Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, December 8, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-7

Yule fundi mkuu alikuwa akijaribu kujiiokoa mikononi mwa yule binti bila mafanikio, na kifo kilikuwa kikimkodolea macho, nikaona lazima nifanye jambo la haraka, nikaweka dawa ile kwenye sindani nikawa namfuatilia yule binti kwa nyuma.


‘Ukimpiga sindano utamuua…’ nikasikia mmoja akisema miongoni mwa wale mafundi, na yule binti akamrushia mbali yule fundi mkuu akawageukia wale mafundi wengine, wao kuona vile wakatimua mbio….


**************Je iliendeleaje, soma sehemu hii inayofuata*****


Nikawa nahaha akilini nifanyaje,nilikumbuka nilivyohadithiwa watu wakipandisha mashetani wanavyokuwa, wanasema watu hawa wanaweza kuongea sauti ya mtu aliyekufa, na hata kama ni mwanamke anaweza kuongea sauti ya kiume. Lakini sikumbuki kuwa wanaweza kuwa na nguvu za ajabu kiasi hili. Yote haya nilihadithiwa, na nilikuwa nikiyawaza akilini, lakini sikuwahi kukutana na mtu aliyekuwa na matatizo hayo ana kwa ana! Na kwa dalili za huyu binti, niliona ni zaidi ya mashetani.



Ilitakiwa binti huyu akamatwe, na kufungwa kamba, kwani wakati mwingine alikuwa akijipiga ukutani, au kupiga ngumi ukutani akionyesha kuwa ana hasira, na vitendo hivyo vilikuwa vikimuumiza mikono na mwili wake. Wenzangu wote wamekimbia, labda tungesaidiana kumkamata na yule fundi mkuu yupo katika hali mbaya, nifanyeje sasa?



Nikaiangalia ile sindani ambayo nilishajaza dawa, lakini nikaona haifai, kwasababu hawa jamaa wamenitahadharisha, nisitumie sindano, lakini kwa utaalamu wangu, sindano hudungwa watu wa namna hii, ili kuwapunguza nguvu walizonazo, nah ii tunaitumia sana hospitali kwa w dawa ikishaingia mwilini awaliorukwa na akili, akipigwa mwili hulegea na kulala. Sasa hawa mafundi wamenionya kuwa mtu mwenye haya madudu, hatakiwi kupigwa sindano, kwani ukimpiga sindano, utamuua!



Hapana hizo ni imani zao tu, na hazina uthibitisho kitaalamu.



Lakini hata hivyo, hata haya wayaitayo mashetani yana uthibitishoo gani kitaalamu, na tofauti yake ipo wapi na waliorukwa na akili, nikawaza huku namwangalia yule bintianavijipiga piga ukutani, nilitamani niinuke nimsaidie lakini mguu ulikuwa kama umekufa ganzi!



Nilijiona sina maana kabisa, kwani mimi ni dakitarii na nina mgonjwa mbele yangu, bado siwezi kutoa msaada wowote, lakini ningefanyaje, kwani nina uhakika mguu wangu umeteguka, kila nikijaribu kuuinua nilikwa napatwa na maumivu, na ulikuwa hausogei…hili sasa ni tatizo, na mganga atajigangaje?

Nikijaribu kupeleka mawazo yangu kwenye imani hizi za mashetani na kuiuliza mengi kuhusiana na imani hizi, na kunipa changamoto kuwa inabidi nitafiti kiundani, imanai hizo na hali halisi za wagonjwa wenyewe, na bahati nzuri kuna mgonjwa huyu ambaye atakuwa karibu name. Je aliwahi kupatwa na matatizo haya kabla? Hilo ni swali la kumuuliza mwenyewe, nikamwangalia pale aliposimama, na sasa alikuwa anajipigapiga kifuani, kuonyesha kuwa yeye ni mshindi.

