Kilikuwa chumba cha chini kwa chini, na giza lilikuwa kali
sana, kiasi kwamba hata masikio hayakuweza kuhisi kitu, zaidi ya jinamizi la
kuhisi kuwa kuna kitu kinapita. Pale kitandani, alilala mwanadada mmoja, akiwa
kavaliwa rasmi, hakutaka kuvalia nguo za kulalia, akijua kuwa yupo vitani. Kwa
hali kama ile hakuweza kumwamini yoyoye, hata yeye mwenyewe hakujiamini, akijua
kuwa anaweza akapitiwa na usingizi.
Akashikilia bastola yake Mkononi vyema na kuhakikisha kuwa
alivyolala, anaweza akajihami bila wasiwasi, akavuta pumzi na kuhesabu dakika
kumi za kupata usingizi, dakika kama hizo kwake zinatosha kabisa, akafumba
macho, lakini haikuwa rahisi rahisi kupata usingizi, kwani kila alipofumba
macho alijikuta kama anaota ndoto mbaya, akaona hakulaliki.
Akafumbua macho na kuanza kuangalai giza, akaona hakuna
tofauti ya kufumba au kufumbua macho, kwani vyote kwake ilikuwa ni giza totoro,
akaona ni vyema akili yake ipange mambo mapema kabla hakujapambazuka. Akawaza;
Huu ni muda wa mwisho katika mpangilio wa maisha yake, na
juhudu zote za kimaisha hapo ndio sehemu ya kujua mbivu au mbichi. Alikumbuka
wenzake alio kuwa nao, ambao, wengine wameshatangulia mbele ya haki, yote ni
kwa ajili ya kufanikisha hilo, alipowakumbuka akaguna na kusema;
‘Hayo ndio matokea ya vita, kuna kufa na kupona, ukifa ,
basi umekwenda kupumzika, lakini ukipona, hutakiwi kurudi nyuma, ….na kuosnga
mbele, ….hadi hapo utakapopata ushindi, uipata ushindi inategema na malengo
yako, kama hukuwa makini unaweza ukajikuta ukiambulia kusononeka huku wenzako
wakifaidi matunda ya jasho, hilo kwa mwanadada huyo alipa kuwa halitawezekana.
‘Mimi ndiye jemedari wa hii vita, hata kama kuna viongozi,
…..wanajiita viongozi, kazi yao kukaa ofisini, lakini mimi ndiye mpiganaji,
nastahili kufaidi matunda ya jasho langu…nitapambana hadi nione kila kitu kipo
mkononi mwangu…’akasema na kunyosha mkono kulenga shabaha…..’ akatabasamu.
Akainua kichwa na kuangalia huku na kule, na pale pale
akakumbuka jambo, …akaanza kuwaza, kuhusu vita iliyopo mikononi mwake, alijua
wapinzani wake wa karibu keshawamaliza, lakini kuna mpinzani mmoja
mkubwa,…..akageuza kichwa na kuangalia mlangoni, …akatikisa kichwa na kusema
kimoyomoyo.
‘Huyu haniwezi, ….’akasema kwa sauti.
Japokuwa haniwezi, kwa silaha, lakini ataniweza kwa akili,
yeye anajua sheria, na kwa sheria anaweza akatumia mbinu kuhakikisa kila kitu
anakipata yeye mwenyewe,….akamkumbuka jinsi
gani allivyoweza kuwahadaa wengine na mwisho wa siku yeye mwenye
akashauri kuwa dawa ya kuwashinda wengine ni kuwaziba mdomo…
‘Kwanini tuwaue, ..hawa ni wenzetu?’ akauliza huyo
mwanadada.
‘Hakuna siri ya watu wengi, hawa wote unaowaona, wakitishiwa
kidogo na polisi watasema kila kitu, dawa yao ni kuwalipua, ..na hakuna haja ya
kutumia mikono yetu, dawa yao ni ndogo tu, ….’akasema huyo mwanaume.
‘Dawa yao ni ipi?’ akauliza.
‘Watajiua wenyewe, ….’akasema na kweli ndivyo ilivyotokea,
kila mmoja aliitwa kwa wakati wake ,akapewa pesa kidogo na kutumwa kwenda
kumwinda, mwenzake,….na mwenzake huyo huyo akapewa pesa kidogo kwenda kumwinda
huyo anayemuwinda yeye, ikawa kuwinda kwa kuwindana, na wakajikuta wakiuana
wenyewe kwa wenyewe.
