Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, December 11, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni mzazi-37




Marejeo: Hebu turejee kule porini pale tulipoishia, unakumbuka ule mvutano wa wale wazee wawili, unakumbuka siku ile ya sherehe ya kumtawaza mfalme mpya, je ilikuwaje hadi huyo mfalme akatawaza, na hasa walipogundua kuwa huyo mfalme aliyejitokeza ni mtoto wa mzee mteule, hebu tuangalie kipande hicho kwanza….

Mara akamuona yule mpanda farasi, ambaye alijua kuwa ni kijana wake, akatabasamu ni kusema kimoyo moyo, sasa basi, utawala ni wetu, wenzetu hawana chao, …..

Akawa sasa hayupo tena kwenye maombi kama wenzake, akili yake ikawa kumuangalia yule kijana ambaye kwa muda huo, alikuwa kainua mkono juu, kuvua lile kofia alilokuwa kalivaa…. Kitendo cha kuvua ile kofia kilifanyiak kwa haraka, lakini kwa mzee, kilionekana kama jambo lilichukua muda.

Yule kijana alipoondoa kofia yake, na kuacha uso wazi, mzee akashituka kidogo, kwanza akapikicha macho kuhakikisha kile anachokiona ni sahihi , isije ikawa ni njozi za kumtisha tu, ...akamwangalia yule kijana kwenye maumbile yake, akakubali kuwa kweli kimaumbile yule kijana mpanda farasi wanafanana kabisa na kijana wake, lakini sasa usoni, aliona sura nyingine,

Akataka kugeuka kuwaangalia wenzake kuwa na wao wanaona hayo mabadiliko, kama anavyoona yeye, kichwa hakikuweza kugeuka, lakini alichofanya ni kugeuza jicho la ndani kwa haraka uapnde wa kushoto n akulia kwake,...aliwaona wenzake wakiwa kwenye maombi, akapikicha tena macho yake kuhakikisha yupo sawa, hayupo kwenye njozi,

Hapo akaiona sura, ..na kuhakikisha kuwa sura ile ni kijana, kijana ambaye ataitawala nchi yao, kijana ambaye wote watamtambau kama mfalme wao, na huenda katika kushika madaraka yake hayo, ataibadili kabisa himaya hiyo, ..

Hilo sio tatizo kwake, mabadiliko ya jamii yanatakiwa yawepo, kwa utawala wowote mpya, na huyo ni mtawala mpya, anahitajika kuleta mabadiliko wanayohitaji wananchi,  lakini je yeye ataweza kuwepo kwenye utawala huo, na je hawo watawala wapya watamchukulia vipi yeye, hapo moyo ukaanza kwenda kasi, na jasho likaanza kumtoka, …

Hali ilizidi kuwa mbaya pale alipokumbuka sheria za nchi, ambazo yeye na wenzake walikuwa ndio wasimamizi, na hakuna mabdiliko yoyote aliweza kuyafanya, …mabadiliko kwake, yalikuwa pale anapohitaji jambo lifanyike kwa maslahi yao, na hapo alikuwa akitumia ngao ya kupiga kura, lakini je kwa utawala huo mpya hilo litakubalika, …jasho likawa linamvuja..

Akaziona zile sheria zikimnyoshea kidole yeye, aliona kama yeye yupo mbele akijihukumu mwenyewe na kutoa kauli kuwa akatupwe ziwani na kuliwa na mamba….

 Mzee hakuweza kuinua mboni za jicho lake tena kuangalia mbele, kwani kilichofuatia hapo, ilikuwa kama mtu aliyechukua sindani na kuuchoma moyo wake,akahisi maumivu makali, yasiyovumilika, kichwa kikawa kinauma mithili isiyojulikana, akaona giza likitanda usoni, na hapo hapo… akadondoka chini, na kupoteza fahamu.

Walinzi wa mzee huyu ambao nao pia walikuwa kwenye maombi yao, wakashituka, na wengine walikuwa wameinua kichwa kuangalia mbele , ili kuona ni kitu gani kimemuathiri mzee wao, na walichoona mbele
kiliwafanya washikwe na butwaa, hawakuamini macho yao, …na hali hiyo iliwafanya wasiharakishe lile agizo, kwani hisia zao zilishawagubika kuwa sasa wana utawala mpya.

Lakini amri ya jeshi ni amri tu, kwa haraka wakamsogelea mzee wao pale alipolala, akiwa katoa jicho , jicho la kushangaa, au jicho la woga, kiasi kwamba kila mtu hapo alijua keshafariki dunia.

‘Bado yupo hai,….’akasema mmoja wa walinzi wake ambaye pia ni mtaalamu wa matibabu, akaamurisha mzee huyo achukuliwe haraka , na watu wengine wasijue nini kinaendelea, …na kweli walifanya zoezi hilo haraka na mzee mwingine akaitwa kushika nafasi yake.

