‘Unasema ana uja uzito, sasa kama ana ujauzito mimi ndio
dakitari, ….’akasema huyo Tajiri, huku akikunja uso, na lile tabasamu alilokuwa
nalo usoni likawa limeyeyuka na uso ukabadilika na kujenga makunyazi, akageuka
kuwaangalia mabaunsa wake, akitaka kuwaambia jambo, lakini akaghairi.
Mama mdogo, na Maua walikuwa wametulia wakimwangalia huyu
jamaa, na waliona huenda muda wowote wakafukuzwa, na Mama mdogo, alijua kama
asipofanya jitihada, anaweza asipate kile alichokitaka, akataka kufunua mdomo
kuongea, lakini kabla hajasema kitu yule jamaa akasema;
‘Kwahiyo mnataka kusema nini?’ Yule jamaa akauliza na
kumwangalia mama mdogo, wakati huo alikuwa akikwepa kabisa kumwagalia Maua,
tofauti na alivyokuwa akifanya mwanzoni, ambapo kila mara akiwa anaongea, jicho
lake lilikuwa halibanduki kumwangalia Maua huku uso ukimeta meta na tabasamu
kilikuwa halibanduki mdomoni.
‘Sisi….tumekuja kukufahamisha, …..utasamehe kama lugha yetu
imekukwaza. Sisi, yaani mwanangu hapa, ana uja uzito, na tuna imani kabisa
ujauzito huo aliupata siku ile…..’akatulia mama mdogo, pale alipoona huyo jamaa
akamwangalia kwa macho ya kutisha.
‘Siku ile ipi…….?’ Akasema Tajiri, akiangalia saa yake.
‘Siku ile ya lile zoezi..’mama mdogo akakatisha pale alipogeuka
na kumuona Maua akimwangalia kwa mshangao. Kwani Maua aliposikia hivyo, mama
yake akisema siku ile ya `zoezi’ akili yake ilimtuma kuwa, mama yake mdogo
alikuwa akijua kila kitu kilichotendeka hapo, na ilikuwa imepengwa
‘Ina maana hilo lilikuwa zoezi na mama yake alikuwa akijua….’akawa
akiongea akilini
‘Haiwezakani, na ni nani atawaamini maneno yenu…mnaweza
mkafanya njama, kwa vile mnaona labda..’akatulia kidogo, na baadaye akaendelea
kuongea,
‘Na…..na hili wengi wanakosea, mimi sio tajiri kiasi hicho,
wapo matajiri bwana, mimi ninajihidi kadri ya uwezo wangu,na kidogo ninachopata
ninajitahidi kushirikiana na wenzangu, lakini wale wenye akili dhaifu wanaona
mimi ni tajiri, na kuniona eti ninagawa pesa….sio hivyo,….na wengi
wanachukuliwa mwanya huo kunibambikia mambo kama haya….’akatulia na akapitisha
macho kidogo kumtizama Maua.
‘Una maana gani kusema hivyo?’ Maua akauliza kwa sauti ya
haraak haraka, ilikuwa suti ya mkwaruzo kama vile anaumwa kikohozi…au koo
limekauka.
‘Sijaongea na wewe binti, …tukiongea watu wakubwa inabidi
utulie kwanza, huo ni utomvu wa adabu…binti mdogo kama wewe unakosa heshima’akasema
huku akimwangalia Maua kwa jicho kali.
‘Sasa hivi unaniona mimi ni mtoto…..eti binti mdogo, na kwa
vile mimi ni mtoto na umeona hivyo, basi sheria itachukua mkondo wake,
kwasababu ulinibaka, na sasa nina ujauzito wako…’akasema Maua.
‘Hahahaha…..umesahaueeh, unakumbuka ule mkanda, …ulijileta
mwenyewe, ukawa unajilazimisha mwenyewe kwangu…..lakini hilo sio hoja sana,
kama mnataka kwenda mahakamani njia ipo wazi, ..lini mnataka kupeleka hiyo kesi
yenu, ….?’ Akauliza kwa dharau.
‘Sio hivyo, mzee…’akasema mama mdogo, na akasahau kuwa huyo
jamaa huwa hataki kuitwa mzee, akasahihisha na kuita na kusema ; `sio hivyo
Tajiri….’akaweka mikono kifuani kama mtu anayeomba jambo kwa unyenyekevu.
