Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, July 14, 2011

Leo ni siku `Diary yangu' ilizaliwa




HAPPY BITHDAY
` DIARY YANGU'

 Nimekuwa nikiwaza sana kuhusu umri, nakujiuliza jinsi gani siku zinavyokwenda na hatimaye mwaka unaisha bila hata kujijua, ulitoka kuitwa mtoto, ukaja ukaitwa kijana, hatimaye baba au mama na kuelekea kuitwa babu au bibi…je ulikuwa unahisi kuwa sasa nabadilika hivi? Unaweza ukajua haya kwa kuona uchomvu wa mwili, na mabadiliko ya kimaumbile, lakini `hisia’ za ndani kuwa sasa huyo navuka mwaka, huyo, nakaribia kuwa baba au mama…`huu kweli ni utukufu wa muumba!

 Nilishangaa leo nilipoambiwa unajua leo ni Birthday ya `Diary yangu’ nikashituka, nilipoangalia tarehe kweli nikaona leo ni siku na mwezi ambao blog hii ilitawadhwa rasmi katika mtandao, na kuonekana kila mahala. Leo ndiyo siku blog yenu, ilizaliwa,tarehe  Tuesday, July 14, 2009 ndipo nilipojaliwa kuweka `kitu’ cha kwanza, ingawaje nilikuwa nimeibuni hii blog siku nyingi kabla!

 Sitaki kusema mengi, nawaachia nyie muitakie heri blog hii kwa kutimiza mwaka mwingine, hatuna cha kuwapa, ambacho kitalingana na shukurani tulizo nazo moyoni, kwa kuwa nasi, kwa kusaidia hili na lile, ilimradi blog hii ionekana bora…na mawazo binafsi ninayopewa kwa ajilii ya kile ninachokito akwenu, ninachoweza kusema ni SHUKURANI ZA DHATI KWENU NYOTE!
 Nini niseme kwa leo, nawaachie nyinyi wapenzi wa blog hii mseme, mtoe ushauri, na kila chema ambacho kitasaidia sio kwangu tu na wengineo, …l
Labda niongeze haya maombi mawili, yakiwa kama mawazo ya siku hii muhimu kwa blog hii.
1.       Blog nyingi sasa zinaanzishwa, na sio wote wenye nia safi na kila chema kinachoanzishwa, wengine wanafanya makusudi ili kukiharibu, na kuwaharibia wale wenye nia njema, ya kuelimishana, kuburudisha nk, na kwao kuharibu ni hulka yao, je mnaonaje kukaanzishwa `umoja wa wanablog’ ambao kila anayetaka anaingia na kuwa ndani ya masharti ambayo yatalinda, yatasaidia na yatazuia wale wenye nia mbaya! Natoa kama `sisitizo’ kuwa mtu anaweza akatengeneza sumu akiwa na nia ya kuwaua wengine, lakini sumu ile ikasambaa na hatimaye ikaja kumdhuru mwenyewe , kama sio yeye ni kizazi chake,…mitandao mingine ni sawa na sumu ya kukiangamiza kizazi chetu…na haya mnayaona madogo kwa leo, lakini athari zake ni kubwa sana hasa kwa watoto, najua mnanielewa nikiongea hivi, sawa ni uhuru kwa kila mtu, lakini tuangalie mbele, tuwaonee huruma hawa watoto wanaokua, wanaojifunza…naombeni tuwe makini kwa hili!
2.        Tumeshuhudia baadhi ya wanablog walianzisha blog zao na walikuwa na mambo mazuri tu, ya kusaidia jamii, lakini wamepotea, hatujui kimewakumba kitu gani, huenda ni jambo dogo la kitaalamu, huenda wanaumwa, huenda wamekosa nafasi ya kuingia kwenye mtandao nk. Katika maisha tunataofautiana kama vidole, kuna wanye vibanda vya nyasi, kuna wenye nyumba na kuna wenye gorofa, hii ni mifano tu, sawa na blog zetu, ..kuwa kuna wenye blog nzuri sana sawa na wale wenye magorofa, ambao wamejaliwa, sio vibaya mkajaribu kuwasaidia wenye nyumba za nyasi, kama uwezo huo upo, kiufundi, kuwatangaza nk…sidhani kama itawavunjia hadhi zenu, nashukuru wapo wamefanya hivyo, hata mimi nawashukuru sana walionisaidia hadi kibanda changu kikaonekana hewani, mungu awazididshie kwa wema wao huo…Nisingependa kuwataja hapa kwani wapo wengi…

