Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, March 27, 2012

Hujafa hujaumbika-11



Basi niakaanza maisha ya ndoa,maisha ambayo sikutarajia kuwa yatakuwa hivyo, mwanzoni nilijua ni swala la muda tu,maana kila mmoja anapoingia katika maisha haya anakutana na mitihani mingi, ikizingatia kuwa mumekutana kila mmoja na tabia yake, na pia kila mmoja na,hulka na hata imani tofauti,....lakini iwavyo mwisho wa siku mnakuja kukubaliana na kuwekana sawa, ndivyo nilivyokuwa najua.

Lakini nilikuja kujau kuwa mambo mengine yakijijenga ukiwa mdogo, yanweza yasiondoke kabisa akilini,....kuna watu wanajikuta wamejijenga na hulka na tabia fulani ambayo hawapendi, kuibadili, kutokana na malezi, au maisha uliyokulia, ....ndivyo alivyokuw amke wangu, na huenda ndivyo walivyo wengi, ...maana nilijitahidi kila jambo kuliweka sawa, kufundiha na kuelekeza,lakini kuna mengine nilishindwa kabisa....’akaendelea kuongea rafiki sikutaka kumkatiza, ....

Siku ya fungate iliisha nikiwa ansema huu kwa vileni mwanzo, nitamuelekeza na ayabadilika tu, nikawa namchukulia kidogo kidogo kama mtoto anayeanza kutambaa, hadi kusimama....nikukumbuka maisha aliyokulia ni yale ya kkijijini haswa, ...vitu kama umeme, maisha ya mjini na mazingira yake ni mwazo kukutna nayo....sikujali sana.

‘Sikiliza mke wangu huku ni mjini na vitu vingi ni tofauti sana, huku usitumie kuni,...na kamani lazima tutaumia mkaa, lakini sio lazima kwasababu kuna umeme....’nilimwambia siku moja akiwa kanunua kuni...tulipofika tu...

‘Mimi nimezeoa kutumia kuni...’akajitetea.

‘Hapana nitakueleekza jisni gani ya kutumia umeme,usipate taabu...’nikamwambia, lakini alijaribu kunipinga kumwingilia mambo ya jikoni, akasema mwanaume haruhusiwi kuingia huko.

‘Huku ni mjini...acaha yale mambo na tabia za kijijini,.....lakini hata hivyo usijali, kwa mfano nikuulize je ukiumwa nani atapika..?’ nikamuuliza.

‘Ni hapo nikiumwa, na utamuita ndugu yangu aje akusaidie kupika, lakini mwanaume haruhusiwi kuingia jikoni, au kushika vyombo....au kufagia ndani....sikubali kabisa,...hapo usiniingile...’akasema.

Nikasema kimoyomoyo, hujakutana na majirani, akina mama wenzako watakufundisha na ukijua hayo utabadilika tu, lakini nikumabie ukweli mke wangu huyo hakupenda kabisa kukaa na kuongea na mjirani mpaka wakawa wanalalamika, ....sikuwajali sana kwa hilo, maana ni heri kwa namna moja au nyingine.

‘Mke wangu mbona unaweka chakula cha moto kwenye jokofu....?’ nikamuuliza siku moja, kapika ugali wake vizuri na kuuweka kwenye sahani, lakini mimi nilikuwa sijawa tayari, na akaona ugali ule utapoa, mara nikashangaa unaweka ndani ya jokofu.

‘Si ili kisipoe....’akasema huku akijiamini kabisa.

‘Hapana hiyo ni kwa ajili ya kupoozea vitu, ....huoni humo kunatoka ubaridi....na ukiweka vitu vya moto, unaweza ukaliua kabisa hilo jokofu...’nikamwambia, na haraka akakitoa kile chakula. Nikawa nasema kimoyomoyo huyu atajifunza haraka tu. Lakini ilikuwa unafundisha hiki kesho hiki kimeharibiwa,....mwisho nikasema itakuwaje,maana mimi nitakwua kazini,je nani atamueleekza hiki au kile na vyombo vingi nilivyokuwa navyo ni vya umeme.

