Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, February 13, 2012

Ndoa ni kupendana sio kuumizana-2




Wakati gari linaondoka niligeuka kuwaangalia watoto wanu wakiwa wamesimama huku machozi yakiwatoka, nikajiskia uchungu mwingi, kwa mara ya kwanza nilianza kujuta, nilijona mtu mbaya sana, nikageuza kichwa haraka na kumwangalia mke wangu ambaye tulikuwa tumemlaza kiti cha nyuma, alikuwa katulia kimiya.

‘Tunakwenda hospitali ipi,...?' bosi akauliza dereva

‘Ya…ya, serikali iliyopo karibu…’ nikasema kwa kigugumizi.

Yule deerva akanielewa kuwa nimechanganyikiwa kwahiyo akachukua maamuzi mikononi mwake na kutufikisha hospitali ya Mwananyamala, tulipofika hapo docta alipomuona, akasema Muhimbili haraka…basi tukatumia taksi ile ile hadi Muhimbili, tulipofika haraka haraka mke wangu akachukuliwa chumba cha wagonjwa mahututi.

‘Sasa bosi mimi naona niondoke naomba nauli yangu, na ujua tumezunguka sana, sio elifu kumi tena….’akasema yule dereva

‘Sasa ndugu yangu unaoana hali ilivyo, nakuomba kitu kimoja, chukua simu yangu hii kama dhamana, nikija kukuleta pesa yako utanirudishia simu yangu…’nikamwambai yule dereva na kumkabidhi simu yangu, ilikuwa na gharama zaidi ya elifu themanini, lakini sikuwa na jinsi .

‘Sawa kwasababu naiona hiyo hali siwezi kukulaumu, lakini naomba kesho uniletee nauli yangu..’akasema yule dereva na kuondoka.

Nakabakia pale kusuburia , ilikuwa kila nikimuona docta akipita nasimama kumfuata kusikia nini kinachoendelea, lakini hakuna aliyenipa jibu, baadaye akaja docta na kuniita pembeni.

‘Wewe ndiye mwenye mke ……?’ akaniuliza.

‘Ndio mimi docta…’nikamwambia kwa mashaka.

‘Hatuna jinsi inabidi tunfanyie upasuaji mke wako, na hali ilivyo ni mawili, huenda tukafanikiwa, lakini ni nusu kwa nusu, tunatakiwa kumuokoa mke wako, hatujui kuhusu mtoto…..’akasema docta

‘Kwanini ….?’ Nikauliza kwa hasira

‘Kwanini tukuuulize wewe, mke alidondoka, au alikutwa na ajali gani…?’ akauliza docta na kabla sijamjibu akasema;

‘Lakini kuna tatizo jingine, kutokana na uhaba wa damu, unatakiwa utafute watu watatu wa kuchangia, kwani mkeo anahitajika kuongezwa damu….’akasema docta.

‘Sasa mimi nitawapatia wapi watu hawo….nakuomba tafadhali msaidie mke wangu….ooh, nitakuwa nimemuua mimi sasa….’nikaanza kulia huku nampigia magoti docta.

‘Huko ndio kukusaida hapa sasa hivi kuna uhaba wa damu na njia pekee ya kupata damu ni hiyo nenda kaahanaike kutafuta watu, ….vinginevyo …’hakumalizia akaondoka.

Nilijipapasa mfukoni kutafuta simu, nikajikuta nikisema kwa sauti ; `nimeibiwa simu, …..nikatoka mbio mbio hadi barabarani, nikataka kudandia gari…na lile gari lilikuwa limeanza kuondoka, likanizoa zoa, na kuanza kunibruza, ilikuwa alimanusa kupitiwa na mgudumu kichwani, …

‘Umeua , umeua,…’ndio sauti nilizozisikia kwa mara ya mwisho,…nikapoteza fahamu…alipofika hapo rafiki yangu akatulia kuniangalia kwa makini.

*******

‘Mke hapigwi kwa fimbo au ngumi, mke hupigwa kwa upande wa khanga….’ilikuwa sauti ya mtu nisiyemjua, nikainua kichwa kumtizama, lakini sikuweza kumuona sura yake, nikataka kusema kitu lakini ile sauti ikanikatisha na kusema;

‘Bado hatujakupa nafasi ya kujitetea, hapa unashitakiwa kwa kosa la kuua mkeo na mtoto mchanga, na adhabu yake ni kuuliwa mara mbili kwa sababu umeua roho mbili…’ile sauti ikasema.

