Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, December 10, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-8

‘Kaenda wapi huyu binti..’ nikauliza kwa sauti.


Nikaita jina lake tena na tena, lakini hakukuwa na dalili ya yeye kuwepo, tukamtafuta nyumba nzima hayupo, ina maana kaondoka , tukaduwaa, kwanini kafikia hatua hiyo ya kuondoka bila kuaga, au hayo madudu yamemtokea tena na kukimbia!

*** Je huyu binti katowakaje, na nini kiliendelea baada ya hapo, endelea na kisa hiki cha dokta***

                                             *******************
                                               *****************
                                                     **********
Tukajadili tufanye nini, ndipo wazo la kwenda kwenye kituo alicholelewa likaja, na tukaelekea huko na wazazi wangu, tulipofika kituo cha kulelea watoto waliokulia katika mazingira magumu kuulizia kuwa Maua kafika huko, tukaambiwa hajafika na wao wanajua yupo kwetu. Tuliwahadithia kilichotokea na hata kufikia kutoroka kwake, na wao wakaishia kushangaa na kusema hawakuwahi kushuhudia tatizo lolote la kiafaya kama hilo kwa binti huyo, na hiyo ni mara yao ya kwanza kusikia tatizo kama hilo, na kwahiyo inabidi tujaribu kumtafuta zaidi.


Tuliojaribu kufiria wapi anaweza kwenda lakini hakuna aliyepata ufununu, kwani wanasema yeye hana jamaa yoyote anayemfahamu na hapo kituoni ndipo alipolelewa na ndio baba na mama yake, na kila anapokuwa mapumziko kutoka kwa mwajiri wake huja hapo kukaa kama nyumbani kwake, kwahiyo hakuna fununu yoyote ya kuweza kusaidia. Na wao wana imani kuwa atakuja siku yoyote kama kawaida yake Tukaamua tusubiri, na kuacha maagizo kuwa akionekana wampe taarifa kuwa bado wao wanamuhitaji na mpango wake wa kusoma bado upo, kwani walishamlipia ada, na anakosa masomo yake.

Siku mbili kwangu ilikuwa kama miezi, na hapo nilihisi kumpenda huyu binti zaidi ya vile nilivyokuwa nikiwaza, kwani yeye kukaa kwake hapo tulizoeana na alijua nini nataka, nini anifanyie, na shughuli zangu za hapo nyumbani alikuwa yeye ndiye mwenye kuzijulia. Nikawa nimemkosa mtu muhimu sana.

‘Itabidi nitoe taarifa polisi watusaidie, huenda tukampata, au tutoe tangazo kwenye vyombo vya habari’ nikamwambia baba yangu, ambaye hakuonekana kujali kuondoka kwake.

‘Polisi ukiwaambia kuwa ulimchukulia kituo hicho, watakuamba, kuna mtu kamchuku kama ulivuomchukua wewe, hawatasumbuka, zaidi ya kuweka kumbukumbu zao. Mimi sioni kuwa kuna umuhimu wowote wa kumtafuta kama unahitaji mfanyakazi mwingine tutapata tu tena mzuri zaidi ya huyo, usijali sana.

Siku mbili, tatu, wiki , wiki tatu zikapita, hakuna dalili yoyote ya Maua. Nikaamua kuachana naye nihangaike kutafuta binti mwingine, lakini hata wasichana ambao nimezoeana nao kwenye sehemu za kazi au katika shughuli zangu za udakitari, hakuna hata mmoja aliyenivutia, nilikuwa namuwaza yeye. Lakini natakiwa nimpate mke wa kuishi naye, nitampata wapi, na wakati ? Nikajiuliza tena na tena, au niwahusishe wazazi wangu tu…nikasema bado sijashindwa, nitampata tu mwingine zaidi ya Maua!

Siku moja wakati nahangaikia kusajili hospitali yangu binafsi nilikuwa nimepitia kwa jamaa yangu mmoja huko Sinza, tukatoka naye kununua soda kwenye duka moja, tukawa tumekaa pale tunakunywa huku tukiangalia wapiti njia, na macho yangu yakatua kwa dada mmoja akiwa kamshika mkonono mtoto mdogo, alikuwa akivuka naye barabara kuelekea upande wa pili. Moyo wangu ulilipuka na nilipotaka kuinuka kuelekea kule alipoelekea rafiki yangu akaja na soda mbili mkononi, na kuniziba mbele yangu.

‘Hebu samhani, umeniziba nilikuwa naangalia kitu kimoja upande wa pili wa barabara’ nikamwambia rafiki yangu, na aliposogea sikumuona tena yule binti na mtoto, labda wamepanda basi au wameingia kwenye nyumba ya jirani.

