‘Baba hali yake ni mbaya sana, ndio maana nikaondoka kwa
haraka…’akasema yule binti, alipopokea simu toka kwa mama yake.
‘Sasa wewe ni dakitari,…aliyehitajika kufika haraka ni
dakitari, wewe unaondoka unaniacha huku….’akalalamika mama.
‘Lakini nimekuachia gari, …mimi nimechukua taksi, ili isije
ikawa vigumu kwako, ….kwakelii hali ya baba ni mbaya sana….’akasema huyo binti.
‘Hali yake ndivyo inavyokuwa hivyo, kila akipata mshituko,
sasa sijui kakumbana na kitu gani tena..’akasema huyo mama.
‘Tutaongea ukifika, ..kwani sasa hivi hana kauli….’akasema
huyo binti.
‘Msiwe na wasiwasi, …huyo mzee kameza hirizi, hafi haraka,
…’akasema mama na kukata simu.
‘Huyu mama vipi….’akalalamika huku akiangalia pale alipolala
baba yake, na baadaye akaingia ndugu yake, na akageuza kichwa kuangalia pale
alipolala baba yake, machoni kulishaanza kujaa machozi.
‘Usilie,…baba atapona tu,…ila mimi namshangaa sana
mama,…’akasema huyo binti mkubwa.
‘Sasa kwanini hukuja naye?’ akauliza yule binti.
‘Nilipopata simu yako, nilimwambia tuondoke, yeye akaniambia
nitangulie nje, nikafika huko kwenye gari, nikamsubiria wee, hakutokea,
nikamfuata, kule ndani walipokuwa wakiongea, nikamuonyesha ishara kuwa
tuondoke, lakini ilikuwa kama hanioni vile…..’akasema huyo binti.
‘Hakuoni wakati anafahamu kuwa baba kazidiwa!’akasema huyo
binti mdogo kwa mshangao.
‘Hakuwa anajua kuwa mzee kazidiwa, mimi uliponipigia simu,
sikutaka kumwambia moja kwa moja kuwa mzee, anaumwa, ila nilimwambia mzee
anatuita, …..’akasema huyo binti mkubwa.
‘Mimi mtu wa kwanza kumpigia simu alikuwa mama, nikamwambia
baba kadondoka,…..nikamsisitizia kuwa afike haraka, akaniambia sawa, muite
dakitari….’akasema huyo binti mdogo.
‘Mbona hakuniambia ,….ni kweli nilimuona akitoka nje
kusikiliza simu, na aliporejea hakuwa na dalili yoyote ya mshituko, wala
hakuniambi kuwa umempigia simu ….oh, mama jamani, mbona anakuwa hivyo, inakuwa
kama vile anataka baba afe…’akasema huyo binti.
‘Walishachokana hawa watu, mapenzi kwao yalishapotea,
….lakini ….’akasita pale walipomuona baba yako akijitingisha
‘Naona kazindukana….’akasema huyo binti mkubwa na kumsogelea
baba yake.
Baba yake akafungua macho na kuangalia, akawa anageuza mboni
za macho na kuangalia huku na kule, halafu akamtizama binti yake, alikuwa kama
anataka kuongea jambo, lakini sauti ilikuwa haitoki, yule binti akainama, ili
asikie nini baba yake anaongea
‘Malikia…..’akasema
‘Malikia,….?’ Akauliza binti yake na baba yake akajaribu
kutikisa kichwa kama vile kukubali, na yule binti akageuka kumwangalia ndugu
yake.
‘Baba Malikia hayupo, alishatoroka….’akasema huyo binti
mwingine
Baba akajaribu kuinua mkono, huku akionyeshea kwa kidole….
Kilikuwa kinaelekea kwenye kabati la viyoo, na yule binti akakifuatilia kile
kidole, na kweli aliona lile kabati likiwa wazi, sio kawaida yake, na haraka
akaliendea.
‘Mdogo wangu uliwahi kulifua hili kabati, au baba mwenyewe
alilifungua, ….?’ Akauliza.
‘Hapana, muda wote niliokuwepo hapa, halikuwahi
kufunguliwa,….’akasema na kumwangalia baba yaoo ambaye alishafumba macho tena,
kuonyesha kuwa karudia ile hali ya kupoteza fahamu.
*******
‘Hebu niambie ilikuwaje?’ akauliza mama wa wale mabinti.
‘Mama kwanini ulipigiwa simu kuwa baba mgonjwa, ukakaa
kimiya, hata bila kuniambia?’ akauliza binti mkubwa.
