Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, December 16, 2010

Au ndio mfumo dume...!

 
  Katika pita pita zangu kwenye vijiwe mbalimbali nimekuwa nikisoma maelezo yakusikitisha ambayo hufanyiwa wafanyakazi wa ndani, na mara nyingi ni wanawake wanaofanyiwa hivyo. Inasikitisha kwa kweli kwasababu huyu binti wa watu ni mnyonge ndio maana kaja kufanya kazi kwako, huyu binti wa watu ni mtumwa ndio maana anadiriki kufanya kazi ngumu kwa malipo kidogo tu, na bado anakuwa hana hiari ya mwili wake, ina maana wewe baba mwenye nyumba umamchukua nguvu zake, mwili wake na utu wake pia.


Mimi sikuishia kusikitika tu, na kulaumu, kwani wengi wetu twafanya hivyo, twasikitika halafu twalaumu. Nikajaribu kutafakari zaidi na kujiuliza , kwanini? Nimekuwa nikjaribu kuangalia maoni ya watu wengi, na watu wengi husema ni sababu ya `tamaa za kimwili za wanaume’. Nikajiuliza ina maana wanaume wana tamaa zaiidi ya wanawake, mbona sisikii wanaume wakilalamika kuwa wamebakwa. Kwa kuwaza hili nikaona nijaribu kuwadadisi wanaume waliowahi kufanya kazi za ndani, au hata kama sio za ndani lakini majumbani mwa watu.

‘Mimi siwezi kuita kubakwa, lakini nafikiri kama ingekuwa mwanamke amefanyiwa hivi nilivyofanyiwa mimi lazima ingeitwa hivyo, kuwa nimebakwa..’ huyu alikuwa jamaa mmoja aliyenihadithia kisa chake wakati anafanya kazi kwa wenzetu walijaliwa.

Anasema, yeye kajaliwa maumbile ya mwili mazuri, kwasababu licha ya kazi anazofanya za suluba,lakini anajitahidi kufanya mazoezi, ili kuuweka mwili wake katika hali nzuri. Na kutokana na maisha magumu, kabla hajapata nafasi hii aliyo nayo ya `urembo wa matangazo’ aliwahi kufanya kazi kwa tajiri mmoja. Na tajiri huyu alikuwa na miradi mingi na mara nyingu husafiri kwenda Kenya au Dubai kuchukua vifaa vyake.

Yeye katika hangaika hangaika yake akapata kazi hapo, ya kuhudumia bustani, na baadaye akawa anafanya kazi za ndani pale msichana wa kazi wa hapo anapokuwa hayupo.Anasema yeye ni mpishi mzuri, na usafi wa kupiga deki, kuosha vyombo kwake ni kazi ndogo sana, na anazifanya kitaalamu kwani anazipenda,

‘Ndio maana nilipopata kazi hii ya urembo na matangazo, nimefurahi sana, kwani napenda mapambo, kupamba, kujiweka mwili usafi, kuvaa vyema na mambo yanahusiana na hayo, kama kula vizuri…siunaniona mwenyewe nilivyo..’ akageuka huku na huko na kutunisha kifua. Kweli ana mwili ule wa kimazoezi haswa.

‘Basi niligundua kitu kimoja wakati nafanya kazi mle ndani, mama mwenye nyumba, alikuwa mara kwa mara akinitupia jicho,…mimi nilikuwa mgeni wa jii hili na nimelelewa kwenye nyumba za kumuogopa mungu, hali hii ilinikera, nikapanga kuwa kama mama huyu ataendelea kunitizama vile mawili, niache kazi au nimwambie baba mwenye nyumba.

Siku moja nikamuuliza yule msichana wa kazi za ndani kwamba kwanini mama huyu anapenda kunitizama kwa macho ya namna ile. Yule msichana alinicheka kweli na kuniita mshamba. Sikumuelewa kwa kweli , kwani yeye ni msichana na nilitegemea angelilaani lile, lakini akanipa maneno ya kunidharau, Sikumjali na nilishikililia msimamo wangu ule ule wa kutojiingiza katika vishawishi vyovyote, kwani niligundua hata huyo msichana alianza mambo nisiyoyataka ya kunitekenyatekenya, na siku moja nikamzaba kibao, lakini yeye aliishia kucheka na kuniita mshamba.

