Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, November 24, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-54



‘Umefuata nini nyumbani kwangu…?’ Maua aliuliza kwa hasira, huku akiwa anaogopa, maana kwa muda ule watu wengi walikuwa wametokatoka katika maandalizi ya hapa na pale, na yeye alikuwa kabakia na shangazi yake ambaye naye alimuaga muda mfupi kuwa anatoka kidogo kwenda kusikojulikana, kwani hakutaka kusema wapi anapokwenda, lakini Maua alihisi kuwa shangazi yake hatakuwa akelekea kwenye biashara zake, lazima atakuwa kaelekea kwa huyo mtu aliyekuwa akimsema….

‘Mpenzi Maua, nakupenda sana, yaani ungelijua ninavyokupenda ungenihurumia na kunipenda zaidi na zaidi, nakuhitaji sana katika maisha yangu,…tangu nisikie kuwa unaolewa na huyo jamaa ambaye hana mbele wala nyuma, moyo wangu umekuwa ukiniuma sana, kwasababu nilikutegemea wewe uwe mke wangu, …wengine waliotangulia niligundua hawanifai, sehemu hiyo ni ya kwako wewe, nikubali uje tufaidi utajiri nilio nao…’yule jamaa akawa anaongea na kusogea karibu na mlango, nia yake ilikuwa hata kupiga magoti, lakini aliogopa wapita njia kutokana na heshima yake,a kaweka mikono mbele kama mtu anayemuomba mungu wake.

Maua alianza kuingiwa na wasiwasi, …na huwa kila mra akikutana na huyu mtu moyo wake unajenga hofu, hasa pale alipowahi kumtamkia kuwa anamtaka kuwa mke wake na kumkatalia, lakini hapo akajitahid na kumwambia, ‘Hivi wewe mwanaume, una akili kweli, yaani umetoka huko kote kuja kuniambia maneno kama hayo, ….ina maana hakuna wanawake kama mimi…, eti unadai tufaidi utajiri ulio nao, utajiri utanisaidia nini kama hakuna upendo, mimi sikupendi ndio maana sitaki kuolewa na wewe…naomba tafadahli uondoek usije ukanijazia watu hapa….’akasema Maua kwa hasira.
‘Mapenzi gani kama mtakuwa mnaishi kwa shida, ..ni kujidanganya tu Maua, mapenzi ni yale yaliyopo ndani ya raha ya utajiri, kila ukitakacho kipo. Na hili nakuthibitishia kwako Maua kuwa nilishakujenegea nyumba yako mwenyewe, na hatii hii hapa,….’akatoka karatasi kumuonyesha Maua, lakini Maua hakutaka hata kuiangalia.

‘Shika uiangalia Maua, imeshaandikwa jina lako, yaani siku tukitoka kwenye kufunga ndoa tu ile nyumba ni ya kwako , ni kiasi cha kujaza haya makubaliano kuwa umekubali kuwa mke wangu, na nyumba inakuwa ni mali yako, sio nyumba tu hata gari, lipo kwa ajili yako, …gari la kwako mwenyewe, yote haya nimeyafanya kwa vile ninakupenda Maua, unataka nifanye nini ili ujue kuwa nakupenda isivyo mithilika…’yule mtu akaongea huku akisogelea karibu na lipokuwa kasimama Maua, na Maua naye alikuwa akijitahidi kuataka kuufunga mlango, lakini alihisi kama mwili unamuishia nguvu….

‘Tafadhali nakuomba usinisogelee , na …..nakuomba u…uondoke hapa karibu na hii nyumba, …’ Maua akawa anaongea kwa shida, na kushangaa kwanini anajisikia vile, akjipa moyo, na kujitutumua, huku akihsisi jasho likimtoka.

