‘Ndugu Muheshimiwa Hakimu, kama nilivyoelezea awali kuwa kuna
baadhi yetu hapa, nimesikia kuwa wanataak kukiukwa yale masharti ya kusema ukweli wote, kwasababu moja au
nyingine wameamua hivyo, au wameshauriwa hivyo, na hii itatufanya tupoteze muda
mwingie kuulizana maswali, lakini nakuhakikishia Muheshimiwa hakimu kuwa ukweli
wote utajulikana kwa kila mmoja wetu.
Niasema hili …kama kuwakumbusha kuwa kila kitu
tunakifahamu….tunao ushahidi w akutosha, kwahiyo nawakumbusha tena ahadi yenu…..’akasema
wakili mwanadada, na kabla hajamaliza yule mwanadada aliyeitwa kutoa
maelezo yake akasema kwa hasira.
‘Kama unajua ukweli wote, na una ushahidi , kwanini
unatupotezea muda wetu, kwanini usiusema huo kweli tukamaliza mambo, kwanini…’akasema
kwa hasira yule mwanadada na hakimu akamkatiza kwa kusema.
‘Nesi, unachotakiwa ni kuongea ukweli na utaongea pale
utakaporuhusiwa kufanya hivyo, huyo hapo ndiye anayeendesha hili jopo hapa,
mimi ni msimamizi na msikilizaji tu,kama hutafuata maelekezo yake, utakuwa unafanya
makosa….ujue upo wapi hapa….!’akasema muheshimiwa hakimu.
‘Muheshimiwa hakimi samahani sana kwa kufanya hivyo, ila ni
yeye kuanza kuleta vitisho, yeye alishatuambai kuwa kila mmoja azungumze ukweli
na tukakubali, sasa ana wasiwasi gani na mimi kuwa sitasema ukweli….kwanini
aanze kuonge hilo niliposimamishwa mimi, ina maana hana uhakika na mimi
kamanitaongea ukweli, …’akasema na kutulia.....
‘Sawa mimi nilikuwa nasisitizia tu,….tutaona kauli yako kama
ina ukweli au vipi, kwa kuanza hebu
tuambie, wewe ni nesi , je kuna kazi gani nyingine unayoijua zaidi ya unesi, na
ingelikuwa vyema ukatuambai ulijifunzia wapi hiyo kai nyingine kama ipo, na
kwanini ulijifunzahiyo kazi nyingine,na kwanini ukachagua unesi badala ya hiyo
kazi nyingine,….’akatulia huku bado akitaka kuuliza maswali mengo kwa pamoja.
‘Sawa muheshimiwa maana naona una usongo na mimi,unaniuliza
maswali mengi kwa mkupuo kama nina ugomvi na wewe….’akamwanglai wakili
mwanadada kwa dharau,na wakili mwanadada akamwangalia bila kusema kitu huku
kamkazia macho….na alipoona wakili mwanadada anamwangalia hasema kitu,
akamwangalia hakimu halafu akaanza kuongea kwa sauti ya chini;
‘Kwa kuanzia tu,mimi ni nesi, na kama binadamu wengine kuwa
wanajaribu hili na lile katika maisha yao, maana katika maisha yetu sisi
Waafrika hatuna dira , kuwa kwa vile nina kipaji hiki nitaweza kufanya kazi
hii, inakuja tu, umemaliza shule, na umeingia kwenye Nyanja hii unaifutilia tu,
hata kama huna kipaji nacho, baadaye unaweza ukajibadili mbele kwa mbele….’akatulia.
‘Nilipomaliza shule kidato cha sita, nilikuwa na hamu sana
ya kuwa askari, na hasa uaskari kanzu yaani askari katika idara ya upepelezi,
nikaomba, na kweli nikakubaliwa,
nikaingia jeshini kwanza, kama kawaida, nikamaliza mafunzo ya awali, lakini
sikupata nafasi niliyoitaka ya uaskari kanzu, nikaingizwa kwenye uaskari wa usalama
yaani polisi wa kawaida tu, lakini sikuchaguliwa kule niliko kutaka, na hili
likanikwanza sana….nikaona nimekwenda sehemu nisiyoitaka, ila hali ya kupokea
amri,sikuipenda,…hata hivyo nikavumilia.
