Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, June 1, 2012

Hujafa hujaumbika-46 hitimisho-4
Mtoto wa familia ya kidocta, alizitoa zile pica kwenye bahasha, na kuanza kuitizama moja moja, na kila aliyoangalia alitamani kuichana au kuitia moto, lakini asingeliweza kutimiza hilo alilopanga kufanya, akaendelea kuzitizama na majina ya huyo mwanamke alieyepo kwenye picha na nyuma ya picha kuna maelezo wapi akaishi.

Alizitizama zile picha kila moja kwa wakati wake, na kujaribu kuvuta kumbukumbu , kama kweli aliwahi kukutana na hawo wanawake, lakini hakuweza kumgundua hata mmoja, akainuka na kwenda kusimama kwenye dirisha aliangalia nje sehemu ambayo mume wake anaweka gari lake, kulikuwa hakuna gari, na inaonyesha kama hapajatumika kwa muda mrefu.

Alikumbuka jinsi walivyopigana majuzi, na ikabidi mume wake huyo ahamie chumba cha wageni, na mara kwa mara alikuwa akiamuka kuhakikisha kuwa hapitilizi na kwenda chumba cha binti yake wa kulea, alishaamua kumlinda kwa nguvu zake zote, …

‘Huyu mtu atakuwa hajalala ndani, sijui atakuwa kalala wapi, nikipagundua, huyo mwanamke wake nitamtoa nyongo….anachezea mali ya mtoto wa mama docta..ngoja leo akija , nitamshika mguu kwa mguu hadi kwa huyo mwanamke wake….’akasema lakini alipowaza jambo, akaona ngoja kwanzaatafakari kazii aliyopanga kuifanya,…kamaitafanikiwa,ataweza kulikomesha hili, sio kwa mume wake tu, hata kwa waume wa wengine ambao wana tabia kama hiyo….

Akakumbuka mawasiliano na mama yake ambaye alimpigia simu akitaka kuomba ushauri, maana kazi anayotaka kuifanya inahitaji mtu mzoefu,…anakumbuka alishawahi kushauriiwa na mama yake aanzishe kliniki yake na iwe kama tawi,…..lakini akakataa, sasa wazo la kuianzisha likamjia, lakini alitaka aianzishe kwa namna tofauti….

‘Bintiyangu unaniangusha, mimi ni docta ambaye nawasaidia walio na matatizo ya ndoa zao, niwafunda wake za watu ili ndoa zao ziwe na furaha, leo nashangaa  kusikia kuwa wewe hupatani na mume wako, unajau unaniabisha….’akasikia sauti ya mama yake akiongea kwenye ubongo wake.

‘Ina maana mimi ndio nimeshindwa kutimiza wajibu wangu au ni mwenzangu, kwani wapi nimeshindwa kutimiza wajibu wangu, najitahidi sana pamoja na majukumu yangu ya kazi,lakini bado natimiza kila jambo linalonistahili mimi kama mke wa mtu….’akajikuta akijiuliza.

‘Hebu niambie tatizo liko wapi, binti yangu…?’akasikia sauti hiyo ikimuuliza.

‘Mama , mimi silioni tatizo, …na kukupigia simu, sio kwamba nimeshindwa, sijashindwa, ila jibu la swali lako kuwa tatizolipowapi, ni kwamba,nimejribu hata mimi mwenyewe kufanya utafiti ili nijue tatizo lipo wapi nimeshidwa, nimejaribu kumweka mwenzangu karibu, kumhoji, kumdadisi, ili niweze  kujua nini anataka,lakini nimeshindwa..’akajitetea

‘Ulipomuuliza nini anataka alisema nini?’ akaulizwa.

‘Anasema yeye kama mwanaume hastahili kuchungwa, anachotaka ni yeye kufanya yake anayoyaona yeye kama mwanaume anastahili kufanya, hataki aulizwe wapi katoka na kwanini kachelewa kurudi,..na kila kihitaji lolote, hataki kusikia nimechoka,sijisikii….mama,inakera…’akasema

‘Ni hayo tu binti yangu, na mambo mengine ya kindoa unamtimizia ipasavyo…?’ akaulizwa.

‘Yote najaribu kumtimizia, lakini wakati mwingine mama unakuwa umechoka,mwenzangu hashibi,…hashibi kabisaaah, uelewe mama mimi ni mfanyakazi, na unavyojua kazi zetu, unatembea ndani ya hospitalini,nenda rudi, panda shuka, ukipima huo umbali uliotembea humohospitalini,ni kama umetembea maili nyingi sana,…..achilia mbali kusemeshana na watu, kushughulikia hawo wagonjwa, unajikuta ukirudi nyumbani umechoka, na ukirudi nyumbani majukumu yanakungoja,…..’akajitetea.

