Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, August 30, 2011
IDD MUBARAK
‘Mimi nimenunuliwa nguo ya sikukuu mpya…’ nikamwambia mwenzangu, naye akadai kuwa hata yeye kanunuliwa nguo mpya, ikawa ubishi kuwa ni ipi ni nzuri kuliko ya mwenzake, ubishi huo ukafanya tukubaliane kuwa kila mmoja aende akaivae nguo yake, halafu turudi tukutane ili tuone nani kapendeza zaidi.
Basi kwa kujiiba, kila mmoja akaipata nguo yake toka majumbani kwao, na tulipofika mahali tukavua nguo za kushindia na kuvaa hizo nguo mpya za sikukuu, zilikuwa bado mpya zimepigwa pasi vizuri, kwa ajili ya kwenda nazo kwenye ibada ya Iddi, kama ilivyo ada kuwa siku ya Idd, uvae nguo mpya ikiwezekana na ukaswali nayo, sivyo kama wanavyofanya watu kuwa ile nguo mpya inakuja kuvaliwa baadaye….
‘Unaona nilivyopendeza zaidi yako..’ nikamkoga mwenzangu, naye akadai hivyo hivyo…na baadaye wakaja marafiki zetu wakawa wanatuangalia kwa jicho la husuda na haikuchukua muda kila mmoja akaenda kwao kuchukua nguo walizonunuliwa na wazazi wao kwa ajili ya sikukuu ya Idd, na ikawa kila mmoja ana nguo mpya. Na kama utoto ulivyo, mpira na michezo mingine haikosekani, tukawa tumejisahau kuwa tumeshavaa nguo mpya, mara tukaanza kucheza mpira, na siku mbili tatu kulinyesha mvua, kwahiyo matope na majimaji machafu yalikuwepo .
Baada ya nusu saa tu nguo mpya, hazikuwa nguo mpya tena, kila mmoja alikuwa hatamaniki, tumechafua zile nguo na wenyewe hatutamaniki, huwezi ua kuwa zilikuwa nguo mpya, na kila mmoja akawa anaogopa kurudi nyumbani na wakati huo jioni imeshafika, lakini ikawa haina jinsi, sasa tufanyeje. Utoto ukatutuma tuzifue, hapo tunachojua ni kufua tu, hakuna cha sabuni , na maji tunayofulia ni maji machafu…si tunafua bwana, tukamaliza na haraka haraka tukarejea majumbani mwetu kila mmoja kwao.
‘We Nanihino, mbona nguo zako sizioni sandukuni, nilikuwa nataka kuziangalia kama zipo sawa, maana ujue ibada ya swala ni asubuhi sana…’ akauliza mama. Nikawa najiuma uma, sina la kusema na nilipobanwa sana nikazionyesha na kudai nimezifua kwasababu nguo mpya inatakiwa kufuliwa kwanza..
‘Mamamama hivi wewe una akili kweli, umezifua au ulizitumbukiza kwenye maji machafu…’ wazazi wetu wa zamani kiboko hakichezi mbali ili bidi wanichape kidogo, na hapo ikabidi niseme ukweli ulivyokuwa,…Na baadaye ikabidi wazazi wajitahidi kuzifua tena, lakini madoa na hadhi yake ya nguo mpya ikawa haipo tena, na hata nilipoivaa kesho yake, haikuwa nguo mpya tena, ….
Jamani hiki kisa kimeniijia kichwani kwa kukumbuka utotoni, na visa vya utoto vipo vingi na vyenye mafunzo ndani yake kwani kila jambo hutokea ili iwe sababu ya funzo fulani ukiamua kutafakari kwa mapana. Na hii leo , na wengine kesho ni siku muhimu sana kwa Waislamu, kwa kukamilisha nguzo muhimu sana ya kufungwa SWAUMU, ndani ya mwezi wa Ramadhani, ni ibada muhimu sana yenye mafunzo ndani yake.
Kufunga kulikuwa sio kujizuia kula tu, bali ilikuwa pamoja na kujizua na machafu mengine,na kwa kufanya hivyo, mtu anakuwa karibu na mola wako, na pia moyo wa muumini huyu hutakasika, ikizingatia kuwa kama mwanadamu tunaishi katika mitihani, kutenda madhambi inakuwa haikwepeki, kwahiyo ilikuwa ni muda wa kuutakasa moyo kwa kutubia hayo madhambi. Na katika kufunga huku, tunakufananisha na gari, kuwa kila baada ya muda fulani gari hufanyiwa ukarabati, maana mwaka mzima unakula tu, na wengine wanakula kwa pupa, kwahiyo kunakuwa na akiba isiyo ya lazima ndani ya miili yetu, na akiba nyingine sio njema kiafya, bali ni uchafu tu, na kwa kufunga uchafu huo huyeyuka, hasa mafuta. Hii ni mifano michache tu ya faida ya kufunga.