‘Nikiwa huko nikaomba nikasomee udaktari, nikaanzia kusomea
unesi, ili baadaye niunganishe na kusomea udakitari,….maana nilikuwa napendelea
hilo pia, kwasababau nilipoona mjomba nii dakitari na mara nyingi nilikuwa
nasikia yupo nje, na mimi nilitaka sana niende nje. Lakini hayo hayakuwa rahisi
kihivyo, nikawa nahaha huku na kule,…nikajiona sina bahati hiyo. Na ndipo nikakutana na na huyu mnayemuita
wakili mkuu. Tukapendana sana,…..’akatulia na kumwanglia wakili mkuu.
‘Akanishauri kuwa yeye kwa vile anakwenda kusoma nje na mimi
sina bahati hiyo, basi nitulia nyumbani, yeye hapendi mimi nifanye kazi hasa ya
uaskari…aliniomba niache hiyo kazi,akirudi atanio…ukumbuke kuwa kazi ya uaskari
bado nilikuwa nayo,lakini nilikuwa mtegaji mkubwa, kwasababu nilitaka niwe
askari kaznzu, sio askari wa kawaida, lakini hata hivyo, nikawa ndani kwa ndani
naijifunza upelelezi, kupitia kwa rafiki yangu mmoja.
‘Wakuu pale wakaniona nina hamu sana na kazi hiyo,
wakaniingiza kwenye hicho kitengo kwa kazi maalumu, na hapo nikaanza kujifunza mabo
mengi kuhusu upelelezi, na hayo ni mambo ya ndani siwezi kuyasema hapa, …..
Nikawa nawasiliana na huyu mkuu, na akawa ananisisistiza
kuwa yupo na nia yake ile ile lakini kwa masharti kuwa niache kazi,yeye hataki
mke askari, na kwa vile nilikuwa nampenda,nikaamua kuacha kazi, na nikawa
najishisha na kazi ya unesi, ingwaje hakuwa na maslahi sana….
Mara nikasikia kuwa huyu mkuu kamaliz amsomo, lakini kwa
kipindi hiki cha mwisho cha kumaliza masomo yake tukawa hatuna mawasilinao
naye, alikuwa kakata kabisa yale mawasiliano tuliyokuwa nayo mwanzoni,nikajua
kuna jambo, nikafuatilia mpaka nikasikia kuwa mwenzangu huyu yupo katika hatua
za mwisho za kumuoa mmoja wa ndugu wa jirani.
Niliumia sana, nikatafuta mwanya mpaka nikawasiliana naye,
naye akaendelea kunidanganya kuwa hayo sio kweli, ila alibanwa na matatizo
yake, ndio maana alikuwa hawasiliani na mimi, msimamo wake upo pale pale…kuwa
akimaliza elimu yake , tunafunga ndoa, na kipindi hicho nilishahamia huko
Kenya,na kuishi na familia yetu iliyopo huko,….na baadaye ndio wakaanzisha hiyo
shule na mimi nikajiunga na shule hiyo ya mjomba.
Kweli ilikuwa ndiyo faraja yangu, maana hayo niliyokuwa
nikifunza humo yalinijenga sana kiakili, na hapo nikajua uzaifu wa kibinadamu
katika hisia na nikichanganya yale ninayojua ya kiuaskari, nikajikuta nina
hazina kubwa sana kichwani.
‘Unasemaulijiunga katika shule ya mjomba na wakati huo
ulikuwa umeshaingia uaskari,kwahiyo mambo ya silaha, na shabaha kwako haikuwa
kitu kigeni?’ akaulizwa.
‘Haikuwa kitu kigeni, na sikuwa nashiriki sana, na kaam
nikishiriki, nakuwa nipo peke yangu, maana sikutaka watu wanijue sana kuwa mimi
nimepitia jeshini….mambo ya shabaha kwangu nikitu kidogo sana,…..’akasema.
‘Una uwezo gani katika kulenga shabaha…?’ akaulizwa.
‘Kama nilivyokuambia mamboya kulenga shabaha ni kitu kidogo
sana, huo kwetu ni kama mxhezo wa kitoto, nilivyowachunguza wote mle hakuna
ambaye angliweza kunifikia, hata kama tungeliwekwa kwenye mashindano, kwahiyo
sikutaka kuingie kwenye mashindano yao waliyokuwa wakiyaweka mara kwa mara ya
kushindana shabaha…’akasema.