Wale askari watiifu wakamfikisha mzee wao huyo kwenye chumba maalumu, na yule mtaalamu akateta na mkuu wa vikosi, na mkuu wa vikosi akawaamrisha wale walinzi watiifu kuwa mmojawapo aende akamchukue bibi tibabu, na baadhi ya akina mama wale ambao wapo karibu na mzee, akiwemo mama mkunga, ..

‘Na wewe nenda kamtafute kijana wa mzee popote alipo, afike na watu wake, maaskari makomandoo , waje huku haraka, hakikisha hakuna kinachojulikana , mkija hapa mkitukosa, kijana wa mzee atawaelekeza wapi mtatukuta.

Wale walinzi watiifu wakatii amri na kutoka pale kwa kujificha, akini hata walipotoka nje, mawazo yao yalikuwa kuhakikisha kuwa walichokiona mwanzoni ni sahihi. Na kwanini mzee wao akadondoka hivyo ghafla, mzee wanayemjua kuwa ujasiri, ..mwenye afya nyingi, na hawajasikia akiumwa ovyo ovyo….

Wale walinzi walipotoka nje, waliona watu wote wakitabasamu, na nyuso zao zikiwa zimeelekea mbele, hakuna aliyekuwa na muda wa kuwafuatilia, kila mmoja alikuwa kashikwa na kumuhe muhe cha furaha, na akina mama walianza kuimba kwa pamoja, huku wakiinua manyoya ya ndge Tausi juu, wakisema;

 `Mfalme mtarajiwa keshafika , Yale waliyoahidiwa yametimia., karibu wetu msifika, wananchi twakutumania, Utupe yaso na shaka, kwa utawala ulotimia…..karibu, karibu ,karibu, ’

  Na wakati huo huo,  jopo la wazee , kundi la mzee mteula lilikuwa likisonga mbele kuelekea kule alipokuwepo yule kijana mpanda farasi, na askari wao walishapewa amri na kusonga mbele, kusimama sehemu ile waliyokuwepo askari wa mzee Hasim, …

Hakuna aliyetarajia fujo, kwani askari wa mzee Hasimu, walikuwa wametulia wakisubiri amri itolewe, lakini  kamanda wa mzee hasimu alikuwa haonekani, na hata kijana wao , mkuu na jemedari wa vikosi vyao alikuwa haonekani….msaidizi wake, akatoa amri kuwa warudi nyuma hatua kazaa wakisubiri amri nyingine….

********

Vikao mbali mbali vya kutengeneza katiba viliendelea kufanyika, kwa kila kundi, kwa kila rika, na kila mmoja alipewa nafasi ya kuelezea ni nini anakihitaji, na zoezi hilo lilisimamiwa na kundi lilikubalika, ambalo lilijumuisha wawakilishi wa kila kundi,ili kuondoa sintofahamu yoyote.

Wakati hayo yakiendelea, shughuli za usama na ulinzi zilikuwa zikiimarishwa kuhakikisha kuwa kundi Hasimu halifanyi jambo lolote baya, lakini cha ajabu, mzee hasimu na kijana wake, na watawala mbali mbali waliokuwa watiifu kwa mzee, walikuwa hawaonekani.

‘Hivi ulisema uliagiza kijana wa mzee aje muongee, kuhusu mambo mambo mbali mbali ya utawa, ikiwemo hili la huyo mtoto aliyeibiwa, …uliambiwaje?’ akauliza mzee mteula wakati alipokutana na kijana wake kwa mara pili.

‘Wasemaje wake walisema kwasasahivi hawapo tayari kwa hilo, na hawajui lolote kuhusu huyo mtoto, kwani alikuwa kwenye mikono ya utawala mpya, na walihakikisha kuwa wapo salama wati wote, hadi vikosi vyetu vilipofika na kushika doria, kwahiyo sisi ndio tunaostahili kuwajibika kwa hilo’akasema huyo kijana.

‘Mimi nilijua tu, kuwa hawa watu watakimbia kutokana na madhila yao, …na kwa hali ilivyo, kama wamekimbia, wanaweza wakaunganisha vikosi vya askari na kuanza kuleta fujo kabla hujasimikwa, ….’akasema mzee.

