Niliambiwa kuwa nahitajika kwenda kumuoma mgonjwa kwani keshazindukana
na anahitaji kuniona mimi, nikajiandaa kwa haraka, na moja kwa moja
nikachujuliwa kwenye gari , hadi huko hospitalini, na tulipofika tulikuta walinzi,
yule dereva aliyenichukua akajitambusliha na kuonyesha ushahidi wa maandishi
kuwa kweli ni yeye, ilikuwa ni utaratibu, lakini wanamjau kuwa ni mmoja wa
dereva wao, tukaruhusiwa kupita baada ya mimi kukaguliwa mwili mzima kuwa sina
silaha yoyote.
Nikaingizwa kwenye chumba cha maalumu cha wagonjwa mahututi,
na pale nikamuona mgonjwa akiwa kalala mipira yote inayohitajika ikiwa imewekwa
mwilini mwake, nikasogea na kusimama mbele yake, alikuwa kafumba macho, baadaye
akayafumbua na kuniangalia, …kwanza aliniangalia kwa makini, halafu kama anatoa
mshangao, akasema;
‘Sasa hivi sitaki kuongea na wewe, bado najisikia vibaya,
ngoja nipumzike kidogo, nitakuona baadaye…usiondoke mbali…’akafumba macho na
mimi nikabakia nimeshangaa, maana niliambiwa kuwa huyo mgonjwa anataka kuongea
na mimi, lakini yeye mwenyewe anasema bado hajisikii vyema.
Nilisimama pale kwa muda mara akaja askari na kuniuliza kuwa
mgonjwa kasema nini, nikamwambia, mgonjwa kazungumza kwa sauti ya shida akasema
anajisikia bado anajiskia vibaya, anahitaji kupumzika kidogo, ataongea na mimi
baadaye, kwahiyo nisubiri,nisiende mbali….
Basi yule mlinzi akaniambia nikakae pembeni, kuna sehemu
wanapokaa madakitari, nikaambiwa nikae hapo nisubiri, ni chumba kidogo,ila unaweza
kuona kule kitandani.
Nilikaa pale kwa muda mrefu hadi usingizi ukanipitia, na mara
nikazindukana, ….sijui ilikuwaje ,ila nilipofumbua macho, niliangalia moja kwa
moja kule kwenye kitanda alipolala
mgonjwa, nikaona daktari kamuinamai mgonjwa,…akawa kama anamwangalia ,
akasimama na kuchunguza ile mipra
iliyokwenda hadi kwenye mashine, akasogea hadi kwenyemipira mmojawapo akaukata
na mkasi…
Nikashangaa, …akasoge kwa nyuma na kusubiri kidogo, akamwangalia mgonjwa, ambaye alikuwa kama
anatingishwa, akasoegea pembeni na mara akasogelea ile mashine ambyo mwanzoni
kwa umbali ule ilikuwa ikionyesha ile mistari ya kupanda na kushuka sasa ikawa
imenyooka, na ikawa inapiga kelele, akasogea mbali na akageuka akawa anakuja
pale nilipokuwa nimekaa, moyo ukaanza kunidunda,…
Alikuja hadi pale nilipokaa, kwa jinsi nilivyokuwa nimekaa pembeni,
hakuniona kwa haraka, alichofanya ni kuvua ile miwani yake, akawa kama
anaipangusa na kitambaa, halafu akageuka,
akaniona, alishituka, lakini akajifanya kama vile hajashituka,
aliniangalia kwa muda bila kusema kitu.Mimi kwa kiherehere change nikamuuliza;
‘Docta vipi,mbona umeukata ule mpira wa mgonjwa huoni kuwa
ndiyo inayomsadiai kupumua…?’ nikamuuliza.
Hakusema kitu, akageuka kutaka na kunitizama, huku akiwa kava miwani,
akasema ;
‘Mgonjwa alishapona, hahitaji ile mipira anampa shida….na
hayakuhusu wewe,….’akaondoka hadi mlangoni, alipofika pale mlangoni, akaataka
kamakurudi, lakini alihisi kuna matu anakuja, akageuka nakuondoka kwa haraka.Mimi
bila kupoteza muda nikaenda pale alipolala mgonjwa nikamwangalia, nilikuta
katulia kimiya, huku macho yamemtoka..