Nikapata safari ya ghafla ya kwenda huko kwetu kijijini,
kulikuwa na bibi mgonjwa, nikapewa kazi ya kumhudumia bibi akiwa kalazwa, na
kumbe muda huo ndipo wenzangu walipanga kuoana, nakiri kuwa kama ningelikuwepo kwenye
hiyo harusi isingelifungwa, vumbi lingetimuka, na bahati yao walipooana
wakahamia huko Dar, ambapo ndipo mume
wake anapofanyia kazi….
Hata hivyo niliapa moyoni kulipiza kisasi, ..kwanini mtu
anidanganye, na hata kunifanay niache kazi yangu, na aheri angeliambia mapema,
lakini alinificha kiasi kwamba sijuia kabisa kuwa huyo ndugu wa karibu ni
nani,…..’akatulia akiomyesha hisia za huzuni.
‘Nilikuja kugundua kwua huyu ndugu wa karibu ni yule hasimu
wangu toka utotoni, ….huyu ndugu wangu wa karibu, yangu utotoni hatuivani,maana
kila akiona nina kitu, ataninyang’anya,na kusnisingizia uongo, kwahiyo sikuwa
napatana naye , ila pacha mwenzake kidogo tulikuwa hatugombani, na hali hiyo
ilibakai hadi tulipokuwa wasichana.
‘Hebu tuambie hapo mlikuwa mnakutana vipi wakati wao
walikuwa wakiishi Kenya, na wewe ulikuwa unaishi huko kijijini kwenu Tanzania…?’
akaulizwa.
‘Kijijini kwetu Tanzania nilikuwa nikienda kwa msimu,lakini
maisha yetu mengi yalikuwa ni Kenya, hawa mapacha walipoletwa kuishi Kenya mimi
niliwapokea, kwasababu kiumri nawapita kidogo, na mimi nilikuwa nikipenda watoto,
basi licha ya kuwa mimi bado mtoto, lakini niliwaona wao ni watoto zaidi,
nikakua nao kwa karibu sana, kama dada yao…..
Tatizo, au mgongano ulikuja baadaye, hasa waliporejeshwa huko
Ulaya walipokuja tena wakiwa wakubwa , maana walikuwa wakija mara kwa mara, sas
ile nyodo ya kuishi Ulaya, ikawa inanikera, kwanini wenzangu wao wanaishi
Ulaya, na kila hatua wivu ukawa unanikera,.. hadi tulipofika ukubwani, moyoni
kwangu nilikuwa sina amani…kwanini kwanini zilikuwa nyingi kwangu,…
‘Kazi niliyokuwa nikifanya ya unesi kwenye hospitali moja,
huko Kenya. Ikaleta migogoro, nikaona nikajaribu bahat yangu Tanzania, na
wazazi wangu wakawasiliana na Mjomba, mjomba akaniunganishia kwa watu
anaowajua, na kwa vile mke wa wakili mkuu yupo huku akaambiwa kuwa ninakuja huko
kwahiyo nitakuwa ninaishi kwake.
‘Nilikuwa sina jinsi maana kuishi nyumba moja na mpnezi wa
zamani ,mpenzi aliniyenihini, ilikuwa ni kazi kubwa sana. Na sikukaa kwao muda
mrefu nikawa nimetafuta chumba sshemu nyingine, nikawa nafika kuwasalamia tu,….
‘Ina maana ulipofika hapo hukupata muda wa kuongea na rafiki
yako huyo wa zamani?’ akaulizwa.
‘Niliongea naye, huyu jamaa msikieni tu, ni muongo namba
moja, nashangaa kwa nini anafanay kazi ya uwakili, au kwa vile aliniona mimi ni
mjinga sijui, maana nilipokuja kwako, muda mwingi tulikuwa
tunakutana,….siunajau tena mkewe anakuwa hospitalini.basi aankuja
kunibemebeleza kuwa nisahau hayo yaliyotokea, kwani ilikuwa ni bahati mbaya,
yeye bado ananipenda…
‘Kwahiyo mkawa wapenzi wa siri….?’
‘Mimi kwangu sikuona kuwa ni wapenzi wa siri, mimi ndiye
mpenzi wake wa asili, ..na ukichanganay na uwongo wake, nikawa anye mara kwa
mara, na hata nilipohamia kweney chumba changu akawa anakuja huko, nilijaribu
kumzuia, lakini jamaa hakukubali, na akaja kuniambia kuwa hawapatani na
mkewe,kwahiyo niwe nampa kampani.
