Mtoto wa familia ya kidocta, alizitoa zile pica kwenye
bahasha, na kuanza kuitizama moja moja, na kila aliyoangalia alitamani kuichana
au kuitia moto, lakini asingeliweza kutimiza hilo alilopanga kufanya,
akaendelea kuzitizama na majina ya huyo mwanamke alieyepo kwenye picha na nyuma
ya picha kuna maelezo wapi akaishi.
Alizitizama zile picha kila moja kwa wakati wake, na
kujaribu kuvuta kumbukumbu , kama kweli aliwahi kukutana na hawo wanawake,
lakini hakuweza kumgundua hata mmoja, akainuka na kwenda kusimama kwenye
dirisha aliangalia nje sehemu ambayo mume wake anaweka gari lake, kulikuwa
hakuna gari, na inaonyesha kama hapajatumika kwa muda mrefu.
Alikumbuka jinsi walivyopigana majuzi, na ikabidi mume wake
huyo ahamie chumba cha wageni, na mara kwa mara alikuwa akiamuka kuhakikisha
kuwa hapitilizi na kwenda chumba cha binti yake wa kulea, alishaamua kumlinda
kwa nguvu zake zote, …
‘Huyu mtu atakuwa hajalala ndani, sijui atakuwa kalala wapi,
nikipagundua, huyo mwanamke wake nitamtoa nyongo….anachezea mali ya mtoto wa
mama docta..ngoja leo akija , nitamshika mguu kwa mguu hadi kwa huyo mwanamke
wake….’akasema lakini alipowaza jambo, akaona ngoja kwanzaatafakari kazii
aliyopanga kuifanya,…kamaitafanikiwa,ataweza kulikomesha hili, sio kwa mume
wake tu, hata kwa waume wa wengine ambao wana tabia kama hiyo….
Akakumbuka mawasiliano na mama yake ambaye alimpigia simu
akitaka kuomba ushauri, maana kazi anayotaka kuifanya inahitaji mtu
mzoefu,…anakumbuka alishawahi kushauriiwa na mama yake aanzishe kliniki yake na
iwe kama tawi,…..lakini akakataa, sasa wazo la kuianzisha likamjia, lakini
alitaka aianzishe kwa namna tofauti….
‘Bintiyangu unaniangusha, mimi ni docta ambaye nawasaidia
walio na matatizo ya ndoa zao, niwafunda wake za watu ili ndoa zao ziwe na
furaha, leo nashangaa kusikia kuwa wewe
hupatani na mume wako, unajau unaniabisha….’akasikia sauti ya mama yake
akiongea kwenye ubongo wake.
‘Ina maana mimi ndio nimeshindwa kutimiza wajibu wangu au ni
mwenzangu, kwani wapi nimeshindwa kutimiza wajibu wangu, najitahidi sana pamoja
na majukumu yangu ya kazi,lakini bado natimiza kila jambo linalonistahili mimi
kama mke wa mtu….’akajikuta akijiuliza.
‘Hebu niambie tatizo liko wapi, binti yangu…?’akasikia sauti
hiyo ikimuuliza.
‘Mama , mimi silioni tatizo, …na kukupigia simu, sio kwamba
nimeshindwa, sijashindwa, ila jibu la swali lako kuwa tatizolipowapi, ni
kwamba,nimejribu hata mimi mwenyewe kufanya utafiti ili nijue tatizo lipo wapi
nimeshidwa, nimejaribu kumweka mwenzangu karibu, kumhoji, kumdadisi, ili niweze
kujua nini anataka,lakini
nimeshindwa..’akajitetea
‘Ulipomuuliza nini anataka alisema nini?’ akaulizwa.
‘Anasema yeye kama mwanaume hastahili kuchungwa, anachotaka
ni yeye kufanya yake anayoyaona yeye kama mwanaume anastahili kufanya, hataki
aulizwe wapi katoka na kwanini kachelewa kurudi,..na kila kihitaji lolote,
hataki kusikia nimechoka,sijisikii….mama,inakera…’akasema
‘Ni hayo tu binti yangu, na mambo mengine ya kindoa
unamtimizia ipasavyo…?’ akaulizwa.
‘Yote najaribu kumtimizia, lakini wakati mwingine mama unakuwa
umechoka,mwenzangu hashibi,…hashibi kabisaaah, uelewe mama mimi ni mfanyakazi,
na unavyojua kazi zetu, unatembea ndani ya hospitalini,nenda rudi, panda shuka,
ukipima huo umbali uliotembea humohospitalini,ni kama umetembea maili nyingi
sana,…..achilia mbali kusemeshana na watu, kushughulikia hawo wagonjwa,
unajikuta ukirudi nyumbani umechoka, na ukirudi nyumbani majukumu
yanakungoja,…..’akajitetea.
