Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, August 29, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-21




`Shemeji upo tayari tuondoke, saa za kwenda kuwaona wanyama imefika…..’ Maneno akashituliwa toka katika mawazo yaliyomfanya apitiwe na usingizi na haraka haraka akageuka kuiangalia sura ya Maua, na pale macho yake yalipokutana na macho ya Maua, akahisi vinginevyo, akarudisha haraka macho yake na kutizama chini , halafu kwa kujiiba akamtupia jicho la haraka kumwangalia Maua machoni, lakini cha ajabu hakuona dalili ya chuki, dalili ya….akajipa moyo kuwa huenda shemeji yake ndiye alitaka iwe hivyo, akasimama na kusema, `Shemeji mimi nilishajiandaa muda mrefu nilikuwa nakusubiri wewe tu…’ akasema Maneno

‘Kwanini hukuniita, maana sijielewi shemeji, sijui ilikuwa ni ndoto…sijui ilikuwaje, hutaamini nilikuwa sitaki kabisa kwenda tena huko porini, naogopa kukutana na lile joka …ooh, sijui ni ndoto au ni joka kwali, maana sijielewi…naogoa sana kota ndoto kama ile tena…’ akasema Maua huku akikaa karibu na alipokaa Maneno kama vila anaogoap kitu fulani na kuendelea kuongea kwa kusema, `sijui nilikuwa porini…na naona kama ni kweli tukio hilo …shemeji ngoja twende tu huko kuwaona hawo wanyama, ila natamani nirudi kwetu haraka, naona tukiendelea kukaa hapa, nitajiua….’ Akasema Maua na kumfanya Maneno abakie kinywa wazi, ina maana Maua hajui kabisa nini kilitokea usiku, ina maana yeye ndiye aliyemshinikiza shemeji yake, ina maana …ooh, mungu wangu sifanyi tena kosa hilo, …nitakuwa mgeni wa nani ikigundulika kilichotokea jana….

Safari ya kuangalia wanyama, iliwafanya wasiwe na kumbukumbu ya tukio la jana, kwani ile furaha ya kuwaona wanyama mbalimbali, na vivutio vya kila namna,viliwafanya kila mmoja awe na mawazo tofauti na mwisho wa siku wakawa wanasimuliana hili na lile kuhusina na mnyama fulani na kwanini yupo hivyo, na hapo Maneno akawa anatoa hadithi zake za utotoni kuhusiana na mnyama huyu au yule na watu wakwa wanamsikiliza kwa utaalamu wake wa kutoa hizo hadithi. Ikawa furaha na muda uliisha kama vile hakukuwa na muda hata kidogo na siku ikaisha ikabidi warudi hotelini kwao, kujiandaa kwa safari nyingine …
**************
Waliporejea hotelini, Maua akamwangalia Maneno kwa makini akionyesha kuwa kuna jambo linamkera na alihitaji mazungumzo na Maneno, ha hapo Maneno akawa anaogopa kuwa sasa inawezekana ikawa ndio mwisho wa urafiki, na chuki itachukua mahali pake, lakini akajipa moyo kuwa huenda hata Maua alikuwa yupo tayari kukubali ukweli, na kilictokea jana ni kwa utashi wake, hajamlazimisha, lakinimara akamuona Maua akibubujikwa na machozi…na baadaye akatulia na nakusema;

‘Shemeji kila nikiwaza tukio la jana naona kama ilikuwa kweli, nashindwa kujua ilikuwaje, hivi kweli shemeji niambie ukweli kulitokea nini,…kwasabau nikisema ni ndoto, nashindwa kukubaliana nayo, naona kama kuna ukweli, na sio ndoto na nina uhakika nilala na mtu jana, …nahisi kuna kitu kimetokea kisicho cha kawaida kwani hata wewe nikikuangalia machoni unakuwa kama unanionea aibu, naoma uniambie ukweli kulitokea nini…, ninauhakika kama sio ndoto jana nilikuwa maporini…sijui nilifikaje, na woga huu niende maporini, hapana ile itakuwa ni ndoto tu…’ akasema Maua huku akitizama juu kama anawaza jambo fulani.

‘Unajua shemeji nilipofika huko kwenye kuangalia wanyama, nililiwazika kidogo na kulisahau tukio zima la jana, lakini wakati tunakuja, nikawa nawaza kiundani..na sasa nimeshindwa kuvumilia, najua unajua lolote kuhusu hilo tukio nakumbuka kwa macho yangu mwenyewe nimemuona mtu…yupo wapi huyo mtu?’ akamuuliza shemeji yake.
‘Ulimuona mtu, ulimuona nani,…ina maana shemeji hujui kabisa kilitokea nini jana usiku…’ akauliza Maneno.

‘Ndio najua kuna kitu kimetokea ndio maana nasisistiza uniambie ukweli, hasa huyo mtu niliyekuwa nimelala naye, nakumbuka, kama sio ndoto lazima kuna mtu….najua kabisa na….oh,, huyo mtu ndiye aliyeniokoa, ndiye aliyenileta nyumbani..yupo wapi huyo mtu, shemeji tusipoteze muda, maana mukiendelea kunifanyia hivi, ninaweza nikafanya jambo baya zaidi….mimi muda wote nilikuwa naona kama ndoto,…kwasababu haiwezekani mimi nitoke mwenyewe hadi maporini, naogopa sana wanyama, hasa nyoka…halafu nizungukwe na joka…mungu wangu nyoka…’ alipotamka nyoka, akaruka juu kama vile analiona hilo joka na analiruka.

‘Shameji ina maana hukumbuki nini kilitokea usiku…haiwezekani….?’ Akauliza Maneno akiwa bado anajiuliza mengi kichwani, kama kweli shemeji yake hakumbuki lililotokea mbona itakuwa kashifa kubwa kwake, mbona….