‘Hukuona kuwa hilo ni kosa, maana huyo ni mume wa mtu , tena
mume wa ndugiu wako wa karibu, halafu manafnya mapenzi ya siri,…..?’akaulizwa.
‘Kwani mimi nilimuita,…. Sijawahi kumuita, hata mara moja,
aseme yeye mwenyewe, ukweli wake kama niliwahi kumuita aje kwangu, yeye mwenyewe
alikuwa akijileta,….kila akipigana na mkewe anakuja kwangu, kama kiota cha
kumfariji,….kuna siku anakuja na majeraha, mimi ndiye nahangaika kumtibia ili
asije akaadhirika huko kazini kwake, na kuna wakati mwingine anakuja kalewa
hajitambui, mimi nafanya kazi ya ziada.Nilifanya hivyo tu kwasababau ni mtu
ninayemepnda, viunginevyo,….
‘Je kwanini hukumwambia mkewe?’ akaulizwa.
‘Kwakeli ilifikia hatua nilitaka kufanya hivyo, nilitaka nimwambie
mkewe kama kamshindwa basi amrudishe kwa mwenyewe, …., nilichofanya ni
kumkataza huyu mwanaume asike kwangu, na alipokuja nikawa sifungu mlango, kumbe
kufanya hivyo ndio niliharibu, nikamshau mbaya wangu, kuwa alikuwa pembeni kama
fisi akiutafuta huo mwanya, kwani jamaa huyu, kwanza aliaanzisha urafiki na
machangudoa, na ndipo akakutana na huyo Kimwana,….
Kwakeli nilijuta kwanini nililifanya hivyo, ..kumfungia nje,
maana hata baaada ya kumbembeleza kuwa nilikosa kufanya hivyo, lakini
hakunijali tena, ….akawa anajirusha na huyo Kimwana.
‘Wewe Kimwana ulimjuanaje?’
‘Kimwana nilimjua hata kabla ….kuna siku alikuja kwangu
akanikuta nipo na huyo jamaa, wakili mkuu, na alivyomwangalia kwa lile jicho nikagundua
kuwa huyu dada keshampenda huyo jamaa, na jamaa yangu kwa vile ni kiwembe,
akavutika..nilijua hapo hapo, lakini kwa muda ule, sikujali sana, maana mimi
huyo sio mume wangu na yeye pia sio mume
wake, chuki ya nini, nakumbuka alikuja hata kuniimbia huo wimbo siku nilipokwenda
kumkanya, kuwa anachofanya sio sahihi….
‘Walipozoeana sana,nikaona lazima nifananye jambo, ndipo
nikakutana na Sokoti.Sokoti, alikuwa rafiki yangu wa kazi za hapa na pale maana
unajua tena kazi ya unesi unalipwa pesa kidogo, na nilikuwa nahitaji pesa, za
kulipia kodi na maisha yangu niliyoyazoea.
‘Kazi gani za hapa na pale…?’ akaulizwa.
‘Mimi kwa siri,bado nilikuwa nafanya akzi za upelelezi wa
kujitegemea, kama kuna mtu anataka nichunguze jambo , ananipa hiyo kazi
namfanyia, Napata malipo yangu,…ni kazi nzuri, ila ni yamsimu , na kazi nyingi
nilikuwa nikipata kutoka kwa huyo Sokoti.
‘Yeye alikuwa akikupa akzi gani?.
‘Mara nyingi zilikuwa kazi za wanandoa,…ingawaje nafanya
akzi yoyote inahitaji upepelezi, lakini kutoka kwa huyu jamaa Sokoti kazi zake
nyingi zilihusiana na maswala ya ndoa….
‘Kwahiyo alipokupa kazi ya kumchunguza mumewakili mkuuu
ilikuwaje,maana unamjau vyema na wewe ni mmoja wa mpenzi wake wa siri…
‘Tuliongea hilo na Sokoti, lakini sikumwambia kuwa mimi ni
mmoja wa wapenzi wa mume wa huyo mke wa siri, akasema ninachotakiwa nikumchunguza
zaidi huyu mwanaume, kuna mengi
tunahitaji kutoka kwake, ….’
‘Mengi kama yapi?’.