‘Niliwashauri mtafute mfanyakazi wa nyumbani mlifikia
wapi….?’ Akauliza.
‘Mama hilo sitalirudia tena kwa sasa, unajua yule binti wa
watu nilyekuambia nilimchukua atusaidiekazi, alichofanyiwa na huyu mume, ni aibu
hata kuongea, achilia mbali huyo mfanyakazi yule ndugu yetu niliyemchukua toka
kule kijijini, naye unajua nini kilichomkimbiza toka hapa, watu wanazani kuwa
labda mimi ni mkali siwezi kuishi na wafanyakzi wa nyumbani, lakini sivyo
hivyo, nimeficha siri za mumewangu tu,….’akatulia na kwikwi za kilio
zikamtawala.
‘Kwahiyo huna mfanyakazi tena hapo nyumbani kwako,anayekusaidia
majukumu mengi ya usafi,kufua …..?’ akaulizwa.
‘Kazi ndogo ndogo ananisaidia yule binti yetu,yule binti
,ambaye nilichukua kijijini akiwa anakula majalalani, tuaamua tumchukue tumlee
kama mtoto wetu…kawa bint mkubwa, nakwa vile kaanza kupendeza, basi mume wangu
keshaanza kumwangalia kwa macho ya tamaa…..’akasema
‘What….huyo sio
sawa na mtoto wenu, nakumbuka mliniambia kuwa huyo mtamfanya kama sehemu ya
familia yenu,,….sasa iweje leo, mimi huyo simuiti kama mfanyakazi wenu wa
nyumbani,huyo ni mtoto wenu….. unasema mumeo anaanza kutoa mate kwa ajili
yake….its too much,….mwanagu njoo
nikufunde, kuna tatizo hapo, kuna kitu umeshindwa kwa huyo mumeo,…..njooo
haraka….’akasema mama kwa hasira
‘Mama, sijashindwa…mama, inaniuma sana, ukisema mimi
nimeshindwa siwei kukuelewa,labda kwa vile humjui huyu mume wangu, nimeshindwa
nini mimi mama, huyu mume anataka nini cha zaidi…lakini hata hivyo mama mbona ….’akaanza
kulia tena….
‘Sasa ndio unalia,…usiniangushe sitaki wanangu muwe
legelege, pambana kiume….mmh,kikike, wewe ni mwaanmke,bwana,wewe ndiye muhusika
mkuu wa ndani ya nyumba yako, ukishindwa kuilea familia yako,akiwemo mume wako,
utachekwa,….nasikitika sanakuona unalia, kulia huko kunaonyesha kuwa mume
kakushinda,kama vipi njoo ukae na mimi wiki mojatu,ukirudi huko utanimbia,…ni
aibu kusikia kuwa mmoja wa binti yangu ana matatizo kama hayo….’mama
akamwambia.
‘Wala sihitaji kuja huko mama,nimeshajua nini la kufanya,
yeye si anajifanya kidume,ngoja nitapambana naye kumuonyesha kuwa mimi ni mwmanake wa shoka….mtoto wa mama
Docta…’akasema huku akikunja ngumi.
‘Nataka kusikia hivyo, sitaki watoto wangu muwe laini laini,
pambana na familia yako, jiulize wapi nimekosa, angali nini mume anataka, na
kwanini awatake hata mabinti wa nyumbani, ndugu zako….ina maana wewe
hutatembelewa na ndugu wa kike,….huyo hujamshibisha, hujamjulia nini anataka…na
miaka imepita hamjajaliwa mtoto, hilo sio kosa lenu, ila jitahidini kupimwa,
muangalia huenda kuna tatizo jingine.
‘Binti yangu ndoa sio lelemama,ndoasio kufika kwa mume kama
mbia,kama mshirika wa biashara, ndoa ni jukumu lako, ukifika ujue wewe ndiwe
mlezi, wewe ndiye kila kitu kuhusu malezi, mume, ni mume tu, yeye anahitaji
malezi yako pia. Mume ni kama mwenyekiti, wewe ni katibu, hebu angalia kazi za
katibu na mwenyekiti, ni mfano dogo tu, ila ni zadi ya hapo….
‘Mama nimekuelewa, hilo niachie nimeshajua nini cha kufanya,
nitapambana naye hadi nionemwisho wake, sihitaji msaada wamtu….’akasema akiwa
kakunja uso kwahasira.