‘Haiwezekani ikawa ni ndoto…nakumbuka kabisa nilikuwa nimezungukwa na joka, kubwa,…lakini mara akaja mtu akaniokoa na kunirudisha hotelini, halafu tukalala naye, halafu, tuka…..ooh, Maneno niambie ukweli kulitokea nini, maana ukinificha lazima ipo siku utaumbuka, maana ninahisi kuna mtu aliniokoa ni nani huyu….na yupo wapi…namuomba nimuone.’ Akaonyesha furaha fulani na kuanza kutoka nje kumtafuta huyo mtu na Maneno haraharaka akamzuia na kumsimamisha, na kuwambia kuwa sio ndoto kuwa kweli alitoka nje, kweli alikuwa kafanya hivyo na kwenda porini, ila yeye kama Maneno hajui jinsi gani ilivyokuwa hadi Maua akafika huko porini.

‘Una uhakika na unachosema Maneno, unajuaje kuwa nilitoka nje na kwenda huko maporini, …’ akauliza Maua huku akimuangalia Maneno kwa macho ya shauku, na baadaye akakunja uso kuonyesha kuwa yupo kwenye kutafakari kuzito akawa akasema `Unasema hujui kabisa nilitokaje usiku na kwenda porini, na hujui kuwa nilikuwa nimezungukwa na joka kubwa?’ akauliza Maua na kumwangalia Maneno usoni, na Maneno akawa anaona aibu kumwangalia Machoni na kugeuka kuangalia dirishani.
‘Unajua mimi sijakuelewa Maua, kwasababu umesema hukumbuki, ina maana kwako ni kama ndoto au sio?

‘Ndio maana nakuuliza, kwasababu hapa nilipo nachanganyikiwa tu, sijui, lakini nilipoangalia lile gauni nililovaa jana nikaliona lina matope, limechafuka lina majani ya porini, lina dalili za udongo, nikakumbuka kuwa hata mimi nilipoamuka asubuhi, nilijihisi sipo kawaida…kuna tendo limefanyika….hapana haiwezekani, ikawa ni ndoto. Alipofikia hapo Maneno akamgeukia Maua na kutaka kujua zaidi kuhusiana na hiyo kauli kuwa ameihisi kuwa hakuwa kawaida…ina maana kuwa….

‘Shemeji mimi naona usijitie kwenye mawazo mazito kama hayo, tulichukulie kuwa ni ndoto na tukubali hivyo iishie hapo, unaonaje?,…ila ni kweli kuwa ulitoka usiku…sasa ulitokaje, mimi sijui labda hizo hisia za kuwepo kwa mtu mwingine, ndio hapo naweza kusema ni ndoto, kwani sijawahi kumuona mtu mwingine humu ndani zaidi yetu wawili …………’ Akasema Maneno huku anamwangalia shemeji yake kwa macho ya aibu, alishindwa kuelezea zaidi, atamuelezeaje kwani hata yeye mambo mengine aliyaona kama miujiza,…hakumbuki nini kilimshinikiza kufanya vile.

‘Shameji unasema ukweli kuwa nilitoka nje hadi maporini,…lakini hukuiniona nikitoka sawa au si sawa? Akauliza Maua halafu alipomuona shemeji yake kanyamaza kimiya akaendeela kusema `mimi nilikuwa naiona kama ni ndoto, ina maana kweli nilikwenda porini, ina maana kweli nilikuwa nimezungukwa na joka,…lakini sasa je ni nani aliyekuja kuniokoa….kwasababu kuna mtu alikuja akaniokoa na hatimaye akanirudisha nyumbani….?’ Akauliza Maua huku akiwa bado anatizama nje kwa hamasa. Na hapo taswira ya usiku ikawa inamjia kichwani na akageuka kumwangalia shemeji yake na macho yao yalipokutana Maneno akainama chini kwa aibu, akijua sasa chuki itaanza. Na hapo Maua akaanza kukumbuka ilivyokuwa hiyo ndoto au ukweli alifnaya hivyo….

***********
Ilikuwa usiku wa manane, wakati Maua aliposhituliwa na sauti ya ajabi kichwani, ni sauti ile ile ambayo ikimjia inakuwa kama ina mamlaka fulani kichwani mwake, inaweza kumuamrisha akafanya jambo ambalo baadaye hajui alilifanyaje, ina kuwa kama mwili unafanya bila utashi wake, na hali hii imeanza baada masiba wa mume wake, hakuwahi kuwa na hali hii kabla. Basii hali hii ilipomtokea, ikawa inamuamrisha atoke pale kwenye hoteli, atoke haraka nje, kwani Mhuja yupo sehemu anamsubiri, bila kuwaza zaidi kuwa huenda ni ndoto tu au ilikuwa sauti ya nini akainuka haraka kitandani, na kutoka nje ya jengo lile la hoteli.

‘Jamani tunawapa tahadhari kuwa mpo eneo ambalo halihitaji mtu kutoka mwenewe na kuingia eneo la mbuga bila mlinzi, au mwongozaji aliyetambulikana, kuna hatari ya wanyama wakali sio wanyama tu , kuna nyoka na wadudu wenye sumu, kwahiyo muwe kwenye hoteli zenu mpaka muda ukifika mtaongozwa na wahusika…’ hayo yalikuwa maneno waliyokuwa wameambiwa walipofika, na kwa hali ya akawaida, lbada uwe jangiri au una nia mbaya, hungeliweza kutoka na kuingia maeneo yenye wanyama wakali, lakini kwa muda ule tahadhari na uwoga huo haukuwepo kwa Maua.

Akatoka nje ya jengo, na alipofika nje ubaridi na upepo wa usiku ukaingia ndani ya mwili wake kupitia kwenye gauni refu la mikono mirefu alilokuwa kalivaa, hakuijali hiyo hali, alichokuwa anakihitaji ni ile sauti inayomuongoza, alichokihitaji ni kufika hapo alipoambiwa kuwa atakutana na Mhuja, akawa anafuata sauti inavyomuamrisha, twende huku pitia hapa…ilikuwa kwa mwendo haraka, hadi akawa kafika mbali kabisa na ile hoteli hadi ndani katikati ya msitu, alipofika hapo , ile sauti ya kumwamrisha ikapotea, akawa kasimama kwa muda akiwa anasubiri maagizo mengine.