‘Mengi kama hayo, ya kuhakikisha kuwa tuna muweka mkononi,…kwasababu
yupo kwenye ngazi za kisheria, tukimweka mikononi tutamvunja nguvu, na akaja
kuniambia kuhusu kazi aliyopewa na mke wa wakili mkuu, na mimi nikaambiwa kazi
yangu ni kupata habari zote, za wateja wetu na wahasimu wake, kwahiyo kwenye
hilo kundi nikawa mkuu wa upelelezi, …na kazi hiyo ikawa ni kazi iliyoweza
kuniingizia pesa ambazo sikutarajia, na pia ndipo nikapata mwanya wa kulipiza
kisasi kwa mhasimu wangu,mtu aliyenisaliti,…
‘Nani uliyweza kulipiza kisasi kwake, mke wa wakili mkuu, au
wakili ,mkuu mwenyewe, au Kimwana?’ akaulizwa.
‘Kwa mke wa wakili mkuu, sikuwa na kisasi anye sana, kwani
nilikuwa nahitaji nini tena kwake,kama ni mumewe, kwake ilikuwa ni jina tu ,
`mume’ na nikiwa na shida naye anajileta mwenyewe,…mumewe ndiye nilikuwa na
kisasi naye, kwasababu ndiye aliyenidanganya, kanidanganya akaoa mke mwingine na sasa kaanzisha mahusiano na
Kimwana,…kwahiyo nilikuwa na kisasi naye, na …..’hapo akatulia.
‘Na nani mwingine uliyekuwa na kisasi naye…?’ akaulizwa.
‘Off course, ni Kimwana,
yeye alikuwa kanichefua hasa kutokana na kauli yake ambayo alikuwa
akinibwatukia,kila ninapokutana naye,..na cha ajabu yeye hakuninyang’anya tu
huyo mke wa mtu, lakini hata nilipimpata mwingine na mwingine,…naye pia alikuwa
akimtaka,….na aliyeniuma sana ni jamaa
mmoja ambaye nilimpenda sana, licha ya kuwa yeye alikuwa hajui, ….nikawa na
mpango nimpate hata ikibidi anioe ili nitulia…
Jamaa huyu nilipomuona tu mara ya kwanza, nilivutiwa naye
sana,nikajaribu kila njia kumpata, lakini haikuwa rahisi na mwenzangu alipogundua
tu, akamuwahi, hata kabla sijapaat muda wa kuongea naye, halafu akaja kunitangazia kuwa huyu
niliyekuwa nikimtaka keshampata
yeyemiminilie tu, kwasababu yeye ni mrembo,na anajua kukipata kila anachokitaka
mimi kwake yeye ni mtoto mdogo sana katika maswala ya kimapenzi, nikaona sasa
huyu ananitafuta ubaya, …kwanini ananitafuta kiasi hicho, hanijui mimi ehe…ngoja,
..
‘Je huyo jamaa uliwahi kuongea naye, kuwa unampenda na yeye
akakubali hivyo…?’ akaulizwa.
‘Niliongea naye akija kutibiwa, lakini naona hakuhisi kuwa
nimemtamanai, na nilijaribu kujibaraguza kwake, lakini nilimuona yupo mbali
kimawazo, ….nikawa natafuta njia ya kimshawishi, …lakini sikuwa namfahamu sana,
nilichofanya ni kumwambia Kimwana, kuwa kuna mvulanammoja nimempenda sijui kama
anamfahamu,
‘Kwahiyo ina maana kwa namna moja,mlikuwa marafiki na
Kimwana?’
‘Kimwana na mimi tulikuwa marafiki wa hivi hivi, kukutana na
kuongea, tuseme mwanzoni alikuwa rafiki yangu, licha ya haya yote, na watu
wengi wanajua hivyo, kwahiyo wakati mwingine tunakutana tunaongea, na
kuhadithiana, na kuanza kutambiana nani idi kuhusu hiki au kile, …tulikuwa kama
Simba na Yanga….na huwezi amini kuna muda tunakuwa tumeshibana sana, na kuna
muda ni kama paka na chui…
Nilipomwambia kuhusu huyo mvulana,akaniambia atanisaidia kunitafutia
, na kweli haikuchukua muda akaja kuniambia keshamjua kuwa ni nani,..’
‘Sasa niambie wapi anaishi, na je ana mke?’ nikamuuliza.
‘Wewe unajali nini, kama ana mke, ni mkewe, yeye ni yeye,
kwani unamtaka mkewe au yeye, kama huwezi hiyo kazi niachie mimi….’akasema.
