Tajiri, aliondoka kituo cha polisi ambapo walikuwa
wameshikiliwa, baada ya taratibu za dhamana kukubaliwa, kwa ubinadamu alitaka
kumdhamini Malikia wa Marerani, lakini masharti yake yalikuwa magumu zaidi,
kwahiyo akaona ni bora arudi nyumbani.
‘Huyu mtu ni hatari, hatuwezi kumkubalia dhamana, hadi hapo
kesi yake itakapofikishwa mahakamani, yeye na mwenzake ni viongozi wa kundi
haramu, ….hawaaminiki, ’mkuu wa polisi wa eneo hilo akamwambia.
‘Lakini dhamana ni haki ya raia….yeye ni mtuhumiwa
tu,..’akajitetea Tajiri.
‘Wewe humjui huyu mtu vyema,…tafadhali achana naye,….tumewachunguza
kwa miaka mingi, na tuna ushahidi wa kutosheleza, …lakini hali ilivyo, ….tuna
wasiwasi mkubwa kuwa ana watu wake wanamlinda, na akipewa mwanya, ….hata huo
ushahidi unaweza ukaharibiwa…’akaambiwa na huyo musika wa hiyo kesi.
‘Kwahiyo unanishauri nini….?’ Akauliza Tajiri.
‘Ushauri wangu mkubwa na wewe kuangalia kesi yako, kwani
hata wewe unahusika kwa namna moja hadi nyingine, japokuwa tuliamua kukutumia
kama chambo,…tafuteni wakili, kwani wakili wenu huyo ni mmoja wa watuhumiwa, na
ni kiongozi wa kundi, japokuwa hakutaka kujionyesha wazi wazi….huyo tutapambana
naye’akasema huyo mkuu, akionekana kuwa na wasiwasi.
‘Basi ngoja nitaangalia nini cha kufanya…..maana najua yote
sasa yapo mikononi mwangu, kuondoka kwa mjomba ni pigo kubwa kwangu….’akasema
ilionekana dhahiri kuwa mkuu wa kituo hicho hataweza kutoa dhamana kwa Malikia
na mwenzake, wakili wa mzee wake, ndipo akaona ni vyema kurudi nyumbani kwanza
ili ajue taratibu za huko zinaendeleaje.
‘Kila –laheri….’akasema huyo mkuu, huku akiangalia
makabrasha yake, na alipohakikisha kuwa kaondoka, akachukua simu yake na
kuongea na watu wake.
Tajiri akiwa njiani alikuwa na mawazo mengi, kwanza alikuwa
akimuwazia mjomba wake, akilini mwake, alijua keshampoteza, mjomba wake hayupo
duniani, na kwahiyo yeye ndio kaachiwa majukumu yote ya kuendeleza miradi na
kuhakikisha haki za familia zinalindwa.
‘Mbona itakuwa kazi kubwa sana, ……’akajisema akilini, na
akakumbuka kuwa ni muhimu akawasiliana na watoto wa huyo mzee, ili kama
ikiwezekana warudi nyumbani, na kuhudhuria mazishi ya baba yao,..
Lakini mbona nilisikia Maua akisema `hajafa…..alikuwa na
maana gani, haiwezekani, kwa jinsi ilivyokuwa, mjomba hayupo tena duniani…ngoja
niwapigie simu watoto wake….’akasema huku akichukua simu yake na kutafuta jina
la mmoja wa watoto wa mzee, akajaribu kupiga zile namba, lakini hali ya
mitandao ikagoma, alijaribu majina yote hakuweza kufanikiwa kumpata hata
mmoja,…
‘Nitawapigia nikifika nyumbani….’akasema na baadaye akafika
nyumbani.
Aliingia ndani, na moja kwa moja akaingia kile chumba
maalumu cha mjomba wake, na ile hali ya kumbukumbu, ya kuwa mjomba wake,
alikuwa akiishi humo ikamfanya asite kufungua mlango, akarudi nyuma na
kusimama. Akawa anamuawaza mjomba wake,….lakini kuna hali ilikuwa haimpi
uchungu sana…akaguna,….
Akauosogela mlango, na kushika kitasa cha mlango, ili
kuufungua mlango,wakati huo alishajipa moyo, na kusema kimoyomoyo, kuwa sasa
yeye ndio anatakiwa kuwa kiongozi, kwahiyo anatakiwa kuwa jasiri, akawa kama
kafumba macho, akazungusha kitasa na huku akivuta tambo za kishujaa...na kitasa
kikazunguka na kujivuta kuuingia ndani kama vile anausukuma mlango…..
