Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, December 16, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-12


Nilikuta nyumba ipo shanghala baghala, na sikumbuki hawa watu kuingia ndani, vyombo, vimedondoka vingine vimevunjikavunjika, baadhi ya viti vimevunjika, na madamu yametapakaa kila kona…palikuwa panatoa harufu ya ajabu ajabu, ikawa inanitia kichefuchefu na nikawa naona kizunguzungu, Nikachukua vidonge vyangu vya kupambana na hii hali lakini kabla sijavitia mdomoni, nilisijisikia kama nainuliwa juu kwa juu nikapoteza fahamu….

                                          
                                                       ****************
******Docta kapoteza fahamu, na mganga hajigangi, je ni kwanini ? Lakini kabla hatujajua hilo hebu tuanze upande mwingine wa akina dada hawa wawili, kuna nini kinaendelea...karibu sana********
                
                                               *********           **********
                                                                ********
Maua alishangaa jinsi mwenzake alivyombadilikia ghafla, kwani kila akimuuliza kitu, Rose anamjibu kwa hasira au ananyamaza kimya, hii sio kawaida yake, mwishowe akaona asikae kimya amuulizie mwenzake kuna nini baya kamfanyia. Hakupata jibu moa kwa moja, Rose alibenua mdomo akajifanya hakusikia hilo swali, na alipoulizwa tena akaibu kwa hasira.

‘Sijakuambia umenikosea kitu, ila sijisikii kuongea na mtu yoyote leo, naona mambo yangu hayaniendei vizuri, kila …. Lakini kwani wao ni nani, usijali ndugu yangu kichwa changu kilikuwa hakijakaa sawa, ila naona nikiwa na wewe utakuwa kikwazo kwangu…’ akasema nakuinuka.

‘Nitakuwa kikwazo kwako, kwa lipi, mbona unaniacha hewani…’ akamfuatilia nyuma, hadi walipofika nje kwenye mti wenye kivuli, wakakaa. Wakati anamfuatilia alijaribu kukumbuka kuwa kuna lolote alilomfanyia Rose, ambalo hakulipenda, lakini hakuliona lolote baya. Akasema leo mimi na yeye mpaka aniambie nimemkosea nini. Rose akakaa chini huku kakunja sura.

‘Mbona hunielewe wewe bibiye, nimekuambia siataki kuongea na mtu leo, hau niongee Kiengereza au lugha ya kwenu…’ akataka kuinuka aondoke ,lakini akafikiria na kuona anafanya vibaya, akarudi akakaa, na kuanza kuchokonoa chini na kijiti.

`Sikiliza Maua, unakumbuka siku niliyokuambia unisindikize kwa yule dakitari Kibonge wa hapo jirani, unakumbuka kulitokea nini…?’ akamwangalia Maua huku kaminya icho moja. Maua akajaribu kukumbuka kulitokea nini siku ile kwani yeye hakuchukulia manani jambo lililotokea siku ile, ila akajaribu kukumbuka ilikuwaje.

Siku ile waliondoka nyumbani baada ya Rose kumuombea ruhusa kwa dada yake kuwa anaomba Maua amsindikize kwa Dakitari kwani alipewa kazi za nyumbani ambazo akimuulizia dakitari ataweza kuzifanya vyema, kwani zinahusina na maswala ya mwili wa binadamu na maumbile yake, na kipengele muhumi kinamhusu mtaalamu kama dakitari aliyebobea katika mambo hayo. Alikumbuka kuwa dakiti Kibonge ni bingwa wa magonjwa ya matumbo.

Walifika kwake na kwa vile walishatoa taarifa kuwa wanakuja, walimkuta akiwa nyumbani, wakabisha hodi, dakitari akatoka akiwa kavaa bukta na vest, alikuwa kashika kitabu. Alipomuona Rose akamkaribisha ndani na kusema alidhani wanamtania kuwa watakuja, na anshukuru kuwa kaja ili asiboreke. Akashangaa kuona kaongozana na msicha nwingine, akamgeukia Maua, na yule dakitari akabakia kaduwaa akimwangalia kwa muda mrefu Maua, kiasi kwamba maua mwenyewe akajisikia vibaya na kuona aibu.