‘Mke wangu hajafa..’nikajitetea

‘Una uhakika gani kuwa hajafa, sisi hapa ndio tumeishikilia roho yake, hii hapa, kama tusipomrudishia basi hana uhai, sasa wewe ndiye uliyesababisha tuipate roho yake, na roho ikifika kwetu ina maana huyo mtu keshakufa nusu, na tukipewa amri tunairisha kwake au vinginevyo tunamkabidhi muhiska na kuipeleka kuzimu..’ile sauti ikasema.

‘Naombeni sana msimuue mkea wanu maana nampenda sana, watoto watabakia na nani..’nikasema huku ninalia.

‘Sasa hivi unajifanya una Huruma, umesahau jinsi ulivyokuwa ukimpiga mke wako kama mtu anayea nyoka, hivi ukimpiga nyoka unatarajia nini, hebu tukuulize?’ ile sauti ikasema.

‘Lakini yeye sio nyoka…’nikasema.

‘Kama sio nyoka, kama sio mnyama, kama sio kiumbe kinachostahili kupigwa na kuumizwa, kwanini umpige mwenzako, na je ni hukumu gani ilipitishwa kuwa utoe kipigo kwa binadamu mwenzako, huoni ili mtu apigwe viboko, au afungwe ni lazima kuwa na mahakama, je ni mahakama gani ilipitisha kuwa umpige mwenzako, na kupiga kwenyewe ni kwa kuumiza..?’ ile sauti ikaniuliza.

‘Hakuna, ila huyo ni mke wangu, na tangu mababu wabafanya hivyo…’nikajitetea.

‘Tangu mababu walikuwa mtu akifa anazikwa na mtu mwingine aliye hai, sasa mke wako kafa utakyubali uzikwe naye..?’ ile sauti ikaniuliza.

‘Nitazikwaje kabla sijafa …’nikajitetea.
,
‘Hilo unaliogopa, wakati lilikuwa likifuatwa na mababu , lakini la kumpiga mkeo ambalo pia lilikuwa likifuatwa na mababu unalifuata kwanini uchague..?’ ile sauti ikaniuliza, nami nikakaa kimiya.

‘Unafahamu nini maana ya mke…?’ ila sauti ikaniuliza.

‘Mke ni mwanamke aliyeolewa kwa mahari..’nikasema kwa kujiamini.

‘Na mume yeye ni nani..?’ ile sauti ikaniuliza tena.

‘Ni mume aliyemuoa mke kwa mahari..’nikasema .

‘Ina maana kama hukuo kwa mahari huwezi kuitwa mke au mume…?’ ile sauti ikaniuliza.

‘Utaoaje bila mahari, ina maana mke hatakuwa na thamani kwako,…’nikasema

‘Ndugu mshitakiwa, una jingine la kujitetea kwanini umemuua mkeo na mtoto mchanga asiye na hatia, kwasababu inaonekana kitendo ulichokifanya ni kuonyesha ubabe, je wewe ungelifanyiwa hivyo ungelikubali, je kama nikichukua panga na kukata mkono wako mmoja utafurahi..?’ ile sauti ikawa inaniuliza maswali mengi, mpaka nikachoka kujibu.

‘Sikiliza nia kubwa ya kukuuliza maswali haya ni kukuonyeha kuwa nyie wanaume mna udhaifu, udhaifu huo unatokana na kujijenea himaya ambayo haipo katika ufamle wa mbingu, na matoke ayake ndiyo hayo, kwanza unakuwa huna amani, kwani kila mara moyo wako unajenga ghadhabu, pili huna amani, kwasababu mwenzako aliyetakiwa kukusaidia wakati wa raha na shida ameguka kuwa adui yako, watoto abao nip ambo la nyumba, wanakuona kama simba, hapo una raha gani, tatu unafukuza baraka ndani ya nyumba, utajiona unafanya akzi lakini wenzako wanakuona hufanyi, na utaishia kufukuzwa kazi, kwasababu huna baraka za familia, …’ na ile sauti ikafifia ..