Akajikuta akipigana kikumbo na mama mmoja aliyekuwa akitoka,
na yule mama akasema `oh, samahani..’ na wakati huo mkoba wa yule mama aliokuwa
nao mkononi ukadondoka. Kwa haraka akainama kumookotea huyo mama mkoba wake, na
kumbe yule mama naye alikuwa kainama kuuokota, wakajikuta wameshikilia ule
mkoba, na ndipo akapata nafasi ya kuinua uso, …
‘Huyu mama anatokea wapi, au ndio wenyeji wameshaanza kuja
kwenye msiba, lakini kwanini waingie huku ndani…?’ akawa anajiuliza wakati
anainua kichwa kutaka kumwangalia vyema huyo mama,
Wakaangalia….na huyo mama akageuza uso haraka na kuanza
kuondoka, …Tajiri moyo wake ulishituka kidogo,..hakujua kwanini….akajaribu
kukumbuka,..akasimama pale mlangoni na huku akimwangalia huyo mama akiondoka
kwa haraka, na yule mama akageuka ….wakaangaliana….
*********
Mama Maua, akili yake haikuwa safi, ….alijaribu kuyawaza
yote yaliyotokea wakati akiwa ndani ya boda boda, akielekea huko alipokuwa mume
wake, hakupenda kuchelewa zaidi, kwani biashara ndio kazi yao, ndio kazi yao na
mume wake, na walihitajika kuchukua mzigo ambao wataondoka nao kesho yake, hadi
huko kwao Singida…
Kila alipomuwazia binti yake, alijiona kama anazidi
kumtelekeza binti yake, lakini kwa hali ilivyo, asingeliweza kufanya lolote,
kwani binti yake alishakataa kuondoka naye, …akakumbuka jinsi alivyojaribu
kumashawishi, bila mafanikio…na hapo akafumba macho, huku akilini akikumbuka
jinsi alivyokuwa akiongea na binti yake;
‘Maua hebu nieleze kiukweli, ina maana ulifikia hatua hiyo,
bila aibu ukalala na huyo mzee..….hadi ukapewa uja uzito na huyo mzee, huoni
aibu mwanangu, kulala na mzee kama huyo, sawa na babu yako….unachotaka kwake ni
nini..ndio huo utajiri….’akawa analalamika mama
‘Mama nakuomba utulizane na haya mambo….naomba usiyaingilie
yatakuja kukuumiza kichwa chako bure,….’akasema Maua huku akikwepa kumuangalia
mama yake usoni.
‘Mimi ni mama yako,….mimi ndiye niliyakulea, na mabaya
yakitokea nahiajika kuwajibia,..mwanangu, sikumbuki kukulea katika tabia ya
namna hiyo…unakumbuka nilivyokulea, na nilikuasa wakati unaondoka kuwa ,
usipende kisicho jasho lako, usiwe na tamaa, epukana na vishwawishi hasa vya
wanaume, kama ana mali yake, ni mali yake, chuma na tafuta chako kilicho halali…mwanangu,nimekosea
wapi mwanangu….,hadi ufanya huo uchafu,…’akalalamika mama yake.
‘Mama haya yaliyotokea sio kwasababu ya ulezi wako, mama
umenilea vyema kabisa…wala usijilaumu kabisa,…hata hivyo mimi sio mtoto mdogo
tena….najua nini ninachokifanya…’akasema Maua akijiskia vibaya, hakupenda
kabisa mambo yaliyotokea juu yake yamuhusishe mama yake, japokuwa safari yako
walipotoka Dar, ilikuwa kwenda kwake.
Kwenda kwa mama yake, ilikuwa kwa lengo jema, kuwa amepata
mume, na huyo mwanaume ajitambulishe kwa wazazi wake, kama utaratibu ulivyo, na
hakujua kuwa kutakuwa na vikwazo vingine,..
‘Mwanangu hata kama unajiona umekuwa mkubwa…bado hujawa
mkubwa, usijidanganye,….kama ungelikuwa na akili za utu uzima, usingelifanya
hayo uliyoyafanya…..hayo yatakufanya uishi maisha yasiyo na amani…jamii
itakutizama kwa jicho baya, kila mtu atakuwa na lake la kukuongelea…’akasema
mama yake.
‘Mama haya yaliyotokea mimi sikupenda, kiujumla yote yaliyotokea, hayakutokea kwa
matakwa yangu….kama kuna mtu wa kumlaumu, …basi umlaumu ndugu yako,…yeye ndiye
aliyeniingiza kwenye masahibu yote hata…na mama naomba usijiweke katika
msononeko,..haya nitayamaliza mwenyewe….usiwe na shaka….vyovyote iwavyo, ni
lazima haki ipatikane, ……’akasema Maua.
