Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, November 16, 2011
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-50
Shangazi wa Maua alikuwa hana raha kabisa , kwani alikuwa keshajiandaa kuondoka na Maua kama walivyopanga, walikuwa wameelewana kuwa wapiti dukani wakaangalia gauni la harusi. Maua alipoipokea ile simu sauti yake iliopnyesha dhahiri kuwa kuna tatizo, na hata kabla Shangazi mtu hajauliza vyema, Maua alisema kuwa ile safari waliyopanga waifanye kesho yake maana hajisikii vyema.
‘Una umwa sana, au ni uchomvu tu, au kutojisikia vyema huko ni kwa vipi?’ akauliza shangazi mtu.
‘Sio kuwa naumwa , hapana ila sijisikii vyema tu, na naona ni bora nijipumzishe kidogo, lakini kesho tutakwenda kwasababu sina shughuli ya kufanya..’akasema Maua.
Shangazi, alivyowaza zaidi alijikuta akiyakumbuka vyema hayo mawasiliano yake na Maua, na kila alivyojaribu kuyapuuzia alishindwa. Kwa uzoefu wake, pale moyo wake unaposita kuhusu jambo fulani, na kulitilia shaka, inabidi alitizae hilo jambo kwa mapana, maana mwisho wa siku hutokea jambo ambalo anakuja kujijutia baadaye. Alikumbuka jinsi moyo wake ulivyokuwa haupendi Maua asafiri na Maneno, lakini akapuuzia na matokea yake yakatokea yale ambayo hakuyataka.
‘Ohh, nahisi kuna jambo huko kwa Maua, …moyo wangu hautilii vyema….’akajikuta akiongea pake yake na kuharakisha kumalizia shughuli zake nyingine na baadaye akapiga simu tena kwa Maua.
‘Maua kama unaumwa niambie nije huko, …’akasema Shangazi mtu.
‘Shangazi nimeshakuambia siumwi, ni hali ya akwaida ambayo hunipata mara kwa mara, lakini baadaye hutulia, nikujisikia vibaya tu, na pia nahisi labda ni uchomvu wa kazi nilizozifanya leo…’akasema Maua.
Hapo shangazi, akaingiwa na faraja kidogo, yeye alijua ni kwanini mwane anajiskia hivyo, hizo ni hatua za mwanzo, na wengine husumbuka sana, na kwa vile Maua hajajua ni nini kinachomfanya hivyo, lazima atakuwa na wasiwasi. Shangazi alivyowaza hivyo, alijiuliza moyoni mwake je ina haja ya kumfahamisha Maua nini kinachomsumbua kwa sasa ili ajihami, au bado aendelee na msimamo wake huo, wa kukaa kimiya hadi ndoa ipite..
Baadaye Shangazi akaamua kuingia kwenye miradi yake, lakini kila aliloshika huki au kile nafsi yake ikawa haitulii, mawazo yake yote yakawa kwa mwanae, …kiujumla alimpenda sana Maua hata watoto wake walifikia hatua ya kulalamika na kumuonea wivu Maua jinsi alivyokuwa akipendwa na mama yao huyo, na kudai kuwa mama yao anampendelea sana Maua kuliko wao.
‘Sio kwamba nampendelea Maua, ila hata kama nyinyi mngelikwua katika nafasi yake ningeliwatendea hivyo hivyo,….’alisema Shangazi mtu bila kuwafafanulia wanae zaidi. Hata hivyo watoto wa mama huyo hawakumchukia Maua licha ya kumuonea wivu, waliendeela kumpenda kama ndugu yao …na mara nyingi walijitahidi kuiga tabia yake, ili na wao wapendwe zaidi kama anavyopendwa yeye, …shangazi mtu alijua kuwa sio kwamba Maua ana kitu kikubwa cha zaidi kuliko watoto wake, ila alifanya hivyo, akijua dhima ya kulea mtoto wa mwenzake.Licha ya kuwa Maua ni moja wa watoto katika familia yao, lakini bado ana wazazi wake, kwahiyo lolote utakalomfanyia kinyume na hisia zake, anaweza kudai ananyanyaswa, na hili hakulipenda kabisa mzazi huyo, lakini hata hivyo, hakuacha kabisa kutimiza wajibu wake wa malezi bora.
Kutokana na tabia hii Maua alijengeka katika maadili mema, hakudeka, na kubweteka, na hata aliposafiri kwenda kwao,wazazi wake walimsifia kuwa kajengeka kimaadili, kinyume na walivyokuwa wakifikiria kuwa mtoto akikulia mjini anakuwa na tabia isiyoendana na madili yao, …
‘Namjua dada yangu hana mchezo na watoto, …’siku moja alisema baba yake Maua.
