Kais, alikimbia , pamoja
na ile hali yake aliyokuwa nayo hakujali, alichojali ni kutokomea mahali
hapo, kwani alijua yule mwanaume ni mmojawapo wa maaskari wa mzee, ambao huwa
ni watiifu kwa mzee, na kutokana na kiapo chao hawajui kuongopa. Kuna imani kuwa
ukishakula hicho kiapo, ukiongopa, humalizi siku, utapatwa na balaa kubwa sana.
Akakumbuka mmoja wa ndugu zake ambaye alikufa kifo cha ajabu
baada ya kutokusema ukweli . Ndugu yake huyo alikuwa ni mmoja wa maskari wa
huyo mzee, na siku hiyo alikuja kumtembelea, na akamkuta akiwa anaongea na kijana
, mjukuu wa huyo mzee. Aliporudi kazini kwake, akakutana na huyo mzee, na huyo
mzee akamuuliza kuwa alimuona mjukuu wake akiwa na Kais.
‘Hapana mzee, sijamuona mzee…’akasema yule askari.i zangu,
‘Una uhakika hujamuona huko ulipotoka, maana nimesikia
alionekana akielekea huko kwa huyo binti muhuni, kama umemuona huko na
unanificha, utakuwa umekiuka kiapo cha utii,…’akasema yule mzee kwa hasira.
Yule askari, moyoni akawa anajuta kwanini alikimbilia kusema
hajamuona, na alifanay hivyo ili kutowaingiza wapendwa hawo kwenye matatizo
hasa dada yake , lakini hakujua kuwa huyo mzee kazamiria nini hadi kufikia
kumuulizia hivyo.
‘Mzee mimi nilikuwa na safari zangu sikuwa na mawazo ya
kuangalia nyumbani kwa Kais, kuwa kuna mtu huko…’akasema huyo kijana.
‘Nilichotaka ni wewe kuniambai ukweli, na kama huo ndio ukweli wako, tutaona, maana
hiyo familia yenu ina walakini, ndio maaan sitaki kabisa mjukuu wangu amuoe
huyo binti. Ukumbuke kuwa kuna malikia mtarajiwa ndiye tunategemea ataolewa na
kijana wetu, sasa kama umemuona huko kijana wangu na hutaki kuniambia ukweli, …’yule
mzee hakumalizia akaondoka.
Ilikuja kugundulika kuwa huyo kijana alikuwa na Kais, baada ya mjukuu wa huyo mzee, kubanwa an
kusema ukweli, kilichotokea na yule askari kuvimba mwili mzima kama puto, macho
yakamtoka, na alikufa kifo cha mateso. Yule mzee akawaita maaskari na kuwaambia kuwa huyo askari amekufa kwa adhabu
ya kusema uwongo.
‘Unapokuwa kwenye kiapo cha utii, ukigeuka nyuma, ukaaliti
kiapo hicho, kifo chako kitakuwa kibaya kama huyo askari, mimi nilimuuliza
swali, ambalo lilikuwa rahisi kwake kujibu, kuwa alimuona kijana wangu aua
hakumuona, akanidanganay kuwa hakumuona…huyu ni askari ambaye anatakiwa anitii,
yeye kavunja ahadi ya utii, …’akasema huyo mzee.
Kila mtu aliyeona hilo tukio aliogopa kabisa kusema uwongo,
hasa maaskari wa huyo mzee, kwani matukio mengi ya vifo vya kutisha yalitokea
pale askari aliposaliti, au kusema uwongo, na kuwafanya wote kuwa maaskari
watiifu wa huyo mzee.
Kais alipokumbuka hivyo, akajua kwa vyovyote yule ni askari
wa mzee, na akikutana na mzee wao, atasema ukweli kuwa ka,muona bado akiwa hai,
na watatumwa watu kuja kumchukua akatupiwe mamba. Ili kuokoka na hilo, akaona
njia rahisi ni kukimbia kabisa kuelekea asipo pajua.
Alikimbia na hadi milimani, sehemu ambayo haiendeki, huko ni
milima, na miamba mikali, ….akapandisha hiyo milima na miamba hadi akatokea
kileleni kabisa cha hiyo milima, na alipofika kileleni, akaona kwa chini, nyika,
na uwanda mkubwa, na kwa mbali akaona watu wakiwa kwenye mashamba.
‘Huku naona ni sehemu tofauti na kwetu, huku kuna maisha, na
neema, ….’akasema na kuanza kushusha ule mlima kuelekea huko chini, akiwa
kachoka, njaa na kiu vikimuandama. Hakujali akijua kuwa baada ya dhiki ni
faraja, na anachohangakia kwa sasa ni hicho kilichopo tumboni mwake.