‘Ndio hivyo….’ Akasema kwa hamaki, na huku kamkazia mama
mdogo macho, hadi mama mdogo akawa anaonyesha kuogopa, na kuwa kama
anajikunyata.
‘Na mimi namuunga mkono kabisa huyu binti, kwani ni vyema
haki ikafutwa, ..na sheria ikachukua mkondo wake, …nendeni mahakamani, na mimi
nitawasaidia kumlipia wakili,….ili huyo mwenye hiyo mimba awajibike, au sio?’
akawa kama anauliza.
‘Mimba hii ni ya kwako, usijidangaye kukwepa, …na kama
ukiikataa…..mimi nitaitoa,…’akasema Maua.
‘Safi sana…kumbe una akili….mimi sijali lolote utakaloamua, …’akasema
huku akitoa tabasamu la uwongo, na dharau.
‘Nikuambie ukweli, ……wengi wameshawahi kuja kwangu kwa wazo
kama hilo, nahisi wengine walifanya hivyo, na hata wengine hawakutaka hata
kuniuliza,….wamefanya hivyo..sasa na wewe uamuzi ni wa kwako…nasikitika kwa
hilo…natumai tumelewana, kama unahitaji gharama yoyote kwa hilo au lile la
kwanza sema,…..’akatoa pesa mfukoni na kuziweka mbele ya meza, pale alipokaa
Maua.
‘Mimi sijaja hapa kwa ajili ya pesa zako, ……wewe ulituma
ujumbe kuwa unanihitaji nije tuonane, na ndio hivi nimekuja…’akasema Maua bila
kujali, bila kumjali mama yake mdogo aliyekuwa akimfinya, ili asiongee hivyo.
‘Na, pili na hili la huu uja uzito, kwa vile umeniharibia maisha
yangu, ….wewe unahitajika kuwajibika , uhakikishe unailea hii mimba hadi hapo
nitakapojifungua,…na nikishajifungua, tutakwenda kupima,kama hii sio mimba
yako, nitakulipa gharama zako zote, na kama ni ya kwako,….’akatulia kidogo.
‘Nitakulipa mara mbili….’akamalizia huyo tajiri, na kwa
haraka, kama vile alikuwa kajiandaa kwa hilo, akatoa karatasi kwenye mkoba
wake, na kalamu, na kuandika maelezo haya;
‘Mimi
Tajiri….nimekubali kwa hiyari yangu, kuitunza mimba ya binti, ….Maua, hadi hapo
atakapijifungua, na akijifungua, ili kuondoa utata, vipimo vya kutambua uhalali
wa huyo mtoto vitafanyika, kama kweli huyo mtoto ni damu yangu, nitamlea,
nitamhudumia kama mwanangu, na kulipa faini yoyote, lakini kama sio damu yangu,
gharama zote nilizotumia atazirudisha……….’ Akaweka saini yake
‘Huu hapa ushahidi , ili kukuonyesha kuwa mimi sio mtu
mbaya,….nimefanya hivyo kwa wengine, kwanini nikufanyie wewe ubaya…hata hivyo,
mmmh, bado nitakuhitaji, …’akatabasamu,
‘Utanihitaji kwa lipi?’ akauliza Maua huku akiwa kakunja
uso, na huku mkono mmoja akiwa kashikilia ile karatasi.
‘Bado wewe ni mfanyakazi wangu, umesahahu mkataba wa ajira,…leo
hii nitahitaji kuitumia ile ofisi, na wewe unatakiwa uwepo kwa ajili ya huduma
mbali mbali….’akamgeukia mama mdogo.
‘Naomba umuelekeze mwanao, ….kama mnataka mambo yaende
kisheria basin a nyie timizeni wajibu wenu, la sivyo, naweza kubadilika….nitaitumia
sheria hiyo hiyo, mkaenda kuozea gerezani, …na ngoja kwanza,….’akafungua mkoba
wake na kutoa kanda za video mbili.
‘Maua nakuhitaji faragha, maana haya ni maswala ya mimi na
wewe, ili kukuonyesha kuwa nakujali, na najali ubinadamu wako…’akasema huku
akiingia chumbani kwake, na Maua akabakia ameduwa, na akili yake akakumbuka
jambo, akautizama mkoba wake, na kukumbuka kitu, bila kumwangalia mama yake
akamfuata huyo Tajiri wake na kuuchukua ule mkoba wake.
Alipofika ndani akamkuta yule Tajiri akiwa kakaa huku kashikilia
zile kanda za video , akiwa anazichezea chezea mkononi, akageuka kumuangaliana
Maua.