Nikarudi pale nilipokuwa nimekaa, nikaona sehemu ya simu ya
kuita dakitari nikapiga haraka, na mara dakitari akaja ;
‘Mbona kaja dakitari hapa na kukata ule mpira kwa
mgonjwa,….?’ Nikauliza.
‘Eti nini….!, dakitari, dakitari gani huyo….?’ Yule dakitari
akashangaa, akaenda pale alipo yule mgonjwa, na kuangalia, akakuta ule mpira
kweli umekatwa, akachukua simu yake na kupiga namba,mara wakaja watu wanne,
wakachunguza na baadaye , wakamfunua yule mgonjwa….
Yule dakitari wa mwanzo akaongea na mwenzake, na yule
mwenzake akaja pale nilipo na kuniambia nitoke mle ndani niende nje, maana wapo
kazini,….nikasita , kwani nilitaka kujua nini kinaendelea, lakini yule dakitari
akawa kanishika mkono na kunivutia nje,… nikatoka, na nilipofika mlangoni
nikageuka kuangalia kule kitandani, nikashangaa, na kabla sijaweza kuangalia
vyema,… yule daktari akafunga mlango haraka, nikabakia pale mlangoni, nikiwaza,
ni kweli nilivyoona au nimacho yangu tu, yanajenga hisia.
*******
Nilipotoka pale hospitalini, sikurudishwa kule kwenye mahabusu,
nilipelekwa nyumbani kwa Mkuu, waliniambia wanafanya hivyo kwa ajili ya usalama
wangu. Nilipouliza ni nani anataka kunizuru, wakasema hawataniambia hilo kwa
sasa.
Nikafika kwa Mkuu, nilikuta ulinzi mkali, nikaonyeshwa
chumba ambacho natakiwa nikae, kama mahabusu, nilijiona huru kidogo, ingawaje
niliitwa mahabusu, nikaonyeshwa kazi ambazo natakiwa kufanya kila siku,
kuhudumia bustani na kazi ndogo ndogo za hapa na pale.
Kesho yake nilichukuliwa na kwenda kule hospitalini,
nikaambiwa kuna gwaride la utambusho , natakiwa kumtambua huyo docta
niliyemuona akiukata ule mpira kwa yule mgonjwa.
‘Ukimuona utaweza kumkumbuka…?’ akaniuliza askari mpelelezi.
‘Ninaweza maana alivua miwani nikamuona vyema
usoni…’nikasema.
‘Hakikisha kuwa unamkumbuka vyema, ni muhimu sana…’akasema
huyo mpelelezi,
Basi gwaride hilo la utambulisho , likafanyika, lakini
sikuweza kumtambua huyo dakitari, hakuwepo kabisa, na wakasema zoezo hilo
limekamilika, nikaambiwa nirudi huko nilipokuwa. Zikapita siku mbili, na ya
tatu, wakaniambia kuwa nimekubaliwa kupewa dhamana, lakini sitakiwi kusaafiri
au kwenda mbali ya hili jiji. Nikashukuru sana angalau nipo huru, licha ya kuwa
nipo kwenye uchunguzi .
Siku hiyo nikiwa
nyumbani kwangu wakanijia wageni , alikuwepo mkuu, mwanadada mpelelezi na mkuu,
walisema kuwa walikuja kwangu kuna mambo wanataka kuyaweka sawa, wanahitaji kunihoji maana kesi imeshakamilika na kesho
yake itakuwa siku ya kuipeleka mahakamani, ninaweza nikahitajika. Nikasema
haina shida.
Wakili mwanadada na mkuu, wakakaa kwenye kiti, lakini wakili
mkuu, yeye alikuw akasimama, akiangalai nje, kwakupitia drishani,nilimuona kama
ana harakaya kutaka kuondoka, kinyume na wenzake, wakisema kuwa hawahitaji muda
wangu mwingi ni maswali machache ya hapa na pale.