Kwa mwezi mmoja, vyombo karibu vyote vya umeme vikawa vimeharibika, na siku moja karibu nyumba nzima iungue na moto, aliwasha `heater’ kwenye ndoo kwa ajili ya maji ya kunywa akaondoka kwenda sokoni, huko akachelewa, maji yakachemka na ndoo ikayeyuka,....fikiria chumba kilikuwaje, kilikuwa kama kuna mvuke umejaa ndani, ...baadhi ya majirani wakaona moshi namvuke ukitokea ndani, ...lakini kwa muda huo mke alikuw hayupo na mlango umefungwa...

‘Sasa tufanyeje maana kunaonekana kuna hitilafu ya umeme humo ndani..na moto ukitokea hapo utatuathiri na sisi nyumba za jirani.’akasema mjumbe.

‘Tuvunje mlango....’akashauri mtu, na bahati nzuri nikatokea, nikaingia ndani..kulikuwa hakuingiliki, lakini nikazima kwenye eneo la kuzima umeme wa nyumba nzima ikawa ndio nimeokoajahazi, ...yalitoke mengi lakini yote nilijua ni kwanini,kwahiyo sikujali sana.
Kitu ambacho kilikuwa kikiniumiza sana ni tabia ambayo hakutaka kabisa kuibadili, tabia ya maisha ya ndani ya mke na mume, yeye alichukulia alivyolelewa kabla ya ndoa ndio hivyo hivyo,...mwili wake ni wake,haruhusiwi mtu kuuona,kuugusa ....vitu kama hivyo, .... nikamshauri na kumeelzsea kuhus maisha ya mke na mume, lakini aliishia kunicheka na kusema hizo ni tabia mbaya za wanaume, hazitaki kuzisikia,

Nilijaribu hata kumletea mikanda ya video ili ajifunze maisha ya ndoa yalivyo, ...alilaani na kulani, kuwa nimemletea ibilisi ndani, ...akawa hataki kabisa hata kuziangalia...

‘Mambo gani hayo ya kishetani....kama unataka kuangalia kaangalie huko huko ..mimi sitaki kuangalia, hizo picha zinazofundisha ubaya...tangu zamani nimekatazwa hayo...kama unataka kuangalia ngalai mwenyewe....’akawa anasema kwahasira.

‘Sikiliza mke wangu, maisha tunayoishi sasa ni ya mke na mume , na hayo ndiyo yanayotakiwa mke na mume wayafanye, sio mambo ya kishetani kati ya mume na mke,....’nikawa namshauri,lakini akawa hataki hata kusikiliza. Nikajiuliza nitumie ukali, labda kazoea kufokewa na kutumia nguvu, ...hapana nikakumbuka maisha aliyowahi kuishi ya kukaripiwa na kutumwa kama punda, ...sikutaka kumrudisha huko.

‘Sikiliza mke wangu, unajua wewe sio mtoto tena, wewe sio yule uliyekuwa ukitumwa kama punda,hapa unatakiwa ujitume mweneywe ujua kuwa hii nyumba na vilivyopo hapa ni vyako, na pia unatakiwa ujifunze jinsi gani ya kuishi na mume wako, mimi sio kaka yako tena, mimi sio mtu baki, mimi ni mume wako ambaye una haki zote, mwili wangu na mwili wako ni halali ya kila mmojawapo iulambiwa kipindi tunafingisha ndoa pale kwenyeule ukumbi....’nikawa natoa darasa.

‘Ule ukumbi wa gerezani kwa watu waliochanganyikiwa, ndio maana walikuwa wakiongea yale mambo yasiyofaa, ...kwasababu wanaokaa huko ni wakosaji siju na sisi tulipelekwa kwa bahati mbaya,....kama ungelifungia hiyo harusi kwenye nyumba za ibada au nyumbani usingelisikia hayo, mimi pale nilitamani kuondoka, maana watu wazima waanongea mambo machafu....’akasema na mimi hapo nikajikuta nikikumbuka siku ile ilivyokuwa....siku ya harusi ya kiaina yake.