‘Huyu ndiye atakuwa faraja yangu, najua wakinikamata hawo
watu, watahakikisha najifungua, na mtoto wangu wanamchukua, ili akulie kwenye
himaya yao na kuwa mtumwa wao, wakati mimi wananifanya chakula cha mamba.
Sikubali mtoto wake atengani na mimi, ….akasema na hakujua kuwa pale alipo ni
kilima kikali.
Majani mabichi,
yalikuwa yametanda, na kuziba makorongo, ambayo mengine yalijaa maji, kulikuwa
ni mashimo ya hapa na pale, kuonyesha kuwa kulikuwa na watu wakichimba hayo
mashimo. Kais hakuelewa waklikuwa wakichimba nini.
Tahamaki, akateleza, na hata alipojaribu kushika yale majani
, haikuwezekana, akawa anaelea hewani kushuka chini, …..akajua sasa ndio mwisho
wa maisha yake, ….
***********
Maua alifunua macho, akiwa anaiwazia ile ndoto ya ajabu,
akajaribu kukumbuka jinsi ilivyokuwa, huku akiwaza ilikuwa na maana gani, na
kwa muda huo kichwa kilikuwa kikimuuma sana, lakini hata hivyo kumbukumbu za
ile ndoto, zilikuwa zikitawala akili yake, …kitu kilichomshangaza ni kuoto kuwa
ana mume, ilihali yeye hana mume, akatulia na kuliwazia lile tukio lilivyokuwa….
Siku hiyo baada ya ndoa yao, alimuaga mume wake kuwa
anakwenda kusalimia nyumbani kwao, na mume wake akamkubalia, akaondoka asubuhi
na mapema, alipofika kwao, akawakuta wanafamilia wao, baba na mama yake hawapo,
hakujua wamekweda wapi, akaona ni bora arudi nyumbani kwake.
Wakati anarudi , njiani alishangaa kuwaona watu
wakimwangalia kwa mshangao, kila mmoja akiwa kama anamsuta kwa macho, kuonyesha
kuwa kafanya jambo baya, au kuna kitu kibaya kimetokea dhidi yake, hakuweza
kuwaliza hawo watu, yeye akaona kwanza afike nyumbani kwake akamuone mume wake,
na ikibidi amuulize yeye ni kimetokea.
Alipofika karibu na nyumbani kwake, akakuta mlango upo wazi,
na kwa ndani akawa anawaona watu wawili, mke na mume,….yule mwanaume alikuwa
kalala chini, na kichwa chake hakionekani na huyo mwanaume alikuwa si mwingine
, bali alikuwa ni….ni mume wake. Alikuwa na uhakika kuwa huyo mwanaume ni mume
wake….sasa anafanya nini na huyo mwanamke
‘Mume wangu anafanya nini na yule mwanamke?’ akajiuliza huku
akiharakisha kuukaribia ule mlango wa nyumba kwao, lakini kila alipokuwa akiukaribia,
unakuwa kama unamkimbia, hawezi kuufikia, akawa anjitahisi kwenda kwa kasi,
lakini ilionekena ukaribu wa macho tu, kwa mwendo ilishindikana kufika.
Hata hivyo, aliweza kuona kila kitu kinachofanyika kule
ndani, ….hasira na chuki vikawa vinamuandama, na alitaka afike pale amshike
yule mwanamke ambaye alionekana akiwa juu ya mume wake…..
‘Yule mwanamke nikimshika, nitahakikisha namchana-chana…’akasema
kwa hasira.
Tahamaki akazindukana na hakuona nyumba wala huyo aliyemuona
kuwa ni mume wake sio mume wake, alikuwa ni mtu ambaye hana uso, uso umefunikwa
na kofia ya ngozi ya wanyama, akaanza kuogopa, ..
Kwa mbali alimuona yule mwanamke akikimbia, ….na huyo
mwanaume kasimama akiwa anamwangalia yule mwanamke anavyokimbia, hakutaka hata kumfuatilia. Maua , akawa anajiuliza huyo mwanamke
anakimbia nini tena, na kabla hajawaza zaidi yule mwanaume akawa keshamgeukia na wakawa wanaangaliana, Maua
akamuuliza huyo mwanaume.
‘Wewe ni nani na kwanini umejifunika huo uso wako hivyo?’
akauliza, yule mwanaume akamwangalia kwa muda bila kumjibu, na baadaye akasema
kwa sauti isiyosikia vyema;
‘Mimi ndiye nilyekuokoa toka kwenye mdomo wa mamba, wewe
ulitakiwa uwe kitoweo cha mamba, lakini nimefanikiwa kukuokoa, ushukuru sana,…kwani
katika histori ya huo mto, hakuna binadamu aliyewahi kutupiwa hao mambo,
aliweza kuokoka,….wale mamba wana njaa, ukitupiwa wanakugombea kama nini sijui…’akasema
huyo mwanaume.