‘Umeona nini, hujaacha udadisi wako wa vitu vidogovidogo, sasa wewe ni dakitari, unatakiwa ukite mawazo yako kwenye taaluma yako ya ubingwa..’ akaniambia huku ananipa soda yangu.

Mimi kichwani nilikuwa bado nahakiki nilichoona, inawezekana kweli akawa Maua, na kama ni yeye nitawezaje kujua wapi anapoishi huku. Nikaamua kuliacha hilo wazo kama lilivyo, lakini nikatafuta njia ya kuja kumtembelea tena huyu rafiki yangu na nijaribu kufanya utafiti wangu, huenda kama ni Maua naweza kukutana naye.

Siku zikapita na sikuweza kwenda kwa yule rafiki yangu tena, na wazazi wangu walikuwa na hamu ya kuitembelea nyumba yangu, kwahiyo tukapanga Jumapili moja kwenda pamoja na wao,

ili na wao waione. Nilijua wakiiona ilivyo, wataondokana na dhana potofu kuwa nyumba hiyo ina matatizo na haifai.

Tulifika pale kipindi cha saa saba mchana, sababu ya foleni ya magari, na tukawakuta mafundi wanapiga rangi na kumalizia, malizia zile sehemu ambazo zilikuwa hazijakamilika. Wazazi walishikwa na butwaa kuiona nyumba nzuri kama ile, wao walifikiria ni nyumba tu ya kawaida, wakanishika mkono na kunipongeza.

‘Nyumba kubwa na nzuri, utakuwa umenunua kwa shilingi ngapi mwanangu, nafikiri kama hizo hela ungeamua kujenga nyumba ya kwako mwenyewe, sio ya kununua ungejenga nyumba mbili..’ akasema baba

‘Lakini hata kama ni nzuri, mbona ulisema mwenye aliondoka mapema hakukaa sana humo, hamuoni kuna walakini…’ akasema mama

‘Walakini , hakuna, hizo ni hisia, wazazi wangu, hii ni dunia nyingine, sio ile dunia ya kuogopa mambao ya kishirikina, kama yapo tutapambana nayo, kwani wao si binadamu kama sisi. Wazazi wangu, mimi nimesomea udakitari, natakiwa nionyeshe mfano kwa jamii kuwa mambo hayo kama yapo ni imani, na imani nyingine hazisaidii, niza kuturudisha nyuma. Fikirieni, watu waje kusema dakitari aliikimbia nyumba kwasabaabu ya kuogopa kulogwa, sijui nini, hamuoni kila mtu naye ataamini hayo, na…’ nikagutuka nilipomuona yule mzee jirani aliyeonana name mwanzoni, akitazamatizama ndani upande wa pili wa ukuta wa nyumba.

Wazazi wangu wakageuka kumwangalia pia. Nikawaambia huyo ni irani yangu aliniambia anaijua historia ya nyumba hii tangu ilipoanzwa kujengwa, na nina hamu ya kukutana naye karibuni, ili niweze kujua ilianzaje, na …’ Nilishangaa kumuona yule mzee akitupa vitu kama unga unga angani huku anazunguka kama tiara. Nikatabasamu lakini wazee wangu walikuwa wameshikwa na wasiwasi, siui walikuwa wakifikiria nini.

‘Huyo mzee anaonekana anafanya mitambiko yake, na watu kama hawo wana imani zao, usiwajali na kuwaaingilia sana, cha muhimu ni kuwasaidia pale wanapohitai msaada, mimi siogopi mambo hayo’ nikasema na kumpiga picha kwa siri yule mzee, kwani huwa napenda kuweka kumbukumbu zangu kwenye computa yangu.

Kwasababu ilishafika muda wa kula, tukaoana tukae tule kwanza, mama yeye akawa anaendelea kutayarisha vitu vingine jikoni, mimi na baba tukawa tumekaa chumba cha maongezi tukipata vinywaji.

Kwa ujumla nyumba ilikuwa imekamilika, na bahati nzuri vifaa vingi vya ndani vilikuwepo na vilichanganya na gharama ya ununuzi wa nyumba, kuanzia meza, makabati, majokofu, vyombo , majiko vitanda magodoro, vilikuwa bado vipya, na ilikuwa haina haja ya kununua vitu vingine, labda matengenezo ya hapa na pale.

Tulikuwa tumebeba vyakula vilivyopikwa tayari, ila kuapsha moto na mambo mengine madogo, na tuliona ni vyema kuwaita mafundi tujumuike nao pale mezani. Walifurahi sana, wakaja na kukaa nasi tukawa tunaongea tukiwa tunasubiri makamilisho ya chakula hicho ambayo yalikuwa yakifanywa na mama na msichana mmoja tuliyemkuta hapo, ambaye walisema ndiye anayewapikia mafundi kwa makubaliano ya gharama zao wenyewe.