‘Hilo nimelifikiria na tuliliongelea na wakuu wote wa ulinzi, na wao wameweka kila aina ya ulinzi, kuhakikisha kuwa kila sehemu kuna askari, na askari wa mzee hasimu wapo kwenye kambii yao, hawaruhusiwi kuingia mjini hadi hapo makubaliano yatakapofikiwa…

‘Kuna ambao wameshajitokeza kujiunga na vikosi vyetu tumewapokea kwa tahadhari, maana wanaweza kuwa ni wapelelezi, …’akasema kijana, mfame mtarajiwa, na hapo akaingia malikia mtarajiwa na kuinama kutoa heshima kwa mzee wao. Mzee wao akainamisha kichwa,, na malikia mtarajiwa akamfikia na kuweka kiganja cha mkono wake kwenye kichwa cha huyo mzee …

‘Malikia mtarajiwa tuambie mumeafikia wapi, maana wajumbe toka makaoni wanaingia kesho, na wewe kwa hivi sasa ndiwe mtawala, mume wako bado hajasimikwa, …mama anatakiwa ashike hatamu wakati wote kuhakikisha kuwa watoto wapo, salama, wanakula, wagonjwa wanahudumiwa….’akawa anasema mzee.

Malikia mtarajiwa akasogea pale alipokaa mume wake, akamshika begani, …mume wake alikuwa kainama chini kuoneysha heshima ya malikia., na aliposhikwa bega akainua kicakainama na malikia akainua kichwa na kuwamwangalia mke wake.

‘Mzee wetu mtukufu, kila jambo linakwenda kama lilivyopangwa, waginjwa, watoto, wasiojiweza wote wanapata huduma zao, ila kupotea kwa huyo mtoto ndio imekuwa ni pigo, sio kwa jamii tu, lakini kwa sisi ambao tulikubali kuchukua dhamana yake, ….’akaema malikia .

‘Kwahiyo mnahisi kuwa ni nani kafanya hivyo?’ akauliza mzee.

‘Uchunguzi wa haraka, unaonyesha kwua ni mzee hasimu na kundi lake, lakini kwa vipi ndio tumeshindwa kujua, na hata kikosi cha siri hakijagundua lolote. Kuna mama mmoja tulimtarajia , mama huyo ni mtaalamu wa kunusa nyendo za mhalafu, lakini hayupo naye katoweka,..’akasema malikia.

‘Yule mama ni mtiifu wa mzee hasimu, hawezi kufanya jambo kama mzee hasimu hajamwambia alifanye, huenda wametoroka naye, huyo msimtegemee sana, ….wapo wataalamu wetu watumie, na kama kuna msaada wowote kutoka kwetu wazee usisite kutuita, tupo kwa ajili yako’akasema mzee na malikia akaondoka baada ya kuagana.

Malikia alitoka pale akimshukuru mungu wake, kuwa hatiamye mumewe mpenzi yupo naye tena, alitamani mzee asiwepo pale, ili aweze kumuonyesha mume wake jinsi gani anavyojiskia, lakini kutokana na pilika pilika za majukumu, wamekuwa wakiwa mbali, hadi hata suiku, wakikitana na usiku sana.

Hata hivyo moyo wake ulikuwa umefurahi, na alijua kuwa akiwa na huyo mume, majukumu yake yatakwenda sawasawa, kwani ni mtu wanayelandana, kimawazo na kitabia, akawa anatoka huku kumbukumbu za siku ile , siku ya maombi, siku ambayo hataisahau katika maisha yake yote

*****

Siku ile malikia mtarajiwa alipochukuliwa na kutolewa nje, akiwa amepambwa kwa vito vya thamani, na kuzungukwa na wasichana warembo, ambao ndio watakuwa wasaidizi wake. Wasichana waliolelewa kwenye nyumba inayojulikana kama nyumba takatifu, ambao walifundishwa elimu yote ya sheria, na mambo ya utawala, pia kulikuwa na akina dada, majasiri, walinzi, wanajua mbinu zote za usalama kutoka kwa mzee hasimu.

Licha ya kuwepo kwa hawo watu, malikia matarajiwa alijiona mpweke, kwani hakuna mmoja wa watu wa mzee mteule aliyeruhusiwa kuongozana naye, eti kwa vile aliyekuwa mume wake kauwawa na mamba, kwahiyo familia nzima sio safi, inaonyesha kuwa wao ni wakosaji, na hawastahili kuwa karibu na malikia mtarajiwa.

Ilibidi kuabliane nao , na ilibidi afanye hivyo, baada ya kushauriwa na mzee mteule, kuwa yeye hapo ni mama wa kila mtu, hatakiwi kukataa, na kusema hawo sio watu wake, hilo ni kosa kubwa, …akatoka nje, na kuanza kuongozwa huku akikanyaga maua mekundu ya waridi ya rangi mbalimbali yaliyokuwa yamemwanga kutoka hapo nyumbani kuelekea kwenye nyumba inayoheshimika.

