YALIYOPITA: `Ugeni huo
kutoka makaoni….mbona wamewahi hivi…,?’ akauliza mfalme mtarajiwa.
‘Hapana huo ni ugeni
wa mzee hasimu na kijana wake na wazee wenzake’ akasema huyo mlinzi
Hapo yule mfalme mtarajiwa akageuka kushoto
kwake , ambapo ndipo wageni wanaposubiria na
kule aliona kundi la watu, na miongoni mwake akiwemo Mzee hasimu na
kijana wake, walikuwa wote wamekunja uso kwa hasira.
Je ugeni huo ulikuwa
kwa heri au kwa shari, hebu tuendelee tuone ni nini kilitokea …..
****
Wapendwa lengo la sehemu hizi katika kisa hiki ni kuona jinsi gani
watawala wenye uchu wanavyopenda madaraka, hasa pale wanapoonja `utamu’ wa
madaraka hayo kwa vile kwao wao wapo hapo kama `ajira’. Na wanashindwa kuelewa
kuwa madaraka hayo ni kwa ajili ya wananchi,baada ya kupata kibali hicho kutoka
kwa hawo wananchi,….
****
Kikao maalumu cha dharura kwa ajili ya kuwasilikiza wageni
waliofika kilikamilika , wageni hawo sio wengine ni mzee Hasimu na kijana wake,
wakiongozana na wafuasi wao. Wenyeji, walipomaliza kuongea na kuwekana sawa,
wakatoka kwenye cha maongozi, ikabidi muhusika wa kukaribisha wageni atoke na
kuelekea kule walipo wageni, ili apate kuwakakaribisha kwenye ukumbi huo
maalumu.
Wageni hawo walikuwa wengi, walikuwepo viongozi waliokuwepo
madarakani kipindi kilichopita, na pamoja nao kulikuwepo maaskari. Na kwa
utaratibu wao ulivyo kikao kama hicho kilitakiwa kifanyike kwenye chumba
maalumuho maalumu hakina uwezo wa kuwaingiza hawo wageni wote na wajumbe wa
wenyeji.
Kutokana na hilo mkuu wa vikao, ikabidi awaombe wageni hawo kuwa wengine
wabakie nje. Waingie wawakilishi tu, ambao wanaweza kutoa hoja za wote, hasa
viongozi wakuu, na wasaidizi wake wachache. Taarifa hiyo haikuwapendeza
wahasimu, wao wakai kuwa wote wamekuja na hoja na wote wanatakiwa kushiriki
kuhakikisha kuwa hoja yao inapita.
‘Lakini mzee wetu muheshimiwa, wewe mwenyewe unaifahamu
sehemu hiyo ya kikao ilivyo, haitawezekana nyie wote muingie humo, na wengine
watashindwa kuingia, je kikao hicho ni chenu peke yenu….?’ Akauliza mkuu wa
wageni.
‘Hilo mtajua weneywe, cha muhimu ni kuwa lazima wote
niliokuja nao waingie kwenye hicho kikao..’akasema huyo mzee.
‘Mzee, hatutaweza kuwaingiza wajumbe wote, wajumbe wako
mlioongozana nao ni wengi kupita uwezo wa chumba chetu cha mikutano maalumu,
chagua wawikilishi wachache …’akaambiwa.
‘Kwanini nichague wajumbe wachache, kwanza niwaambieni, kuwa
tumekuja hapa kukutana na huyo mnayemuita mfalme wenu mtarajiwa na wawakilishi
wake wachache, hatuhitaji watu wenu wengi, kwanza wa nini,… na madai yetu ni
kwa huyo mtu wenu mliyemlazimishia kuwa ni mfalme mtarajiwa…nyie wengine hatuwahitaji…’akasema
mzee kwa hasira.
‘Sawa mzee tumekusikiliza hoja yako, kama nia yako ni
kuhakikisha watu wako wote uliokuja nao wanashiriki, basi, hicho kikao itabidi
kikafanyikie sehemu nyingine na sio sehemu hii maalumu ya vikao vya kukutana na
mfalme….na labda tukakifanyie kwenye uwanja wa mapambano’akaambiwa.