Siku moja huyo msichana akawa hayupo, na nikapata kazi za kusafisha ndani, nilipomaliza mama mwenye nyumba akaniambia nikadeki chumba chao wanacholala, nikafanya hivyo, akaniambia niondoe mashuka ya kitandani nikayafue, nikafanya hivyo, akaniambia niyapige pasi nikafanya hivyo, akaniambia nitandike mengine kitandani nikafanya hivyo, na wakati natandika kitandani, nimeinama kumbe huyu mama alikuja pale chumbani kimya kimya, akiwa na kanga moja, nilipogeuka tu….

Nilijitahidi sana kupambana naye na mwisho kwa vile nilikuwa na nguvu akaniachia na kunishangaa…

‘Wewe mwanume gani wewe…unataka kunionyesha nini…hutaki kazi sio, kwanza nitamwambia baba mwenye nyumba kuwa ulikuwa unataka kunibaka…wewe siunajiona mjanja sio…’ yule mama akainua simu kutaka kumpigia mume wake.

Nilikuwa nimetahayari, na sikujua huyu mama anataka nini kwangu, Ina maana mume wake hamtoshelezi au anataka kunjaribu kimapenzi. Nikasema hapana hapa kwangu haoni ndani. Nikamwomba asipige simu aache tu, tuongee, akaacha halafu akanisogelea. Nilimuomba sana kuwa mimi ni mtu wa dini hayo anayotaka mimi nifanye siwezi namwogopa mungu, akaanza kunishikashika…Nilipokataa akanizaba kibao cha nguvu. Sijawahi katika umri huu kipigwa kibao kile..iliniuma sana!

Hakuniachia akasema sasa atapiga simu polisi kuwa nilitaka kuiba, kwani kuna muda aliniona nikitizama kwenye kabati lake, lakini muda huo nilikuwa natafuta shuka linaloendana na kitanda chake, mimi sijawahi kuiba kwenye maisha yangu. Akasema wakati nafanya hivyo alikuwa kachukua picha na kweli akanionyesha simu yake inayochukua picha, kuwa kweli alinichukua bila mimi kumuona. Akaniambia yeye akiwaambia polisi watamuamini.

Nikasema heri nifungwe kuliko kujidhalilisha, nikatupa vitu vyake chini na kutaka kuondoka. Alinidaka na kukuru kakara zikaanza, sijui alinifanya nini, nilijikuta nimezidiwa, na baada ya hapo nililia sana. Mimi ni mtu wa imani ya dini, mpaka leo nikikumbuka najuta kwanini nilikuwa mdhaifu siku ile, kwasababu kwa nguvu asingenishinda, lakini pale alifanya kitu ambacho kilinilegeza, akafanya alilofanya basi…lakini mimi sijui kama naweza kusema kuwa nimebakwa, au…!

Alipoishia hapa, jamaa yake aliyekuwepo hapo alicheka sana, akamwita `mrembo mshamba’ akasema maneno ambayo sikuyaamini sana.

‘Hiyo kesi ungeileta kwetu, wenzako tunatafuta vitu kama hivyo hatupati, wewe …mshamba wa kutupwa, halafu eti unadai eti umebakwa, mwanaume habakwi…ukisikia mwanaume analalamika kabakwa huyo sio rijali..’

Hapo ndipo hoja yangu ilipo kuwa je ina maana wanume tu ndio wana tamaa za kimwili au kwasababu wanume hawalalamiki kuhusiana na maswal kama haya, ambayo wakati mwingine wanalazimishwa kufanya matendo hayo bila ridhaa yao, na wanogopa wakilalamika wataitwa sio marijali…hebu tulione hili swala kiundani zaidi. Ni kwanini hali kama hizi zinajitokeza hasa siku hizi? Kabla sijatoa maoni yangu nataka nisikia kutoka kwenu, na kama yupo mwanaume aliwahi kufanyiwa hivyo atoe ushahidi …au mnaogopa kuitwa `sio marijali”. Au ndio mfumo dume huo!

Ni mimi: emu-three

12 comments :

Anonymous said...

