Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, December 2, 2010
Kusalimiana na kutembeleana ni baraka njema
Katika mila na desturi zetu za kiafrika, swala la kutembeleana na kujuana hali ni muhimu sana. Na hutaamini, watu na shida zao, umasikini wao na njaa zao utawakuta hawapitizi siku bila kwenda kuwasalimia wenzao, na ngalau wakae kidogo kubadilishana mawazo!.
Jana nilikutana na jamaa yangu, yeye kabahatika kumuoa Mrangi, wakati yeye anatoka kanda ya ziwa , na bahati nzuri kaishii ughaibuni. Sasa kakutana na mila ambazo kwake anasema imekuwa `mtihani’
`Bwana ukifika kwa wakwe zangu, inabidi usahau muda, kwani mmmh…’ akacheka kidogo .
`Kama imetokea bahati mbaya umewakuta wakwe au jamaa za wakwe wapo kumi, unakibarua pevu. Manake taratibu zao, inabidi usalimie mmoja baada ya mwingine. Hutakiwi utoe salamu za ujumla, kama kule kwetu, tunaojifanya wazungu.
‘Jamani habari zenu hapa..’
‘Huko kwa wakwe zangu urangini, haipo hiyo. Utakaa, utaongea, kwa unyenyekevu, halafu unaanza kumsalimia mmoja, mmoja, na kusalimia huko sio hujambo, mmmmh, hapana mtaulizana habari zote, ukimaliza mmoja unamgeukia mwingine mmmmh,
`Jaribu kufikiria watu kumi wote uwasalimie mmoja, mmoja, kila mmoja uchukue wastani wa dakika tano…utaondoka saa ngapi. Na mara nyingi salamu inatakiwa ije baada ya kula!...’ akaguna na kutazama saa.
Bwana mimi nitawachunia kuwatembelea, manake hakuna kitu ninachokijali kama muda..’ akaangalia saa yake tena, ‘ Na sasa hivi nina miadi na jamaa yangu mmoja, kuna dili nafuatilia. Akainuka, na kuaga kuondoka. Jamaa yangu huyu licha ya kujali muda, lakinii angalau anajaribu kuwatembelea wenzake na kuwajua hali, lakini wapo majirani wengine, hata sura sasa nimewasahau,…
Alipoondoka niliwaza sana, nikatafakari , kuhusu `muda’ unaodaiwa na watu wengi, kuwa `hawana muda’ hivi kweli huo muda tunaujali kihivyo. Mbona unakata dakika 90 kuangalia mechi za mpira, mbona unakata saa nzima kwenye baa kunywa, mbona…lakini kusalimiwa jirani yako unadai huna muda!
‘Ok, labda unaogopa watu wengine na taratibu zao kama huyo mwenzetu aliyeona kabila hilo, lakini Je kusalimiana tu kunachukua muda wote huo.
Kwa maoni yangu hata salamu ya ujumla, ya `hamjambo hapo, halafu ukaishia inatosha kuliko kutokusalimiana kabisa. Kwani mimi nioanavyo hii ndio moja ya mila zetu, na mila hizi ndizo zinazojenga udugu. Utakuwata mtu hamtembelei jirani yake, yeye akitoka kazini ndani ya nyumba yake ambayo imezungushiwa geti, ukitaka kumuona mpaka uwe na miadi naye, vinginevyo utasimama getini upige kengele mpaka uchoke…haya yametoka wapi, ndio uzungu huo!
Ni kweli muda ni muhimu, muda ni thamani, ukiupoteza hauji tena, lakini pia tuthamini udugu, tuthamini utu wetu, tujuane hali, kwani kuna leo na kesho. Utajifungia ndani ye geti lako, mara moto huo, mara tatizo hilo, mara hiki kimetokea, na unahitaji msaada, je watu watavunja geti lako? Na geti lenyewe limetegewa umeme…hayo ni maenedeleo sikatai, lakini mara moja kwa wiki nenda kawaone jirani zako wajue hali, angalau weka nusu saa ya kuwatembelea jirani zako, kwa wiki inatosha.