*********

‘Jamani sio mara ya kwanza, mjue kuwa hata wafungwa wana haki zao, sio kwasababu umefungwa ndio huruhusiwi kuoa au kuolewa, ila ukioa au kuolewa, bado una majukumu yako, ya kutumikia kifungo chako, utakachobahatisha na kufunga ndoa, na mke au mume wako watakuwa wakija kukutemebelea, na tunajaribu kutafuta njia za kisheria ili mkitemebeleana kuwa na faragha kidogo...’akasema askari mmoja ambaye ni mkuu wa kile kituo, na watu wakashangilia.

Mimi kwa muda ule nilikuwa sijaelewa nini kinachoendelea maana niliamshwa asubuhi, na askari akaniambia nijiandae maana leo ndio siku yangu ya kesi, ....

‘Hapana umekosea fande sio leo...’nikamwambi nikiwa na uhakika kwani tarehe zote za kesi yangu zilikuwa kichwani.

‘Ina maana unanifanya mimi mjinga, unampinga afande, umeanza kuwa na kiburi au umeshazoea kukaa hapa ndio maana unakuwa na kiburi, uliktakwia uwe huko gereza kuu, huko ungekoma ubishi, na ulivyo laini laini, ungegeuzwa chakula cha ...’akasema yule askari huku akiniangalia kwa nyodo.

‘Afande sio kwamba nakukaidi ila nakumbuka kabisa tarehe yangu ya kesi sio leo, na siku mblili zijazo....’nikamwambia.

‘Sasa sikiliza nenda kaoge, ujiandae naenda kukuletea nguo maalumu, kuna nguo maaumu zimeshaletwa hapa, kwa ajili ya kesi yako hiyo, kama itaamuliwa vinginevyo, ujue hufiki huku tena, moja kwa moja gereza kuu..unanisikia, nakupa dakika kumi tu za kuoga,unaoga kama mwanaume, sio kujirembaremba hapa...’akasema huyo askari na kuondoka.

Mimi sikufanya ubishi nakaelekea sehemu yakuoga,na bahati nzuri kipindi hicho kulikua hakuan mahabusu wengi, hakukuwa na foleni,au ile ya kuoga kundi zima pamoja, ...nikamaliza kuoga na kutoka, ..n hat akabla sijafika kwenye chumba cha mahabusu, mara akaja yule askari akiwa kashikilia nguo.

‘Haya vaa hizi , una bahati kuwa wewe unavalishwa suti...unajau unavaa suti ili ukisimama mbele ya hakimu asione kuwa mnanyanyaswa, na hukumu ikitolewa, unabadili suti, unavaa suti maalumu za kifungwa, ndivyo ilivyo.....’akasemana kucheka.

‘Sawa fande nashukuru sana....’nikasema na kuzichukua ziel nguo...’nilishangaa ni inafanana kabisa na moja ya suti zangu nilizonunua huko Ulaya, ni hzi zilikuwa maalumi kwa ajili ya harusi......’niliiangalia ile suti nikasemakimoyomoyo, labda ni kufanana tu, nikavaa.

‘Umependeza kweli mfungwa...hata hivyo utaivaa kwa masaa, ikifika jioni utakuwa na sare maalumu, ...sare na namba yako ...unasikia mfungwa....utakuwa ukiitwa kwa namba...mfungwa namba fulani....’akasema huyo askari, ambaye kila mara anapokuja hapo anaishia kunisimanga utafikiri mimi nina kosa.

‘Sawa afande , lakini ipo siku utagundua kuwa mimi sina kosa kabisa....hayo yote ni maonevu....’nikasema nay eye aliishi akucheka.

‘Kwani mwizi au muuaji anayakubali makosa yake....sheria ndiyo itamuhukumu,lakini katu muuaji hakubali kosa lake,labda awe amechanganyikiwa....haya upo tayari, kaa pale usubiri...’akasema huyo askari na mimi nikatii na kwennda kukaa sehemu ya kusubiria wageni. Nikisubiri nini kitafuta baadaye, maana huku ni mwendo wa kusubiri,kila kitu mpaka uambiwe....