‘Hebu ondoka, naona sijisikii kuongea na wewe….kama una haja ya kushuhuida ndoa yangu ikifungwa, nenda kasimama pale uliposimamisha gari lako,kwani majibu yangu umeshayapata na ulishayapata siku nyingi, cha muhimu nenda kamtafute mwingine, wapo wengi wanaopenda utajiri, wazuri na warembo sana kuliko mimi mara mia, ….’akasema Maua kwa kujitutumua huku akimuomba mungu ampe ujasiri na kuondokana na mtihani huo na akakusanya nguvu kutaka kuufunga mlango, lakini huyo jamaa akauwahi na kuuzuia kwa mikono wake.

‘Sikiliza Maua, mbona unanifanyia hivyo, hivi kweli unamuelewa huyo jamaa unayetaka kuolewa naye,unauhakika kama siyo yeye aliyemfanya mume wako atokomee huko alikotokomea,ili akupate wewe, unauhakika kweli kuwa mume wako alikufa kwenye hiyo ajali, kama sio mbinu za huyo jamaa, yako kumfanya mume wako ndondocha , anateseka huko alipo, ili akupate wewe kirahisi….fungua macho na fikira zako, maana kama angelikuwa kafa kama wengine, ungehisi hivyo….nina uhakika kuwa moyo wako haujakubali kuwa mume wako hajafariki, niambie ukweli hapo ulipo unaamini kweli kuwa mume wako kafa…?’ akauliza yule mtu na kwamwangalia Maua kwa makini.

‘Usiniletee ushirikina wako , kwanza nasikia hata utajiri wako ni wa kishirikina, ndioa maana hukai muda mrefu na wanawake…nenda zako sitaki kusikia hayo maneno yako tena…’akasema Maua huku akiingiwa na uchungu kwa kauli ile na kujikuta machozi yakimtoka kwa wingi, hayo maneno aliyotamka huyo jamaa yakawa yakirejea ubongoni mwake kwa mfulullizo `unaamini kweli kuwa mume wako kafa…’ni kweli hajawahi kuamini hilo, na hata siku alipomtamkia Maneno kuwa yupo tayari kuolewa na yeye,alitamka tu,lakini hakuwa makini , alijiona kama msaliti…alimwangalia tena yule tajiri ambaye alikuwa bado kashikilia mlango na huku kamkodolea macho.

‘Hayo ni maneno ya watu wasiopenda maendeleo ya wengine, utajiri wangu nimeupata kwa jasho langu,na kwasababu wao ni wavivu hawataki kuhangaika, wakizania kuwa utajiri unakuja hivihivi, wanaishia kunionea wivu, wanabakia kusema maneno ya kashifa kama hayo. Maua utajiri huu nimeupata kwa shida sana na ni kikuhadithia hutaamini,…’yule jamaa akaachia ule mlango na kuegemea pembeni yake huku kageuka kuangalia gari lake.

‘Maua usione watu matajiri ukafikiri wameibuka tu ghafla, watu wanakuwa wametoka mbali, wampitia majaribu mengi, huwezi amini kuwa nimeanzia na genge, nikapanda nikashuka nikaingia kwenye duka, nikapanda nikashuka, kidogo kidogo, …nikawa nafanya bisahara za kutoka mikoani, kidogokidogo,hadi duka likapanuka, baadaye nikapata mkopo na kuanzisha kampuni ya biashara,…na sio kirahisi hivyo, ndio kama zipo njia nyingine, lakini ni miongoni mwa juhudi zangu…’akamgeukia Maua.
`Maua mengine yanasemwa sana,….lakini sifanyi kwa kumuibia mtu, nafanya kwa kutafuta , sio kwa jasho la mtu mwingine… sio jambo rahisi tu kama wanavyozania watu. Na nikuambie Maua mengina yamejitokeza nifanye pale tu nilipokuona, sijawahi kuingilia maisha ya mtu mwingine, ila imadiriki kuafanya hivyo kwa ajili ya kukutaka wewe…nimeshindwa,kuona unachukuliwa an mtu mwingine wakati nakupenda….hapana, …’akasema yule mtu na kugeukia pembeni.
‘Kwahiyo hapo una maana gani…?’akauliza Maua.