‘Mimi sipendi ugomvi, wala uhasama na watu, hasa warembo
kama wewe…sioni haja ya wewe kubeba kisu,..kisu cha nini, unataka uniue, kwa
kosa gani nililokufanyia, hayatoa hicho kisu, njoo nichome nacho…’akasema na
kumuacha Maua akiwa kaduwaa, hakujua ni kwa vipi huyo mtu kagundua kuwa aliweka
kisu kwenye mkoba wake.
‘Nilisahau nikaja nacho…’akasema Maua akionyesha uso wa
kushangaa.
‘Haina shida mrembo…mimi sina ubaya na wewe, na nasikitika
sana kwa hayo yaliyotokea, …huenda ndivyo, ..lakini wakati mwingine nafsi
inajuta, ….nakumbuka siku ile sote tulikuwa tumelewa, lakini mimi nalewa mara
nyingi, sihamaniki,…sipotezi ufahamu na kufanya yasiyotakikana, ….hata hivyo
pombe ni pombe, pombe haina rafiki…’akawa
bado kashikilia zile kanda za video.
‘Nilipoangalia tena hizi kanda za video, kuna kitu kimekuwa kikinisuta,
na kujiuliza yote haya ni ya nini,…ni kwa ajili ya kupata utajiri, mbona
utajiri ninao, …nataka nini tena,….hapana nikaoana kuwa haya yanatosha, kama ni
utajiri wa zaidi, hautanisaidia kitu….’akawa macho yake yameangalia kwenye
mkoba wa Maua.
‘Mimi sioni haja ya kukuumiza zaidi, naomba utoe hicho kisu
chako, unichome hapa,..’akaonyesha kidole chake kwenye moyo wake, na huku
akimsogelea Maua.
‘Ili moyo wako utulie..au sio…hata mimii nimechoka,
nimechoka kutenda makosa, madhambi, dhuluma,..na wengine wananiita eti mbakaji,…..sikumbuki
kubaka, kwasababu nina ushahidi, kwa hatua, kwa kila jambo langu, nakuwa na
kumbukumbu….huenda hata hili litakalofanyika hapa, litakuwa na kumbukumbu yake….’akaangalia
juu.
Maua naye akaangalia juu, akaona kitu kama kinamulika, kipo
kama tochi, hakuelewa kina maana gani, lakini akili yake ikamkumbusha picha za
video alizowahi kuona kuwa kwenye chumba kunaweza kuwekwa kitu kinachonasa
matukio, na ukifanya jambo unaonekana, akashituka..
‘Kwahiyo ina maana umefanya hivyo, ili kujihami,….?’ Akauliza
Maua.
‘Sio kujihami, hiyo ni kawaida yangu…popote ninapokwenda
ninakuwa na wataalamu wangu wa kuweka kumbukumb u zangu, sina shida, siogopi,
kwanini nifiche, …’akasema.
‘Sasa kwanini safari zako za kuja huku ni za kificho, …na
hukai hoteli moja kwa muda mrefu,…?’ akauliza Maua.
‘Hayo ni mambo ya kawaida, pamoja na hayo, bado nina maadui…hawo
maadui hawajali sheria…hao ndio nawakwepa, lakini sikwepi sheria…ndio maana
naweka ushahidi….’akazingalai zile kanda.
‘Siku ile niliuaharibu ule mkanda ulionionyesha, hiyo
mingine imetoka wapi?’ akauliza Maua huku kashikilia mikono mbele bila kuogopa.
‘Mikanda kama ile inawezekana kitengenezwa mingi….lakini
nimena kwako wewe haina haja, nitaharibu kumbukumbu zako, na hizi ni mikanda
nilizokuwa nimerokodi, na..kama tutakubaliana nitakukabidhi, uziharibu
mwenyewe, na ungelikuwa mtaalamu wa mitandao, ningekuonyesha wapi kulipokuwa na
hizo kumbukumbu ukaizifuta zote….’akasogelea komputa yake.
Mkono wa Maua ukawa unatikisika kwa hasira, kuna kiu
kilikuwa kikimuhimiza afanye lile alilokuwa kakusudia na hakikujali kuwa kuna
kumbukumbu, …hakikujali kuwa kufanya hivyo, kutamletea matatizo,
‘Unaogopa
nini, maisha yako yameshaharibiwa, na aliyeharibu ni huyo hapo, tumia nafasi
hiyo, ukimaliza, vunja kila kitu…’sauti ikamwambia.
