Mwanadamu ni kiumbe mwenye huruma sana, lakini ile huruma
ikimtoka na ikatawala chuki,anaweza akageuka akawa na nafsi mbaya kuliko
unavyofikiria, hili niwaambie muelewe,….’akaendelea kuongea mwanadada wkili
tukiwa tunamsikiliza kwa makini,, akaendelea kusema;
‘Chuki iliyopandikizwa kwa sababu ya mapenzi, inakuwa haraka
kama isipozibitiwa, nasema hili nikiangalia visa ndani ya kisa hiki ambavyo matukio
yake yalitokana na mapenzi. Kusalitiana kwa mapenzi, kutokuzijua ndoa zetu, na
mmoja kati ya wanandoa kutenda kinyume na makubaliano ya ndoa.
Tumrudie mmoja wa wahusika katika kisa hiki ambaye tunaweza
kumuita binti wa docta, huyu mwanadada ambaye alitoka katika familia ya
madakitari walioijua ndoa na wakawa walimu wa kuzijenga ndoa za watu, lakini….
*******
Kwakweli huyu mwanadada licha ya kuwa alijitahidi sana kuijenga
ndoa yake, na taka kutaka kugundua nini kilichombadilisha mumewe, lakini
alijikuta kigonga ukuta, ila kimoja alichokigundua mapema, na ambacho aliona
kuna njia mbadala ya kuweza kuwasaidia, ni kuchoka kwingi kwasababu ya majukumu
ya kazi yake, lakini hata alipogundua njia mabadala,bado alijikuta akishindwa
kutokana na kikwazo cha mumewake,….
‘Mume wangu kazi hii
ya kuajiriwa naona inanichosha sana, na naona inawezekana ikawa ni moja
ya chanzo cha mimi na wewe kuwa mbali kimwazo, na hata kimwili..nimeonelewa
kuwa,…’siku moja alimwambia mume wake na kabla hajamaliza alichotaka kuongea
akakatishwa kauli yake.
‘Kwahiyo unataka kusema nini…?’ akakatishwa na mumewe, huku
akiwa kaangaliwa kwa uso wa dharau.
‘Nataka tulijadili hili kwa pamoja, ili kama inawezekana
nisiwe nafanya kazi masaa mengi, hili linawezkana mume wangu, kama
tutakubaliana,… lakini ili liwezekane, ina maana mimi mshahara utapungua…’akasema.
‘Hata ukipungua mimi linanihusu nini mimi, toka lini
nikaishi kwa kutegemea mshahara wako,…hatuna watoto, ni huyu binti yako, ambaye
hahitaji gharama…ni uamuzi wako kuamua….fanya utakalo?’ akasema kwa hasira.
‘Tatizo lako wewe hutaki kuwa karibu na mimi, kila nikjaribu
kukuweka sawa, ili tuwe pamoja, unanisukuma kwa maneno makali, unajua mimi ni
bindamu, itafika sehemu na mimi nitasema basi,liwalo na liwe…nitachoka mume
wangu…na haitasaidia kitu…..’akasema huyo binti.
‘Useme basi au usiseme basi, mimi sijali,wewe amua
unalotaka,…kwanza unanipotezea muda wangu hapa bure….’akasema na kuinuka kutaka
kuondoka.
‘Sikiliza mume wangu, wewe ni mtu mzima,….kwanini hutaki
kuniskiliza amimi hata mara moja tu, nini nimekufanyia kibaya mpaka unione
siona maana kwako,….niambie ili nijue, ili tuweze kuishi maisha ya raha kama
mume na mke……’akasema.
‘Siwezi kusikiliza utumbo, kila unachoongea hakina maana
yoyote,….kwanza wewe unataka raha gani, hebu jiulize nini hasa unataka mimi na wewe tukae tuongee, utanipa nini cha kunifurahisha, huna mtoto, umejikalia tu hapa,….raha
gani unataka wewe….’akasema na kumwangalia mkewe kwa hasira.
