Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, September 22, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-29



‘Sijui kama kuna kitu kinauma kama kumfumania mwenza wako akiwa anafanya lile tendo, …inauma sana na kama huna moyo wa subira unaweza ukaua…’ alisema docta Adam wakati akiongea na Docta Rose, hizi zilikuwa kumbukumbu siku za mwanzoni za kujuana kwao...
‘Na hakuna kitu kinachaouma kama kusalitiwa, imefika siku ya ndoa umejiandaa na watu wanajua kuwa leo unafunga ndoa , mwisho wa siku mwenzako haonekani…’ akasema Docta Rose. Na wote wakakaa kimiya kidogo kila mmoja akijaribu kutafakari tukio lililowahi kumtokea mpaka wakafikia kusema hivyo...

Siku Adam alipomfumania mke wake na mmoja wa marafiki zake wakubwa, ni huyo alikuwa ni zaidi ya rafiki, kwani ni mtu aliyemwamini na kumtegemea ndio maana alimchagua na kumpa kazi ya kumsaidia kumpata mwenza wake wa maisha , alimpa cheo cha ushenga, lakini hakuamini kuwa huyu mshenga kafanya hayo aliyofanya....

Toka siku aliposhuhudia tendo hilo akawa hamuamini tena mtu yoyote. Hata hivyo baada ya kumfuania mke wake na huyo mshenga wake, alishangaa ujasiri alioupata siku ile…hakuamini kuwa angelikuwa na ujasiri huo, kwani wakati anaingia mle na panga mkononi akiwa na hasira na nia ni kuhakikisha anaugawa mwili na kichwa…akiwa kalishikilia panga mkononi akaingia chumbani, lakini alipowaona wale watu, wakiwa wanashughulika, akajikuta anaishiwa nguvu…na cha ajabu alichofanya siku ile, ni kutokufanya lolote, aliwaangalia mara moja tu na kuhakikisha kwa macho yake mwenyewe mchi ukitwanga ndani ya kinu,…

‘Siku ile niliingiwa na ujasiri wa ajabu , nilikaa kimiya, nikayameza machungu, sikusema kitu, nilikuwa kama mtu haamini anachokiona, kama ndoto au mtu anayetizama picha za kikubwa…sikutoa kauli yangu kabisa siku ile, nilichofanya ni kulitupa lile panga chini, kwa nguvu na lile panga lilitoa sauti kubwa, sauti ambayo Iliwagutusha wazinzi wale,na ile sauti nadhani iliwavunja nguvu zao za viuongoni na nahisi kila sehemu ilinywea kama vile wamemwagiwa maji ya barafu, …nakumbuka kabisa jinsi nyuso zao zilivyosawajika pale walipogeuza vichwa vyao na kuniona kuwa ni mimi niliyesimama mlangoni. …’ akasema Adam wakati akimsimulia Rose

‘Kweli huo ni ujasiri wa aina yake, hata mimi ingawaje yaliyonikuta ni machungu, lakini ile hatua ya kumuona mwenza wako anazini na ukashuhudia kama ulivyosema, kinu kinatwanga ndani…oh, mchi unatawanga ndani ya kinu, ningefanya jambo baya sana….lakini hatua hiyo ni njema sana, ilionyesha jinsi gani ulivyojawa na moyo wa busara, na hivyo nivyo inatakiwa kuwa na maamuzi ya busara hasa kwa kipindi kigumu ambacho kinatesa ubongo, kipindi ambacho unapambana na jambo lenye kuondoa amani moyoni, cha muhimu ni kujaribu kuchuja hatua utakayochukua, kwani ukiharakisha na chuki ikakutawala akili yako, maamunzi yatakayokua yanaweza kuwa mabaya ambayo mwisho wa siku utajilaumu….’ Akasema Docta Rose.