Maua sisi wanaume wengi tunahangaika kwa ajili ya warembo kama nyie….sikudanaganyi, silali kwa ajili yako, na nitajitahidi kuhakikisha kuwa unanikubali…hadi hatua ya mwisho… Ama kwa hawo wanawake nilio-oa awali na baadaye tukashindana nao, ni kwasababu hawana upendo wa zati, walikuja kwangu kwa ajili wanataka mali, nilipowapa majukumu wakashindwa…., hatukuwa tunakubaliana na mmbo mengi, na nikawatimua, nafikiri yote ni kwasababu nafasi hiyo ni ya kwako…wewe nimekuchunguza na kukugundua kuwa tunaweza tukaishi pamoja, kwanza mchapa kazi, una nidhamu, mzuri…oooh,…..’akasema huyo jamaa huku akiwa kaangalia juu, kama anajenga taswira fulani.

‘Mhh, wanaume bwana, una uhakika gani na hilo, ..kwasababu wote uliowaoa na kuwaacha wameolewa na wanaume wengine na wanaishi kwa raha mstarehe,…kweli walishindwa kwako kwa wengine waweze, sema ukweli baba una yako yasiyobebeka….’Maua akajikuta anaongea na alishangaa kwanini anashindwa kuchukua uamuazi wa kuufunga ule mlango na kuondoka, mwili ulikuwa kama umekufa ganzi…’Maua alianza kuogopa, hasa pale mawazo mabaya ambayo yanaongewa kuhus huyu mtu yalipomjia akilini.

*********
Tajiri Papaa, kama anavyojulikana, anamiliki kampuni kubwa ya kibiashara, ambayo huagiza vitu mbali mbalimbali toka nje na kuuza kwa jumla na rejareja, ana magari ya safari, mabasi kwa malori, ana taksii nyingi zilizosambaa hapa nchini, na miradi mingi sana, na hakuna asiyemfahamu kwa utajiri wake. Watu wamekuwa wakijiuliza wapi alipoupatia huo utajiri, na mwishowe wakahisi huenda kuna namna.

Wanawake wengi wamekuwa wakinaswa kwa utajiri wake huo na wengi wamejitahidi kuolewa na yeye, lakini kila aliyeolewa , hakumaliza mwaka, aliachika, na kila aliyeachika hajawahi kusema kwanini kaachika, na hakuna aliyeingiwa na wazo la kudadiisi zaidi,…na hata hivyo huyo jamaa sijui ni kwasababu ya utajiri wake, huwa hachukui muda anaoa mke mwingine haipiti muda anaacha na kuoa , na wengine wakahisi kuwa huenda nia yake sio kuoa, bali ni kuwachezea wanawake, na kuwaacha.

Siku Maua alipokutana na tajiri huyu ni kipindi ambacho alikuwa na majonzi makubwa ya kupoteza mume wake, akiwa njiani akitokea hospitalini, alikuta gari likisimama mguuni mwake, na mara akatokea jamaa mtanashati, kavalia nguo za kifahari, ana urembo wa kuvutia, akamsogelea Maua ..
‘Maua ngoja nikusogeze hadi nyumbani, najua labda hunifahamu, mimi ni Tajiri Papaa, na nakupa poel sana ya kupotelewa na mume wako, na huenda atapatikana tu, yote ni mapenzi ya mungu, na kama utahitaji msaada zaidi mimi nipo tayari kukusafirisha hadi huko Mwanza tukajaribu kuhakikisha,…’akasema huyo mti kwa moyo wa huruma.

Maua hakupenda kupata huo msaada, lakini aple alipokuwa alikuwa hajisikii vyema, na kama isingelikuwa masaada wa hilo gari asingeliweza kufika nyumbani. Alijuta kwanini alijiamini , kwani shangazi yake alimmwambia asiondoke apke yake kwenda hospitalini, lakini akasema hakuna wasiw asi, anakwenda kuchukua dawa mara moja atarejea nyumbani, lakini alipotoka hospitalini, akawa ahajsikii vyema, akajitahidi kufika kituoni, lakini usafiri ukawa wa shida, ndipo akaamua kuchukua mdogo mdogo, kama kujipa zoezi,….