‘Ningekuambia, ungelikatisha mazungumzo, na yale yalikuwa
mazungumzo muhimu sana…..baba yako mara nyingi inamtokea hivi, sio mara ya
kwanza, na anayejua jinsi gani ya kumsaidia ni dakitari wake, hata
ningelikuambia wewe ungelifanyaje,..wewe ni dakitari wake….msifikirie kuwa mimi
simjali, namjali sana, ndio maana najaribu kuyaweka mambo sawa….’akasema mama.
‘Kuyaweka mambo sawa kwa vipi, kama humjali baba akiwa
anaumwa, ….mambo gani utayaweka sawa….wewe kama mke wake, ulitakiwa ukimbilie
haraka, ili ujue ni jinsi gani ya kumsaidia, hata akija dakitari, akukute upo
naye…hayo mambo mengine yapo tu, lakini baba akiondoka hatutampata
tena…’akasema huyo binti.
‘Hahaha…sasa hivi mnajifanya kumjali baba yenu, miaka
mingapi mpo huko Ulaya, hamtaki hata kufika kumuona baba yenu, leo hii
mnajifanya mnamjali, basi mjue kuwa mimi nilihangaika naye sana, mpaka ikafika
muda moyo, akili ikawa imekufa ganzi, ….kwani kuna wakati, kila mkibishana naye
inakuwa hivi …kila siku,…utafanyaje, …..mlitaka na mimi nife kwa kihoro…akiongea
mimi nitulie….hapana, ….’akasema huyo mama.
‘Mama huyu kama kweli unamjali kuwa ni mume wako, na
unahitajia kuwa naye, muda wa kumuonyesha upendo ni wakati kama huo….unafikiri
kwanini akamuona Maua ni mtu muhimu sana kwake….ni kwasababu alifika akiwa
hivyo, na Maua akamjali….kiasi kwamba baba …alihisi tofauti…..kuonyesha kuwa
alichotendewa na huyo binti hukuwahi kumfanyia…’akasema huyo binti.
‘Nyie watoto….chungeni ndimi zenu, hiyo kauli yenu siipendi
kabisa….hamjui ni kitu gani kilitokea nyuma, hamjui jinsi gani nilivyohangaika,
hamjui jinsi gani nilivyiwahangaikia hadi mkapata hiyo nafasi ay kwenda
Ulaya,,….kama isingelikuwa mimi msingelifika huko kamwe, baba yenu alikuwa
hapendi…sasa leo mnaanza kunigeuka..’akasema mama yao kwa uchungu.
‘Mama hakuna aliyekugeuka, na tulishakuambia tunakushukuru
sana kwa hilo, ndio maana baba aliposema anakuacha, tukaamua kujitenga naye,
ila baadaye tulifikiria sana, tukaona kuwa tendo hilo sio sahihi, baba alikuwa
sahihi kwa upande wake, ….’akasema huyo binti.
‘Yupo sahihi kwa vipi?’ akauliza mama.
‘Kutokana na matendo yako, …mfano mnzuri ni huu….hebu
angalia tangu ufike hapa, hujamsogelea baba, …angalia kuonyesha kuwa
unamjali….’akasema huyo binti na akanyamza pale alipomuona baba yake akiwa
anajitingisha tena.
‘Docta alisema akijitingisha safari hii…atazindukana moja
kwa moja….’akasema huyo binti na kumsogelea baba yake. Mama yao alikuwa kakaa
pale pale, alipokuwa amekaa na binti zake , hakuinuka, alikuwa kainama chini
huku kashikwa kichwa. Binti wale walimwangalia mama yako na kumpa ishara asogee
pale alipo baba yao…
Mama aliwaangalia, na baadaye kweli akainuka na kuja kukaa
karibu na pale alipolala yule mzee. Yule mzee, akamwangalia huyo mama akawa
kama anakunja uso, akagueza kichwa pembeni. Yule mama akageuka na kumwangalia
binti yake mkubwa akasema;
‘Unaona….’yule binti yake mkubwa akamuonyesha ishara kuwa
asiongee kitu.
Mzee, akageuza kichwa na kumwangalia binti yake mkubwa,
ilionyesha wazi kuwa alitaka kusema kitu, na yule binti yake mkubwa
akamsogelea, na yule mzee, akasema;
‘Maua yupo wapi?’ akauliza.
‘Baba Maua yupo kwao…..’akasema yule binti.
