, lakini umekuwa na uchungu zaidi
ya ndugu wa kuzaliwa tumbo moja,….hebu fikiria baba hata kutoa dawa hata siku
moja hawajawahi kufanya hivyo…sasa sijui leo wameona nini hadi kufikia hatua ya
kuja kumchukua, hawa watu wana lao jambo …!’ nikasema kwa hasira.
‘Unajua nilipambana nao, lakini baadaye nikaona kwanini
niwazuie…..huenda kweli wana dawa nzuri, zitamsaidia mgonjwa, basi nikawaacha
wakambeba wakaondoka naye, na nilifanya hivyo kwasababu mume wako, baadaye alipenda
iwe hivyo, nafikiri baada ya kuona vurugu imezidi,…kwakweli mue wako mwenyewe aliweza
kuongea na mimi, akanisihi sana niwaachie wamchukue, na hata dawa nilikuwa
sijampa, ndio nilikuwa karibu kumlisha , wkaingia….oh na ili kuondokana na
vurugu hiyo, mume wako akasema ngoja wanachukue,….’akasema babu
Basi nilivyosikia hivyo sikuweza kutulia tena, moyo uliniua
sana, …na kwa vile nawajua sana hawa watu, nilijua kabisa akifika huko hatapata
huduma yoyote….wana lao jambo,….mimi sikukubali, nikamwambia babu yako ni
lazima nifike huko kwa mume wangu, maana mimi ndiye ninayejua anatakiwa ale
nini, na wao wanaweza wakamtelekeza…..babu akasema ni sawa, lakini ni lazima
tuongozane naye, maana hawaamini sana hawo watu wanaweza wakanidhuru,…’akasema
mama akiwa kashika shavu.
‘Basi tukaondoka na babu yako, akiwa na panga lake mkononi,tukaongozana
naye, na tulipofika huko, hatukupewa nafasi ya kumuona, walikataa kata kata,
wakisema kuna miiko ya hiyo dawa anayotumia, hatakiwi kuonana na mtu yoyote
zaidi ya yeye na huyo mganga wake.
Basi tulikaa pale tukisubiria kama tutaruhusiwa kumuona,
lakini walikataa kata kata, na hata ilipofika jioni, tukarudi nyumbani.
‘Baba hii sio haki, kwanini wananifanyaia hivi hawa watu,
hawajui kuwa yule ni mume wangu na nina haki ya kuonana nay eye…..?’
nikamuuliza babu yako.
‘Mwanangu vuta subira, usilazimishe jambo, ….kila jambo huja
kwa maana maalumu, hawa kuna kitu wanakitafuta kutoka kwa mume wako, na wanajua
akiwepo na wewe hawatakipata….’akasema babu yako.
‘Kitu gani hicho…?’ nikauliza.
‘Kwakeli sijui, sisi tuvute subira, na tuombee kuwa
wamemchukua kwa wema, najuta kuwa sikuwahi kumpa ile dawa, na kama angekunywa
angalau kidogo, angelipata nafuu, sasa sijui huko watampa dawa gani….’akasema
babu.
Tukafika nyumbani, na nilipofika nikahisii mabadiliko mle
ndani, vitu vilivurugwa, na sijui hawa watu walikuwa wakitafuta nini…na
nikaanza kuvipanga, taratibu ili huenda nikagundua kuna kitu gani kinakosekana,
na wakati nahangaika kupanda vitu, ghafla mlango ukagongwa,..
‘Ni nani mwenzangu..?’nikauliza kwani babu yako aliaga
kwenda kwenye eneo lake, kuangalia ujenzi, japokuwa umesimama.
Na mara yule mtu akaingia na babu yako alikuwa nyuma yake,
na nilivyowaangalia machoni nikagundua kuwa kuna taarifa mbaya. Miguu ikaanza
kutetemeka, mwili ukaisha nguvu kabisa.
WAZO LA LEO: Mkishaona mjue nyie ni kitu kimoja, onyeshaneni
upendo zaidi pale mnapokuwa kwenye shida,…hasa kipindi mkiwa katika hali ngumu. Onyashaneni upendo
pale mmoja anapokuwa anaumwa, ujue wewe ndiwe upande wa pili wa mwili wa mwenzako,
usiondoke karibu yake, kwani ukiondoka karibu yake, upande uliobaki ni mbovu
hautaweza kuhimili kusimama peke yake. Kumbuka rafiki wa kweli ni yule
anayekufaa wakati wa dhiki.
Ni mimi:
emu-three
9 comments :
Howdy I am so excited I found your blog, I really found
you by mistake, while I was researching on Yahoo for something else, Regardless I am
here now and would just like to say thanks for a tremendous post and
a all round entertaining blog (I also love the theme/design), I don't have time to browse it all at the moment but I have saved it and also added your RSS feeds, so when I have time I will be back to read a great deal more, Please do keep up the excellent work.
Take a look at my blog ... http://www.babesflick.com/category/273/lesbian-porn/
kusema ukweli kaka unajua kutoa mafundisho kwa njia ya hadithi. ubarikiwe sana.
It's hard to come by experienced people in this particular subject, however, you sound like you know what you're talking about!
Thanks
Here is my homepage; http://www.cfnmfever.net/
duhhh ndugu wa mimi..Aminia sana..kuanzia kisa mpaka Wazo la Leo..unawazisha kwa sauti sana..MUNGU azidi kukubariki sana sana..tutafika tuu...
Pamoja sana.
Today, I went to the beach with my kids. I found a sea shell and gave
it to my 4 year old daughter and said "You can hear the ocean if you put this to your ear." She put the shell to her ear and screamed.
There was a hermit crab inside and it pinched her ear.
She never wants to go back! LoL I know this is completely off
topic but I had to tell someone!
Feel free to surf to my page paid surveys, http://paidsurveysb.tripod.com,
Saved as a favorite, I love your site!
Here is my blog post; quest bars
Wow, marvelous blog layout! How long have you been blogging for?
you made blogging look easy. The overall look of your web
site is excellent, as well as the content!
my homepage ... minecraft.net
Hey there! Do you know if they make any plugins to help with SEO?
I'm trying to get my blog to rank for some targeted keywords but
I'm not seeing very good results. If you know of
any please share. Appreciate it!
Have a look at my blog post: free music Downloads (twitter.com)
If you are going for finest contents like me, only pay a quick visit this web site everyday for the reason that it presents feature
contents, thanks
Here is my web-site - free minecraft games
Post a Comment