Tukiendelea pale tulipoachia kuhusu kisa cha binti wa
kijijini,
Binti huyu aliyeathiriwa na kutendwa, kutokana na kuvunjwa
kwa ahadi ya ndoa ya utotoni, ndoa iliyokuwa baina ya Msomali na huyo binti na
mshahidi walikuwa Mungu muumba Wa viumbe na malaika wake. Ilikuwa ni ndoa ua
utoto, lakini….Haya tuendelee na kisa hiki;
%%%%%%%%
‘Hivi kweli niwaulize, kuna ndoa ya utotoni ambayo inaswihi,
mimi najua ili ndoa ikubalike ni lazima watu wawe na umri unaojulikana kuwa
hawa wamepevuka kiakili, na pia ili iwe ni ndoa ni lazima kuwe na wafungishaji
ndoa na pia wawepo mashahidi, …sasa mnapotoka kunitupia lawama mimi kuwa eti
ndiye niliyesababisha hadi huyo binti kuathirika kisaikolojia, nashindwa
kuelewa,…ikizingatia kuwa wewe ni mwanasheria unayajua hayo yote kuliko mimi…’nikajitetea
pale nilipoona wakili mwanadada akitulia.
‘Ndio hilo unaloongea ni sawa, sijakataa,na wala sijasema
ndoa hiyo inakubalika kisheria, ila mwenzko aliichukulia kuwa ni ndoa kamili, najua
kuwa haikuwa na yale mambo muhimu yanayohitajika kuitwa ndoa, na kwa ujumla haiswihi
kuitwa ndoa, ni michezo ya utotoni, lakini nikuulize wewe wakati mnaifunga ile
ndoa ulikuwa na dhamira ya kweli kuwa unaoa, au mlifanya kama mchezo tu,
ulikuwa ukimpenda kiukweli au ulikumwa mchzo wa kitoto…?’
‘Niseme kiukweli, wakati tunaifunga ile ndoa, nilikuwa na
dhamira ya kiukweli kuwa naoa, na baada ya tukio lile, nilimuona kama ni sehemu
ya mwili wangu, na hata leo nahisi hivyo, lakini ujana na damu yangu kuchemka, nikasalitika,
na niseme …yakatokea yaliyotokea, …..’nikajitetea.
‘Sasa unaona hilo, mwenzako ilikuwa zaidii ya hilo,
alijizuia kwa kila hali akijua kuwa ana mume,….toka siku ile,…na siku ile alipokufumania
akajua umehini ndoa, na akaathirika kiukweli, na ndio chanzo cha matatizo yake
ya kiafya hadi leo hii..
‘Una maana gani kusema hadi leo hii, kwani una habari zake, kuwa
yupo wapi, …?’ nikajikuta nauliza
‘Usiwe na pupa kwani sio wewe peke yake unayetaka kujua hayo
, nataak kila mtu aelewe hatua kwa hatua, ili mwisho wa siku muone athari
zinazotokana na kusalitiwa katika `kupendana’husuani kwenye ndoa.Tujue kuwa sio
wote wenye uthabiti wa kuvumilia matatizo, ndio maana unaona wengine wakipata
matatizo kidogo tu wanaathirika na wengine wanadunda, hata iweje, ni hula na
maumbile ya kibinadamu.
Tukirejea pale tulipoishia kuwa binti huyu kila akipata
mchumba, ndoa hiyo inakuwa haifungiki, ama kunatokea ajali au matatizo ambayo
yanaisimamisha hiyo ndoa.Na haikutoka mara moja, ni zaidi ya mara tatu,….Hutaamini
hayo, lakini yalitokea kwa huyu binti,na ukianglian sana inapotokea hivyo,
anayeathirika sana akilini ni nani….mara nyingi anakuwa ni mwanamke…hayo ni
maumbile
Kwa mtizamo huo na maneno ya yule mtaalamu wa mwanzo wa
sili, na histora ya matatizo yake ikaonekanahivyo, kwa hawa wazazi na pia kwa jamii na wanajamii
waliobahatika kulijua hilo tatizo kuwa kweli huyo binti anatawaliwa na huyo
jinni mahaba. Hapa muwe makini,muone jinsi gani hawa wataalamu wanavyojua
kuzichota hisia za watu kisaikojia, sio kwamba na wapinga, lakini sio kweli
kuwa wote wapo sahihi kwa yale wanayoyasema.
Wazazi kusikia hivyo,wakaamua kulifungia kazi hilo tatizo,
kwa wataalamu ,huku na kule, na kila wapofika wimbo ni huo huo, ….mtoto wenu
ana meshetani, anatawaliwa na jinni, ….je ni nani hataacha kuamini hayo, hasa
kwa wazazi wa binti,.., zaidi ya wataalmu sitawote wanasema kitu hicho hicho,wakajua
ni kweli, sasa wanatakiwa kuliondoa hilo shetani,..wafanyeje.