‘Haiwezekani, kikao kama hiki kinahitaji huo ukumbi si
vinginevyo….sisi tunahitaji kuongea na huyo mtu, na kama mnataka tukaongelee
uwanja wa mapambano, kwanza ajivue huo ufalme mliomvika isivyo halali, kwahiyo
tukue tunaongea na mtu ambaye sio mfalme mtarajiwa….’akasema mzee huyo
akiwaangalia watu wake ambao walimuunga mkono, kila mmoja akionyesha kuwa yupo
pamoja na mzee wao.
‘Mzee wewe ni mtu
tunayekuheshimu sana,…na tunashangaa kushinikiza jambo ambalo unaona kabisa
halitawezekana, hatutaweza kuingia wajumbe wote kwenye chumba hicho, sisi
tunakuambia kuwa, chagua wawakilishii wako wachache na wengine wasubiri nje’, ‘akaambiwa na yeye
akawasogelea watu wake na kuteta nao, na ghafla wakaanza kuingia kwenye huo
ukumbi, wote kama walivyokuja, na ukumbi ukawa umejaa, kama vile kikao hicho
kilikuwa ni cha kwao peke yao…
Mfalme mtarajiwa alipoambiwa hilo, hakujali, akamuita babu yake na wazee wachache
na wawikilishi wake wawili, wakaingia kwenye hicho kikao, na alipoingia wale
wageni wakaanza kuzomea kwa kuonyesha kuwa hawamtambui huyo mfalme , …
Mfalme mtarajiwa hakujali, akakaa kwenye kiti chake, na mzee
mmoja mzungumzaji mkuu akaanza kukifungua kikao, alianza kwa kutoa salamu,na
wageni wale wengine wakaitikia wengine wakawa wanaendelea kuzomea,…yule
mzungumzaji akaanza kuongea kwa kusema;
‘Wazee wanasema, hekima ni ukomo wa elimu, ukikosa hekima
hata kama una elimu kiasi gani, hujaelimika, ukikosa hekima hata kama utakuwa
kiongozi mwenye nguvu kiasi gani hujawa kiongozi bora, hekima ndiyo inayokuendesha
wewe kujua lipi ni jema na lipi baya na lipi lifanyike kwa wakati gani, na kwa
watu gani, na ni vipi uishi na wenzako..
Ndugu zanguni,poleni na safari na tunaomba samhani kwa
kuwasubirisha kidogo, na tunashukuru kuwa mumemkubali kiongozi wetu , ndio
maana mkashinikiza kikao hiki kifanyikie hapa, na wote mkawa na hamu ya kuongea
naye…’ akakatishwa na kuzomewa.
‘Ndugu zanguni, …ukweli unauma,….na ukweli upo, hata kama
utaupiga chenga, ….hali halisi inajionyesha na ipo zahiri, ..ila kama
nilivyotangulia kusema, nawaombeni sana tujitahidi kuwa na hekima, kwa
kuheshimi kikao muhimu kama hiki, na sehemu muhimu kama hii…..’akasema
mzungumzaji akinama kidogo kuonyesha heshima ya kuwaomba, na wale watu
wakatulia kumsikiliza.
‘Baada ya kuanza kusema hayo, ninaomba nikifungue kikao hiki
kwanza kwa kuwaomba wageni wetu ajenda zenu, maana mumesema ajenda hizo
mtazitoa ndani ya kikao, na hatuwezi kuendesha kikao bila mpangilio maalumu, je
mnayo ajenda gani muhimu?’ akauliza.