‘Ni kweli, lakini Maua usije ukajivika ngozi ya kondoo, kujifanya una tabia nzuri, kumbe kisiri siri una yako…’akamuasa mama yake.
‘Na wewe mama sasa umeanza, nitakuwa na yangu yepi, ….mimi mnavyoniona ndivyo nilivyo, sina mambo ya kujificha ficha…’akajitetea Maua.
‘Usija ukamuabisha shangazi yako, maana sisi tumeshamuamini, …kumbuka kujiheshimu kama walivyojiheshimu wazazi wako, tumeoana tukiwa hatujui mapenzi ya na tukawapata nyie ndani ya ndoa, sasa usije ukafanya kinyume chake…’akasema baba yake.
‘Na ikitokea hivyo, nitamchamba wifi kianamna yake, nitamwambia ikowapi, ..ooh, mwanangu haya ni mazungumzo tu, mengine yote yanategemea uvumilivu wako, ukumbuke duni ahii imejaa vishawsihi vya kila namna , dunia hii ina mitihani ya kila namna, lakini yote kuishinda ni kuwa na subira, ni kuwa mvumilivu…mungu atakuasaidia mwanangu..’akasema mama yake.
Shangazi mtu alipoona akili yake haitulii vyema, inakuwa na mashakamashaka kuhusu Maua, akaona ili kuondoa sintofahamu hiyo kwenye akili yake ni bora aende nyumbani kwa Maua akutane naye ana kwa ana. Huku akili yake ikimshauri kuwa ni vyema apasue jipu, maana akiliacha hivyo hivyo linaweza likasabaabisha maumivu makali, lakini je ndio wakati muafaka huo, apana, nia yake alitaka baada ya ndoa tu, ndioo ataweka mamb hadharani,…lakini hata hivyo atakuwa kakiuka maadili ya kiimani. Akawaza hilo kwa makini, mwishowe akasema ngoja afike huko na akutane na Maua na mengine yatajileta yenyewe.
Akiwa njiani alikumbuka kauli ya kaka yake kuwa ahakikishe mtoto wao haingii kwenye maswala ya kuiabisha familia yao,
‘Dada hakikisha huyu mwanetu anakulia katika msingi mema, kama akimpata mume hakikisha wanaona haraka iwezekanavyo, hatutaki mimbakabla ya ndoa…’hii ilikuwa kauli aliyopewa kabla Maua hajampoteza mume wake, na baada ya mume wake kutoweka, na kuaminika kuwa keshakufa, wazazi hawa walikutana na shangazi akapewa jukumu la kuhakikisha kuwa huyo binti haingii kweney mitego mibaya, ..
‘Kama atapata mume utuambie haraka, hakikisha wanaoana, hatutaki mipango ya kubebeshana mimba kabla ya ndoa, …’shangazi alikumbuka kauli ya kaka yake, ambaye alimuheshmu sana, na hakupenda kabisa kumuabisha.
‘Kaka mimi mnanijua vyema , malezi yangu sio ya kubahatisha…nitahakikisha anapata mume mwingine na kabla hajaharibikiwa…’alitoa kauli hii kwa kujiamini,…sasa leo mambo yameharibika , je kaka yake akijua itakuwaje, na wifi yake ambaye anatafuta mwanya wa kumta makosa….hapana hili hawatalijua mpaka ndoa ipite…akasema kimoyomoyo.
‘Lazima nikaongee na Maua mapema, asije akaumwa na kukimbilia hospitalini, najua kwa vyovyote akienda huko docta atamgundua na siri itafichuka na taaarifa hizi zinaweza zikavuja..’akawa anawaza huku akiwa na wasiwasi mkubwa.
Alikumbuka siku alipomgundu akuwa ana mabadiliko yasiyo ya kawaida , na hisia zake zilimfanya amuulize Maua.
‘Maua hivi upo sawa,kweli hebu niambie una miezi mingapi kabla hajaziona siku zako…’alikumbuka siku alipomuulizia Maua baada ya kumuhisi kuwa hayupo sawa.
‘Shangazi nawe, kwani nina mabadiliko, gani, mbona kuumwa huk nimeanza tangu mume wangu alipopotea, na kuziona siku zangu sio tataizo huwa naweza hata kufika miezi mitatau na hata nikipmwa naonekana sina ,…ujauzito….kwanini niwe mjauzito, kwa mimba ya nani,,,,shangazi naona unanichuria….’akasema Maua.
‘Kama nikujichuria unajichuria mwenyewe, kwa matendo yako, na mabadiliko ya mwili …wewe hujioni, lakini sisi wenye uzoefu tuemshaliona hili,….itabidi twende ukapime…’ akasema shangazi mtu.