‘Unajau siku ile Rose, niliwaangalia na nikama kama vile siwaoni , nikafungua kabati la nguo, na nadhani wote pale walijua kuwa nachukua bastola, huwa ninayo bastola yangu na nina kibali nayo…lakini walichoshuhudia ni tofauti kabisa, nilichukua nguo zangu za maichezo, nikaziweka karibu na kitanda,…wakawa wananiangali huku wametoa macho ya uwoga… nikavua nguo zangu za kazini, nikavaa zile nguo za michezo, wao bado wameshikwa na bumbuwazi ……wakijua najiandaa kwa shari, …oooh’ Docta Adam akacheka kicheko cha machungu.

‘Basi nikavaa nikazirudisha zile nguo zangu za kazini kwenye kabati nikatoka taratibu , nilipofika mlangoni, nikafanya kama vile askari bosi anavyomuitikia salamu askari wa chini yake, nikafunga ule mlango wa chumbani na nilipofika varandani nikawaza, kwanini sijachukua hatua yoyote, nikataka kurudi ndani, lakini sikuweza kufanya hivyo, nilichofanya ni kuhakiksha nimefunga milango ya nyumba vyema…, na kwa hasira nikatoka kwenda uwanjani,…nilikimbia mara nyingi kwa kasi ya ajabu, hadi karibu ya kuzimia.…

‘Baadaye nikaelekea ziwani, huko nikawa natembea ufukweni nikitafakari nini cha kufanya, hasira , chuki, na hamu ya kulipiza kisasi zilinitanda…lakini nilikuwa najiuliza kisasi cha vipi na kwa nani…, na hapo nilikuwa na lengo moja tu la kuachana na huyo mwanamke, kutoa talaka…maana kila mara lile tukio lilikuwa likitanda katika ubongo wangu…hiyo ndio ilikuwa nia yangu…kuachana kabisa na huyo mwanamke, na ndivyo niliamua hivyo, lakini ….haikuwa rahisi kiasi hicho…!’ alikumbuka Adamu siku walipokuwa wakiongea na Rose na Rose alionekana kumuonea huruma sana, na akamsogelea na kumpitisha mikono mgongoni mwake kama kumpa moyo kuwa sijali hayo na mambo ya kupita tu.

‘Ndiyo hayo nayajua, kuona ianweza ikawa rahisi sana , lakini kuacha …mmmh, kwasababu kila kitu kina utaratibu wake,…ndio umemfumania, …na hiyo ni sababu tosha ya kumuacha mwenzako, kama sikosei, lakini….’ Akaondoa mkono wake mgongoni kwa Adam, na kusogea pembeni halafu akasema,

`Cha muhimu ni kujipa moyo, kuwa kila jambo lina mwisho wake, ….na ubaya hauna heri…’

‘Kweli Rose la nilijipa moyo nilipotoka pale uwanjani, nilirejea nyumbani lakini sikumkuta mke wangu, na sikujali kuwa kaenda wapi, nilishamtoa moyoni mwangu…..sikuwasilina na yoyote na wala sikuwa na haja ya kumsimulia yoyote, ….nilikuwa kama vile mtu kapagawa, ….hata kazi siku ile sikuweza kufanya, …., lakini cha ajabu watu walikuja kuipata, sijui ni nani aliwaambia, kwani nilishangaa hata siku ile palipofanyika kikao cha wazazi wangu na wazazi wa mke wangu baba mkwe akiliongelea hilo tukio,,….maana mimi sikuwahi kumwambia mtu, nilichofanya baadaye ni kwenda kwenye baa, na kuanza kujifunza kunywa pombe, kitu ambacho sikuwa nacho kabla…

‘Hapo ndipo uliharibu Docta Adamu, unajiadhibu mwenyewe…kosa afanye mwingine, wewe ujitese, ulitakiwa kwa busara uliyoifanya mwanzoni uendelee nayo hivyo hivyo….pole sana, lakini hujachelewa, hakikisha kuwa pombe unaiacha, kama ni adhabu umeshajiadhibu mwenyewe vya kutosha,cha muhimu ni kujirudi na kuanza maisha moja baadaye mbili, baadaye unasimama kama vile halikutokea jambo kama hilo…..nasijui baada ya hapo mnaishie na mkeo?’ akamshauri Docta Rose, na kuuliza hilo swali akiwa na shauku ya kujua nini kilitokea baada ya hapo, na Adamu akamwambia;