*******

Ilikuwa siku ya tatu, ndio nazindukana, na nilipojaribu kuinua mguu , ulikuwa mzito, halikadhalika mkono, ulikuwa umebeba kitu kizito, nikaanza kuita kwa sauti;
‘Mke wangu upo wapi…’

‘Mkeo leo unamtambua mkeo, au unatak kumpiga…’ilikuwa sauti ya kike, na nilipofumbua macho nikakuta naangaliana na shemeji yangu, shemeji yangu huyu aliwahi kuja nyumbani siku moja akakuta nikimpiga dada yake, siku hiyo akataka kumchukua dada yake arudi naye kwao….

‘Jamani nisameheni, nimetubu sitarudia tena…’nikasema kwa uchungu.

‘Hahaha…nabado utatubu sana, chukua hii karatasi yako inatoka kazini kwako….’akasema sheemji yangu huyo bila hruma akanipa barua ambao nilijaribu kuifungua kwa mkono mmoja, kwani ligundua kuwa mkono wa pili ulikuwa umefungwa muhogo…na pia mguu mmoja ulikuwa nao umefungwa muhogo.

Barua ilikuwa fupi kuwa nimeukuzwa kazi kwa kuisababishia kampuni hasara ya mamilioni ya pesa, kwazni siku ya zamu yangu sikuwepo na mashine yanu niliiacha ikinguruma, imelipuka na kusababisha moto…
‘Hawa watu waongo, mimi niliondoka mashine ikiwa haifanyio kazi, kwanza siku hiyo haikuwa na umeme….’nikajitetea.
‘Uliizima, au ulisahau kuuzima,, maana nilivyosikia ni kuwa hukuizima na umeme uliporudi ikawaka ….’akasema shemeji yangu.
‘Huo uwongo wa hali ya juu, umeme ukikatika mashine inajizima yenyewe, ukirudi mpaka uiwashe tena…nani katunga huo uwongo au ni huyo jamaa toka Uhindini kwasabu hanipendi ndio maana kafanya visa hadi nikafukuzwa kazi, ole wake nikitoka hapa, nitamfuata nyumbani kwake na kumuonyesha kuwa mimi ni mwanaume…’nikasema.


Basi masiku yakapita, hadi mwaka ndio nikaanza kutembea, mke wangu naye alikuwa karudi kwao, alichukuliwa an ndugu zake pamoja na watoto. Ulikuwa mwaka wa amchungu, maana niligeuka kuwa omba omba, nikaweka kitambaa njiani kuomba ili nipate pesa ya kula, nilifanya hivyo kwa mwaka mzima, maana nilikuwa siwezi kutembea au kufanya akzi nzito.

Siku moja nikakutana na mtu nisiyemjua akaanza kunipa maisha ya matumaini , yeye ndiye alinibadilisha maisha yangu, kutoka kwenye chuki kwenda kwenye upendo. Nilikuwa kama mtu aliyezibuliwa masikio , nikautua mzigo wa dhambi, mzigo wa chuki, mzigo wa hasira ,mzigo wa visasi, nikawa mtu mpya.

‘Upendo wa dhati, kujaliana, na kuhusrumiana, ndio misini inayojenga ndoa, bila hiyo misingi ndoa haijakamilika,…’ haya ni baaadhi ya maneno yake, na mengine alisema kuwa ‘ndoa hujengwa na mke na mume, bila mshikamano ndoa hijakamilika, na furaha ya ndoa ni mashirikiano kati ya mke na mume, bila masikilizano, ushirikiano kati ya mke na mume hauwezekani…’aliniambia mtu huyu wa ajabu.

‘Mke ni sehemu ya mwili wako, kama wewe ulivyo sehemu ya mwili wake, itakuwa ni ajabu sana kama utaumiza sehemu ya mwili wako, ..unalijua hilo, je unaweza ukaukata mkono wako, unaweza ukajiumiza kwa makusudi sehemu ya mwili wako?’akaniuliza lakini hakutaka nitoe jibu kwani aliendelea kuongea kabla sijamjibi kitu, akasema;

‘Kwahiyo ukimpiga mkeo ni kama umejipiga mwenyewe, na matokeo yake utapata maumivu, maumivu hayo yanaweza yasije moja kwa moja, usiyahisi hapo hapo, yanaweza kuja kwa namna nyingine, unaweza ukakutana na mitihani ya mabalaa mbali mbali katika maisha yako, mara kazi huna , mara unashika pesa haishikiki, mara unaibiwa , yote haya ukija kuchunguza ni kwasababu hakuna upendo ndani ya ndoa yenu,…ukichunguza labda unamnyanyasa mkeo, …au hakuna maelewano vyovyote iwavyo, na kwa namna hiyo umemuumiza mwenzako,….lakini hujui kuwa hata wewe umejiumiza mwenyewe….

