Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, January 4, 2011
mwenye kovu usidhani kapoa-2
Familia hii ya baba yangu mdogo ilikuwa ya watoto watano, watoto wa kike walikuwa watatu na watoto wa kiume walikuwa wawili. Baba mdogo alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni moja hapa jijini, yeye ni dereva na fundi makenika pia. Mke wake, yaani mama mdogo ni mjasiriamali, yeye alikuwa akifanya biashara zake ndogo ndogo za hapa na pale , kwahiyo kimaisha familia hii haikuwa na shida ya kubadili mboga, na kumudu hiki na kile, na uzuri walikuwa na nyumba yao hapahapa Dar.
Baba yangu mdogo alikuwa na upendo sana, kwa mimi ninayemjuwa, kwani nimeishi naye na upendo huo sio kwa watoto wake tu hata kwa sisi ambao ni watoto wa kaka yake. Na wakati mwingine ilionekana kama anatupendeela sis zaidi kuliko watoto wake mwenyewe hasa mimi, nilionekana kipenzi chake cha karibu sana kiasi kwamba alikuwa anafanya upendeleo wa wazi kwangu ili watoto wake na wao waonyeshe bidii na juhudi shuleni, ili wawe kama mimi, kwani watoto wake walikuwa bado kwenye shule ya msingi na mimi nilikuwa nipo sekondari kidato cha sita.
Ilikuwa nikirudi likizo, baba yangu huyu alikuwa akiniandalia vyema, na alinijali sana kuliko hata anavyonifanyia baba yangu mzazi, kwahiyo nilimpenda sana. Na kwahiyo hata wadogo zangu walinipenda hivyohivyo, licha ya kuona kuwa napendelewa zaidi yao. Na mimi nikawa nawasaidia sana kimasomo ninapokuwa likizo. Na wakati wote walipenda likizo zote niwe nakuja hapa Dar badala ya kwenda kwa wazazi wangu huko mikoani, lakini isingewezekana kuwa hivyo kila likizo....
Licha ya baba huyu kunipendeela mimi zaidi , lakini upendo kwa familia yake ulikuwa mkubwa sana. Na baba yangu mdogo huyu alikuwa mcheshi na alikuwa karibu sana na watoto wake, kiasi kwamba walikuwa hamuogopi kama watoto wengine wanavyomuogopa baba. Alikuwa na tabia ya kurudi na kitu chochote mkononi kwa ajili ya watoto, na mara nyingi kwa vile anajua kuwa watoto wanpenda chips, basi alikuwa kipita sehemu wanapotengeneza chips na kuja nazo nyumbani, au mara nyingine anakuja na soseji, au nyama choma.
Kwa mapenzi ya watoto wake alikuwa alihakikisha kuwa lazima awaone kabla hajalala, na wakati mwinghine anarudi usiku sana, lakini lazima awaamushe na kuwasalimia, kuwauliza hali na kama wana matatizo yoyote , halafu huwapa zawadi alizokuja nazo. Watoto wakawa wanampenda hata kuliko wanavyompenda mama yao. Na kama unavyowajua watoto, wakawa hawalali mpaka baba arudi, ili wapate zawadi, hasa chips na soseji.
Ikatokea siku moja mama mdogo akawa kasafiri kwenda kijijini kwetu kusalimia na safari hiyo akawachukua watoto wadogo watatu , na kuwaacha wale wakubwa wawili, ambao walikuwa binti mmoja wa ambaye alimaliza darasa la saba na alikuwa akisoma `pre-form one’ kwa ajili ya maadalizi ya kwenda kidato cha kwanza. Mdogo wake huyu binti aliitwa Denis yeye ndio alikuwa kaingia darasa la saba, na kila mmoja alikuwa na chumba chake. Maya alikuwa katika ule umri ambao wasichana huwa wanapendeza na mashallah alijaliwa umbo, sura …!