Mama aliposikia hivyo, kwanza aliinama, akilini akawa
anajijutia, akijua kabisa yeye ndiye aliyemtoa mtoto wake kwa ndugu yake , na
ilihali anajua tabia mbaya za huyo ndugu yake, …japokuwa waliishi pamoja
walipokuwa wadogo na walielewana, lakini ndugu yake huyo alikuwa na tabia ya
ubinafasi hasa kwenye pesa.
‘Namfahamu sana ndugu yangu huyu, naijua tabia yake ya
utotoni, lakini sikujua kuwa ataendelea nayo….ndio maana hakuweza kuishi na
mwanaume wake wa kwanza…aliachika, na kila aliyejaribu kuishi naye, hakuweza
kumvumilia…..sikujua kuwa namtelekeza mwanangu…..’akawa anaongea huku machozi
yakimlenga lenga, akageuka akitaka kutoka nje, akasema;
‘Kwanza yupo wapi huyo mama yako mdogo, nasikia mliongozana
naye kuja hapa…., nataka nionane naye….oh, simu, nahisi ni mume wangu
ananiita..’akakatisha maneno yake , pale simu yake ilipolia. Na kweli alikuwa
mume wake, akasikiliza huku bado akiangalia huku na kule kama anatafuta
kitu,…alimsikia mume wake akimsisitizia kuwa anahitajika haraka, kwenye maswala yao ya bisahara.
‘Ninakuja mume wangu….’akasema na kukata simu, akamwangalia
Maua.
‘Mwanangu, mimi nimefikia uamuzi kuwa tunaondoka pamoja,
sitakuwa na amani nikikuacha tena hapa au nikikuacha uendelee kuishi na mama
yako mdogo, ….tuondoke zetu, hatutashindwa kuishi pamoja, na hata kama una uja
uzito, tutajitahidi tutaitunza hiyo mimba utajifungua, na mtoto tutamlea
wenyewe, ….nimekulea wewe …sitashindwa kumlea mjukuu wangu, au …?’ akasema mama,
hakutaka kusikia mengine zaidi, alikuwa yupo radhi waondoke naye kuliko
kumuacha hapo akaolewa na huyo mzee.
‘Mama wewe ondoka,….mimi sitoki humu hadi kieleweke,….wao
ndio walioniharibia maisha yangu, na kwa hilo, itabidi nihakikishe haki zangu
zote zinapatikana, sitajali umri….wala …sijui kitu gani…’akasema Maua.
Mama Maua akatulia, akamwangalia mwanae, na baadaye akasema;
‘Haya mwanangu, ….kama umeamua hivyo, ….siwezi
kukulazimisha, ila naomba, tuwasiliane ili nijue imafikia wapi…’akasema mama na
kumgeukiwa yule mzee, safari hii, alimwangalia kwa jicho baya, hakutaka hata
kusema naye,lakini yule mzee, akasema kwa sauti ya taratibu;
‘Nakuomba usiwe na wasiwasi na binti yako,…yupo mikono
salama,… mimi nitahakikisha haki zote za huyu binti yako zinapatikana, mimi
sikujua hilo la ujazito, nahitajia kuongea naye zaidi, …hata hivyo, kama ana
uja uzito, nipo tayari kumuhudumia, na hata mtoto nitamlea kama
mwanagu…’akasema huyo mzee.
‘Utamlea kama mwanao…au ni mwanao..hiyo `kama’ ina maana
gani…hata kama u mzee, lakini kama umeshamuharibia maisha yake, kwa kumbebesha
huo ujauzito, ujue huyo ni mwanao….sasa hiyo `kama’ inatoka wapi?’ akauliza
mama Maua.
‘Inahitaji niongee naye, ….’kabla hajamaliza simu ya huyo
mama ikaita tena, na yule mama akaipokea na kusema `nakuja….’ akakata simu na
kuanza kuondoka,…
‘Mama usiwe na wasiwasi, haya nitapambana nayo, ….naomba
usiyaingilie…’akasema Maua.
‘Mwanangu, ..uwe makini , hasa kwa huyo ndugu yangu-mama
yako mdogo, anaweza akakutumbukiza shimoni,namfahamu sana yeye anathamini sana
pesa, na yupo tayari kufanya lolote kwa ajili ya pesa, hatajali kuwa wewe ni
mtoto…mimi nakuomba, ukiona vipi rudi nyumbani,…sisi biashara inachanganya,
tutasaidiana…’akasema mama yake.
‘Huko sikanyagi kabisa, hadi hapo, nitakapohakikisha mambo
yangu yamekwenda shwari,….hadi hapo nitakapohakikisha nimejifungua, …..na haki
yangu imepatikana, na hili ndilo lililonileta huku, itakuwa nimefanya nini
kufunga safari yote hadi huku halafu niondoke bila kujua majaliwa na masahibu
haya…hata kama wana kesi,….lakini najua huyu mzee, ni mzazi wake….’akasema
Maua.