‘Mume wangu kuhusu swala la kupata mtoto nilshakuambia twende tukapime ili tujue nini
kinafanya tusiwe na mtoto, umelipinga hilo, na hutaki kabisa kuhangaika nalo,
…au una mipango yako, ya kuniletea watoto wa nje,…..’akasemahuyo binti wa docta.
‘Nilishakuambia mimi na mwanaume humu ndani, nini nafanya ni
juu yangu,hata nikileta watoto hapa yanakuhusu nini….wewe si huzai, acha
nikatafute watoto nje..’akasema huku akiwa keshafika mlangoni.
‘Unajuaje kuwa mimi sizai, huenda tatizo liko kwako,….mimi
ni docta,kama ningelikuwa na tatizo ningelishajua,na ningelishakuambia ….mimi sina
tatizo lolote, kama lipo tatizo huenda lipo kwako, au linaweza likahusu sote
wawili, katika kukamilika kwa swala zima la uzazi,….ndio maana nashauri twende
sote tukafanay uchunguz wa kina,….kwanini hilo liwe gumu kwako….au umeshajipima
ukajigundua kuwa una matatizo mwenyewe….’akasema huku akimwangalia.
‘Eti unasema nini wewe mwanamke…’akageuka kwa hasira,
‘Nasema hivi, kama hutaki kupimwa huenda umeshajigundua kuwa
una matatizo, ….’kabla hajamaliza jamaa alishamfikia kwa hasira akiwa kainua
mkono kutaka kupiga kofi, lakini mkewe akasogea mbali na kushika kiuno.
‘Hivi wewe unaona kupigana sio suluhisho la haya
matatizo,….au kwasababu ya mila zenu ambazo kupiga wanawake mnaona ni
ufahari,….nakuomba mara nyingine tena, kuwa sitavumulia hii hali, ….kwanza
nakushangaa wewe ni wakili , una jua nini maana ya sheria, …’akaongea na kabla
hajamaliza akaone mwenzake akiondoka, na alipofika mlangono akasema;
‘Kama unaona mimi nina matatizo, subiri,….si unaona mimi
nina matatizo, eeeh, nitaanza kukuleta watoto wan je,uje ulee, nafikiri ndio
dawa yako,….’akasema na kuondoka.
Binti Docta, alikaa kwenye kiti, akashika kichwa, akawaza,
na kuwazua, akawa anajisema akilini mwake kwa huzuni,
‘Hivi jamani ndoa inakuwaje ngumu, kwanini tushindwe
kuelewana, …hivi kuna tatizo,..hivi, mimi nina tatizo gani kwa mume wangu, sina
mvuto, sijui mapenzi…au kuna tatizo gani…mungu wangu lini na mimi nitaipaat
raha ya ndoa, nimeosa nini mimi mungu, naomba unisaidia , …naomba uisaidie ndoa
yangu,…kama kuna kosa nimelitenda naomba unionyeshe njia….’akawa anaongea huku
machozi yana mtoka.
*********
Profesa Sokoti , kama anavyojulikana, alitizama tarakilishi (komputa) yake
kwa makini, akawa anaangalia sura za mabinti mbali mbali aliowaweka humo ndani,
amekuwa na tabia ya kuweka kumbukumbu za wateja wake kwenye tarakilishi yake, na sasa alikuwa akiweka
kumbukumbu ya mteja wake wa hivi karibuni, huku akikumbuka mahojiano yake na
yeye;
‘Mume wangu nampenda sana,na nimejaribu kila njia ya kutaka
tuongee naye, ili tuweze kusaidiana, lakini imekuwa vigumu sana, kama unavyojua
kuwa mimi ni docta, na pamoja na udakitari wangu,nimezaliwa ndani ya familia
inayojua vyema maisha ya ndoa, …..ningekuwa huko ,nafikiri tatizo hili
lingeshaisha, lakini sitaki kuihusisha familia yangu kwanza…..
