Maua anasema maumivu ndiyo yaliyokuwa akilini mwake, na
mwili wote ukawa kama umekufa ganzi, na kwa muda huo hakuwa anajua nini
kinachoendelea, kuna muda alihisi kuwa yupo hewani,ikimaanisha kuwa amebebwa,
na kwahiyo atakuwa anapelekwa ufukweni, ambapo anatakiwa akajifungua
tu,anatupiwa mtoni, akaliwe na mamba.
Kuna muda kutokana na maumivu, alikuwa akipoteza fahamu kabisa,
na alipozindukana kwa safari hii ndpo akasikia kilio cha mtoto mchanga, hapo akajua
keshajifungua, akajitahidi kujiinua ili amuona mtoto wake,angalau aione sura
yake, kwani huenda hataiona tena , akainua kichwa kwa shida, huku macho yakiwa
yamejaa machozi, na bahati nzuri yule mkunga akajua nini mama huyo anakihitaji,
akamleta yule mtoto karibu yake.
‘Mtoto wako mnzuri, ..ana afya njema, usiwe na wasiwasi atalelewa
vyema kabisa, na akikua atapata mume jasiri wa kumuuoa,ila wewe, huhitajiki
tena kweney ardhi hii,na sisi tunatimiza wajibu wetu, kutokana na maagizo
tuliyopewa, hatuna jinsi ya kukusaidia…’akasema huyo mkunga.
Maua alijaribu kufunua mdomo, akitaka kusema, wamlee mtoto
wake vyema, lakini mdomo haukuweza kufunuka, akawa anaongea kihisia hisia, na
kuomba kwa mungu mtoto wake asije akaangukia kwenye mikono mibaya na kupata
taabu.
Maua anasema; ‘Nilimwangalia mtoto wangu kwa macho ya
huzuni, nikijua kuwa ndio mara ya mwisho kumuona, na sijui atapelekwa kulelewa
na nani, na hilo sikuwa na jukumu tena, kwani pale nilipo nilikuwa kama mfu tu.
Baadaye yule mtoto akaondolewa mbele yangu, na mimi
nikafungwa fungwa na ile ngozi niliyokuwa nimelalia wakati wa kujifungua, wao
walihakikisha kuwa hakuna damu inadondokea kwenye ardhi yao. Wakanifunga kama
gunia au furushi bila kujali uchafu na damu zote zilikuwa zikizagaa mwilini
hata kuingia mdomoni na puani. Nikahisi
maumivu na ilikuwa kama nakaribia kupoteza fahamu na mara nikasikia wale
wakunga wakisema;
‘Tumeshamaliza kazi yetu, mnaweza kumchukua mtu
wenu..’akasema mkunga mkuu, na mara wakaja maaskari wanaume wenye nguvu, wakaniinua
juu kwa juu, huku wakihimizana kuwa wahakikishe hakuna damu yoyote inaangukia
chini, na walipofika ufukweni, wakaniweka kwanza chini, na mmoja akasema;
‘Mbona leo ziwani kupo kimiya, sioni mamba hata mmoja upande
huu, nilitaka nione jinsi gani anavyomtafuna mtu, maana ….huyu dada, namuonea
huruma, lakini ….’mmoja akasema.
‘Wewe huwaoni hawo mamba, lakini wao wanatuona, wewe subiri
tukishamrusha kwenye maji utakavyoona vumbi lao, ….huoni yale kama macho
yanatutizama kule mbele’akasema mmojawapo.
‘Mimi ninawasiwasi, huenda mizimu na wazee hawalipendi hili
tunalotaka kulifanya, hamuoni kuwa huu ni uuwaji , na tunamuua mtu asiye na
hatia?’ akauliza mmojawapo.
‘Wewe unaona hivyo, lakini wakuu wameona vinginevyo,sisi
kazi yetu ni kutimiza wajibu wetu kama maaskari watiifu, na kama ni lawama
watazibeba wao wenyewe, …’akasema mmojawapo.