Sasa kama dakitari nichukua hatua gani, nikajiuliza, kwani nilishawekwa njia panda, je akinijia nisimpige sindano, nimuachie, na nikimuacha atanizuru, nikamwangalia yule fundi alivyolala pale chini siui keshakufa au ana hali gani, nikawaza na mimi nitakuwa vile pindi huyu binti akinikamata tena, sina nguvu za kumkabili kwa sasa.

Hapana, akija sindano itatumika, ili nijiokoe mwenyewe, kama itamzuru, kama itamuua, hayo ni maswala mengine! Kwani ni lipi bora., nife mimi au afe yeye, nikajiuliza,. Kama dakitari unatakiwa umuokoe mgonjwa, hiyo ni moja ya kazi zetu. Lakini kwa dharura kama hii ungechukua uamuzi gani, je Nitamuokoaje katika hali kama hii, zaidi ya kumpunguza nguvu zake za ajabu, na njia rahisi ni kumchoma sindano!



Wakati nawaza haya, huyu binti alikuwa kaanza kuzunguka huku na kule huku ananguruma kama simba, na kutamba kwa sauti kubwa ya kiume kuwa atawamaliza watu wote, hasa wale wanaoingia katika milki yake, atawaua wale wote wanaomchukua kiti wake.Kiti wake? Ni nani huyu kiti wake? Au labda …inawezekana kiti wake ni huyu binti!.Lakini jina la huyu binti haitwi kiti, anaitwa Maua, sasa huyu kiti ndio nani…?



Mara simu yangu ikaita, …oh, balaa, simu imeniumbua, kwani yule binti alisimama ghafla na akawa anatafuta mlio unapotokea, nilipoitizama nikaona ni rafiki yangu, nikaipokea haraka na kumwambia aje na gari la wagonjwa haraka iwezekanavyo, kwani nipo hatarini. Kwa sauti niliyoitoa kwa rafiki yangu lazima atajua kweli nipo kwenye hatari, alikata simu haraka, nami huku nikatafuta njia ya kupoteza muda ili huyu binti asinidhuru



Nikawa nazunguka kwa kutambaa huku na kule kumkwepa kila anapogeukia mahali nilipo. Kutembea kwake kulikwa kama roboti, au ajitu lenye nguvu, kwahiyo anapogeuka hutumia muda sio kama anavyogeuka akiwa katika hali ya kawaida. Kwahiyo mimi nilikuwa natumia ujanja huo, akigeuka taratibu kuelekea nilipo nahama upande mwingine, lakini baadaye akatambua ujanja wangu, akanigeukia haraka kunielekea pale nilipokaa nikasema sasa nimekwisha. Nikaishika ile sindano mkononi, nikiwa nimejiandaa, akinijia mimi naipachika mwilini mwake popote!

Alianza kunisogelea, nikawa namuonyeshea ile sindano ili aogope, lakini alikuwa akija huku mikono kainyosha mbele, kuwa anakuja kunikaba, au kunimaliza kwa mikono yake. Sura yake ilishabadilika kabisa, nywele alizokuwa kazifunga kichwani zilikuwa zimeachia na kumfunika sehemu kubwa ya uso, lakini macho yake yalikuwa makubwa na meupe. Ule weusi ulikuwa ukionekam mdogo sana. Sauti anayotoa ni ya kiume, na anaguruma kama samba.

Nikajaribu kukumbuka kama kuna sehemu niliisoma yenye maelezo kuwa ukimkuta mtu kama huyu umsaidieje, sikumbuki zaidi ya kumdunga sindano hii ya usingizi. Nikasema potelea mabli akija mbele yangu mimi nitamdunga, kwani hizo nyingine ni imani za watu, kuwa akidungwa sindano atakufa.