Usiku wake baba alichelewa sana, hawa vijana wawili wakaamua kwenda kulala, na baba akarudi na kwa vile alikuwa na ufunguo wa akiba, alifungua mlango bila kuwaamusha , na akaelekea chumba chake. Na kama kawaida alikuwa na zawadi. Alifika chumba cha Denis, akamkuta kalala fofo, na hata alipomuamusha hakuamuka, siunajua tena mipira na michezo ya mchana kutwa, kijana huyu alikuwa kachoka sana, Baba akamuwekea zawadi yake kwenye kimeza cha kusomea kilichokuwepo karibu na kitanda.
Baba mdogo akaelekea chumba cha binti yake, akagonga kidogo, na binti sio mlalavi akagutuka na alijua kuwa ni baba yake, akakrupuka na khanga moja na kufungua mlango. Baba akamwambia aje chumbani kwake akachukue zawadi yake. Maya hana wasiwasi kwani mara nyingi wanafanya hivyo. Akajifunga vizuri khanga mbili , na akatoka kuelekea kwa baba, huku moyoni akisema, atazifaidi zawadi peke yake, kwani mdogo wake akilala inakuwa shida kumwamsha.
‘Hodi baba, mimi Maya,…’ Maya akagonga mlango wa chumba cha baba, na baba akamwambia aingie. Na alipokuwa akiingia mlangoni baba mtu akamwangalia kwa macho ya tamaa. Alisema moyoni, mtoto huyu yupo kama mama yake nilipomuoa, anafanana, sawa kabisa. Akilini ibilisi akaanza kucezacheza.
‘Kaa kula chips zako hizo hapo na soda, mimi ngoja nijimwagie maji…’ Akatoka kuoga, na alikuwa kipepesuka kama mtu aliyelewa. Lakini mzee huyu hata kama kalewa vipi hajionyeshi, ana nguvu za ajabu. Akaoga harakaharaka, huku akilini akiwaza mengi, na akarudi chumbani kwake, na kumkuta binti yake anadonoadonoa zile chips, zilikuwa zimemshinda kwani ilikuwa usiku sana na usingizi ulishajaa machoni akaona ni heri aziache hadi kesho yake.
Baba akarudi toka bafuni na taulo kiunoni, na kuanza kumuuliza binti yule habari za masomo, na habari za siku nzima kama kawaida yake, lakini anavyoongea alikuwa akionyesha kulewa kinamna fulani, alisema Maya wakati ananihadithia. Baba anakunywa lakini pombe haimuathiri, na pale nilimuona kama anaigiza ulevi, sio kawaida yake , sijui kwanini alikuwa akiigiza vile.
‘Najuta sana dada kwa kumwamini baba kiasi kile, najuta kwanini niliamuka peke yangu kwenda kwa baba, wakati mdogo wangu Denis, kalala, labda ni uroho wa chips, kuwa nile peke yangu au ndio siku ilipangwa hivyo haya yanikute…’ akainama chini akiwaza.
‘Baba mimi naona nina usingizi, nitazila hizi chips kesho, na…’ akapiga miayo nakujinyosha. Na baba mtu akamangalia mwanae anavyojinyosha , maumbile yale yakamkumbusha mbali, akajilamba mdomoni. Ibilisi akamnong’oneza kitu, na yeye akatabasamu, akamwangalia binti yake akiinuka pale alipokuwa kaka, naye akainuka pale kitandani alipokuwa kaka na taulo.
Binti wakati kainuka kuondoka, akiwa anajifunga vizuri khanga yake, na huku anajilambalamba mdomo kwa utamu wa chips, akaukaribia mlango, na wakati ananyosha mkono kufungua mlango, akasikia bega likishikwa kwa nyuma, akageuka kuangalia vipi, baba kaona nini begani kwake, na kabla hajasema kitu mkono ukaziba mdomo……
Yaliyotokea hapo, ilikuwa unyama, ambao sio tu ulimuumiza huyu binti, lakini ulimuathiri sana kiakili, na hata ukiwa naye karibu utagundua kuwa ana tatizo la kiakili.