‘Lakini nimeshakupatia mtu ambaye alishafanya hiyo kazi, na
jana tu nimeongea naye akasema alikupa mjina yote, ya wanawake wanaoonekana
kuwa wana mahusiano ya karibu na mumeo, …unataka nini zaidi….tuwafanye kitu
mbaya…?’akauliza
‘Hapana sitaki kumfanya mtu kitu mbaya, mimi tatizo langu ni
mume wangu, hawo, nitajua nini cha kufanya baadaye,kwanza nikutane nao
mwenyewe. Kwasabbu gani, tatizo hili limekuwa kubwa sana sio kwangu tu,
nimekutana na akina mama wengi waliopo kwenye ndoa wakilalamika kuhusu swala
kama hilo ….sasa nimetuliza kichwa changu nikaona kuna haja ya kufanya
jambo….’akatulia.
‘Jambo gani..?’ akauliza.
‘Kule Kenya mama yangu ana kliniki ya kuwasaidia watu wenye
matatizo ya ndoa, sasa na mimi nataka kuanzisha kitu kama hicho hicho hapa
nchini,….lakini kinamna yangu, na malengoyangu..’akasema na kuwa kama anawaza
kuhusu hilo jambo.Na Sokoti akasema kimoyomoyo, ` na mimi nina malnego yangu
hapo hapo….tutabanana hapo hapo…’ halafu akasema;
‘Wewe unanishangaza kweli, kama mwenyewe umesema ndoa
imekushidna utawezaje kuwashauri wenzako….hebu niambie unataka tufanye nini, labda
wazo ulilonalo ni sawa na wazo langu, ila nilikuwa naogopa kukuambia,…’akasema
huyu mtaalamu.
‘Nimegundua kuwa wanaoharibu ndoa za watu ni hawo wakina
dada wanojipitisha mitaani,,...mimi nataka nianzishe kitu kama shule, ambayo
hatua ya kwanza ni kuwakuasanya hawo akina dada, na mpango wangu wa mwazo ni kuwapata
hawo akina dada wanaotemeba na mume
wangu..’akasema nakutulia.
‘Mambo si hayo,….hilo mbonakazi rahisi tu….enedelea kuleta
vitu,…maana leo wewe ndiye mtaalmu wangu,….’akasema huyo jamaa akiegemeza
kichwa kwenye kiti chake.
‘Kwanza itaonekana kama nawasaidia, lakiini baadaye,….tunawaita
hapo shuleni,…tunawafunda, huku tukiwajau undani wao,…lazima kilammoja
ajieleze, najua umeshawajua kiundani, lakini mimi kuna jinsi nataka kuwajua,
…halafu hawo hawo tutawatumia kama fimbo ya kuwachapia hawa wanume wasiotulia
kwenye ndoa zao….’akatulia na kumwangalia huyu jamaa.
‘Safi kabisa…wewe kichwa,…nakuaminia docta, sikujua kuwa
wewe jembe la nguvu, mke wa shoka…naona tukiwa pamoja, tutafaya jambo kubwa
sana, niambie ..ehe, hebu ongea, sasa umafika pale nilipopataka,…..’akasema
akiwa na shauku.
‘Usije ukawazia tamaazako, ukaweka njaambele, sitaki uhuni huo,…nakukanya
mapema, maana wewe nakujau tabia zako….sitaki kufanya ubaya, mimi sitaki kufikai
hatua ya ubaya, lengo langu lina maana ya kuwapa fundisho hawo wanaume, na pia,
kuwa karibu na hawo mabinti. Kwahivii sasa nataka unisaidie kuhusu hili, wewe
ni mtaaalmu wa saikolojia, …..au sio..?’ akasema kama anauliza na
jamaaakadaikia kwambwembwe…
‘Na wewe ni docta, ….au sio?’ akasema huku akitabasamu.