Akasimama mmmoja wao, aliyekuwa mpambe wa mzee hasimu
anayejulikana kwa kuongea, akasema;
‘Ili tusipoteze muda, mimi namkaribisha kiongozi wetu wa
siku nyingi, mtawala aliyeendesha jamii yetu kwa muda mrefu, na mnfahamu kwa
kazi yake nzuri, ndio maana leo mpo hapa, karibu mzee wtu mkuu, mzee Hasimu;
Mzee hasimu kwanza akasimama, na baadaye akakaa,
hakuinamisha kichwa kuonyesha heshima, akaanza kwa kusema;
‘Ajenda yetu namba moja ni kuwa huyo mnayemuita mfalme
mtarajiwa aondoke kwenye kiti alichokalia maana hakubaliki na hana sifa ya
kukikalia hicho kiti, vinginevyo, tutakuwa tunavunja hadhi ya hicho kiti, na
ajenda yetu ya pili ni kumtafuta mfalme mtarajiwa , ambaye ana hiyo hadhi,
…’wenzake wakashagilia.
‘Na ajenda yetu ya tatu, ni kufuata sheria kama
zilivyotuagiza kuwa kama kutakuwa na tatizo kama hili la kulazimisha uongozi,
huyo aliye lazimisha ni sawa na mvamizi, …….wa nchi na baya zaidi anaingia
sehemu takatifu na kukalia kiti kitukufu,…’ Mzee huyo akawa anaongea na wenzake
wakawa wanamshangilia.
Alipomaliza kuongea, Mzee mteula akasogea pale alipokaa
mfalme mtarajiwa baada ya kumuona kama anataka kuinuka kuondoka kwenye kile
kiti kama alivyosikia katika moja ya ajenda, kwa jinsi anavyomjua mjukuu wake,
angeliweza kufanya hivyo, ili kuleta amani,na huenda, akatii yote yaliyosemwa
na wahasimu, yeye akasogea pale na kumshika mjuu wake kwenye bega.
‘Wazee wenzangu na wajumbe wengine , mimi nisingelipenda
kuliingilia hili, ila nilikuwa nataka niwarejeshe nyuma, kipindi ambacho
alifika yule mtabiri, wazee wenzangu mnakumbuka vyema siku ile, alivyosema…’
Watu wakaguna na kusema;`mmmmmmh, kaanza huyo…’
‘Narejea maneno ya huyo mtabiri, ambaye wote tulimuheshimu
na kuheshimu maneno yake kuwa ni muhimu na yana nguvu, mnakumbuka alisema
nini…..’akatulia hapo kidogo na kuigiza sauti nzito, na huyo mtabiri;
‘Siku ikifika atatokea mtu, kutokea machweo ya jua,…na miali
ya jua itakuwa inamchoma yeye kwa nyuma, huku akiwa kapanda kipando maalumu,
huku akiwa kaongozana na kundi la watu, waliosalimu amri kwake…yeye atakuwa
hajui kuwa ndiye mfalme mtarajiwa, ….
Hapo akatulia hapo na kuongea sauti yake ya kawaida kwa
kusema;
`Mimi nitataja baadhi ya sifa ambazo alizitaja huyo mtabiri,
moja ya sifa hiyo ni kuwa ,mtu huyo atakuwa,…, atakuwa ni jasiri….atakuwa na
hekima, atakuwa mtu wa watu anayejali watu bila kubagua,….atakuwa ndiye mume wa
malikia…..’aliposema hivyo, wakazomea na mmoja akasema
‘Ni mbinu zenu hizo, mlimteka malikia ili aolewe na kijana
wenu, hizo ni minu zenu, hatkubali hilo….’wakasema.
‘Hebu tuanalieni kiukweli, …kama alivyosema mwenzangu katika
utanguzi wake kuwa ukikosa hekima huna elimu, hata uweje, unaweza ukatumia
elimu yako bila kujali madhara ya baadaye, na kwa manufaa yako binafsi, hiyo
haitakuwa ni elimu,…na halikadhalika ukiwa kiongozi ukakosa hekima hutaweza
kuwaongoza watu wako kwa busara, utaweka masilahi yako mbele…’watu wakacheka na
kukebehi.