Mara akili ikamrejea na kuwa kama kazindukana toka kwenye usingizi , na alipoangalia huku na kule akajikuta katikati ya msitu na kwa mbele aliona kama kitu kinavunja vunja majani , mara kukawa kimiya, woga ukaanza kumuingia,, akawa anajiuliza nipo wapi, ….ooh, nipo msituni, e nimakujaje hapa, akawa anawaza, bila jibu, akaangalia huku na kule lakini hakuona kitu, sauti yam situ mkali…na milio ya wadudu wa usiku…

Mara akasikia sauti kama radi ikitanda hewani, akaziba masikio na mwili ukamzizima kwa woga, akaangalia huku na kule akitaka msaada, lakini inavyoonyesha yupo mbali kabisa na hoteli. Akaanza kutembea kwa kunyata kudogo kidogo, kuelekea asipokujua, lakini kila alipokuwa kitembea alihisi kuwa kuna kitu kinamneyemelea kwa nyuma, akawa anaongeza mwendo na hicho kitu, sijui ni mnyama nacho kikawa kinaongeza mwendo, ….simba…alipogundua hilo akatamani kuanza kukimbia, lakini kuna auti ikamwambia dawa ya huyu mnyama sio kumkimbia unatakiwa urudi kinyumekinyume, mapaka uhakikishe umeondoka maeneo ya umbali wake…

Alifanya hivyo kurudi kinyume kinyume…akawa anarudi kidogokidogo hadi akawa upeo wa mbali wa kile alichogundua kuwa ni simba, halafu akageuka na kuanza kukimbia, alikimbia ,alikimbia hadi miguu ikawahina nguvu tena, na alifika sehemu akawa kakanyaga kitu kama laini lakini ni kama sponji, akasimama na kuangalia chini….ooh…akajikuta mwili umekufa ganzi nyoka…cha ajabu badala ya kukimbia akawa kasimama pale pale…

Alikuwa nyoka mkubwa ambaye hajawahi kumuona katika maisha yake, alikuwa haoni kaanzia wapi, na akawa kama anajiviringa, kumzunguka….akawa hawezi kutikisika,na kukawa na kitu kama sauti ikiwa inamwambia kama wimbo kuwa wakati umefika wa mwana kurudi tumbani, na kusahau machungu yadunia, na sauti nyingine ikawa inamwambia kuwa akimbie, yupo kwenye hatari, lakini miguu ilikuwa imekufa ganzi, haibanduki pale iliposimama na mara sauti ila ya mwanzo ikamwambia tena sasa wakati wa kwenda kumuona Mhuja umefika, subiri hivyo hivyo, sasa huhitai sumu au kamba ya kujinyongea….

Alipotajiwa kamba ya kujinyongea , akaukumbuka kuwa alipotoka nje aliculkua kamba, lakini hakujua ni ya nini, na alipotizama mkononi akajiona ana kamba,…kamba ya kuinyongea, akawa kaishikilia, lakini alipoambiwa kuwa haihitaji tena ile kama akaitupa chini, na huku miguuni, alihis lile joka lijijiviringa miguunii mwake kama mtu anayemfunga migu yote miwili kwa kumzunguka, lakini lilikuw ahalijambana kiasi cha kuweza kuhisi hivyo, cha ajabu kichwa cha lile joka kilikuwa hakionekani…..’

Mara akamuona mtu anakuja,…ooh, keshafika mtu wake aliyeambiwa watakutana naye…hatimaye keshafika, kumbe ni kweli …mpenzi wake, huyo keshafika, watu waongo bwana, eti kafa, sasa huyu ni nani..na wakati anawaza hili, huku akiomba huyu mpenzi wake afike haraka pale alipo ili amuokoe na yule nyoka anayetaka kumviringa,akagundua kuwa nyuma ya yule mtu pia anakuja simba, kwahiyo yule mtu akawa nakuja kama anakimbia, na nyuma yake huyu simba naye anaongeza mwendo…ooh, yule mtu anakimbizwa na Simba, mungu wangu nitamuokoaje mume wangu….na wakati miguu haiinuki, akawa anawaza na wakati anawaza mara yule mtu akamkaribia, na ghafala akamshika na kumvuta, lakini badala ya kuvutika, wakajikuta wanapaa hewani, ina maana yule nyoka aliwarusha akiwa na lengo la kuwabana, lakini cha ajabu kilichotokea ni kuwa yule Simba aliyekuwa akimkimbiza yule mtu alichukua nafasi ile aliyokuwa kasimama Maua, na akawa kazingirwa na yule nyoka, kukawa ni vuramai.

Hapo kumbukumbu ikamtoka hakumbuki zaidi ilikuwaje, ila baadaye alijiona yupo hotelini kwao anapandishwa kitandani…..na baadaye kukawa ni raha ya ajabu..ooh, mpenzi wangu umerudi m nakukabidhi mwili wangu wote ….oooh, ikawa ni raha ….na mara kukapambazuka, hamuoni yule mtu wala hakumbuki ilikuwa ni ndoto au ni kweli….

**********
Shameji nimekumbuka alikuwa ni ‘Mhuja…’akasema Maua. ‘Huyo mtu alikuwa ni mume wangu, ….kama haikuwa ni ndoto, basi ni Mhuja nilikuwa naye jana, kweli sasa nimeamini kuwa yupo hai, nimemuona mwenyewe kwa macho yangu, akiniokoa toka katika lile joka, akanifikisha hapa nyumbani, ….ooh, mungu mkubwa hatimaye sasa, ….lakini yupo wapi Mhuja, hebu muite,…Mhuja, mhuja….mpenzi wangu upo wapi….’ Maua akawa anaita kwa sauti na mara akakurupuka na kukimbilia nje kama mwehu, na kumuacha Maneno akiwa anashangaa tu. Baadaye Maua akarejea akiwa bado ana macho ya kutafakari..