Kwanza walifuata hayo waliyoambiwa na wataalamu wa kiasili ,
dawa za kufukiza, sijui maji ya baharini, kuku mwekundu,…vitu vingi tu, ….lakini
wapiiiii….tatizo likawa linajirudia ingawaje si mara kwa mara ila ni pale tu
inapofikia huyu mwanadada kapata mchumba au rafiki wa kiume.
Basi wazazi wakaona hilo sasa tuwaendee watu wa dini, wakawatafuta
waombezi wa kidini, wakaombewa, na wao hawakuchagua dini gani, kila wanayemuona
ni mtu aliyesomea dini na anajua jinsi gani ya kumuombea mgonjwa aliyeathirika
na mshetani, wanamuomba atoe msaada huo.,….imani ni kitu cha pekee yake na
mungu hamtupi mja wake, baada ya maombezi hayo, hali ilionekana kuwa imetulia, lakini sasa likazuka
tatizo jingine.
Kila mwanaume aliyakutana na huyo binti, akampenda, wakakubaliana
na hata kufikia hatu ya kujimbulisha kama wachumba, mwanaume huyo akirudi
nyumbani kwao kutoa taarifa, akiulizwa na mwanamke gani, akamtaja huyo
mwanamke, naambiwa wewe, unataka kufa na jinni mahaba, shauri lako, angalai
wenzako, mtoto wa nani na anni wako wapi sasa,…achana naye , wanawake wapo
wengi, katafute mwanamke mwingine usiingie kwenye balaa….
Basi ikawa mkosi kwa binti huyu, wanaume wengi, wakawa wanamuogopa,
na hali hii ya kunyanyapaliwa, ikamuathiri zaidi, akajiona ni mwanamke wa
mikosi, kuwa yeye sio mtu wa
kawaida,..na kuanzia hapo, akawa hataki urafiki na wanaume, chuki ikajijenga
akilini, na hasira kwa wanaume ikazidi.
Chuki hiyo ilikuwa kwa wanaume wote,na wakati huo, akili
yake haikuwa ikitambua kuwa chanzo cha yote hayo ni athari iliyojijenga akiwa
msichana mdogo, kuwa yeye bado nafsi yake ipo kwenye pendo la mwanzo, pendo
lake na mvulana wa utotoni na ujanani ambaye ndiye aliyeathiri akili na nafsi
yake….
‘Mume wangu, mimi naona tuhame kabisa hapa, maana kwanza biashara
haiendi vyema, pili, binti yetu anaathirika kisaikolojia,turudi kwetu, ama
kijijini au mahali pengine , ambapo watu hawajui lolote kuhusu binti yetu….naona
anateseka sana’akasema mke.
‘Hilo wazo lako sio baya, hata mimi nilishaliwaza hilo, sio
kuliwaza tu, bali nilishawasiliana na ndugu yangu anayeishi huko Dar, ana jengo
lake lipo sehemu nzuri ya kibiashara, tutahamisha baadhi ya shughuli zetu na
nyingine zitaendelea kuwepo hapa, …bado mambo machche ya kisheria kama leseni
lakini hilo litakamilika hivi karibuni….’akasema mume.
‘Je na huyu binti yetu kuhusu kazi yake ambayo keshaianza
hapa itakuwaje?’ akauliza mke.
‘Hilo nalo nimeshalifanyia kazi,
kuna nafasi nyingi zakazi za madakitari huko Dar, na ni swala la yeye kupeleka
vyeti vyake hukoo na barua ya maombi, atapata kazi hilo halina shida…sisi
tuanze tu kujiandaa.
Na binti yao akafahamishwa, na
yeye hakuwa na pingamizi, na safari ya kuja Dar ikakamilika
Sasa turejee kwa familia ya madakitari, familia ambayo baba,
mama na watoto wote walibobea kwenye fani hii ya udakitari, na hata kufikia hatua
ya kuanzisha kliniki yao, na sio kliniki tu,bali kikawa chuo cha kufundisha
madaktari au watu waliotaka kujua maswala
ya kimaumbile,hulka na hisia hasa katika maswala mazima ya mahusiano, huku
kwetu tunaita kufundwa, wao waliyaweka kitaalamu zaidi.
‘Unataka kuoa au
kuolewa, una matatizo ya kindoa, una matatizo ya uzazi, una matatizo ya
kifamilia na mengine mengi, fika kwa kliniki ya mama Docta, …’ hilo ni moja
ya tangzao lao, ukifika huko Kenya utalikuta.
‘Unasema Mama Docta,ina
maana ni yule mama aliyetoroka hapa nchini…..?’ nikauliza huku nikiwa nimewaka
kwa hasira.