‘Hili linajionyesha hadi hapa,….nyie ni viongozi wa jamii,
nyie ndio vichwa vya wale mnaowaongoza, mumeaminika kwa kila kitu, je hii
mnayoionyesha hapa ni nini….? Hamuoni kuwa mnakosa hekima , hata ya kikao
muhimu kama hiki…jamani tuangalienei mbele, tusijali ubinafsi wetu, hatutaki
uongozi kwa ajili ya sifa,…
‘Uongozi ni kwa ajili ya wananchi na wale unaowaongoza, kama
wewe ni kiongozi ukawa kwanza unajali maslahi yako, unataka kila kitu kikubwa
kiwe chako,….una kasoro…na ninaweza kusema hukustahili kuwa kiongozi, …kiongozi
bora ni yule kwanza anayewajali watu wake, na ikibidi kama ni njaa, kama ni
maslahi, kwanza uhakikishe watu wako wameshiba, kabla hujaweka tonge mdomono
kwako..’watu wakecheka kwa dharau.
‘Ni nani kati yenu aliwahi kufanya hivyo….kuhakikisha kuwa
wananchi wanapewa kipaumbele, kabla ya kujali maslahi yake….ni nani
aliyehakikisha kuwa wananchi wanasikilizwa hoja zao, matatizo yao…njaa yao,
kabla hajalitizama tumbo lake. Ni nanli aliyekuwa tayari hata kupoteza maisha
yake kwa ajili ya wananchi wake? ….’akawaangalia na hapo walikaa kimiya.
‘Sisi kama wazee ambao tumepitia wakati mgumu, tumeshuhudia
umwagaji damu wa hali ya juu, ndugu wa damu, tumeuana kama wanyama,…na baada ya
hapo ni chuki , visasi, ….ubinafsi, nah ii yote ni mdahara ya umwagaji damu,
unapoua usifikiri ndio mwisho wa yote, damu ya mtu itakuandama….
‘Sisi nduguzanguni, naombeni tujaribu kukumbuka tulipotoka,
tujaribu kuangalia mambo kwa upeo wa mbali, kwasabbu uongozi sio ajira, ukiweka
mbele kuwa kiongozi upo hapo kwa ajili ya tumbo lako, ukasahahu hekima nzima
kuwa wewe upo kwa ajili ya watu, hutakuwa umetenda vyema…
‘Sipendi niongee mengi, maana kuongea sana, hakusaidii, kinachohitajika
hapa ni hekima, …na ili tufanikiwe hili, nafikiri ni vyema tukaangalia sifa za
huyo kiongozi aliyetabiriwa, je haendani sawa na huyo kiongozi aliyejitokeza
siku hiyo, kama haziendani nay eye ni
nani mwingine, ambaye anazo hizo sifa na
ina maana kama ni hivyo, siku hiyo haikuwa na umuhimu kwetu…
‘Kama tulikubali kuwa siku hiyo ndiyo siku iliyotabiriwa, na
siku hiyo ndiyo huyo kiongozi atatokea, na akatokea, lakini sisi tunaona siyo
yeye, je ni lini atatokea, na huenda mndai alitokea ikafanyika hujuma, je ina
maana yule mtabiri alisema uongo, kwani kama mnavyokumbuka, alisema siku hiyo
hata ifanyike vipi, huyo kiongozi atajitokeza.
‘Na hata hivyo, waamuzi wakubwa ni wananchi, je wananchi
wanasemaje kuhusu huyo kiongozi, wanamkubali au hawamkubali, na kama yupo
mwingine ambaye kafanyiwa hujuma, je wananchi wanamkubali….hayo ndiyo ya
muhimu, hata kama tutakimbilia kumuondoa huyo ambaye hamumkubali kwa sababu
zenu, bado tunahitaji rizaa ya wananchi wote...
‘Hatumkubali, …’wakasema kwa sauti….
‘Nyie I sehemu ndogo sana ya wananchi, na ka ingeliwezekana
kuzifungua nafsi zenu, wote hapo mlipo mnamkubali , lakini kutokana na
shinikiozo na propaganda potofu, sasa hivi mnapinga, lakini mkumbuke kuwa hicho
mnachokifanya kitakuja kuwashitaki baadaye, kwasababu mnahini ahadi na utabiri
…..’ kabla hajamaliza mara akaingia askari, na kumng’oneza Mzee Hasimu sikioni.
