Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, November 30, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-55


Tukiendelea na kisa hiki, nakuomba urejee sehemu ya kwanza kabisa wakati tunaanza hiki kisa, ambapo utakuta muhusika ambaye ndiye aliyekuwa akituhadithia kisa hiki ni Maua, hatua ya hitimisha tutakutana na mhusika mwingine. Kabla ya kufika kwenye hitimisho, tutamalizia sehemu hii ambayo inaturejesha pale tulipoanzia. Kisa hiki kina hatua sita, na hatua ya saba ni hitimisho, hitimisho hili ndilo litaelezea nini hasa kilitokea, hadi kufikia hapa tulipo, kwasababu kila jambo lina chanzo chake, wengi wetuu tunapenda kuangalia juu, juu, bila kujali asili ya jambo. Mhusika mkuu ndiye atakuchukua jukumu la kuhitiisha kisa hiki, na hatujui hitimisho hili litakuwa an sehemu ngapi, tuwe pamoja,tuone

********
Vigelegele vilitanda hewani, ikimaanisha kuwa kuna shughuli , na shughuli yenyewe ni ya heri. Vigelegele hivyo vilimshitua Mua toka katika dimbwi la mawazo, na kujikuta akisema, `hivi hii ni kweli au naota, ina maana ndio naolewa tena,….oh, ndio hivyo tena nitafanyaje, yote ni mapenzi ya mungu, kama alipanga iwe hivyo, hakuna wa kumpinga, ndoto yangu ya kuwa na wajukuu na mume niliyempenda imeshayeyuka, sasa naolewa bora kuolewa, sijui, kama itabadili ile ladha ya upendo niliyokuwa nayo awali, sijui…mungu wangu nisaidie ….’akasema akajikuta akiinua mikono juu na kujifuta usoni,...

Mikono yake ilikuwa imejaa majii ya machozi, na kilichosambaa usoni ilikuwa maji ya machozi. Maua akasimama toka pale alipokuwa amekaa kwa muda, aliona ni vyema kujishughulisha na hili au lile, ….hali ile ya kubakia peke yake, alishaizoea, lakini kutokana na shughuli iliyopo mbele yake alihitajika kutokubakia peke yake, alitakiwa kuwa na mpambe wake, …lakini mpambe wake alikuwa kiguu na njia, hatulii, ana mambo mia kidogo. Kila mara alikuwa kipokea simu za wateja wake, na wakati mwingine, ailibidi aombe zarura kukimbili ajambo fulani, atachukua pikipiki ya haraka, na baada ya dakika kadhaa kesharudi, …

‘Maua hapa tumecheza bugu, huyu mpambe kweli mpambe, lakini usitie shaka, ilimradi tupo name, hakitaharibika kitu…’akasema shangazi yake aliporudi na kumkuta Maua yupo peke yake. ‘Shangazi usijali mimi hali kama hii nilishaizoea, …’akasema Maua kujikosha, lakini moyoni aliona ni bora kuwa na mtu kuliko kubaia mwenyewe, alishangaa kwanini alikuwa na waiswasi isivyo kawaida, na katika kumbukumbu zake,hakuwa na tabia hiyo, hali hiyo ilimkumba tu baada ya kuonana na huyu tajiri, tangu siku ile alipopata masaada wa gari na kuanza kuonana naye, moyoni akawani mtu wa wasiwasi .

Alipomkumbuka huyu Tajiri, mara akakumbuka tukio la jana , ni tukio ambalo liliacha gumzo mitaani, na Maua akalitafsiri kama moja ya vikwazo vya kufikia sehemu nyingine ya maisha, maisha ya ndoa ya pili. Kikwazo hiki kilimpa fundisho, ingawaje fundisho hili halikumwingia akilini, hasa ukizingatia kuwa yeye hana tabia ya kuamini mambo ya imani za giza. Alijikuta akimwanza Tajiri Papaa, hakuamini kutokana na maeno ya watu aliyosikia, kuwa tajiri huyu mkubwa angeliweza kujihusisha na mambo hayo ya kishirikina….hapana, kwake yeye alijua kuwa watu wanaojihusisha na mambo hayo ni watu masikini, watu wa hali ya chini, ….

