Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, November 4, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-45



Ingawaje Rose kwa muda mwingi hakuwa makini kumsikiliza Inspekta, lakini kuna wakati alijikuta akivutika kumsikiliza, na hata muda ulivyozidi kwenda mazungumzo ya Inspekta yalimfanya Rose amsikilize na hata baadaye akajikuta akiacha mawazo yake yaliyokuwa yamemtinga kichwani na kuanza kuongea na Inspekta, kwani hoja alizokuwa akizitoa zilimpa haamsa sana, na kumuona ni mtu mwenye hekima sana.

Akaanza kuzichuja zile hoja, na kila alivyozitizama kwa mono wa mbali, alikiri kimoyomoyo kuwa kweli kuna haja ya kushirikiana na vyombo vya dola ili kukomesha mauajai yanayoendelea ndani ya nchi yao wenyewe, …kwanini ndugu kwa ndugu waishie kuuana, kwasababu ya mali, au kwasababu ya uvhu wa madaraka, au kwasababu gani…lakini ukichunguza sana raia wa kawaida wanaingizwa kichwa kichwa bila kujua nini kinachoendelea, na mwisho wa siku wao ndio wanaoumia.

Lakini hata hivyo bado nashindwa kujituma kwa hili, kwani kila nikiwaza, kwa makini kutokana na hali ilivyo, nashindwa kutambua ni nani anayestahili kuaminiwa, katika hawa waliopewa dhamana , hasa ya madaraka, …Rose akajikuta anajiuliza kichwani ni ni nani wa kumwamini, maana kila anayejaribu kumwamini, mwisho wa siku anamkuta kuwa na yeye anahusika katika kuididimiza nchi katika lindi la umwagaji damu, na ukimchunguza zaidi utakuta anafanya hivyo sio kwa maslahi ya taifa, bali ni kwa maslahi yake binafasi..

‘Inspekta nimekuelewa sana, lakini mpaka leo simuoni mtu wa kumwamini, naona kila mmoja yupo kwa ajilii ya maslahi yake, wengine wanafanya hivyo kwa njia ya kuboresha ajira yake tu, ili mwajiri wake amuona wa maana, lakini kiundani hana nia hiyo, wengine wanafanya hivyo kwa ajili ya kujilimbikizia mali kwa ajili yake na familia yake, lakini sio kwa malengo ya nchi, wengine, ..yaani ilimradi hakuna mwenye kujituma kwa uazalendo, kwa ajili ya taifa, hakuna, ….nimefikia hatua simwamini mtu tena, hasa wanaume…’akasema Rose.

‘Sikulaumu kwa hilo, kwa hali inavyoendelea hapa nchini kwenu, inabidi uwe makini sana, maana unajikuta ukiulizwa na hali ilivyo kuwa unataka uwe upande wao, ili uwe rafiki nao, na ule nawo, au uwe upende wa pili yake uwe adu wao…’akasema Inspekta na kuangalia nje, huku akiwaza maisha ya nchini kwao, alitamani sana arudi nyumbani kwao, kwani licha ya uamsikini ,na hali ngumu ya uchumi , lakini kuna kitu muhimu sana, ambacho hapo alipo, hakipatikani, ..amani.

‘Unajua Rose, kwetu tuna matatizo ya kiuchumi, hali ni ngumu kwa ujumla, maana gharama za maisha zimepanda sana, na kila kukicha unawaza leo nitakula nini, lakini tunashukuru sana, kuwa watu wanapendana, hakuna umwagaji damu wa kiasi hiki, licha ya tofauti ndogo ndogo za kikabila, kiimani na hata kiuchumi, …watu wetu hawajafikia hatua ya kuingia msituni na kuwindana kama wanyama, ….hapana sisi tumejitahidi sana kwa hilo, na hili ndilo linalotakiwa, kama unataka ushindani kwanini usiingie kwenye ulingo wa siasa, ukapambana na serikali kisiasa, ni kazi zahiri tu, sio kushika silaha, maana mwisho wa siku utakuwa huwaumizi hawo watawala unawaumiza raia wasi kuwa na hatia ….’akasema Inspekta.

‘Inspketa kweli wewe mwanasiasa, ndio maana nyie tunawaita Waswahili, maana mnajua kuongea saana, hata kuliko matendo…Natamani nije kuishi huko kwenu, lakini ….’akasema Rose na kukatisha.
‘Karibu sana kwetu, nitafurahi kama ukiolewa huko kwetu, …’akasema Inspekta huku akitabasamu na baadaye akasema ‘ Endelea na mazunguzmo yako naona kama umekatisha jambo, umesema lakini nini..?’akauliza Inspekta.

‘Hapana, ..huweze kuikimbia nchini yako kwasababu ya hali mbaya, unatakiwa uishi na watu wako uwasaidie kwa hali na mali,…kukimbia tatizo hakusaidii, nitakuwa masaliti wa taifa langu, najua ipo siku mambo yatakuwa mazuri…., unajua Inspekta, tungeongea sana,…lakini hapa nilipo namuwaza mgonjwa wangu tu…maana mmmh…sijui atakuwa katika hali gani….’akasema Rose na baadaye alijishitukia kuwa ameshaanza kuongea yale asiyotakiwa kuongea.