‘Shemeji , nahisi una tatizo kubwa, na hili tatizo inabidi tulifikishe hospitalini haraka iwezeanavyo, na naona hata safari ya Ngorongoro inabidi tuikatize, tutaifanya siku nyingine, kama kweli hukumbuki kilichotokea jana, basi, hilo sasa ni tatizo kubwa, sitaweza kukaa kimiya na kukuacha uteseke, jiandae tuondoke,….’ Akasema Maneno huku akimwangalia shemeji yake kwa macho ya aibu, aliogopa kabisa kama atamwelezea nini kilitokea jana, basi itakuwa balaa,…hasa alivyogundua kuwa kumbe mwenzake alikuwa anajua kuwa aliyemuokao usiku ni Mhuja na…

Hata Maneno alipojaribu kutafuta njia ya kulielezea lile tukio la jana lilivyo, alishindwa kwani hata yeye aliiona kama ndoto, inagwaje yeye anakiri kabisa ilikuwa sio ndoto, lakini angemuelezeaje Maua , kwa kushindwa kulielezea lile tukio na kushindwa kumfichua Mhuja ambaye Maua anadai kuwa yupo kukazua kubishana na hata Maua akawa hataki hata kula, anadai kuwa ana uhakika kuwa Mhuja yupo na Maneno anajua hilo , anachofanya ni kumdanganya,…ikawa hakuna maelwano hata Maneno akataka kusema ukweli, lakini Maua akawa hasikilizi , na Maneno akaona huo sio wakati muafaka wa kuomngea ukweli wote, ni bora asubiri wakati muafaka, kwani Maua alikuwa kama kapandisha jaziba, na hata kumuita shemeji yake mzandiki, mtu anayependa yeye ataseke, ili baadaye amkose kabisa mume ki kabisa kuongea na shemeji yake,…

‘Kama mimi nipo hivyo ili iweje, kama mimi nipo hivyo na huyo Mhuja utamuita nani, kwanini yeye awepo hai na awe anakuja na kujificha kama kweli anakuali na kukupenda,…kama kweli anakupenda kama unavyodai kwanini akuache uteseke hivyo….hiyo ni ndoto tu, ni akili yako inakuadanganya Maua, Mhuja keshakufa…’ akasema Maneno na alijikuta akizabwa kibao kufungwa mdomo. Akashikwa na mshangao kwani kibao hicho kilitokea bila kudhaniwa, na Maua akaonyesha kweli kakasirika, akasema kwa jaziba

‘Usirudie kauli yako hiyo, kauli hiyo nilishaikubali kabla ya tukio la jana, lakini baada ya tukio hilo la jana sikubali tena kuwa Mhuja keshakufa, Mhuja yupo hai, na jana nilillala naye, kama unakubali kuwa jana nilitoka usiku, jana nilizungukwa na joka, na kwanini usikubali kuwa alikuja Mhuja kunikoa, na hata akanifikisha hapa nyumbani tukalala naye na hata…kwasababu yote hayo nayakumbuka…na niliyaona kama ndoto…’ akasema Maua huku anaonyesha uso wa furaha, kuonyesha kuwa kweli ana uhakika kuwa alikutana na Mhuja. Hapo Maneno alibakia kutahayari, kwani kwa hali ile inaonyehsa dhahiri kuwa, Maua anajua kuwa aliyemuokoa ni Mhuja, sio yeye Maua na kama atajua kuwa aliyemuokoa kule ni yeye Maneno, basi , litazuka jambo kubwa sana, na huenda ikajengeka chuki kubwa sana, na itafika kwa shangazi mtu….ooh, nitamuambiaje yule shangazi, kwahiyo lazima kuhakikisha kuwa sehemu hiyo ya mkanda anaikatwa kabisa…….
***********
Safari ya kurudi Dar ikafanyika haraka haraka na walipata bahati ya kuondoka kwa ndege, ilikuwa ni baada ya kukutana na watalii waliozoena nawo wakasema wapo tayari kutoa ufadhili wa ndege, kwani wao walikuwa wakiondoka kwenda Dar, na walitaka kupata wenyeji ambao watawatembeza Dar, na hata Zanzibar, na kwa vile katika kukutana nawo hapo Arusha, walitokea kumpenda sana Maua , kwa vile alikuwa nao karibu akiwafundisha Kiswahili, basi wakamchukulia kama mwalimu wao, na hata baadaye alipokuja Maneno kujiunga katika mazunguzmo ya kuwafundisha Kiswahili, wageni hawo wakaiona wamepata watu waliowataka, kwahiyo wakapewa ufadhili huo wa kuapnda ndege hadi Dar.
Kesho yake Maneno alipokuja kumuona Maua , alimkuta akiwa na uso wa furaha sana, akamuulizia vipi mbona anafuraha sana, Maua akamwambia;

‘Shemeji hawa watalii wamenipa tenda, na tenda hii inanihitaji niende Zanzibar na wao, kwani wanataka mtu kama mimi ambaye nitakuwa nawo bega kwa bega, kwanza wanataka kujifunza Kiswahili, pili wanataka mtu kama mkalimani wao, na mimi wametokea kunipenda name naona itanisaidia kuliko kukaa hapa na kuanza kuchanganyikiwa kwa mawazo …. nimeona niwe nawo kama awalivyoniomba, na animeongea na shangazi kanikubalia, sizani kuwa kitaharibika kitu, kwahiyo kesho tunaondoka na wao kwenda Zanzibar…’ akasema Maua.
‘Lakini shemeji unakumbuka tumekatisha ziara yenu ya kwenda Ngorongoro kwasababu ya afya yako, kwasababu unahitajika kumuoma dakitari bingwa wa magonjwa ya akili…mimi nisingependelea uende hiyo safari yako na hawo wazungu, mimi naweza kuwatafutia mtu mwingine atakayewafaa, nakuomba kesho twende kumuona huyo dakitari bingwa..tafadhali Maua’ akasema Maneno.