‘Usinione mimi wa kuja nimeshajua kuwa umemtamani, mimi kazi
ya kumchunguza kuwa yeye ni nani na anaishi wapi sishindwi kuifanya, ila wakati
mwingine nalinda heshima yangu, na kwa vile umeshanichukulia huyu jamaa
mwingine, nataka ujue kuwa huyo ndiye atachukua nafasi yake, kwahiyo
tusiingiliane,…..’nikamwambia.
‘Yeye siku hiyo hatukubishana sana na walahakuniambia kitu
zaidi, ila nilipokutana naye siku nyingine, akaniambia kuwa huyo mwanaume
keshaenda kijijini kwao na keshaoa,…ila yeye atahakikisha kuwa anampata kwa
hali yoyote ile, hata kama keshaoa, na
wote wawili anawajua , anamjua mke na mume vyema kuliko wanavyojijua wao…ooh,nikavunjika
nguvu,sikujua kuwa huyo mwanaume keshaoa, na halafu Kimwana anatarajia kuivunja
hiyo ndoa.
‘Kwahiyo wewe ulikuwa hujui kuwa bosi wako Sokoti, kafanya
mpango na Kimwana kwa ajili ya kuipata nyumba?’akaulizwa.
‘Hilo nilikuja kuambiwa baadaye sana, na mpango wa huo wa
nyumba ulikuwa wa kikundi kizima, tulitakiwa tuufanyie kazi, lakini mwenzetu
alipofanikiwa akatugeuka,…..kwa kuhusu mapenzi na yeye, sikutaka tena, maaan ni
mume wa mtu, na hata niliposikia kuwa kesharudi hapa Dar, sikuwa na haja tena naye,
ila kazi niliyopewa ni hiyo ya kuhakikisha tunafanikiwa kuipata hiyi nyumba….’akasema.
‘Kwani hiyo nyumba ilikuwa na nini cha zaidi?’ akaulizwa.
‘Mpango huo wa nyumba, anaujua zaidi Sokoti, nahisi ni kwa
ajili ya kuweka mitambo yake, n anis sehemu nzuri ya biashara,…..zaidi aanjua
yeye’akasema na kutulia.
‘Kwahiyo wewe kuhusu Msomali, uliachia ngazi?’ akaulizwa.
‘Kwakweli mimi nina utaratibu wangu,msione kuwa nimemganda
sana wakili mkuu, mkazania kwua ninapenda kutembea na waume za watu, mimi
ninajiheshimu, ila ni wakili mkuu, alikuwa mpenzi wangu wa siku nyingi, …..’akasema.
‘Kama ni hivyo kwanini uendelee kuwa na uadui na Kimwana?’
akaulizwa.
‘Mimi na Kimwana tutaendelea kuwa madui mpaka mwisho,maana
yeye aliahidi mbele yangu kuwa kila mwanaume nitakaye mpata ataninyang’anay,
huwezi amini kuwa hata hiyo nyumba aliyojenga mpya, nilikuwa nimepewa mimi
mwanzoni, ikiwa inaanza kujengwa, na Kimwana akaja kuipita kinamna ambayo wala
sijui ilikuwaje,….’akasema
‘Kwa vipi?’akaulizwa.
‘Ile nyumba na eneo lake lilikuwa la tajiri mmoja, tajiri huyo aalikuwa kutibiwa siku moja,
nikamsaidia sana, kipindi hicho, na alipopona, akahidi kuwa atakuja kunitafutia
zawadi, basi siku moja nikakutana naye, akanionyesha hiyo nyumba ikiwa katika
ujenzi wa wali kabisa, mimi kwa vilenapenda kumringia Kimwana nikaenda kumwambi
kuhusu hilo,kama rafiki yangu …’akatulia kwa muda.
‘Ilikuwa ni kosa, maana wiki haikupita, nilimuona Kimwana
akijirusha na huyo mwanaume, kwa muda huo sikujali nakajua hiyo ni tabia ya
Kimwana, kwasababuu sikuwa na mpango na huyo jamaa wa kimapenzi, nikaoana
kwangu mimi haijalishi sana.