Toka asubuhi nimekaa pale hadi mchan unaingia, ...ilichosha na nikajikuta nasinzia, na mara likaja gari, gari, ni gari la mkuu wa kituo kile, likasimama,na akatoka askari aakmfungulia mkuu wake, na mara akatoka mkuu akiwa na suti yake safi, akanijia na mimi haraka niaksimama.

‘Wewe ndiye Msomali.....?’ akaniuliza.

‘Ndio mimi, mtoto wa Msomali...’nikasema.

‘Kwaini uitwe Msomali , wakati wewe ni Mtanzania...?’akauliz ahuku akinikagua na ile suti niliyovaa, ilishaanza kunipwaya, maana siku nilizokaa mle mahabusu ilikuwa ni adhabu tosha.

‘Hata mimi sijui kwanini, ila najua sisi ni Watanzania...’nikasema.

‘Nyie ndio tunawakaribisha hapa nchini halafu mnakuja kufanay vurugu...dawa yenu inachemka...’akasema kwa sauti ya kiaskari. Mimi sikujibu kitu nilitulia kimiya akamgeukia askari na kusema;

‘Huyu tunaondoka naye, kamanilivyokuambia, kila kitu kipo tayari,...’akasema na kunigeukia mimi;

‘Unasikia wewe Msomali, natakuita Mtanzanai, sitaki hilo jina la Msomali sawa....ni hivi tunakwendaleo kusikiliza kesi yako na hukumu itatolewa huko huko, ukitoka huko ama unakwenda nyumbani kwenu au unelekea gerezani, sitaki kukuoan tena kwenye mahabusu hii, .....’akasema na mara akaingia ndani ya gari.

Yule askari akanisogelea na kunisukumi kwenye gari, akasema; `haya ingia humo ndani ya gari, una bahati sana kupanda gari la mkuu....lakini ni mara ya kwanza na ya mwisho, utakuwa ukipanda lile gari kubwa lililozungushiwa nondo..kwaheri mfungwa...’akasema kufunga mlango.
Tukaondoka pale na gari likiw aan mwendo kasi, na nilishangaa, maana nilijua kwua tuanelekea mahakamani, lakini lakini ule mwendo wakasi uliishia kwenye ukumbi mmoja unaoitwa ukumbii wa magereza...na gari likasimama’

‘Haya shuka tumefika, kwani kesi yako itafanykai humu ukumbuni kwasababu za zarura...’akasema yulemkuu, nikatoka kwenye lile gari na askari mmoja akanishika mkono kuiongoza ndani ya ukumbi....

Nilishikwa na butwaa maana niliona kama naota, kwani kilichonipokea wakati naingia mle ni vigelegele na shangwe....

‘Hii maana yake nini...?’ nikauliza.

‘Kwani ukiona hivi kuna maana gani...?’ akaniuliza yule askari.

‘Kuna maana kuwa kuna harudi, au shughuli fulani....ndio najiuliza harusi ya nani?’nikauliza kwa mshngao.

‘Usijali utayajua mbele kwa mbele, wewe twende huku, maana mimi ndiye nitakuwa mlinzi wako wa karibu na pia nitakuwa mhusika wako wakaribu vile vile, ....’akaniambia yule askari akiniongoza hadi kwenye viti vilivyoopo mbele, huku nikizidi kushangaa, mbona napelekwa sehemu ile maalumu ya wageni mashuhuri, ....

Nilipokaa tu mara vigelegeel vikatanda ukumbini, na mara wakaja wakuu wa dini , wakasogea mbele yangu na mara vigelegele tena kwa shangwe na vifijo, kwani kulikuwa na watu wengine wanaingia, na kwenye kundi hilo nikamuoana binti harusi kavalishwa na kufunikwa mwili mzima...sikuweza kujua kuwa ni nani huyo bibi harusi, na ni nani muoaji...