Baada ya tukio hilo la kinyama, binti usiku ule ule aliondoka na kwenda kwa shangazi yake, akiwa anavuja damu, na akiwa na maumivu makali. Hakuyajali yale maumivu au kuvuja damu, mbiombio hadi kwa shangazi yake ambaye hakuwa akiishi mbali na hapo nyumbani.
‘Njiani alikuwa akiomba gari lije limgonge afe, alitamani kama kungekuwa na aina ya sumu ainywe na maisha yaishilie mbali, hakuamini kuwa baba yake mzazi anaweza kumfanyia kitu kama kile, je kweli ni baba yake huyu, na siku nyingi analewa, haiwezekani iwe ni pombe imemfanya amfanyie vile. Alilia sana, hadi alipofika nyumba ya shangazi yake. Akagonga na shangazi yake akaamuka haraka akijua kuna tatizo kubwa limetokea.
‘Kumetokea nini Maya, vipi , mbona upo hivyo, ingia ndani haraka, usiku huu jamani, mumeingileia na majambazi,..Macho ya shangazi yakatua kwenye miguu ya yule binti na kuona damu ambayo ilikuwa imekoma kutoka kutoka, lakini ilionyesha dhahiri inatokea wapi. Shangazi mtu kwa mawazo ya harakaharaka akdhania huenda yule binti yupo katioka siku zake, na imekutana na tukio la majambazi kwahiyo huyo binto alishindwa kujijua kuwa …
‘Hebu Maya niambia haraharaka na…’ akamwonyesha kwa kidole miguuni
‘Shangazi, baba kani…kani…baka…’ akasema na kudondoka chini, akazirai.
Shangazi mtu hakuamini yale maneno, akamchukua yule binti wanguwangu akamuweka juu ya kochi akakimbilia ndani na bahati nzuri kulikwa na mai ya moto yalikuwa kwenye chupa ya chai akayamimina kwenye beseni akarudi na kuanza kumvua yule binti nguo na kumsafisha na kumpaka dawa anazozijua kuwa zitamsaidia.
Binti akazinduka na kuanza kukimbia, shangazi akawa anakazi ya kumshikilia hadi akatulia na akaanza kumhadithia kwa ufupi nini kilitokea.
‘Sikiliza Maua, usiseme lolote kwa yoyote, wewe kaa hapa mimi asubuhi hii, naona saa hizi ni saa kumi, nitadamkia huko kwa kaka, wewe tulia, atanitambua huyu mtu, yaani kaka, kaka kashikwa na ibilisi gani., Kaka mpezi wa watoto, jinsi gani ananvyowapenda nyie,…siamini. Unasema kweli Maya, au kuna mtu kawaaingili ana unafikiria ni baba yako…we tulia, njoo huku ulale, mimi nitamuonyesha kuwa hili alilofanya ni janga katika familia.
‘Shangazi mimi sina usingizi…mimi naenda polisi….’ Akasema Maya.
‘Nishakuambia hili niachie mimi, ukienda polisi ndio itakuwa nini, wataishia kukuchungulia, uzidi kuaibika, na …itakuwa aibu kubwa kwenye familia. Wewe lala, kunywa kidonge hiki cha usingizi, nitapambana na kaka kesho, hawezi kuiabisha familia yetu, hapana, hapa kuna jambo...huyu kalogwa, haiwezekani kaka yule yule ninaye mjua mimi...'. Maya akapokea kile kidonge na kukimeza na bahati nzuri usingizi ukamshika hadi asubuhi.
Kesho yake shangazi akadamkia kwa kaka yake , yaliyoongelewa huko hutaamini,...kaka alikutwa kama kachanganyikiwa, akawa mdogo kama sisimizi, akampigia magoti dada yake kitu ambacho hajawahi kukifanya maishani...damu ni nzito kuliko maji, na kesi ya nyani kwa tumbili, ikafikiwa mamuzi kuwa hata mkewe akirudi asiambiwe na swala hilo likazimwa kiaina. Na mpaka mama mdogo anafariki hakubahatika kujua kisa hicho, Mama mdogo alifariki kwasababau ya maradhi mengine, lakini hakuwahi kujua tukio hilo, kwani waliolijua ni muathirika, shangazi na mimi niliambiwa kwasababu nilikuwa karibu sana mdogo wangu huyu.