Ukapita mwezi, nilipokwenda kuangalai ile nyumba na kiwanja,
nikakuta nyumba imeshafikia juu, na nilipouliza nikaambiwa kuwa ni kazi ya
Kimwana. Nikaenda kumuona yule tajiri, nikaambiwa yupo Ulaya, nikatafuta
mawasiliano naye, akaniambai kuwa Kimwana kamfanyia kitu kibaya sana, ndio
maana kampa yeye hiyo nyumba, ili aije akamuumbua….
‘Je kwanini mkawa katika ushindani wakati wanaume wapo
wengi, kwanini mkawa mnagombea wanaume..hamuonai kuwa hiyo ni aibu kwa
wanawake, tene warembo kama nyie na kwanini msiongee yaishe…?’ akaulizwa
‘Nilikuja kumwambia wazi wazi kuwa yeye anachezea moto,
uliofunikwa na majivu,..yeye hanijui kuwa ni mimi nani,….hutaamini mwanamke yule
alikuwa na kejeli na kiburi,alikuwa hajali, aliniambia kuwa yeye hajali kuwa
mimi ni nani, kwani hata wakuu wa usalama wanamnyenyekea sembuse mimi kijike
kisicho na hadhi..aah, nikaoan lazima bile bifu naye, …ndio hivyo tu…’alisema
huyu nesi akionyesha uso wa dharau.
‘Kwahiyo visasi na chuki ni katika ushindani wa kimapenzi
kuna jingina lazaidi hadi kufikia hatua hiyo mliyokuwa mumefikia?’ akaulizwa
‘Wewe hujawahi kuwa karibu na Kimwana…..’akasema na kutulia
‘Kwa vipi hebu tueleze wewe uliywahi kuwa karibu nay eye….’akaambiwa
‘Kauli zake, kejeri, na tabia ya kuchukulia wenzake kile
unachokipata,… ilionyesha wazi kuwa hanitakiii mema, sio waume tu,hata wa kimaendeleo,kanifanyia
mengi mabaya..kuonyesha kuwa etu haniogopi, hata pale alipoambiwakuwa katika
kazi yetu hiyo mimi ni bosi wake, yeye akasema hana bosi katikalolote lile.
Kwa tabia hiyo, tukaanza
kumuwinda…yeye alipogundua kuwa namuwinda akaniambia ama zangu ama zake,
keshajua kuwa simtakii mema,..mimi nikamwambia kajipalia mkaa, mambo bado ndio
yanaanza…., kwanza nilianza kukusanya machafu yake yote, na kila mwanaume
anayekutana naye, anaishia kuzalilika, yeye anashangaa kesho yake mapicha yapo hadharani,..na
huyu mwanaume wake anageuka kuwa adui yake. ….maana anajua kuwa Kimwana ndiye
kapangaiwe hivyo,kumbe sio…..
Nilihakikisha
hakipati hicho anachokitaka , kama alivyonifanyia mimi, na kama akikipata,
hakipati kwa raha….`skendo’ zikawa zinamuandama….na wanaume wote aliokuja kuwa
mrafiki naye, wakamuona kama nyoka… Hilo lilikuwa pia ni moja ya kazi zetu na
Sokoti, kwani Sokoti naye alishamchoka,….lakini hata hivyo, mimi mwenyewe
nilikuwa na yangu. Nikawa napata pesa nyingi
kivyangu, lakini kwa nia ya kumkomesha KImwana.
‘Mbona hapo siwaelewi,
mimi najua Kimwana alikuwa kundi moja na Sokoti, na wewe kama ulikuwa
kundi moja na Sokoti, ina maana wewe na Kimwana mlikuwa kundi moja, au sio?’
akaulizwa.
‘Mwanzoni kabisa, Kimwana alikuwa hajui kuwa tupo kundi
moja, mimi nilikuwa najua Kimwana yupo kwenye kundi, na hakujua nini
kinaendelea , maana mimi ndiye mkuu wa upepelezi, na ili jambp lifanyikelazima
nilifanyie kazi mimi,…nilikuwa nastahili hadhi yangu namalipo makubwa, lakini
hutaamini Kimwana, alikuwa yeye anadai zaidi, na alisema yeye ndiye kila kitu
kwenye kundi, na Sokoti akawa anamtizama tu…akasema huku akitabasamu kwa
dharau.
`Umesema kulikuwa na mwanaume mwingine uliyempenda, na Kimwana akakuwahi huyo mwanaume ni nani?’