‘Kwanini ukaniokoa, ….?’ Akauliza Maua na hapo hapo
akakumbuka, akashika tumbo lake,…haraka akainuka, akaangalia huku na kule…
‘Yupo wapi mwanangu?’akauliza huku akianza kusimama,
‘Sasa hivi ndio unakumbuka
mwanao, hujui zimepita siku ngapi tangu upo hapa maporini, …’akasema
huyo mwanaume, na kumuacha Maua akiwa akishangaa.
‘Yupo wapi mwanangu..’akauliza Maua huku machozi yakimtoka kwa
wingi.
`Tulia kwanza,…usiwe na wasiwasi, mwanao yupo salama,
umeshasahau kuwa ulitakiwa ukishajifungua wewe utupiwa kwenye mto wa mamba, na
mtoto wako anachukuliwa kulelewa kwa
ajili ya kuja kuitumikia sehemu inayojulikana kuwa sehemui takatifu…umesahau kuwa ulipojifungua
tu, maaskari watiifu wa yule mzee, walikutosa kwenye mto?’ akaulizwa.
‘Hujanijibu swali langu, mtoto wangu yupo wapi?’ akauliza
Maua, huku bado akiwa haamini, alijua kuwa yupo kule kule alipojifungulia, na
akili yake ilikuwa haijakaa vyema.
‘Jibu la swali lako nimeshakupa, …..wewe unachotakiwa kwa
sasa ni kujali afya yako kwanza, hayo ya mtoto kwako wa sasa hayakuhusu…na
sijui kama unaweza kumpata tena….sijui, kwani wakikushika hawo maaskari watiifu
wa mzee, watahakikisha safari hii utatafunwa huku wanakuona…’akaambiwa.
‘Eti nini, ya mtoto wangu hayanihusu, unajua jinsi gani
nilivyoteseka kuilea hiyo mimba, unajua jinsi gani hiyo mimba ilivyonitesa
mimi, jinsi gani kuwepo kwa hiyo mimba, kulivyo niharibia maisha yangu yote, na
yale matarajio na ndoto zangu, zote zilivyoyeyuka kwa sababu ya hiyo mimba,….
hadi kufikia hatua hii, ….’akasema kwa uchungu.
‘Kama ni hivyo, una haja gani ya kuhangaika kumtafuta huyo
aliyeweza kukutia kwenye machungu kama hayo, nafikiri ni bora usionane naye tena, maana ukimuona
atakuwa akikukumbusha hayo machungu, ni bora ukatulia ukamsahau katika akili
yako’akaambiwa.
‘Kama mzazi huwezu kuyashahu hayo machungu,…hata kama huyo mtoto yupoje, hutaweza kuyasahahu
machungu yake, …kwasababu uchungu wa mwana aujuye ni mzazi…’akasema Maua
akiinuka, na lengo lake lilikuwa kwenda kujitosa kwenye ule mto, aogelee hadi
huko alipo mtoto wake.
‘Sasa unataka kwenda wapi?’ akaulizwa.
‘Nataka kwenda kumfuata mtoto wangu, nataka nikamchukua
mtoto wangu, nikamlee mwenyewe..’akasema Maua huku akianza kutembea kuelekea
kule ulipokuwa ule mto. Yule mwanaume akawa kasiamama anamwangalia tu
Maua alitembea kwa shida, huku kichwa kikimuuma, na akawa anasikia miumivu
mengine ya tumbo lakini kwa vile yalizidiwa na maumivu ya kichwa, hakuyajali sana hayo, hakujali hayo maumivu, mawazo yake yote yalikuwa kwenda kumtafuta
mtoto wake alipo, na ili ampate, alijua ni lazima aogelee kwenye huo mto wa mamba hadi afike ng’ambo
ile ya pili, kule alipojifungulia.....kwa muda huo hakujali kuwa kwenye mto huo kuna mamba wenye njaa kali.
Alipofika tu kwenye ule mto, cha kwanza kukiona ni mamba aliyeruka
hewani akitaka kumdaka…akarudi kinyume nyume huku akipiga yowe,..kichwa kikawa
kinamuuma sana, na nguvu zikawa zimemuishia, akadondoka chini, na wakati huo
huo mamba yule alikuwa keshatoka kwenye maji anakuja pale alipolala.
Hakuweza kufikiri tena akafumba macho, huku akiyasubiri hayo meno makali ya huyo mamba, kichwa, kilikuwa kikiuma kupita kiasi, akaona heri, basi huyo mamba amumalize tu, ili aondokane na hiyo shida, na mara akahisi akanyakuliwa juu kwa juu, na hakuweza kuona kitu
zaidi ya kuzama kwenye giza nene
.