‘Hebu nikuulize swali, huyu mama aliyetoroka hapa ana umri
wa kuweza kuzaa watoto wakubwa wakuolewa…jinsi ulivyomuona wewe?’ akauliza
wakili mwanadada.
‘Hapana ,…yule mimi nilishakutana naye, hana umri huo,licha
ya kuwa anavaa miwani mikubwa na nywele zake ni nyingi, nafikiri ni za bandia,
..huwa kama akaficha sura wakati wote, lakini ukimwangalia kwa karibu,sio mtu
mzima wa kuwa na watoto wakubwa kiasi hicho,,maana mwanamke aliyezaa mabinti
waliofikia umri wakuolewa,hajifichi….’akasema mkuu.
‘Sasa… mbona hapo mnanichanganya, hebu endeelea tusikukatize…huenda
nikapaat jibu…’nikasema.
‘Ndio maana nawaomba mnipe nafasi,maana mimi nimelifanyia
hilo utafiti wa kina, najua kila kitu, kuhsu hawo watu, mkianza kunikatisha-katisha,
nitalipua lipua na hamtaelewa vyema….’akasem wakili mwanadada.
‘Haya endelea…’nikasema huku nikajaribu kumkumbuka huyo docta
mama, sikuwahi kukutana naye uso kwa uso, nilikuwa namuona kwa mbali tu….
Ukumbuke kuwa ndani ya kliniki hii, pia alipitia binti ,aliyekuwa
mchumba au mke wako wa utotoni, na hapo ndipo alipopatia mafunzo mazuri ya uzazi, hulka za kimaumbile, na ukichanganya
na fani yake ya udakitari, basi akaamua kuusomea kabisa udakitari bingwa wa matatizo ya kina mama , na kwa vile
alishaanza kutibu hapo, kusaidia na hata kufundisha wengi wakawa na yeye
wanamuita mama-Docta.
Kwa jinsi alivyofaulu, na kuweza kufikia kiwango cha hali ya
juu, katika kliniki hiyo, au chuo hicho,wenyewe waliamua kumchukua kabisa awe
mmoja wa dakitari wao, au mwalimu wa chuo hicho, lakini mara ikaja hiyo hoja ya
kuhama hapo Kenya na kuja huku Dar,ikabidi asamehe kwanza hiyo nafasi, kwani
hata yeye alishachoka na hali iliyopo hapo, kila mtu anamnyoshea kidole yeye,
kuwa ni mke wa jinni mahaba.
Yeye mwenyewe baada ya kusoma sana na kupata mafunzo hapo,
na kukutana na mama mtaalmu mwenyewe,akajijua kuwa sio mambo ya mshetani kama
wanavyojua watu, lakini ni athari za kisaikolojia na hutaamini huyu mwanamama
alikuja hata kulifichua hilo, katika
kumsaidia huyu binti, alichimbua historia ya huyu binti ahdi akagundua chanzo
cha matatizo hayo ni nini …nakweli huyo binti akakubaliana na huyu mama kuwa
kweli chanzo cha hayo yote ni athari za
yale yaliyojijenga akilini mwake akiwa mdogo,..
‘Sasa nitaondokaje na hili tatizo ,nifanyeje mama docta…?’akamuuliza
huyo mama.
‘Kwani inavyoonekana bado akili yako inampenda huyo mtu, lakini
kwa yale uliyoyaona na kwa jinsi ulivyokuja kuona kuwa huenda mwenzako alikuhadaa,
mapenzi kwako yakaanza kuingiwa na wivu, na chuki za kutaka kulipiza kisasi, ….inawezaisiwe
kwa kutumia nguvu, lakini kwa kutaka kumuonyesha yeye kuwa ni mbaya, akili
ikawa inahagaika kutafuta njia,..na ikiwezekana umrudishe katika iel hali
mliyokuwa nayo, akili imekuwa ikimtafuta,….mwili hautaki…kunatokea mgonganoo
hapo, ‘ akasema huyo mwanamama.
‘Nakushauri kama
inawezekana jitahidi ukutanae na huyu mwanaume,au tafuta mume ambaye
ataweza kuteka nfsi yako,akuoe,..mume ambaye ataweza kukusahaulisha hayo yote yaliyojijenga
akilini mwako, muelewevu…..’akapata huo ushauri na kila mara alijaribu kukutana
na huyu mwanamama,na kwakuw akaribu naye sana, na hata aliposema anaondoka,mama
yule alimuomba sana abakie, lakini haikuwezekana.
Naomba tuwe tunawasiliana, na kama ukibadili mawazo, nitafurahi
sana,na ikibidi tunaweza tukafungua tawi huko Dar, nipi mbioni kwahilo….