‘Mke wangu hakuonekana nyumbani siku hiyo na hata siku ya pili yake, na wala sikuwa na haja ya kujua wapi amekwenda, achilia mbali huyo mshenga, kwasababu kwa mfano kama ningelikutana na huyo mshenga wakati huo nimeshaanza kunywa, …sijui kama subira ingekuwepo tena …lakini kesho yake akaja baba mkwe…

‘Aaah, nilijua tu, mzazi kwa mwana…mmh, ikawaje docta…ooh, leo sio docta ni mgonjwa wangu…alisemaje baba mkwe?’ akasema Rose akitabasamu. Tabasamu ambalo kila mara Docta Adam analikumbuka, na ndipo moyo wake ulipoanza kujenga hisia ya kumpenda huyu binti. Ndio alipokutana naye mara ya kwanza alimvutia sana, lakini alikuwa na majonzi , alikuwa bado anaiheshimu ndoa yake, ….lakini kila mara walipokuwa wakikutana na huyu binti, alijikuta akihamasika kumpenda zaidi na zaidi huu binti…

‘Mwanangu nimemuona mwenzako karudi nyumbani, na alivyokuja sikumuelewa kabisa, kaja analia, na tukamdaidisi sana, lakini hajatuambia kitu chochote,…namjua sana mwanangu, hana tabia ya kulia lia ovyo, huwa ana ujasiri wa ajabu, hupamabana na matatizo yake hata kupigana na ….namjua hivyo, sio yeye tu hata dada zake, labda ndio maana watu wanatusema vibaya….lakini yeye sio sana kama ndugu zake, anapenda kujitetea mwenyewe kwa mikono yake, pale anapochokozwa sasa sijui….maana mke na mume wana yao, hebu niambie kuna nini kinaendelea kati yako na mkeo…?’
Adamu alitulia kwanza kitafakari asema nini, na baadaye yakamtoka haya maneno ‘Baba kama mke wangu hajakuambi akitu chochote, ina maana hakuna jambo lililotokea kati yangu na yeye, kama mumemuulizia vyema na hakusema neno…basi hakuna jambo, …mimi sijui kabisa kama kuna nini…na wala sijui kuwa kaja huko kwako..!’ akasema Doacta Adam

‘Sasa mnaishije, yeye awe anatoka tu bila kukuaga, bila sababau halafu aje analia…sikuelewi mwangu, lazima kuna sababau , unajua hata ,mama yake kajaribu kumdadisi lakini hajasema kitu hadi nikaamua kuja mwenywe kukuona kwanza…. ‘ akatulia yule mzee akitafakari , hakuamini alichoambiwa na Docta Adam, akasema baadaye `Mwanangu, mimi najua ndoa ilivyo, nahisi kuna jambo,ndio maana nikaona ni vyema nije nikuone mwenyewe, nia tuongee kiume, kuna jambo gani ambalo limetokea, mumepigana, ….mumekorofishana,…au kuna nini, na hata kama mumekorofishana kuna utaratibu za kufua, sidhani kuwa ni jambo jema kufukuzana hivyo kienyei enyeji maana ndivyo inavyoonekana, labda ungenipa sababu nyingine, au sio,…na unavyoniambia hapa sasa hivi nawatilia mashaka, katika mahusianao yenu, …kwanini mnaishi kienyeji namna hiyo, kwanza wewe ni msomi, unajua taratibu za ndoa, au huo usomi hausaidiaa inapofikia kwenye maswala ya ndoa…..hapa inavyoonekana , kama mnaishi hivyo, ina inakuwa nyumba isiyo na taratibu njema, nyuma isiyojulikanai mume ni nani na mke ni nani…au nimekosea mkwe wangu?’ akasema yule mzee.