Mwanzoni alitembea vizuri, lakini alipofika mbele kidogo akajihisi kizunguzungu, na moyo kumwenda mbio, akakaa kidogi kwenye mti weney kivuli, na baadaye akaanza kutembea, na alipoona kuwa hataweza, ndipo akaamua kuchukua taksi, au usafiri wowote utakaomfikisha nyumbani, inagwae alishatembea nusu ya safari, na wakati anasubiri, ndipo akatokea huyu jamaa.
Maua aliwahi kusikia sifa za huyu mtu, kwakweli anaonekana ni jamaa mkarimu,na utajiri wake ulikuwa umemvika, kwani hakujivunga kwa kuvaa vyema na hata gari lake lilikuwa ni la kifahari,

‘Maua usijal;I sana, najua hali uliyo nayo, lakini yote ni mapenzi ya mungu, cha muhimu ni kujikaza, ingawake ni kazi kubwa sana, lakini jitahidi sana,…Mhuja alikuwa mmoja wa watu niliowafahamu katika kazi zangu za biashara na nashukuru kuwa amewahi kunisadia sana, na niliposikia hilo tukio, nikasema nijaribu na mimi kutoa msaada wangu, na kama ulivyosikia mimi nilijitolea kuchangia usafairi wa ndege wa kumchukua Maneno, na nilikuwa tayari kwenda nay eye….’akasema huyo jamaa

‘Ahsante sana, nashukuru sana, nilisikia hivyo, lakini sikuwahi kukutana na wewe na kukupa ahsantezangu, mungu akubariki sana…’akasema Maua.

‘Usijali, mimi nipo pamoja na wewe na kama kuna lolote unahitaji, mimi nipo tayari kukusaidia bila matatizo, kwasababu leo kwako kesho kwangu, hayo yote hakuan anayeyaomba, na ukikwamba usikose kunipigia simu, na nitaitahidi kuwa karibu na wewe kuhakikisha kuwa hupati shida, kwasababu ya wema wa mume wako, na hata hivyo sioni kwanini wewe upate shida wakati tupo watu wenye nafasi ya kusaidia..’akasema yule mtu kwa maneno yaliyojaa huruma na Maua akamshukuru na kuteremka ndani ya lile gari la kifahari, kwani walikuwa wameshafika nyumbani kwake.

Na wakati wanaagana yule jamaa akamshika Maua mkono na kumsindikiza hadi mlangoni, na wakati anataka kuondoka, akatoa bulungutu la pesa na kumshikisha Maua mkononi huku akisema kuwa hiyo ni sehemu ndogo tu ya kuhakikisha kuwa Maua anaishi maisha bora sawa au zaidi ya alivyokuwepo mume wake. Maua alitaka kuzikataa zile pesa, akinyosha mkono kumrudishia yule mtu, lakini mara akatokea Shangazi na Maua akarudisha mkono wake ili kuzificha zile pesa zisionekane na shangazi yake na yule akaharakisha kuingie kwenye gari na kuondoka.

‘Maua yule ni nani, sio Tajiri Papaa….mungu wangu, usije ukadanganyika na utajiri wa huyu mtu, ndio ana utajiri sana, na anaonekana mrembo, lakini utajiri wake ni wa pesa chafu, na ujiulize kwanini tajiri kama yule hakai na mke, leo kaoa huyu , mara kaacha, kesho kaoa huyu , mara kaacha, kuna nini ndani ya amisha yake,….achana kabisa na mtu huyu….’akasema Shangazi yake.

‘Shangazi mbona sina mawazo hayo, yaani hii hali ya huzuni imeisha lini hadi niingie kwenye tamaa za naman hiyo, wala sikuwa na habari ya huyu mtu, alichofanya nikusaidia usafi baada ya kunikuta njiani, na akaniambia kuwa ndiye aliyesaidia katik usafiri wa Maneno kwenda Mwanza , kwahiyo nilifurahi kuwa nimemuona na kumshukuru….shangazi, mimi sitapenda mume mwingine zaidi ya Mhuja, na nitamsubiri hadi atakaporudi, najua bado yupo hai….’akasema Maua kipindi hicho hakukubali kabisa kuwa Mhuja keshapotea duniani.