‘Sasa ndugu yangu kinachotakiwa ni kutubu dhambi zako, na ili utubu kiukweli nenda kamwangukie mkeo, umuombe mpaka akusamehe,…jitahidi sana maana asipokusamehe, imekula kwako, hakikisha kuwa anayasahau yale machungu uliyompatia, machungu ambayo yeye aliyapata moja kwa moja, lakini wewe yamkuja kukupata kwa namna nyingine, yamekusababishia hali uliyo nayo sasa, na usipowahi, unaweza ukapotea kabisa, …kiujumla umejiumiza mwenyewe….’akasem yule mtu na hata kabla sijamuuliza swali akapotea….

‘Akapotea akaenda wapi, kwani alikuwa ni nani, ina maana hukuwahi kumuona tena….?’nikamdadisi kwa aswali mengi kwa mpigo.

‘Ilikuwa kama mtu aliyezinduliwa kwenye usingizi mzito, wenye ndoto a kutisha maana nilipoamuamuka tu, nikainuka pale na sijui nilipataje ile nauli, nilikwenda hadi kwa ndugu wa mke wangu ambapo walikuwa wakiishi kwa hapa Dar, nilipofika sikumkuta, nikaambiwa karudi kwao na watoto….nguvu zikaniishia.

Nilihangaika nikakopa nauli hadi nikapata hela ya kutosha kunifikisha huko kijijini, nikafunga safari, hutaamini njia nzima nilikuwa nikiomba…kila maombi ninayoyajua , nikitubu hadi machozi yananitoka, na kwa ujumla safari niliiona ndefu isiyo fikika harakka, lakini hauchi hauchi kukacha, nikafika kijijini.

Nilipofika tu nikaongoza moja kwa moja nyumbani kwao mke wangu, badala ya kufika kwetu kwanza, nilipofika niliwakuta watoto wanacheza nje, wamechafuka, na waliponiona tu, wakakimbilia ndani mbio mbio, huku wakitoa macho ya uwoga, nikabakia kuduwaa, ina maana familia yangu imefikia hatua hiyo ya kuniogopa na kunikimbia, kama wameona mnyama fulani…sikukata tamaa, nikaisogelea ile nyumba, nikapiga hadi na mara akatokea mke wangu,…..

‘Samahani sana mke wangu, nisamehe kwa hayo niliyokusababishia, nakuomba uyasahau yaliyopita,sitarudia tena, ….’nikaongea kila kitu kinachostahili, na mke wangu alikuwa ananiangalia tu, kama mtu anayeangalia sanamu.

‘Umechelewa …nilikusubiri sana nikakata tamaa na nasikia kuna mtu mwingine anataka kunioa,,,tutakurudishaia mahari yako, maana ndiyo iliyokuwa ikikutia kiburi….au unasemaje…unachohitaji si mahari yako isipotee bure….?’akasema mke wangu kwa nyodo.

Nilimuomba kwa kila njia lakini sikufanikiwa, na wakati namuomba mke wangu kwa hata kupiga magoti, mara akaja ndugu yake na baadaye wazazi wake, wote wakanifukuza kama mwizi. Ikabidi niondoke pale hadi nyumbani kwetu, ambapo nilipojaribu kuwaomba ndugu zangu hawa wanisaidie kumrejesha mke wanu, wao waliniona mtu wa jabu sana, kwanini najifanya mnyonge kwa mwanamke, wakasema wapo tayari kunitafutia mke mwingine, kama nihitaji mke.

Niliwaona kama watu wasio nitakia maisha mema, nilijaribu kuwaelimisha, lakini nilionekana kuwa nimelogwa. Nikawa naishi pale nyumbani kwa unyonge, hata kula sili, na ndugu zanu waliponiona nimezamiria hivyo, wazee wa kwetu wakaenda kukutana na wazee wa mke wangu na kikao cha familia mbili kikatayarishwa na kwenye wazee hauharibiki neno, yakaja matunda mazuri, kuwa maombi yangu yamekubalika, na faini juu….