Niliposikia hayo maneno toka kwa huyu mzee, ukizingatia ndiye mzazi wa mtu aliyenifanyia hayo mabaya, ….nilitaka kupasuka kwa hasira, hasa kwa kauli zake hizo, lakini nikavuta subira na kusema kwa taratibu ….‘Baba kama mwenzangu hajawaambia lolote, basi ujue hakuna tatizo. Labda yeye mwenyewe alikuwa na hamu y akuja kuwaona wazazi wake, akapitiwa na kuondoka bila kuniaga, labda ni hivyo, kwa vile hakuniaga akawa na wasiwasi huo, mwambieni arudi tu, sitamfanya kitu…’ nikamwambi hivyo baba mkwe nakumbuka siku ile nilikuwa sijanywa nahisi kama ningelikuwa nimekunywa, ningeongea mabaya kwani aliendelea kunidadisi kwa kila hali kujua kuwa kuna nini, nilijua kabisa kahisi kuna kitu…haingeliwezekana mtu arudi nyumbani hivihivi na aakiwa analia , lakini sikumwambia chochote zaidi ya kusimamia kwenye msimamo wangu kuwa hakuna lolote lililotokea.

‘Waw, inanifurahisha sana hiyo mbinu, ….nahisi kama watu wangelifanya hivyo, mmmh, labda mambo yangelikuwa shwari, kuliko kuchukua sheria mkononi, ukapiga hata ukaua…au wengine wanafanya mambo ya ajabu wanajiua wenyewe, unatendewa wewe ubaya halafu unajiadhibu mwenyewe…ajabu kabisa, mmmh, ilikuwaje Bosi…?’ akauliza Rose,

‘Baadaye baba mkwe akaondoka na siku iliyofuata mke wangu akarudi na kuendelea kufanya mambo yake kama kawaida,…utafikiri hakufanya kosa, …. lakini hata hivyo kila mara alikuwa hajiamini, na alikuwa kama anatazamia kuwa nitafanya jambo baya, kwani kila nikimuita, huwa kama anashituka, au akaniona nimetokea , hata kama likuwa akiongea na watu hunywea…anakuwa hana raha….’ Akasema Adam akiwa kama mtu anayewaza mbali…na hata muda huu wakati anayafikiria hayo alifanya vile vile kushika kidevu na kuangalia juu huku anawaza kwa undani…

Hayo yote yalikuwa ni mawazo ya Docta Adamu akiwamuwaza Rose, na siku ile muhimu ilibakia kwenye ubongo wake kama kumbukumbu muhimu sana, ndio ile siku aliyoamua kumhadathia Rose kuhusu maisha yake na mkewe, ambayo kwa sehemu kubwa ilikuwa kichwani mwake, hakuwa hi kumsimulia mtu hadi alipokutana na Docta Rose, na alifanya hivyo baada ya kumuona kuwa ni mtu muhimu sana kwake, na anaaminika, na alimgundua hivyo tangu siku ile alipoamua kumajiri kama msaididzi wake kazini na sasa anatamani awe msaidizi wake wa maisha, lakini….!, Na cha ajabu alichogundua na kushangaa ni kuona jinsi moyo wake ulivyokuwa mwepesi kumsismulia kila kitu kilichokuwa moyoni mwake…! Alipofika hapo Adam alishika kichwa na baadaye kushika shavu, akaendeela kutafakari mazungumzo yale na Rose ambayo kila akiyawaza anatamani dunia igeuke na Rose amtambua jinsi gani alivyo jaa moyoni mwake, …na ile sauti yake wakati anamhujo ilimfanya atabasamu, ….hasa pale alipomuuliza `ilikuwaje baadaye …

‘Basi Docta Rose, maisha yakaendelea, ingawaje mwenye kovu uisidhani kapoa, na asiyefunzwa na wazazi wake dunia itamfunza tu….. Siku zikaenda , na hilo tukio likawa kama limesahaulika lakini sivyo ilivyokuwa kwangu, lilinitesa sana …na ndio maana nikawa nakunywa kupitiliza, na cha ajabu sikuwahi kumuona yule rafiki yangu , yule mshenga wangu, niliskia tu kahama, alihamia kwao kijijini …na anshukuru kuwa sikuwahi kuoanana naye hasa kipindi hiki ambacho nakunywa kupitiliza…’

Adamu alijielezea kuwa alikuwa akinywa sana, huwa akitokakazini anapitia baa analewa, na akirudi nyumbani anakuwa sio yule Adamu waliyemjua, alikuwa akiona kosa ni ngumi mikononi. Na mara nyingi akiwa amelewa, hupiga kama anayepigana na mnyama, kwani usoni kwake alikuwa akiona lile tukio aliloliona siku ile alipomfumania mkewe na mshenga wake, ilikuwa sasa anapiga kupita kiasi na mkewe akawa naye anapigana, kwahiyo kila mara ni ugomvi na majirani wakawa wamechola kuamua.