Maua alipowaza haya, yalimfanya kuwafikiria matajiri wengi anaowafahamu ambao utajiri wao hauna tofauti na utajiri wa jamaa huyu. ‘Kama ni hivyo basi haina maana ya kuwa tajiri……’akajikuta akisema, akiwaza kuwa huenda asilimi kubwa ya matajiri ambao utajiri wao umetokea ghafla huenda wanajihusisha na mambo hayo, lakini hata hivyo, akili yake iilikuwa haikubali kusadiki hivyo, licha ya tukio la jana ambali liliganda kwenye vichwa vya kila mmojawapo kuwa tajiri Papaa utajiri wake umetokana na nguvu za giza….

Kitu cha ajabu baada ya kupata taarifa kuwa tajiri huyo kapata ajali mbaya sana , kwani alipotoka pale alikuwa kama mtu aliyepagawa, labda kutokana na kuona aibu, au kuzalilishwa, au vinginevyo, aliondoa gari lake kwa mwendo wa kasi sana, na karibu agonge watu, na alipoingia barabrani, aliendelea na mwendo huo wakasi huo wa kasi, bila kujali magari mengina na kujikuta akikosakosa kugongana na magari mengine.

‘Wewe muhuni, hujui kuendesha gari nini…,’ madereva wengine walisikika wakimtukana na wengine hata kusimamisha mgari yao pembeni na kutoka nje wakiwa na lengo la kumfuta kwa kumkimbiza kwa miguu, lakini kila aliyeliona hilo gari, kwanza alishangaa, kwani mwenye gari hilo ni mtu anayejulikana sana, na anajua kuendesha vyema, aleo imekuwaje, na wengine wakahisi huenda gari lake limechukuliwa na wezi, na huyo mwizi alikuwa akitafuta njia ya kukimbia nalo.

‘Siamini kuwa ndio yeye, lazima kuna jambo…’wengine waksema huku wakiingia ndani ya mgari yao na kondoka. Lile gari lilipofika kwene njia panda, ambapo lilitakiwa kupinda kushoto au kulia, kwani barabnra hiyo ilifika kikomo na kutengeneza matawi ya barabra mbili ya kwenda kushoto au kulia, gari hilo halikufanya hivyo, likafululiza moja kwa moja na kupanda tuta kubwa lililokuwa mbele yake. Tuta hilo lilikuwa kubwa sana, na ukilivuka hilo tuta unandokea kwenye shimo kubwa sana.Shimo hilo limetokana na uchimbaji wa kokoto, kwani eneo hilo mwanzoni lilikuwa likichimbwa kokote, baadaye likapigwa marufuku na serikali, hata hivyo kokoto zilikuwa hazipatikani tena, kwahiyo kukabakia gema kubwa sana.

Inasemekana mwazoni kulikuwa na barabara inayokatisha hapo kwenda moja kwa moja, lakini mvua na uchimbaji wa kokoto, zikaporomo hiyo barabara na ikawa haipitiki tena, na wachimbaji wa kokotoa wakaibomoa kabisa. Lile gari lilipofika eneo hilo halikugeuka kushoto au kulia, lilinyosha moja kwa moja, na kukutana na hilo tuta kubwa na mbwele yake likagonga mti wa umeme uliokuwa ambao ulikuwa pembeni kabisa la hilo shomi, na kama isingelikuwa huo mti wa umeme, gari hilo lingeserereka na kuzama kwenye hilo gema.

Kilichotokea ni hilo gari kugeuka juu chini, kichwa kikigeukia huko lilipotoka. Ule mti wa umeme uliinama lakini haukudondoka. Gari lile kwa ajili ya mwendo kasi lilipanda lile tuta kubwa na lilipogonga ule mti, likaguke juu chini, na haikuchukua muda likawaka moto. Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema ilichukua muda mchache sana kwa gari hilo kuwaka moto, na bahati nzuri, haikuchukua muda mrefu, gari la kuzima moto likawa limefika, kwani magari hayo hayapo mbali na hapo tukio lilipotokea.Gari la zima moto lilipofika liliwahi kuuzima ule moto kabla haujawa mkubwa,...

Maaskari polisi na uaslama barabrani wakawa wmaeshafika na kuanza kufanya kazi yao.
‘Afande mbona hakuna mtu humu ndani…’askari mmojawapo akawauliza wenzake.