Aliyeanza kuniuliza maswali ni mwanadada wakili, akaniuliza
, naweza kumuelezaje yule docta aliyefika siku ile kule hospitalini. Nikawaelezea
jinsi anavyoonekana, na niliwatizama wote kuangalia kuwa nani mwenye umbile
sawa nay eye, sikuweza kumlinganisha na yoyote, ila nikaona kama anakaribiana
na …, nikasema.
‘Umbo lake linakaribiana sawa kidogo kama huyo wakili wenu
mkuu…’nikasema na yule wakili mkuu akageuza kichwa na kuniangalia mra moja,
halafu akawa akageukia huko alipokuwa akiangalia, na baadaye akauliza swali
bila ya kuniangalai aaksema.
‘Una uhakika na hilo…maana ni muhimu sana kwetu…?’akaniuliza
huyo wakili mkuu.
‘Nimesema kiumbile wanakaribiana, sina uhakika zaidi ya
hilo…’nikasema.
Waliniuliza maswali mengine, na baadaye waliporizika wakaondoka,
na siku inayofuata akaja wakili mwanadada, na tukawa tunaongea mambo mengi,
baadaye akaniuliza swali ambala waliniuliza jana yake.
‘Una uhakika ukimuona huyo docta hata leo unaweza kumkumbuka
vyema..?’ akauliza.
‘Kwanini nisimkumbuke, sura yake haijanitoka, lakini kuna jambo
nataka nikuulize kwanza’nikasema.
‘Uliza….unataka kuuliza kuhusu nini, uliza tu,…?’ akasema na
kuniangalia kwamashaka huku akijaribu kutoa tabasamu,licha ya kuonekana
kukerwa, hakuwa na uso wa furaha, nikajua labdani kwasababu ya kazi nyingi.
‘Mna uhakika kweli kuwa yule mgonjwa kafariki ?’
nikauliza,na yeye akawa kama kashituka na kuniangalai bila kunjibu kwa muda
akasema;
‘Kama mgonjwa alikuwa akipumulia mshine, na ile mashine
ikaondolewa mipira kabla hajazindukana anaweza akapona…wewe mweyewe unakiri
kuwa ulipoingia ulimkuta kakodoa macho kuonyesha kuwa uhai
haukuwepo….hukumgusa,kuhakikisha ?’ akaniuliza.
‘Sikumgusa, na kweli kama mtu alikuwa akipumulia
mashine,ikiondolewa, sizani kama anaweza kupona, na kweli nilipofika pale
niliona ile mishale ya kuonyesha uhai ilikuwa imesimama, na hata mgonjwa mwenyewe alionyesha kabisa kafariki, maana
alikuwa katoa macho….lakini…’nikasema.
‘Lakini nini tena….usihisi vitu kama hivyo, unachotakiwa ni
kusema ulichokiona,sio kuhisi,…..nikuulize swali,kwanini unamashaka, na kwanini
ukaniuliza hilo swali?’akauliza wakili mwanadada, nikawaza kwa muda, nikashindwa
la kuongea, maana hisia zangu siku ile zilinisuta, nilikuwa na uhakika kabisa,
kuwa yule mgonjwa alikuwa kafariki, ingwaje sikumgusa, lakini wakati natoka pale
mlamngoni niligeuka nakaona kama yule mgonjwa alikuwa kaka kitandani akiongea
na wale madakitari, …huenda ni hisia zangu tu,…sikusema kitu tena.
‘Una mshaka gani..?’akaniuliza tena wakili mwanadada.
‘Hapana, maana hisia zangu zinanituma kama huyo mgonjwa,……hapana,
unajau mimi ninakuw ana mahisia ya ajabu,huenda ni kuchanganyikwia tu, ila
natamani nimuone huyo…hayo maiti kwa kwanza ili nihakikishe mwenyewe…..’nikasema.
