Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, July 1, 2011

Dawa ya moto ni moto-28

             


    Maua alipotoka kule nyumbani kwake, alikuwa kachanganyikiwa ...alikuwa hata hajui aende wapi, akaona vyema ampitie Bosi, huenda akampa ushauri wa maana. Lakini hata alipomfikia Bosi kumuelezea nini ameona kutoka kwa mume wake, alishangaa kumuona Bosi hashituki sana, na alionekana akiwa na mawazo yake mengine, lakini baadaye akamshangaza zaidi, pale Bosi alipokimbilia kumwambia kuwa eti aachena na mumewe,  wawe wapenzi ili mwisho wa siku waoane…
‘Nilishakuambia huyo sio mume wa kuishi naye hamuendani kabisa, achana naye, mimi na wewe tuwe wapenzi, na kwasababu mke wangu anashinikiza talaka, mimi ukinihakikishia kuwa tutaoana …nitampa huyo mke wangu talaka yake anayotaka, halafu mimi na wewe tunaoana….wewe huoni kuwa mimi na wewe twaendana…’ Akasema bosi bila kujali hicho alichoambiwa na Manua.
‘Hivi wewe una akili kweli, nakuambia jambo la maana, kuwa kuna picha za kutuzalilisha, na picha hizo zimechukuliwa kwenye CD, na huenda hata ile DVD, iliyopotea atakuwa nayo huyu mume wangu kwasababu inavyoonyesha ndio wao waliofanya hivyo ili kuchuma pesa, …..wewe unakimbilia mambo ya mapenzi..mapenzi gani kwa muda kama huu….sikuelewi kabisa, au wewe unaoan sawa…wewe hujui kuwa nipo hatarini’ akasema kwa hasira Maua
‘Hilo najua, lakini lazima kuwe na mikakati…kwani wsiwasi wako ni nini hata wakionyesha huo mkanda, …kama tuna lengo moja kuwa ni wapenzi wa kweli,… wataishia patupu wakisikia tumeoana…lakini lazima kwanza nikuelewe msimamo wako, maana kama hutakuwa nami, huoni kama…oops’…hapo Bosi akaduwaa, akiwaza mengi, kuwa kama baba mkwe wake anajua hilo, kama mke wake alimuonyesha ile DVD, …kwasasa hana lake, na iliyobakia ni kuhakikisha anamganda huyu Maua ili asije akadhalilika, lakini kama Maua naye atatuppwa nje ya malii ya baba yake, basi hana maana kwake..
‘Kwahiyo mume wako ndiye mshirika wa mpiga picha, …kwahiyo…lakini hebu kidogo, najaribu kufikiri hawa waliomuua mpiga picha, walikuwa wanatafuta nini…nahisi ni huo mkanda…mbona CD, kama hiyo na DVD, nimeviona kwa mke wangu, lakini cha ajabu nilipovichukua nyumbani kwangu kesho yake asubuhi vikapotea kimiujiza, ..nina uhakika mke wangu atakuwa kavichukua…nina uhakika kuwa kuna mahusiano kati ya mke wangu na huyo mpiga picha…sasa mambo yanazidi kuwa magumu…’ hapo Bosi akaanza kutembea mbele na kurudi nyuma, huku akiwa kainama chini kuonyesha kuwa anawaza jambo fulani
‘Mimi nina uhakika mume wangu yupo nyuma ya matatizo hayo yote na huenda baba yangu atakuwa keshapewa hiyo CD, na kama baba yangu kaiona hiyo CD, kama nimjuavyo, basi ataninyang’anya kila kitu au nitaishia kama mama yangu alivyofanywa, … lakini kuwa kama mama sidhani kama …siwezi kujiua kwa pombe, nitapambana naoo mpaka mwisho…baba hawezi kunifanyia hivyo,kwanza mimi nami nina uhuru wangu, lakini je uhuru bila mali , uhuru bila …’ Maua alipofika hapo akashika kichwa, na kusema `sasa nitaumbuka..’ akamtizama Bosi , na Bosi alikuwa mbali akiwaza maisha yake yatakavyokuwa
‘Bosi sasa tufanyeje, maana huyu mtu ndio katoweka na hatujui kapeleka wapi huo uchafu , na najua kwa vyovyote atakuwa kaamua kumpelekea baba , akijua huko ndipo kwenye usalama…sasa..sijui nifanyeje..’ Maua akawa anaruka ruka kwa wasiwasi.