‘Shemeji ina maana mimi umeniona ni tahira au sio, kuwa mimi nina ugonjwa wa akili kwasababu ya kukuambia ukweli. Hilo huniambii kitu, wewe mwenyewe kwa kauli yako umenikubali akuwa kweli ilikuwa sio ndoto…umeniambi wewe mwenyewe kuwa kweli nilitoka usiku, ni kweli au sio kweli, ukanimabi kuwa nilizungukwa na joka kubwa ni kweli au sio kweli…lakini hujaniambia ni nani nani aliyeniokoa, ni nani alilala na mimi usiku, kama sio Mhuja…niambia kama sio Mhuja ni nani..kwasababu nimemuona kwa macho yangu mawili…unanifanya mimi tahira sio…ngoja nirudi hii safari …nitamtafuta Mhuja hata kama ni kwa gharama yoyote, najua…yupo hai….’ akasema Maua akiwa na hasira, na mara wakaja wale wegani wao na mazunguzmo yakabadilika…

Na kweli kesho yake Maua wakaondoka na wale watalii, kuelekea Zanzibari, lakini Maneno hakuwa na amani kwa safari hiyo, alitamani aondoke nao, kwa ajili ya usalama wa Maua, alikuwa anajua kabisa huyo mtu bado yupo katika tahadhari na anatakiwa kuwa karibu na mtu anayemfahamu, je akichanganyikiwa huko kama ilivyotokea huko Arusha, nani atajulia, alijaribu kumshauri Maua….lakini Maua alikataa katakata, na kusema yeye sio mgonjwa wa akili kama wanavyomuita ana matatizo ya kiakili…na hata hivyo, hawa wageni wataongezewa gharama ambayo haikuwepo katika mipangilio yao, na alishakubaliana nao kuwa yeye ataongozana nao, bila wasiwasi, yeye anajiona yupo mzima, wasiwe na wasiwasi na yeye…

Maneno akabakia akiwa hajui afanye nini, aliikuta akiwa katika majuto makubwa, kwasababu kwanza alikuwa keshaweka miadi na yule dakitari bingwa mtaalamu wa akili kuwa watakuja na Maua, akaona haitakuwa vyema akibakia kimiya, akamwendea mwenyewe huyo dakitari bingwa kuonana naye, na ikibidi apate ushauri wa kitaalamu. Akamwendea hospitalini kwake na kumuelezea hali halisi ilivyokuwa na yule dakitari bingwa akamshauri kuwa alivyofanya ndio sahihi, lakini lazima waje pamoja na huyo Maua, yeye atajua jinsi gani ya kumuelezea ukweli ulivyokuwa, na ingawaje uwezekano wa kutokea kutokuelewana upo, lakini haitachukua muda kama swala hilo litanyamaziwa hivyo hivyo, kwani huyo muathirika, yeye kajenga hoja kuwa huyo aliyekutana naye ni aliyekuwa mume wake, na hisia hiyo haitamuondoka akilini mwake mpaka apate ukweli wa tukio lenyewe.

Alipotoka hapo kwa huyo dakitari bingwa akarudi nyumbani kwake na kupata taarifa nyingine kuwa shangazi wa Maua alikuja na atarudi baadaye anamazunguzmo na yeye, ya muhimu sana…! Kauli hii ikamtia wasiwasi, mazunguzmo ya muhimu sana, akaanza kuwaza, afanye nini, kwani shangazi yule ndiye mlezi na mzazi wa karibu wa Maua na anakumbuka mazunguzmo yao wakati wanamuaga kwenda kutalii mbuga za wanyama alimwambi mwanzoni kama utani, lakini baadaye akawa anatoa kauli za ukali, za vitisho, alianza kwa kumwambia; `Maneno nakuona ulivyo mwingi,..maneno-maneno, kama jina lako lilivyo, ni sawa inatia moyo kwa kuwa mwanentu anahitaji maliwazo kama hayo, ila nakuomba halahala mti na macho usije ukatumia tatizo la shemeji yako kwa ajili yako..nawajua sana nyie wanaume, huyo ni mwanangu nimemlea mwenyewe, anahitaji muda wa kukaa na kutafakari kabla hajaingia kwenye ndoa tena, najua kweli ni vyema akapata mume kama wewe, mtu anayemjali, lakini …nakuomba tafadhali usije ukaanza ….ukaanza….’ Shangazi hakumalizia yale maneno lakini Maneno aliyaelewa, na kumuahidi kuwa kamwe hatafanya dhambi hiyo

‘Shangazi hivi mimi huniamini, unafikiri kwanini nipokaribu sana na Maua, sio nafanya hivi kwa uchu..hapana, ni kwasababu mimi na Mhuja tulikuwa marafiki wa ukweli na hili nataka jamii ilithibitishe hilo kuwa kwa hivi sasa mke wa rafiki yangu yupo kwenye shida, yupo kwenye dhiki, siyo ya kihali bali ya kihuzuni, ya kimoyoni ambayo inayohitaji mtu wa karibu wa kumliwaza, na mimi ndiye rafiki wa mume wake wakiukweli,….’ Akasema Maneno.