Nesi akanyamaza kidogo halafu akasema kwa sauti ya nguvu, ‘Wapo
wengi, lakini ambaye nilimpenda halafua nikaambiwa kaoa huko kijijini kwao anaitwa
Msomali,…’
‘Msomali huyu huyu…?’akaulizwa.
‘Ndio huyu huyu,…huyu mnayemuona hapa mahakamani, lakini
alikuwa hajui hilo…’
‘Kwahiyo kuwindanakwenu kulikuwa na malengo gani, kunyang’anyana
au zaidi ya hapo, ….maana unasema mliambina ama zako ama zake, hii ilikuwa na
maana gani?’ akaulizwa.
‘Kwa vyovyote vile, …kunyang’anyana,kuumbuana,..kuwindanakwakila
hali….’akanyamaza
‘kwahiyo hu mpango ulijulikana katika kundi,nikiwa
namaanakuwa hata Sokoto alijua hilo?’akaulizwa.
‘Yeye alijua hilo kuwa huyo Kimwana sasa ni adui wa kundi,
na kama tukimuachia atakuja kusema kila kitu, kwahiyo nilipewa kazi ya kutafuta
njia ay kumziba mdomo,….’
‘Kumzina mdomo kwavipi?’akaulizwa.
‘Kwa vyovvyote vile, lakini cha muhimu asiweze kuongea
lolote….’akasema.
‘Hata kumuua….?’ Akaulizwa.
‘Kwani ,nini maana ya kumziba mdomo,kwa mtu kama
Kimwana,..hivi nyinyi mnafikiri mngeliweza kumziba mdomo Kimwana kirahisi,rahisi
kwa kumfanyoa vitimbwi tu …mtu ambaye aliamua kufanya maasi,kuaharibu ndoa za
watu,kuchonganisha watu, kuibia watu kiujanja,….huyu mtu mnamuonaje nyie,….mimi
sioni njia nyingine ya kumziba mdomo mtu kama huyu, ….’
‘Kwahiyo ukaamua kumuua?’akaulizwa.
‘Sio rahisi hivyo…..wakili mwanadada…jaribu tena …’Nesi akasema
na kucheka.
NB Ngoja niishie hapa maana naona kama mwisho mwisho
unakaribia, swali ni je huyu anaweza kuwa ndiye muuaji, hebu rudi nyuma kidogo,
uangalie sifa za muuaji, je anazo, kumbuka wakatu maujai yanafanyika huyu nesi aliachwa hospitalini...ua, tukumbushane maana hata mimi husahau
Kuna watu wanasema naandika kwa urefu sana wanataka kwa ufupi zaidi, je mnasemaje kuhusu hilo, niwe nafupisha ziaidi?
WAZO LA LEO:Ubaya hauna kwao, yoyote yule anaweza akawa
mbaya au mwema.
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
Salaam kaka, yaani leo ndio imenoga hasa kwa kuwa umeandika kwa urefu. Hao wanaotaka uandike kwa ufupi nafikiri hawajui riwaya maana yake ni nini. Wewe ni mwandishi wa riwaya na si mwandishi wa taarifa za habari!
Riwaya ni kazi andishi ya fasihi ambayo kwa kawaida ni ndefu zaidi kuliko hadithi fupi.
Urefu wa riwaya, maana yake ni kwamba msuko simulizi umejengeka vizuri, kuna wahusika wengi, inaenea muda mrefu, na mada zake ni nzito na pana kiasi.
Mifano mizuri ya riwaya kwa lugha ya Kiswahili ni Nagona au Mzingile, riwaya za mwandishi Euphrase Kezilahabi. (imetoka: http://sw.wikipedia.org/wiki/Riwaya)
Ole wako utuletee viduchu, hapa ni riwaya zilizoshiba!
Mambo yanazidi kukolea hapa...kazi nzuri mie naona si ndefu kutisha Tatizo ni kwamba waTz hatujafunzwa tangu utotoni kusoma vitabu...Pamoja daima!!
Nawashukuruni kwa kunipa moyo kuwa kumbe nikifanyacho nipo sahihi, hata kama wengine wamekubali kimiya kimiya sio mbaya, na kuna wengine wamenipigiasimu kuniambia kuwa nipo sahihi, yote ni heri.
Nitajitahidi kufanya lile ninaloweza, licha ya kushindwa kuchapisha vitabu, lakini ipo siku.
Tupo pamoja daima.
Post a Comment