‘Wameshajiua, na pesa badi ipo mikononi mwetu….’akasema huyo
mwanaume.
‘Kweli wewe mjanja…’akasema huyo mwanamke.
‘Ndio katika maisha haya lazima uwe mjanja, vinginevyo,
hutaweza kushinda, …na ilivyo hivi sasa huwezi kumwamini yoyote, na dawa ya
ushindi ni kubakia peke yako, kama walivyosema hakuna siri ya watu
wawili’akasema na huyu mwanadada alipokumbuka hayo maneno, akainuka haraka pale
kitandani.
Kama mshale akajikuta yupo sakafuni akiwa tayari kwa lolote,
akapapasa macho…huku akijiuliza kichwani, ina maana kweli aliona kitu, au ni
macho yake tu, au ni hisia zake akiwa kwenye mawazo ambayo yaligeuka kuwa kama
ndoto, ….akawa kapiga goti, mwendo wa kuwa tayari kama mkimbiaji wa mbio, akalenga
bastola yake kwenye kile alichohisi ni mtu….
Kile kitu hakikosogea, akajivingirisha mara mbili na
alipotua alikuwa karibu na kile kitu alichokiona, kulikuwa hakuna kitu,…ni
mlango, lakini ulikuwa umefunguliwa nusu, na yeye alikumbuka kabisa kuwa alkuwa
kaufunga, japokuwa sio kwa ufungua, akainuka na kuegemea ukuta, huku bastola
ikiwa tayari kwa lolote lile;
‘Huyu kama ni huyu mshenzi, ni lazima nimuondoe, kwanza
atakuwa kaonyesha kutoniamini, najua hatuaminiani, lakini yeye keshajionyesha
mapema…nisipomuondoa yeye anaweza kunimaliza, na mimi sasa nahisi
kuchoka….’akasema huku akijaribu kuondoa uchomvu wa machoni.
Taratibu akawa anajisogeza hadi kwenye kiwashio c lakini
yule mwanamke alihisi kulikuwa na kitu kabla, akasogea ukutani na kha taa
ukutani, akawasha taa, kinyume na makubaliano yao.
‘Kwanini unawasha taa?’ sauti ikasikika nyuma yake na haraka
akageuka bastola ikiwa mkononi.
‘Nilijua tu kuwa umeingia chumbani mwangu, na hili ni
kinyume na makubaliano yetu’akasema.
‘Ni kweli lakini katika hali tuliyo nayo, hakuna wa
kumwamini mwenzake…’akasema huyo mwanaume, naye kiwa kashikilia bastola
mkononi.
‘Ni nini unataka?’ yule mwanamke akauliza.
‘Bila shaka unajua ni kitu gani nakitaka….nimeshahisi kuwa
unaweza ukanisaliti muda wowote, kwahiyo ni bora tukagawana kila mtu akajua
ustaarabu wake’akasema huyo mwanaume. Yule mwanadada akaona kidole cha yule
jamaa kikicheza cheza kwenye kiwambo cha kufyatulia, akajua huyo jamaa ana
dhamira ya kweli ya kumuua, akawa anatafuta sehemu ya kuchupa, wakati na yeye
akifwa keshakifikisha kidole chake kwenye kiwambo cha kufyatulia risasi. Hapo
ujanja ni kupata…
******
Akiwa kitandani usingizi ulikuwa hauji, na alijua kuwa
vyovyote iwavyo, hivi sasa polisi wanaweza wakawa wamejizatati na kugundua
mengi kuhusu kuroroka kwao, na huenda wameshagundua kuwa sasa hivi wapo Dar.
Japokuwa usingizi haukuwepo, lakini mara kwa mara kulikuwa
na usingizi wa mang’amung’amu, ulikuwa unamjia na kuondoka, na kila ulipomjia,
alijikuta anawaza kama vile anaota,….
‘Watu wote wanauhusika ambao wanaweza kujua wapi tulipo
wameshaondoka dunia, waliobakia ni wale ambao hawajui lolote, ….mtu wa hatari aliyebakia
kwa sasa ni huyu mwanamke, na kwa hali ilivyo, siwezi kumwamini hata kwa
sekunde moja, …yapo mawili, kugawana na kila mmoja akashika njia yake, au
kummaliza kabisa….’akasema huku akivuta sigara yake.