Baada ya tukio hilo mdogo wangu huyu alikataa shule kabisa na kuondoka kwenda kuishi kijijini kwa baba yangu mzazi na hakuwahi kuwaambia wazazi wangu kwa kina, ila tu aliwaambia haelewani na wazazi wake anaomba aishi huko kijijini, na kweli ikawa siri kati yetu wale tuliobahatika kujua hili tukio, yaani mimi shangazi, muathirika wa tukio hilo na baba mzazi aliyemfanyia unyama mwanae. Hadi mama mdogo alipofariki nami nikapata nguvu ya kukitoa hiki kisa kwenu, hasa kwa ajili ya kumsadidia huyu mdogo wangu.
Hivi sasa mdogo wangu huyu ni mdada mkubwa lakini hajaolewa na hana mpango huo, anasema kovu la jeraha lile halitaisha abadani na mwenye kovu usidhani kapoa. Nilimshawishi asahau na amsamehe baba yake, yeye alisema, kovu halitafutika, ila kwa baba yake keshamsamehe kwani binadamu ni mkosaji na haoni kwanini aendelee kumchukia, kama yeye kakiri kuwa kafanya kosa na katubu kwa Mungu, nay eye kamsamehe, lakini hataki kumuona kabisa, licha ya ushawishi wangu wa mara kwa mara na pia kasema hataki kabisa kuolewa, kwani wanaume wote ni sawa, na anaogopa mumewe asije akambaka mwanae kama alivyobakwa yeye. Yeye kaamua kuwa mwanakijiji,
Je wewe uliyebahatika kusoma kisa hiki unamshauri nini huyu dada. Toa ushauri wako, na umpe jinsi gani ya kuyashinda haya masahibuu yaliyompata. Kumbuka leo kwake kesho kwako, au kwa jamii yako, ukilizuia leo kwa ushauri utaokoa jamii kwa janga hili na kwa mola utakuwa shahidi. Ahsanteni sana
Ni mimi: emu-three
13 comments :
Jamani hili ni tatizo la kidunia, sio hapa tu bongo hebu ingieni humu msome
:http://www.dailymail.co.uk/news/article-562377/Pictured-Inside-cellar-father-locked-daughter-24-years-repeatedly-raped-her.html
Kwa ushauri wangu kwa huyu binti, kwanza hatua hiyo kubwa aliyofikia kumsamehe baba yake inaonyesha kuwa anaweza pia akayasahau yote yaliyopita.
Kosa lililofanyika nii kuyamaliza kienyeji na haya ndiyo yanazidi kulikuza hili tataizo, ukisoma wikii pedeia hapa utaona malezo mazuri sana. Jinsi janga hili lilivyo la ubakaji na data zake kidunia.
http://en.wikipedia.org/wiki/Rape_statistics
Zaidi nampa pole sana huyu dada na mungu amjalie asahauu hayo yote. Ila nawaasa ULEVI NI KIVUTIO KIKUBWA SANA KWA UBAKAJI, CHUNGENI SANA HILI.
Hakika ni kweli kabisa nami napenda kumuunga mkono mchangiani aliyetangulia wa 9:19AM kuwa hatua aliyofikia Maya ni kubwa sana ya kumsamehe babake. Na ni kweli walifanya kosa kutoripoti polisi hata kama ni baba kwani swala hili kama tunalididimiza kwa kumaliaz kindugu ubakaji hautaisha. Pole sana Maya na mungu awe nawe. Jaribu kusahau hata kama kovu haliponi.
hata kama ni tamaa,huwezi kumtamani mtoto wako,huyo baba alikuwa shetani tu,na alikuwa anaficha ushetani wake kwa kujifanya anawajali watoto wkae kumbe fisadi
da pole sana dada kwa yalokufika ushauri wangu ni huu naomba kubali kuolewa kwani hujafa hujaumbika mambo yote mwachie mungu najuwa inauma sana sana lakini ndo ishatokea utafanya nini na utakaa ivyo mpaka lini
wanaume wengi wapo kama watoto wanaweza fanya chochote
usikae tu ivo kama ikitokea riziki olewa ujipatie vitoto vyako naamini utapata jaraja
Pole sana Dada,Dunia ina mambo hii.