Mimi katika kuchangia hili, naweza kusema kuwa kubakwa kwa wanaume ni mara chache sana, kwani wanamue wenyewe `wanapenda hivyo', na swala la kutafuta upenyo tu, au kwa vile wanawaogopa mabosi wao ndio maana hawaweze kuwaamba kuwa wanatka wafanyiwe hivyo.
Nasema hivyo kwasababu kimaumbile, wanaume hawaumii. Lakini wanawake wanaumia na mawili, kimwili kwasababu maumbile ya kike yanhitaji matayarisho kabla ya hilo teno, pili wanaumia kiakili, kwasababu wanapofanyiwa hivyo thamani yao kwa mwili inakuwa kama inapungua, sio sawa kama wanaume!
Nini kifanyike, kama nilivyosoma hoja yako kwenye blog fulani la muhimu ni kuangalia utaratibu wa mume na mke `kuhakikisha, kama umtu wa safari hakikisha humuachi mwenzako na njaa, pili elezaneni ukweli kuwa chkula aina hiyo hakikushibishi, na mtafute jinsi ya kukiboresha chakula chenu. Kwasababu nyama zote ni sawa, tofauti ni majina ya mabucha tu!
Muogopeni mungu, na tunzeni ndoa zenu!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

"Ni kwanini hali kama hizi zinajitokeza hasa siku hizi?"

Mimi nadhani ni kutokana na upatikanaji wa habari kirahisi zaidi ndiyo maana tunasikia sana kuhusu habari hizi. Enzi zile za redio Tanzania na gazeti la Uhuru na Mzalendo habari hizi ungezisikia wapi? Lakini naamini kwamba mambo haya hata wakati ule yalikuwepo japo yalikuwa hayaripotiwi kama ilivyo sasa.

Unajua, umenifanya nifikiri jambo. Hata hapa Marekani wanaume wanaofanya mapenzi na watoto ambao hawajafikisha miaka miaka 18 hupewa adhabu kali zaidi kuliko wanawake wanaotenda kosa lile lile. Utakuta mwalimu wa kiume anafanya mapenzi na mwanafunzi wa kike wa miaka 15 anaishia kupigwa mvua 25 hadi maisha na mwalimu mwanamke anapofanya mapenzi na mwanafunzi wake wa kiume mwenye miaka 15 basi ataishia kufungwa miaka mitatu au kupewa kifungo cha nje. Hata katika ubakaji hali ni ile ile - wanaume ndiyo hula mzigo zaidi. Nadhani mdau hapo juu amegusia mambo ya msingi. Ngoja tuone wengine wanasemaje.

malkiory said...

Nadhani wanaume sisi tunaudhaifu wa kimaumbele (hormonal systems), kisaikolojia na huwa tunao udhaifu katika kutawala hisia zetu ukilinganisha na akina dada, sasa haya yanapokutana na mazingira ya wivishawishi toka kwa akina dada zetu hapo ndipo mambo yanapokwenda kombo. Lakini kwa yeyote anayebakwa awe mwanamke au mwanamume nadhani madhara ya kimwili na saikolojia hujitokeza kwasababu tendo lile linakuwa limefanyika bila ridhaa.

Simon Kitururu said...

Swala hili sio linajitokeza zaidi siku hizi- Jambo hili lilikuwepo tokea zamani sema tu siku hizi linaongelewa kwa uwazi zaidi na mahali pakuviongelea pameongezeka ukizingatia zamani hata magazeti ya udaku hayakuwepo.:-(


Wanaume hubakwa na kama ANONY alivyosema hapo juu -tofauti ni kwamba akibakwa mwanamke anaweza hata kupata mimba tukiachilia mambo mengine mengi zaidi kuliko MWANAUME.

Ingawa mwanaume pia akibakwa anaathirika KIASIKOLOJIA kama mwanamke tu hasa kama huyu ambaye kwa tendo hilo anajisikia kachafuliwa na pia kamkosea MUNGU wake.

Kuna demu aliwahikutaka kunibaka ila nilivyostukia nikamshauri ngojea nimsaidie tu tusijechaniana nguo bure wakati mchezo wenyewe na shamrashamra zake zilishanitia munkari kimurua tu.:-(

Ngojea niende kutubu!:-(

emuthree said...