Mzee hasimu akamshika mfalme mtarajiwa bega, na kuinama
kumng’oneza, wakaangaliana, na mzee akawageukia watu na kusema;
‘Kwa bahati nzuri, wenzetu wa makaoni wametumwa wajumbe,
ambao watasimamia hiki kikao kwa ajili ya kupata suluhu, ….kwahiyo tuwe
watulivu wakiingia na wao wataendesha shughuli yote ya kuhakikisha kuwa
tunafikia muafaka..narudia tena, sisi ni ndugu, na udugu wetu ni wa damu, hatuoni
kwanini turejee tena kwenye umwagaji damu, …..’akasema na wajumbe wale wakawa
wanaingia.
Wajumbe walipokaa, na mzungumzaji kuwakaribisha, …ndipo
kiongozi wa msfara huo akasema;
‘Nakumbuka mlisema aliwahi kuja mtabiri, ambaye amewaatbiria
wengi, na waliofuta hayo waliyotabiriwa wameneemeka ,na waliopinga wamekuwa
kwenye uhasama wa kudumu, na wanajutia kwanini walipinga….sasa niwaulize swali,
japokuwa nimewambiwa wengi ya waliopo humu ni wale wanaompimga kiongozi huyo mpya.
Lakini hiyo haijalishi kitu, kwani tukitoka hapa tutakwenda
kukutana na wanachi ambao nimesikia wameanza kujikusanya kwenye uwanjwa mkuu,
….sehemu yenu ya kihistoria ambapo mliuana kama sio ndugu, na hili hatutaki
litokee tena, na kwa minajili hiyo, ni bora kama hakutakuwa na muafaka , itatubidi
tuchukue uamuzi mgumu…..ili kutokukaribisha tena hiyo hali…
‘Kwanza kabisa, inabidi tule kiapo, kiapo hichoo ni cha
kuhakikisha kuwa makubaliano yote yanapitishwa, na yakipitishwa hapa
atakayeyapinga, mnajua ni nini kitampata, lakini hata hivyo, inabidi tule amini
ya kukubali au kupinga yale aliyowatabiria mtabiri wenu, kuwa je yalikuwa ni
kweli, na kama ni kweli mnayakubali, na kama mnayakubali, na matokea yake
yametokea, je kuna nini kimtendeka hadi tusiyakubali tena….
‘Pia huyo kiongozi zliyejitokeza anakubali kuwa kweli
hajafanya hujuma yoyote, na kama anakubali na kula hiyo amini, je ni nani
mwingine ambaye anahisi alihiniwa, na kumbe ndio yeye alitakiwa kutokea hapo, …akazuiwa
,…kama yupo na anakubali kuwa kweli ndio yeye, na yeye anatakuwa kula hiyo
amini, na wenyewe mnajua madhara ya hiyo amini ukiwa unaongea uwongo…
‘Na nyie mnaomuunga mkono mnatakiwa mle hiyo amini kuwa
mnakubalina na hilo, na ya kuwa mnamuunga mkono huyo kiongozi wenu mnayekubali
kuwa ndiye yeye na kafanyiwa uhaini,..tukimaliza hilo….tutakwenda kwa wananchi,
na wao watathibitisha kuwa kweli ni nani kiongozi wao….’akasema huyo
muwakilishi na kazi ya kugawa hayo maji ya yamini ikaanza kugawanywa…
‘Vuramai ikaanza,….baadhi ya wajumbe wakaanza kukataa
kuyapokea hayo maji…
‘Naomba kila mtu aliyekuwepo hapa ndani aaypokee haya maji,
kwani nyie ndio wajumbe mnaowakilisha wenzenu,..na kuyapokea na kuyanywa, sio