Nilimtupia jicho yule mlinzi alyerushiwa nje ya mlango, nilimuona hasogei, hata kuhema sikuona dalili hiyo, inawezewkana keshakata roho, kwani kipindi kile alichokuwa kanininginizwa, juu kwa juu, ulimi ulitoka nje, kuonyesha kuwa yupo katika halimbaya. Sasa itakuwa tatizo , haya ni mauaji. Nikamgeukia huyu binti ambaye alikuwa sasa ananikaribia, na mimi nikawa narudi kinyumenyume hukui nimechuchuma, kwani mguu mmoja ulikuwa umetegeuka.

Kwa mbali nikasikia king’ora cha gari la wagonjwa kikikaribia, nikawa naomba mungu huyu binti azidi kuchelewa kunifikia. Mungu wangu nisaidie, maana sasa sina jinsi, lazima nimdunge sindano, je sitamuua binti wa watu…

Ghafla akasimama, kama mtu aliyepigwa ganzi. Nikamuona anayumbayumba, na mara akadondoka chini kama gunia, na mara akawa anarusha rusha miguu, na kukoroma, halafau akawa kimya…nikapata nguvu za kujikongoaja, na hapo maumivu ya mguu yakaanza kusikika, na mlangoni akaingia rafiki yangu dakitari na wasaidizi wake wengine wanne.

‘Vipi kumetokea nini hapa?’ akaniuliza huku akijaribu kumwangalia yule binti na wengine walikuwa wakimshughulikia yule fundi.

‘Nashindwa hata kukuelezea, hili kwasasa, hili ni tukio la mwaka, katika maisha yangu ya udalitari hii ni mara pili, lakini hili limezidi kiasi…’ nikasema huku namwangalia yule binti pale alipolala.

Walimbebea yule mlinzi kwenye machela, walisema hali yake ni mbaya inabidi akimbizwe hospitali, na huyu binti alikuwa keshazindukana na akawa anashangaa kumetokea nini! Nilimhadithia rafiki yangu kwa kifupi, akasema inabidi tuwaarifu polisi kama lolote litatokea kuhusiana na yule fundi. Na polisi walipoelezwa walifika haraka na kuchukua maelezo, na wakafuatilia nyuma gari lili la wagonjwa. Niliwaomba wasimfanye lolote huyo binti kwani alichofanya hakijui, na bahati nzuri askari wale walielewa, kwani walisema wanajua matatizo hayo, lakini maelzo yanahitajika kwa kumbukumbu.

Binti yule akaamuka na tukamsaidia hadi kwenye gari, na tuliona hakuna haja ya kumpeleka hospitali tuliridi nyumbani, na nilipowahadithia wazazi wangu walishangaa sana, wakaulizia kule alipolelewa huyu bintiu wakasema haijawahi kumtokea hata siku moja kitu kama hicho, hiyo ni mara ya kwanza.

Mama alishamuita kiongozi wa dini akawa anamsomea, au kumuombea yule binti, na baadaye yule kiongozi wa dini akasema, yeye haoni tatizo lolote kwa huyo binti kwa sasa inawezewkana alipitiwa na pepo mbaya, cha muhimu ni yeye kujihami kwa kuwa mcha mungu. Nikamwangalia kwa Huruma sana yule binti, kwani mweneywe alishakata tamaa kuwa kazi sasa basi na huenda tukamfukuza mle ndani. Nilielewa hili , nikamhakikishaia kuwa mipango yetu ya kumundeleza kishule na mipango yake ya kazi ipo palepale, asiwe na wasiwasi.

‘Je katika kumbukumbu zako, ulishawahi kukutana na tatizo kama hili?’ nikamuulizia

‘Mimi wala sijui ni tatizo gani, mimi sijawahi hata siku moja, kusikia hali kama hii, mimi …hata sijui kumetokea nini…mimi ninachokumbuk, nilipoingia mle ndani kwenye nyumba ile, niliskia kichwa kinaniuma sana, na mara moyo ukaanza kunienda mbio, na nikawa sijitambui tena, na sikuelewa kilichofuata, hadi nilipozindukana pale, nilijiona kama nilikuwa usingizini tu!’ akasema kwa kushangaa.