Kwa kulinganisha `sasa' na `zamani' matendo haya kwangu naona ymezidi kwasababu kuna chachizo nyingi zimekuwepo hasa huu `utandawazi' na `mazingira tunayoishi sasa'
Wkati tupo kwenye daladala, alikuwa kakaa msichana mbele yetu, na suruali aliyovaa ya kubana, nyuma ilikuwa kama wanaume wanaovaa `kata nini sijiu' lakini yeye ilizidi kwani hata chupi aliyovaa ni zile zinazositiri sehemu ndogo sana, na kwa ujumla nyuma huku alikuwa `uchi' na hata alipoinuka hakujali kuifunika, na kwa vile magari yetu ni `mfumo wa mbilikimo, ilibidi ainame huku anatoka,...walioanza kumshambulia yule dada ni wanawake wenzake...
'Hivi wewe msichana umefundwa, kweli, hivi wewe mwanamke una wazimu..hivi....' walimshambulia kila mtu na lake.
Yeye akajibu, `kila mtu na hamsini zake, yeye ana uhuru wa kuvaa anavyopenda, kama wamewashwa wkanywe maji...' akatoka, na huku anachezesha makalio yake!
Hii nataka kukuonyesha kuwa `siku hizi' kuna kuzarau maadili, kuna kuiga kusikofaa, kuna picha, video magazeti yanayochochea hamasa, na kwahiyo madhara yake ni kuibuka kwa wale waliokuwa wanajificha makucha yao na kuionyesha hadharani!
Lakini kingine kikubwa, ni kuwa wananyumba hawajaliani `kindoa' licha ya kuwa sasa yapo madarasa ya kila aina ambayo `zamani' hayakuwepo, kama watu wangesoma, wangejifunza mengi na ndoa zingekuwa sehemu ya furaha, ...ni hayo kwa sasa, karibu tuchangie mada hii muhimu!

Anonymous said...

Swala kubwa hapa ni lipi, kuwa siku hizi mambo haya yamezidi au ni kwanini mambo haya yapo, au tamaa hizi zinasababishwa na nini?
Mimi kwa kuchangia naweza kusema kuwa `imani za dini hazipo, imani za kumfanya mtu aogope kuwa hili ni baya hazipo na kama zipo ni mdomoni tu. Na hii inachangia pia na serikali kutokuweka sheria za kuwabana watu kama hawa `wabakaji' mfano kesi moja ilitokea jamaa kambaka mtoto wa miaka sita, kesi hiyo ilichukua muda sana, sijui walikuwa wakitafuta ushahidi gani, wakti jamaa huyo alipatikana `live' na mtoto aliharibika sehemu zake za siri...!
Toeni adhabu kali, na wanandoa `msibaniane' toshelezaneni. Mimi nina imani kuwa `tendo la ndoa likifanyika kivyema, mtu mzima unaweza ukakaa wiki bila kutamani.
Samahani kama nitakuwa nimetumia lugha isiyofaa, lakini huo ndio ukweli.
Nimefurahishwa na kijiwe chako M3, NITAKUWA NAKUTEMBELEA.

CALL ME 'DIVA' said...

Haya mambo ya wanawake kulazimisha ngono kwa wajakazi au wafanyakazi wao ilianza toka zamani , hata kwenye biblia kuna hadithi ya Joseph na mke wa bosi wake, alimlazimisha mapenzi alipokataa akamsingizia kutaka kumbaka na ikapelekea Joseph kufungwa jela. Hili suala linachochewa zaidi na wakinadada kuolewa na wanaume wasio na mapenzi nao wala kuwatosheleza kimapenzi ila tu wanaamua kuolewa kwa sababu ya pesa na mali alizonazo mwanaume huyo. Sasa unakuta mwanamke anatokea kujawa na hamasa na hamu za kimapenzi na anakosa mtu wa kumtimizia haja zake na kupelekea kulazimisha mapenzi na mwanaume aliye chini, wakati mwingine anaweza kuwa mfanyakazi wake au hata ndugu wa mume. Mwisho wa siku anayeumizwa ni huyo huyo kijana. Jamani wanawake wenzangu, hata wanaume, suala la kufunga ndoa na mtu ni kiapo cha maisha. Tuwe makini sana na kile tunachofuata ndani ya ndoa, nacho kikubwa kiwe ni MAPENZI. Hakuna utumwa au ufungwa mbaya hapa duniani kawa wa MAPENZI

emuthree said...