‘Mbona ananiangalia hivi, au nimevaa vibaya, au sijachana nywele zangu, lakini nakumbuka nimezichana vyema, kwanini aniangalie hivi..’ alijiuliza sana Maua bila kupata jibu, mwishowe akasema moyoni, siji tena safari hizi kwa watu! Hilo ndilo muhimu analolikumbuka, zaidi ya hapo, ni kuwa mara kwa mara yule dakitari alikuwa akimwangalia, na baadaye akawa anamdadisi kwa maswali mengi, badala ya kundelea Rose, na hali ile ilimfanya akose raha. Alishukuru sana, ilipofika muda wa kuondoka, na alikuwa wa kwanza kutangulia nje, na hakugeuka nyuma mapaka alipofika nyumbani.

Akamwangalia Rose na kusema ‘Lakini mimi sielewei kwani kuna ubaya,gani yeye aliniangalia sana na sikujisikia vyema kwakweli, ndio maana sikupenda kwenda kwake tena, nakumbuka amekuwa akipiga simu kuwa anataka tuongee na yeye lakini siunajua tena kazi za hapa nyumbani ningeondokaje nimuachie nani, na hata hivyo niende kwake kufuata nini, mimi siumwi, sina masomo kama yako, niataondokaje hapa, wala sitaki kwenda huko…’ akasema huku anafikiria.

‘Basi wewe ndiye uliyenifukuzia ndege wangu, yule dakitari alishadata kwangu kabla ya wewe kumshitua mtima wake, na sijui wanaume wanatizama nini, hivi kweli nikuulize Maua, swali moja, niambie bila kuficha, mimi sio mzuri?’ akajiangalia na kujigeuza huku na kule. Maua akacheka na kumuona mwenzake kapagawa.

‘Kwani uzuri ni nini, mbona wewe u mzuri sana, mimi mwenyewe natamani niwe kama wewe, umzuri, msomi na wazazi wako wanajiweza. Mimi sina lolote, sina wazazi, sina urembo, na sijui maisha yangu yatakuwaje baadaye, ni mtu wa kuruka ruka kama ndege asiye na kiota …lakini yote maisha..’ akasema Maua huku kashika shavu.

‘Mmmh, jamani sasa umeanza, hivi kwanini hayasahau yaliyopita, mimi nilikuwa nauliza mambo mengine ya maana sasa wewe…, sasa unaanza kuleta uchuro hapa, sitaki kilio, kwanza mimi ndiye mwenye kutakiwa kusikitika kwa sasa, kwani wewe umenirushia ndege wangu…unaona alivyokuja Docta, unayemuita Docta wako, alishadata kwangu pia, kuonekana kwako tu, kosa…kooosa, naona sasa nikipata mtu mwingine, sitaki nikuone karibu…unasikia, sitaki akuone rafiki yangu wa kiume, kama nikipata mwingine, najua nitapata. Hawa wanaojiita madocta, wakafie mbali, sibabaiki na wao, kama ni udocta na mimi nitaupata karibuni,…’ akafyoza na kutema mate chini.

‘Unasikia Maua kama wakipiga simu kuniulizia waambie wakafanye nini…?’ akainuka kuondoka, na kugeuka kumwangalia Maua akisubiri amjibu swali lake, lakini Maua alikuwa kaka kimya akimwangalia usonii kwa mshangao, hakujua anatakiwa ajibu nini.

‘Tatizo lako Maua, hujui Kiswahili, huelewi, nimekuambia hivi wakipiga simu, hawo madocta wako, naona madocta wanawashwa na wewe, waambie hivi mimi, Rose, nimesema `WAKAFIE MBALI..WAFANYE NINI…?’