‘Haiwezekani , hebu angalia vizuri, …”akasema mwenzake, ambaye naye alijaribu kumsaidia mwenzake kutizama ndani ya mabaki ya lie gari,lakini hawakuona dalili ya mtu au kiwiliwili cha mtu, hata walipoongezeka kuwa watatu, hawakuweza kuona chochote. Hata mashine maalumu ya kulitanua lile gari, lilipoletwa na kutanua lile gari, ili kuona vyema kwa ndani halikusaidia kitu, kwani kulikuwa hakuna dalilia ya kuwepo mtu mle ndani.

‘Hakuna mtu humu ndani, ina maana basi huyo dereva aliwahi kuruka kabla ya kutokea hii ajali…’akasema askari mmojawapo. Na hapo ikabidi waanze kazi ya kuwahoji watu, walioshuhudia hiyo ajali kuwa walimuona huyo dereva akiruka baada ya kutokea hiyo ajali au kabla hilo gari haligonga huo mti wa umeme na huenda wamuwahi kuona wapi alipoelekea.

‘Hakuna mtu aliyeruka, mimi nililiona kabisa hili gari likija, nilikuwa nimesimama hapa kwenye tuta nikalaiona hili gari likija kwa mwendo kasi, na wakati ule nilijua litapinda kushoto au kulia, lakini cha ajbu kilanyosha moja kwa moja, utafikiri lilikuwa linakuja kunigonga mimi, karibu linigonge, nikaruka pembeni na kuliangalia linavyoparamia tuta na kugonga huo mti wa umeme, likageuka juu chini na kuwa kama lilivyo hivyo, na ghafla likawaka moto…’akasema shuhuda.

‘Kwa jinsi lilivyosema kuwa lilikuwa likienda kwa kuyumayumba, ilionekana basi kulikuwa hakuna dereva ndani, lilikuwa limewashwa na kuachwa kutembea lenyewe, ….maana kama unasema lilikuwa limenyosha barabara, linakwenda kwa mwendo kasi, na kuyumbayumba, na halikujali kupinda kushoto au kulia, huoni kuwa lilikuwa linakwenda bila dereva…?akauliza askari.

‘Alikuwepo dereva, ingawaje huwezi kuona kwa ndani kwasababu limewekewa `tinted’, lakini mimi nilikuwepo kule gari lilipotokea, nilikuwa nimefika pale kumshusha mtu mmoja aliyenikodisha kwenye pikipiki yangu kufika hapo kwenye shughuli ya harusi. Nilipomshusha pale, nikawa nimesubiri, kama nitapata mteja mwingine wa kuondoka naye, na mara kukatokea mzozo…nilikuwa kwa mbali kidogo, sehemu ambapo gari hilo lilikuwa limewekwa, na mara mweney gari hilo akaja huku kazingwa na watu, na watu wengine wakawa wamelizingira hilo gari, wakiwa na nia ya kumzua huyo jamaa asipate nafasi ya kuingia kwenye gari lake…’akawa anaonge Yule mwendesha pikipiki kwa hamsa, utafikiri anatangaza mpira.

‘Mimi nikalisogeza pikipiki langu pembeni maana, isije ikaacha mlengwa na kunitio hasara, likaliwasha kabisa kutaka kuondoka, maana pia naogoap vurugu, …mara huyo jamaa mwenye gari, akiwa kifua wazi, sijui kama alikuwa akipigana na mtu,au vipi, lakini ilionekana shari limasmbaratika, kifua wazi, ….mzee mzima anaonekana akiwa katahayari, na kwa mbele nilimuona mama shughuli,…mama mmoja mashuhuri sana, akiwa anongea kwa jaziba, nafikiri ndiye aliyekuwa akipambana na huyu jamaa. Na bahati nzuri huyo jamaa akaingia ndani ya gari lake, nilimuona kwa macho yangu dereva wa hilo gari akiingia ndani na kuondoaka kwa mwendo kasi, karibu agonge watu, na mimi nikaondoka na pikipiki langu nikawa namfuatia kwa nyuma…’akasema huyo jamaa mwenye pikipiki.