‘Tatizo hapa kuna ubaguzi, kila ikifikia ukoo wa hali ya
chini, amri zinakuwa tofauti na za wale wa hali juu, na hili linaleta
manung’uniko miongoni mwa watu. Kama haki haitendeki, kama hakuna usawa katika
maamuzi ya kijamii, hakutakuwa na amani kamwe’akasema huyo askari ambaye
alionekana na huzuni kuliona lile tendo likifanyika.
‘Ukianza kuwaza hivyo,hata hii kazi itakushinda,….’akasema
askari mwingine.
‘Lakini nyie hamuoni, kuna koo, watu wake wakisema neno,
linachukuliwa kwa uzito wa hali ya juu, lakini kuna koo, nyingine hata kama
wanachoongea ni cha ukweli, na cha haki hawasikilizwi, watu wanachoangalia ni
nani anayetoa hoja,kuliko ni nini sheria inasema kwa mataji huo tutaiangamiza
nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe’akalalamika yula askari.
‘Kwani wewe shida yako ni nini, wewe hujatoa maamuzi, wewe
kazi yako ni kutekeleza, kama ni lawama sio juu yako wewe’akasema mwenzake.
‘Mimi kama binadamu ina niuma, kuona kuwa kuna watu
hawatendewi haki, kuna jamii, kuna ukoo nyingine hazipati huduma, au nafasi
sawa na jamii nyingine, ukiuliza unaambiwa unaleta uchochezi. ..’akasema huku
akimwangalia yule mwanamke ambaye alishaviringwa kwenye ile ngozi kama maiti.
‘Tatizo lako wewe ni muoga, huna lolote jingine…’askari
mwingine akasema huku akimalizia kazi ya kumfunga funga yule mwanamke, ili
kuhakikisha anaondoka na damu zake zote.
‘Mimi ni kweli naogopa sana,maana hata sisi watekelezaji
tuna fungu la lawama,kwani leo ni kwa huyu kesho inaweza ikawa zamu yetu, huwezi
jua, ….na hata hivyo, balaa likitokea halitachagua ni nani wa kumwangamiza…itakuwa
kama zile gharika tunazosimuliwa na wazee wetu’akasema na kusogea pembeni.
‘Wewe kama unaogopa kaa pembeni, ngoja sisi tutimize wajibu
wetu, sisi ni askari, tukipewa amri, hatutakiwi kusita, ni kutekeleza tu, mengine
watajua wao watawala, na hiyo gharika ikitokea, ni kifo cha wote, ….haya inua
huko, angalia huko, unaona hiyo damu ….’akasema mmojawapo, akimuelekezea
mwingine, na yule askari mwingine akawa kaka pembeni akiangalia ziwani, na
macho yake yalikuwa kama yameona kitu cha jabu, lakini hakuweza kusema neno.
Katika kuinua inua damu chache ikawa imedondokea chini, na
hili halikutakiwa kabisa, na kwa imani zao inaashiria kuwa kutatokea jambo,
kwani wamakiuka miiko. Na wale maaskari wakaogopa,wakijua ikijulikana wao
watabeba lawama, mmoja wao akasema
‘Ifukie hiyo damu haraka…’na mwenzake akafanya hivyo, huku wakiangalia huku
na kule, na bila kupoteza muda, au kuangalia vyema kule kwenye mto wa mamba,wakajiandaa
kumrusha huyo mwanamke kwenye maji, wakahesabu moja mbili tatu….
********
Kais, alifikishwa kisiwa, sehemu iliyotengwa kama jela, kila
mkosaji hupelekwa hapo, na kuachwa aishi peke yake, bila chakula wala maji,
baada ya siku kadhaa anakutwa ameshakufa , au kuliwa na wanyama, au kumezwa na
chatu. Hii ndio adhabu aliyopewa baada
ya kupatikana na hatia ya kudanganya.
Kais mwanzoni hakuogopa, akijua keshatimiza ahadi yake kwa
mtu aliyempenda,akijua kwa vile hata huyoo mwanaume anampenda huenda akafanya
juhudi za kumuokoa, masaa yakawa yanakwenda, masiku na miezi ikapita.