‘Nataak unielewe, usilichukulie hilijambo juu kwa juu,
nataka utaalmu wa hali ya juu, nataka tumtafute mwanasheria ambaye ataliweka
kisheria, na awe tayarai kujibu mapigo ya kisheria, na nitajitahidi kitengo cha
sheri anachofanya mume wangu nikidhibiti kinamna,unaweza hilo….?’ Akauliza.
‘Hiyo kwangu ni kazi rahisi, hao hao mabinti watatumika,
wewe utaona ….mimi sio mchezo, huwa nikipata upenyo kidogo tu, utacheka, huku
wengine wanalia,….’akasema huku akitingisha kichwa.
‘Tatizo lako, una tamaa, naomba sana usije ukaweka tamaa
mbele, utaharibu kila kitu…unaona, lengo langu ni kujenga mtandao ambao utaweza
kufanya jambo, lisiingilie sheria, na sheria ikiingiliwa tujue jinsi gani ya
kupambana nalo…kwasababu ujue mume wangu ni mwanasheria, ni mwanajeshi,…anajua
kupeleleza, akija
kugundua , utafia jela….sasa nataka asigundue lolote,….huku
anapata kichapo ….mpaka arudi kwenye msitari….
‘Unajua wewe nilishakusoma tangu awali, ulikuwa ukizunguka
zunguka, hata mimi nilikuwa na wazo kama hilo,….lakini nilikuwa naogopa,maana
mumeo ni sio mtu wamchezo. Kwahiyo kwanza kuna akina dada wengi wanahitaji hilo
somo, tunaweza tukawapata kwa wingi….kwanza tunawavuta kama njia ya kuwaboreshea
amisha yao, ili wapate ndoa,…..mwisho wa siku, wanakuwa chambo,…..hilo wazo
niachie mimi,…..hapa umefika, ila tunahitaji pesa ya kuanzia, nyingi
kidogo…’akasema.
‘Sasa hapo ndio tatizo,na mimi kwa ujumla sina pesa ya
kuanzia….lakini nipe muda…’akasema huyu mwanadada
‘Sikiliza dada yangu, pesa sio shida, , ….mmmh, …hiyo
itapatikana kwa hawo hawo wanaume uchwara, kwasababu pesa zao ndizo
zinazowavuruga….mimi hilo nitajua jinsi gani ya kulifanya,…..kwanza yupo rafiki
yangu karudi ni mitambo ya nguvu…..wewe utaona, usiwe na shaka……wewe jiweek
sawa kimwalimu, mengine niachie mimi…’akasema huyo jamaa
‘Sawa, kama umenielewa hamna shida, lakini mimi sitaki
nijulikane sana kuwa nipo kwenye kundi hilo, nitakuwa nakuja kama mtaaalmu wa
kufunda, na kwasababu nimepata mafunzo kidogo toka kwa mama,nitajua jinsi gani
ya kuongezea maarifa,…..nikija kwenye hiyo shule,nitakuwa tofauti sitaki kabisa
mtu anijue mimi,utakayelijua hilo ni mimi na wewe tu, wewe uwe msimamizi wa kila kitu….sawa?’
‘Mimi nimekuelewa kabisa, usiwena shaka…’akasema huku
akiandika kitu kwenye kumbukumbu zake.
‘Nafikiri ili twende sawa, nataka umtafute mwanadada
anayefanana na mimi, awe anashika nafasi yangu kama sipo….hilo unalionaje
….?’akasema
‘Huyo mbona yupo tu….wewe utaonavitu vyangu,…wewe utakuwa
kama kivuli….nyuma ya pazia,…mambo yanaenda kimiya kimiya…safi kabisa’akasema.
‘Haya naona wewe kila unakijua , unakielewa,….ngoja
nikiachie wewe…’akasema huku akitaka kuondoka
‘Sawa, lakini kuhusu mumeo itakuwaje, maana kweli nitafanya
hivyo, na wateja wetu, au wanafunzi wa mwanzo watakuwa hawo wanawake
wanaotembea na mumeo…lakini mumeo ni mkali wa kupeleleza, atakuja kulijua
hilo,..huoni ni bora nianzie kwake, kumuweka sawa kwanza…..?’akasema na
kukatishwa.