Tatizo alilo nalo Maya ni kuwa ameshindwa kujitanabahisha kati ya yeye, babake na wanaume.
Kinachotendeka ni kuwa anatembea bado na babake badala ya kuachana naye aendelee na maisha yake. kama anaamua kutoolewa kwa sababu ya babake na huo uwoga wa kuwa mumewe atakuwa mbakaji! Huu ni ujinga na atakuwa anadhani anajisaidia kumbe anajiumiza...babake ama mwanaume yeyote yule hana uhusika wa moja kwa moja na maisha yake ya baadaye bali yeye mwenyewe.
Kuna kisa cha watawa wawili wa kanisa katoliki (baadhi yenyu mnakijua) waliokuwa wamechelewa kuvuka mto walipokuwa wakirudi konventini.
walipofika kwenye ufukwe wa mto wakakuta binti wa umri kama wa Maya alipobakwa akiwa ameshindwa kuvuka tokana na maji kuwa mengi! Walijadiliana jinsi ya kufanya na mmojawapo wa watawa hawa wa kiume akamwambia mwezie kuwa itakuwa vema kama watamsaidia binti huyuili avuke.
mwenzake alikataa kwa madai kuwa kama watawa 'hawaruhusiwi kumgusa mwanamke na hivyo itakuwa dhambi ya mauti kufanya hivyo'.
Mtawa huyu aliyetaka kumsaidia akajitolea akambeba mgongoni na kumvusha huku mwenzake akimlaumu 'kwa nini amembeba mwanamke kwani ni dhambi na wafikapo konventi itabidi wamuite padre apate kuungama!'.
Mtawa alimvusha binti na kumuacha hapo akiendelea na safari yake. Njiani mtawa huyu akawa analaumu mwenzake kwa dhambi aliyoifanya zaidi ya mara tatu.
wakati wakikaribia konventi alipomweleza mwenzie juu ya dhambi hiyo mwenzake akajibu kwa unyeyekevu kabisa: NDUGU YANGU, NIMEMBEBA YULE BINTI MGONGONI MWANGU NA KUMVUSHA NG'AMBO YA MTO. Nimemtua na mimi ni mwepesi bila mzigo wowote!
Sasa inaonekana kuwa wewe nndo mwenye dhambi na utapaswa kuungama kwa padre kwa kuwa UMEMBEBA KTK KICHWA CHAKO, AKILINI MWAKO NA MOYONI MWAKO. Tafadhali mshushe twendelee na safari"
Hilo ndilo linalotokea kwa Maya...mwambieni asitembee na babake....kwa kuwa tangu abakwe bado anaendelea kubakwa na babake kwa kuwa hajamtua moyoni, akilini, na kichwani kwake.
huo ni mzigo alojitwika...ana uhuru wa kuendelea kuubeba (kwa kisingizio cha wanaye watabakwa na baba yao-je kama atazaa wa kiume tupu yeye ndo atawabaka wanae?) ama kuutua aanze upya maisha yake na kutimiza malengo yake.
Ni hayo tu mkuu!
Ahsante sana Chacha kwa nasaha hii,natumai mhusika ataifikisha kwa huyo dada, kwani anasubiri kwa hamu maoni yenu ili naye apate nguvu na changamoto la kumtoa gizani, na haya uliyosema yanaweza yakamsaidia sana, kwani umeyahusisha na kisa katika vitabu anavyoviamini. Shukurani mkuu
Sometime unakuwa hujui la kufanya ama kumpa mtu ushauri mpaka mwenyewe upitie kile kile alichopitia na utapata "uelewa" zaidi lakini kuwa"label" wanaume wote kwamba wako sawa, namuombea tu kwa Mungu amsaidie na aondoe mawazo hayo japo ni tukio ambalo hatoweza kulisahau maishani mwake, kama binadamu unahitaji kuendelea ukisahau yote hayo.