‘Nyie wanaume nawajua sana, hayo Maneno yako yasije yakawa maneno kweli, maana tutakosana kabisa, …hili nakuhakikishia hata ikibidi kukufunga nitakufunga, sina mhezo na mwanagu..’akaongea shangazi akionyesha udhabiti wa kauli yake, halafu akazungumza kihekima kwa kusema ` Ndio ninakushukuru sana kuwa umemjali sana mwenzako na umemuonyesha upendo wa dhati, kuwa hata kama mwenzake hayupo lakini ana mtu anamjali na kumlinda, lakini kila kitu kina muda wake, na muda wa mengine, kama yapo, usubiriwe,… kwasababu mimi sio mtoto mdogo, najua kabisa nini kilichopo moyoni mwako, hata kama hujafikia kuniambia, ila kama ni hivyo nisingependa kamwe yatokee haraka hivyo,…

‘Mimi sio mtoto mdogo, na ukumbuke mwanetu ana heshima zake, sio mwenzake kafa, inakuwa kama vile, kufa kufaana, haipo hiyo, kila jambo kwa muda wake, nielewe kauli yangu, …nakuomba tafadali sana, tafadhali, usinije ukaniona mbaya kwasababu mimi mwenyewe nipo, na nilikuwa tayari kuwa naye kwa lolote lile, lakini wewe mwenye uliniomba kuwa kwasababu Mhuja alikuwa rafiki yako ungelipendelea kuhakikisha kuwa mkewe anaishi maisha mazuri na hata ikifikia muda kampata mwenzake wewe utakwua tayari kuhakikisha kuwa kweli anamfaa, hapo utasimama kama kaka mtu…sasa isije ikatoka kwenye ushemei na kuwa mengine …kwahiyo narudia tena, linda heshima ya mwanangu na linda heshima yangu…’akasema shangazi mtu.

‘Shangazi nakuhakikishia kuwa kama litatokea kama unavyonidhania wewe niweke ndani, na nitamuomba hakimu anifunge maisha, mimi na Mhuja ni zaidi ya ndugu, leo hii nimsaliti kirahisi hivyo…hapana Shangazi hilo halitatokea kamwe, kwanza nitamuanzaje huyo shemeji yangu!..’ akasema Maneno na huku moyoni akiongezea kwa kuwaza akisema kimoyomoyo `Shangazi kiukweli kama binadamu nakubali kuwa hamasa hizo za kumpata mtu kama Maua zipo hilo nalikukubali, na…mmh, shangazi ningelitamani nimapte mtu kama Maua katika maisha yangu, lakini sio kwa kipindi kama hiki, nitauweka wapi uso wangu,’ akamwangalia shangazi yake akatabasamu akasema;

‘Shangazi unaonekana huniamini kabisa, uwe na amanikabisa kwanza huyo shemeji mwenyewe siunamuona alivyo, utamwiingiaje,kwa mambo kama hayo, hapana, namuheshemu sana, na niyailinda heshima yangu…nakuhakikishia hilo shangazi…’akaongea kwa heshima.

‘Sawa Maneno ukumbuke sana kuwa ahadi ni deni,… ila wengi waliahidi kama wewe na mwishowe wakaumbuka, na kwangu utaaumbuka kweli, sina utani…mwanangu kapitia hatua ngumu na sasa kaanza kutulia naomba safari yenu iwe ya heri…’akasema shangazi mtu,

`Je heri yenyewe ndiyo hiyo…?’ akajikuta anajiuliza Maneno kwa sauti, huku akiwaza mengi kichwani, je shangazi yake huyo anamuhitaji kwa lipi, ….huenda Maua kashamwamia nini kilitokea huko Manyara, na shangazi anataka kujua ukweli ulivyo , na kama anataka kujua ukweli ulivyo yeye Maneno atamwamba nini,….?
*************
Maneno alikuwa kama anaota ndoto mbaya, akashituka toka usingizini na kuiona akihema kama vile mtu aliyekimbizwa, akakurupuka kitandani na kusimama, alivaa nguo za baridi kwani alikuwa kalala na nguo nyepesi, kwasababu ya uzoefu wa safari, alijua avae nguo gani na nguo gani ziwe karibu na kitanda kwa ajili ya dharura…alihisi kuwa kuna harati, lakini hakujua ni hatari gani, alichofanya ni kutoka kule chumbani kwake, na alipotoka pale chumba caha mapumziko akakuta mlango wan je upo wazi…tumeingiliwa na mwizi, ilikuwa wazo lake la kwanza..

‘Maua, upo, Maua…’ akaita huku anagonga mlango wa chumba cha Maua, lakini hakusikia sauti yoyote, akataka kuufungua mlango lakini akasita, huenda shemeji yake kalala na huenda kalala vibaya, kuingia bila ruhusa inaweza ikaleta muonekano mbaya..akagonga tena na tena, alipoona kimiya, akaangza kuona wasiwasi na hapo akakumbuka tukio la jana, jinsi alivyomuona shemeji yake akiwa kabadilika alikuwa kasimama mlangoni huku anaangalia kamba, kwanini alikuwa akiingalia ile kamba, na alipomuuliza kulikoni akawa kama kakurupuka toka usingizini na kukimbilia ndani.

Akaona subira imemshinda akafungua mlango na ulikuwa haujafungwa kwa ndani, kinyume na alivyo Maua tangu wafike hapo huwa anafunga mlango kwa ndani, labda kwasababu ya usalama, kitu ambacho Maneno hakukipenda, lakini aliona asimshinikize shemeji na huenda akamzania vibaya kuwa anaomba iwe hivyo ili pate mwanya wa kua kumsumbua, kitu ambacho Maneno hakuwana cho kichwani kabisa..
Alipoingia chumbani alikuta shua lipo chini, ..na kitandani hakuna mtu…akageuka huku na kule , lakini hakuona dalili ya mtu, akaanza kuingiwa na wasiwasi, …akatika haraka mle ndani hadi nje,wazo lake la kwanza ilikuwa kuiangalia ile kamba ambayo shemeji yake alikuwa akiingalia mchana, alisahahuu kuiondoa pale,kwani jinsi sheemji yake alivyokuwa akiingalia alihisi alikuwa na maana yake,….ile kamba haipo, …akaanza kuwaza vibaya, akakumbuka hadithi za watu waliojiua kwa kamba.