‘Nakuomba kwanza utulie najaribu kufikirii nini la kufanya, najua watu kama hawo watadai pesa..ndilo lengo lao, wakidai pesa, hapo ndipo pakupambana nawo,…kwanza tuliza akili, pili jiandae na hilo litakalokuja…hakikisha una pesa za kutosha…, tukizipata hizo , tutawapa kwa mara ya kwanza, halafu tutawasikiliza nini kitafuata baadaye…lakini kabla ya hapo, tusikuze tatizo ambalo halijatokea , litakushinda hata kabla halijakufikia, jiamini kuwa likija nitapambana nalo, vyovyote iwavyo…kujipa matumaini ndio siri ya ushindi..’ akasema Bosi akionyesha kutokuwa na wasiwasi kabisa.
‘Lakini  wewe umesema mpiga picha mlimkuta kauwawa, huoni kwanza mumeingia kwenye kesi ya mauaji, tatizo juu ya tatizo…au mlimuua nyie?...maana mimii siwaelewi kabisa, mnaua mtu bila huruma, hapana..mimi sasa naogopa kuwa haya mambo yanatupeleka pabaya..’ akasema Maua.
‘Nani kaua wewe…nilikuambia kuwa, tulipofika tulikuta mtu keshauliwa na Maneno hayupo, ina maana kuna watu walikuwa mbele yetu na walikuwa wakifuatilia jambo fulani, kwa huyo mpiga picha na inawezekana ni mtu wao, ambaye aliwasaliti…’ akasema Bosi.
‘Watakuwa nani hao…na ina maana Maneno kakamatwa kwa mauaji au ndio anatafutwa na polizi?’ akasema Maua na kabla hajamaliza simu yake ikaita, akaipokea bila kutizama nani kampigia.
‘Nani…ooh, baba samahani nilikuwa sijui ni wewe…unasema ..unaniita, wapi..napajua..kuna nini…ooh, nitakuja baba ….’ Akageuka kumtizama Bosi , na Bosi aliposikia neno baba akabakia mdomo wazi…na kabla hajasema kitu naye simu yake ikalia, na akamtizama Maua halafu akatizama nani aliyempigia
‘Baba mkwe ananipigia, na…sitaki kuongea naye, najua ni mambo yao yakulazimisha talaka, …sitaki kutoa talaka kirahisi hivyo…mpaka kieleweke…’ akasema huku anaitizama ile simu ikilia …mpaka ikanyamaza, halafu ikaita tena na tena.. na mwisho akaamua kuipokea.
‘Halloh, …’ akaitikia kwa sauti ya mkwaruzo , na ikabidi akohoe ili huo mkwaruzo uondoke‘Ndio nimekusikia baba, nitakuja…sawa, nitakuja, …sawa Hoteli naijua vyema, ..hakuna matatizo…’ akakata ile simu na kusonya
‘Hawa watu wanazania kuwa utajiri wao utanifanya mimi niwe mnyonge wao, wanasema tukutane `Ufukweni hoteli’ bila kukosa…kwanini maswala kama hayo yafanyikie hotelini…hawa wana lao jambo..’ akasema Bosi, na kumuacha Maua kinywa wazi …`Kwanini hata yeye ameambiwa na baba yake anamuhitaji kwa mazunguzmo lakini anatakiwa wakutane Ufukweni Hoteli…
                                                            ***********
 Inspekta akiwa anamsikiliza Docta aliangalia saa yake na kujikuta  akiwa na nusu saa tu ya kukaa hapo, akataka kumwambia Docta aongee yale ya muhimu kwanimuda umekwisha, lakini akaona anaweza akakosa yale ya muhimu kwa kukimbilia ofisini ambapo hatapata la maana , bali ni kusihia kubishana na masaidizi wake….
‘Unasikia Inspekta…leo usiku ndio kilele, na unatakiwa ujipange uje sijui na kikosi au na nini…lakini subiri nikumalizie hayo niliyosikia kwa huyo jamaa yetu..namnukuu, nitaongea kama mimi ndio yeye ili yakuingie vyema’ akasema Docta, .. …
‘Nilipofanikiwa hatua ya kwanza ya kupta kazi katika nyumba ya adui wangu namba moja, nikageukia mbinu nyingine, …kwani ukumbuke nilikuwa na maadui wawili, kwahyo kwa adui wa pili nilikuwa na mbinu nyingine kabisa, na haya yote niliyapanga kitaalamu kwa kuweka ratiba ya muda….kwangu mimii hiyo ilikuwa kazi rahisi kabisa, nilishafanya mengi zaidi ya hayo nikiwa huko Ulaya, ambapo ni sehemu yenye uangalizi mkubwa, sembuse hapa bongo, kwangu ilikuwa rahisi kabisa.