‘Muiteni aje hapa…..yeye ndiye dakitari wangu…’akasema na
mama aliposikia hivyo akainuka pale alipokuwa amekaa akasogea pembeni, na
alionekana akipiga simu.
‘Baba Maua hawezi kuja hapa, anajiandaa kwa safari, wanataak
kurudi Dar…
‘Eti nini,….’akasema yule mzee, akakunja uso, akatulia kwa
muda,….halafu akaanza kutikisika.Yule binti alipoona hivyo, akamwambia
mwenzake;
‘Muite dakitari haraka……’ yule
mwenzake akatoka nje, na kwa vile dakitari alikuwa hajaondoka, akaingia na
kuanza kumshughulikia huyo mzee, na baadaye akauliza;
‘Kuna kitu gani mumeongea naye
ambacho kimemfanya ashituke tena …..naombeni kama mnamjali mzee wenu, jaribu
kutokumuongelesha vitu ambavyo havipendi, na kama kuna kitu amakihitaji, na
kinawezekana hakitamdhuru, mfanyieni….msikilizenu, mnatakiwa muwe karibu
naye….sio kumkwaza tena….’akasema dakitari.
‘Kuna binti mmoja
anamuhitajia,…….sasa kutokana na msuguano na mama tunashindwa kumuita aje
hapa’akasema huyo binti.
‘Je huo msuguano ni bora kuliko
maisha ya baba yenu…? Kwani akiitwa atakuwa kaharibu kitu gani, maana tangu
awali nilivyokuwa nikimuhudumia na kila akipata nafuu, amekuwa akitaja jina la
`Maua’ je huyo Maua ni nani….ni mtoto wake mwingine?’ akauliza huyo dakitari.
‘Hapana , wala hana udugu na
sisi….tutamuita kama ni lazima,lakini muda kama huu ….usiku umeshaingia,
hatuwezi kumuita , tusubiri mpaka kesho…’akasema mama yao.
‘Sawa hii dawa niliyompa, itaweza
kumlaza hadi kesho, cha muhimu msimsumbue tena, kama hamuwezi kumsaidia kwa
hilo analolihitajia, ni bora mkawa mbali na yeye, na kama kuna mtu hamtaki
kumuona, ni bora asionekane, kwani kuna jina alilitaja mwanzoni, ilionyesha
kabisa ana chuki nalo…..’akasema huyo docta.
‘Jina gani hilo?’ wakamuuliza.
‘Malikia….’akasema huyo docta.
‘Lakini malikia hayupo, sasa
kwanini amtaje mara kwa mara…’akasema huyo binti.
‘Huenda alikuwa akitaka kuwaambia
jambo kuhusu huyo malikia,….vuteni subira, wala msimsumbue kutaka kujua zaidi,
…kwani kipindi hali ilipokuwa mbaya ni nani aliyekuwa naye?’ akauliza.
‘Ni mimi, …..wenzangu walikuwa
hawapo…..’akasema yule binti, na docta akasema;
‘Polisi watakuhoji ……’akasema huyo
docta akiondoka.
‘Hamna shida…..’akasema yule
binti.
**********
Polisi mpelelezi, akiwa kasimama mbele ya binti na mama yake,
alikuwa kashikilia kidaftari chake kidogo, na akawa anaandika jambo, akainua
kichwa na kumwangalia mama na binti yake.
‘Huyu mzee, inaonekana aliona kitu,…je ni nani aliyekuwepo
hapa wakati anapatwa na huo mshituko?’ akauliza.
‘Mimi nilikuwepo, ….nikatoka nje kidogo, baada ya kusikia
kuwa mama mmoja, wanayependa kumuita mama mdogo, amefika, nikawa naongea naye,
na kwa muda huo nilishawapigia simu polisi,….’akasema huyo binti.
‘Huyo mama ndiye yule tuliyemkamata,….?’ Akauliza.
‘Ndio huyo huyo…..’akasema
‘Sasa kwanini mzee, alisema aachiwe…?’ akauliza.
‘Mzee mwenyewe hakupenda huyo mama akamatwe,….mimi ndio
niliwapigia simu polisi waje kumkamata,…baadaye sijui mzee alijuaje……’akasema.
‘Na wakati anatoa hiyo amri kuwa huyo mama aachiwe ni muda gani…..?’ akauliza.