‘Shangazi mbona unaniwazia vibaya hivyo, nina mimba itoke wapi, ….shangazi ,kama sina ujauzito utanipa nini, tupinge shangazi,,,,’akasema Maua kwa utani.
‘Kama unao nitakupa mume haraka iwezekanavyo… kama huna nitakununulia zawadi nzuri sana…’akasema shangazi mtu, huku moyoni akiwa na mashaka na mabadiliko ya mtoto wao huyu.
‘Zawadi gani, ujue hiyo ni ahadi,,,,?’akauliza Maua kwa hamasa.
‘Nitakununulioa mkufu wa dhahabu utakaouvaa siku ya haruisi yako…lakini kama una ujauzito sijui nitauweka wapi uso wangu…’akasema shangazi, kipindi hicho Maneno alikuwa hajakubaliwa kumuoa Maua.
‘Haya shangazi we uandae kabisa huo mkufu wa dhahabu, sina wasiwasi…na usiwe na wasi wasi na mimi, umeniela mwenyewe, siwezi kabisa kukuangusha kama ni mimba nitaipatia ndani ya ndoa….’akasema Maua huku akiwa akikumbukia siku moja walibishana na mume wake kuhusiana na hilo na hata kuahidiana, mumewe alimwambia kama ataambiwa safari hii ana ujauzito atamnunulia gari…
‘Utaninunulia gari, unasema kweli mume wangu…?’akauliza Maua.
‘Nasema ukweli,…’akasema mume wake, na siku hiyo walipokwenda kupima na kuambiwa kuwa hakuna ujazuzito, Maua akakata tamaa kabisa ya kupata mimba.
‘Maua mbona mapema sana kulifikiria hilo, ilimradi docta kasema hakuna mwenye tatizo kati yetu, basi ni swala la muda , siku mungu akpenda tutatapata mtoto, bado mapema sana kukata tamaa, hilo wala lisikutie mashaka…’akasema mume wake.
‘Sawa mume wangu unafikiri kinachoumiza ni nini, mimi kama mimi naweza kusema ipo siku, navuta subira, lakini tatizo ni wapambe, watu baki, hawakupi muda huo, kila mkiongea, hivi wewe utapata mtoto lini, …hivi wewe vipi…’akasema Maua
‘Hawo usiwajali, mungu kawapa midomo ya kuongea, na huwezi kuwazuia, cha muhimu ni sisi wenyewe kuwa na moyo wa dhati, kuwa ipo siku tutampata mtoto,….unajau Maua nakupenda sana, sipendi kabisa nione unanyong’onyea kwa jambo hilo, …usijali mpenzi…’akasema mume wake.
‘Nashukuru sana mume wangu kwani umenipa faraja kubwa, nakupenda sana mume wangu na nitajitahidi sana kutowajali wapambe, …wewe ni faraja la moyo wangu, namuomba mungu asitutenganishe,…maana sijui nitaishije…’akasema Maua.
‘Mungu mkubwa, tupo pamoja mpenzi wangu…’akasema Meme wake, na maneno haya akiyakumbuka Maua yanamtonesha sana moyo wake, haamini kuwa ndio hivyo tena, mume aliyemepnda hayupo tena duniani. Na siku alipoongea an shsngazi yake kwa maneno yanayofanana yay ale aliyoahidiana na mume wake, kwa utani ule ule aliowahi kufanya na mume wake, moyo wake ulikumbuka mbali sana…na kwa minajili hiyo, ya kukata miezi mitatu bila kuona siku zake hakuwa na wasi wasi wowote kuwa ni mja mzito.
‘Na dalili kama hizi nilishaziona wakati nipo na mume wangu, ….sioni haja ya kwenda kupima….’Alimwambia shsngazi yake siku alimpomshauri kufanya hivyo.
Leo akaamuka vibaya, akawa hajisikiii vyema na hata safari aliyoipanga na shangazi yake ya kwenda kuangalia gauni la harusi akaiona haina maana, …akaamua kuahirisha kila kitu na bila kumwambia mtu akaondoka kueleka huko hospitaini,…lakini nian sio kuchunguza kuwa ana ujauzito, hilo hakuliwekea maanani, nia yake ilikuwa kujiangalia mwili wake kwa uumla, kwanini anajisikia vibaya kiasi hicho, huenda kuna tatizo jingine….hakuamini pale alipoambiwa kuwa ana ujauzito, na hapo taswira ya shangzi yake akiwa na hasira ilitanda usoni mwake, akajua sasa ana kesi ya kujibu, sasa …..