‘Ina maana unataka ukaikague hiyo maiti yake uhakikishe kuwa kafa,kama unahitaji hivyo ninaweza kukufanyia
huo mpango, haina shaka,….’akasema wakili mwanadada.
‘Hapana…. sio hivyo,
..haina haja, kama wewe umethibitisha hilo, haina haja….’nikasema na kutulia
kimiya, na baadaye huyo wakili mwanadada akaondoka,na kuniambia niwe mwangalifu
katika majibu yangu, na pia niwe mwangalifu kiusalama, nisiondoke ondoke sehemu
yoyote bila kutoa taarifa. Nikasema nitafanya hivyo.
Ilikuwa usiku wa saa
sita hivi, nikiwa nimechoka sana,nilipata kibaraua sehemu, na nilifanay hiyo
kazi hadi saa kumi, nilipotoka hapo nikaenda sehemu nikapata chakula ambacho
nilikichukuliwa kama mla wa siku, na kurudi nyumbani kwangu, sikutaka kutembea
sehemu nyingine yoyote maana nilishakanywa kuwa kuna watu wanataka kuniua.
Ilipofika saa sita za
usiku, nikasikia mtu anagonga mlango, nikashituka, kwanza niliogopa kabisa kumfungulia, lakini alipoondelea kugonga, ikabidi nimuulizekuwa yeye ni nani...
‘Mimi ni askari usalama usiwe na wasiwasi….’akasema huyo
mtu, nikafungua mlango kwa mashaka.
‘Mbona unaniamusha mudakaam huu ,kuna tatizo …?’ nikamuuliza.
‘Kwasababu ni muhimu sana, na nimetoka kufuatilia mambo
fulani kuhusu hii,kesi, na nimeona kabla sijalala niwe na uhakika na jambo moja
dogo tu, usijali,na samahani kwa kukusumbua, najua unanikumbuka…’akasema ,
aliposema `unanikumbuka' nikamwangalia, sikuwa nimemwangalia vyema mwanzoni,baada ya kusema yeye ni askari usalama,nilishaju labda ni mmoja wa hawo walinzi niliowaona hapo nje.
‘Lakini muda kama huu, jamani…aaah, ni wewe tena, mimi
nilijua tumemaliza mchana,…’nikalalamika.
‘Hatuna muda maalumu kwetu, tukihitaji jambo au tukigundua
jambo, lazima tulifuatilie, na mimi nimegundua kitu, unajue pale tkupokuja
mchana kukuhoji ulinitia mashaka kidogo, angalia yako kwangu ilinitia mashaka,
ndio maana nimekuja kukuuliza vyema, nataka kuhitimisha taarifa
yangu….’akasema.
‘Sawa lakini nilisema wewe unafanana na huyo docta
kimaumbile, sio kabisa kabisa,….’nikasema na muda huo tukawa tumetizamana uso
kwa uso, na mwanga toka dirishani ukawa uammulika usoni, na kwamuda huo alikuwa
hajavaa miwani, akili yangu ikagundua kitu, sikuwahi kutizamana naye uso kwa
uso jana yake,…,laini sasa tulipoangaliana nikakumbuka na mwili ukaanza
kunisisimuka,a…..kilichoniponza ni kutokuwa mvumilivu, nikamuuliza swali;
‘Kuna ndugu yako ni docta…?’ nikamuuliza.
‘Kwanini unaniuliza hivyo…?’ akasema.
‘Kwasababu nahisi kama unafanana na yule docta, nakumbuka kabisa yule docta alipovua ile miwani,
mnaonekana kufanana naye kabisa hata sura….’nikasema.
‘Una uhakika na hilo,..? ‘ akaniuliza kwa sauti kali kidogo,
halafu akailegeza na kusema
‘Ndilo maana nimekuja kukuona tena, nilitaka kujua kuwa
kweli unakumbuka vyema,…usiwe unahisi , uwe na uhakika na hilo uliloliona,
ukihisi na kuongea kitu ambacho huna uhakika nacho utaenda jela,..mimi sio
docta, na walsinandugu docta, chunga sana mdomo wako,…’akasema na kutabasamu.
