Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, July 1, 2011

Majuto ni mjukuu

                                                          picha toka swahilitime.blogspot.com

‘Niruke ni siruke,…rukaaa, niruke nisiruke rukaa....’ huu ulikuwa wimbo wa watoto niliowakuta wakicheza mchezo wa kuruka, toka juu ya ukuta wa nyumba ambayo haijakamilika mpaka chini kwenye mchanga, ambao ulilundikwa kwa ajili ya kujengea, nilipowaona nikaingiwa na wasiwasi, nikaona kama mzazi ni bora niwakemee, waache kile kitendo…nilipowakaribia wakakimbia, nikashukuru angalau nimesaidia kuokoa hatari ile, lakini nilipoondoka wakarudia tena,…kwasababu nilikuwa nawahi kazini, sikuweza kurudi tena, …
 Jioni wakati narudi nikasikia kwa jirani wakilalamika kuwa mmoja wa watoto waliokuwa wakiruka pale kavunjika mkono, na wazazi wake walikuwa wakihangaika huku na kule ili wapate vijisenti kwa ajili ya matibabu ya mtoto, wanadai kuwa walipofika hospitali ya wilaya waliambiwa wampeleke Muhimbili, wanajua kuwa matibabu atapata lakini kwa haraka kiasi gani, na pia kwa vile mtoto anatakiwa kulazwa kuna huduma za vyakula  nk, kwahiyo pesa inahitajika, watazipata wapi, wakati baba mtu kazi yake kubwa ni kulewa…
Nikawaza mbali sana, kwani baba wa huyu mtoto tuliwahi kusoma naye, alikuwa na akili sana, …lakini alikuwa na tatizo moja kubwa ambalo lilimfanya badala ya kutumia akili yake aliyobarikiwa na mungu akawa anaizoofisha kwa sigara,…mara akaanza kulewa, na nasikia alipofika huko mlimani akawa kaanza kutumia unga, na madawa ya kulevya na akili ile aliyokuwa nayo ikawa haina maana kwake kabisa...
‘Jamaa huyu bwana ana akili kweli, licha ya kuwa analewa kupundukia lakini akiingia darasani hutaamini, …anawashinda wote waliokuwa wakikesha kusoma …tunashangaa sana, siku moja alilewa sana na kesho yake ni mtihani, tukajua hataweza kabisa kufanya huo mtihani, lakini ilipofika asubuhi akamuomba jamaa yake mmoja amsaidie kumshika mkono angalau aingie darasani, alipofika alichukua muda mchache akawa kamaliza ule mtihani na kati ya waliofaulu alikuwa mmojawapo, na wengi walifeli ule mtihani…’ akasema jamaa aliyewahi kusoma naye mlimani.
 Mimi niliposikia hivyo nikajiuliza  elimu ya mtu huyu ina maana gani kwake, ina maana ya kufaulu mtihani, na kupata sifa kuwa `ana akili sana..’ kwasababu elimu inamfundisha mtu kujua baya na zuri, lakini mwenzetu huyu hajui kabisa kuwa ulevi kupindukia, uvutaji bangi kutumia madawa ya kulevya ni hatari katika maisha yake…labda anajua kinadhari lakini inapofika kivitendo haonyeshi kujua, keshabobea na kuathirika...
Sasa kaoa ana familia, na kama wasemavyo wahenga maji hufuata mkondo, mtoto wake wa kwanza hasikii na hakamatiki, kutwa yupo kijiweni, na inasadikiwa anaanza anza kuvuta bangi..na wazazi wengi wameanza kulalamika kuwa anakuwa kishawishi kikubwa kwa watoto wengine, lakini cha ajabu darasani anafanya vizuri…nikakumbuka akili ya baba yake, na baba yake hutamba, mwanangu ana kichwa kama cha kwangu…’
‘Sawa, ana kichwa kama cha kwako, lakini sasa kaumia anahitaji matibabu, kisa ni michezo yake, kisa ni utukutu wake, sasa unahangaika kutafuta hela, huna hela, wewe hela yako  inasihia ulevini..ndugu elimu yako inafaida gani kwako na kwa jamii…’ akamuuliza jirani yetu.
‘Sasa mumekuja kunisaidia au kunisimanga, …kama hamtaki kunisaidaia ambaeni….siwezi kushindwa kumtibia mtoto wangu…kwanza mnajua mimi nina digrii ngapi…kama serikali ingejua umuhimu wangu sasa hivi ningekuwa waziri…’ baba mtu akiwa bwiii, alianza kubwabwaja, kama isingekuwa mkewe majirani tungeondoka, lakini ilibidi tupitishe michango ili mtoto akasaidiwe…
Jamani majuto ni mjukuu, ingawaje jamaa huyu anaendelea kulewa, lakini siku akiwa mzima na akili zake huwa anajuta sana, kuwa kilichomsababisha kulewa ni makundi mabaya…tamaa ya kuiga na mwisho wa siku akaiwa hawezi kuacha tena ,na matokea yake, kawa teja …elimu yake haina maana kabisa….hivi kweli uwe na elimu na elimu yako isiwe na manufaa kwako?
Jamani  nazungumza hili kwa masikitiko makubwa, kwani kila kukicha vijana wengi wanaingia katika janga hili, la madawa ya kulevya,…hili janga linazidi kukua, na kizazi kinaangamia , taifa la kutegemewa linapotea..tusaidianeni kuokoa hiki kizazi  kabla hatujachelewa kwani mwisho wa siku  tutakuwa tumechelewa tujue …majuto ni mjukuu!

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Hawa ndio zao wakipata mshahara mtungi kwa kwenda mbele, hajui familia wala nini...halafu anajiita msomi, soma uelimike sio soma ujionyeshe kwa watu..usituone kimya mkuu tupo pamoja na wewe na twapenda sana visa vyako...usichoke kutuandikia hata kama watu hawaweki comments ujumbe umefika!

Anonymous said...

Mimi naona nichangie kidogo kwa hili,huo mtindo wa makonda wanawalipa hawa waitwao wapiga debe, utaona hata gari limejaa lakini huyo mpiga debe analipwa halafu mwanafunzi anasukumwa nje...hawa wote ni wahuni wa kuvuta bangi, tunawalea wenyewe vituoni
Kwanini kusianzishwe vijiji au sehemu vijana kama hawa wakawa wanatumika halafu mwisho wa siku wanapata ujira wao...!

emu-three said...

Vitu vingine ni changamoto za kimaisha, na kipaumbele. Ni kweli wapo hawa jamaa na kila siku wanaongezeka, lakini mara nyingi jamii au serikali haiwezi kumlazimisha mtu kujituma, hasa unapofikia umri wa utu uzima, na wao kama vijana, kujiunga na kusema sasa tumechoka kukaa barabarani tumebuni hiki na hiki, tumejiunga hivi na hivi, twaomba wafadhili..nafikiri wangepatikana....lakini useme, serikali ianze mshike mshike...sijui kama katiba inaruhusu, labda kama kuna kifungu cha wazururaji.
Makonda wanadai wao wakati mwingine wanafanya kama kuchangia kuisaidia hii jamii, maana usipowapa, wataishia kuwa vibaka..na vitu kama hivyo, nilitegemea kuwa watu wataisoma hii na kutoa maoni...nakushukuru sana wewe Any. kwa kuliona hili