Tulikuwa tunakwenda
Morogoro, ilikuwa asubuhi sana, kibaridi kilikuwa kikali na costa tuliyopanda
ilikuwa na mwendo mkali ajabu….maana tulipoteza muda mwingi pale Ubungo
kutokana na foeni za magari,…kwenye hilo basi pembeni yangu alikuwa kakaa jamaa
mmoja, aliyevalia ile inayoitwa suti ya vipande vitatu, na mawani meusi
machoni, nikajua nipo ni mtu wa watu,-kama sio muheshimiwa basi ni mkuu wa
watu, kaamua leo, apande basi, na kuacha gari lake, huenda lipo kwa fundi,kwahiyo
nahitajika kuwa makini. Siunajua tena unatakiwa uishi na mtu kutegemeana na
alivyo.
Cha jabu Jamaa huyu alikuwa haongei,…moyoni nikajua huenda
lugha inampa shida, hawa wenzetu waliosoma nje, wanapata shida sana kuongea Kiswahili,
basi nikamkubali hivyo, na mimi nikakaa kimiya. Kila nilipopata nafasi nikawa
namchungulia kwa kujiiba, na mara nyingi
alionekana kukunja uso pale watu wanapozungumza maswala ambayo hakupendezwa
nayo….nikajua ahee, kumbe Kiswahili anakisia labda kuongea ndio kunampa shida…,
na kama ni maswala anayopendezwa nayo, alikuwa akitikisa kichwa kuonyesha
kukubali,na hata kutabasamu....nikajisema moyoni, ahaa, huyu jamaa anaonekana
mwingi wa hekima na busara, hataki majungu....
Foleni ilikuwa kali, na hadi kutoka pale ubungo na kuingia
Kimara ilichukua karibu saa nzima, kwahiyo tulipotoka hapo dereva akataka
kufidia huo muda, akakanyaga mafuta kisawasawa. Tukifaka sehemu, nikamuona jamaa
akihangaika, na kila mara alikuwa akijaribu kusimama, na akawa anamuangalia
kondakita, mara anaangalia nje, na kusema; `ndio penyewe…’
Sikuelewa ana maana gani, na mara nyingine akawa anawaangalia
abiria, na watu mle ndani walikuwa wakiongelea mambo yao na kucheka, hakuna
aliyekuwa na habari na yeye sipokuwa mimi niliyekuwa nimekaa naye, kilikuwa
kiti cha watu wawili, na kulikuwa na yale mapazia ya dirishani kwahiyo yaliweza
kumfunika muheshimiwa,….huku mziki kwenye hilo gari ukisikika kwa sauti kubwa,
mara huyu jamaa akaniuliza;
'Hivi leo hakuna sehemu ya kuchimba dawa….maana mara nyingi
tunasimama eneo hili?' akaniuliza, na hapo nikajua kuwa kumbe ni mwenzetu hata
kuchimba dawa anakufahamu, nikaingiwa na kujiamini,nikijue huyu ni mswahili mwenzetu hapo nikasema;
'Ulimsikia konda alivyosema, hakuna kulala, moja kwa moja
hadi Moro, lkn kama umezidiwa mwambie konda...'nikamwambia, yeye akainama chini
na kuchukua chupa ya maji aliyokuwa nayo tangu awali, akamalizia maji
yaliyokuwemo.
'Oh, hapa nilipo, nikisimama tu nimeadhirika...na nina mwiko,
nalinda miiko,....siunajua tena mambo ya miiko….'akasema, na hapo nikamuongezea
sifa nyingine kuwa sio mwenzetu tu, bali ni mwafrika asilia, maana wengine
wakisoma wanasema wao wamezaliwa Afrika kimakosa, lakini huyu alionekana kuwa
mwafrika asilia...
'Una matatizo ya kibofu...?' nikamuuliza, nikiwa namtania,
maana nilishjiamini kuwa kumbe hana shida, unaweza ukaongea naye hata kama ni
utani
'Sio hivyo, na sijui .....oh, samahani sana, ....sijui kama
utanielewa, lakini inabidi nifanye hivyo…'akasema na mara akachukua ile chupa
ya maji aliyokuwa nayo, na kuhangaika kujifungua vifungo vya suruali, na huku
akijificha…kwa kulivuta lile pazia, limfunike….na kwa vile kile kiti kilikuwa
kirefu , watu wa nyuma hawakujua ni nini kinaendelea, na hata mimi nikajifanya
simuangalii, na kujaribu kukaa vyema ili kumlinda asionekane na watu wa upande
wa pili…, maana nilijua kuwa huenda jamaa alikuwa kazidiwa sana.