Tukawa tumekaa pamoja tunakula na mafundi wakawa wanahadithia mambo wanayokutana nayo wanapofika asubuhi kufanya kazi zao za ufundi. Mmoja alisema, kila siku lazima wakute damu sehemu ya mlangoni, na sio damu ndogo, na damu nyingi ni kama Ngombe kachinjwa au mbuzi. Tunazisafisha na kesho yake unakuta tena damu nyingine.

Mwingine akasema, akiwa ndani amewahi kusikia milio ya ajabu kama vitu vinatembea darini, na akipanada juu kuangalia haoni kitu, ….

‘Lakini sisi tumeshajenga nyumba nyingi zenye vituko zaidi ya hivi, kwetu tunaona kama jambo la kawaida, ila hapa pamezidi…’ akasema mmojawapo. Mimi nilishachoka kusikia haya maneno, na sikuyatilia manani sana, lakini baba akawa anayaulizia kiundani zaidi, kiasi kwamba nikawa sipati raha.

‘Nyinyi mnahisi ni kwanini kuna watu wanachinjia nyama zao hapo au kuna mauzauza gani..’ akauliza baba.

‘Hawa ni watu wanajaribu kukatsiha watu tama, wana wivu tu, lakini wengine wanasema huenda kuna mashetani wanaishi humu, na damu ndio chakula chao, kwahiyo kuna mtu anawalisha hiyo damu…zingatia nyumba hii ilikaa muda bila kuishi mtu…’ akasema fundi mmoja.

‘Sasa mnataka kutuambia nini, kuna maini humu ndani au mashetani..’ akauliza baba.

‘Majumba mengi yasiyoishi watu yanakuwa na mambo hayo, kinachotakiwa kabla ya kuhamia ni kuita wataalmu wasome na wenyewe wataondoka tu…’

Na baadaye mmojawapo akaanzisha mjadala wa hali ya fundi wao mkuu. Nikawaambia hali yake inaendeela vyema, kwani asubuhi hiyo nilimpitia nyumbani kwake na kesho atakuwa pamoja na wao, wasiwe na wasiwasi tena…

Na mara tukasikia sauti ya ajabu, kama ukunga, au mwangwi…lakini ni ya mtu ikitokea jikoni, au sehemu ya mbele ya jikoni…hatukuwa na uhakikia. Iliporudia mara ya pili, nikahisi imetokea jikoni…

Nikamwangalia baba, ambaye naye alikuwa katega sikio kusikiliza kuna nini. Nikainuka haraka kuelekea huko jikoni, kwani mtu aliyekuwa huko jikoni ni mama na msichana mmoja ambaye huwapikia mafundi. Nilipofika nilimshangaa msichana yule kasimama huku kashika kichwa kakodoa macho na kuduwaa. Nikaelekeza macho yangu kule anapotizama,…

Ni mimi: emu-three

11 comments :

Fadhy Mtanga said...

nafurahi kuwa msomaji wako mzuri...keep it up

Jane said...

Mmmmmmh!!! hii story inaniacha speachless kila siku maana ni vitisho kila kukicha.

Anonymous said...

Mhh, angalau unapunguza makali ya kuogofya, kidogo raha, kidogo kitisho...mmh, ungeongeza `mapenzi' kidogo, kwani kuna wapenzi wa mambo hayo...sio mimi lakini..lol

pamela said...

jamani jamani hayo matisho sa bimkubwa kakutwa na nini?? kweli doc alikuwa mbishi cjui ndani ya mauzauza kama hayo bado ana hamu na hiyo nyumba hata kama ni nzuri kiasi gani amani inatakiwa itawale

Anonymous said...

Hongera sana miram but imsoory ure name is confuse me idont ure girl or boy but ilike blog ilike the stories kwakweli niko radhi hata nisile mchana niingie net nisome visa si mchezo uko juu miram

Anonymous said...

Hongera sana miram but imsoory ure name is confuse me idont ure girl or boy but ilike blog ilike the stories kwakweli niko radhi hata nisile mchana niingie net nisome visa si mchezo uko juu miram

Anonymous said...

But miram mbona ile ya nani kama mama ujaiendeleza jamani its very best story for sure najifunza mengi inshort Be Blessed

chib said...

Mimi naomba uendelee kuwa hivyo hivyo kivuli. Inanipa raha kutoa komenti kwa mtu nisiyenjua kabisa.
Lkn, booonge ya stori

Simon Kitururu said...

Mkuu! DUH! Sikio linaendelea kutegwa hapa kama kawa......

Faith S Hilary said...

jamani jamani I hope mama kasalimika...uuuuuuh...

elisa said...

mi jamani naendelea kutoa ombi ungekua una update kila siku...maana wengine ..tumeshakua wagonjwa wa kufuatilia..lol