Hayo ndio maombi yangu kwa leo
Na nahitimisha kwa kusema HAPPY BITHDAY `DIARY YANGU’ …NA NAWATAKIA KILA-LAHERI WAPENZI WOTE WA BLOG HII. TUZIDI KUWA PAMOJA!

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

11 comments :

samira said...

happy birthday diary yangu siku zimeenda
pia nachukua nafasi hii kukupongeza miram3 kwa kuwa nasi kutujali kipindi chote hiki hujali mvuwa wala juwa upo nasi umeonyesha upendo wa dhati kwetu sisi wafuatiliaji wa blog hii hata kama kuna ugumu gani unakuwa pamoja na sisi
nakupongeza sana m3
hongera

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana "DIARY YANGU" kwa kutimiza miaka miwili, hongera pia kaka M-3 kwa kulifanikisha hili, kwani bila wewe kaka hakuna Diary yangu,.

Tumejifunza mengi sana na moja binafsi huwa naliona kila mara ni hili la uwezo wako wa kuandika, nimejifunza mengi mno na unanitia moyo sana kila nipitiapo hapa kwani napenda pia kuandika ila nguvu kama zako ndo sina....!!
Hebu naomba niwe mwanafunzi wako kama utapenda ili nami nitimize azma yangu..

Kila la heri kaka...na ubarikiwe sana na DIARY YANGU!!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Happy Birthday 'Diary Yangu"

Tuko pamoja....Hilo dongo lingine nimeliona na limenigusa....lol!

ANID UPDATES said...

heri ya kuzaliwa mwanalibeneke mwenzetu, nakutakia kila la heri katika harakati zako hizo za kutupa simulizi nzuri kuopitia katika blogu yako

Anonymous said...

happy birthday Diary yangu. Uzidi kutuletea mambo moto moto.

Subira

Anonymous said...

Hongera na pongezi kutimiza miaka miwili. kweli kazi ipo ukiwa bado mchanga na mdogo katika dunia na ulimwengu wa elimu uliojaa maendeleo na mashindano nakupa shahada kuwepo hewani mpaka leo na mafanikio mema nakuombea mola akupe umri na ramadhani uifunge baraka .kheri na matamanio yako yatimie ameen.

mumyhery said...

Hongera sana na kila mwanakwetu, kaza mkanda tupo pamoja!!!

Rachel Siwa said...

Hongera sana ndugu,nakutakia kila la kheri na baraka katika yote,Pamoja!

EDNA said...

HAPPY BIRTHDAY DIARY YANGU.KEEP UP THE GOOD WORK.TUPO PAMOJA MKUU.

Faith S Hilary said...

Ok nimechelewa...lakini blog si bado ina miaka miwili ile ile au? Hehehe! Hongera kaka kwa kuiendeleza vyema, sisi tunaofurahia kazi yako tutakuwa pamoja nawe hadi sijui ifikishe miak mingapi! Always pamoja :-)

Anonymous said...

Jamani my Boss. kwanza nasikitika sana kwani mi sikuwepo hewani takribani wiki, network huku kwetu inasumbua sana. Namshukuru Mola leo nimeipata. Naona sijachalewa pia, HAPPY BIRTHDAY DIARY YANGU. Nina kipolo cha kusoma story zote leo. Sijui nitaacha wapi na muda wenyewe wa kunyang'anyana na mwajiri.

TUPO PAMOJA.