‘Niliwashauri mtafute mfanyakazi wa nyumbani mlifikia wapi….?’ Akauliza.

‘Mama hilo sitalirudia tena kwa sasa, unajua yule binti wa watu nilyekuambia nilimchukua atusaidiekazi, alichofanyiwa na huyu mume, ni aibu hata kuongea, achilia mbali huyo mfanyakazi yule ndugu yetu niliyemchukua toka kule kijijini, naye unajua nini kilichomkimbiza toka hapa, watu wanazani kuwa labda mimi ni mkali siwezi kuishi na wafanyakzi wa nyumbani, lakini sivyo hivyo, nimeficha siri za mumewangu tu,….’akatulia na kwikwi za kilio zikamtawala.

‘Kwahiyo huna mfanyakazi tena hapo nyumbani kwako,anayekusaidia majukumu mengi ya usafi,kufua …..?’ akaulizwa.

‘Kazi ndogo ndogo ananisaidia yule binti yetu,yule binti ,ambaye nilichukua kijijini akiwa anakula majalalani, tuaamua tumchukue tumlee kama mtoto wetu…kawa bint mkubwa, nakwa vile kaanza kupendeza, basi mume wangu keshaanza kumwangalia kwa macho ya tamaa…..’akasema

What….huyo sio sawa na mtoto wenu, nakumbuka mliniambia kuwa huyo mtamfanya kama sehemu ya familia yenu,,….sasa iweje leo, mimi huyo simuiti kama mfanyakazi wenu wa nyumbani,huyo ni mtoto wenu….. unasema mumeo anaanza kutoa mate kwa ajili yake….its too much,….mwanagu njoo nikufunde, kuna tatizo hapo, kuna kitu umeshindwa kwa huyo mumeo,…..njooo haraka….’akasema mama kwa hasira

‘Mama, sijashindwa…mama, inaniuma sana, ukisema mimi nimeshindwa siwei kukuelewa,labda kwa vile humjui huyu mume wangu, nimeshindwa nini mimi mama, huyu mume anataka nini cha zaidi…lakini hata hivyo mama mbona ….’akaanza kulia tena….

‘Sasa ndio unalia,…usiniangushe sitaki wanangu muwe legelege, pambana kiume….mmh,kikike, wewe ni mwaanmke,bwana,wewe ndiye muhusika mkuu wa ndani ya nyumba yako, ukishindwa kuilea familia yako,akiwemo mume wako, utachekwa,….nasikitika sanakuona unalia, kulia huko kunaonyesha kuwa mume kakushinda,kama vipi njoo ukae na mimi wiki mojatu,ukirudi huko utanimbia,…ni aibu kusikia kuwa mmoja wa binti yangu ana matatizo kama hayo….’mama akamwambia.

‘Wala sihitaji kuja huko mama,nimeshajua nini la kufanya, yeye si anajifanya kidume,ngoja nitapambana naye kumuonyesha kuwa mimi ni mwmanake wa shoka….mtoto wa mama Docta…’akasema huku akikunja ngumi.

‘Nataka kusikia hivyo, sitaki watoto wangu muwe laini laini, pambana na familia yako, jiulize wapi nimekosa, angali nini mume anataka, na kwanini awatake hata mabinti wa nyumbani, ndugu zako….ina maana wewe hutatembelewa na ndugu wa kike,….huyo hujamshibisha, hujamjulia nini anataka…na miaka imepita hamjajaliwa mtoto, hilo sio kosa lenu, ila jitahidini kupimwa, muangalia huenda kuna tatizo jingine.

‘Binti yangu ndoa sio lelemama,ndoasio kufika kwa mume kama mbia,kama mshirika wa biashara, ndoa ni jukumu lako, ukifika ujue wewe ndiwe mlezi, wewe ndiye kila kitu kuhusu malezi, mume, ni mume tu, yeye anahitaji malezi yako pia. Mume ni kama mwenyekiti, wewe ni katibu, hebu angalia kazi za katibu na mwenyekiti, ni mfano dogo tu, ila ni zadi ya hapo….

‘Mama nimekuelewa, hilo niachie nimeshajua nini cha kufanya, nitapambana naye hadi nionemwisho wake, sihitaji msaada wamtu….’akasema akiwa kakunja uso kwahasira.