‘Kwanini sasa ulimfuta nyuma, wakati unasema unaogopa vurugu, na unamfahamu mtu mwenyewe aliyeingia ndani ya hilo gari, ulimuona kabisa kwa sura yake kuwa ndiye mwenye gari..?akauliza askari huku akiandika kweney kijitabu chake.

‘Ndio , nani asiyemfahamu huyo jamaa, ni mashuhuri sana, hata wewe mwenyewe unamfahamu, huyu ni Tajiri Papaa, na aliondoka pale kwenye tukio utafikiri kuwa sio yeye, utajiri wake wote siku ile ulionekan sio wa maana, maana watu walikuwa wakiimba, ‘kumbe papaa ni mchawi…’ akasema yule mwendesha pikipiki.

‘Kwahiyo aliondoka kwa mwendo kasi kutokana na mzozano huo, na ukahakikisha kuwa kaingia ndani ya gari, ukamfuatilia kwa nyuma, na kuhakikisha kwa macho yako kuwa hakuruka….?’akauliza yule askari kwa haraka haraka, huku akiwa kama haamini yale maneno.

‘Ndio nilihakikisha kabisa akiingia ndani ya gari, shati lilikuwa limekatika vifungo, alikuwa kifua wazi, akawa kama anataka kulifunga hilo shati, lakini baadaye aliacha na kuingia ndani ya gari, nilikuwa karibu naye kabisa, akaingia ndani ya gari na kuliwasha, nimeshuhudia kwa mcho yangu mwenyewe…akaondoka nami nikamfuat anyuma,….’akasema yule dereva wa pikipiki.

‘Ulimfuatili kwa karibu karibu au ulikuwa umbali fulani ..?’akauliza skari mwingine.

‘Nilimfuatilia kwa karibu sana, maana nilikuwa na hamu ya kujua wapi aneleekea baada ya lile tukio, na hata kama angeliruka vipi ningeliweza kumuona, barabara ipo wazi…na kwa mwendo ule kama alngeliruka, tungelimkuta akiwa kavunjika vunjika barabarani….’akasema na kuonyesha kwa mikono jinsi kulivyo wazi, kuwa mtu akitoka barabrani na kukimbilia kokote ungeliweza kumuona kwa uzuri …’

‘Sasa yupo wapi, au gari lilipogonga pale kwenye nguzo labda alirushwa na kudondokea chini ya hilo bonde….?akauliza askari mwingine huku akichungulia bondeni.

‘Huko kote nimeshakagua mkuu hakuna mtu au dalili ya mtu kudondokea huko, na angerushwa vipi na kama unavyyona gari limebonyea hivi kama chapatti, lakini hakuna mlango uliofunguka na viyoo vya mbele vimevunjika kama hivi, havijatawanyika, vilelala kama chapatti, unaona vilivyo….’aksema Yule askari akionyesha vile viyoo

`Kama angerushwa kwa mbele, viyoo vingeacha uwazi, lakini angali kulivyo, hakuna uwazi huku. Hili gari ni la thahamani sana, hata viyoo vyake sio vile vya kawaida, vipo kama plastic vile, haivivunjiki ovyo, unaona vilivyo, kwahiyo kama mtu angelirushwa na kutokea mbele ya viyoo hivi vingelivunjika na kuacha uwazi, hapa hakuna uwazi, angalia na huku kwenye viyoo vya pembenei halikadhalika, ….’akawa anaonyesha askari kwa mikono huku akikagua

‘Hakuna hata tone la damu ndani ya gari….’akasema askari mwingine aliyekuwa akikagua na kuandika maelezo yake kwenye kitabu chake.

‘Haya ni maajabu, ina maana huyu mtu aliyeyuka ghafla na kupotea hewani..?’ akasema askari mwingine.

‘Huyo mwanga, nilijua tu utajiri wake wote ule ni wa kimazingara, haiwezekani akaibuka kuwa tajiri kwa ghafla vile, familia ayo naijua vyema, haikuwa na utajiri wowote, yeye kaanza na biashara ndogo tu ya genge, mara duka, mara huyo maduka, kampuni, magari..haiwezekani, kuna kitu…sasa simnaona…kapambana na waliomzidi kete…’akasema jamaa mmoja, na wale askari walikuwa wakiendelea kuandika andika mambo yao, hawakuwa na la zaidi la kuwahoji hawo watu, kwani walishaanza kuingiza mambo ambayo hayaandikiki.
Wadadisi hawakuishia hapo waliamua kwenda hadi nyumbani kwa huyo tajiri, lakini walikuta mageti yamefungwa, na wafanyakazi walipoulizwa walisema bosi wao kasafiri, hawajui kasafiri kwenda wapi na hawajui kuwa atarudi lini.