‘Kama nilivyokuambia kuwa mimi nilipokuwa huko Ulaya nilisomea udaktari, kwahiyo nikiwa katika sura nyingine huwa naonekana dakitari, tena dakitari bingwa..bingwa wa magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kisukari..hutaamini kuwa nilisomea hayo yote na nilikuwa nimeiva..utanipeleka wapi nishindwe, sikusomea hilo tu, bali hata kubadili maumbile ya sura, na naweza kutumia ujuzi huo kwa kutumia vifaa vya kuvaa, mtu akabadilika kabisa kwa sura aitakavyo…na ukichnanganya na mambo ya kimazingaumbwe…hapo utajaza mwenyewe….sio hayo tu, utaalamu wa madawa, jinsi ya kuyachanganya…lakini huko achana nako kwanza.
 Nilipofika hapa bongo kitu cha kwanza nilichokifanya nikuanzisha kiliniki yangu ndogo, nikaisajili, kwa vile nilikuwa na taaluma hiyo, na nina viambatishi vyote haikuwa vigumu na nikapata baadhi ya madakitari wakanipa shavu, basi nikaanza kupata wateja,…ni rahisi sana kwa nchi hii yetu, kwasababu watu wengi hawaangaiki kuangalia undani wa dakitari au kiliki iliyoanzishwa , mtu anaumwa akiona kibao cha hospitali, na humo kuna dakitari bingwa….basi anajua ndipo mahali pakuponea, …hata hivyo kiukweli nilikuwa najua kazi hiyo, sio utani, lakini niliifanya hayo kwa malengo mengine kabisa.
Sifa yangu na ubingwa wangu ukafika kwa adui yangu namba mbili…nikajua kwa vyovyote atakuja tu..na hili ndilo lengo langu na nilijua kuwa huyu jamaa kwa  ajili ya pesa zake na matatizo yake lazima akisikia kuna bingwa wa matatizo hayo atakuja, na kweli siku moja akaja kwenye kiliki yangu na akaniambia matatizo yake kuwa ana sukari na shinikizo la damu, nikamwambia kuwa mimi ni bingwa wa magonjwa hayo asiwe na wasiwasi kabisa.
‘Sasa naomba uwe dakitari wangu kabisa, nitakulipa …ina maana muda wowote nikukihitaji uwe tayari, ..’ mimi nikamwambia hiyo haina shaka, akasema kuwa yeye hafanyi mambo kwa mdomo anahitaji mkataba wa kuwa mimi nitakuwa dakitari wake , nikamwambia hivyo ndivyo ilivyo, lazima tuandikishane, basi mkataba ukatengenezwa , akatafutwa wakili , tukaridhiana, na kazi ikaanza, nikawa mara kwa mara nafika kwake kwa ajili ya matibabu yake na wakati mwingine, kumtibia mkewe, au watoto..na hilo ndilo kusidioa langu,…kazi ikaanza ndani ya  adui wangu namba mbili…na ukumbuke hapo nafanya nikiwa na sura ya udakitari,…na kwa makubaliano yangu, asubuhi mpaka mchana, nafanya shughuli zangu, labda kuwe na dharura, kwahiyo asubuhi mapaka mchana nakuwa nani…mfanyakazi wa nyumbani kwa adui yangu namba mbili…!
Inspekta akagwaya, ….
                                         
                                                              *********
Hata mimi nikagwaya, naona tukutane sehemu ijayao katika muendelezo wa hitimisho la kisa hiki, samahani kwa kuandika sehemu hii kiduchu, lakini ni kwa aili ya kuandaa sehemu inayokuja ambayo itakuwa na matukio makubwa...!
Enhanced by Zemanta

2 comments :

Faith S Hilary said...

Yaaaaaani inazidi kunoga na inapendeza kwa kweli...sad ndio tunaelekea mwisho wa story yenyewe...nipo kama kawa kaka

emuthree said...

Ni kweli wangu,bila kufika mwisho story haitanoga,na mwisho wa kisa ni mkasa au sio? Tupo pamoja