Wakati jamaa yangu ananipa nasaha hizi, nikakumbuka jirani zangu akina: Adeladally Kavishe-Adela, Allen Sean Phillip , BongoCelebrity , Candy1's Little World , Chachandu Daily-Bashir , Chakula Kitamu na Kichungu-Matondo, Changamoto Yetu-Mubelwa , Dina Marios , Dira yangu-Fungua jicho-Innocent, Foward Ever Backward never-Malkiory , Hadubini my 0-scope-Chib, Haki-Hakingowi , Hapa Kwetu-Mbele , Health & ShowBiz news -Abdallah Mrisho, Karibuni Nyasa-Markus Mpangala , Karibuni Nyumbani-Nicky Mwangoka , Kijijini kwetu-Chacha o'Wambura , Kijiweni, Nyegezi-Kamalaluta, Kisima cha Fikira-RSM Bona bana , Libeneke La Globu ya Jamii-Michuzi, lukwangule entertainment-Msimbe , Maggid mjengwa , Maisha na Mafanikio-Yasinta , Mamapipiro-Dina Ismail , Mawazoni- Mt.Simon Kitururu , Mitiki-Kilimo kwanza-Bennet, mumyhery collections-Mumyhery , Mwananchi Mimi-Fadhy Mtanga , Mzee wa Matukio Daima-Francis Godwin , Mzee wa Mshitu-Yahaya Charahani , Najua Wajua-Seif Salum Nyahbingi Worriors , Dinahicious, Sophie's Club-Sophie ,Strive for Life-Edna , SwahiliTime-Chemi C.Mponda , Tegelezeni-MaisaraWastara , Tustaarabike-Je huu ni uungwana-Mrope, Umoja ni Nguvu-Muungwana , Upepo Mwanana-tembemwana , Utambuzi na Kujitambua-Kaluse , Wanamuziki wa Tanzania-Kitime , Wavuti , na wale anynonimous, akina Jane, Pamela, Elisa, BN, nk.
Hawa jirani zangu, najaribu kupiga hodi kila siku kwenye nyumba zao, na wengine nawakuta wapo, tunapeana habari za hapa na pale, lakini wengine siwakuti, na nimeshangaa, wengine karibu mwezi na zaidi siwakuti nyumba kwao, nyumba imefungwa, hawa watu wapo wapi?
Lakini kuna wengine wapo, lakini ndio wale wa geti kali, nyumba zao ukitaka kufika lazima uwe na miadi nao, ndio ni mataifa makubwa,lakini hata iweje, utaifa kubwa wako, hauzidi utu na ubinadamu, hauzidi uafrika na jadi zetu za kutembeleana. Ikiwa mwenzako kila siku au mara moja kwa wiki anakuja kwako, wewe umenata nyumbani kwako kwa kisingizio kuwa `upo busy’ manake nini, manake ni kuwa hutaki kutembelewa, wenzako wanajipendekeza kwako.
Sio vizuri jamani, tutembeleaneni, hata kama kwetu ni vibanda vya nyasi, lakini ni nyumba, na waishio humo ni binadamu, ukiwaona ukawasalimia utapata Baraka kwa mungu baba. Kwani kusalimiana na kutembeleana ni baraka!
Wakati mwaka unaishia jaribu kufanya tathimini ya jirani zako uliowatembelea, na waliokutembelea na linganisha, kama waliokutembelea ni wengi zaidi ya uliowatembelea basi una kasoro, una ubinafsi….
Ni hayo tu, ni wazo la wiki majirani zangu!
Ni mimi: emu-three
10 comments :
Ujumbe umefika, manake we kila siku kwa mwenzako, habari gani hujambo, kila siku kwake, yeye haji kwako manake nini...hataki uje kwake! Mchoyo huyo!...wala sio uzungu, ni uchoyo na roho mbaya, hata kam akuna geti, wangapi mageti yapo bado tunasalimiana!
Ujumbe umepokelewa. Binafsi napenda nikupongeze kwa ushiriakiano na michango yako ya dhati kwa wadau wengine. Ubarikiwe.
Habari ndo hiyo imesomeke hata kama ni kimya kimya. Mwenzangu wanakwambia mtu wa kwanza kutoa msaada ni jirani yako kwa sababu yuko karibu, sasa wewe ukiwa matawi jirani yako atakuwa nani??????? Asante kwa ujumbe mzuri M3 umefika kwa wengi maana najua kila aliyepita hapa ameupata.