‘Haya kila-laheri mwanangu,….maana naoana unanichanganya, na
wala sijui ni nini kinachoendelea kati yako na mama yako mdogo, na
inavyoonekana hutaki kunihusisha kwenye mambo yako, …..na mama yako mdogo,
haya…mimi naondoka, ….’akasema mama Maua na kufungua mlango.
Maua alipomuona mama yake anaondoka, akashika shavu, mkono
ulikuwa kidevuni, akawa kazama kwenye mawazo , …na hata hivyo moyoni aliona ni
bora iwe hivyo, kwani kwa hali ilivyo, mama yake atakuwa kaondoka na fikira
nyingine tofauti, na jinsi mambo yalivyo….yeye aliona ni bora iwe hivyo,…hadi
hapo muda muafaka utakapofika….akagueza macho kumwangalia yule mzee, na yule
mzee, alikuwa kaangalia nje,…kwa kupitia dirishani, alionekana kuwa na mawazo
yake.
Ilikuwa kipindi hicho mama Maua anaongea akimuaga mwanae
huku anatembea upande upande, huku akiwa anajaribu kugeuza kichwa kumwangalia
binti yake, huku anaangalia huko anakokwenda , na alipokaribia kitasa cha
mlango akatulia, akijua akitoka hapo, keshamuacha mwanae, na hajui ni nini
majaliwa yake, …akahisi kitasa kikizunguka, akageuka…..na mlango ukafunguka, hakutaka
kuangalia tena kwa binti yake, akatoka kwa haraka na hapo akajikuta akipigana
kikumbo na jamaa mmoja aliyekuwa naye anataka kuingia.
‘Oh samahani..’akasema mama Maua, huku akiokota mkoba wake
uliokuwa umedondoka chini, baada ya kupigana kikumbo na huyo jamaa. Na kwa muda
huo akili yake ilikuwa ikiwaza mengi, na aliona ni vyema kumuwahi mume wake
huenda wakapeana mawazo , huenda wakashauriania, wakaja naye ili kumshawishi
binti yao waondoke naye.
‘Huyu anaweza akawa mmoja wa watoto wa huyu mzee….’akasema
huku akiinama kuokota mkoba wake, na kumbe huyo jamaa na yeye alikuwa kainama
kuuokota huo mkoba, na hapo akajaribu kuinua uso kumwangalia, wote wakajikuta
wameshikilia ule mkoba, na wakajikuta wanaangaliana.
Mama Maua akili yake haikuwa hapo, alimwangalia mara moja,
na kuuchukua mkoba wake, na kuanza kuaondoka kuondoka, ….alipofika mbele
akageuka kumwangalia yule jamaa tena, na kumbe yule jamaa na yeye alikuwa
kasimama pale mlangoni, akimwangalia, wakajikuta wanaangaliana…
********
NB: Kidogo kidogo tutafika, japo kwa kuchechemea.
WAZO LA LEO: Kunapotokea
tatizo, wengi hukimbilia kunyosheana vidole,…hata kama mmojawapo anajua kuwa
ndio yeye katenda hilo kosa, sio vyema,…na sio sahihi, cha muhimu ni kutafuta
njia ya kulitatua hilo tatizo kwa pamoja,….na huenda ikaleta heri na mshikamano
kutokana na hilo tatizo.
Ni mimi:
emu-three
6 comments :
Hapa pana noga kweli ...tupo pamoja ndugu wangu..Kazi nzuri kwelikweli...Wazo la leo bonge la ujembe nimependa mno.
Hello There. I discovered your blog the usage of msn. This is an extremely well written article.
I will be sure to bookmark it and return to learn more of your useful information.
Thank you for the post. I will definitely comeback.
Here is my website :: mouse click the up coming website page
My brother ѕuggesteԁ I might like this wеb ѕіte.
He waѕ entirеly right. Тhis post аctually mаdе mу ԁay.
You cаnn't imagine just how much time I had spent for this info! Thanks!
My webpage: http://www.glowingcasino.com
Also see my web site - http://www.glowingcasino.com
Pleasе let mе knoω if уou're looking for a writer for your blog. You have some really great posts and I feel I would be a good asset. If you ever want to take some of the load off, I'd absolutely
loѵe to ωrіte some cοntent foг уour
blog іn eхchange fοr а link back to mine.
Please blast me an е-mail if interesteԁ.
Regards!
Visit my homeρage casinoer
Hongera sana unaenda vinzuri napenda sana.
Nashukurini nyote kama tupo pamoja,...na nitafurahia kama tutakuwa pamoja, hadi mwisho wa kisa hiki,....kuna mengi nimefunika, lakini kisa kinafikia ukingoni,...TUPO PAMOJA
Post a Comment