‘Una maana gani kusema hivyo,….kwani,ni…mbona… ?’nikakawa
nimeshikwa na kigugumizi, na akawa kama anataka kuondoka akasema;
‘Kwasabbu kesi itaanza kesho na wewe unatakiwa twende
ukawaangalia mdakitari wote tena kuhakikisha hilo, ili kama unaweza kumkumbuka huyo
dakitari uliyemuona…..inawezekaan siku ile hukuwa makini katika utambuslho ule,
….’akasema huyo wakili.
‘Lakini kazi hiyo nilishaifanya, na sikuweza kumuona docta
yoyote anayefanana na huyo niliyemuona…labda kama kuna mwingine kaongezeka..’nikasema.
‘Haina shaka, ….tutaona hapo kesho, tukijaliwa,….hata hivyo
naona kuna kitu kinafanyika nyuma ya mgongo wangu, tusubiri hiyo kesho, tutaona
mwisho wake….na nakukuanya tena, usiwe unajibu kutokana na hisia zako,…ukijifanya
mjanja uanongea saana, utajiponza…..haya lala salama na omba sanamungu wako…..’akasema
na kuanza kuondoka na mimi nikaongea kujikosha,hasa palenilipomuona kuwa
amekasirika.
‘Mimi ….nilisema kuhisi na kulinganisha tu muheshimiwa, sikuwa
na maana mbaya kwako wewe muheshimiwa, nilipewa hicho kibali cha kumuona huyo mgonjwa,
tu, mengine yaliyotokea mimi sikujua kuw ayatatokea, na sio kuwa ni wewe
niliyekuona…, nafafanisha tu muheshimiwa niwie radhi,kama nimekosea, nitachunga
mdomo wangu…’nikasema.
‘Haina shida….’akasema na kuondoka.
Alipoondoka yule wakili nikapokea simu, kutoka kwa wakili
mwanadada, akaniuliza kuwa nilitembelewa na nani, nikamwambia, akasema amekuja
baada ya kusikia kauli yangu kuwa huyo docta niliyemuona anafanana na huyo
wakili, aliamua kuja kuthibitisha kumbukumbu zangu kuwa una uhakika na hilo
ulilolisema,….’akasema.
‘Lakini swali mliloniuliza lilitaka nilinganishe na umbile, `anafananaje', ningejibuje bila kulinganisha na kitu ninachokiona,kosa langu hapo
lipo wapi…..?’ nikauliza.
‘Ndio maana nahitaji uwe makini katika majibu yako, sema
kile ulichokiona usijibu unavyohisi,,…sawa..kama kuna lolote bonyeza simu yako
pale nilipokuonyesha,na hakikisha humfungulia
mtu mlango kwa hivi sasa uwe makini, …
‘Lakini nakumbuka mlisema kuwa kuna walinzi wananilinda,
nanimeona walinzi hapo nje wakiwana silaha,….’nikasema
‘Ndio wapo walinzi, lakini huwezi jua, ukio na mashaka,
tumia akili yako, usiwategemee sana,, ….’akasema na kukata simu.
Sikuweza kupata usingizi, nilihakikisha kuwa nimefunga
mlango vyema , kitanda changu kipo eneo la dirishani, hapo ikanitia wasiwasi,
nilichofanya ni kuweka mito, mfano wa mtu aliyelala, nikahukua kigodoro kidogo,
na kujilaza chini ya meza yangu kubwa, ….hayo niliyafanay kutokana na zile
hisia zangu zinavyonijia.
Nilizindukana toka kwenye usingizi, ilikuwa kama saa tisa
hivi, nikahisi dirisha likiguswa, na mara nyavu za dirisha zikakatwa, sikusogea
pale nilipo, niliinua kichwa kwa mashakanakutizamadirishani ….nikasubiri.
