Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, January 3, 2011
mwenye kovu usidhani kapoa-1
‘Dada sijui nikuambie nini ilivyotokea siku ile, jicho lilinitoka, pale nilipomuona baba YANGU MZAZI kavua nguo na kubakia uchi…sijawahi kumuona baba yangu au mtu mzima akiwa katika hali ile. Na sura ile huwa inanijia kichwani au ndoto zinanijia kinamna ya kutisha, huwa linakuja jitu kubwa kama shetani likiwa na maumbile kama hayo. Sikumini, baba yangu mzazi , sikuamini, na mpaka leo siamini kuwa kweli huyu ni baba yangu aliyenizaa mwenyewe.. ‘ Akatoa machozi na kuinama, halafu akaendeela kuongea huku analia
‘Dada mkanda ule ulianza pale wakati natoka mle chumbani baada ya kula zile chips alizonipa baba, nikaona nizibakize ili nizimalizie kesho yake, nilikula kwa haraka halafu nikjisikia kushiba, kwahiyo nikainuka haraka na kumwabia baba ahsante, nikaanza kutoka, mara nikashangaa, nimeshikwa begani kwa nyuma, nikadhani ni baba ananiondoa kitu begani, sijakaa sawa akaniziba mdomo…, mimi najua ni baba, kwahiyo hayo yote niliona kama ananifanyia mdhaha Fulani…’
‘Mara akanivua nguo khanga nilizokuwa nimejifunga, nikaanza kuingiwa na wasiwasi, sina kawaida kabisa ya baba kunivua nguo, kama nikitaka kuoga, au… tangu nilipojua kukaa uchi ni vibaya,hasa kwa wakubwa hasa wanaume, sijawahi tena kuvuliwa nguo na baba, au kumkalia uchi. Kwa umri niliokuwa nao nilikuwa binti, matiti yalishakuwa makubwa…na..akili za usichana zilishanikaa kichwani. Ingawaje mara nyingine baba anaweza kusaidia kunivalisha nguo, lakini sio nikiwa uchi kabisa. Leo nikashangaa kwanini baba ananivua nguo zote na kuniacha uchi. Hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi.
‘Nilivyomwangalia usoni, nilimuona kama kalewa vile, na alikuwa …sijui macho yake yalikuwa vipi, yalikuwa tofauti na baba ninayemjua mimi. Nikaanza kujinasua kwa baba, lakini alikuwa na minguvu, akanishika kwa nguvu na kunivuta ile khanga niliyokuwa nimeishikilia kujinga kwa mbele na baadaye akanivua chupi kwa kuichana, na kunitupia kitandani, …’
‘Baba vipi leo, kuna nini, mbona hivi unataka kunifanya nini…’ nikamuuliza huku najizuia uchi wangu na mikono, na wasiwasi ulishaniingia, kwani siye kabisa baba yule ninayemjua. Akaonyesha kidole mdomoni kuwa nifunge mdomo wangu. Kabla sijakurupuka pale kitandani nikimbie, akanidaka na kunirudisha kitandani. Nikaona sasa baba ana nia mbaya, nikaanza kupigana kufa na kupona , lakini ilikuwa kama katoto kanampapasa baba yake. Akanishika vimkono vyanguu na kuniminya kitandani.
‘Baba jamani unanimiza, baba unataka kunifanya nini, nitasema kwa mama…baba..babaaaaa‘ Nililia kwa nguvu na kupiga kelele, kwani niliskia kama kisu kikipenya sehemu zangu za siri, na kikawa kina nikata kwa kurudia rudia. Nilihisi maumivu ambayo sijawahi kusikia. Nililia na sauti ikaisha nikazimia. Nilipozindukana, nilimkuta baba kainama kashikilia kichwa. Hakutaka kabisa kuniangalia machoni…
Niliinuka haraka nikaokota zile chips alizokuwa kaniletea, ambazo zilikuwa zimebakia nikampiga nazo usoni, halafu nikamtemea mate na kumwambia.
‘Wewe sio baba yangu tena, na mungu atakulaani kwa tendo ulilonifanyia…’ nikatoka Mbio, nikakimbilia nyumbani kwa shangazi, sio mbali sana na hapo. Nikamuelezea shangazi yangu ilivyotokea, na kabla sijamaliza nikazimia, nilipozindukana nilikuta keshanisafisha damu na kunipaka dawa, na maumivu yalikuwa yameisha.…!
Dada mimi tangu siku ile nimeapa kuwa sitaolewa, kwani nimeona wanaume wote kwangu ni wanyama, na kwanini niolewe kuna raha gani…’ akasema mdogo wangu huyu. Nilimwangalia kwa Huruma sana kwani nakumbuka kisa hiki kilivyotokea miaka kadhaa iliyopita, hutaamini hili nitakalokuhadithia, ila ni kweli tupu, kwani huyu aliyefanyiwa hivi ni mdogoo wangu, kwa baba mdogo.