Wakati anatembea, mawazo yake yote yalikuwa kwa aliyekuwa mume wake, hakupenda kukubali kuwa mume wake ameliwa na mamba, ….alikuwa mara kwa mara akikumbuka kauli yake;

‘Mke wangu uwe mvumilivu sana, kwani tupo kwenye kipindi kigumu, kipindi cha mageuzi, na kipindi hiki kina mitihani mingi, lolote linaweza kutokea, na likitokea jambp loloye liwe baya au zuri, lipokee kwa moyo mkunjufu, ukijua kuwa yote ni kwa matakwa ya muumba…’

‘Kwanini unasema hivyo mume wangu?’ akauliza.

‘Ni ukweli usiopingika kuwa sisi ni wanadamu, kuna leo na kesho, sisi wanadamu sio mali kitu, angalia watu wanaumwa, wanaokufa, wanaoumia, hawapendi iwe hivyo, lakini inawatokea, na wao ni wanadamu kama sisi, …sisi sio malaika, yote hayo yanaweza yakatufika, na yakitufika hatuna budi kuyakubali, kwani hayana budi yatufike…cha muhimu ni kuvura subira’akamwambia mume wake.

‘Yote uliyosema ni sawa, lakini cha muhimu ni kuweka matumaini mema, kuwa mambo yakuwa vyema, naahisi kuwa nitajitahidi nirudi na tuwe pamoja , tuweze kulijenga hili taifa, kama wewe ni malikia na watu wamekukubali, basi natumai hata mimi ndiye mfalme mtarajiwa, kama sio mimi, ….’hapo hakumalizia.
Malikia alikumbuak sana sehemu hiyo, alipotaka kumuuliza kwanini hajamalizia sehemu hiyo babu yao akaingia na kuwakatiza katika hayo maongezi,…

Malikia akawa anaongozwa kuelekea nje, na kwa mbele kwenye njaia panda, akaona sehemu iliyojengwa jukwa na kiti kilichopambwa na kuzungukwa na maua, hapo wanasema ndipo atakaa kwa muda, ili majasiri wote wamuona, majasiri hao mmojawapo ndiye atakayekuwa mume wake.

‘Jasiri huyo lazima atoke kwenye vizazi vyetu, lakini anatakiwa awe tofauti, na wanasema huenda akatokea upande ule mionzi ya juo ya kuzama itakapotokea, lakini ni lazima awe ni kizazo cha jamii zao, …yeye atatenda maajabu ambayo hayajawahi kuetendwa na wengine’aliambiwa siku hiyo.

‘Lakini mume wangu mbona ametenda maajabu mengi, kwanini hawamkubali kuwa ndiye mfalme mtarajiwa’akamuuliza babu yake siku moja.

‘Siku ya mavuno ndiyo siku mfalme matarajiwa ataonekana, ..hiyo ndio siku mtabiri alisema, alisema hata kama malikia ataolewa, lakini kama kaolewa na mtu ambaye sio anayefaa kuwa mfalme, ni lazima baya litamkuta huyu mwanaume na malikia atakwua huru kwa mafalme mtarajiwa….’aksema babu yake.
Na alipowazia hilo, akaanza kuingiwa na wasiwasi, kwani mume wake kweli haonekani, inawezekana kweli akawa hakuwa anayestahili kuwa mfalme, ….

‘Haiwezekani, ina mana kijana wa mzee hasimu ndiye anayestahili kuwa mume wangu, kuwa mfalme mtarajiwa haiwezekani, hapa kuna jambo limefanyika, na kama lipo mungu lifichue ….’akawa anaomba na mara mlio wa ndege wa matumaini ukasikia na kikundi cha watu, wakaonekana kwa mbali mmojawapo akiwa kapanda punda.

Alinua kichwa juu, na kuiona miali ya jua la kuchwa ikitokeza toka huko linapozamia, na mara muda wa maombi ukafika na yeye kama wanajamii wengine akaingia kwenye maombi ya moja ya maombi yake ni kumrejesha mume wake, mpenzi…na alipoinua kichwa akamuona mtu akiwa kwenye punda…

Kwa hisia zake, akaiona sura ya mume wake ikija kama taswira, na akainama tena kuomba, na alipoinua kichwa teana akamuona yule mwanaume akivua kofia,…hapo hakuweza kuvumilia, akageuka kushoto na kulia, akawaona wenzake wakiwa kwenye maombi, akamwangali yule mwanaume, hakuweza kuvumilia akasema; 

‘Mume wangu amerudi….mume wangu amerudi, mfalme mtarajiwa….’akawa anaongea na kuanza kwenda kumkimbilia lakini wale walinzi wakamzuia…walihitaji amri ya kumruhusu, kuondoka hapo, na hakuna aliyekuwa tayari kutoa amri hiyo, kwani wahusika walikuwa hawapo.

WAZO LA LEO:   Tusikate tamaa tunapokumbwa na misuko suko, yote ni sehemu ya mitihani ya kimaisha.Omba mungu, mshukukuru kwa yote, ipo siku utafanikiwa.


Ni mimi: emu-three

No comments :