‘Haiwezekani, shemeji yangu atakuwa kapatwa na nini..mbani anakuwa kama kachanganyakiwa, kama ningeliua hili mapema ningelimpeleka hospitali akaonane na dakitari bingwa wa mambo ya akili…’ akajikuta akiongea peke yake…

‘Sasa nitamtafuta wapi..naumbuka jinsi walinzi wa hapa walivyotukanay kuhusiana na hali ya hapa kuwa watu wasitoke nje wenyewe, au kuingia msituni…’akaanza kuogoa mwenyewe, maana alisikia mngurumo wa simba…ooh, kama Maua yupo huko…mungu wangu mtoto wa watu keshaliwa na Simba. Maneno ni muongeaji ,lakini kw ahatarii za wanyama, ….hakuweza kuwa na uajsiri huo, akaona akamuulizie mlinzi…lakini kabla hajafika mbali akaona kitu kimedondoka chini…alipokisogelea akaona ni picha ya mtu…akawasha taa ndogo aliyokuwa nayo…picha ya Mhuja..

‘Maua keshaingia msituni na huenda kaeshajinyonga…’ akasema na bila kwenda kumuona mlinzi akaanza kufutaili hisi ake zilivyomtuma, kuwa huyu mtu atakuwa kapitia hapa, akwa anatembea harahaharaka hadi alipofika sehemu fulani, akaona kitu kikitingishika kwa mbali , mara kukapita kitu kama mshale kukatisha barabra…oh, fisi au chui..akasiamama, kurudi nyuma sasa mbali kwenda mbele kunatisha.

Wakati anawaza hili kwa mbele kidogo akaona kitu cheupe…yule sio mtu yule..akaaingiwa na mashaka, isije akawa mwanga..akaanza kumfuatili taratibu, lakini badaye akasikia kitu kama kinakuja nyuma yake, akaingiwa na mashaka, haraharaka akaongeza mwendo kuelekeak kule alipoona hicho kitu cheupe, alifanya hivyo kwasababau ya kuogopa kuwa kunakitu kibaya kipo nyuma yake…akaongeza mwendo kama anakimbia, ilimfanya afikie pale alipoona kile kitu jwa haraka…

‘Maua….ni Maua, mbona kaganda kama kasimamishwa na kitu, akamfikia haraka na kumdaka na mara kitu kwa chini kikajifunga haraka na kuwafanya watupwe huku na kule….bahari yao , maana kilichokuwa kikiwafuata nyuma kilikutana na mzunguko wa jaoka kubwa na kuwafanya wao wanasuke na kuikuta wamelala chini na kwa haraka Maneno akamzoa zoa Maua na kukimburuza mbali …huku akishuhudia vurumai la Simba na nyoka chatu…hakuwa na muda wa kungalia, akambeba Maua begani na kuanza kukimbia naye hadi Hotelini.

Maneno hakuweza kulala kabisa, alipomfikisha Maua hotelini akiwa kachoka, akamwela kitandani kwake na alipomuona yupo salama, na kazindukana ingawaje alikuwa kimiya haongei lolote, lakini alimkagua na kumuon ahana jeraha lolote, aliinuka kuondoka, lakini akashangaa kuona mkono wake umekamatwa...

‘Shemeji tafadhali usiondoke, …naogapa..naogapa kuna kitu kinaniandama kinaniamrisha kujiua…’ akasema kweli akionyesha macho ya uwoga, …Maneno akawaza sana na kumsogeza Maua kitandani halafu akajifanya kama kalala pembeni yake, akiwa na nia kuwa akimuona kapata usingizi anaondoka zake, lakini haikuwa hivyo, kila akipogeuza kichwa kumuangalia alimkuta shemeji yake macho yapo wazi lakini hayapepesuki ni kama yamefunuka tu na hata alipojaribu kupitisha mkono mbele yake kama vile atayapepesa, lakini alikuwa hivyo hivyo tu.

Huyu mtu halali jamani…mbona shida hii.. mbona yupo hivi, kama…ooh, ikifika subuhi cha kwanza kwa dakitari, hili sasa ni balaa….mungu wangu mtoto wa watu , nitasemaje…..’ akajikuta akisema mwenyewe na akajaribu kukaa macho wakati wote, alikuwa anakaa kwenye kiti, na wakti mwingine anasogea kitandani kukaa pembeni, na mwishowe akajikuta kajilaza kitandani pembeni na alipolala shemeji yake na usingizi ukamchukua…
********
Ilianza kitu kama ndoto, akajaribu kujizuia, lakini baadaye akawa anavutika na hamasa ikamshika na kuzifuata hisia zake, na hisia hizo zikambadili akili kabisa na kujiona kama mtu anayeelea kwenye bahari isiyoelezeka, juu ya maji ambapo huibuka na kuzama, lakini kwa mtindo wa aina yake, na jinsi muda ulivyozidi kwenda, na akili nayo ikawa haiona chochote zaidi ya raha isiyomithilikai, na hatimaye uzalendo ulimshinda,…. kilichotokea baadaye ilikuwa kama miujiza na baada ya heka heka ambayo kwake ilikuwa kama ndoto, ndoto ambayo aliiombea siku nyingi itokee hivyo, na muda huo aliombea ndoto hiyo iendelee tu, awe anagolea tu, awe anapiga mbizi nz kuibuka tu, hakutamani kabisa kufika ukingoni, kwani raha yake ni ya ajabu, lakini hatimaye mwisho ukafika, na ulifika kwa kasi ya ajabu na kutua ukingoni…oh kwanini nimefika ukingoni, siwezi kurejea tena nyuma, siwezi kuogelea tena, siwezi kupiga mbizi tena, ….akafungua macho yake..oooh, ina maana ni kweli , …. kilichotoeka baadaye ikawa kutahayari..mungu wangu sasa nimefanya nini, oooh, hili sasa ni balaa..mungu wangu imekuwaje nimeshindwa na udhaifu huu….nimevunja ile ahadi…