Mara nikaitwa pale waliposimama wale watu wa dini wa kufungisha ndoa, nikasimama huku nikiwaza mengi, kwanini nihusishwe nah ii ndoa,...lakini kabla sijauliza yule muendeshaji wa shughuli akasimama na kusema;

‘Hii ni harusi ya kipeke sana, maana mtu anasubiri kuhukumiwa, ama aende jela au arusii uraioanai, alkini hukumu yake inakuwa kifungo cha ndoa.....’mara watu wakacheka na kushangailia.

‘Ndugu yetu mpendwa, kwanza tukupe pole sana na mateso ya mahabusu, ndio ukubwa huo, dunia hii kabla hujafa hujaumbika....huwezi jua, leo unaamuka mzima jioni kilema, leo unaamuka tajiri, jioni masikini, ...na pia unaweza ukaaamuka mfungwa na baadaye unakuwa bwana harusi....’watu wakshangailia.

‘Hili limefanywa kinamna, ulitakiwa kuwepo mahakamani asubuhi, lakini kwa dharura, hukuwepo ...tulifanya hivyo makudi, n ahata hivyo haikuwa haja, ...hukumu yako leo ni hapa, wewe kwa mujibu wa utaratibu, unahukumiwa kifungo cha ndoa...kazi kwenu watu wa dini mhukumuni....
Vigelegele na shangwe vikatawala ukumbini,..... na mara akanisogelea mtu wa dini na kuniuliza maswali mengi, lakini sikuwa mvumilivu, nikauliza kwanini yote haya yanafanyika na hata simjui huyo bibi harusi...

‘Humjui bibi harusi, unatucheeksah kweli,....wewe si ulitaka mwenyewe ukapendekeza kuwa unataka umuoe binto Yatima. Ukiwa huko huko mahabusu....au umesahau....’akasem yule mtu wa dini na mara akaja mjomba na ndugu zangu wengine

‘Tumefanikiwa....alikuwa keshapanda basi kuondoka kwennda kijijini....’akasema mjomba

‘Bahati kubwa sana, ingeshindikana leo ingekuwa jambo jingine, mambo yanakwenda shwari maana hata huko mhakamani wamesema hakuna tatizo, inaweza kufanyika maana muuaji keshakamatwa na kukiri kosa.

‘Ni nani huyomuuaji, aliyenifanya niteseke kiasi hiki....’nikauliza kwa hamasa

‘Hayo kwasasa hayakuhus.u la muhimu ni kufunga ndoa yako....haraka mana unahitajiwa mahakamani saa nane, kusikiliza linaloendelea kama utaendelea kushkiliwa aua utaachiwa...’akasema yule askari ambaye alikwua habanduki karibu yangu.
Na hapo moyo ukatulia na harusi ikafungwa...

*******

Nikiwa katika moja ya darasa maalumu la kujaribu kumfundisha mke wangu, na leo ilikuwa maalumu kwa kutoka, ilikuwa kazi kweli kumshauri...hasa ilipofiki sehemu kuwa akaziweke nywele zake tofauti na alivyozoea, yeye anapendelea kusuka tu,..

‘Nywele zangu haziweki hayo mauchafu..kamwe sitaki....’akasema na kukataa kata kata, lakini leo nilizamiria nikasema kwa ukali;

‘Hapana leo lazima ukabidli nywele zako kidogo, ili uone tofauti...’nikamwambia kwa sauti ya ukali kidogo. Akainua uso kuniangalia, hapo sikucheka, kama kawaida yangu, akaona kweli nimezamiria, akasema kwa upole;

‘Haya, kama ni lazima sawa,lakini sipendi kaisa,...’akasemakwa shingo upande.

‘Nikampleka kwenye saluni ya karibu, na kumuacha hapo,baadaye nikampitia kumchukua, kweli alibadilika,na nilitaka awe hivyo kwasababu tulialikwa kwenye sherehe moja, ....huwa hapendi kutoka, na akitoka huwa kajitanda khganga zake, ni nadra sana kumuona katembea kichwa wazi, ...leo nikaona nijaribu kumfanya aonekane tofauti, na kweli huko saluni walimbadili..