‘Ni muda mfupi tu,….alipochukuliwa huyo mama, mimi nilikuwa
nje, mara simu yangu ikaita, kuangalia ni simu ya baba, nikataka kukimbilia
ndani, lakini nikaona niipokee, huenda ni kitu anataka kuniagiza, ndio akasema
kwa hasira;
‘Ni nani kakuambia uwaite polisi wamkamate huyo mama,
hakikisha anatoka haraka,…waambia ni mimi nimatoa hiyo amri, aachiliwe haraka,….akasisitizia
kuwa hayo aliyoyafanya huyo mama tutayamaliza wenyewe, sikustahili kuwaita
polisi…..na mara simu ikakatika…..’akasema.
‘Ilikatika , kama kawaida, au unahisi ilikatika ghafla…..?’
akauliza.
‘Kwa muda ule nilijua kuwa Ilikatika kawaida, lakini nahisi
kama ilikatika ghafla…nakumbuka kabisa…na ndipo nikaingiwa na wasiwasi na wakati
huo nilikuwa nikiongea na mmoja wa walinzi….nikamwambia nakwenda ndani
kumwangalia mzee....’akasema huyo binti. Yule askari akawa anaandika kiti
kwenye kidaftari chake.
‘Huyo mlinzi uliyekuwa ukiongea naye, yupo hapa sasa hivi?’
akauliza.
‘Hapana, …..kwanini unaliza hivyo,….maana niliongea naye
ooh, kweli alikuwa kama ananipotezea muda, maana alikuwa akinihoji
saana….lakini ni kawaida yao….siwezi kumshuku lolote….’akasema.
‘Kama ni lazima nitakuita kwenye gwaride al utambulisho, ili
unionyeshe huyo askari..kwasasa sioni kama kuna umuhimu,…kuna jambo muhimu la
kufuatilia…’akasema na kuandika kitu kwenye kidaftari chake, halafu
akamwangalia yule binti na kusema;
‘Kwahiyo hakuna aliyeingia kwa huyo mzee, kwa muda wote , ulipokuwa
ukiongea na huyo mama mdogo ….kwa vile mama yako na ndugu yako hawakuwepo, hata
wafanyakazi walikuwa nje,….si ndio?’ akauliza.
‘Walipofika hawo polisi na kumchukua huyo mama, mimi
nilitoka nje kabisa, kuhakikisha kuwa huyo mama anafikishwa kwenye vyombo vya
usalama, ila nakumbuka kuna baadhi ya polisi walibakia nyuma, sio ndani ya
nyumba, ila ndani uwani….nilijua ni wale wanaolinda kila siku, maana huwa
wanabadilishana mara kwa mara, kwahiyo huwezi kujua yupi ni yupi…..’akasema
huyo binti.
‘Lakini kwa kumbukumbu zako, huwezi kuwakumbuka walikuwaje?’
akauliza yule askari mpelelezi kwa mashaka.
‘Siwezi kuwakumbuka vyema, maana sikutilia maanani,… ila nakumbuka
alikuwepo mmoja mwanadada …..’akasema huyo binti.
‘Katika kundi nililolituma kulikuwa hakuna askari
mwanadada…..na hapo ndipo ninapotilia mashaka, huyo askari mwanadada katokea
wapi…, nilipowahoji askari wanaolinda hapa, waliniambia hivyo hivyo, kuwa
kulikuwa na askari mwanadada….huenda huyo alitoka kwenye kundi alilolituma
mwenzangu, maana walikuja askari makundi mawili’akasema na kuchukua simu yake
na akawa anaongea na mwenzake, halafu akasema;
‘Fuatilia kundi la askari waliokuja hapa kwa mzee, na
…..yah, ni kweli, inawezekana ndio yeye…..kuwa makini na nyendo zao…muulize,…..’akakata
simu na kuwageukia wanafamilia;
‘Na mzee wenu alipozindukana aliweza kuongea…?’ akauliza.
‘Aliongea kwa shida,…..nilipofika alitaka kuniambia jambo,
na kwa mbali nikasikia akitaja jina na kunionyeshea kwa kidole kwenye
kabati….’akasema huyo binti.
‘Alitaja jina gani?’ akauliza huyo askari.
‘Alitaja jina kama `Malikia….na baadaye akawa anamtaja Maua
na akawa akinionyeshea kitu kwenye kabati la viyoo, na nililikuta limefunguliwa
, kitu ambacho sio kawaida yake, kabati hilo muda wote limefungwa, na ufungua wake
anakaa nao mzee peke yake….’akasema huyo binti.