Baadaye huyo jamaa hakuishi hapo, akawa kila akipata upenyo anakuja kwa Maua na kuongea kidogo na akiondoka huacha hela nyingi tu, na akaahidi kumfungulia Maua duka kubwa la biashara,, lakini kwa Maua ilikuwa ni kama mbuzii anapigiwa gita, hakuwa akimsikiliza, ila kiheshima, akawa anamkaribiosha na kuitikia yale yanayofaa kuitikiwa lakini muda mwingie, mawazo hayakuwepo hapo, na ilikuwa kama vile hakuna mtu anyeongea naye.

‘Maua nakuona kila siku nikija hapa unakuwa mbali, na inakuwa kama vile sipo, unaonaje tukisafiri nchi za nje, ili uondoe mawazo, twende kama Miami, au …Ufaransa, au ncho yoyote unayopenda, ili uondoe mawazo, unasemaje..?’akauliza huyo tajiri.

‘Hapana, nipo katika majonzi ambayo hata kama nitakwenda wapi, haitasaidia kitu, nashukuru sana kwa kuwa name katika wakati huu mgumu, na nisingependa kukuudhi kwa lolote, ila nakuomba usihangaike sana, na mimi, kwani sina chochote ninachokiona zaidi ya kumbukumbu za mume wangu, na sitaona kingine zaidi yake, nakuomba tafadhali usihangaike na mimi na kuwa na mawazo yoyote kuhus mimi…tafadahali na nitafurahi kama utaondoka tu, …’akasema Maua na siku hiyo alikataa kata kata kupokea chochote kutoka kwa huyo jamaa.

Baadaye huyo jamaa akaamua kupitia kwa shangazi mtu, kuomba kama inawezekana amuoe Maua, ilitarajiwa itakuwa hivyo, kwani shangazi alishahisi ujio wa huyo jamaa utaandamana na habari kama hiyo, shangazi hakumkatisha tamaa na alimwendea Maua kumpa hiyo taarifa…
‘Shangazi unasemaje…hivi mimi watu wananionaje….sitaki mwanaume yoyote hata awe tajiri wa kupindukia, mimi najua mume wangu atakuja…’akasema Maua na kuanza kulia.

‘Sio kwamba nimekubali hilo ombi, ila ni wajibu wangu kufikisha ujumbe, na kama nilivyokushauri awali , kuwa huyo jamaa akikuona uue kuna kuachika, sijui kwanini inakuwa hivyo, kwani wengi walioolewa na yeye na hata kuachika hakuna aliyetoa siri ya kwanini imekuwa hivyo….sisi kama wazazi tunakuombea upate mume , na tunakuomba ukubali ukweli kuwa Mhuja hayupo, ….’hayo yalikuwa maneno ya shangazi yake kipindi hicho.

Kulifuta mlolongo wa kutokuelewana kabisa kati ya Maua na huyo jamaa, kwani lifikia hatua akawa kama analazimisha na ndipo Maua akapiga marufuku kwa huyo jamaa kuja nyumbani kwake tena, lakini hakukata tamaa, mpaka Maneno akaingilia kati karibu hata ya kugombana na huyo jamaa. Na ukajengwa uadui kati ya Maneno na huyo jamaa, kwani Maneno hakuwa anapendeela ukaibu wa huyo jamaa na Maua, lakini kwa uda ule hakupenda kuingilia kwa karibu, na alipopata ile safari ya Arusha akaona ndio nafasi ya kucheza karata yake ya ushindi.

Leo jamaa huyu hapa mlangoni na kaja siku ambayo hakutaka kabisa kuonana naye na alishampiga marufuku kuja nyumbani kwake, lakini hakukoma,....