‘Ohh shemeji nisamahe sana, sijui imetokeaje kuwa hivyo…’ alijikuta akiongea , kwa wasi wasi ,lakini hakusikia kauli ya shemeji yake…shemeji yake alikuwa akihema kuonyeshga kuwa yupo kwenye usingizi mzito na sasa macho yake yalikuwa yamefumbwa, tofauti na ilivyokuwa usiku usiku…alipohakikisha kuwa kweli shemji yake kalala, akainuka kitandani, …..oh, nipo uchi…nilivua nguo saa nagapi, kabala hajapata jibu, akazitafuta nguo zake ambazo zilikuwa zimekunjamana na shuka zito walilokuwa wamejifunika, na akiogopa kumwamusha shemeji yake, akaziona na kuzivaa nguo hizo haraka, haraka huku akijuta kwa tendo hilo,…lakini hata hivyo hakumbuki kabisa kuwa alifanya vile kwa hiari yake mwenyewe…

‘Nani atakubali hilo,… kuwa kweli sikulifanya hivyo kwa hiari yangu, je kama sio kwa hiari yangu, ina maana shemeji….hapana, sikumbuki kunilazimisha’ akajikuta akiongea peke yake. Huku akitoka mle chumbani haraka haraka, alipofika chumbani kwake akakimbulia bafuni, alipomaliza kuoga, akatamani arudi tena kule chumbani kwa shemeji yake, lakini akaona haifai kufanya hivyo, akatoka na kukaa kwenye chumba cha mapumziko, ili kuhakikisha kuwa shemeji yake atakuwa hayupo katika hali mbaya, ya kuhamaki au ya furaha…kwanini iwe ya furaha, …anamua shemeji yake, singelipenda kabisa tendo kama lile, lakini ….hata mim sikupenda itokee hivyo…ngoa nimsubiri, ilii nimuone sura yake ya kwanza tukionana usoni nitajua hisia zake…akajisemea, huku akizidi kuwaza matukio mazima ya jana, hakuweza kuamini kilichotokea…na utashangaa, tukio la mwanzo la harati, halikuwa lipo kichwani mwa Manenoa tukio lile la hatari ambalo Maua alitoka usiku wa manane na kupotea maporini, yeye alikuwa akiwaza tukio lililotokea baada yake hakuweza kujua lilitokeaje…

Hivi ndivyo ilivyokuwa shangazi, nakuhakikishia kuwa sikutumia nguvu, sijui ilikuwaje, tulijikuta tupo tupo kwenye hali hiyo, nakuapia kwa jina mungu, sikumlazimsiha siku…mbaka….na hata yeye inavyoonekana hajui kabisa nini kilitokea, na hata alipoamuka yeye alijua ni ndoto, ila mimi nikamwambi akuwa kweli alitoka nje, …na alihakiki hilo baada ya kuona nguo zake kuwa ni chafu…, na baya zaidi sijui ni hisia zake au vipi anayemuhisi kuwa alimuokoa, anayemuhisi kuwa alilala laal naye ni Mhuja,…na ana uhakika kabisa na hilo, na hilo lilimfanya achanganyikiwe kabisa kuwa kweli kamuona Mhuja, ndipo nikaona tukiendelea kubakia kule linaweza likazuka zengwe….

‘Unajua Maneno sikuelewei mpaka hapo, kwani inavyoonyesha wewe huoni kuwa umefanya jambo baya sana, na unakumbuka tulichoahidiana siku ile wakati mnaondoka…mimi ni mtu mzima, nilishahisi kuwa una mipango yako kichwani, na ni vigumu sana chui na mbuzi kulala zizi moja, wakati chui ana njaa, na mbuzi ni mgonjwa, hana hata nguvu ya kujitetea…unaona lililotokea….umachukua uzaifu wa mwenzako, kuwa kachanganyikiwa, kuwa....ooh, masikini mwanangu Maua,mbona ana wakati mgumu sana,...sasa, kama nilivyokuambia awali na ukakiri mwenyewe kuwa ahadi ni deni…sasa….

Je shangazi atachukua hatua gani kwani ahadi imeshavunjwa…tuzi kuwemo….

NB: Sehemu hii ni ngumu kidogo, na nilipoiandika nilijikuta najiuliza mwenyewe je inawezekana kweli, lakini ndivyo ilivyokuwa imetokea,....sasa swali kweni wapenzi wangu, je kama ungelikuwa wewe ni Maneno ungelifanyaje, na kama ungelikuwa wewe ni Maua ingelikuwaje kwasababu mpaka hapo anaamini kuwa aliyekutana naye ni Mhuja, na je kama wewe ungelikuwa shangazi mtu, ungelichukua hatua gani...?

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

Wewe kweli ni mkali, chaajabu ni kuwa hata wewe mwenyewe ni miujiza, wengine wakuita mdada, wengine mkaka, engine mkuu, mimi nakuita mkali wa visa

Anonymous said...

Ohh, Maneno alikuwa na ajenda ya siri...kaona mwenzake hana fahamu njema, kwani inavyoonekana hapo Maua alikuwa sio yeye....huwa inatokea na wengine baadaye huja kuita mashetani, lakini ni akili inakuwa imetatika, sasa mwenzetu nana akaona hapo hapo. Kama mimi ningelikuwa shangazi kungechimbika, dawa ni kumkamua, ...zimtoke ngombe...lol

Yasinta Ngonyani said...

Hapa itakuwa shida kidogo kutua uamuzi naona nisubiri kinachoendelea maana mambo ya kuota ota si vema...

Anonymous said...

Kwangu mimi maneno hana hatia hata kidogo, ikizingatia kuwa kwanza kama binadamu, na kama mtu mwenye mapenzi kwa Maua na kwa khali waliyokuwa nayo usiku huo.Hana hatia kabisa kama ningekuwa nimesomea sheria ningesimama kumtetea, kwa sababu hakuna anayekumbuka nani alimuanza mwenzake.