‘Oh…..sasa nimeelewa….hapo ninaamini kabisa kuwa huyo mtu
yupo hapa jiijini kesharudi, tofauti na tulivyokuwa tukifikiria mwanzoni kuwa
anatumiwa watu kufanya shughuli zake…na hapa alikuja kufuatilia nyaraka , na
huenda ni nyaraka muhimu sana,…tutawanasa tu…’akasema.
‘Nyaraka gani hizo?’ akauliza mama wa wale mabinti.
‘Tunahisi hivyo…..huenda ni za urithi, au za mambo ya
kibiashara, au za kibenki….hilo tutaligundua..’akasema huyo askari….’akasema
huyo askari mpelelezi.
‘Mnaweza kunionyesha hilo kabati…..?’ akasema na wale
mabinti walimpeleka hadi kwenye hilo kabati, na yule askari akalichunguza, ….
‘ Tutachukua alama za vidole, japokuwa jinsi ninavyowafahamu
hawa watu hawawezi kufanya makosa hayo, watakuwa wamevaa kitu kwenye mikono yao
kuzuia alama hizo…’akasema.
Yule askari mpelelezi akaondoka huku akitoa tahadhari kuwa
watu wawe makini na wasiondoke hapo bila kibali maalumu, na alipoondoka tu yule
askari, yule binti mwingine akaingia na kusema;
‘Wakina Maua wameshaondoka,….eti wameondoka na basi la
kwanza la alifajiri, wakati tiketi zao zilikuwa za basi la saa mbili…’akasema
huyo binti.
Yule binti akasema na kwa mama yao, aliposikia hivyo,
akainuka na kutoka nje, alikuwa akiongea na simu.
‘Hivi mama anaongea na nani, na kwanini kila akiongea na
huyo mtu anakuwa kama anatukwepa hataki tusikie hicho anachoongea?’ akauliza.
‘Nikuambie kitu, nilipofika kwa mama Maua, nimekuta naye
akijiandaa kuondoka, eti kapigiwa simu kutishiwa kuwa asipohamisha biashara
yake, ataingiliwa na majambazi….’akasema huyo binti.
‘Na aliposikia hivyo, hakuwafahamisha polisi?’ akauliza.
‘Anasema huyo aliyempigia simu, kamshauri kama msamaria
mwema, akamwambia akienda polisi haitasaida cha muhimu ni yeye kuondoka hadi
hapo hali inapokuwa shwari…..’akasema huyo binti
‘Kwahiyo anakwenda wapi?’ akauliza ndugu yake
‘Anakwenda kijiji kwao….anasema hata hivyo, alikuwa mbioni
kuondoka, kilichombakisha hapa ilikuwa ni binti yake Maua, na kwa vile Maua
kaondoka, haina haja ya yeye kuendelea kuwepo, ….’akasema
‘Au ni mama huyo anayefanya haya yote…?’ akawa anaongea kwa
sauti ya chini chini, hakutaka sauti isikike. Na ndugu yake akawa anaangali
huko nje, akiwa na wasiwasi na mama yake, akasema;
‘Sijui, …lakini dada, hili tatizo ni kubwa, inabidi tumbane mama, ….mpaka atuambie huyo anayeongea
naye ni nani, vinginevyo, inabidi tumuondoe huyu mama hapa mjini haraka
iwezekanavyo , kwani akiendelea kukaa hapa baba atakuwa na hali mbaya…pili mama
anaweza kujikuta anaingia matatani na polisi…’akasema huyo binti.
‘Nani aondoke,..siondoki hapa hadi hapo mzee wenu atapokata
roho…..’Mama akaingia, ni kama vile alikuwa akiwasikiliza nini wanachoongea.
‘Mama hivi hujui hatari inayokukabili….’akasema binti yake,
na kabla hawajaendelea kuongea , wakasikia sauti kutoka ndani, ikisema;
‘Malikia…huyo-o-o-ah….mkama….te.’wale mabinti wakakimbilia
ndani na kumuacha mama yao akiwa amesimama.
NB TUPO PAMOJA
WAZO LA LEO: Tuwapende na kuwasaidia wazazi wetu, kwani bila wao usingelikuwa mtu fulani.
Blog yenu inawatakia kila-laheri katika siku-kuu ya pasaka, tushehekee vyema kwa amani na upendo.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
hermes replicaKelly Hermes Handbags yoxi Hermes BeltsAuthentic Hermes Bags aewb
Post a Comment