*******
Shangazi alipofika kwa Maua alikuta mlango umefungwa, akauliza majirani, wao waksema wamemuona akitoka, lakini hakusema anaeleeka wapi,….Shangazi akahamaki, akatoka mbio, na kuchukua taksi, alishajua kuwa Maua lazima atakuwa kaamua kwenda hospitlini, na taksi ilipemeleka moja kwa moja hadi hospitali yao wanayotibiwa mara kwa mara, huko akaambiwa hayupo. Akapiga simu yam AUA ilikuwa inaita tu haipokelewi.
‘Sasa atakuwa kaenda wapi Jumapili hii,leo hana akzi, …na mara nyingi huwa hatoki nyumbani..’akawa anajiuliza na wakati anatafakari hili akaumbuka jambo, na bila kusema kitu akaingia kwenye taxi nyingine, ilipofika njiani ikakutana nafoleni kubwa sana, …akawa analaani,na shinikizo la damu likawa linamapnda kwa wasiwasi.
Alichofanya ni kutoka kwenye ile taksi na kuchukua pikipiki, na kabla hajachukua hiyo pikipiki akapiga tena simu na safari hii alimpata Maua, …hakusikilizana naye vyema kwasababu ilikuwa barabarani, mingurumo ya magari, na makelele, lakini hata hivyo alimpa maneno amabayo kama atayafikiria haatweza kufanya hilo jambo alilozania kuwa huenda Maua anataka kulifanya, ilibidi amwambie ukweli, akamwambia mweney pikipiki atafute njia za mikato, na wakaingia vichochoro na baadaye wakatokea barabara kuu, walipokuwa waaningia barabara kuu, wakakutana na gari la Maneno, likasimama.
‘Shangazi unakwenda wapi haraharaka hivi, na pikipiki, nakumbuka uliniambia kuwa wewe hupatani na pikipiki, leo imekuwaje, au ndio hiyo foleni imekuponza…?’akauliza Maneno.
‘Ukiona hivyo ujue kuna jambo, kuna sehemu nawahi kidogo, sasa nilipofika hapo nyuma, nikakuta foleni kubwa, basi nikachukua pikipiki…lakini..’akasema Shangazi mtu akitafuta mwanya wa kumkwepa Maneno, lakini haikuwezekana.
‘Basi njoo nikuwahishe huko unakokwenda, …’akasema Maneno na kumuulizia yule mwenye pikipiki anadai kiasi gani, na hata kabla Shanagzi hajasema lolote, akawa keshamlipa mtu wa pikipiki na shangazi akawa hana jinsi ila kukubaliana na Mkwe wake mtarajiwa, na akaingia kwenye gari la Maneno.
‘Shangazi nina jambo nilitaka kukuulizia, maana nimefika kwa Maua sijamuona, na kama tulivyoahidiana leo ilikuwa siku ya kwenda kuangalia gauni la harusi, au mlishabadili siku ya kwenda huko, niliona nimpitie nimchukue halafu nije kwako …kwasabaabu gari lipo kwanini mhangaike na usafiri mwingine, sasa nimefika kwake hayupo, na sizani kuwa leo ana kazi yoyote,..’akasema Maneno akiwa na wasiwasi.
‘ Kwa ujumla , leo ilikuwa tufanye hivyo, lakini baadaye alinipa taarifa kuwa anajisikia uchomvu, akaona tuahirishe hiyo safari, sasa nahisi atakuwa kaenda kwenye hospitalini mojawapo ambayo tunapenda kwenda kuangalia afya zetu, sina uhakika sana, hebu tupitie tumuangalie, kabla sijaingi akwenye mishemishe zangu…’akasema Shangazi akijaribu kutafuta njia ya kumhadaa mkwe wake, kwani hapo hakuwa na ujanja wa kusema vinginevyo, ila alipanga wakifika hapo kwenye hiyo hospitali atamwambia amsubiri nje, na yeye ataingia ndani kuonana na Maua, kama kuna lolote limefanyika, atajua nini la kufanya.
NB. Naona tuingie kwenye sehemu ya hitimisho, kwani naona hata uchangiaji unaanza kuzorota, nan a lengo langu tukimaliza hiki kisa kinakuwa tayari kwa kutengeneza kitabu, sijajua kwa vipi, maana sina vyenzo na hata wapi pa kuanzia, naomba ambaye anaweza kunisaidi kwa hili anipe tafu.
Ni mimi: emu-three
2 comments :
Ndugu wa mimi wewe kibokoooo!!Pamoja sana tuu ndugu yangu
Usiona kimya tunakusoma ingawa hatuweki chochote...na najua hii ni muhimu kuweka chochote maana ndo unapata moyo. Ila kumbuka tupo pamoja. kila la kheri.
Post a Comment