Nilimuangalia mdogo wangu huyu ambaye sasa ni dada mkubwa na alistahili sasa awe na watoto, lakini hutaamini kuwa kashikilia msimamo wake huo, hadi leo. Ni msimamo ambao wengi wamefikia kumona labda ana mataizo ya kimaumbile, lakini kwa vile mimi najua nini kilitokea na imekuwa siri yetu kama alivyotuapisha shangazi kuwa iwe siri, na akisema mtu atajuta.
Mdogo wangu huyu baada ya tukio aliamua kuhama kabisa hapa mjini na kwenda kuishii kijijini. Na huko akaamua kujishughulisha na mambo yake. Shangazi yatu huyu alijua kuwa kabakwa, na kaka yake, lakinii undani wa nini kilitokea hakuweza kunihadithia, mimi nilikuja kuhadithia na mdogo wangu mwenyewe jinsi gani ilitokea na baada ya kupata kisa hicho, nikakata mguu wangu kabisa kwenda kwa baba yangu huyu mdogo, ingawaje alikuwa baba yake niliyempenda sana kama nitakavyowahadithia kwenye kisa hiki cha `mwenye kovu uisdhani kapoa, …
‘Siku ile nilikuwa kama nimepagawa, na nina uhakika kama ningerudi tena kwa baba nikapata kisu ningemchoma na kumuulia mbali. Hata nilivyomuhadithia shangazi baadaye niligundua kuwa nimefanya makosa kwani ilikuwa kama kesi ya tumbili kumpelekea nyani. ..’ Alipofika hapo, alinitizama na kuanza kutoa machozi. Nilifurahia hilo tendo, kwani mtu aliyevumilia machungu akilia , hupunguza uchungu, na alilia kwa muda na baadaye akaniangalia, akatabasamu na kuanza kunihadithia ilivyotokea.
Kisa hiki ni ushahidi wa moja kwa moja wa mtu aliyetendewa tendo hili. Huenda usiamini, wewe unayesikiliza au kukisoma hiki kisa unaweza ukasema haiwezekani, baba amfanyie mtoto wake mwenyewe tendo kama hilo, haiwezekani. Lakini ilitokea, na baya zaidi wanandugu wakalimaliza kiundugu na mpaka leo baba huyu yupo na mdogo wangu huyu yupo lakini mdogo wangu huyu hajakanyaga kwa baba yake huyu tangu alipokimbia siku ile. Na amesema yeye hana baba, huyo sio baba yake. Lakini ........
Lakini, ...hebu tuona kisa hiki na hii lakini ina maana gani, kisa hiki kifupi ambacho tutakiita `mwenye kovu usidhani kapoa’
Ni mimi: emu-three
11 comments :
Heri ya mwaka mpya kwako...naona tumerudi tena..leta mambo..
Mambo hayo Elisa, nimeona tushituane na hicho kisa cha mdau, ..Natuma mwaka uliumaliza salama na sasa upo shwari kufuatilia visa vyetu, karibu sana tuwe pamoja.
Hivi hujafanikiwa kujisajili hapo pembeni kama MPENZI WA BLOG?
hapana sijafanikiwa ..hebu niambie nifanyeje ?
Mwaka tulimaliza salama kabisa. Mungu ni mwema.
mhu baada ya kisa mkasa, acha tuendelee tuone mwisho!!!
Mmmmmmmmmmm!Jamani sijui mama alikuwa wapi maskini weeeeeeeee!
Ni hatari sanaaaa!!!!!!!!!
BN
oooooh...unajua nilivyoanza kusoma nilidhani ni kisa cha kutunga kumbe kimetokea kweli. Matukio haya yanasikitisha kwa kweli yaani kupita maelezo. Nipo mpaka mwisho kama kawaida M3 and welcome back
Elisa Ni rahisi tu, wewe hapo pembeni kuna sehemu imeandikwa `FOLLOW' UNAPOBOFYA, NA UKIBOFYA UNAFUATA MAELEKEZO.
Kuna boksi litatokea linasema `usign in kwa kutumia e-mail yako wewe kama e-mail yako ni ya Google, bofya Google, na itatokea sehemu ya kuingiza e-mail yako na password, ukimaliza hapo utakuwa umejisajili, sidhani kama kuna zaidi
Candy hili tukio ni la kweli, na ningefurahi watu wangeta maoni na kumfaraji huyu dada, kwani bado `kovu' la moyoni linamsakama, tumuombee mungu asahau hayo machungu, kwani yeye mwenyewe keshasamehe! Soma sehemu ya pili utapata maeelzo zaidi
Mimi naamini ni tukio la kweli na kama ulivyosema inabidi tuache kuiga ni jinsi gani mabinti zetu wanavaa. mmmhh ngonja niendelee kusoma tuone mwisho wake na hapo ndo nitasema zaidi...mweeeh!
Inasikitisha na kuhuzunisha. Kwa vile ushahidi ndiyo hivyo ulishatoweka sidhani kama kuna la kufanya tena. Huyo baba alistahili kifungo cha maisha jela.
Hatari
Post a Comment