Kweli leo alikuwa tofauti, sio yule binti aliyekuwa kakonda, anatia huruma,...mwili wake ulishakuwa msichana mrembo, nilijaribu kumbadili hivi ili nione atakuwaje, mengi aliyakubali,

lakini kuna mengine hakukubali kata kata...na tulivyorudi kwenye hiyo sherehe tukakaa faragha huku nikijaribu kuwa karibu naye, na hata kumkumbatia,.... hakunisukuma kama alivyozoe, nik
amwambia;

‘Mke wangu u mzuri kweli, na leo umekubali ukazitenegneza hizo nywele zako umependeza kweli kweli, ....’nikamsifia.

‘Mimi nimefanya kama ulivyotaka....kwa leo tu, lakini sipendi kutengeneza nywele zangu kuwa hivi ..napenda kusuka tu, na kesho naenda kusuka, sitaki kabisa kuonekana hivi naonekana kama muhuni....’akasema huku akijiangalia kwenye kiyoo nikiwa karibu huku tunajiangalia pamoja kwenye kiyoo, kweli alikuwa tofauti, binti mrembo.

‘Unajua mnapoona mnakuwa kitu kimoja, mke na mume ni mwili mmoja, mwili wako ni wangu na wangu ni wako’nikamwambia na hapo nikawa nimemuuzi akasogea pembeni na kuongea kwa hasira;

‘Mwili wangu ni wangu sio wako,...mimi na heshimu mwili wangu, na sio wa kuitizamwa ovyo, mimi sio muhuni wa kufanya mambo ya kihuni....kama unahitaji wahuni unaweza kwenda kuwatafuta mitaani, lakini sio mimi....’nilishangaa alivyokasirika na kuondoka kufanya kazi zake za ndani.
Unajua mimi ni mvumilivu sana, na ni mwalimu mnzuri, lakini mambo mengine nilishindwa akbisa kumshawishi huyu mke wangu,yapo niliyofanikiwa , lakini sio maisha ya ndani ya mume na mke, ..mke huyu hakukubali kabisa, ....

‘Utabadilika tu ni swala la muda....’nikasemakimoyo moyo.
Muda ulipita na miaka ikapita, hakukubali kubadilika kwa maswala ya ndani, nikasema nifanyeje nitafute mwanamke aje amfunde ndani, au nifanyeje...nikaongee na shangazi yake aje amuelekeze,labda ananiogopa mimi, lakini mimi ni mume wake, nitachekwa kama nikishindwa hilo...nikawa katika mitihani kama hiyo.

Mengine hayafai hata kusema , maana ikifika usiku ilikuwa kama vioja, mwenzangu anahakikisha kuwa taa zimezimwa, kava nguo zake, na hataki umwangalie....na mambo mengine ni mshie mshike....nikajaribu kila mbinu za kumfundisha, lakini haikubadili kitu....lakini hata hivyo tukabahatika kupata mtoto, ...huta baada ya kupta mtoto tabia yake ya ndani ilikuwa hivyo hivyo, ...licha ya kuwa mambo mengine alijfunza kama kutumia umeme na kazi za ndani.

Kazini kulikuwa na sherehe za mara kwa mara, ukumbuke mimi ni meneja katika moja ya vitengo huko kazini,kwahiyo wakati mwingine nahitajika kuhudhuria sherehe na mke wangu, mke wangu hakukubali sherehe kama hizo, nilipompeleka mara moja akaona kulivyo akasema yeye hararudia tena.

‘Mke wako hatumuoni bosi,vipi ni mke wa ndani tu...’akauliza mmoja wa mabinti tuaofanya nao kazi.

‘Ana kazi zake nyingi, sio rahisi kuja kwenye sherehe zetu...’nikajitetea.

‘Basi mimi nitakuwa namuwakilisha kama hutojali...’akasema huyo binti, alikuwa binti mrembo, na kutokana na kazi zetu tukawa tumezoeaan sana, huwa kama hakuna kazi tunaongea sana mambo mengi,.....na kwahiyo tukajikuta tupo karibu sana na yeye haat ikawa tunakwenda kula pamoja na jioni nampitisha nyumbani kwake.

Wakati mwingine nilikuwa najiuliza kwanini binti mnzuri kama huyu hajaolewa, na katika maongezi yetu siku moja nikamuuliza...