Hakika umenena kwani kuna wati wanajali sana muda na pengine hata sio muda. Ni kweli sisi waafrika hatujali muda utakuta mtu anakwenda sehemu na mara anakutana na jamaa basi wanakaa na kupiga gumzo. Pia hii inatokana na mazingira mtu aliyokulia kwa kweli . Haya nami napenda kukupongeza kwa ushirikiano /utembeleaji wako bila kuchoka Maisha na Mafanikio. Ahsante:-)
Bonge la ujumbe Mkuu!
Mie nashukuru sana kwa wewe kutoacha kunitembelea. Nami hapa napita sana hata kama siku nyingine ni kimya kimya. Kuna sehemu sina cha kusema cha zaidi nikawa naguna tu ``Mmmmmh!´´ ikachukuliwa vibaya ingawa nia yangu ili kuwa nikusabahi kuwa jirani nimepita!
Tuko pamoja!
Lakini kwani jirani HATA KAMA YEYE anajiona BABU KUBWA kuliko wengine - asiyetaka kutembelea wengine ni lazima abembelezwe?
Yaani hapo umeongea kweli. Mimi huwa najaribu kila siku lakini sio blog zote ninazozijua ila najaribu kutembelea kila siku na hapa pia sikosi, najua pia sio kila siku nina jambo la kusema ila naona kwamba nimeongeza namba kwenye kaunta na pia nimejifunza kile kilichoandikwa. Wapo ambao sijui tuseme wako busy ama muda ila ndio hivyo, unaendelea kuonyesha support. Umesema kweli na shukrani nyingi saaaaaaana kwa mchango wako unaoonyesha kwenye kijiji changu..wazungu wanasema "I can't thank you enough" ila ninachoweza kufanya ni kuja kijijini kwako pia...naishia hapa
"Lakini kwani jirani HATA KAMA YEYE anajiona BABU KUBWA kuliko wengine - asiyetaka kutembelea wengine ni lazima abembelezwe?"
Mkuu nakumbuka kuna usemi wa maandiko, utanisahihisha kama nitakosea, unasema `mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe..'
Hii ina maana kuwa kile unchokipenda wewe, basi mfanyie na jirani yako vivo hivyo, au sio.(najua hapa wengine wataguna, jirani yangu anapenda tungi, ina maana na mimi pia...). Labda mkuu ututafsirie vyema huu usemi!
Ina maana pia ukiona jirani yako anakwenda sivyo ndivyo, mshike mkono umuonyeshe njia, vinginevyo atapotea, na huenda kupotea huko kukasababisha na wewe kuingia matatani!
Ni kweli, `muda' ni muhimu, wengine wakikutembelea, kama akina sisi tutakaa, mpaka mmmmh(utaandika maneno mengi) ! Lakini mvumilie ndio ujirani mwema!
Nawashukuruni sana majirani zangu, nia ya hoja hii ni kupeana mawaidha, au mahubiri mema, huenda nikawa nimekosea, lakini ndio misingi ya blog nyingi, kutoa hoja uonavyo inafaa, na wengine wakasoma, wakachangia, wakaguna, wakapitia, na kama inafaa watafaidika wenye kufaidika, kama haifai, unaweka kama kumbukumbu!
Karibuni sana, mimi ni jirani yenu tu!
Nanukuu ``Mkuu nakumbuka kuna usemi wa maandiko, utanisahihisha kama nitakosea, unasema `mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe....Hii ina maana kuwa kile unchokipenda wewe, basi mfanyie na jirani yako vivo hivyo, au sio....''
Mimi naamini kumpenda jirani yako kama ujipendavyo wewe sio lazima iwe umfanyie umpendaye upendavyo ufanyiwe kwa kuwa kuna watu vijulikanavyo kabisa ni VIBAYA ndivyo wavipendavyo kwa hiyo kama wanapenda wengine wajulikanao kutokupenda hayo labda sio busara kuwafanyia.
Ni kama vile MZAZI anaweza kuwa anafanya ajuavyo kabisa havimfai mtoto kwa hiyo itakuwa si HEKIMA kumfanyia mtoto ambavyo vyajulikana kuweza umiza mtoto.
Au kwamfano mimi binafsi si siri kama unanitembelea kwangu utastukia kuwa ni mtu wa KILEVi na haki ya nani najua madhara yake ingawa bado sijaamua kuacha na kwakuwa najua MADHARA yake siwezi kumfanya nimpendaye ambaye hahusudu pombe anywe pombe ,...