‘Rose usiwe na wasi wasi na mimi, najua unamsema nani..huyo mgonjwa wako namjua sana…, licha ya kuwa mwanzoni umejaribu sana kunikwep kunijibu hilo swali langu,…lakini mimi najua, na namjua huyo mtu…ila ninachokuomba ni kusaidiana, hasa kwa kupitia huyo mtu, kwani najua atakuwa kiunganishi kizuri na hawa watu, naomba tusaidieni,…saidia taifa lako, kwa ajili ya amani yenu, kwasababui mimi nimeletwa hapa ili tushirikiane na nyie, kusaidia taifa lako, natamani sana na nyie muwe kama sisi, muondokane na hili balaa la vita vya mara kwa mara,….Nikuulize Rose, ukiwa kazii kwako unafurahia mgonjwa wako wakikata roho,..tena labda ndio ulikuwa ukimshughulikia …?’ akauliza Inspekta.

‘Swali gani hilo Inspekta, itakuwa haina maana ya mimi kuitwa Docta, nikuambie ukweli , kama kuna kitu kinaniuma ni pale ninapompokea mgonjwa, halafu nishindwe jinsi ya klumtibia haraka na kupona, imeniuma sana kufanya kazi kwenye hospitali za pesa, maana wanakuja watu hawana uwezo kabisa, …na masharti yetu ni kuwa lazima uwe na uhakika wa malipo kabla haujamtibia, basi mimi nimekuwa nikivunja hayo masharti , na ndilo limenifnaya nimpoteze ajira yangu…lakini…’Rose alizungumza kwa uchungu.

‘Ina maana wameshakufukuza kazi…?’akauliza Inspekta.

‘Hawajanifukuza kazi, ila wameniondoa kwenye nafasi niliyokuwa nayo mwanzoni, na najua ndio njia ya kunichanganya kichwa na baadaye watanitafutia vyanzo vya kunifukuza kazi, na mimi sikubali, nimeona bora niache hiyo kazi yao mapema nitafute sehemu nyingine, kwasababu akufukazaye hakuambii toka…’akasema Rose.

‘Nilijua tu , hawo watu wana msimamo wao,kuwa ili uwe upande wao ukubaliane na misimamo yao,na hukubaliani nayo ukawa unafanya tofauti ujue watakuondoa na huwa hawakuachii hivihivi, …chunga sana binti, …hawa watu sio wema kabisa, unajua hatima yake ni nini..? akauliza Inspekta, akiwa anamwangalia Rose kwa macho ya huruma.

‘Inspekta unafikiri mimi naogopa kufa, kama nia yao ndio hiyo, basi siku zangu zimepangwa nifa kwa njia hiyo, lakini sitakubali kuwa mtumwa wao, na kama ndivyo walivyo kama ulivyonielezea, basi mimi na wao sina basi, na hata huyo Adam akija kwangu, nitamtolea nje kama simjui kabisa…’akasema Rose.

‘Hapana usichukulie haraka hivyo, ndio maana nilikuwa nataka mazungumzo nawe, najua ni jambo la hatari sana, lakini vyovyote iwavyo bado upo kwenye hatari, kama hawa watu wataendeela kuwepo na misimamo yao hiyo, jambo jema ni kuondoa huo uozo, na hatutaweza bila kushirikiana a watu wema kama nyie ambao mpo ndani yao, kimakosa…sasa nakuomba, wewe jifanya kama vile bado upo nao, ili tujue nini kinachoendeela humo ndani, sio kwamba ujitumbukize moja kwa moja, hapana, , hivyo hivyo ulivyokuwa mwanzoni inatosha, sisi tutawanasa kwa njia zetu, kwasababa wa o hujificha kama kinyonga…’akasema Inspekta.

‘Inspekta, mimi hiyo sio fani yangu, nakuomba unisamehe kwa hillo, nitajitahidi kusaidia pale ninapoweza, lakini sio nipoteze muda wangu kwa kuwachunguza, siwezi kazi hiyo, nimesoema udakitari kutibu watu …sio kuwa mpelelezi…naona tumefika, kuna zaidi Inspekta….’akasema Rose na mara simu yake ikaita, akaitoa na kusikiliza huku akitoka nje ya gari

‘Hapana, …wewe nenda hotelini kwako, naweza nikakufuata, hapa nipo azini,… dunia ya sasa imevaa tambala bovu, huwezi jua ….’akasema Inspeta huku akimwambia dereva wake ajifanya kama anaondoa gari kwa mwendo wa taratibu,…huku akitaizama huku na kule kwa makini, na alipogeuka ule upande Rose anapoelekea , akahisi kuna mtu anamfuata Rose kwa nyuma, kama alivyotegemea …akafungua mlango wa gari huku gari likiwa kwenye mwendo na kushuka haraka, …akaigusa bastola yake ,na kujihisi kakamilika, maana nchi uskiwa na kitu kama hicho unajihakikishia usalama fulani, lakini aliona sio muafaka wakuitoa,... akaanza kumfuatilia yule mtu kwa mbali, na kwa tahadhari..

NB, Nawatakia ijumaa njema, ..wapendwa wangu, nipo kwenye hali ngumu, ndio maana sitoi kila siku , na nikitoa ni kidogo kama hivi, lakini heri kidogo kuliko kuacha kabisa…tuombeanae heri tu.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Mimi said...

Nawe pia mpendwa. tunashukuru hata hicho kidogo tutashiba tu.

emu-three said...

Nashukuru sana mimi kwa kuniunga mkono kimatendo, ubarikiwe saana