‘Huyu kummaliza sio kazi rahisi….kupambana naye ni sawa na
kupambana na `bataliani’, ni sawa na
kupambana na kikosi kizima cha makomandoo….’akasema huku akigeuka kuangalia
bastola yake iliyopo pembeni mwake.
‘Sasa nifanyeje?’ akajiuliza.
‘Aaah, mimi ni mwanaume bwana, siwezi kushindwa na
mwanamke…’akasema na akatupa kile kichungi cha sigara, akaweka mkono wake
kitandani kuikamata ile bastola yake, hakujua kuwa wakati anajinyosha, ile
bastoal aliisogeza bila kujua,..
Mkono wake, ulipotua pale alipokuwa kaiweka bastola yake
akajikuta anapapasa hewa,…hali ile ilimshitua sana, akainuka kwa haraka na
kuangalia huku na kule, akiwa tayari keshahisi kuwa mwenzake keshaingia na kumuwahi,….
Alipohakikisha kuwa hakuna mtu, akageuka kuangalia
kitandani, hakuwa na uhakika,…mtu pekee mwenye uwepesi, kiasi hicho ni huyo
mwanamke,…hakuna mtu mwingine anayemfahamu angeliweza kuingia haraka kiasi
hicho na kuichukua bastola yake, ….akasema huku akiangalia kitandani, …akaiona,
kumbe wakati alipopitiwa na usingizi alikuwa kaisogeza ile bastola mbali na
pale alipokuwa kaiweka….
‘Dawa ya kuondokana na huu wasiwasi ni kuhakikisha kuwa nipo
peke yangu, kwani nikiwa karibu na huyu mwanamke ambaye anabadilika kama
kinyonga sitaweza kuwa na amani….huyu mwanamke kanifanya nikaitelekeza familia
yangu, yote nikimjali yeye zaidi,…lakini namjua hapo alipoa anatafuta njia za
kunimaliza, kwasasa sina maana kwake…’akawa anaongea peke yake.
‘Kwana jiulize kama ni mpenzi wangu wa kweli, kwanini
hakupenda tukalala chumba kimoja….’akasema huku akipuliza moshi wa sigara juu,
‘Kwa mtaji huo ana lake jambo, na mimi nimeshashituka, dawa
ni kumuondoa ….’akasema huku akiwa kaishikilia ile bastola mkononi, akaangalia
mlango unauelekea chumba alipolala huyo mwanamke.
‘Yeye peke yake ndiye aliyebakia , ambaye anajua kila kitu,…lakini
lazima niwe na sababu za kumuendela , oh, sijui huyu jamaa tuliyemtua atakuwa
keshamaliza hiyo kazoo tuliyomtuma,…sijapata taarifa yoyote, na kwa jinsi
ilivyo siwezi kumpigia simu kwa sasa.
‘Lakini kwa jinsi ninavymfahamu huyu jamaa yangu, … docta
kwa sasa atakuwa maiti, kama kweli huyo
mtu tuliyemtuma kafanya kama tulivyomuagiza,…..’akasema huku akiangalia kule
mlangoni huku akikumbuka maagizo yake aliyompa yule mtu waliyemtuma kummaliza
docta.
‘Pesa hii hapa, hakikisha unakwenda kummaliza yule
docta,…yule tuliyekuonyesha mchana, uhakikishe kakata roho, ndio uje uchukue
sehemu yako iliyobakia, na kama haikutokea hivyo, wewe mwenyewe utakuwa
marehemu…’akamwambia huyu jamaa.
‘Mimi tena mkuu, hiyo kwangu ni kazi rahisi, ila naomba
nikirudi hapa pesa yangu iwe tayari, maana sitaki kuishi haya maisha tena,
nataka nitubu dhambi zangu niachane na hizi kazi za kuua watu wasio na hatia…,’akasema.
Huyu jamaa alikuwa mtu wao muhimu sana, huwa akzi yake ilikuwa ndio hiyo….kuyakatisha
maisha ya watu, na huwa akitumwa hafanyi makosa.
Jamaa hakujua kuwa wenzake walikuwa na malengo mengine,
walijua kazi yake imekwisha kwahiyo akirudi kuchukua pesa yake iliyobakia na
yeye utakuwa mwisho wake,…..kubakia kwake hai kungeliwaweka hawa jamaa kwenye
wasiwasi na yeye ni lazima amalizwe.