‘Hivi huyu docta kabadilika lini, mbona tabia hii hakuwa nayo kabla…’ akauliza jirani mmoja

‘Wewe unajifanya huoni, huyo mkewe mnamuonaje, mtu alifanya nyumba danguro, anawaingiza wanaume leo huyu kesho huyu, unakumbuka hata aliwahi kutembea na mshenga wao…’ akasema jamaa mmoja.
Matatizo haya yakawafikia wazazi na ikabidi wakutane wanandugu kulijadili hili tatizo, na ndipo Adamu akawaambia kuwa yeye haui kitu, anayejua ni mke wake kama kweli anania njema, aongee yote anayoyajua, lakini kama anaona hana kosa, basi …hakuona kosa, mkosaji ndiye anatakiwa akubali na kutubu madhambi yake,…..

‘Mimi nimekuelewa mkwe wetu na mengi tumeyasikia toka kwa majirani, maana toka siku ile mwanentu arudi nyumbani bila taarifa yako, tuliamua kulifanyia kazi hilo swala,, na tumegundua mengi na baya zaidi ni kuwa mwanetu alifikia hatu ya kufanya makosa mabaya….mabay sana, wewe mwanetu unadiriki kutembea na mshenga wako….una nini wewe…’ akasema baba mkwe.

‘Sasa mwanetu, tumaliangalia sana hilo swala na tumemuita mtoto wetu na kumkanya, na ..kwakweli limetuuma sana, na tunachokuomba kama binadamu kukosa kupo, na kusameheana kupo, tunakuomba umusamehe, ….ila nakuomba kukupa kama funzo, usinielwe vibaya, ila nakuomba uwe mkali, usiwe mpole, hili nakudokeza tu mwanangu…’ hakuamini kauli hiyo kama inatoka kwa baba mkwe wake.
Baadaye kikao kiliisha , na Adamu alikubali shingo upande, na kujifanya kuwa mambo yamekwsiha, lakini moyoni alishaamua kuwa aishi kivyeke vyake, na ikibidi ni kugeuza nyumba uwanja wa mabondia, Akabadilika kabisa hata huko kazini walimshangaa, akawa mabogo na kuanza kujifunza tabia ambayo hakuwa nayo, …..

Mkewe naye akawa hajali, akawa kajifunza mume wake muda gani anakuwepo , muda gani anafnaya nini, na kurudia uchafu wake, hakujali tena…..na Adamu naye akawa hafuatilii tena, yeye na kazi akitoka kazini kinywaji….na baadaye akajiona anajiumiza kwanini aishi maisha ambayo hayana amani, bado alijiona hana amani na kazi yake ilikuwa inataka amani , ili aweze kupambana na wagonjwa, …na ndipo bahati nzuri akakutana na docta Rose, akamshawishi na kukukabli kuacha kazi serikalini na kuja kujiunga naye, akampa cheo cha msaidizi wake.

Kwakeli baada ya kumuajiri Docta Rose, alianza kuona mabadiliko…Docta Rose licha ya kuwa na yeye alikumbana na mikasa mibaya, lakini alikuwa jasiri wa kupamabana na hayo matatizo na kwa vile ni moja ya jambo alilolisomea akawa kama dakiari wa dakitari mwenzake, na Adamu akaanza kubadilka na kurejea katika hali yake ya mwanzoni, aligundua kosa analilofanya la kulewa, na anamshukuru sana docta Rose, kwani ndiye alimyemsaidia kutokana na tatizo hilo, alipewa maoni na mara kwa mara wakawa wanaongea na hata ikafikia kumuona ni mtu muhimu sana katika maisha yake, akawa msiri wake mkubwa, akipata tatizo nyumbani anakutana naye anamshauri na mara nyingi akifuata ushauri wake anajikuta anakwepa matatizo ambayo yalimfanya awe bondia asiye na leseni.

Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho wake, Docta Adam akashindwa kabisa kuelewana na huyo mwanamke, hata ushauri wa Rose hakufua dafu, na alipomfumania mkewe mara nyingine, akaliweka hadharani, maana hili alitafuta ushahidi na kuwaita wazazi wa huyo binti kuja kushuhudia , na ndipo akaidhinisha talaka , na ikawa mwisho wa kuishi na huyo mwanamke tena,…
‘Afadhali sasa nina amani ni bora kuishi peke yangu kuliko kuishi na mwanamke kama yule, mimi katika misha yangu nilijua kuwa waume ndio wakaorofi , lakini sasa nimegundua kuwa binadamu wote ni wakosaji, awe mume au mke, …..na kama nitaona mke mwingine, inabidi nifikirie sana kwa makini…’ akamwa mbia Docta Rose.

‘Hilo hata mimi nakuunga mkono, …wewe ulikuwa ukinilaumu mwanzoni kwanini nawachukia wanaume, kuna mambo yanatokea unashindwa kuvumilia na kuwajumuisha wanaume wote kama wote ndivyo walivyo….hata mimi sitaki kuolewa tena…’ haya yalikuwa maneno ya Rose, kipindi cha mwanzoni, lakini jinsi walivyozidi kuzoeana, ndivyo Docta Adam alipogundua kuwa Rose, angemfaa sana kuwa mkewe, kwanza ni mzuri, msomi na tabia yake inakwendana sana na anavyotaka yeye, lakini haikuw rahisi kumshawishi bint huyo kutoka na mdhila aliyokutana nayo. Na hata alipofikia hatu akuwa kamshawishi na anakaribia kuwa karibu naye akaibuka huyo mgonjwa na kumbadili tena Rose, …..na sasa ilionekana wazi kuwa hatafanikiwa tena.

Baada ya kumalizana na mkewe, akujua mambo yameisha, mara akasikia siku moja anaitwa mahakamani mkewe alikuwa kamshitaki, na ikabidi awe anafika mhakamani na kupoteza muda wake jambo ambalo hakulitaka, lakini kwa vile ushaidi wa mambo mengi ulishawekwa wazi basi ikawa kesi haikuweza kumbana sana Docta Adam, lakini alimauriwa kugawana baadhi ya mali waliyochuma wakiwa pamoja, hilo akalikubali na kutoa kile kilichokubalika, na akajua mambo yamekwisha …

Ghafla huyu kaja tena na sasa anapambana na marafiki zake, hili hakuweza kulivumilia, hasa ple alipomuona anatoa kipigo kwa Rose,….alipandwa na hasira na kuanza kupambana naye kwa ukali zaidi na kujikumbushia ubondia wake tena, wakati alishaamua kuuchana nao, akajikuta wanapigana na mtalaka wake kama maadui wa kutaka kuuana, na mwisho wake akajikuta yeye anaswekwa ndani huku mwenzake akicheka na kudai kuwa bado kabisa huo ni mwanzo tu na hata huyo hawara wake asipite kwenye anga zake, akimuona ajiandae kupambana na mke jeuri, na huwa anpenda kujiita hivyo –mke jeuri.

Baada ya lile vurugu na mke jeuri …watu wakawa wamemchukua yule mwanamke pembeni, na Adamu akaona yameisha, akakumbuka miadi yake na Rose kwahiyo haraka alipageuka pale alipokuwepo Rose anajua kuwa Rose yupo hakumuona, akakuta hayupo akawauliza watu ambao walishajaa hapo nyumbani kwake, kitu ambacho alikiona kama fedheha, lakini hakuwa na jinsi, akawauliza baadhi ya watu anaofahamiana nao kuwa wamemuona Docta Rose, wale watu walisema walimuona ila aliondoka mapema tu vurugu zilipoanza kati yake na aliyekuwa mkewe. Hapo Docta Adamu hasira zikamshika akamrudi yuie aliyekuwa mke wake na kuanza kumpiga tena, na yule mwanamke alipoona anazidiwa nguvu akakikimbilia kile kibao chenye misumari alichokuwa kakitumia mwanzoni na kumbandika nacho Adamu usoni, na kama isingekuwa watu, alishaamua kumtoa macho Docta Adam…..