‘Wewe mwanaume, nilishakupiga marufuku usikanyage hapa kwangu, kwanini hunielewi, nakuomba tena kwa mara ya mwisho sitaki kukuona hapa nyumbani kwangu, na sasa hivi nitakuitiwa polisi maana unajifanya kiziwi….’akasema Maua.

‘Hahaha utaniitia polisi …Maua usifike huko, maana hakuna polisi anaweza kunikamata kwa kosa gani, kwa kosa la kuja kukuto9ngoza, au kukusaidia kukuzuia usiolewe na huyo hohe hahe, ili uje ukale utajiri wa bure….Maua nakupenda sana, …’akasema yule jamaa akijaribu kuufungua mlango.
‘Wewe mtu umefuata nini hapa nyumbani…?’ ilikuwa sauti ya shangazi na Maua akashukuru sana kuwa shangazi kaja ataokoa jahazi. Yule jamaa akasogea pembeni na kusalimia kwa adabu, kuonyesha kuwa ni mtu mweney heshima zake.

‘Nakuuliza umefuta nini hapa, maana nimefika kwako sijakukuta, nikaambiwa umetoka …nataka kujua kwanini hukomi kuifuta futa hii familia, tulishakukataa bado unang’ang’ania, na isitoshe unaleta mambo yako ya kishirikina ndani ya familia hii…unafikiri hatukujui….’akasema shangazi nan je watu wachache walishaanza kuja...

‘Mama tafadahli sikuwa na nia mbaya, nilikuwa kuonana na Maua mara moja, nakuomba unielewe, nilitaka tu kumkanya Maua kuwa kunikataa mimi ni kosa kubwa sana,….’akasema huyo jamaa.
‘Kwahiyo ndio umeamua kumwangiwa usiku haikutosha umeamua kuja hadi mchana na uchawi wako….sasa nakua dakika tano uwe umetoweka hapa nyumbani kwangu, la sivyo nitakuumbua….’akasema shangazi mtu.

‘Mama hayo yametoka wapi tena, mambo ya uchawi sijui, nini …nakuomba nipo chini ya miguu yako niombee kwa Maua aachane na huyo anayetaka kumuoa, aje tukaishi kw raha mstarehe…nilishamnunulia gari, nyumba….sasa hivyo vyote anaviacha kwa ajili ya huyo jamaa…mama hebu fikirieni hayo kwa makini kabla hamjafanya makosa….’akasema huyo jamaa.

‘Hivi wewe hiunielewi eeh, jamaa mnamuona huyu jamaa , utajiri wake wote ni wa kishirikina, kama mnabisha mimi nitawaonyesha….’akamsoegelea yule jamaa, na watu wengi walishakusanyika, ….kabla yule jamaa hajajua nini kitakachofuata shangazi akamshika shati la yule jamaa na kulivuta kwa nguvu, likafunguak vifungioa, na haraka kabla yule jamaa hajajua nini kinachoendelea, shangazi akakiona kile alichokitaka, akalivuta lile shati kwa nguvu na kushika kamba iliyokuwa imeonekana kuvaliwa shingoni mwa yule jamaa, akaivuta...

‘Wewe mama vipi mbona unakosa adabu, unataka kufanya nini….’yule jamaa akaanza kujitetea lakini alishachelewa, kamba ile ilivutwa kwa nguvu na kukatika, na shangazi akawa, keshaivuta na mwisho wa ile kamba lilioenekana bonge la hiriszi nyekundu….akaitupa mbali kabisa mahali waliposimama watu ili waione.

‘Mnaona hiyo…huo ndio uchawi wake wa kuwangia watu usiku…’akasema Shangazi.
Watu waliokuwepo hapo wengine walikimbia, wengine waliisogelea ile hirizi, na yule jamaa kwa aibu akaikimbilia kuiokota, mlakini watu wakaipiga teke na kwenda mbali zaidi…
Msimruhusu akaichukua, lazima tumkomeshe na uwanga wake…’watu wengine wakasema na mmojawapo akaichukua na kusema watu walete mafuta ya taa, na kweli utafikiri ilipangwa, mafuta ya taa yakapatikana haraka...