‘Hayo kuhusu mume wangu niachie mwenyewe, cha muhimu ni
jinsi ya kuwakusanya hawo wote wanaotembea na mume wangu, wakikubali,….na
nikakutana na wao uso kwa uso, …nitajua nini la kufanya….utaona matokea yake
baada ya miezi kazaa, ikifikia hatua ya kuwachapa viboko hawo wanaume
wasiotosheka an ndoa zao, nitakuachie wewe na….’akasema huku akiangalai nje,
‘Na wataalamu wenzangu ambao wapo, hilo lisikutie shaka,…hapo
tupo pamoja….kama utadhibiti huko kwenye usalama, shwari kabisa …na hilo ni
rahisi tu, …hawo hawo akina dada tutwatumia kuhakikisha kuwa hakuna cha usalama
au jeuri yao, watanywea wenyewe….hilo niachie.’akatikisa kichwa na yule mwanamama akamwangalia huyo jamaa kwa
mashaka, lakini akasema kimoyomoyo, nitahakikisha kuwa hafanyo baya lolote,
akasimama na kuondoka.
Alipoondoka huyu mwanadada , huyo jamaa akainua simu na
kumpigia mmoja wa rafiki zake akaongea naye kwa muda mrefu halafu, akampigia na
mwingine, na mwingine….alipohakikisha kuwa kawasiliana na watu wake maalumu,
akairudia komputa yake na kuanza kuangalia zile picha,alipofika kwa picha
mojawapo, akatabasamu, na kusema;
‘Sasa pesa nitapata, nikiwa na pesa, nitafanikiwa, ndoto
yangu, warembo wote…..hasa huyu,….’ Akawa anaangalia picha mojawapo kwenye
komputa yake….akaanza kucheka kama mtu aliyechanagnyikia, akasema;
‘Sasa mambo yanajileta yenyewe, kipindi kigumuu
kimmeshapita,…wanajileta weneywe,….na huyu ndiye mke wa kuoa,…..sijui kwanini
anapata shida…na mwanume ambaye wala hajui kuwa yupo hai….sasa hiki kidume
kisichotosheka na mke wake eti kinamtaka….nitakikata ulimilimi wake,….sijali
cha usalama wake…nikigusa pale penyewe,atatulia,….mfuko ataufungua kilaini…’akasema
na kukumbuka siku alipokuja huyu mwanadada ambaye anamtaka awe mke wake,…
*********
‘Kaka yangu mimi nimekuja hapa kwako baada ya kupata ushauri
toka kwa rafiki yangu, sikupenda sana, kuja sehemu kama hizi, ila nahisi kila
siku zinavyozidi kwenda nazidi kuchanganyikiwa, hasa nilipogundua kuwa mtu
niliyempenda keshaoa,….
‘Nilishakuambi kuwa mtu kama huyo , najua jinsi gani ya
kumweka sawa, lakini nikupe ushauri wa bure,kama keshaoa,huna haja ya
kuhangaika naye,…wewe kwanza mzuri,…wanaume wengi wanakutafuta, ….yaani mimi
mwenyewe kama ungenipenda, mbona utawaoan wanaume wengien hawana maana,…pili wewe
una kazi yako ya maana, …udakitari, kwanini ujihanganisha na mtu ambaye sasa
ana mke wake na …
‘Huo ndio ushauri wako..au ndivyo unavyowafanyia wateja wako?’
akauliza.
‘Ushauri wangu utategemea kuhusu historia yako, naomba tafadhali
usinielewe vibaya, haya ngoja nikuhoji kidogo, na uniambie kila kitu
nitakachokuuliza, bila kificho….utaona maajabu yake…na kuhakikihsia kuwa
nitakusaidia ufanikiwe katika maisha yako…’akasema.