kwamba umeingia moja kwa moja kwenye kibano cha ahadi, wewe baada ya kunywa
utatakiwa kukubali au kukataa hayo utakayoulizwa;
‘Maswali utakayoulizwa ni kuwa je unamkubali huyo kiongozi
aliyejitokeza siku hiyo kuwa ndiye aliyetabiriwa, kama unamkubali utasema
unamkubali, kama humkubali utasema humkubali, na kama huna jibu, utakaa
kimiya…..maana kuna ambao hawana jibu kwa sasa, huenda wanaogopa…
‘Kama unamuogopa kiongozi wako, lakini huigopi imani
yako,….unaweza ukakaa kimiya, lakini ki imaniz etu mtu kama wewe hutaweza
kupata baraka katika amali zako,hili sihitaji kukufundisha maana nyote hapa sio
watoto wadogo, na nyote mnajua madhara ya kiapo majanga yake hayapimiki,…yakianza
hutamtemea kiongozi wako kuwa atakuja kukusaidia , hapi ni wewe na familia
yako…,
‘Sasa basi, kama umeingia humu ndani, na umekuja kuwakilisha
wenzao ni lazima ukubaliane na matakwa ya kikao, kama unahisi hutaweza kuhimili
majukumu na msharti ya kikao, ikiwemo hili la kula imini, na kumtetea kiongozi
unayemuona kuwa kweli ndiye mfalme mtarajiwa ni bora uinuke na utoke nje…..’
hapo akatulia kwani kabla hajamaliza huo usemi wake, mzee hasimu aligeuza
kichwa na kuwaangalia watu wake kwa macho ya kuwatisha
Lakini hata hivyo hutaamini…..hakuna aliyejali macho ya huyo
mzee, karibu nusu ya wajumbe wake walinuka na kuanza kutoka nje wakiwemo wazee
wake watiifu,……na hata pale mzee hasimu alipowalazimisha wasitoke, hakuna
aliyemsikiliza, na baada ya nusu saa wakabakia wajumbe wachache tu ambao
walionekana kuwa ni ndugu wa karibu sana wa mzee hasimu, na hapo yule
msuluhishi akamgeukia mzungumzaji wa kikao, akasema;
‘Naona wajumbe wamepungua sana, na kikao kama hiki kinahitaji
wajumbe nusu kwa nusu, ili tuwe na muafaka kamili, ….tunaomba muwakaribishe
wajumbe wengine waliopo nje, kama wapo tayari kwa hili tunaloendelea nalo
waingie, kama hakuna ambaye yupo tayari kukubalina na hayo tuliyoongea basi
inabid mliopo humu ndani tuendelee na tukimaliza hape tutaanza zoezi jingine…
Alipoamliza hivyo wajumbe wengine wa mzee hasimu wakaanza
kutoka, na hatimaye walibakia wajumbe watano tu, mzee hasimu na kijana wake, na
wasaidizi wa karibu wa mzee hasimu, …..
‘Mzee, hasimu, naona wajumbe wako wamekukimbia je unalo la
kusema …..?’ akauliza mzee hasimu, na mzee hasimu akageuka nyuma hakuamini
macho yake, akamwangalia kijana wake na kijana wake alikuwa kainama chini,….
Mzee Hasimu akakohoa na kusema; `hawo ni waoga, na katika
vita hutakiwi uwe muwoga, sisi tuliobakia tupo tayari kwa hilo…’akasema na
wenzake wakamwangalia kwa macho ya wasiwasi, hata kijana wake alionekana wazi
akiwa na wasiwasi, na mzee akamshika bega kumtuliza.