Labda kama akiamua kufungua moyo wake akamkaribisha mwanaume mwenye upendo, inaweza kusaidia akasahau yote hayo ila at the end of the day, yeye ndio muamuzi wa maisha yake. I wish her loads of luck in life pia pole sana kwake
...by the way Chacha hiyo story nimeipenda kweli na ushauri wako ndio umeelezea vyema.
hebu nitafakari kwanza, kabla sijaongea kitu!!!
nimejaribu kufatilia kwa kina kisa cha ndugu/dada yetu huyu ambaye amekuwa na chuki kabisa na wanaume kwa kosa lililofanywa na baba yake mzazi.
kwa ushauri wangu(najua inauma)ila kama ameshamsamehe baba yake toka moyoni na kama anamwamini MUNGU kwa kila jambo basi ajue kuwa hata MUNGU amemsamehe babaye.si wanaume wote wako hivyo hivo atoe nafasi moyoni ya kupendwa akiamini kuwa yale ni majaribu tuu.pole sana dada.
Huyo dada anahitaji kufanyiwa counselling na wataalamu wa hiyo fani ili kuondoa jinamizi alilonalo kutokana na kuwa sexually abused. Mbaya zaidi mtu aliye mu-abuse ni mtu aliyempenda na kumuamini kwa hiyo inakuwa ngumu kwake kuwaamini wengine pia.
Na hizo lawaza haziko kwa baba yake tu, bali kwa mama yake mzazi subconciously kwa kutompa ulinzi, kwa shangazi kwa kushindwa kumsaidia. Na zaidi walipolifanya siri na kumbebesha huyu binti mzigo wa heshima ya familia wamezidi kumuumizakisaikolojia.
Ni rahisi kwa wengine kusema asahau lakini kisaikolojia si rahisi hivyo, na eti kusema watoto wa kiume hawawezi kubakwa na baba zao ni kujidanganya kwani hawa ndio victims wakubwa lakini kama kawaida inafanywa siri kubwa. Watoto wengi wa kike na kiume wanakuwa abused na watumishi wa ndani na ndugu wa karibu kwa sababu kila siku tunawaonya kuwaogopa strangers wakati watu tunaowaamini na wao wanaowaamini ndio wabaya zaidi.
Coming back to the girl,she need counselling, tena proper counselling kwa wataalamu wa mambo hayo ambako ataongea and she will go through the process of saikological healing, sio rahisi itamchukua muda na akipata bahati ya kupata mume ambaye ni understanding atamsaidia kwenye healing process.
Nina mengi ya kusema lakini ngoja niishie hapa kwanza, siku nyingine nikipita kijiweni hapa naweza kuongeza japo lingine!
Shukurani anyn. 29-1-2011 1:51 am. Na nawaombeni watu kama nyie kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yenu. Mkumbuke kuwa mtu kama huyu mapa imefika mahali pa kutoa kisa chake kwa jamii, imefikia mahala pabaya.
Kuna watu wenye taaluma hizi za counselling, kutoa mawazo nk, mnapoona visa kama hivii msichukulie kama hadithi...kuna watu jamani wanateseke...lakini tusemeje jamani. Tunajitahidi kutoa visa kama hivi..sio kujifurahisha tu...lakini wapo watu yamewakuta makubwa, na watu wa kuwasaidia ni sisi...
Ipo siku kama iikiwezekana, na kama itatokea miujiza watu kama hawa wafanikiwe kwasababu ya maoni yenu, tutawaweka `live' muwaone, na..tutashukuru sana. MUNGU AWALIPE NYOTE KWA WEMA WENU HUU. KIDOGO UKITOA/MAWAZO, NI KIKUBWA SANA KWA WENGINE, ...
mimi ningesema yalopita yamepita naomba amsamehe baba yake. hazidishe maombi Allah hatamsaidia
Post a Comment