‘Pambana naye, usishindwe majukumu yako ya nyumbani,
ukishindwa wenzako watakucheka, na wakijua udhaifu wako, watamchukua mume wako
kijumla….chunguza hawo wanaomvuti mume wako wana nini cha zaidi, ukijua fanay
zaidi yao….sioni kwaniniushindwe….’mama yake akasema.
‘Nitapambana naye,…tutaona…na nitajua nini walicho nacho cha
ziaidi,na mimi nitawaonyesha kuwa najua
zaidi….utasikia siku yeke….’akasema.
*******
‘Binti Maringo, Kimwali, Kimwana,…..mama Docta…’aliposoma
hilo jina akashituka, anachojua yeye mama docta ni jina ambalo huitwa mama
yake, na ndugu yake pacha,….anakumbuka kuwa hata yeye alipenda kulitumia hilo
jina alipokuja mara ya kwanza, alikuwa kijiita hivyo, lakini hilo jina
halikudumu sana….hakulipenda.
‘Mama Docta ni nani huyu,….?’ Akajiuliza, akachukua simu na
kumpigia mtu wake ambaye kampa kazi hiyo ya kufuatilia nyendo za mume wake.
‘Hebu niambie huyu mama docta ni nani?’ akauliza.
‘Ni dakitari mmoja, ndivyo anavyoitwa, ….’akasema huyo mtu
wake.
‘Yeye mara kwa mara wanakutana wapi na mume wangu?’ akauliza.
‘Mhh,hawana sehemu maalumu, mume wako mara nyingi ndiye
anatemfuata, hasa baada ya kukosana Kimwana, kimwana alikuwa rafiki yake wa
mara kwa mara, kila akitoka hapo kwako anakwenda huko kwa Kimwana, lakini
baadaye akakutana na huyu mama Docta, kipindi anaumwa, naonahap ndipo
alipokolea,….’akasikia maneno hayo na hasira zikampanda.
‘Kwahiyo analala huko huko,au?’ akauliza.
‘Sijawahi kuona akienda kulala huko huko,maana huyu
mamadocta ni mkali sana kwa wanaume, hapendi wanaume…’akasema.
‘Kama hapendi wanaume,mbona anampenda mume wangu?’ akauliza.
‘Mume wako ndiye anayemtaka…kiukweli inavyoonekana ndivyo
hivyo,kuwa mumeo ndiye kazimia kwa huyo docta, huyo docta ni mrembo kweli, na
kinachowafanya wanaume wengi wazimie kwake, ni huko kutokupenda
wanaume,…unavyomjua mume wako, alivyo akadai yeye hatongozi mke akashindwa,..
wakati mwingine unaona kabisa, mume wako akihangaika kuongea na huyo mama
docta, lakini huyo mama docta anaonekana kukataa….’akasema huyo mtu wake.
‘Lakini kwenye hii picha wanaonekana kabisa wakibusiana…na
inanichefua kweli hii picha…nikikutana na huyu mwanamke ataniona kuwa mimi ni nani...’akasema.
‘Kwenye hiyo picha hapo, alikuwa akilizimisha hilo busu,
niliwakuta wakati wanapata chakula cha mchana, na kama kawaida mume lazima
apate kichngamsha kichwa, nafikiri baada ya kukolea akaona afanye hicho
unachokiona hapo, mwenzake alikuwa hakubali…., akamshitukizia kumbusu, mumeo kweli
naye hajatulia…..lakini kwanini anafanya hivyo humshibishi nini….?’ Akauliza
huyo mtu wake.
‘Mimi sijakupa kazi ya kunichunguza mimi, kuwa nafanya nini
na mume wangu, unanisikia lakini,, kazi yako ni hiyo kumchunguza mume wangu anafanya
nini na hawo wanawake, usianzekunichefua, maana nyie wanaumelenu moja,….sasa
nataka kazi moja kutoka kwako…..njoo hapa kesho tutapangane jinsi ya kuifanya,….’akasema
na kukata simu.
NB: Ni kazi gani hiyo, tuendelee kuwepo. Samahani kwa kuchelewesha
kuweka sehemu hii, nilichelewa kufika kijiweni, na bosi akaingia mapema,
ikabidi nitulie kwanza. Hata hivyo sijaweza hata kuipitia, nimeiandika kwa
haraka, kama kuna makosa tusadieni kusahihisha. Tupo pamoja
WAZO LA LEO:
Ukitenda jambo kwa mwenzako, au kusema neno kwa mwenzako, kwanza jiulize je
mimi nikitendewa hivyo, au kuambiwa hivyo nitafurahi, isiwe mkuki kwa nguruwe
tu, kwa binadamu uwe mchungu.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Post a Comment