Kwanza nilihisi labda ni wezi, lakini mbona
nimeambiwa kuwa kuna walinzi wananilinda kwa nje,nikasubiri…
Mara nikaona kitu kikijitokeza, ni kurunzi
ndogo,ikawainamulikapalekitandani, na mara
kikatokeza kitu kingine, ….moja kwa moja nikajua ni sehemu ya mbele ya
bastola, ikaelekezwa pale kitandani,…ambapo
nalala, risasa zikafyatuliwa tatu mfululizo,…..tufu-tufu tufu…., lakini hiyo
bastola haikutoa sautii, nafikiri walikuwa wameweka kitu cha kuzuia risasi, na
baadaye kimiya kikatanda.
Haikupita muda akaja, wakili mwanadada, akagonga mlango na
kujitambuslisha, na mimi nikamfungulia, akaniangalia usoni kwa mashaka na
kuniuliza nini kimtokea, nikamhadithia akasema anahisi kati ya walinzi kuna
ambao sio waaminifu, hajajua ni nani, lakini hilo watalimaza leo hii.
‘Kwa vipi….?’ Nikauliza.
‘Tumeona tukizidi kuvumilia mambo yatazidi kuwa mabaya, na
uhai wako utakuwa hatarini, tuna ushahidi wa kutosha kwa sasa, na huyo aliyekuja
kwako na kukata nyavu za dirisha alikuwa akifuatiliwa kwa karibu, nashindwa alifikaje
na kufanya hivyo, wakati wapo walinzi hapo nje….’akasema wakili mwanadada.
‘Kwani ni nani huyo….?’ Nikauliza huku nikiwaza mengi
yaliyotokea, na wakili mwanadada akaniangalia kwa makini, na kabla haongea
kitu, mara mlango ukagongwa na aliyeingia alikuwa mkuu, na yeye akanitizama kwa
uso wa wasi wasi, akaniuliza.
‘Vipi upo salama….?’ Akauliza.
‘Nalijua mlitajia mtaikuta maiti, au sio,..lakini kama
unavyoona mkuu nipo salama…ila mpaka sasa siamini kuwa nipo hai, …hapa nilipo
mwili mzima unatetemeka..’nikasema na mkuu akamgeukia wakili mwanadada nakusema;
‘Usituelewe vibaya kabisa, ….’akasema na na bila kuongeza
neno akamgeukiwa wakili mwanadada na kusema;
‘Mtu wetu katoweka,…..’akasema.
‘Unasema nini mkuu….toka muda gani, mbona sielewi, mambo
mengi yanatendeeka sivyo kinyumena tulivyopanga,….atakuwa kaendawapi huyu mtu?’
Akauliza kwa huku akiwa katoa macho ya kushangaa..
‘Nahisi keshagundua kuwa yupo matatani, …maana kulipopambazuka
tu, akawa haonekani, na simu zake zote hazipatikani, na mkewe anasema hajui
mumewe aliondoka muda gani, na hajui wapi alipokwenda, maana jana yake
walikorofishana, na kila mmoja alilala kivyake,….’akasema mkuu.
‘Ina maana wanalala chumba tofauti….?’akauliza waliki
mwanadada.
‘Wana chumba cha akiba, huwa wakikorofishana mmojawapo anakwenda kulala kwenye hicho chumba chao cha akiba,
kwahiyo yeye hakuona ajabu alipoamuka na kumkuta mumewe hayupo, ndivyo
wanavyoishi, ….ila kilichomtia mashaka ni kuona kuwa abadhi ya nguo hazipo, na
moja ya sanduku la kusafiria halipo, kuonyesha kuwa huyo mtu kaondoka
safari….’akasema mkuu.
‘Na huyo mkewe yupo wapi kwa muda huu..?’ akauliza.
‘Kashikiliwa kituoni, tunaona njia peke ya kumnasa huyu mtu
ni kumshikilia mkewe…..’akasema mkuu.
‘Hapana msifanye hivyo, muachieni na inatakiwe iwe kama
hakuna mtu anayemfuatilia, tutamnasa tu, sizani kama katoka nje ya hili jiji,atakuwa
kajificha kwenye moja ya nyumba zake ndogo, wasambaze vijana wako waaminifu….’akasema
wakili mwanadads.