******
Tukija kwenye familia yetu hii ya madakitari, ukumbuke kuwa
binti mmoja alijiengua ndani ya family ahiyo mapema, na kuja kufanya kazi huku Dar, na ushawishi huo ulitokana na
urafiki uliokuwepo kati ya binti huyu na mavulana toka Tanzania, ambaye
walikutana huko chuoni walipokuwa wakisoma Ulaya. Ingawaje walikuwa wakisoma
fani tofauti, lakini wakajikuta wakipendana…..
Na wazazi hawakuwa na pingamizi maana siku hizi watoto
wakikutana popote, na wakapendana, hakuna udadisi tena wa family ahiyo ipoje,
kuna matatizo gani ya kurithi, hayo wanasema kuwa yamepitwa na wakati, ….wazazi
wakabariki uchumba huo, na ilipifika sehemu wazazi wanataak kukutana,
ikawapeleka wazazi wa binti kusafiri hadi nyanda za ziwa. Nia na lengo ni kujua
wapi huyo mvulana anatokea.
Walipofika huko, wakajikuta kumbe asili yao ni moja. Maana
familia hiyo ya madakitari,asili yao ni huko huko mikoayaziwani,Tanzania, ila wazazi
wao walihamia huko Kenya muda mrefu na wakazaliana huko Kenya kukawa ndio
nyumbani.
Ikawa ni shangwe wenyewe walisema ng’omba karudi zizini.
Basi, ndoa ikahalalishwa na kufungwa ndoa ya kifahari, baada ya ndoa bwana yeye
alikuwa akifanyia kazi Dar, na ikabidi amfanyie mipango mke wake na yeye akafanyie
kazi huko Dar, na hapo ndipo maisha yao yalipoanzia…
‘Mimi nataka tuwekane wazi, unakumbuka wakati tupo chuoni,
kuwa mimi sitaki mambo ya kuchungwa, amri za ajabu ajabu,mimi nakuhakikishia
kuwa nakupenda, na sitakusaliti kamwe, na na wewe nataka iwe hivyo hivyo,
nakuomba sana, tuchunge misingi ya ndoa, na kama kuna tatizo tuambiane,mimi
najua sana maisha ya ndoa kinadharia na najua mengi katika mwaswala ya
mahusiano, tutasaidiana ukiwa muwazi kwangu,….’akasema mwanandoa huyu.
‘Kwani una wasiwasi gani na mimi,…mimi nakupenda, na
kilichonifurahisha ni kuwa unajua mapenzi,ila mimi ni mume wako,…unatakiwa utii
amri za mume wako, na sio ujiwekee mashari yako,haiji namna hiyo….unajua mila
na desturi zetu zilivyo,…..mume ndiye kichwa cha familia, usiniletee mamabo ya
Ulaya hapa….’akasema kiutani, lakini kumbe moyoni mwake, haikuwa ni utani.
Bwana huyu kila akikutana na wenzake, ambao walitoka pamoja
huko kijijini wakawa wanamcheka kuwa katawaliwa na mke,anafugwa,wenzao wanandoa
lakini wana uhuru, wanakutana kwenye mabar, wanakunywa ,wanabadilishana mawazo,
…..yeye kila mra yupo nyumbani, kusaidina na mkewe kupika, wakawa wanamzihaki,
na kweli kauli na maneno ya wenzake yakaanza kumteka akilini, akaona hayo
maisha anayoishi na mkewe, sio sahihi,hatayaweza, akaanza kubadilika….
‘Mume wangu unatatizo gani….’akaja kuulizwa na mkewe,ambaye
ni dakitari, dakitari anayejua mambo hayo, lakini wahenga walisema kinyozi
hajinyoi, na penye miti hapana wajenzi. Mume akaanza kujenga dharau,
mkeatakufundisha nini,mke anajua nini…
‘Mimi sina tatizo,…..kwani kuna shida gani,…?’akauliza huku
akiwa kakunja uso kiaskari.
‘Naona mabadiliko,huwi karibu na mimi tena,na huo mtindo
wakunywa pombe kupitliza umeuanzia wapi, hebu niambie una tatizo gani ili
niweze kukusaidia….’akauliza mke.
‘Nimeshakuambia sina tatizo,….kwani wewe unataka nini,mimi
ni mwanaume,natakiwa niwe huru,sio kufundikwa ndani kama mwali,…..unanielewa,…na
kazi yangu ilivyo, nahitaji kuwa hivyo,..usijifanye kwavile ni dakitari unajua
kila kitu,kwangu hujui kitu kuhusu ndoa….’akasema kwahasira na kuondoka,…
Mambo yakaanzia hapo…..
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
mambo yanazidi kuwa matamu... leo umetuonjesha tu.
Duuhh Hongera sana Ndugu wa mimi,nafurahi mnoo kuona kazi inaendela vyema, Mungu azidi kukubariki kila iitwapo leo.Pamoja daima ndugu wa mimi!!!!!!
Post a Comment