‘Usijali ndugu, kazi zetu hizi zina malengo, na sote
twatarajia hivyo, ..kuwa tukimaliza hii kazi, itakuwa ni hitimsiho la kutulia, ….ama
kwa raha , au ….moja kwa moja, …yote sawa,….wewe kakamilishe hiyo kazi, na
mshiko wako utaukuta hapa ukikusubiri…’akaambiwa na yeye akaguna na kuondoka.
Alipoondoka yule jamaa, akageuka na kuingia chumbani kwake,
huku akiwaza hatima yake, akijuliza je na yeye kazi hiyo ikimalizika atafanyaje,
na yeye akatubu dhambi zake na kutafuta sehemu ya kuishi, maana hatarajii kuwa
polisi watatulia ….ni lazima watamtafuta usiku na mchana,…akachukua sigara yake
na kuanza kuvuta huku akiangalia mushi wa sigara ukipotea hewani.
`Nii muhimu kwanza
huyu jamaa arejee…huyu huyu jamaa kabla sijammaliza, ninaweza kwanza kumtumia
kummaliza huyu mwanamke,….’aliposema huyu mwanamke, akawa anaangalia chumba
kinachoangaliana naye, japokuwa ilikuwa giza kali, lakini aliweza kuona sehemu ile
ya mlango kwa hisia.
‘Lakini siwezi kumuua huyo mwanamke mpaka niipate ile hundi,….’akasema
akikumbuka kuwa ile hundi ya kuchukulia pesa ipo mikononi mwa huyo mwanamke.
‘Nitakwenda kumpa taarifa kuwa kazi ya kummaliza mtu wetu
muhimu imekamilika, iliyobakia ni kupanga jinsi ya kwenda benki kuchukua hizo
pesa…hizo pesa hazina maneno, maana mmojawapo wa wathibitishaji wa kuchukua
pesa za mzee ni mimi….hiyo haina shida, ilimradi tumeshapata sahihi yake….’akakuna
kichwa.
‘Kwanza ni jinsi gani ya kugawana, maana huyu mwanamke,
haaminiki….’akakuna kichwa huku akiangalia lile giza lililotanda mbele,
lilikuwa giza nzito…na kila akiliagalia alihisi maisha ya kaburini, ambayo
anahisi kuwa kuwa giza lake litakuwa kama hilo.
‘Aaah, kwanini naingiwa na wasiwasi wa kufa….’akachukua
sigara yake na kuitia mdomoni. Huku akivuta moshi kwa kasi kabla haujaupuliza
nje, akasema kwa sauti ndogo;
‘Ni lazima niwe makini na huyu mwanamke…ok, lakini kwanza lazima tukubaliane, ….tugawane
kila mmoja ashike mshiko wake….’akatupa kile kipande cha sigara na kuinuka pale
alipokuwa amekaa na kuanza kutembea kule kulipokuwa na mlango, huku akiwa
kashikilia bastola yake, hakumuamini yule mwanamke.
‘Na kama nitamkutaka kalala, nimammaliza hapo hapo…’ akasema
huku akifungua mlango taratibu wa kile chumba ambacho ndicho alipo huyo
mshirika mwenza, ambaye kwa sasa alimuona kama adui yake.
Mlango ulipofunguka, haraka akachepuka, na kuurudishia
mlango kwa taratibu, hakuamini kuwa angeliweza kuingia kirahisi hivyo,…kwa
makubaliano yao, huyo mwanamke hakustahili kuufunga mlango kwa ufunguo, ..na
kweli ilifanyika hivyo…lakini kama alivyomfahamu huyo mwanamke, asingeliweza
kuingia bila kupata pingamizi,….
‘Oh, simba wa vita kazidiwa….na inaashiria kuwa mwisho wake
umeshafika, sasa kazi ni moja, ni kummaliza kabla hajanishitukia…. …’akawa
anaongea akilini. Akasogea taratibu, akichelea kugusa kitu ambacho kitatoa
sauti, akakumbuka pale walipokuwa wameweka begi lenye nyaraka na ushahidi mbali
mbali, na humo waliweka kitabu cha hundi.