Baadaye ugomvi ukaisha,Adamu akiwa ma majeraha, akaingia ndani kwake na kujiganga, huku akilaani kwa kuharibiwa mipango yake, akajaribu kumpigia simu Rose, lakini simu ilikuwa ikisema unayempigia hapatikani, na kwa hasira akaibamiza simu yake chini na kukimbilia bafuni kuoga, na baadaye akaingia chumbani kwake kulala, lakini kabla hajaweka ubavu vyema, mara akasikia hodi mlangoni, na ahodi yenyewe ilikuwa ya fujo…kwa hasira akatoka chumbani hadi varandani na kufungua malango akiwa na nia ya kupambana na yoyote aliyegonga mlango. Alipofungua mlango akakutana ana kwa ana na polisi…alipowaona hawo watu akajua sasa mambo yameharabika…wale maaskari hawakupoteza muda wakaonyesha vitambulisho vyao na kujitambulisha na nini lengo lao…walisema kuwa wamekuja kumkamata kwa kosa la kupiga na kujeruhi…

‘Nimempiga nani, nyinyi hamuoni kuwa na mimi hapa nina majeraha…’ akasema Adam akionyesha sehemu alipojifunga na plasta.

‘Ungelikuja polisi kutoa taarifa kama kweli uliingiliwa na huyo mwanamke , hii unaonyesha kuwa wewe ndiye uliyejifanya mbabe, unapigana na mwanamke kama unapigana na mwanaume mwenzako, twende utajitetea huko huko polisi…’ akaambiwa na hata alipoleta ujeuri mwisho wake alikubali na kwenda kituo cha polisi, na alipofika huko wanoko wake wasiompenda wakashangalia na kumsweka ndani, na kwasababu ilishafika usiku hakukuwa na wa kumdhamini hadi asubuhi yake, ambapo taratibu za dhamana zilianza kutayarishwa, ….



Ni mimi: emu-three

6 comments :

chib said...

Pamoja na kwamba shughuli zimenibana sana, lakini sikosi kutoa muda kupitia hapa na kufaidi riwaya.
Big up

Anonymous said...

M3 jamani utatuua kwa pressure ya kusubiri posts zako. Maua anaendeleaje na Maneno? Shangazi naye je? Unasubiri utupeleke kwa Maua akiwa ashajifungua! Kazi nzuri jamani me mwenzenu nashinda kwenye blog yako nikisubiri segment ifuatayo sijajua unapost baada ya siku ngapi ngapi!

Anonymous said...

Mmmmmh! story inasisimua hiyo, asante walau leo tumekuona. kazi nzuri.Jane

samira said...

ni nzuri m3 naomba kuuliza vipi rose aliuza madini yake kule mjini alipoenda na sweetie sikumbuki sehemu hii ilikuwaje

Simon Kitururu said...

Mkuu CHIB kanisemea. Mie nakajitabu kwa jinsi niprintivyo!

Na Samira kachokoza ninjiulizacho pia!

emuthree said...

Wapendwa hapa nilipo nasikitika sana maana niliwahi mapema ofisi nikijua kuwa mpaka saa 2 nitakuwa nimeandika sehemu inayofuata lkn kukatokea vikwazo juu ya uwezo wangu. Kwa hali kama hii najiuliza hivi kweli kuna haja ya kusherekea uhuru kama hawa jamaa wanatoka huko kwa uhindin na kuja kutufanyia hivi. Lakn sitokata tamaa cafe zipo ! Kama ningelikuwa na computa na neti mbona kila siku ningelikuwa natoa kitu .Naombeni dua zenu,niushinde huu mtihani!