‘Kasafiri toka lini…?’akauliza mdodosai mmoja. ‘Kaaga asubuhi kuwa anasafiri, na hajarudi…’ akasema mlinzi.

‘Kwenda wapi…hamjasikia kuwa kapata ajali..?akauliza tena huyo jamaa. ‘Hatujasikia kitu kama hicho, ….’akasema huyo mlinzi , ambaye hakutaka kuhojiwa zaidi.

*********

Maua alijihisi hali isiyo ya kawaida, ilikuwa kama mtu kaleta moto ndani chumba, kkawa na joto lisilo la kawaida, akajihisi hawezi kuvuta hewa, hewa ilikuwa nzito kupita kiasi. Akaona heri asimame na kulifungua dirisha lote na hata ikiwezekana afungue na milango, akajaribu kuinua kichwa pale alipokuwa kakiegeemza kwenye sofa, lakini hakikuweza hata kutikisika, akaanza kuingiwa na wasiwasi, …

Mbona hali hii ni ya jabu kwake, inakuwaje mwili mzima unalegea, unakuwakama umepooza. Akaona ni heri amuite shangazi yake, akajaribu kutoa sauti, lakini sauti haikutoka. akiwa katulia kimiya, akimsubiri mpambe wake ambaye alitoka aliahidi kuwa atarudi muda sio mfupi, na aliambiwa sivae hilo gauni la harusi mpaka arudi.

Maua hakupendezewa, tabia ya kuvaa nguo watu wengine wakiwa wanamchungulia, lakini kwa vile ni siku maalumu, akaona asalimu amri. Yeye kwa muda huo alikuwa varandani na gauni la harusi lilikuwa limehifadhiwa vyema chumbani mwake. Na akiwa kajimpumzisha alishangaa kuona mwili mzima ukimusiha nguvu, alishangaa kuhisi mwili mzima ukilegea kila kiungo kilikuwa kama sio chake hali ili ilimshitu sana, kwani ilimkumbusha siku ili ilipomtokea, na siku ilipotembelewa na Yule tajiri, Tajiri Papaa.

Na kitu kama hisia kikamteka ubongo wake, alikuwa akiona sura ya ajabu, ile sura alishaahi kuiona, ikiwa imevaa vitu vilivyoficha sura ya Yule mtu, na safari hii, licha ya kuwa sura imejificha, lakini ilionekna kuwa ina hasira, chuki na haikuwa ina lepe la huruma,….Maua akajau leo kuna baya litatokea, na akaanza kuogopa, akajaribu kufunua mdomo kuataka kupiga ukulele,lakini mdomo ulikuwa kama sio wake, hakuweza hata kufunua sehemu yam domo, mdomo ulikuwa mkavu kupita kiasi.

Akaanza kuomba, kwani kiichobakia na ambacho kiliwezekana ni hicho peke yake, kuwa ubongo na akili na kuwaza zilikuwepo,lakini mwili peke ndio haukuweza kufanya kitu, akoamba , akaomba… Mara nyuma ya ile sura kukatokea sura nyingine kubwa sana, sura hiyo ilifunika sehemu kubwa na ile sura ya mwanzo ilionekana ndogo, …na kama ilihisi kuwa kuna kitu nyuma yake, ile sura ikagaeuka nyuma, na kuanza kutetemeka, na baadaye ikadondoka chini na kuteyuka, na ile sura ya mwanzo ikazidi kuwa kubwa na kuwa kama inafunika sehemu yote ya upeo wa macho wa Maua.

Maua lihisi kuwa sura ile alishaiona kabla lakini hakuweza kuitambua vyema, na baadaye ile sura ikapotea na ile hali ikaisha, na Maua akaweza kufunua mdomo na kujikuta akiita `shangazi….’.