‘Mimi kama nilivyowashauri, mambo haya yapo, na kuyakwepa kwake nikuwa msafi, na kuwa mcha mungu. Hawa wadudu wanapenda sana watu waovu, watu wasio mcha mungu. Na wakipata upenyo wa kumwingia binadamu wanaweza wakakutesa sana. Na inawezekan hiyo nyumba mliofikia ina matatizo, na bora mtafute watu waisomee, …’ akasema na kuahidi kuwa atakuja twende naye kwenye hiyoi nyumba.

‘Wewe umewkenda kununua nyumba bila kutushirikisha, sasa unaona mambo yake haya, mimi nahisi nyumba uliyonunua ina matatizo..’ akasema mama

‘Mama ile ni nyumba tu, kama nyumba nyingine, na nimeinunua kihalali kabisa, stakabazi zote ninazo, na sio kuandikishana tu kiholela, nimeenda mpaka serikalini, na kuhakikishiwa kuwa hakuna matatizo sasa iwe na matatizo gani!’ nikajitetea.

‘Wewe huijui dunia hii, watu wabaya, watu wanaweza wakawa wametupia mambo machafu humo ndani, ili tu kuwasumbua wenzao, …’ akasema tena mama.

‘Chamuhimu sasa nikutafuta njia ya kugundua nini tatizo, inawezekana tatizo sio nyumba kama tunavyowaza, inawezekana huyu binti ana matatizo yake, lakini alikuwia hajijui, wewe ni dakitari mpime, na tafuta labda ana malaria au tatizo jingine’ akasema baba, na mimi nikamuunga mkono.

‘Wewe baba nanihii, watu kama hawo nasikia hawapigwi sindano, usije ukakurupuka ukampiga sindano mtoto wa watu!/’ Akasema mama kunionya. Niliwaza kwanini sindano haitakiwi kwa watu kama hawa!

‘Kwani hata sindano kidogo ya kupima damu itamletea matatizo, na sasa hivi hali yake ni ya kawaida, kwahiyo sidhani kama itamuathiri, ngoja niende naye hospitalini akachunguzwe vyema afya yake. ..’ nikasema huku najiandaa kuondoka.

‘Maua…Maua…’ nikawa naita, lakini sikusikia mtu kuitika, nikaingiwa na wasiwasi, huenda huyu binti kazidiwa, nikaelekea chumbani kwake, niligonga mlango mara nyingi bila majibu, ikawa haina jinsi, nikaufungua, nikakuta chumba kitupu, hakuna mtu…na hata baadhi ya nguo zake hazipo…

‘Kaenda wapi huyu binti..’ nikauliza kwa sauti.

Nikaita jina lake tena na tena, lakini hakukuwa na dalili ya yeye kuwepo, tukamtafuta nyumba nzima hayupo, ina maana kaondoka , tukaduwaa, kwanini kafikia hatua hiyo ya kuondoka bila kuaga, au hayo madudu yamemtokea tena na kukimbia!

Ni mimi: emu-three

4 comments :

elisa said...

hii ni kali kuliko zote M3 ..haya sisi tunasubiria kinachofuatia...

Jane said...

Mimi kwanza nashukru umerudi, jamani mbona ningekuwa mimi hiyo nyumba ningeazna kutafuta mnunuzi??? Harafu huyo binti nae sijui ndo yameshaweka makazi kwake au yenyewe ndo yalimpeleka pale ili kumpa salaamu huyo kaka sasa nae haelewi somo???? Mmmmh! ngoja tusubili tuone mwisho wake japo inatisha. Kazi nzuri

Pamela said...

duh hii ni hatari mtt wa watu kakutwa na balaa gani maskini pole kwake dr nae anawasiwasi na mpenzi wake wa siri

Anonymous said...

Mmmmmmmmmmm!!!!!! ni kweli ni kali kuliko.

BN