‘Sawa mzee, tunashukuru kwa hilo, na naomba mgawaji wa hayo maji
awapelekee hawo wajumbe, na wote waliopo humu ndani,…..je nyie wengine mpo
tayari kwa zoezi hilo?’ akauliza huyo muwakilishi, na hata kabla hajamaliza
watu wate walisema kwa sauati
‘Tupo tayari…tuna amini kabisa kuwa mfalme huyo hapo mbele
ndiye yule mfalme mtarajiwa…’
Mzee hasimu akakunja uso kwa hasira, na wakati huo alikuwa
kashika kiriba cha maji aliyoletewa, akionyesha ukakamavu kuwa yeye haamini, na
akawaangalai wenzake kwa macho ya ya kuwapa moyo, …kijana wake, alionyesha wazi
kuwa ana wasiwasi, na hata yale maji aliyopewa alikuwa kayashikilia kwa mbali
kabisa …
‘Kijana wa mzee Hasimu , wewe nasikia ndiye uliyependekezwa
an kundi lako kuwa ndiye mfalme mtaarjiwa, ….wewe ndiye unatakiwa uwe mfano,
kwa vile unauhakika kuwa wewe ndiye mfalme mtarajiwa, …tunakuomba usisite
kuyanywa hayo maji, kama kweli ni haki yako, kama kweli upo kwa ajili ya
wananchi, na kama kweli ulidhulumiwa nafasi yako, basi wakati wa kuonyesha hili
ndio sasa,…je upo tayari..
Kijana mtarajiwa akageuka kumwangalia mzee wake, ….mzee wake
alikuwa kamkazia jicho, akageuka upande wa msaidizi wake, na mshauri wake mkuu,
huyo alikuwa kainama chini, na hakutaka kabisa kumwangalia, akamgeukia jemedari
wake wa majeshi, ambaye yupo tayari kufa na yeye, na kwa mara ya kwanza
ali,muona huyo jemedari kaangalia chini….
Akilini akakumbuka madhara ya maji hayo ya kiapo, ambayo
aliwahi kusimuliwa na huyo huyo mzee wake, kuwa kama utayanywa na ukasema
uwongo, ….haipiti hata nusu saa, ….mwili mzima unaweza ukaanza kuharibika kama
mtu aliyemwagiwa tindikali, au maji ya moto, au unaweza ukapoteza uwezo wa
kuona, hapo hapo, au unaweza ukavimba tumbo,…kama mtu aliyepuliziwa upepo hadi
lipasuke…..
‘Mjukuu wangu katu hata siku moja usije ukakubali kunywa
maji ya yamini kama unajua kuwa yamini hiyo ni kweli na wewe unasema uwongo…ni
bora usinywe, babu yangu aliwahi kuyanywa hayo maji ya yamini akijua kuwa ni
mzaha,…..alipomaliza kunywa tu, mwili wake ulianza kubadilika kama vile
kamwagiwa maji ya moto…
‘Hili nililishuhudia kwa macho yangu mwenyewe…alipiga ukulele,
kwani maumivu yake ni makili sana,lakini hakuna aliyemsaidia, kwani ukimsaidia
na kumuonea huruma na wewe yanakukuta hay ohayo….kwahiyo aliachwa na baada ya
nusu saa, walikuwa mtu kaiva kama nyama iliyobanikwa,…lakini kufa hafi…na
anaita watu wamuue, ili asiendelee kuteseka na mates ohayo…
‘Dawa yake hapo ni yeye kukubali ukweli, kuwa alikosea, na
….hapo atakata roho, na mwili wake unatupiwa mamba……’akamwambia babu yake. Na
alishangaa kumuona leo akimshinikiza akubali uwongo….akatikisa kichwa,..
‘Haya ni wakati wa kuyanywa hayo maji, tunaanza kwa mfalme
mtarajiwa, wewe ndiye unayetetea ufalme wako, upo tayari kuyanywa hayo maji?’
akaulizwa mfalme mtarajiwa,..na mfalme mtarajiwa akapokea kile kiriba cha maji
na kusema;
‘Nipo tayari muheshimiwa,…..’
‘Haya kunywa hayo maji, …ukijua kama ni uwongo, basi hayo
maji yatafanya kazi yake na kama ni ukweli, hayo maji yatakuongezea ujasiri,
….hekima na uwezo wa kuitawala nchi hii kwa amani na upendo, na hakuna
atakayewea kukudhuru, kwani uma wa wananchi waliokusubiria miaka mingi watakuwa
nyuma yako…haya kunywa hayo maji…na wale wote wanaomuamini, ambao wapo nyuma
yake, wanywe hayo maji.