NB Angalau siku isende bure, nimekileta kipande hiki, ambacho kitahitaji marekebisho baadaye kwenye kitabu tukijaliwa.
WAZO LA LEO: Kwa wale wenye imani: Kama umejaliwa kuwa na uwezo, uwakumbue wenzako ambao hawajajaliwa, ukikumbuka kuwa hicho utakachojitolea kwao ndicho chako, ndiyo akiba yako ya maisha baada ya hapa.
Ni mimi:
emu-three
7 comments :
[b][url=http://www.uggsoutletnow.com/]www.uggsoutletnow.com[/url][/b] Today, everyone is looking to make a buck by selling you the get prosperous brief schemes when in fact, all necessary is time, endurance, and concentrate. we are able to settle as rapidly as 7 days offered we can easily obvious title. we are able to settle as quickly as seven days supplied we can clear title.
[b][url=http://www.onlinesaleswebsite.com/]www.onlinesaleswebsite.com[/url][/b] Then how to acquisition a sneakers that could overall look your frame of thoughts auspiciously is definitely an significant position. That is the accuracy that there are various brand names of aerial heel footwear, but christian louboutin nude pumps nonetheless stands in a very major situation amid them. As is acknowledged to us, christian louboutin sneakers is heralded for its adequate activity and various design and style and type.
[b][url=http://www.louisvuittonoutletmart.co.uk/]louis vuitton handbags[/url][/b] Providers have to devote in their product sales crew growth equally as skilled sports activities groups follow their craft each working day. Product sales can be a career, one of several several professions where ongoing teaching is just not required to always execute from the job. Nonetheless, it really is crucial to achievements.
[b][url=http://www.onlinesaleswebsite.com/]louis vuitton outlet[/url][/b] With lots of women purses and handbags that happen to get sometimes impacting this current market, it comes about for being genuinely tough choose for suitable purses and purses to match just about every ethnical capabilities or perhaps occasions. Be sure that you go for baggage which may be tasteful, exquisite, classy as well as realistic at the same time. Most ladies purses and handbags are usually viewed as an excellent expenditure independently which makes it rather crucial to help you out to subject material label standard factors that produce a marvelous select options.
[b][url=http://www.cheapuggsstore.com/]cheap ugg boots[/url][/b] Should you wish to very own an elegant wallet, you could possibly opt for one particular from Monogram Vernis wallets. Unequal types can constantly satisfy your requirement. In addition to, monogram canvas tote bags are appealing and modern. Considering the fact that then, the girl Authentic Louis Vuitton Damier Canvas Hampstead PM Bag grew to be Princess Diana closest go along with. She normally took aspect in some principal campaigns with it. ConsequentlyLady Dior unfold all around the earth.
rules "the husband son thanks thanks GHD IV.
"She is beautiful north face outlet store.
gEre ghd nz sale check it again the rest of the still operating int.
1hDsi 4tOah ghd straightener
Longchamp jjceavgl Longchamp Pas Cher kxdooqqi Sac Longchamp qpppfrnb Longchamp Soldes ajdndncq Longchamps apbbvexl
ugg znglngcb botas ugg kuuwnzpc ugg españa
Your own wrіte-up haѕ сonfirmеd benefiсial to us.
It’s extremely іnformative and you're simply certainly extremely experienced of this type. You possess popped my own sight in order to various thoughts about this specific subject together with intriquing, notable and reliable content.
My web blog - wiki.nexuiz.com
Here is my website :: phentermine
I visit day-to-day a few sites and blogs to read
posts, except this blog offers quality based writing.
my webpage; grupa kreatywna
ttpEjfetYr [url=http://stefanie.iconosites.com]abrahfamse1[/url]
znqKtozcQk [url=http://stefanie.iconosites.com]abrahfamse1[/url]
qmwGxzpwOn [url=http://stefanie0723.tripod.com]abraamgsen2[/url]
koqXvgbrOb [url=http://stefanie723.webs.com]abrahamsden[/url]
wteVhosxYy [url=http://stefanie723.webs.com]abrahamsden[/url]
aisPifglQy [url=http://stefanie723.webs.com]abrahamsden[/url]
bdmOhczhCb [url=http://stefanie0723.tripod.com]abraamgsen2[/url]
xdqGjdafTp [url=http://stefanie0723.tripod.com]abraamgsen2[/url]
ctgAfmxpTe [url=http://stefanie723.webs.com]abrahamsden[/url]
pfrZqjvuTp [url=http://stefanie0723.tripod.com]abraamgsen2[/url]
aphFgnohTq ycbKgunbFz
Post a Comment