‘Sogea hapa kwenye hii komputa uone wapi ninapohifadhi
kumbukumbu zangu,…..unaona hata haya yanoyotea hapa, yanahifadhiwa humu, unaona…..’akawa
anaonyesha. Na Maua macho yake, yakawa yanaangalia yale matukio ya liyotokea
siku ile…
Akaanza kutetemeka, ….akahisi mwili ukibadilika, akajaribu
kufunua mkoba wake, ili aichukue ile dawa, lakini hakuiona, akaanza kubadilika,…..sauti
isiyo yake ikatokea.
‘Sasa nimekuaj mwenyewe, nimekuja kulipiza kisasi….kwa
mtendo uliyomfanyia kiti wangu…’sauti nene ya kiume ikaongea. Tajiri, akageuka
huku na kule kutafuta wapi sauti inapotokea, hakuona mtu mwingine zaidi ya
Maua.
Alishangaa, alipomtizama Maua, sio yule Maua aliyemjua, sura
ya mvuto, na macho ya malegavu kama alivyopenda kuyaita, na kuyaona, hayakuwepo
tena…..kilichoonekana ni macho meupe, macho yaliyojaa hasira na uchu wa kuua,
meno yalikuwa yametokeza nje, na hata mate kumtoka mdomoni, ….
‘Kumbe wewe ni shetani…..’aaksema huyo Tajiri
‘Hahaha….wewe hujioni, wewe nishetani zaidi ya ibilisi,
mangapi mbaya uliyowahi kufanya ,ambayo hata sisi mashetani hatukuwahi
kuyafanya…umesahau, ..umefanya mabaya mangapi, umeua watu wangapi, umebaka watu
wangapi..ili tu uweze kupaat utajiri….eti ili upate utajiri mpaka upate vigoli,
upate mwili wa binadamu,…huo ni ushetani, huo ni zaidi ya ushetani….’sauti ile
ikasema.
Tajiri, akahisi hatari, akawa anasogea nyuma, na Maua akawa
anamsogelea, …hadi wakafika mwisho, nyuma ni ukuta, na meza, …..Maua kwa haraka
akatoa kile kisu kwenye mkoba wake….
‘Sasa leo ndio mwisho wa yote hayo, unahitajika uje huku
kuzimu, tukawe pamoja….’ile sauti ikasema …
‘Hapana…nisameheni, sitarudia tena, nitahakikisha namuoa na
kumtunza huyu ….wewe. huyo binti…’akawa anasema huku akili yake ikikumbuka
ahdithi za mashetani, kuwa mtu anaweza akatwekwa an mashetani, akaabdilika na
kuwa kama hivyo, na kwahiyo huenda Maua ana hayo mashetani, na asipoyabembeleza
anaweza kuuwawa…
‘Semeni mnataka nini……?’ akauliza akili ilipokumbuka mambo hayo ya mashetani.
‘Tunataka roho yako…..’Maua akainua kile kisu juu
**********
NB: N I kazi sana kuandika sehemu kama hii asubuhi asubuhi,
kwani ina mambo mengi, lakini sehemu hiyo inatosha kwa leo
WAZO LA LEO:
Uzuri wa sura, katu hautadumu , lakini uzuri wa tabia, matendo mema, hudumu
milele. Tujitahidi kuwa wema wa tabia, na kutenda matendo mema.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Hongera sana miram mimi sikosi hata siku moja kuangalia blog yako maana napenda sana hadithi pia unajitahdi kuandika hadith ndefu hakika inabamba big up!
Nashukuru sana Mumy Victoria, na nakukaribisha sana tuwe pamoja na wewe kama una kisa chochote kilete , hata kwa ufupi, mimi nitajua jinsi gani ya kukiendeleza....TUPO PAMOJA
Waoo nashukuru miram kuna kisa kimoja kinasikitisha sana kimemtokea frnd wangu ntajitahidi nikupe hata kwa ufupi naamini kitawasaidia sana wasichana.pia nakumbuka kuna kipindi nilisoma blog yako ukatuomba radhi kuwa comp ya ofcn uliyokuwa unatumia umeachishwa kazi hukuruhusiwa kunyonya hata hadith zetu najua ushapoa lkn nilisikitika sana nawish sasa una yako pole sana pia kumbuka ubinadamu kazi? ilike ure blog sana
Post a Comment