Kais, akawa anaishi
peke yake lakini hakukuta tamaa, na alijitahidi kutafuta chakula , huku
akijificha kila anapoona watu wanapite kwa mbali. Hakutaka kabisa kurudi kwao,
kwani alijua kikutana na huyo babu wa mume wake atamuua, alikumbuka jinsi
alivyokuwa akitaka kutoa kisu pale alipojua kuwa mjukuu wake kamuoa mtu
asiyestahili, na kama asingelikuwa mzee mwingine kuingilia kati, sasa hivi
angeshakuwa maiti.
‘Mzee mwenzangu, usije ukafanya jambo baya sehemu kama hii,….’yule
mzee mwenzake alimkaribia na kumshika ule mkono uliokuwa tayari unata kisu pale
kiunoni, tayari kufanya jambo ambalo lingeashiria umwagaji damu, na ilikuwa sio
sehemu ya kufanya tendo kama hilo.
Kiimani zao mzee, kama yule akiinua kisu tayari kwa kufanay
teno la mauaji, hatakiwi kukiriudiaha hivi hivi, vinginevyo inatakiwa kuotoa
kafara,na ndivyo alivyofanya huyo mzee baada ya kutoka hapo, alichinja mbuzi,
na kutoa kafara.
‘Huyu binti anatakiwa kushiktakiwa kwa kudanganya na
kuifedhehesh familia na ukoo wetu, ..’akasema huyo mzee, na wazee mashuhuri
wakakutana haraka na hukumu ikatolewa, kuwa huyo binti hastahili kuolewa tena
na mjukuu wao,kwani kwanza ni muongo, pili kaifedhehesha familia na ukoo, na
kwahiyo anatakiwa kuhukumiwa.
‘Adabu yake ni kutengwa na familia na ukoo, na hilo
litafanyika kwa yeye kutupwa kwenye kisiwa cha kifo, akaliwe na nyoka, au akafe
na njaa’akasema mzee anayetoa hukumu.
‘Imekubalika,….’wakakubali wenzake, na binti huyo
akachukuliwa juu kwa juu na kupelekwa nje ya eeno hilo, ambapo unavuka mto, na
kufikia sehemu ya mwiinuko kwenye miamba mikali had sehemu iliyo kati kati ya
miamba, ambapo watu hawawezi kufika, na hapo aliachwa.
Walipomfikisha hapo, walimuachia maji kidogo na punje chache
za karanga, kama walivyoamrishwa, na kuondoka zao.
Kais,alibakia pale akiwaza jinsi gani atafanya, kwani alijua
kama atatulia pale pale, ni lazima atakufa sio kwa njaa tu, bali kuliwa na
wanyama wakati hasa michatu. Na muda ulikuwa umekwenda sana, na hapo wakati
anawaza akakumbuka jambo.
Alikumbuka kuwa wakati anachukuliwa na wake askari bibi
alimsogelea kama anamuaga na haraka na kwa uficho, akamwekea kikasha kwenye
ukunjo wa nguo yake, hakujua ni kitu gani kwa muda ule. Alipokumbuka
hivyo,akakitfuta kwenye ule mkunjo akagundua kuwa ni kiksha, kubunda
kilichofungwa kama binzari, akakifungua na kukuta unga, akaunusa, na kupiga
chafya.
Akili yake ikaanza kuwaza ule unga ni wa nini, ndipo
akakumbuka, kuwa unga kama huo, alimsikia bibi yake akisema kuwa ukijipaka
harufu ya kibinadamu inapotea, kwahiyo hata kama ni mnyama mbaya hataweza
kugundua kuwa kuna binadamu mahali hapo. Na harufu kama hiyo huwafukuza wanyama
wabaya.
Akauchukua ule unga na kujipaka mwili mnzima, na kwa vile
alikuwa anahisi kiu akaona atembee tembee, huenda akapata choc kwani anavyojua
kwa mbele sana ndipo ule mto wa mamba hote cha kula. Alitembea kwa muda, na
kupanda kwenye miamba, na kushuka hadi akatokea sehemu ambayo mto unaanzia, na
hapo akajua kuwa keshaokoka, maana hapo anweza akaishi, na kupata maji, na
alihakikisha anajenga makao yake, kwani kama atarudi huko kwao, atatupwa na
kuliwa na mamba, yeye keshatengwa na jamii, hana ndugu tena, na maisha yake
yapo mikononi mwake mwenyewe.
Alichofanya ni kutafauta sehemu salama, akajua kuwa juhudi
zake ndzo zitamuokoa, akaanza kutafuta sehemu yenye maji salama, na baadaye
akaanza kutafuta samaki na chochote kinacholika,…
‘Mito mingu huku inaishi mamba, ukiinama kunywa maji, au
kunawa, wanakuvamia’akakumbuka hiyo kauli toka kwa bibi yake, na kwahiyo
walikuwa wakiogopa kukaribia kwenye mito au mabwawa yaliyotuama na hata
wakipita maeneo kama hayo huwa wanaogopa kuinama kunawa,kwani wanasema mamba
yeye akiwa majini anakuona na anatulia kimya ukiinama tu anakuvamia.
Siku zikaenda, …mwezi ukaisha, miezi ikapita,akagundua kuwa
yeye ni mja mzito, kwahiyo kwa vyovyote anatakiwa kutafuta njia a kuondoka hapo
mahali, kwani kuishi peke yake inaweza ikaleta matatizo, na alijua kuwa
kiutaratibu zao, mtu akiwa mja mzito, hatakiwi kuzurika mpaka ajifungue.
‘Lakini siwataki tena watu wangu, wameshanisusa, na wanajua
nimeshakufa, nitatafuta njia ya kutoka huku, na kwenda nchi nyingine…’akasema
na kuanza safari ya kutafuta njia ya kuondoka hapo, alitembea sana, hadi
akatokea kwenye mto kubwa, akaukumbuka kuwa huo ndio ule mto wa mamba.
Mara kwa mbele akaona kitu cha ajabu,mwanzoni alijua kuwa ni
mamba,lakini baadaye akaona kuwa ni kitu kama gunia,…au furushi la kitu
kilichofungwa kwenye ngozi ya wanyama, na ilionekana kam gunia. Akalifuatilia
kwa macho, kwani lilikuwa likitembea juu ya maji, kama mtumbwi.
Mara ghafla akaona maji yakitibuka, akatoka mtu, ambaye
kumbe alikuwa ndani ya maji huku kalishikilia hilo gunia akiogolea ndani kwa
ndani, kama vile hataki aonekane. Na alipofika ukingoni, akatjitokea na
kulibeba lile gunia hadi sehemu kavu.
Kais, alijificha akiogopa, kwani alihisi huenda ni hawo watu
aliowahi kusikia kuwa wanakula nyama za watu na huenda huyo mtu alikuwa keshamuua mtu na hapo anataka kumfanya kitoweo. Lakini kitu cha ajabu ni huyo mtu kuwa
ndani ya mto huo wa mamba bila kuliwa na hawo mamba,…
‘Huyu mtu alikuwa kajifunika uso wote, inavyoonekana
hakutaka kabisa sura yake ionekane,kwani aliachia sehemu ya macho ya puani, na
mdomoni, lakini sehemu nyingine zote zilikuwa zimefunikwa na kofia kubwa,
alilolivaa.
Mara akamuona yule mtu akilifungua lile furushi, na kweli
ndani yake kukatokea mtu , ambaye alimuona kama ni mwanamke.Na yule mwanamke
alikuwa kalowana damu, akahisi kuwa huenda huyo jamaa alimuua huyo mwanamke
kabla ya kumleta sehemu hiyo, akasubiri aone nini hatima yake.