...ingawa huwa si zinguki kivile kwa wavutao aina zozote za moshi kuanzia SIGARA , bangi mpaka majani ya mpapai wanao jaribu kutaka nivute nao NIKISTUKIA ni kwa upendo WAO KWANGU ndio maana wananikarimu kabla hawajastukia MIE sio mwanachama kivile katika uvutaji chochote!
Nanukuu``Ina maana pia ukiona jirani yako anakwenda sivyo ndivyo, mshike mkono umuonyeshe njia, vinginevyo atapotea, na huenda kupotea huko kukasababisha na wewe kuingia matatani!....´´
-hapa napo ni pagumu kinamna kwa kuwa unaweza kukuta tukichukulia mfano mambo ya IMANI unaweza kukuta unaweza kukuta kila jirani yako kwa mtazamo wa imani yako unaweza kuamini kapotea kwakuwa hafuati DINI yako, dhehebu lako,....nk. Cha ajabu na wao kwa imani yao wanaona wewe ndio uliyepotea na wao wakijaribu kwa kila njia kukuokoa kwa kujaribu kukushika mkono usiendelee kupotea. Na katika hilo mnaweza kujikuta mnapoteza mpaka ujirani mwema kisa KUNA MAMBO na amini aliyepotea mwenye kuridhika na aendako labda si kila mara ni sahihi kufikiria kuwa afanyayo ni UJINGA na kupotea kwa kuwa mwisho wa malumbano mnaweza kujikuta hata mbele za muumba wenu kutokana na malumbano yenu ya kuvutana mikono kuonyeshana njia wote ndio mmezidi kupotea uchochoro wa aliko MUUMBA.
Nanukuu:``.....nia ya hoja hii ni kupeana mawaidha, au mahubiri mema, huenda nikawa nimekosea,....´´
Kwa mtazamo wangu hujakosea KABISAAAA MKUU!
Pamoja sana MKUU!
Nanukuu: ``Mkuu nakumbuka kuna usemi wa maandiko, utanisahihisha kama nitakosea, unasema `mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe..Hii ina maana kuwa kile unchokipenda wewe, basi mfanyie na jirani yako vivo hivyo, au sio.(najua hapa wengine wataguna, jirani yangu anapenda tungi, ina maana na mimi pia...). Labda mkuu ututafsirie vyema huu usemi!''
-Mimi naamini kile unachokipenda sio lazima umfanyie umpendaye jirani yako kwa kuwa kunatuvipendavyo ambavyo twajua madhara yake kwa hiyo haitakuwa ni upendo kumfanyia mwenzio.Ni kama tu MZAZI ampendaye mwanaye kwa ya kikubwa ayapendayo inaweza kuwa si hekima na upendo kumfanyia MTOTO.
Na mimi binafsi kama wengi wajuavyo ni mtu wa KILAJI na najua madhara yake kwa hiyo kama wewe sio mtu wa MTUNGI mie sikupi pombe kwa upendo kama jirani.
Tukumbuke kuna wajidhuruo wakijua madhara!:-(
Nanukuu:``Ina maana pia ukiona jirani yako anakwenda sivyo ndivyo, mshike mkono umuonyeshe njia, vinginevyo atapotea,..´´
-Hii nayo na wasiwasi nayo mara nyingine hasa nikichukulia mfano wa IMANI . Kwa imani unaweza kufikiria JIRANI yako kapotea kwa kuwa sio dini au tu dhehebu lako na yeye pia akifikiria ni wewe umepotea.Kwa kujaribu kumshika mkono umuonyeshe njia na yeye kukushika mkono kukuonyesha njia-mnaweza kukuta mnavutana mikono, mnavunja ujirani na mwisho hata MUUMBA mumgombaniaye naye anawaona wote mmepotea.:-(
Nukuu:``....nia ya hoja hii ni kupeana mawaidha, au mahubiri mema, huenda nikawa nimekosea,...´´
-mie sioni ulilokosea MKUU!
Pamoja SANA tu MTU wangu!
Mkuu unajua COMMENT ya kwanza niliambiwa -is too long -nikajaribu kufupisha !:-( Smamahani kwa kutuma mara mbili hoja zilezile!:-(
Post a Comment