Akainuka pale haraka haraka na kukimbilia mlangoni, lakini alipofika pale mlangoni badala ya kufungua mlango akajikuta akijicheka na kusema kimoyomo kuwa ni zile zilikwua kumbukumbu za uwoga kwasababu ya tukio la jana, uwoga huo ulimwingia kwasababu, habari zilizozagaa kuwa licha ya gari la huyo jamaa kupata ajali mbaya na kuungua lakini huyo jamaa hakupatikana akiwa ndani ya hilo gari. Ina mama hakufa kama watu walivyozania na alitokaje ndani ya lile gari, alipaa hewani kama mwanga, na kama alipaa hewani na kuepuka hiyo ajali, basi anaweza kuja hapo kiajabu vile vile.

Alipowaza hivyo mwili ukaanza kumuisha nguvu tena, moyo ukaanza kumwenda mbio, na kushindwa kabisa kusogea pale mlangoni alipokuwa kasimama, …safari hii hakuipa muda ile hali akaomba kwa juhudi zake zote, na mara kukawa kimiya na hali ya chumba ikawa shwari, na hewa ikawa kama kawaida, Na muda huu aliomba shangazi yake aingie haraka, ….na alipoona hata mpambe wake harudi haraka kama alivyoahidi , akaamua kuingia chumbani ambalo gauni la harusi lilikuwa limewekwa …

‘Huyu mpambe naye vipi kaeleeka wapi muda wote huu, alitakiwa tuwe naye sambamba, lakini ana pilikapilika kila mara kaitwa huku na kule kwenye pilika pilika zake….’akajikuta akilalamika peke yake.

‘Ndio ana shughuli zake, lakini sio muda kama huu, alishajitolea kwa shughuli hii, basi alitakiwa kila kiti akiweke pembeni kwanza mpaka shughuli hii iishe….’akaendela kulalamika.

Alijipa nguvu, na baadaye ile hali ikaanza kumuishia na nguvu zikaanza kumrejea tena baada ya kupumzika kidogo, ndipo akaingia chumbani kwake na kulichukua gauni lake la harusi, lililokuwa pale kitandani….

Maua akajiuliza kichwani, mbona fahamu hii hikuwepo kabla, kwani siku ya kulionunua nilikuwepo, nikasema swa hilohilo, nakumbuka niliitikia tu kwasababu kila mmoja alikubaliana nalo, rangi yake ilikuwa inakwendana na rangi yangu, mampmbo ymekaa vyema….lakini akili yangu haikuwepo kabisa. Ndipo nikakumbuka kwanini siku ile nilisita kulikubali haraka hilo gauni…licha ya kuwa nilisema sawa, lakini moyo hakuwa razi nalo…nikakumbuka.

Niliinama pale kitandani na kuliinua lile gauni, sasa nimekumbuka vyema, nikajisema kimoyomoyo, `hivi hawa watu wana maana gani kunichaulia gauni kama hili, utafikii sikuwepo wakati wa kulichagua hilo gauni….’akasema Maua huku akitabasamu.

Gauni lile lilikuwa sawasawa na guani alilolivaa Maua kwenye harusi yake ya kwanza, kwa kila kitu, utafikiri ni lille lile gauni, limechukuliwa na kurudishwa dukani, lakini Maua alikumbuka gauni lake la harusi alishalipiga mnada, aliamua kufanya hivyo, pale alipoamua na kutoa kauli kwa Maneno kuwa yupo tayari kuolewa na ye ye, …kwani ndilo lililokuwa limebakia, baadhi ya vitu vingine alikuwa kavichoma moto siku walipofanya dua ya mwaka ya kumrehemu aliyekuwa mume wake, siku ile aliamua kuchoma kila kitu kilchokuwa kikimkumbusha siku zake za nyuma, isipokuwa hilo gauni, na akalipiga mnada baadaye …

Tupo pamoja ni mimi wenu: emu-three

3 comments :

emuthree said...

Sehemu nimeiandika kwa kupitia kwenye computa ya mtu na ilivyo imekuwa vigumu kuidurufu . Natumai inasomeka.

Anonymous said...

Inasomeka mkuu lete vitu.Nikuulize ina maana ndio pale uliposema unajishikiza wamekutoa?

samira said...

m3 i hope upo ok masikini vipi wamekutowa pale dunia hii binadamu mitihani tumeumbwa nayo
mkasa mzuri tupo pamoja