Maua akaendelea kukaa kimya, na Rose akakasirika na kukimbilia ndani. Na kweli Rose siku hiyo hakuataka kabisa kuongea na mtu alijifanya ana kazi zake za shule na kujifungia chumbani na hali hii ilimfanya Maua akose raha, na kuwa kwenye dimbwi la mawazo, hakujua nini kosa lake, akahisi sasa hapo hana muda tena, inabidi atafute kiota kingine. Akakuna kichwa, `niende wapi sasa, sitaki kuishi kwa watu wasionipenda, hapa Rose atafanya kila hila niondoke, najua hili, yeye anapendwa sana na dada yake…sijui nirudi kwa Docta wangu, lakini njia kule ni nyeupe, ila ….mmmh yale marue rue..najua atanitaka niende kwenye nyumba yake tena, je yakinitokea tena nitafanyaje..’ akakuna kichwa na kuinuka kwenda kufanya kazi za ndani.

Usiku ukawa umeingia, na wazazi walikuwa hawajarudi, walishapiga simu kuwa watachelewa sana. Na, wakati huo Rose alikua kaja kumsaidia mwenzake kazi za nyumbani. Kwa muda ule alioneka kubadilika na akamuomba msamaha Maua, kuwa yamekwisha ni mambo ya kawaida tu , asijali. Ila akumbuke alichoagizwa. Baadaye wakamaliza kazi za ndani, wakala chakula cha usiku na Rose akachukua vitabu vyake kuanza kusoma, huku anaangalia Runinga.

Maua naye akachukua kitabu chake alichokuwa kanunuliwa na Docta wake akawa anakisoma, na kabla hajajituliza vyema,mara mlango ukagongwa, na wote wakageuka kuangalia mlangoni. Ni nani saa hizi, muda wa wazazi wao kurudi bado, sasa ni nani muda kama huo, mawazo yao yalifikiri wezi, kwahi hali kama hiyo ilishatokea kwa jirani yao, kagongewa mlango akidhania kuwa ni mgeni, kumbe walikuwa wezi, wakawavamia na kuwaibia kila kitu.angaliana kwa woga, kila mmoja akimtegea mwenzake aende kufungua mlango…!

‘Wewe nani…’ Maua akauliza kwa wasiwasi na aliyegonga akawa kimya kidogo halafu akagonga tena. Na maua akarudia kuuliza, na huyo mtu akajibu, alipojibu, Rose akainuka harakaharaka pale alipokaa kwenye kiti na kuonyesha uso wa wasiwasi…

Je ni nani huyo! Na kwanini Rose ashituke kiasi hicho,tuendelee kuwepo!

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

4 comments :

Upepo Mwanana said...

Duuuuh!

Jane said...

Mmmmmh! hapo ndo tatizo letu wasichana linapokuja, sasa mwenzangu wamonea kijicho mwenzio hata hajui ni nini kinakuwa kinaendelea vichwani mwa hao madoctor!!!! Hata huyo aliyekaa nae siku nyingi hakuwahi kumtamkia chochote, sembuse huyo aliyemuona siku moja tu????. Kazi ipo hapo. Tupe mambo M3, japo nitakumiss maana naenda likizo si unajua tena mambo ya access si kote but nitajitahidi hata kwa sm nitakuwa naperuzi mara moja moja. Jamani wadau merry xmas na happy new year kwenu nyote na amani ya Bwana iwe nanyi nyote.

emuthree said...

Usijali Jane, ndio mipangilio ilivyo, mapumziko kidogo ili mwili upoe, ili uwaone ambao hujawaona siku nyingi, ili ujumuike na fammilia kwa sana...haya ya mitandao, yapo tu.
Nitakumiss sana, na nashukuru kuwa simu yako ina `vyote'
Hata mimi siajua utaratibu wa huyu ninajishikiza kwake...ila nitawahabarisha, na kwa vile internet cafe zipo...tutaitahidi hivyohivyo...karibuni sana!

Faith S Hilary said...

Merry Christmas and Happy New Year to you too Jane!!!!! hayaaa mgeni gani huyu