Mara akafanya alichofanya na kuendelea kujihudumia na, chupa ya nusu lita karibu ijae….na
ashukuru kuwa sauti ya mziki kwenye hilo gari ilikuwa kubwa, kwahiyo hakuna
aliyesikia ile…borooooo!
'Oh, afadhali...ningeadhirika,...samahani sana, haja
ilinibana kweli, na haya...mambo ya miiko, la sivyo ningelimsimamisha
konda,....aah, mambo haya bwana....nikifika kijijini nitayamaliza....maana huyo
mtaalamu kaniambia nikitimiza kila jambo, udiwani ni wakwangu mwakani tena..hata
nikitaka ubunge, nitaupata…ni kazi kweli…' alitamka hayo maneno na kunifanya nishituke.
'Kumbe ni muheshimiwa, ...'nikajisema moyoni.
'Unajua huwezi kuamini haya mambo, hata mimi nilikuwa hivyo, ...lakini sasa hatua kwa hatua nimeshatimiza
karibu kila kitu…'akasema. Sikuweza kumsemesha maana ile hali niliyoiona
usingeliweza kuongea, na hicho anachoongea na jinsi alivyo, haiviendani kabisa....nikawa
najifanya kulala.
Mawazo yangu yalikuwa ni jinsi gani atavyoweza kutupa ile
chupa iliyojaa haja yake…na kama
angelitupa nje, ningelimshambulia, kwa maneno, maana watoto wataokota hizo
chupa na wengine wakiona kitu kama maji wanaishia kuchezea,…nikashukuru kuwa
hakutupa, akawa kaweka mapajani kwake…
Tulipofika sehemu, nikamuona akiniangalia kwa
kujificha,....mimi nikajifanya nimelala, mara akafungua ile chupa,
aliyohifadhi haja yake, ....na
hutaamini, jamaa akaiweka mdomoni,....akamimina....ile haja yake yote
tumboni,...huku akiwa kafumba macho kuonyesha kuwa hakupendezewa na hicho
anachokifanya...mimi sikuweza kuvumilia, nikafungua macho ya mshangao
nikamuuliza...
Mbona hivyo...huoni huo ni uchafu...'nikasema na mara
akanifinya kuashiria kuwa ninyamaze, akasema;
'Oh, sasa nimeokoka, mambo safi kabisa.....nimepona, sina shida
tena.....'akasema.
'Vipi mbona unaongea peke yako...?' nikamuuliza kujifanya
sikuliona hilo alilolifanya.
'Hakuna shida.....nimemaliza shida yangu, na kila kitu
kimeenda kama ilivyotakiwa nifanye,...sina wasiwasi tena, maana ningeliweka wapi huo
mzigo, ni mwiko...sitakiwi kufika nao ukweni,... sitakiwi kutupa....sasa
nimeuhifadhi mahali pake, na...nikifika kwa mtaalamu naumwaga ..'akasema akionyesha furaha Fulani usoni
'Unajua maana yake ....hiyo
inaashiria kumwaga sera, .kazi imekwisha, hata nikitaka ubunge mwakani, ninataupata..bila
shida..haya mambo ukiyajulia, hayakupi shida.......'akasema huku akiitupa ile
chupa nje,....na kwa haraka akachukua leso yake, akajifuta mdomoni.....
Sikuamini,...na wewe
sijui kama utaamini, lakini ndivyo ilivyokuwa....
WAZO LA LEO:Uongozi sio hisia za kishirikina, uongozi ni
wewe na wale unaowaongoza, ukawatendea kile walichokutuma, huwezi ukacheza na
nguvu za giza huku umewasahahu waajiri wako, waliokupigia kura,...ukazania
utafanikiwa, tusijidanganye kwa hilo, kwani ahadi ni deni,.....timiza ahadi
yako, kama ulisema kweli, na kama umeshindwa kwa yale uliyoahidi, rudi kwa
waliokutuma waambie ukweli, kwani mkweli siku zote hufanikiwa
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment