Hakimu alichelewa kuingia na hatukujua ni nani atasimamishwa
kujielezea, …na leo kulikuwa na watu wengine wameongezeka,….sikujua ni nani
hawo watu, nakwamba je ni miongoni mwa wahusika wa hiyo kesi au ni watu wa
sheria tu. Nhunguza kwa macho kama kuna ninayemfahamu, lakini wote walikuwa an
sura ngeni kwangu.
Kwamuda ule sikuwa ninajali sana kuwepo kwao,nilikuwa na
mawazo yangu kichwani, na nilipotua jicho langu upande wangu wa kulia nilimuona
kumwangalia yule mwanadada, rafiki wa wakili mkuu, naye ilionekana alikuwa
akiniangalia maana nilipogeuka kumwangalia aligeuza kichwa chake na kungalia
mbele kwa haraka.
‘Haya wakili mwanadada, tuambie ni nani anahitajika kwasasa
kuleta maelezo yake maana naona muda umekwenda sana….?’ Akauliza hakimu.
‘Wazungumzaji wetu wawili waliopita mke wa wakili mkuu na
rafiki yake,walikuwa hawajamaliza malaezo yao, naona ni vyema kwanza tukamsimamisha mke wa
wakili mkuu, na baadaye tutamsimamisha rafiki yake, tuendelee kusikiliza yao,
sehemu tuliyoachia.
Mke wa wakili mkuu, aliposimama kwanza aligeuka kumwangalia
rafiki yake, ambaye aliinua mkono na wakashikana kama vile wanapeana moyo.
Kweli walionekana ni marafiki alioshibana. Yule mwanadada, alikwenda moja kwa
moja pale mbele na alipokaa kwenye kiti
akageuka kumwangalia mume wake ambaye kwa muda huo alikuwa kainama chini.
Na mimi kwa muda ule nikawa nimwangalia kwa makini yule
mwanamke, nikajaribu kujiuliza kwanini aliamua kufanya jambo kama lile, na
kwanini ni rafiki mkuu wa huyo mwanadada mwingine, au ni kwa vile wanasema
waliwahi kukutana huko Kenya. Nilipofikia hatua hiyo, ya kuwa walikutana huko
Kenya, nikajaribu kumuwaza mtu niliyemfahamu, ….lakini sikuweza kuwaunganisha
kuwa huenda akawa ndiye huyo ninayemuwaza.
Nikamwangalia yule mwanadada akiwa katulia, haonyeshi
wasiwasi,….nikawa najiuliza ni nini
ataulizwa na wakili mwanadada, ….maana kwa mtizamo wangu, huyo mwanadada huenda
akajaribu kupindisha habari zake ili wasije wakaonekkana kuwa wao ndio walioua,
wau waliua kwa bahati mbaya,….naikawa na matumaini kuwa huenda leo ndio mwisho
wa maelezo yao, na ndio diku ya kumjua muuaji, ….vinginevyo itakuwa ni kupotezeana
muda tena.
Kwangu mimi niliona kama kupoteza muda, ….maana kila kitu
kipo wazi, watu wamekubali kuwa walizamiria hivyo, wkachukua bunduki, sasanini
kitafuta kama sio kuua, …ngoja nimsikilize huyo mwanadada kamaatasema nini
leo,maana …..dunia hii kuna mambo, kama walivyosema, hujafa hujaumbika…..
Wakili mwanadada akasimama na kumsogelea yule mke wa wakili
mkuu pale mbele,akamwangalia ,nilihis ni yale macho ya uwakil, yasiyo nawoga,
yenye ujasiri, kama askari aliyena djamira ya kweli, akauliza swali.
‘Hebu tuambie, siku ile mlipoamua kwenda kufanya yale mlioyokuwa
mumekusudia kuyafanya wewe na rafiki yako ilikuwaje,?’
‘Siku ile tulipanga tukutane nyumbani kwangu, na kwa vile
rafiki yangu alikuwa likizo , ilikuwa ni rahisi kwake, na mume wangu alikuwa
anaumwa kalazwa hospitalini. Na mimi siku hiyo ilikuwa siku ya mapumziko.
Rafiki yangu alikuja nyumbani mapema, na tukapata muda wakujipangavyema, na
kupeana majukumu.
‘Kwakeli kila mmoja alikuwa na hasira zake moyoni dhidi ya
Kimwana, maana taarifa nilizozipata mimi mwanzoni ni kuwa huyo mwandada hayupo
hapa jijini, …lakini mwenzangu aliniambai kuwa bado yupo, na anatamba kuwa
hawezi kukamatwa na polisi, kwa vile wote wapo mikononi mwake,…akiamua anawalipua
mara moja,…na pia atahakikisha waume za watu wenye wake lakini wake zao hawajui
kutunza waume, yeye ataifanya hiyo kazi, kwa thamani kubwa…
‘Una maana gani kusema kwa thamani kubwa..?’ akaulizwa.
‘Yaani hawo wanaume watamlipa gharama kubwa, kamaunavyoona
anajenga nyumba ya gharama kubwa, anagari la kifahari…..navitu kama
hivyo…’akasema huyoo mwanadada aklionyesha wivu usoni.
‘Hebu tukumbushe, mlijuaje kuwa yupo wapi,kwani kama sikosei
kwa muda ule Kimwana alikuwa anatafutwa na polisi?’ akaulizwa.
‘Rafiki yangu alikuwa keshapata taarifa zote, na kama
unavyokumbuka kwenye maelezo yangu ya mwanzo nilivyoelezea,tulishakwenda kule
kwenye nyumba iliyopo karibu na nyumba ya Kimwana na kugundua wapi anapojificha
,kwahiyo, hilo halikuwa gumu kwetu tena, na tulishajua kuwa ni siku gani
anakuwepo hapo, na kwa muda gani…’akasema.
‘Haya endelea na maelezo yako,….’akasema hakimu alipoona
wakili mwanadada katulia.
Basi kwanza tuliangalia mkanda mmoja wa ujasusi, mkanda huu
unafundisha jinsi gani ya kufanya upelelezi,jinsi gani ya kumuwinda adui
yako,na pia jinsi gani ya kuweza kumuwinda
adui yako bila hata ya yeye kujua, na jinsi gani gani ya kutumia silaha, ili
usije ukajulikana kuwa ndio wewe uliyeitumia.
Kwahiyo jambo la kwanza tulilolifanya, licha ya kuwa na
uhakika, kuwa mara kwa mara tulikuwa tunafanya hivyo na mume wangu,
tunapoirudisha ile silaha, tukiwa tumetoka kuwinda, …..Tukaifuta ila silaha
vyema, kuhakikisha kuwa haina alama za vidole na hapo nyumbani kulikuwa na
vitambaa mbali mbali vya kufutia alama za vidole, ….’akasema.
‘Ulijuaje kuwa ni vitambaa maalumu vya kufutia alama za
vidole?’ akaulizwa
‘Mimi na mume wangu mara kwa mara tunakwenda kuwinda na mume
wangu alishanifundisha kuwa ni vyema kwa usalama wa silaha ni kuhakikisha kuwa
ni safi na haina alama ya mtu yoyote, ili kama itatokea hatari,mtu kuitumia, iwe ni rahisi kumgundua….kuwa ni nani
aliyeitumia kwa mara ya mwisho….
‘Ina maana hizo silaha zilikuwa zinzwekwa wapi, …?’
akaulizwa
‘Kulikuwa na chumba maalumu ambacho hata msichana wetu
palenyumbani haruhusiwi kuingi, na mimi na mume wangu ndio wenye ufunguo wa
hicho chumba..’akasema.
‘Endelea kuelezea…’akaambiwa.
Kwahiyo mimi na rafiki yangu tulihakikisha hayo yote
tumeyafanya, na baada ya kuisafisha ile silaha, na kuiweka risasi,…tukiwa tumevaa
soksi za mikononi,…tulivaa hizo soksi za mikononi mapema, kabla hatujaishia
ile silaha, na tulihakikisha kuwa hakuna
anayeigusa hiyo silaha kwa mikono mitupu, tukiweka ile silaha kwenye mfuko
wake, ambao kama umeubeba inaonekana kama mtu aliyebeba gitaa, na sio rahisi
mtu kujua kuwa umebeba silaha.
Tulichukua gari langu hadi huko Mbezi, na tulipofika hapo
tuliliacha hilo gari, mbali kabisa na nyumba zile, na tukatembea kwa miguu hadi
kwenye lile jengo, na bahati nzuri, kulikuwa hakuna watu kwenye hilo jengo,
kulikuwa kimiya kabisa, tukapanda hadi gorofa ya juu, ambapo ungeliweza kuona
kule ilipo nyumba ya kimwana.
Tulipofika tukatafuta sehemu yetu ambayo tuslihaichagua
tukawa tunasubiri muda muafaka, tulipoangalia kule kwenye nyumba ya Kimwana, tulimuuona
Kimwana akiwa anatembea huku na kule,ilionekana alikuwa akikagua nyumba yake,
na hakuonyesha wasiwasi wowote, na hili likawa faraja kwetu.
Tulipoona kuwa muda muafaka umefika na Kimwana yupo kwenye
kile chumba chake,..tukajiandaa kufanya lile tulilokusudia, na mara tukasikia
gari likija eneo lile la jengo tulimuokuwa, lakini likapita na kwenda kusimama
kwa mbele,…kweye lile gari, walitoka watu wawili, wakawa wanatembea kuja kwenye
lile jengo, walifika wakawa wanakagua kwa nje, lakini bahati nzuri hawakupanda
juu, na baaadaye wakaondoka, lakini hatukujua wameeelka wapi, maana walipita
kwa nyuma ya jengo ambapi tusingeleiweza kuwaona..hata hivyo gari lao,
tuliliona likiwa bado limesimama pale pale.
Mara kwenye eneo la nyumba ya Kimwana kwa nyuma nikaona mtu
anaelekea kwenye dirisha, na kusimama pale dirishani, akiwa anaangalia ndani ya
chumba alipokuwa Kimwana, ni nyuma ya lile jengo.Nilipomchunguza vyema nilimgundua
kwa haraka kuwa anafanana ni mume wangu.
Sikuwa na uhakika sanakwa muda ule, alikuwa kasimama akichunguza huku na kule, kila
nilivyomwangali vyema niliona kabisa ni mume wangu, niliona ajabu, maana najua
kabisa kuwa mume wangu ni mgonjwa, kalazwa hospitaloni, sasa amekujaje pale, na
baadaye sikumuoan tena, nikahisi walipanga na huyo Kimwana, na atakuwa kaingia
ndani,na uchungu,wivu na hasira vikanizidia.
Wazo langu kwa muda ule lilikuwa ni kwamba mume wangu
ananidanganya kuwa anaumwa, kumbe anakuja hapo kukutana na hawara yake, Hasira
na chuki dhidi ya Kimwana zikazidi kunipanda, nikaichukau ile silaha kwa hasira
na kuielekeza kule alipokuwa Kimwana, …..na rafiki yangu,akawa kama anaogopa,
nikamwambia;
‘Kama unaogopa, ondoka mapema, mimi siwezi kuona huyu Malaya
anatembea na mume wangu, nimuache hivii hivi, sasa hivi nimemuona mume wangu
akiingia kwenye hilo jengo, ina maana wanakutana humo, huku mimi najua kuwa
mume wangu ni mgonjwa, ….’nikasema kwa hasira na rafiki yangu akaniambaia kuwa
sio huenda sio yeye, lakini mimi nilikuwa na uhakika kuwa ni mume wangu. Lakini
kabla hatujajiweka sawa mara tukaona watu wengine wawili , mke na mume wakielekea
kwenye hilo jengo, nje ya geti.
Yule mwanaume alikwenda moja kwa moja kule kwenye geti
wanapokuwa walinzi, na tulimuona akiongea na walinzi, na cha ajabu yule
mwanamke yeye alikwenda nyumba ya ile nyumba na kupanda kwenye ukuta kwa nyuma
ya jengo na kuingia ndani ya lile jengo,…na mwenzangu kwa wakati huo, alikuwa
anamwangali yule mwanaume aliyekuwa akiongea na walinzi na ilionyesha kama
anamfahamu,naakaniambia kwa hasira.
‘Ina maana huyu mwanamke Malaya anawapanga wanaume kwa zamu,…kamamumewako
yupo , ndani huenda anasubiri mume wako atoke na huyo mwanaume aliyepo pale
mlangoni ataingia zamu yake ikifika,….. kweli huyu ni Malaya hastahili kuishi..
hata mimi siwezi kumuona akiwachukua wanaume wa watu bila aibu, nipe hiyo
silaha maana mimi nina shabaha kuliko wewe..
‘Hapana niachie mimi maana ndiye mwenye hasira na huyu mtu….kanichukulia
mume wangu …hapana hii ni kazi yangu…wewe kaa pembeni maana hata mimi nina
shabaha…’tukawa tunaigombea ile silaha, na mara tukasikia sauti y akingora cha
polisi ikilia kwa nje, na muda huo huo tukasikia kama mtu anakuja pale
tulipokuwa, tukakimbilia kwenye chumba kingine kijificha.
‘Ni nani huyo? Nikauliza
‘Sijui, …’mwenzagu akasema.
‘Mbona umeiacha ile silaha pale, mtu anaweza akaiona na
kuichukua..’nikamwambia mwenzangu.
‘Pale nilipoificha sio rahisi kuoenekana, lakini nenda
kaichukue wewe…’akaniambai mwenzangu, akionyesha uwoga,….nikawa na wasiwasi
sana, na kwa muda huo nje kile king’ora cha polsi kilikuwa kikikaribia sana
maeneo tuliyokuwa na ikabidi tujifiche , tukawa na mashaka,…tulijificha pale
kwa muda,hadi tulipohakikisha kwua hicho king’ora kimepita, na hakuna shaka
tena.
Mara tukasikia sauti kama ya yowe…mara moja, kamaa `aah,
nakufa….’ Likitokea kwa nje, na nahisi kama lilitokea kule kwenye nyumba ya
Kimwana….na nahisi kama niliskia sauti ya kitu kama kuvunjika kwa kituhivi, …mimi
nina ufahamu sana na mlio wa bunduki yetu,…. moja kwa moja nilihisi ni sauti ya
silaha iliyopigwa ,ambayo ina kiwambo,kuna mlio fulani kama umeshaitumia sana
unaweza kuujua, sio mkali sana, lakini kuna mlio wake,,nahisi kmaniliusikia, na
hapo nikawa na wasiwasi, kuwa huenda kuna mtu kaitumai silaha yetu,…
Nikatoka pale tulipokuwa na kunyemelea kule kwenye chumba ambapo
tulikuwepo kabla, na ambapo ndipo kwenye silaha,…nikafiuka pale ambapo
nilimuona rafiki yangu akiificha, nikapatwa na mshituko wa ajabu,….sikuamini
macho yangu,nikamuita mwenzangu, …
‘Silaha mbona siioni pale ulipoiacha una uhakika hukuiweka sehemu
nyingine??’nikamuuliza
‘Usinitanie, silaha niliweka pale pale, umeangalia vyema
kwenye ile mifuko ya cementi iliyotumika…,maana sio rahisii mtu kuioana umeangali vyema, ?’
akaniulzia mwenzagu bado akiwa na waasiwasi akiw abado kajificha,nalionekana
wazi anaogopa kutoka pale alipojificha,
na baaadaye akatoka na wote tulikwenda pale
tulipoiweka ile silaha, na kweli hatukuikuta…maana mifuko ilikuwa imeondolea
kuonyesha kabisa kuna mtu kaichukua...’
‘Mna uhakika kweli wakati mnakimbia mliiweka hpo mlipokuwa
mnasema, huenda…..?’akauliza wakili mwanadada.
‘Nina uhakika huo, hatukuondoka nayo wakati tunakimbia,,
silaha hiyo kwa wakati huo alikuwa kaishika mwenzangu, na wakati
tunakimbia,nilimuona kabia akiisokomeza ndani ya mifuko ya cementi iliyokuwa
imepagwa humo,…kulikuwa na mifuko ilitumika, ikaachwa hapo,ilikuwa mingi…. na
tuliporidi tulitafuata kila sehemu yote haikuwepo..tukachanganyikiwa na ukumbuke
nilisikia kabisa sauti kama ,mlio ambao naujua kabisa ni mlio wa ile silaha
inapopigwa ikiwa imewekwa kiwambo cha kuzuia sauti, kuna sauti ndogo unaisikia.
‘Ina maana unahisi ilitumiwa wakati mumejificha…?’akaulizwa
‘Nilihisi hivyo,lakini sikuwa na uhakika, maana silaha
haikuwepo, ….lakini hata hivyo, kuanakitu kingine kilizihirsiha kuwa
imeshatumiwa,….’akasema
‘Kitu gani?’akaulizwa
‘Harufu ….harufu kama ya baruti, huwa silaha ikitumika kuna
ule moshi wake, unanuka ….niliusikia, na hata mwenzngu aliuhisi, tukawa
tumeduwaa, na mara.. tukasikia nyingi upande ule wa nyumba ya Kimwana,
tukaangalia, na kule tuliona yule mwanamke aliyekuwa akipanda ukuta, akiwa
kainama na pale chini kuna mtu kalala…
‘Unaona kule, inaonyesha Kimwana kalala chini,isije ikawa, kuna
mtu kaitumia silaha yetu, na kumuua Kimwana….’nikasema nikiwa na mashaka
nauwoga mwingi
‘Haiwezekani, ni nani mwepesi kiasi hicho na alijuje kuwa
tupo hapa, na akajua kuwa tutakimbia akaichukua
ile silaha na
kuitumia,haiwezekani,…’akasema mwenzangu.
‘Sasa hapa sio salama tena, lakini siwezi kuodno kabla ya
kuipata hiyo silaha, ni silaha ya mume wangu na inajulika kuwa yeye ndiye
anaimiliki, lazima tutafute kwanza….’nikasema.
‘Muda huo haupo,kama kuna mauaji , na polisi wanakuja, huoni
kwamba tutakuwa hatiani,na mfano kama kweli Kimwna kauwawa, na polisi wakatuona
tupo hapa, tutasema nini,tuasema tulikuwa tunafanya nini huku, hebu twende
zetu, tuondoke hapa haraka…’aliniambia
mwenzangu….’akasema mke wa wakili mkuu.
Wakili mwanadada akageuka na kumwangalia rafiki wa mke wa
wakili mkuu,halafu akageuka kwa hakimu na kusema;
‘Muheshimiwa hakimu, naomba nimsimamishe rafiki wa mke wa
wakili mkuu, aendeleze sehemu hii, ni shemu muhimu sana tunahitaji kuyasikia maelezo ya pande zote mbili, na kama kuna kitu mwenzake kasahau
tupate kukisikia’
Hakimu akasema ni sawa lakini mke wa wakili mkuu arudi kwanza
kukaa, na kama atahitajika tena ataitwa. Mke wa wakili akarudi kukaa na
walipisha na mwenzake, wakakumbatiana kidogo na kuachana,
Rafiki wa mke wa wakili mkuu akaelekea pale mbele na kwenda
kukaa kwenye kile kiti kilichoweka pale mbele, alionyesha uso usio na furaha,
nikadhania kuwa labda huenda ni kwa vile niliongea naye nab ado alikuwa na
hasira na mimi…..au ni kutokana na hayo maelezo aliyotoa rafiki yake, huenda hayakumfurahisha,
au kuna sababu nyingine anayojua yeye mwenyewe….nilimwangalia akiwa katulia
pale mbele akisubiri kuulizwa swali;
‘Kama ulivyomsikia mwenzako yeye anasema wewe ndiye
uliyekuwa na hiyo silaha,kabla haijatoweka,je kwa muda wote ulikuwa umevaa
soksi mkononi?’ akaulizwa.
‘Ndio,sikuwahi kuzivua hadi niliporudi nyumbani kwa rafiki
yangu, yaani mke wa wakili mkuu….’akasema.
‘Wakati mpo pale uliwahi kumuona mtu yoyote …?’ akaulizwa
‘Kwa pale kwenye jengo, sikuwhi kumuona mtu, ili tulisikia
sauti za watu,wakipanda, kuja juu, na hata baadaye tulipokuwa tunaitafuta ile
silaha, tulisikia sauti za nyayo za watu,wakishuka au kupanda juu,lakini
hatukuwahi kuwaona.
‘Hamkujaribu kuangalai kuwa ni watu gani?’ akaulizwa
‘Kwa hali tuliyo nayo, hatukuwahi,maana mawazo yetu yote
yalikuwa kwenye kutafuta hiyo silaha,na hata tulipohisi huenda Kimwana kauliwa,
hatukuwa na mawao ya kuangalia zaidi, na nilipomshauri mwenzagu kuwa tukimbie,
tulitoka hapo haraka, nakukimbilia pale tulipoweka gari letu.
‘Je mlipofikakwenye gari, mlilikuta kamalilivyo, na hapakuwa
na gari jingine, au pikipiki?’akaulizwa.
‘Tulilikuta kama lilivyo, ..nakumbuka vyema ,kulikuwa na
alamaza michoro ya kuonyesha kuwa kulikua napikipiki iliyokuwa imepita
hapo,….maana kulikuwa na mchanga, na kitu kikipita kinaacha alama…’akasema
‘Una uhakika alama hizo hazikuwepo kabla?’akaulizwa.
‘Hazikuwepo kabla, nina uhakika huo, maana tulipoteremka
kwenye gari, nilimwambia mwenzagu tuhakikishe kuwa tunaliacha mahali ambapo
hata mtu akilisogelea tunaweza kujua,kwahiyo tuliangalai sehemu zote kwa
makini….nina uhakika kabisa alama hizo hazikuwepo kabla.
‘Swali hili ni muhimu sana, maana katika maelezo yako
sikusikia ukimuelezea huyo aliyekuwa akikusadia kukupa taarifa, na kwa maelezo
ya mwenzako alisema wewe ulimwambi kuwa kuna mtu anawasaidia kuwapatia taarifa
ambazo ulikuwa ukimpa mwenzako,….je ni nani aliyekuwa akiwasaidia kuwapa hizo
taarifa?’akaulizwa.
‘Ni..ni nesi,…yule pale…’akasema nakumuonyeshea yule
mwanadada nesi kidole, yule nesi kwa muda huo alikuwa katulia,na aliponyoshewa
kidole akaonyesha kama kushituka. Na kusema kwa sauti ya kujihami;
‘Mimi…’
Wakili mwanadada akamwangalia huyo mwanadada kwa muda,
halafu akageuka kumwangalia huyo rafiki wa mke wakili, na kusema;
‘Kwahiyo ina maana huyu nesi, alikuwa akijua kuwa mtakwenda
huko kwa Kimwana, na pia ina maana kuwa yeye alijua yote ambayo mlikuwa mkiyafanya?’
akaulizwa.
‘Ndio kwasababu yeye ndiye aliyekuwa akinipa taarifa na
mipango yetu, yeye ndiye aliyekuwa akinisaidi
katika uchunguzi wa kujua wapi alipo Kimwana, na kilaninalotaka
kulifanya nilikuwa namwambia yeye, na yeye alikuwa akinishauri nifanye nini kwa
wakati gani.
Na kipindi
nilipomwambia lengo letu , alifurahi sana, na akasema yupo tayari kutusaidia
maana hata yeye ana hasira na huyu Kimwana,….na akasema yeye atakachofanya cha
kutusaidia ni kuhakikisha anamtafuta huyo
Kimwana,na kujuwa wapi alipo, kwani
kwa tetesi za watu wengi, ilijulikana kuwa hayupo hapa jijini, lakini yeye
alisema lazima atakuwepo humu jijini, lakini anajificha tu,….’akasema
nakutulia, na alipomuona wakili mwanadada hamuulizi swali akasema’
‘Na kweli alitusaidia sana maana sio kujua tu wapi Kimwana
alipo, lakini pia alichunguza na kugundua ni muda gani Kimwana anakuwepo hapo kwenye
jengo lake. ...’akasema huyo rafiki wa wakili mkuu. Na mimi nikajaribu
kumwangalia yule nesi ambaye alionekana kama kukerwa na yale maelezo maana kuna
muda alikuwa akipanua mdomo kutaka kubisha,lakini hakuweza kutoa sauti.
Wakili mwanadada akamgeukiwa yule Nesi akamwangalia, na yule
nesi naye akamwangali huyo wakili mwanadada kwa macho ya kujifanya haogopi
kuangaliwa na yupo tayari kwa lolote, na baadaye wakili mwanadada akageuka na
kumwanglia hakimu na kusema;
‘Ndugu Muheshimiwa, naomba sasa tumsimamishe huyo nesi,
tusikie upande wake, kama unavyoona yeye anahusika….,ukikumbuka kuwa yeye ndiye
aliyekuwa na wakili mkuu hospitalini, na yeye alijua kuwa wakili mkuu katoka
hospitalini, na kwenda huko kwa Kimwana, na pia yeye alijua kuwa hawa akina
dada wawili watakwenda huko kwa Kimwana,…na pia yeye ni mpelelezi wa Sokoti,
….kwahiyo yeye ni kiungo mzuri wa matukio haya yote.
Hakimu akamwangalia nesi kwa muda halafu akasema;
‘Sawa,..haya Nesi tunakuomba upite mbele…ni zamu yako,
tunataka kuskia maelezo yako’
NB Je huyu nesi atakuwa na nini cha zaidi, ukumbuke kuwa
yeye aliachwa hospitalini na wakili mkuu…sasa ilikuwaje? Na je wewe unahisi ni
nani muuaji?
WAZO LA LEO:
Mnapoishi zaidi ya mmoja, ni vyema tukajenga tabia ya kuhurumiana,kujaliana na
kuoneana huruma. Katika nyumba nyingi hasa za wapangaji, au kwenye mjumuiko wa
watu, kuna baadhi ya watu wanafungulia redio au runinga zao, au simu zao kwa
sauti kubwa, kiasi kwamba inakuwa kero kwa wengine. Huu sio uuwangana.
Tujue kuwa sote hatupo sawa, kuna wengine wagonjwa ,
hawapendi sauti kubwa.Kuna watoto wadogo wamelala, kuna wengine wanahitaji
kutuliza vichwa vyao hawapendi sauti kubwa sana,yote hayo tujaribu kuyafikiria,
kwani ni vyema ukampenda jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Lete ,mambo mkuu, naumia kwa kusubiri!
Post a Comment