Mara yule mtu akacmhukua yule mwanamke na kumsogeza karibu
na mto, akaanza kumuogesha yule mwanamke, hadi alipohakikisha kuwa damu mwilini
zimekwisha, akasogea pembeni na kuwasha moto, akachukua majani na chombo kidogo
alichokuwa kakibeba, akachota maji na kuyawekea jikono pamoja na unga unga, na
baadhi ya majani.
Haikuchukua muda yale maji yakawa yanachemka,na yule mtu
akachukua yale maji kwenye gome la kononokono, alilolitumia kama kikombe, na
kuchukua yale maji yaliyochanganyika na ile dawa kumnywesha yule mwanamke.
‘Mbona hafanani na hawo watu wanaokula watu,huyu anaonekana
kama tibabu, anamtibia huyo mwanamke…’akasema kimoyo moyo, akiwa kachuchumaa pale
alipojificha. Muda aliokaa pale alijiona mwili umechoka, na hali aliyo nayo,
hakuweza kukaa mtindo ule kwa muda mrefu, akajiinua, na kufanay vile alitoa
sauti.
Yule mtu kule akasikia,na kuinua kichwa kuangalia ka
tahdhari, akatoa kisu chake na kuanza kufuatilia huko aliposikia sauti, lakini
kabla hajafika mbali,mara ikasikika sauti nyingine,akasimama, na kwa tahadahari
akageuka, kumbe ni yule mwanamke,alikuwa keshazindukana.
Akawa katulia, huenda alikuwa akijiuliza afanye kitu gani
kwanza, kwani yule mwanamke alikuwa akigaragara, kuonyesha maumivu, na pale
alipokuwepo sio mbali na kwenye mto, na kulikuwa na muinuko, na kwa vile huyo
mwanamke alizindukana na akawa kama anajinyonga, na bila kujua yupo wapi, akawa
anaserereka kuelekea kwenye maji,.
Na kwa mbali walionekana mamba wakisogelea ufukweni,
walishanona chakula.Yule mwanamume akaona hana jinni ni bora arudi kwenda
kumuokoa yule mwanamke, na hapo Kais akaona ndio muda wa kutoka pale alipokuwa
kajificha, na kama inawezekana akimbie au auatafute sehemu nyingie, lakini kwa
hali aliyokuwa nayo, akaona huyi mtu anaweza kuwa msaada kwake.
Akamsogelea….na mara mamba akaruka toka kwenye maji,
kumrukia yule mwanamke,na yule mwanaume naye akaruka kama mbizi kumuwahi yule
mwanamke…..
*****
NB:Haya muda unakwenda kwa kasi, tuishie hapo kwa leo.
WAZO LA LEO: Kabla
hujamuhukumu mwenzako jichunguze kwanza nafsi yako, huenda wewe ni mkosaji zaidi ya
huyo uneyemuhukumu.
Ni mimi:
emu-three
6 comments :
kwakweli kipaji chako ni cha pekee sana. hongera sana. nafurahi kwamba umekipangilia vyema na sasa tunakwenda pamoja, mwanzoni ulikuwa unanichanganya kwa kuweka visa kibao kwa mara moja! asante sana kwa kuyafanyia kazi maoni yangu. umefikia wapi kuhusu kutoa kitabu? u have a great talent in writing stories!
Nashukuru sana mkuu hapo juu, nashukuru kuwa nawe umenielewa, mm mtindo wangu wa kutunga hivi visa ndivyo ulivyo, ili kuleta tofauti kidogo na taratibu nyingine. Tupo pamoja, na nitajitahidi kadri niwezavyo, ili tuweze kuwa pamoja
Kisa kinavutia japo kinatisha hongera kaka
Nakupa hongera kweli una kipaji, na mm sioni ubaya wa mtiririko, unajua watu wengine wamezoea mtiririko wa moja kwa moja mapaka unajia nini kitafuata, lkn ww ni tofauti big up
bear grylls messer
Here is my blog :: bear grylls messer
Ubarikiwe saana, kazi ya mikono yake ikupe riziki ya halali. Tupo pamoja M3
Post a Comment