Lakini kuna kitu kingine, ambacho ni vyema tukakijua kuhusu adui njaa, tunamuita adui kwasababu akiingia mahali madhara yake ni makubwa, kuna watu kama tunavyoona katika vyombo vya habari wanakufa kwa njaa, hawana chakula, hata kile cha mlo mmoja, …hebu fikiria mtu analala anaamuaka anashinda, na sio siku moja tu, ni masiku na miezi mpaka mwili unakunjamana, na hatimaye wengine hufa kwa ajili ya njaa. Kwa waliofunga vyema somo la njaa limepatikana, na hata akimuona mwenzake analia njaa, atingiwa na huruma kwa imani ile aliyoijenga ndani ya mfungo wa Ramadhani. Kwa somo hilo tueleekeze imani zetu kwa wenzetu wanaokufa kwa njaa huko Somalia, …tuwaangalie jirani zetu tunaoishi nao ambao hawana uwezo, wakati sisi tunakula na kusaza, …
Wakati nawaza haya nikakumbuka hicho kisa cha utotoni, kuwa sasa la mgambo limelia, shetani anafunguliwa, ile imani na huruma iliyokuwepo ndani ya mfungo wa Ramdhani itapotea kabisa, ule utulivu ulioonyeshwa ndani ya mwezi wa Ramadhani utapotea, tunasahau kuwa ndani ya mwezi wa Ramadhani tulikuwa tunatayarisha nguo mpya,…kwa kujitakasa, na kuwa kama mtoto aliyezaliwa leo, kama nguo mpya ya sikukuu, nguo ambayo haina madoa doa ya uchafu, lakini baada ya siku moja tu, hutaamini kuwa mtu huyu alikuwa kama nguo mpya, hatamaniki tena, kesharudi kwenye maasi, keshamsahau mola wake, na chuki , uadui na uhasama umeshakita ndani ya mioyo yao…nguo mpya sio nguo mpya tena…
Umri wa binadamu ni mfupi sana, na hebu angalia jinsi gani siku zilivyokwenda haraka, maana na yake ni kuwa na hata umri wa masiha yetu ndivyo yanavyokwisha kwa haraka hivyo-hivyo, juzi tuulikuwa tukiitwa mtoto, jana tu tukawa tunatambua ujana, leo mzee, keshakutwa tutaitwa jina jingine, je una uhakika kuwa utapata muda mwingine wa kuifua nguo yako iliyochafuka, angalau ionekane mpya tena….TUTAFAKARI KWA KINA
Kwa niaba ya blog hii tunachukua nafasi hii kwa kuwatakia wote, IDD NJEMA, kwa kusema IDD MUBARAKA
Ni mimi: emu-three
12 comments :
IDD MUBARAK Mkuu! Na asante kwa posti yenye bonge la ujumbe Mkuu!
Minali-faidhina Mkuu Iddi njema na wewe na familia yako
Eid Mubaraka nawe pia na watu wote katika dunia hii. Ujumbe wa leo nimeukubali nimeupenda sana maana unamfanya mtu mwingine pia akumbuke na atafakari.
idd mubarak kwa wote
Asante kwa ujumbe mzito M3....Minal Faidhina Eid Fitrl nawe pia na familia yako Mungu azidi kukupa afya njema.
IDD njema kwako pia,sikupatii picha EMU3 utakavyolisulubisha pilau lol...
Minal faidhina na kwako pia.. Ujumbe ni mzuri na tumeupokea n'hop 2taufanyia kaz effectivelY..
shukran mkuu
My brother suggested I might like this web site. He was totally
right. This post actually made my day. You can not imagine simply how much
time I had spent for this info! Thanks!
My website - calories burnt walking
I absolutely love your site.. Great colors & theme.
Did you develop this site yourself? Please reply back as I'm wanting to create my very own blog and want to find out where you got this from or just what the theme is called. Appreciate it!
Have a look at my site ... pozycjonowanie stron www
After checking out a handful of the blog posts on your website,
I truly like your technique of writing a blog.
I added it to my bookmark webpage list and will be checking back soon.
Please check out my web site too and let me know
what you think.
Have a look at my web blog ... www
Hey There. I found your blog using msn. This is a very neatly written article.
I will make sure to bookmark it and return to read more of your
helpful info. Thank you for the post. I'll definitely return.
my web blog ... fototapety dla dzieci (fulfordit.zendesk.com)
Post a Comment