Ndugu yangu, nilibadilika, hutaamini, maana hata watoto waliniona kama baba mpya, ingawaje sio siri, ilichukua muda kuwajengea ujasiri na hata kuniamini kuwa mimi sio simba-baba, hata mimi kuna wakati nilikuwa najisahau, lakini najisahihisha hapo hapo. Nilichofanya ni kuwa karibu na familia yangu na kila kidogo nilichopata nilinunua vijizawadi kwa mke wangu, na watoto, na hapo nikajenga ukaribu na familia yangu, na kila siku kwa kufanya hivyo, tukaimarisha pendo lililopotea….

Ndugu yangu nakumbukaa siku ya kwanza nilipomletea mke wangu zawadi, hakuamini, aliwaita watoto, na wote wakaniangalia kwa mshangao, kilichofuata hapo ni mke wangu, kutoa machozi , hakuamini kuwa mimi ndio yule mume wake ambaye alikuwa akiniona tu, anachofanya ni kujiandaa kwa shari, na shari yenyewe ni kipigo..

Nikajua kweli mahaba sio yale wanayozania watu tu, mahaba ni ule ukaribu, kujaliana, kusaidiana, ..mahaba ni matendo mazuri yanayomfanya mwenzako ajisikie raha, na mwisho wake ni kilele kisichoelezeka,…ni jinsi mtakavyokuwa karibu kama ulivyowaona wale njiwa pale…..na mungu huwapa baraka, baraka katika maisha yenu na kipato chenu. Hutaamini kwani haikupita muda nikapata barua kuwa ninaitwa Dar, nahitajika nirejee , sikuamini….

Nikarejea huku Dar na familia yangu na kesho yangu, nikafika kazini, …niliambiwa uchunguzi umegundua kuwa mimi sio niliyesababisha hiyo hasara ni yule bosi wetu, alifanya makusudi kunikomoa, na sasa amefukuzwa kazi, naa kurejea kwao, na kampuni itanilipa mishahara yangu yote nilipokuwa nyumbani, na mkataba wangu utaendelea kama kawaiida. Fikiria hiyo mihela, sikutegemea, kwanu ilikuwa ni mihela, maana sikutarajia kulipwa hela hizo kwa mkupuo …nikaanza kujengea nyumba yetu…na haikuchukua muda nikapata nafasi ya kusoma…

Na nilipomaliza kusoma tu, nikapandishwa cheo, na neema ikawa inazidi kila siku ndani ya familia, na kila siku nilikuwa nikijaribu kujifunza jambo jipya la kumfurahisha mke wangu na yeye halikadhalika, ina maana kila siku kwetu ilikuwa ni fungate, na jinsi tulivyozidi kupendana, tukawa hatujui kununiana tena, hatukujua kukwaruzana tena, ….chuki , kuumizana , kununiana…ikawa historia, mke wangu akawa sehemu ya mwili kama mimi nilivyo sehemu ya mwili wake….sisi tukawa na Valentina ya kudumu siyo ya mara moja kwa mwaka.

`Rafiki yangu, mimi, kweli nimeamini kiushuhuda kuwa ndoa ni kupendana, ndoa sio kuumizana,… na ndani ya ndoa kuna siri kubwa ya mafanikio ambayo waandoa wengi wanaisahau…’ ndivyo ilivyomalizia rafiki yangu huku akiinuka kuwaangalia tena wale njiwa na huku akisema;

'Ndio maana nilipowaona wale njiwa wakionyesha upendo ambao sisi wanadamu tumeusahau, nikakumbuka mbali sana…kwaheri tukijaliwa tena…’ Akaaga rafiki yangu na kuniacha nikitafakari hayo yaliyomtokea ambayo ni fundisho kwetu kwa wenye kutafakari.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Rachel Siwa said...

Yaani kwanini umuumize kama wewe yamekushinda wachie wengine!!!!!Pamoja ndugu wa mimi!!

Yasinta Ngonyani said...

Simulizi hii hakika ni fundisho kubwa SANA kwa wanandoa na wale wanaotarajia kuwa kwenye ndoa. Bila UPENDO katika ndoa hiyo sio ndoa. Ninajiuliza hivi tangu mwanzo hakumpenda mke wake? Nimependa huu mfano wa njiwa. Maana unamfanya mtu afikirie mbali. Kazi nzuri ndungu yangu....