‘Pambana naye, usishindwe majukumu yako ya nyumbani, ukishindwa wenzako watakucheka, na wakijua udhaifu wako, watamchukua mume wako kijumla….chunguza hawo wanaomvuti mume wako wana nini cha zaidi, ukijua fanay zaidi yao….sioni kwaniniushindwe….’mama yake akasema.

‘Nitapambana naye,…tutaona…na nitajua nini walicho nacho cha ziaidi,na mimi nitawaonyesha  kuwa najua zaidi….utasikia siku yeke….’akasema.

*******

‘Binti Maringo, Kimwali, Kimwana,…..mama Docta…’aliposoma hilo jina akashituka, anachojua yeye mama docta ni jina ambalo huitwa mama yake, na ndugu yake pacha,….anakumbuka kuwa hata yeye alipenda kulitumia hilo jina alipokuja mara ya kwanza, alikuwa kijiita hivyo, lakini hilo jina halikudumu sana….hakulipenda.

‘Mama Docta ni nani huyu,….?’ Akajiuliza, akachukua simu na kumpigia mtu wake ambaye kampa kazi hiyo ya kufuatilia nyendo za mume wake.

‘Hebu niambie huyu mama docta ni nani?’ akauliza.

‘Ni dakitari mmoja, ndivyo anavyoitwa, ….’akasema huyo mtu wake.

‘Yeye mara kwa mara wanakutana wapi na mume wangu?’ akauliza.

‘Mhh,hawana sehemu maalumu, mume wako mara nyingi ndiye anatemfuata, hasa baada ya kukosana Kimwana, kimwana alikuwa rafiki yake wa mara kwa mara, kila akitoka hapo kwako anakwenda huko kwa Kimwana, lakini baadaye akakutana na huyu mama Docta, kipindi anaumwa, naonahap ndipo alipokolea,….’akasikia maneno hayo na hasira zikampanda.

‘Kwahiyo analala huko huko,au?’ akauliza.

‘Sijawahi kuona akienda kulala huko huko,maana huyu mamadocta ni mkali sana kwa wanaume, hapendi wanaume…’akasema.

‘Kama hapendi wanaume,mbona anampenda mume wangu?’ akauliza.

‘Mume wako ndiye anayemtaka…kiukweli inavyoonekana ndivyo hivyo,kuwa mumeo ndiye kazimia kwa huyo docta, huyo docta ni mrembo kweli, na kinachowafanya wanaume wengi wazimie kwake, ni huko kutokupenda wanaume,…unavyomjua mume wako, alivyo akadai yeye hatongozi mke akashindwa,.. wakati mwingine unaona kabisa, mume wako akihangaika kuongea na huyo mama docta, lakini huyo mama docta anaonekana kukataa….’akasema huyo mtu wake.

‘Lakini kwenye hii picha wanaonekana kabisa wakibusiana…na inanichefua kweli hii picha…nikikutana na huyu mwanamke ataniona kuwa mimi ni nani...’akasema.

‘Kwenye hiyo picha hapo, alikuwa akilizimisha hilo busu, niliwakuta wakati wanapata chakula cha mchana, na kama kawaida mume lazima apate kichngamsha kichwa, nafikiri baada ya kukolea akaona afanye hicho unachokiona hapo, mwenzake alikuwa hakubali…., akamshitukizia kumbusu, mumeo kweli naye hajatulia…..lakini kwanini anafanya hivyo humshibishi nini….?’ Akauliza huyo mtu wake.

‘Mimi sijakupa kazi ya kunichunguza mimi, kuwa nafanya nini na mume wangu, unanisikia lakini,, kazi yako ni hiyo kumchunguza mume wangu anafanya nini na hawo wanawake, usianzekunichefua, maana nyie wanaumelenu moja,….sasa nataka kazi moja kutoka kwako…..njoo hapa kesho tutapangane jinsi ya kuifanya,….’akasema na kukata simu.

NB: Ni kazi gani hiyo, tuendelee kuwepo. Samahani kwa kuchelewesha kuweka sehemu hii, nilichelewa kufika kijiweni, na bosi akaingia mapema, ikabidi nitulie kwanza. Hata hivyo sijaweza hata kuipitia, nimeiandika kwa haraka, kama kuna makosa tusadieni kusahihisha. Tupo pamoja
WAZO LA LEO: Ukitenda jambo kwa mwenzako, au kusema neno kwa mwenzako, kwanza jiulize je mimi nikitendewa hivyo, au kuambiwa hivyo nitafurahi, isiwe mkuki kwa nguruwe tu, kwa binadamu uwe mchungu.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

emu-three said...
This comment has been removed by the author.