Alimuhoji yule dada, na hatiamye akagundua kiini cha tatizo
hilo,akampa ushauri, kwamba, kwanza anatakiwa kuhudhuria hapo kwake, kwa ajili
ya `kuweka mambo sawa’ ….pili, yeye anataka atafute mbinu za kuonana na huyo
mwanaume, ili ajue jinsi gani ya kumfungulia njia, na hata ikiwezekana,
ataichafua hiyo ndoa iliyopo na hatimaye huyu mwanadada anaweza akarudi tena
kwa huyo mume…
‘Sitaki kuharibu ndoa
za watu, keshaoa, haina haja, ila ninachotaka ni kupata ushauri w ajinsi
gani nitaondokana na hayo mawazo, maana kila mara namuwaza yeye tu,….nakuwa
kama nimechanganyikiwa,….’akasema huyo mwanadada.
‘Hilo tutalimaliza ….usitie shaka,….limefika kwa mwenyewe,
mimi nitahakikisha nakusaidia wewe, na kuna jambo moja muhimu, nahitaji akina dada kama nyie
waliosoma, kuna wazo limenijia sijalifanyaikazi kwanza, nikiliweza hilo, nataka
kufungua shule au sehemu ambayo, nitakuwa antoa semina na ushauri nasaha wa
mambo hayo ya ndoa, sijaweza kuliweka sawa hilo….’akasema huku akiwaza .
‘Hilo ni wazo jema,…kama nilivyokuambia nimewahi kuhudhuria
shule kama hizo najue mengi kuhsu ndoa na mataizo yake, lakini wakati mwingine
unazidiwa maana kama wasemavyo kinyozi hajinyoi….’akasema.
‘Ni kweli,mimi kama nitafanikiwa hilo, nataka nikuombe wewe tutakuomaba
uwe nafika, unajau wewe ni mwelevu, na msomi, ukikutana na akina dada ambao
wanahitaji ushauri wa misha, itakusaidia na wewe kuyasahau machungu yako,
….kama upo tayari nitawasiliana na wewe….’akasema.
‘Kwanza tutatue tatizo langu,…hayo mengine yatafuata, mimi
napenda sana kazi ya namna hiyo, kama
kuna shule kama hiyo, nitajitolea, haina shaka, itanatajai kufunguliwa
lini?’ akauliza.
‘Hivi karibuni, nitakujulisha….’ akasema huku akiwa haamini,
maana kila anayekutana naye na kumwambia jambo hilo anakubali kiharaka sana.
Akajua sasa mambo yanajileta yenyewe.mlakini katika wateja waliowahi kufika
kwake, huyu aliweza kuiteka nafsi yake, na akaona kuna haja ya kumjua vyema,
…kwanza alitaka kumjua huyo mume wa huyu mwanadada ambaye anapendwa kihivyo...
Alitaka akimjua awe ni mmoja wa chambo chake katika mambo
anayoyakusudia, na ikiwezekana ahakikishe kuwa huyu jamaa anakuwa hohehahe kiasi kwamba
hakuna mwanamke atakayemjali tena,…kila atakalolifanya limwingiza pabaya,....na hatimaye huyu atamweka huyu mwanadada kwenye himaya yake. yake.
‘Mjini hapa, mtoto mzuri kama huyu anahangaika na lijanaume
lisilomjali,….kwanza nachafua huyu mtu,na huyu dada,nitajua jinsi ya kumhadaa,
atajileta mwenyewe…cha muhimu huyu mwanaume, nitamchanagnya kabisa, kazi
hapati, …nuksi itamuandama, kitaalamu….mpaka ajitie kitanzi……anacheza na
Profesa …..mmh,sasa pesa nje nje….
Baada ya kumalizana na huyu mwanadada, akaingia dada
mwingine….dada huyu alipoingia, alismama kwanza bila kusema neno, akamwangalia hho
la dharau, huku kakunja uso,kinamna bila kusema neno, halafu baadaye akasogea
na kukaa kwenye kiti..