Nashukuru sana Diva kwa kutukumbusha kisa hicho katika vitabu vya maandiko matakatifu, kama sikosei kwenye kitabu kingine huyo kijana aliyetakwa na mke wa huyo bwana mkubwa anaitwa Yusuph!

Mbele said...

Shukrani emu-three kwa kuleta kisa hiki, ambacho ni changamoto na mtihani mkubwa. Nawashukuru wachangiaji waliotangulia. Kwa namna ya pekee namshukuru Diva kwa kutuingiza katika masuala ya ndani zaidi ya nafsi.

Sasa tukizingatia kuwa huenda huyu mama alikuwa akiumia na kuteseka kwa sababu labda ya mume wake kutokuwepo, au kutojali, na pia labda kwa sababu ya kibinadamu ya kuvutiwa na huyu kijana, inakuwa vigumu kumlaumu huyu mama, maana hatuna uwezo wa kumlaumu wakati sisi wenyewe tungeshindwa mtihani wa aina hiyo. Mwenye haki ya kutoa hukumu ni Mungu.

Nikiongezea hapo hapo, naona kuna mtihani mkubwa kwa msingi wa dini. Dini inatufundisha kuwasaidia wenye shida, wanaoteseka.

Iwapo huyu mama angeanguka kwenye ngazi na kuhitaji msaada, tunategemea huyu kijana amsaidie, na hata kumbeba hadi kumpeleka kitandani akapumzike, kumpikia uji na kumkandakanda vizuri. Ninaamini dini inaruhusu hayo.

Sasa inakuwaje kwamba mama alipoumwa na tatizo la hii ninihino, kijana huyu anasema yeye ni mtu wa dini, hawezi kutoa huduma hiyo?

Yaani hata kama huyu mama ataanza kuchanganyikiwa sababu ya tatizo la ninihino, ni sahihi aachwe achanganyikiwe hadi aokote makopo? Najua tunasema kuwa dini inataka hivyo. Lakini tujiulize: hii ni dini kweli au ukatili?

Hebu tutafakari: njaa ni maumbile, na tunapaswa kuwapa chakula wenye njaa. Njaa ya ninihino nayo ni maumbile. Inakuwaje marufuku kutoa msaada unaohitajika?

Na iwapo huyu kijana angeamua kutoa huduma ya ninihino, akajieleza mbele ya Mungu kwamba alikuwa anamsaidia binadamu katika shida, tunadhani Mungu atamwadhibu kijana huyu? Mimi sijui. Mwenye hukumu ni Mungu.

Nikiendelea na hii tafakari, naona nitachanganyikiwa kabisa :-)

emuthree said...

Nashukuru sana Mdau na jirani mwema Mbele kwa kutoa hoja yenye changamoto, na kutuweka katika kuwaza, hivi kweli ukiwa na njaa, au ukiwa unaumwa, unaomba msaada unapewa!
Mama wa watu hatujui anaachwa `hivyo hivyo' kwa muda gani, ujue hawa watu wanaofanya kazi za masafwa wana `nyumba ndogo' kwahiyo wakija nyumbani na kukuta `wali ule ule wa kila siku' mmmh, anasema nimechoka sana mke wangu, kazi nyingi, safari nk, mama watoto anashukuru...
Sasa kaona biriani...kila siku inapita karibu na mdomo wake, uzalendo umemshinda...kaipupia, na hii ingekuwa upande wa pili, ingeitwa KUBAKWA...AU nimekosea, lakini kwa kijana wa kiume, mmmmh!
Swali ni kwanini, na ifanyikeje, ili hali hii itulie.
Maibu wanayo wanandoa, lakini wanabania kuelezea. Haya nashukuruni. Endeleeni kutoa mawazo, nami naweka sehemu inayofuata ya kisa chetu! Nilishindwa kuiweka Ijumaa kwasababu ya mtandao. Samahinini sana!

Anonymous said...

kweli miram3..hayo maneno yapo na hayatakwisha ...kazi iko ....

Anonymous said...

Many people find it hard to believe that cat discipline is
possibl. ' in 1997 followed in 1999 by the group's major-label debut Guerrilla Warfare, which reached No.
As a result, some parents are continuing to protest and
ethically ban hip-hop as nothing more than "music with an attitude.

Feel free to visit my weblog: 2013 new rap songs