‘Jamani jamani mnataka kufanya nini….’yule jamaa akawa anahangaika kuitafuata ile hirizi yake, na alikuwa kama kachanganyikiwa, lakini hakuna aliyempa nafasi hiyo, watu walimzonga wakimzomea, `papa kumbe mwanga,papa kumbe mwanga…’na baadaye akaona aibu na kukimbilia kwenye gari lake ambapo watu walishalizunguka, na huku wanamuimbie `papa kumbe mwanga….’akapata nafasi ya kuingia kwenye gari lake huku ile hirizi yake ikitiwa mafuta tayari kwa kuiinguza, yeye haraka akaondoa gari kama mwehu, na aliondoka pale kwa mwendo kasi ajabu…..

Ile hirizi likuwa kila ikiwekwa moto haiwaki, watu wakawa wanahangaika nayo, mapaka wakatokea wazee ambao walijitambulisha kuwa wametokea kwa Maneno , wakaichukua ile hiriz na kuifungua , na baaadaye wakawasha moto , na kuungua, kulitokea harufu kali, na ikalipuka kama bomu. Na wakati hayo yakiendelea mara akaja mtu na kusema kuna ajali mbaya imetokea, gari la papa limepanda tuta la barabara na kugonga nguzo ya umeme, likalipuka…..

NB; Haya niambieni kuhusu tukio hili, je limetokea sababu ya nguvu ya giza, jamaa hatujui kuwa yupo hai au vipi, na ndoa hiyoooo, inanukia, je huko kwa akina Sweetie nako vipi, tuwepo katika mfululizo huu, na inabidi nipitie kuona kama tuhitimishe au kuna sehemu imebakia, na zaidi nategeema kutoka kwenu, nipeni maoni tuwe pamoja, kama hamtojali


Ni mimi: emu-three

7 comments :

fetty said...

hizo ni nguvu za gizaa kabisaa yaonekana huyo jamaa alikuwa mshirikina....
sasa na shangazi mtu alijuaje papaa kama alikuwa na hirizi kubwa namna hiyo hapo cha cha....
hongera kwa kazi nzuri

AMMY K or MIMI said...

tuendelee jamani usikatishe. tumalizie uhondo wote.

Anonymous said...

Duh, mbona ajabu kabisa!naomba kuuliza, huwa unatunga stori hizi saa ngapi? au ukiwa unaandika ndio hapo hapo unaendelea kupata mtiririko wa hadithi?

samira said...

m3 mimi kila siku naona hakuna ndoa kwa mauwa nahisi sweetie atajitokeza tu pili jamaa uchawi wake umemponza shangazi mzito sana tatu maneno haowi apo
wacha tuone itakuwaje

emuthree said...

Kuna mtu kaniulizia hizi stori naziandika saa ngapi. Mara nyingi naziandika asubuhi sana kabla ya muda wa kazi. Na mara nyingi ninapoanza kuandika ndipo mtiririko unakuja wenyewe kichmani si kwamba nimeandika mahali ili baadaye ninakili kwenye komputa. Nikifika hiyo asubuhi mara nyingi siandiki moja kwa moja kwenye blog naandika harakaharaka kwenye microsoft word halafu nacopy na kupaste kwenye blog.

Anonymous said...

wajua nikikumbuka kule mwanzo maua ilikuwa afunge ndoa ya pili na akaona kama mzuka wa mume wake wa zamani(Mhuja) umekuja akapoteza fahamu. Na kule tunaona mgonjwa wa Rose fahamu zimemrejea na anajua kuwa pale si nchi kwake. so tupe uhondo wa kipande kilichobaki.

emuthree said...

Samahanini kwa kuchelewesha muendelezo wa kisa hiki ni sababu zilizo juu ya uwezo wangu. Najaribu kutafuta internet cafe jirani na ninapoishi lakini bado kuna tatizo la umeme. Najikuta nipo kwenye vikwazo kila ninapotaka kuandika sehemu inayofuata. Sijakata tamaa