Mfalme mtarajiwa akainua kiriba juu na hapo hapo akaanza
kuyanywa yale maji, na watu wake wakafuatia na kuyanywa mwaji waliogawiwa….na
wengine nje wakaingia kila mmoja akitaka kuyanywa hayo maji, …na hata watu wa
mzee hasimu wakajiunga kuyanywa maji kwa kiapo kuwa wanamkubali huyo mfalme
kuwa ndiye mtarajiwa….na baada ya kuhakikisha kuwa wote wale wanaomkubali huyo
mfalme wamekunywa hayo maji, ikabakia zamu yam zee hasimu na kijana wake…
‘Haya ni zamu yako mzee, na kijana wako….naona hata
wasaidizi wako wamekukimbia…’akasema huyo mzungumzaji kwani kweli,. Kwa muda
huo walibakia mzee hasimu na kijana wake. Mzee hasimu akamgeukia kijana wake na
kusema;
‘Kijana wangu,…hivi ni vita, na unapokuwa kwenye vita
unatakiwa uwe jasiri, unatakiwa upiganie kile unachoona ni haki na halali yako,
mimi nimekuwa nyuma yako, na ,mimi ndiye mwalimu wako..na sitaweza kurudi nyuma
kwa hili, kama upon na mimi basi kunywa haya maji…’ yule mzee akainua kiriba
cha maji na kuanza kuyanywa…..
Kijana yule alipomuona mzee wake anafanya hivyo, na yeye
akiwa anatetemeka mkono akainua maji na kuanza kuyanywa, kwanza alianza kwa
fundo dogo, baadaye akaongeza, na lipoona yananyweka akaanza kuyanywa kwa kasi
kama alivyofanya mzee wake…..na alipomaliza, kugeuka kumwangalia mzee wake,
macho yakamtoka kwa pima….akaanza kutetemeka…..
NB Je ni kweli kula amini kuna madhara, kama yapo kulitokea nini katika kisa chetu hiki,
hebu tuwe pamoja kwenye sehemu hii muhimu, nawatakia wikiendi njema
WAZO LA LEO:
Katika maisha yako, katika shughuli zako, na kwa kila jambo unalotaka kulifanya
jenga tabia ya kuwa mkweli na jitahidi kutenda haki. Ukiwa mkweli na ukasimamia
kwenye haki, katu hutashindwa kwa lolote lile, katu hutayumba katika maisha
yako, baraka amani na upendo, vitakuwa ndio maisha yako.
Twawatakia IJUMAA
NJEMA
Ni mimi:
emu-three
8 comments :
Good answer back in return of this matter with firm arguments and telling all concerning that.
Take a look at my web page ; satilik daireler ankara
bear grylls messer
Feel free to visit my website bear grylls messer
Mh hapo hata mimi natetemeka... I wish hata huyo kijana wa mzee Hasimu angekataa maana anajua fika ni uwongo uliotengenezwa. thanks for writing, weekend njema kwako pia
I’m not that much of a online reader to be honest but your sites really nice,
keep it up! I'll go ahead and bookmark your site to come back down the road. All the best
Feel free to visit my web page ; panota.com
Simply want to say your article is as astounding.
The clearness in your post is just great and i could assume you're an expert on this subject. Well with your permission let me to grab your feed to keep up to date with forthcoming post. Thanks a million and please continue the gratifying work.
Also visit my weblog : cleaning house
I almost never write comments, however I browsed some of the remarks on "Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-41".
I actually do have a couple of questions for you if you don't mind. Is it only me or does it appear like a few of the comments come across like they are left by brain dead visitors? :-P And, if you are writing on other online social sites, I would like to follow you. Would you list of every one of your public sites like your Facebook page, twitter feed, or linkedin profile?
My blog :: lacustomfinish.com
kaka mbona kimya kunani.
[url=http://buyallopurinol.download/]buy allopurinol[/url] [url=http://clomid.click/]clomid[/url] [url=http://colchicine.pro/]colchicine[/url]
Post a Comment