‘Haya niambie umeniitia nini….
‘Kimwana unakumbuka tulipotoka….mimi najua siri zenu zote,
na kama nitawafikisha polisi mtafungwa wewena huyo kidume chako, mtafungwa kifungo
cha,maisha,…..nimekuambia achana na huyu muhuni,njoo nikuoe tuishi pamoja,……’
‘Niambie ulichoniitia, usinipotezee muda wangu….’akasema huyu
mwanadada huku akiangalia saa yake.
‘Poa mtoto,…nakuona sasa huna muda wakupoteza, sawa siku
hizi wewe matawi ya juu…sio mbaya, ila sasa kuna dili ya nguvu, kama utatulia
vyema, tutatengeneza pesa ya nguvu….na hapo ndipo utakapo niona kuwa mimi nina
akili ya ziada, hili jambo nilikuw nalo siku nyingi, lakini nilikuwa sijaliweka
kwenye kazi zangu, sasa kaja mtu wa haja, ana
pesa, ana wadhifa,…..na ni wale watu walioshikilia mpini katika
serikali….
‘Niambie nini umeniitia..
‘Wewe siunataak pesa, kwa mfano ukiwa unaingiza shilingi
milioni kadhaa kila mwezi na hizi ni lazima uzipate, na kila kazi utakayoifanya
unaweza ukaingiza milioni haya ishirini,…..
‘Wewe sasa umechanganyikiwa,kazi gani hiyo ya kuweza kupaat
pesa nyingi kiasi hicho, na utazipaat kwanani,…, sisi tumejitadi kufanya kazi
ya kufumaniwa kwa kupanga, na kudai pesa nyingi, lakini hatujawahi kupta psa
nyingi kiasi hicho,hiyo ni ndoto ya Alinacha,…….’akasema.
‘Sikiliza hii dili ni ya majembe ya nguvu, wewe mweyewe utaona….wewe
nisikilize kwanza, nitakuonyesha hatua kwa hatua….ninakuhakikishia kuwa kama
utatulia na kufuata hayo utakayoelekezwa, utamiliki nyumba ya kifahari,
utamiliki gari, na kila ukitakacho, lakini kwanza utimize hayo nitakayokuambia,
…unasikia kwanza kabisa,unatakiwa uende shule maalumu ya kujua nini huyu mwanaume,
ujua nini ndoa, ujua nini kuhusu mahusiano, na……
Mambo ndipo yalipopikiwa hapo……wajanja wakatumia udhaifu wa
ndoa za watu, na hatimaye,...yakatokea yaliyotokea……lakini je yalitokeaje,.....! Tuwe pamoja katika sehemu
nyingine ya hitimisho la kisa hiki..
WAZO LA LEO:Mpango wowote wa kujichumia mali usio halali ,mwisho wake ni
madhara. Watu sasa hivi hujiingiza
kwenye njia nyingi za kutafuta mali, bila kujali `uhalali wake’….hata kama kwa kufanya
hivyo wataumiza watu wengine, ilimradi kama wao wamefanikiwa,
basi wanaona ni halali yao,…na hata kufikia kunadi kwa kusema `mjini hapa’.
Kumbuka, kuwa utajiri wa namna hiyo hauna mwisho
mwema,kwasababu kupata kwako ni kuumia kwa wengine, …na hujui maumivu gani
waliyoyapata hawo wenzako uliowadhulumu, ujue hukumdhulumu yeye peke yake, kama ana familia basi hata familia yake imeumia. Je unajua wamumia kiasi gani, na hujui wamelia kilio gani kwa mungu, na ukumbuke
kuwa dua ya mwenye kudhulumiwa haina kizuizi,
..najionya kwanza mimi mwenyewe na wewe pia kuwa tuwe makini katika kutafuta rikiki zetu.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Nimependa sana wazo la leo...tuko pamoja M3
Precious tupo pamoja,nashukuru kuwa nami kama kawaida
Post a Comment