‘Mimi sijawa tayari kuishi ndani kama mke, ...kuolewa sio jambo la kukimbilia, hata hivyo, kila jambo lina muda wake...’akaniambia siku moja nilipomuulizia. Na sikutaka kumdadidi sana kuhsu hilo, kwani nilikuwa nikikwepa kujiingiza mweneywe kichwa kichwa...naiheshimu ndoa yangu.

Siku zilivyozidi kwenda nikaanza tabia ya kunywa sana pombe, hii nilianza kama mchezo,ili nikirejeanyumbani, nisiwe na mawazo mengine zaidi ya kulala, sikupenda kumsumbua mke wangu, kwani jioni alionekana kuchoka sana kwasababu ya kazi za nyumbani, na kama nilivyoelezea awali, hakuwa mcheshi sana wa kuliwazana, hayo kwake aliyoaona kama uchafu, ...au uhuni kama alivyopenda kusema.

Sio kwamba nilikata tamaa ya kumfundisha, nilijitahidi lakini ndio hivyo tena, ilionekana kashikili amsioamo wake, basi ikafika mahali nikaona bora niwe naknywa sana, nikirudi simsumbue, ni kuuchapa usingizi, kumbe nilikuwa nikjiharibu bila kujua, ....maana ili ufaidi pombe , unahitajika uwe na wenzako, na vyema zaidi wakawemo marafiki wa jinsia tofauti pembeni, nilianza kama mchezo na baaadaye ikawa mazoea.

Siku moja, kwenye sherehe zetu nilikunywa sana, ...na wakati tunarejea nyumbani ikabidi nimchukue huyo binti nimpitishe nyumbani kwake, kwasababu ilikuw anjia moja, tukafika kwake, na yeye pia alionyesha kulewa , hata wakati akiteremka kweney gari langu, akawa anapepesuka, ikabidi nimsaidia kumshika mkonoo hadi nyumbani kwake anapoishia.

‘Yaani najisikia vibaya hata kupanda kitanda siwezi, naomba tafadhali unifikishe kitandani, halafu ndio uondoke..bosiii, tafadhali....’akaniomba, nikafanya hivyo,.... lakini tulipofika kitandani maombi mengine yakaongezeka.

‘Yaani unaniacha nikiwa na nguo bosi, nisaidie kunivua...viatu, gauni...na....tafadhali bosi usiondoke...siwezi kabisa kukaa peke yangu, najiskia vibaya, ...’nikakamsaidia hili likaja jingine, na hapo ilikuwa kosa,...kilichofuata hapo ni jogoo la asubuhi ndilo lililonifanya nizindukane...

‘Oh, kichwa kinaniuma...’nikalalamika huku nikishika kichwa,kweli kilikuwa kikiuma saana.

‘Pole sana mpenzi inabidi ukazimue...’sauti ya kilevi levi iliongea pembeni yangu, na niliposiki hiyo sauti, nikashituka, maana kauli na sauti kama hiyo sijawahi kuisikia toka kwa mke wangu...nikakumbuka,....nilikurupuka hapo kitandani na kumbe looh, nipo uchi wa kuzaliwa, haraka haraka nikavaa nguo, mbio nikatoka nje, ....nilifika nje gari halipo....

NB:Tuishie hapa kwa leo, lengo ni kukuonyesha jinsi nilivyoanzakubadilika na matokeayake yatakuwaje, tuwepo sehemu ijayo. Kama nilivyosema kisa hiki na mahsusi kwa wale wandoa, watarajiwa na wanaopambana na misuko suko ya ndoa...tusaidieni kwa maoni.

WAZO LA LEO: Kuuliza sio ujinga, kama unataka kweli kujua, ni ukijua fanyia utafiti kua ni kweli au sio kweli. Mara nyingi tunachukulia tetesi au mambo mengine juu kwa juu, kama zilivyo, na matokea yako


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

tunasoma visa vyako, lakini tupo maofisini, ni kwa kujiiba...hatupati muda wa kuchangia, ila tunakujali sana. mungu akuzidishie