‘Hilolimeshafanyika, na ….kweli tumamuachia huyo mke wake,
alikuwa nahitaji muongee na yeye,anasemani muhimu sana….’akasema mkuu.
‘Sasa kazi imeanza,ni muda wakuwa waangalifu kuliko
sikunyingine zote, na ulinzi mkali unahitajika, na tunahitaji watu watu
wanaoaminika, …kutoweka kwa huyu jamaa kunatuweka kwenye mashaka makubwa, sijui
ana mipango gani, …hapa naingiwa na mashaka kuwa lolote baya linaweza likatokea…’akasema
na kumgeukiwa wakili mwanadada na kuendelea kuongea kwa kusema;
‘Nashauri, tumuondoe huyu mtu hapa haraka, ….ni bora aje
akakae kwangu…’akasema mkuu na kabala hajaendelea kuongea nikasema kwa haraka;.
‘Hapana mimi siendi popote, ….hisia zangu hazimwamini mtu yoyote
tena, naona nitajilinda mwenyewe kuanzia sasa, maana lililotokea usiku wa leo, limenipa
fundisho,nitajua wapi pa kwenda na jinsi gani nitajilinda, nahisi sina usalaam
tena, nikiwategeema nyie….’nikasema huku nikiwa na mawazo mengi.
‘Usijali upo kwenye ulinzi, yote yanayofanyika
yanafuatiliwa kwa karibu….huo ulikuwa mtego…ila…’akasema wakili mwanadada
nakumwangalia mkuu, akitaka kusema kitu.
‘Niwaulize kama nisingelikuwa na wazo hilo la kujificha , na
kuweka mito kama mtu aliyelala, ningekuwa wapi saa hizi,….kama ni ulinzi wa
namna hiyo wa kiniweka mimi kama chambo, sikubali tena, nimechoka na matatizo,…..’nikasema
na wakili mwanadada akniangalia akionyesha uso wa kutahayari, akageuka
kumwangalia, alitaka kusema kitu, lakini mkuu akawahi nakusema.
‘Mungu yupo pamoja na wewe, tunakubali kuwa kuna kosa
limefanyika, na hilo tumeshalisawazisha, mengine ni mambo ya ndani,kama yupo
mtu nyuma ya hili tutamshughulikia, na hilo tunalifuatilia kwa karibu….ujue
kila kitu hutokea ili iwe ni sababu …na hata kama tungeliweka ulinzi wanamna
gani,kama lilipangwa kutokea lingelitokea tu,…hapa tuliweka watu, tukijua
hakuna mtu atakayefika kwako, lakini wamefika….nahisi kuna mtu anatusaliti….’akasema
mkuu huku akikwepa kuniangalia machoni.
‘Kwamtaji huo, mimi nitajilinda mwenyewe, sihitaji ulinzi
wenu tena, kwani nimegundua kuwa kil nikIutegemea ulinzi wenu, nijikuta naingia
kwenye matatizo, angalia kama leo, kama nisingejihami mwenyewe, nini ingetokea,,….’nikasema
na wote wakaniangalia huku wametahayari usoni.
NB: Tunakuja sasa kwenye hitimisho, ambapo maswali mengi yaliyokuwa ymejificha yatagundulikana, nii nanii huyo yupo yuma ya haya yote, je mgonjwa aliyekufa ni nani, na kwanini hisia za msimuliaji zinasema `hajafa' hayo namengine mengi tutakuja kuyaona. Tupo pamoja
WAZO LA LEO: Tujaribu sana kuchunga ndimi zetu hasa pale tunapohisi jambo bila kuwa na ushahidi nalo, Unaweza ukongea jambo kwa nia njema tu, kumbe ile kauli ikatafsiriwa vibaya,na matokeo yake ikaleta dhahama, kwahiyo ni bora kukaa kimiya kama huna ushahidi kuliko kuongea kutokana na hisia zako ukazusha mikangano isiyo ya lazima. kama walivyosema wahenga,bora nusu shari kuliko shari kamili.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kazi nzuri iliyoenda shule
Post a Comment