‘Kwana nichukue ile hundi na stakabadhi ya malipo…’ akasema
akiiufuata ule mkoba, baada ya kuthibitisha kuwa mshirika wake kalala….na
akakumbuka walivyokubaliana mchana, kuwa yeye kwa vile anaruhusiwa kuchukua
pesa za mzee, na ni mmoja wa watu waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuthibitisha
malipo kama mwanasheria wa mzee. Hakuwa na mashaka kuwa watakwama kuzichukua
hizo pesa.
‘Mimi sina shida, wewe kaa na hilo begi…., kwani najua
mwisho wa siku mimi kama mwanasheria ndiye nastahili kwenda kuzichukua hizo
pesa…’najua mzee yupo mahututi, hajaweza kuwaambia benki lolote, au polisi
kwenda kuzuia malipo yoyote. Hilo nina uhakika nalo, kwani niliwasiliana na
muhasibu wao akasema hakuna chochote,….mzee hali yake ni mbaya, hajitambui.
‘Kwahiyo kinachohitajika ni uharaka wetu….’akasema mshirika
wake.
‘Ndio hivyo mpenzi, ukiwa na mimi ujua upon a kichwa….kila
jambo linakwenda kwa mahesabu , situmii nguvu, natumia akili…..kwahiyo kaa na
hilo begi, ili kukuthibitishia kuwa mimi ninakuamini….’akasema
‘Sawa….umeshinda kwa sasa, lakini safari nyingine, …sitaki
kusikia hilo neno mpenzi…..mpenzi wako ni mkeo,…..toka humu ndani nenda kwako’akasema
huyo mshirika.
‘Imekuwa hayo…..’akasema huyo mwanaume.
‘Ndio hivyo, na nahitajia kulala….sitaki usumbufu, nenda
kwenye chumba chako, …ole wako uje kunsisumbua, nitahakikisha risasi zote
zilizopo kwenye hii bastola zinaishai kichwani mwako….’akasema huyo mwanadada,
akikunja uso kuonyesha kutokufurahishwa na hiyo hali, na wakati huo huyo
mwanaume akitabasamu, huku akiogopa ile sura aliyoiona kwa huyo mwanadada,
inayoashiria chuki, na ukatali wa kuua.
Akatoka na kwenda chumbani kwake, huku akisema kimoyomoyo,
nitarudi tena hapa, na nikirudi hapa, huo uso nitausawazisha, ama kwa chombo
cha moto, au kwa pesa…..
Wakati anawaza hayo alikuwa kachuchumaa pale chini akiwa
kashikila lile begi, alihisi kitu, sauti, akaangaza macho, hakuona kitu zaidi
ya giza nene…akataka kuinuka na kuhakikisha vyema, lakini kwa lile giza, hata
kama huyo mwanamke atakuwa kaamuka, asingeliweza kujua kuwa yupo humo ndani, na
kwa makubaliano yao , kwa ajili ya usalama, walitakiwa wasiwashe taaa.
Akalishika lile begi alizingusha sehemu ya kufungulia, huku
akipapasa , na akiwa anatizama mara kwa mara kule alipolala mhasimu, wake,
vidole vikitafuta sehemu ya kufungulia,, hakutaka kuondoka na begi lote,…akashika
zipu yake, na kuivuta, na sauti ya mkwaruzo wa ile zipu ikasikika, ….akatulia,
na kutega masikio, akaona kimiya,…
‘Bado kalala…’akasema na kuendelea na shughuli yake, lakini
kabla hajaivuta ile zipu tena, taa
zikawaka, na yeye kwa haraka akasimama akiwa na bastola yake mkononi, tayari
imelenga kwa adui yake. Na kwa kujihami akasema;
‘Kwanini unawasha taa,…’
akasema kwa sauti ya kukwaruza ikiashiria wasiwasi mwingi, huku kidole
kikicheza cheza kwenye kiwambo cha kufyatulia bastola, hakuwa na mzaha tena,
alijua akichelewa yeye , mwenzake atamuwahi, na muda kummaliza huyo mtu ni huo,
kukipambazuka, huenda akakosa kila kitu.
Akakiza kidole chake huku akijiandaa
kuruka kwani alijua kuwa mwenzake anaweza akawa nay eye kafyatua bastoa yake.
Mlipuko mkubwa ukasikia, na kilio cha maumivu....
WAZO LA LEO:Aliyezoea ubaya, akitendewa ubaya huhisi machungu mara mbili, kwani mkuki ni kwa nguruwe.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment